Udalali wa Daktari.

Egypt's Dar Al-Ifta

Udalali wa Daktari.

Question

Je! Nini hukumu ya daktari kufanya udalali kwenye maabara za kupima vipimo mbali mbali vikiwemo vya mionzi badala ya kumuelekeza mgonjwa kwenye maabara hiyo? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Baadhi ya madaktari kwa makubaliano pamoja na maabara au kituo cha mionzi kuwapeleka wagonjwa na kupewa kiasi maalumu cha pesa au kupata manufaa mengine ya mali.
Daktari akifanya hivyo, basi anajifananisha na dalali, kwa sababu anakuwa kama chombo cha kuuza manufaa au huduma kwa mgonjwa, Mullah Ali Al-Qari alisema: "Dalali: ni mtu aliye kati ya muuzaji na mnunuzi kwa ajili ya kukukamilisha kuuza, naye ni mwenye kuhifadhi kitu". [MArqat Al-Mafatiih 5/1910, Ch. Dar- Al-Fikr].
Dalali ni mfanyabiashara kwa hivyo ana hukumu yake, imepokelewa kutoka kwa Qais Ibn Abi Gharzah R.A. alisema: "Tulikuwa katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. tukiitwa madalali, basi Mtume S.A.W alitupitia akatuita jina zuri zaidi kuliko jina lile, akasema: Enyi wafanyabiashara. Hakika uuzaji una maneno ya upuuzi na kula viapo, basi changanyeni uuzaji kwa Sadaka". [Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawood, At-Tirmidhi, An-Nasaai, na Ibn Majah]
Labda iliyokaribu zaidi ni kwamba anayechukua dalali ni katika zawadi, nayo kulingana na lugha ni jina la kitu anachopewa mtu kwa kufanya kitu fulani, na kisheria ni kujitolea kitu maalumu kwa ajili ya kufanya kazi fulani inayojulikana au isiyojulikana yenye ugumu kuifanya. Kama alivyosema Al-Khatwib Al-Shirbiniy katika kitabu cha: [Al-Iqnaa 3/183, Ch. Mustafa Al-Halabiy].
Kwani mgonjwa haendi kwa daktari akiwa anataka dawa au vipimo vya mionzi au vipimo vingine, bali kitu hiki daktari humtaka mgonjwa akifanye kulingana na hali ya ugonjwa wenyewe, na kuna uwezekano wa mgonjwa kutohitaji chochote katika hivyo.
Hukumu katika suala hili kwa kuzingatia yaliyotajwa hapo juu kuwa asili yake ni kuruhusiwa, ni sawa tukijaalia kuwa kazi hii ni kama udalali au ni zawadi, lakini kwa sharti kwamba faida hii ithiathiri tabia za daktari, akamlazimisha mgonjwa kwa asiyohitaji kwa mfano, na ikiwa atafanya hivyo wakati huo hukumu yake ni kumzuia, na pengine ndivyo kilichofanya sheria ikachagua kumzuia, na pengine hii inaweza kuwa ni sababu ya ufuatiliaji wa idadi kubwa ya makosa katika suala halisi, na inajulikana kwamba kuondoa madhara hupewa kipaumbele kabla ya kuleta manufaa, vile vile na kufunga njia zinazoweza kufikisha katika haramu huzingatiwa kama dalili ya kisheria kama manufaa yakithibiti, na wakati kukiwapo madhara kwa ajili ya kuhalalisha kazi iliyotajwa hapo juu, kuonesha kwamba kuna ukiukaji kwa suala halisi, ni lazima kutoa Fatwa kwa kuzuiwa.
Orodha ya maadili ya matibabu iliyotolewa na Waziri ya Afya na Makazi No. 238 ya 2003, na katika kifungu cha 8:
Daktari hawezi kufanya kazi zozote zifuatazo:
(A) Masaada wa watu wa kati katika mazoezi ya taaluma, ikiwa kwa malipo au pasipo na malipo.
(B) Kuruhusiwa kwake kutumia jina lake katika kutangaza madawa ya kulevya, au matibabu mbalimbali au kwa madhumuni yoyote ya kibiashara kwa namna yoyote.
(C) Kuomba au kukubali zawadi au malipo yoyote kwa ahadi au kuelezea dawa au vifaa maalumu kwa wagonjwa, au kuwapeleka hospitali, au mahala pa uuguzi au maduka ya dawa au sehemu yoyote maalumu ya kufanya majaribio ya matibabu na vipimo, au kwa ajili ya mauzo ya vifaa vya tiba .
(D) Kufanya ushauri wa matibabu katika maduka, ambayo lengo lake ni kuuza madawa, vifaa vya matibabu, ikiwa kwa bure au kwa mshahara au kwa malipo.
(E) Kufanya ushauri wa matibabu kupitia makampuni ya mawasiliano ya simu.
(F) Kuuza madawa yoyote, maelezo, au vifaa vya matibabu katika kliniki yake, au katika wakati wa kufanya kazi yake, kwa madhumuni ya biashara.
G Kugawana malipo yake pamoja na yeyote miongoni mwa wenzake, isipokuwa kama atashirikiana nao katika matibabu kwa ukweli, au kuwa mpatanishi kati ya daktari mwingine au hospitali kwa namna yoyote.
Kifungu cha “C” kinajumuisha maana iliyo katika swali.
Kulingana na maelezo yaliyotajwa hapo juu, hairuhusiwi kwa daktari kufanya udalali au kuchukua zawadi kutoka katika maabara ya vipimo na makampuni ya dawa kwa ajili ya kuwaelekeza wagonjwa sehemu hizo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas