Kuhakiki Uwepo wa Ujauzito Kabla ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhakiki Uwepo wa Ujauzito Kabla ya Kumuoa Mwanamke Aliyezini Naye.

Question

Ni ipi hukumu ya kuhakiki uwepo wa ujauzito kwa mwanamke aliyezini naye kabla ya kumuoa, awe mwanamke ni Muislamu au katika watu waliopewa Kitabu, na ikiwa atasilimu mwanamke wa waliopewa Kitabu, ni ipi hukumu ya kuhakiki uwepo wa ujauzito kwake? Na je inazingatiwa kuhakiki uwepo wa ujauzito ni sharti la kusihi kwa ndoa? Na muda wake unakuwaje? 

Answer

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa Njema za Mwenyezi Mungu, na Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake, na Masahaba wake, na waliomfuata. Na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu ameharamisha uzinifu na kuufanya kuwa na adhabu kali ya jinai, lengo ni Waumini wajitenge nao na kusalimika kwa jamii zao na maovu, mabaya na athari zake zenye kubomoa maana ya ubinadamu na misingi yake bora. Mwenyezi Mungu Amesema: {Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya} [AL ISRAA, 32].
Kosa la uzinzi linazingatiwa ni katika madhambi makubwa ambayo humwangamiza mtendaji wake ikiwa hajafanya haraka kuleta toba kabla hajapitwa na muda. Mwenyezi Mungu anasema: {Na wale wasiomwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, wala hawazini – na atakaye fanya hayo atapata madhara. * Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka. * Isipokuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu} [AL FURQAAN, 68: 70].
Wanachuoni wametofautiana kwa yule aliyetekwa na shetani kisha akazini na mwanamke baadaye akajutia kitendo hiko na kuleta toba kwa Mwenyezi Mungu, kisha akataka kufunga naye ndoa huyo mwanamke ndoa ya kisharia iliyo sahihi, je katika hali hiyo anapaswa kuhakiki uwepo wa ujauzito na huyo mwanamke au hapana?
Kusudio la kuhakiki uwepo wa ujauzito hapa ni kutaka kuhakiki uwepo wa ujauzito na kizazi cha mwanamke, kwa maana kujiridhisha kuwa hana ujauzito, na hilo ni kumwacha ndani ya muda unaokadiriwa na Sharia, na kusudio la kumwacha: Ni pana zaidi ya kuacha kumuingilia au kuacha kumwoa, kwani hayo mawili yanaingia kwa sababu zinazo wajibisha kuhakiki uwepo wa ujauzito.
Amesema Sheikh Zakaria Al-Ansariy: “Kilugha ni kutaka kuhakiki uwepo wa ujauzito. Kisharia kumpa mwanamke muda kwa sababu ya umiliki - kutokea au kuondoka - ili kuhakiki uwepo wa ujauzito huwa ni ibada, na hili ndilo asili kinyume na hivyo ni lazima kujitenga kama vile kumwingilia kijakazi mwingine kwa kudhani kuwa ni kijakazi wake”. [Kitabu: Fath Al-Wahhab - Shareh Minhaj Al-Tulab, 4/467, Ch. Dar Al-Fikr].
Amesema Al-Gamal katika kitabu chake: "Mwanamke kinyume na kijakazi ni ishara kuwa - kwa maana ya kuhakiki uwepo wa ujauzito - kuna kuwa kwa mwanamke huru” hilo ni kama mfano wa kujiweka mbali mwanamke huru kwa adhabu ya uzinifu kwake.
Asili ya uhalali wa kuhakiki uwepo wa ujauzito ni Hadithi iliyopokelewa na Abu Daud, Ahmad na Hakim na kupitishwa na Ibn Hajar ndani ya kitabu cha: [Talkhis Al-Kabir 1/304, Ch. Taasisi ya Qurtubah - Misri) Hadithi inayotokana na Abu Said Al-Khudry R.A. kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Haingiliwi mwanamke mjamzito mpaka ajifungue, wala asiyekuwa mjamzito mpaka amalize hedhi”.
Vilevile Hadithi iliyopokelewa na Ahmad kutoka kwa Abu Daud Hadithi ya Ruwaifa’a Ibn Thabit Al-Ansari R.A. ambapo siku moja alikuwa akiwahutubia watu baada ya kushambulia kijiji miongoni mwa vijiji akasema: “Enyi watu, hakika si semi kwenu isipokuwa kile nilichosikia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akiwa anasema, siku ya Hunain alisimama Mtume na kusema: “Si halali kwa mtu mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kunywesheleza maji kwenye shamba la mwingine - kwa maana: Kuleta mtoto kwa mwanamke mateka - na kumpata mateka mwanamke asiyebikira mpaka amnunue”.
