Kabla ya Kuuza Muuzaji Ameweka Shar...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kabla ya Kuuza Muuzaji Ameweka Sharti la Kutohusika na Kasoro.

Question

Nimenunua gari kwa mtu lililotumika na akaniwekea sharti la yeye kutohusika ikiwa itaonekana kasoro yoyote ile, nikalipa na kuchukua gari, baadaye nikagundua kuwa kuna kasoro ambayo kama kasoro hii ningeiona wakati ule wa kununua, basi nisingelinunua. Je kile kitendo cha muuzaji cha kuweka sharti la kujiepusha ikiwa kutakuwa na kasoro ni sahihi kisharia au hapana? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Muuzaji anapaswa kumfahamisha mnunuzi kasoro zilizopo kwenye kitu anachokiuza na wala haifai kuficha, ikiwa atamfahamisha kasoro iliyopo na mnunuzi akakubali kununua pamoja na kasoro hiyo hapo muuzaji anakuwa hana kosa na kulazimika mnunuzi kukubali, hakuna haja kwa muuzaji kuweka dhamana. Ama ikiwa muuzaji hakuweka wazi kwa mnunuzi kasoro zilizopo na kumficha basi muuzaji anapata dhambi, kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Si halali kwa Muislamu kumwuzia ndugu yake kitu chenye kasoro isipokuwa ikiwa amemwelezea hiyo kasoro”. imepokelewa na Imamu Ahmad, pia Ibn Majah na Hakim katika kitabu chake cha Mustadrak.
Na imekuja katika kitabu cha Imamu Bukhari na Muslim kutoka kwa Ibn Hazzam toka kwa Mtume S.A.W. amesema: “Wawili Wenye kuuziana wana hiyari ikiwa bado hawajaachana, wakiwa wakweli na wawazi, basi hubarikiwa kwenye mauzo yao, na wakiwa ni waongo na kuficha hufutwa baraka kwenye mauzo yao”.
Kama vile kuficha kasoro ni katika udanganyifu, na udanganyifu ni haramu kutokana na Hadithi iliyopokelewa na Imamu Muslim katika kitabu chake inayotokana na Abu Huraira Mtume S.A.W., anasema: “Mwenye kufanya udanganyifu si katika sisi” pamoja na dhambi zake lakini mauzo ni sahihi kwa kauli ya wanachuoni pamoja na kuthibiti hiyari kwa ujumla kwa mnunuzi, lakini wanachuoni wana maelezo ya kina katika suala la hiyari.
Ikiwa muuzaji ameweka sharti kwa mnunuzi la kutohusika kwake na kasoro ya bidhaa au kitu anachouza pamoja na kufahamu uwepo wa kasoro hii lakini akaficha, basi wanachuoni wametofautiana katika usahihi wa sharti hili kwa kauli tofauti:
Kauli ya Kwanza: Ni kuwa sharti hilo ni sahihi, na muuzaji hahusiki kabisa na kasoro hiyo, kauli hii pia imesemwa na wafuasi wa Abu Hanifa. Anasema Al-Kasaniy alipokuwa anazungumzia sharti za kuthibiti hiyari: “Miongoni mwa aliyoyasema: Kwetu sisi ni kutoweka sharti la kutohusika na kasoro katika kuuza na ikiwa ataweka, basi hakuna hiyari kwa mnunuzi, kwa sababu sharti la kutohusika na kasoro ya kitu kwetu sisi ni sahihi” (Kitabu Badaii Al-Sanaii, 5/276, chapa ya Dar Al-kutub Al-Elmiya). Ndani ya kitabu Al-Hidaya cha Merghinaniy kinasema: “Mwenye kumwuza mtumwa na kuweka sharti la kutohusika na kasoro iliyopo, basi mnunuzi hawezi kumrudisha kwa kasoro hata kama mwuzaji hakutaja idadi za kasoro hizo” (6/396, kimechapishwa na Fath Al-Qadir, chapa ya Dar Al-Fikr).
Kauli ya Pili: Kuweka sharti ni batili na muuzaji anahusika, isipokuwa ikiwa muuzaji huyo amemfahamisha mnunuzi na kukubali, ni kauli ya madhehebu ya watu wa Imamu Hanbal, na inafahamika pia katika pokezi za Imamu Malik, na kudhihirika kwenye kauli za Imamu Shafi, isipokuwa Imamu Malik na Shafi wameondoa suala la mtumwa, kwani sharti linafaa ikiwa muuzaji hafahamu kasoro iliyopo lakini sharti halifai ikiwa anafahamu, na akaongeza Imamu Shafii kwa upande wa wanyama, na kuhusisha - Imamu Shafii - kufaa sharti la kutohusika kwa upande wa mtumwa na wanyama kwa zile kasoro za ndani ambazo muuzaji hazifahamu tofauti na kasoro za nje au za wazi ambazo muuzaji anazifahamu, Imamu Malik akaondoa kauli kwenye kasoro za mtumwa ziwe za wazi au za ndani.
Katika kitabu cha: [Al-Kafy cha Ibn Abdulbarr]: “Haifai kutohusika na kasoro kwa kuuza kitu au bidhaa ya chakula au kinywaji au vyenginevyo katika vitu vyote vyenye kuuzwa isipokuwa kwa mtumwa maalumu, na atahusika na kasoro yule mwenye kuuza ukiondoa mtumwa, isipokuwa ikiwa ameainisha hizo kasoro na kuzitaja na mwenye kuuziwa akaona, ikiwa muuzaji amejitoa kwenye kasoro zilizopo kwa mtumwa kwa yule anayemwuzia, kisha akamwuzia kwa sharti la kutohusika na kasoro anakuwa bado ni mwenye kuhusika na kasoro anazozifahamu, lakini anakuwa hahusiki na hizo kasoro ikiwa muuzaji mwenye hazifahamu, na ataapa kuwa yeye hafahamu hizo kasoro ikiwa mnunuzi atadai” (2/712, chapa ya Maktabat Ar-Riyadh Al-Haditha).
Katika kitabu cha Al-Bayan wa At-Tahsil cha Ibn Rushd (babu): “Kuna masuala. Na akasema Imamu Malik: Haifai kuuza kwa sharti la kujitoa kwenye kasoro kwa mnyama hata kama wataweka sharti kwenye kitu chengine, lakini mnunuzi akigundua uwepo wa kasoro atakirudisha, kwetu sisi hakuna sharti isipokuwa kwa uuzaji wa mtumwa” [7/317, chapa ya Dar Al-Gharb Al- Islamiy].
Na akasema Ibn Rushd (mjukuu): “Wanachuoni wametofautiana katika suala la kufaa kwa mauzo haya, na sura yake ni: Muuzaji kumwekea sharti mnunuzi kuwajibika kwa ujumla na kasoro zote atakazozikuta kwenye bidhaa au kitu alichonunua… ama kwa upande wa Imamu Malik: Kinachofahamika kwake ni kuwa sharti la kutohusika linafaa katika zile kasoro anazozifahamu muuzaji, lakini hilo ni kwa upande wa kuuza mtumwa” [3/200, chapa ya Dar Al-Hadith- Kairo].
Na akasema Al-Mardawiy: “Ikiwa atamwuzia na kuweka sharti la kutohusika na aibu zote bado atahusika” vilevile lau atamwuzia na kuweka sharti la kutohusika na kasoro atahusika zikiwepo, na madhehebu haya katika hilo hakuna shaka yoyote, na kauli hiyo pia ni kwa upande wa jopo la wanachuoni” [Kitabu Al-Insaf, 4/359, chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby].
Anasema Al-Khatib As-Sherbiniy: “Lau atauza mnyama au asiyekuwa mnyama kwa sharti la kutohusika na kasoro zilizopo au akasema: Nimekuuzia kwa sharti la kutorudisha kwa sababu ya kasoro, kauli ya wazi zaidi ni kuwa hatohusika na zile kasoro za ndani kwa mnyama ambazo hakuzijua muuzaji tofauti na zile alizozijua kwa maana ya kasoro zilizotajwa, atahusika na kasoro zisizokuwa kwa mnyama kama vile kasoro kwenye mavazi na nyumba, wala zile kasoro za wazi kwa mnyama ima akiwa anazijua au hapana, wala kasoro za ndani za mnyama anazozifahamu, na kusudio la kasoro za ndani kama alivyosema Sheikh wangu: Ni zile mara nyingi si zenye kuonekana”. [Kitabu cha Mughny Al-Muhtaj, 2/450 – 432, chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]. Wafuasi wa madhehebu ya Abu Hanifa wamechukua dalili zifuatazo za kufaa kuuza kwa sharti:
Ya Kwanza: Ni inatokana na Hadithi ya Umm Salama amesema: “Kuna watu wawili miongoni mwa Maansari walikuja kwa Mtume S.A.W. wakiwa wametofautiana kati yao katika masuala ya mirathi na kufahamika kuwa hakuna ushahidi mzuri kati yao, Mtume S.A.W. akasema, nyinyi mmeniletea malalamiko yenu, lakini mimi ni mwanadamu na huenda mmoja wenu akawa na hoja zaidi na nikahukumu kufuatana na hoja hizo kwa kumzingatia kuwa ni mkweli, nitakaye mpa haki ya ndugu yake Muislamu, basi afahamu haki hiyo ni kipande cha moto atakuja nacho shingoni mwake siku ya kiyama, basi wale watu wawili walilia na kila mmoja akawa anasema ni haki yangu, Mtume S.A.W., akasema: Ama kwa kusema hivyo basi nendeni na mkagawe ardhi sehemu mbili kisha mkusudie kupeana haki, kisha muipe umuhumu, kisha kila mmoja wenu amhalalishie mwenzie”. Imepokelewa na Imamu Abu Dawud na Hakim pamoja na At-Tabraniy katika kitabu cha Al-Kabir.
Ufahamu wa dalili katika Hadithi hii ni kuwa kutohusika na haki isiyofahamika ni jambo linalofaa, na kasoro iliyopo kwenye kitu chenye kuuzwa ni katika haki isiyofahamika.
Ya Pili: Ni Hadithi iliyotokana na Imamu Tirmidhiy na kusahihishwa na Hadithi ya Amr Ibn Auf kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Waislamu wana masharti yao”. Hadithi kwa ujumla wake inaingia ndani yake sharti la kutohusika na kasoro.
Ya Tatu: Kama walivyochukua dalili kuwa kutohusika ni kuondoa haki, nayo hata ikiwa na maana ya kumiliki na kutojua, lakini kutokujua hakuzuii umilik, bali kunapelekea kuzaliwa mvutano, dalili ni kufaa uuzaji wa kubahatisha na ndani yake kuna aina ya kutofahamika lakini hakupelekei mvutano, kuongezea pia sharti la kutohusika limeridhiwa na mnunuzi naye amekubali kwa hiyari yake na kuingia kwenye mashirikiano ya kibiashara au kutoridhia. [tazama: kitabu cha Badaii Al-Sanaii, 5/172, na Mukhtasar Ikhtilaf Al-Ulamaa cha At-Tahawiy, 3/154, chapa ya Dar Al-Bashair - Beirut, na Fat-h Al-Qadir, 6/398]. Ama watu wa mtazamo wa pili wamechukua dalili zifuatazo:
Ya Kwanza: Maandiko ni yenye kukataza kufanya udanganyifu, kama Hadithi ya Abu Huraira kutoka kwa Mtume S.A.W., amesema: “Mwenye kufanya udanganyifu si katika sisi” pia Hadithi nyengine Mtume S.A.W., amekataza uuzaji wa udanganyifu Hadithi zilizopokelewa na Imamu Muslim, hakuna shaka kuwa uuzaji kwa sharti la kutohusika na kasoro hakuna tofauti na uuzaji kwa udanganyifu na ulaghai, lakini sehemu ya ulaghai na udanganyifu ni ile kasoro aliyoificha muuzaji, lakini kama hajaficha basi hakuna ulaghai wala udanganyifu ikiwa mnunuzi atagundua.
Ya Pili: Amepokea Uqba Ibn Amir kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Si halali kwa Mwislamu kuuza kitu hali ya kuwa anajua kuwa ni tatizo isipokuwa akiweka wazi” imepokelewa na Ahmad, Ibn Majah na Hakim, na kutajwa na Imamu Bukhari.
Lakini inajibiwa kuwa wajibu wa kufahamu kasoro haukataani na uwekaji sharti, kwani inawezekana kufahamu mnunuzi kasoro pamoja na kuwekwa sharti la kutohusika.
Upande wa kuhusishwa wanyama ni kuwa wanyama wanakula katika hali zote mbili, hali ya kuwa wazima na hata wakiwa wagonjwa hivyo inakuwa ni ngumu kugundua maradhi waliyonayo, kama vile hubadilika kwa uasilia wake ni mara chache kufahamu kasoro, hivyo muuzaji anahitaji kuweka sharti la kutohusika, ili kujiridhisha kuuza bila kurudishwa, lakini Imamu Shafi amehusisha kasoro zile za ndani, kwa sababu zile za nje si zenye kufichika hivyo hawezi kuweka sharti la kutohusika na kasoro hizo.
Kauli inayopewa nguvu katika masuala haya kwa upande wa fiqh ni madhehebu ya Abu Hanifa, hasa uwekaji sharti muuzaji kwa mnunuzi kunamfanya mnunuzi kujinasihi mwenyewe na kuchunguza kile anachonunua kabla ya kukubali kununua, hivyo hakuna ndani yake ulaghai wala udanganyifu, na mnunuzi ni mwenye kujiamini mwenyewe ikiwa atataka atachukua na akiwa atataka basi ataacha, lakini pamoja na hayo sheria za kiraia za Kimisri zimesimama kati na kati katika kauli mbili, imechukua rai ya kwanza kwa upande mmoja na rai ya pili kwa upande mwengine, ambapo sheria kifungu namba 447 inasema ifuatavyo:-
A- Muuzaji atawajibika kuweka dhamana ikiwa kitu kinachouzwa wakati wa kukabidhi hakitakuwa na sifa timilifu ambazo mnunuzi anahitaji ziwepo, au ikiwa kitu cha kuuzwa kina kasoro inayopunguza thamani yake au manufaa yake kwa upande wa lengo linalokusudiwa kunufaika nalo ambalo litakuwa wazi kwenye makubaliano, au lipowazi kutokana na asili ya kitu chenyewe, au lengo ambalo limewekwa, na anaweka dhamana muuzaji kutokana na kasoro hii hata kama muuzaji huyo atakuwa hajui uwepo wa hii kasoro.
B- Pamoja na hayo muuzaji haweki dhamana kwa kasoro ambayo mnunuzi alikuwa anaifahau wakati wa kununua, au alikuwa anaweza kuifahamu yeye mwenyewe kama angefanya uchunguzi yakinifu, isipokuwa ikiwa mnunuzi atathibitisha kuwa muuzaji amemhakikishia kuwa kitu kinachouzwa hakina hii kasoro, au akathibitisha kuwa muuzaji amefanya makusudi kuficha kasoro hii kwa ulaghai na udanganyifu.
Kipengele cha 453 cha sheria hiyo hiyo kinasema kuwa inafaa kwa wenye kuuziana kufanya makubaliano maalumu ikiwa ni kuzidisha muda wa dhamana au kuupunguza au kuondoa kabisa hii dhamana, kwani kila sharti linaloondoa dhamana au kupunguza muda wa dhamana linakuwa ni batili ikiwa muuzaji amekusudia kuficha kasoro ya kile kinachouzwa kwa kulaghai.
Kinachofahamika katika mada ya pili ni kuwa, inafaa kwa wenye kuuziana kukubaliana kuondoa dhamana nayo ni kutohusika na kasoro hapo baadaye, na hili ndilo linalo elekezwa kwenye rai ya kwanza, kama vile inavyofahamika katika kipengele hicho hicho kuwa, kufaa huku kuna sharti kwa kile ambacho muuzaji ikiwa atajua uwepo wa kasoro na kuificha kwa njia ya udanganyifu, hili ndilo linalofahamika kwenye mtazamo wa pili.
Kinachofahamika kwenye kipengele cha kwanza ni muuzaji kutobeba jukumu la kasoro ambazo mnunuzi anazifahamu ni sawa sawa ameziona yeye mwenyewe au kwa kufahamishwa na muuzaji, hili pia ndilo linaloelezewa kwenye kipengele cha pili, nayo ni jitihada nzuri.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia: Mtazamo wa Kisharia na kikanuni uliotolewa katika Fatwa hii ni kuwa: Inafaa kisharia mnunuzi kumhusisha muuzaji na kasoro za kitu kilichouzwa kwa sharti la muuzaji kutoficha kasoro iliyopo kwa lengo la kuleta udanganyifu kwa mnunuzi.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas