Uuwiano katika Ndoa.

Egypt's Dar Al-Ifta

Uuwiano katika Ndoa.

Question

Kijana mmoja amejitokeza kutaka kumchumbia binti yangu wala siioni kasoro yoyote kwa huyu kijana katika tabia zake na Dini, lakini elimu yake na kiwango chake cha kijamii yeye na familia yake ni cha chini kuliko viwango vyetu vya kielimu na hata kijamii, je anazingatiwa kijana huyu kuwa na Uuwiano na binti yangu? Au elimu na kiwango chake kijamii havina uhusiano na Uuwiano? 

Answer

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa Njema za Mwenyezi Mungu, na Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake, na Masahaba wake, na waliomfuata. Na baada ya hayo:
Masuala haya yana pande mbili.
Upande wa Kwanza: Ni upande wa Kifiqhi, na
Upande wa Pili: Ni upande wa kikanuni (kisheria) inayotumiwa kwenye kanuni za mambo ya ndoa.
Kwa upande wa Kifiqhi: Uuwiano katika ndoa unamaanisha usawa kati ya mume na mke kwenye mambo maalumu, wametofautiana wanachuoni wa Fiqhi katika kuainisha mambo haya, watu wa Imamu Abu Hanifa wanaona kuwa cha kuzingatiwa katika utoshelezaji ni Dini, familia, uhuru, ujuzi na mali. Rejea kitabu cha: [Radd Al-Muhtar, 3/84, Ch. Dar Al-Fikr], watu wa Imamu Shafi wao wanaona kuzingatia familia na kutokuwa na kasoro pamoja na Dini, wema na ujuzi na uhuru. Rejea kitabu cha: [Tuhfat Al-Muhtaj, 4/270 Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya], ama kwa upande wa watu wa Imamu Hanbal kumepokelewa mapokezi mawili kutoka kwa Imamu Ahmad, moja yao: Ni kama madhehebu ya Imamu Shafi - ukiondoa kipengele cha usalama wa kutokuwa na kasoro - na pokezi lengine limezingatia utoshelezo wa Dini na familia na kutofautiana na vipengele vingine. Rejea kitabu cha: [Al-Inswaf, 8/107, Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby], na wanaona watu wa Imamu Malik kuwa Uuwiano ni kufanana katika Dini na kukosekana kasoro. Kitabu cha: [Al-Sharh Al-Kabir cha Al-Dardir, 2/148 chapa ya Dar Al-Fikr].
La kuzingatiwa katika kuainisha wanafiqhi mambo ya kutosheleza ni kuwa tofauti ya Maimamu wa madhehebu kuhusu mambo ya Uuwiano na tofauti kwa Maimamu wa madhehebu moja kuhusu mambo haya ni dalili kuwa yanayozingatiwa katika Uuwiano ni yenye kutofautiana, makadirio yake yanarejea kwenye kufahamika kwake kwenye jamii kwa maana yana athirika kutoka na muda pia sehemu, kwa hiyo hayajaainishwa mambo ya kutosheleza kama vile ilivyoainishwa katika mfano ugawaji wa zaka, hivyo kumeibua tofauti kati ya wanachuoni wa Fiqhi, na kuainisha baadhi yanayozingatiwa miongoni mwa hayo chanzo chake kimekuwa ni kutokana na mazingira ya watu, kwa sababu hiyo kumekuwa na tofauti ya baadhi ya hukumu za utoshelezaji kwa kutofautiana na sehemu pamoja na wakati, na linaonesha hilo kutokana na yale yaliyonukuliwa na wanachuoni wakati wa kuzungumzia Uuwiano, katika kitabu cha: [Tuhfat Al-Muhtaj cha Sheikh Ibn Hajar Al-Haitamiy] wakati wa kuongea kwake juu ya ujuzi: “sifa ya tano ujuzi… mwenye ujuzi wa chini”. Amesema Mutwaliy: Hakuna katika ujuzi fundi seramala na mchoma mikate. Na akasema Ruyaniy: Yanazingatiwa hayo kutokana na desturi za nchi, kwani kilimo huenda kikapewa nafasi zaidi kuliko biashara ndani ya nchi fulani na kwenye nchi nyingine ikawa kinyume. Na uwazi wa maelezo ya wengine ni kuwa mazingatio katika hilo ni kutambulika kwake kwenye jamii, ambao wenye mtazamo kuwa yale yenye tamko au andiko hayazingatiwi kutambulika kwake kwenye jamii kama ilivyoelezwa. Na yale yasiyo na andiko au tamko huzingatiwa ni katika mazoea ya nchi. Je kusudio ni nchi inayofungwa ndoa au nchi ya mwanamke? Yote yanawezekana, lakini la pili lipo karibu zaidi, kwa sababu kipimo ni aibu kwa upande wake na kutokuwepo aibu kwake, hivyo hufahamika kutokana na mazoea ya watu wa nchi yake, kwa maana nchi ambayo inafanyika hiyo ndoa, na imetajwa kwenye kitabu cha: [Al-Anwar] kuhusu mambo ya ujuzi na huenda kwa kuzingatia mazoea ya nchi yake mwanamume”. [7/281 Ch. Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Amesema Al-Kasaniy katika kitabu cha: [Al-Badii]: “Hawezi kuwa masikini mwenye Uuwiano na tajiri, kwa sababu ufahari wa mali ni zaidi ya ufahari wa vitu vingine, na hasa ndani ya zama zetu” ni ishara ya kuwa amezingatia katika hukumu hii mazoea ya muda wa hukumu hii dhidi ya kufahamika muda wake.
Kisha akasema: “Ama ujuzi, ametaja Al-Karkhiy kuwa Uuwiano katika kazi na kuzalisha kunazingatiwa kwa Abi Yussuf, na imetajwa kuwa Abu Hanifa amejengea jambo hilo kutokana na mazoea ya Waraabu ya kufanya kazi hizi hawakusudii kazi fulani, hivyo hawazikosoi hizi kazi, akajibu Abu Yussuf kuhusu mazoea ya wenyeji kuwa wanachochukulia kuwa kazi hivyo wanakosoa na kutia kasoro kazi za viwango vya chini za uzalishaji, ukweli hakuna kati yao tofauti”.
Na akasema Ibn Hamam katika kitabu cha: [Fath]: “Ikiwa itathibiti kuzingatia Uuwiano, basi inawezekana kuthibiti undani wake ni kutokana na mazoea ya watu katika yale wanayoyadharau na kuyatia kasoro, na kutumia mazungumzo yenye udhaifu katika hizo kazi” [3/296, chapa ya Dar Al-Fikr]. Rejea: (Waraka wa kazi uliowasilishwa na Dkt. Marawan Muhammad Mahruos kwenye jopo la wanafiqh ya Kiislamu nchini India katika kongamano lake la kumi na tatu.
Lengo la kuzingatia Uuwiano katika vitu vilivyopita ni kufikia usawa katika mambo ya kijamii kwa lengo la kuleta utulivu wa maisha ya ndoa, na kufikiwa furaha kati ya wanandoa wawili, ambapo mwanamke hatawatia aibu au kasoro wazazi wake kwa kuelewa kwa mujibu wa mazoea, pamoja na hayo Wanachuoni wa Fiqhi wametofautiana katika kufikia lengo hili ambapo Uuwiano
Unakuwa ni sharti katika ndoa kwa rai mbili:
Ya Kwanza: Ni kuwa Uuwiano hauna uhusiano katika masharti ya ndoa, inafaa ndoa hata kama itakosekana ulingano, na hili pia ameliona Sufyan Al-Thauriy na Hassan Al-Baswariy na Hamad, pamoja na Ibn Hazm Kitabu cha: [Al-Mughniy, 7/33 na kitabu cha Al-Mahaliy, 9/151].
Ya Pili: Nayo ni maoni ya Jamhuri ya wanafiqhi: Kuwa Uuwiano ni sharti lenye kuzingatiwa katika ndoa, na haya yanaangaliwa pia na madhehebu zote nne, pamoja na kutofautiana kati yao je hilo ni sharti la kusihi au la lazima? Na tofauti kati ya ulazima na kusihi ni kuwa Uuwiano ni sharti la kulazimika kwa ndoa maana yake mwanamke pindi anapoolewa na mwanamume asiye na Uuwiano naye ndoa inakuwa ni sahihi, na wazazi wa mwanamke wana haki ya kupinga hiyo ndoa na kutaka kuvunjwa ikiwa ni kulinda madhara ya aibu kwao, isipokuwa kuondoa haki yao ya kupinga inalazimu, hata kama Uuwiano utakuwa ni sharti la kufaa kwa ndoa lakini haitafaa kiasili.
Wametoa dalili wale wasioona uwepo wa Uuwiano katika ndoa kauli ya Mola: {Hakika Waumini ni ndugu} [AL HUJURAT 10], na kauli yake Mola: {Basi oeni mnaowapenda katika wanawake} [AN NISAA 3]. Na alimwamrisha Mtume S.A.W. Fatma bint Qais, ambaye ni kutoka kabila la Quraish aolewe na Usama Ibn Zeid, naye Usama ni katika wafanya kazi wa nyumbani, anasema Ibn Hazmi: “Waislamu wote ni ndugu wala haizuiliwi kwa mtoto wa mtu asiye elimika kuoa binti wa kiongozi wa kabila la Hashim, na mtu fasiki ambaye amefikia kiwango cha juu cha kuwafanyia ufasiki Waislamu -madamu tu hajawa mzinifu- Uuwiano kwa mwanamke ni mbora wa Kiislamu, na vilevile mbora Muislamu mwanamume anatosha kwa mwanamke Muislamu ambaye ni fasiki maadamu tu hajawa mzinifu” kitabu cha: [Al-Mahaly, 9/151, Ch. Dar Al-Fikr]. Kama vile Uuwiano si jambo lenye kuzingatiwa katika mambo muhimu ya ndoa nayo ni damu, ambapo hakukuzingatiwa Uuwiano kati ya mwenye kufanya kosa la jinai na aliyefanyiwa hilo kosa katika kisasi, hivyo kutozingatiwa kwenye ndoa ni bora zaidi. Rejea kitabu cha: [Badaii Al-Sanaai, 2/317].
Jamhuri ya wanachuoni wamechukua dalili ya sharti la Uuwiano kwa ujumla katika ndoa kwa dalili zifuatazo:
1- Kauli ya Mtume S.A.W.: “Wala wasiolewe wanawake isipokuwa kwa wenye kulingana nao wala wasiozwe isipokuwa na wasimamizi” Hadithi hii imetoka kwa Darqatniy na Baihaqiy.
2- Bibi Aisha amesema: amesema Mtume S.A.W.: “Chagueni sehemu ya kuweka tone lenu la manii, na waozesheni na wenye kulingana nao, na wawaoe” imetoka kwa Ibn Maja na Hakam.
3- Kuoza msimamizi anayemsimamia na kukosekana Uuwiano wa matendo katika haki ya mwingine pasi na ruhusa yake, haikubaliki ni sawa na kumwoza pasi na ruhusa yake. kitabu cha Al-Mughniy, 10/ 388.
4- Muundo wa masilahi kawaida unakuwa kati ya wenye kulingana, na ndoa imewekwa kisharia kwa muundo wake, wala hakuna masilahi kati ya wasiolingana, kwani heshima inakataa kuwa inaongozwa na mwoga, na kusababisha kwa hilo kasoro, kwa sababu uduni wa kitanda unachukiza kuleta aibu kwake mwanamke na kwa wasimamizi wake, na kwa kuongezea katika hilo mtoto huenda akaitwa jina la baba jambo ambalo litaongeza aibu.
Dalili ya Ibn hazmi na wenzake sio katika nguvu ya dalili ya jamhuri ya wanachuoni, wala hawapingani na dalili ya jamhuri, kwani undugu wa Waumini ni thabiti kwa andiko la Qur`ani Tukufu, kinacholazimisha usawa wao ni usawa katika haki na wajibu, wala hakuna shaka kuwa usawa huu haupingani na ubora katika yale yaliyozoeleka kama ubora wa elimu riziki na kazi, wala halipingani hilo na kauli yake Mtume S.A.W, aliyoitoa katika hotuba yake ya kuaga: “Fahamuni kuwa hakuna ubora kwa Mwarabu dhidi ya asiyekuwa Mwarabu, wala asiyekuwa Mwarabu kwa Mwarabu, wala mwekundu dhidi ya mweusi, wala mweusi dhidi ya mwekundu isipokuwa kwa ucha-Mungu” imepokelewa na Ahmad. Kupishana ubora ni jambo lililothibiti katika Hadithi inayozungumzia ubora ndani ya Siku ya Mwisho. Rejea: kitabu cha: [Nail Al-Autar, 5/100, Ch. Dar Al-Hadith, Cairo].
Kama vile kutozingatiwa kwa Uuwiano katika kisasi si kipimo, kwa sababu kutozingatiwa ni kuwa kisasi kimewekwa ili kulinda haki ya msingi ya uhai ambayo watu wote wapo sawa kwenye haki hiyo, matajiri na masikini. Na kwa ajili ya hii haki vimepiganwa vita na kumwagika damu pasi na kuchunga Uuwiano kati ya muuaji na mwenye kuuliwa, na kutozingatiwa kwake kunaleta tofauti katika hili, tofauti na ndoa, kwani yenyewe imewekwa kisharia ili kudumisha maisha ya pamoja na kutengeneza familia na kutozingatia Uuwiano katika hilo kuna leta tofauti katika makusudio haya.
Hili ni kwa upande wa kifiqhi masuala ya kuzingatia Uuwiano, ama kwa upande wa kanuni hakika ya kanuni ya Kimisri haijaweka wazi katika mada zake katika masuala haya, isipokuwa kanuni imefuata madhehebu ya Jamhuri. Angalia: Encyclopedia ya Fiqhi katika hali za kanuni za ndoa ya mwanasheria Muhammad Azmiy Al-Bakri. [1/330 chapa ya Dar Mahmuod], imekuja katika waraka wa ufafanuzi kwa ajili ya marekebisho ya kanuni za ndoa namba (100) ya mwaka 1985 kuwa hukumu ya kanuni maalumu ya kanuni za ndoa ikiwa hakuna tamko lake, basi hutolewa hukumu kwa kufuata kauli yenye nguvu kutoka madhehebu ya Abu Hanifa, isiyokuwa madhehebu hiyo ni katika hukumu zinazovuliwa, nazo ni zile zinazotekelezwa katika masuala ya Uuwiano, tunafahamu kuwa ikiwa madhehebu ya Abu Hanifa -ambayo imechukuliwa kanuni kutoka madhehebu hiyo- inasema kuwa mwanamke anaweza kujioza mwenyewe pasi na msimamizi, isipokuwa yenyewe imetoa hadhari kwa wasimamizi “Yamekunjua katika mambo ambayo yanazingatiwa Uuwiano katika ndoa ili mwanamke asitumie vibaya haki hii na kuiegemeza katika kujioza mwenyewe kwa mwenye kutaka pasi ya kuipa umuhimu kwa yale yanayoizunguka hii ndoa, na yanayotokea miongoni mwa matatizo ya kijamii yasiyokwishaa mfano kawaida ya mifumo hii, kwa hili wanafiqih wa Imam Abu Hanifa wameweka tahadhari katika masuala haya na kupitisha kwa walii au msimamizi kutaka kuvunja ikiwa mwanamke atajioza mwenyewe pasi na ruhusa ya msimamizi wake pale inapokuwa ndoa haina Uuwiano kwa mwanamke, isipokuwa ikiwa itaondoka hali ya kutokuwepo Uuwiano au ikapotea baada ya kufungwa ndoa, na hili ni katika ubora wa Fiqhi ya Imamu Abu Hanifa ambayo inazuia mlango mkubwa wa mpasuko na mivutano unaoweza kujitokeza katika mifumo mingi ambayo mwanamke anachukuwa maamuzi kivyake na kwa utashi wake pasina ruhusa ya walii au msimamizi na hayo ndio tunayoyashuhudia ndani ya zama zetu hizi, hasa kile kinachoitwa (Ndoa ya Urfi kati ya vijana wa Vyuo Vikuu).
Kutokana na maelezo hayo: Walii au msimamizi ana haki ya kuivunja ndoa ikiwa mwanamke au msichana amejioza mwenyewe pasina kuwepo Uuwiano na mume pia kinyume na ruhusa ya msimamizi, kwa kukamilika masharti ya kufungwa kwa ndoa basi ndoa inakuwa ni sahihi yenye kufanya kazi na walii anakuwa hana haki ya kuvunja ndoa hata kama itafungwa kinyume na ruhusa yake - kutokana na yanayofanyiwa kazi katika kanuni za ndoa - na kupelekea hilo kuwa mchumba aliyejitokeza kwa binti wa muulizaji hazingatiwi ni mwenye Uuwiano kwake binti, ambapo hali ya kijamii na kazi ni katika nyenzo za Uuwiano unaozingatiwa katika ndoa, nazo hapa zinakuwa hazijafikiwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


 

Share this:

Related Fatwas