Na kauli yake Abu Dawud: “Si halali kwa mtu mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Kiyama kumwingilia mwanamke mateka mpaka atakapomnunua”.
Kutokana na hayo inaonesha wazi kuwa chanzo asili cha hukumu ya kuepukana na ujauzito ni kutibu kadhia ya umateka na ujakazi, na hii haimaanishi hukumu kuhusika na hayo tu, isipokuwa hukumu inazunguka pamoja na sababu yake katika hali ya kuwepo na kutokuwepo, kila upande unaofikiwa na asili ya sababu ni sawa sawa katika hukumu.
Hekima ya kuhalalishwa kuhakiki uwepo wa ujauzito huku ni kufahamu uwepo wa mimba ikiwa ni kuzuia kuchanganya kizazi, na hilo ni kwa kuwa kulinda kizazi ni moja ya makusudio makubwa ya Sharia ambayo huitwa makusudio matano ya Sharia, nayo ni: Kulinda nafsi, akili, dini, kizazi na mali.
Lakini je hekima hii inazingatiwa ni sababu kamili inayozunguka pamoja na hukumu ya kisharia kuwepo na kutokuwepo? Au yenyewe ni sehemu ya sababu? Au sababu ni kitu kingine? Au yenyewe maana yake haikubali kiakili? Haya ni sehemu ya tofauti ambayo inapelekea kuwepo kwa mitazamo tofauti na mielekeo ya kifiqhi.
Watu wa Hanbal wanaona kuwa si halali kwa mwanamume kuoa mwanamke aliyewahi kuzini naye kabla ya kuleta toba na kuhakiki uwepo wa ujauzito, kwa katazo la kuoa mwanamke mzinifu madamu tu haijaondoka kwake sifa ya uzinifu, ambapo huondoka sifa ya uzinifu kwa kuleta toba na kumaliza eda… amesema Al-Bahutiy katika kitabu cha: [Kashaf Al-Qinaa, 5/83, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya – Beirut]: “Ni haramu mwanamke mzinifu kwa mwanamume aliyezini naye ikiwa itafahamika kuzini kwake mpaka pale atakapo leta tofa na kumaliza eda yake, kwa kauli ya Mola: {Na mwanamke mzinifu haolewi ila na mwanamume mzinifu au mshirikina} [AN NUUR, 3].
Amesema Imamu Malik: Mwenye kuzini na mwanamke kisha akamwoa kabla ya kuhakiki ujauzito ndoa inafutwa, kutokana na ulazima wa kulinda maji ya ndoa yaliyo halali kuto changanyika na maji ya uzinifu yaliyo machafu, akasema Al-Hatwab katika kitabu cha: [Mawahib Al-Jalil, 3/413, Ch. Dar Al-Fikr]: “Ni sawa ikiwa amezini naye au ameziniwa na mwanamume mwingine, haifai kwake kumwoa mpaka ahakiki hali ya ujauzito unaotokana na uzinifu, ikiwa atamwoa ndani ya muda wa kujiridhisha na hali ya ujauzito itafutwa hiyo ndoa”.
Na akasema Ibn Al-Arabiy mfuasi wa Malik katika kitabu cha: [Hukumu za Qur`ani, 3/338 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya]: “Ibn Masoud anaona kuwa mwanamume pindi anapozini na mwanamke kisha akamwoa, basi watu hao wanakuwa ni wenye kuzini kipindi cha kuishi kwao”. Na akasema Ibn Abbas: “Mwanzo wake ni uchafu na mwisho wake ni ndoa”. Akasema Ibn Umar mfano wa maneno hayo, na akasema: “Hii ni kama mfano wa mtu ameiba tunda kisha akalinunua”. Imamu Malik amechukua kauli ya Ibn Masoud, akaona kuwa hawezi kumwoa mpaka ahakikishe uwepo wa ujauzito unaotokana na maji machafu. Imamu Shafiy na Abu Hanifa wanaona maji hayo hayana utukufu, anaona Imamu Malik kuwa maji yanayotokana na uzinifu hata kama hayana utukufu, lakini maji yanayotokana na ndoa yana utukufu, na katika utukufu wake ni kutomwagiwa kwenye maji machafu na kuchanganya haramu na halali, na kuchanganya maji dhalili na maji yenye nguvu na utukufu”.
Madhehebu ya Imamu Shafiy ni kuwa inafaa kuoa mwanamke mzinifu na inafaa kumuingilia pasi na kuhakiki uwepo wa mimba, ni sawa sawa kwa ule aliyezini naye au mwingine, na hii ni kutokana na kuwa maji yanayotokana na kitendo cha uzinifu hayana utukufu na wala haipaswi kuyalinda, na vilevile lau yatafungamana maji ya uzinifu na kupelekea kuwepo mtoto, basi inafaa kumwoa mwanamke huyo mwenye ujauzito unaotokana na kitendo cha uzinifu na kumwingilia.
Amesema katika kitabu cha: [Nihayat Al-Muhtaj, 7/167 Ch.Dar Al-Fikr]: “Ama asiyeingiliwa na mmiliki wake na ikiwa hajaingiliwa anaweza kuolea na mtu amtakaye, ikiwa ataingiliwa na mtu mwingine ataolewa na aliyemwingilia, na vilevile na wengine ikiwa maji si yenye utukufu, au umepita muda wa kuhakiki ujauzito”.
Amesema Al-Shabramalsiy: “Kauli yake: (ataolewa na amtakaye) kwa maana ya haraka, kauli yake: (Ikiwa maji si yenye heshima na utukufu) kwa maana yanayotokana na uzinifu”.
Na katika kitabu cha: [Mughniy Al-Muhtaj, 5/84 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya: “Inafaa kuoa na kumwingilia mwanamke mja mzito unaotokana na uzinifu ambapo hakuna utukufu wowote kwake”.
Na wamesema watu wa Abu Hanifa, inafaa kumwoa mwanamke mzinifu pasi na kuhakiki mimba, hii ni kutokana na kutokuwepo utukufu wowote kwenye maji yanayotokana na kitendo cha uzinzi, hakuna haja ya kulinda kutochanganyika na na maji mengine, lakini ikiwa mwanamke ana ujauzito unaotokana na uzinifu haifai kumwingilia pamoja na kufaa kuoa, na hii ikiwa ujauzito ni kwa sababu ya kuzini kwake na mwingine, kinyume na hivyo basi inafaa kumwingilia.
Imekuja hivyo kwenye Fatwa ya Al-Hindiya, 1/281 Ch. Dar Al-Fikr: “Ikiwa ataonekana mwanamke anazini kisha akamwoa ni halali kumwingilia kabla ya kuhakiki kwao, na akasema Muhammad: “Haipendezi kwake kumwingilia madamu haja hakiki, vile vile katika kitabu cha Hidaya”.
Amesema mwanachuoni Ibn Hammad katika kitabu cha Fath Al-Qadir, 3/241 Ch. Dar Al-Fikr: “Kauli yake: "Ikiwa ataolewa na ujauzito uliotokana na kuzini" na mwingine "Inafaa kumwoa" tofauti na kauli ya Abu Yussuf, na kauli ya Shafi ni kama kauli yetu, na kauli ya wengine ni kama kauli ya Abu Yussuf. Ama ikiwa ujauzito unatokana na uzinifu wa huyo mwanamume, basi inafaa kumwoa kwa makubaliano ya wanachuoni, kama ilivyo kwenye Fatwa ya Adhahira iliyoulizwa: “Mwanamume amemwoa mwanamke mwenye ujauzito uliotokana naye, basi ndoa ni sahihi kwa kauli ya wanachuoni wote, na inafaa kumwingilia kwa kauli ya wote”.
Amesema pia Abu Hanifa kuwa ikiwa mjakazi amezini haipaswi kwa bwana wake kumhakiki ujauzito isipokuwa ikiwa amepata mimba kutoka na uzinifu, na sababu yao katika hilo inapelekea kuondoa hukumu pia ya kuoa, imekuja kwenye kitabu cha: [Al-Mabsut kwa Sarkhasiy, 13/152, Ch. Dar Al-Maarifa]: “Ikiwa mjakazi amezini na mtu basi haipaswi kuhakiki mimba kwa kuangalia hedhi, kwa sababu hakuna utukufu kwenye maji yanayotokana na uzinifu, na Sharia imeweka hukumu ya mzinifu ni kupigwa mawe, hakuna katika uzinifu kuhakiki mimba wala eda, amesema Zafar: Ni juu yake kuhakiki ujauzito kwa kuangalia hedhi ikiwa ni kulinda maji kutochanganyika na maji mengine. Katika kitabu cha Jamii Saghir imetajwa kauli ya Muhammad amesema: “Kilicho bora kwangu ni kutomwingilia mpaka kuhakiki mimba kwa damu ya hedhi, ikiwa atakuwa na ujauzito unaotokana na uzinifu hatomkaribia mpaka ajifungue, kwa sababu ikiwa atamwingilia atakuwa anamwagilia maji yake shamba la mwingine, na amesema Mtume S.A.W.: “Mwenye kumwamini Mwenyezi Mungu na kuamini Siku ya Kiyama, basi asinywesheleze maji yake shamba la mwingine”. Sababu hizi hazileti taswira ya kuwepo tofauti katika kile ikiwa mume ndiyo aliyezini na mwanamke kabla ya kumwoa hata kama atakuwa na ujauzito unaotokana na maji ya uzinifu, kwa sababu wakati huo hatonywesheleza maji yake shamba la mwingine isipokuwa lenyewe ni shamba lake, wala hakuna zuio la kuchanganya maji ya aina mbili, asili kwenye maji ya zinaa ni kubomoa hayana mazingatio yoyote.
Ambalo linapewa nguvu kwetu katika mitazamo ya kifiqhi - na Mwenyezi Mungu Anajua zaidi - ni kauli ya kufaa kumuoa mwanamke aliyezini na mwanamume hata kama atakuwa na mimba, hata kama dhana yake ikiwa na nguvu kuwa mimba inatokana na yeye, na hili ni kwa sharti la kuleta toba na dhamira ya kuanza maisha mema ya ndoa, pamoja na hayo tunasema inapendeza kujizuia kumuingilia baada ya kufunga ndoa ili kuhakiki mfuko wake wa uzazi kutokuwa na maji machafu yanayotokana na uzinifu, na hilo ni kwa kumwacha mpaka apate damu ya hedhi - kama hukumu asili ya kumuepusha mjakazi na yule huru na adhabu ya uzinifu pamoja na kulaaniwa - na kubainika kutokuwa na mimba, na hii ni kutokana na haki ya mtoto atakayezaliwa ambapo kunaweza kuwa na hali tofauti kwa wazazi hao hao kuwa anatokana na maji halali au haramu jambo ambalo linaweza kuleta athari mbaya katika mashirikiano ya kila siku hapo baadaye, ikiwa ataachwa kisha ikabainika alama za mimba inayotokana na maji ya aliyezini naye hapo hakuna ubaya wa kuishi maisha ya ndoa, kwa sababu katazo ni kunywesheleza maji yake shamba la mwingine, na hili ni shamba lake wala sio shamba la mwingine, wala hakuzingatiwi kuhakiki ujauzito katika masuala haya kuwa ni sharti la kusimamia usahihi wa kufunga ndoa.
Na kwa mtazamo huu ambao tumeuchagua unapelekea kufikiwa makusudio mengi ya Sharia takatifu, kama kufungua mlango wa toba na kutambua makosa, na kumsitiri mkosefu ili asifedheheshwe, na kumpa fursa mpya ya kuanza maisha mazuri ya ndoa, na kumlinda mwanamke kutopotea ikiwa itapelekwa mbele ndoa mpaka pale itakapo hakikiwa hali ya ujauzito kwani huenda mwanaume akajitenga na kumwacha akihangaika peke yake na athari za dhambi na kuingia motoni kwa fedheha, vilevile miongoni mwa makusudio ya Sharia ambayo yanafikia mtazamo ulioteuliwa ni kulinda heshima ya mwanadamu asiye na dhambi yoyote ikiwa atazaliwa kutokana na uzinifu wa wazazi wake, kauli ya kufaa kuoa kunatoa fursa kuzaliwa kwake kwenye kitanda cha baba yake, na kunasibishwa na huyo baba wala hatatiwa aibu kwa kuitwa mtoto wa zinaa, huondoka adhabu na kero kwa watu wake na jamii yake na kuepukana na shari uhalifu na uharibifu kutokana na mitazamo ya watu kwake pamoja na dharau yao kwake, tofauti kati ya mambo mawili ni kama tofauti kati ya uhai na kifo, kulinda heshima ya mwanadamu ni muhimu kwenye maisha inazingatiwa kukosekana kwake ni kifo. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na mwenye kumuokoa mtu na umauti ni kama amewaokoa watu wote} [MAIDAH, 32].
Hivyo inabainika kwenye maelezo yaliyotangulia kuwa hakuna tofauti katika hukumu iliyotajwa kati ya kuwa mwanamke ambaye ameziniwa na mwanamume ni Muislamu au ni katika wanawake wa watu waliopewa Kitabu, kwa sharti la kuwa ni katika wanamke halali kwa mwanamume kuwaoa pasina kuangalia tukio la uzinifu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas