Mipaka ya Uso wa Mwanamke Katika Hi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mipaka ya Uso wa Mwanamke Katika Hijabu.

Question

Je, ni lazima mwanamke kufunika sehemu inayoanza chini ya kidevu hadi shingoni, kwa kuzingatia kuwa siyo sehemu ya uso, au sehemu hii ni miongoni mwa uso ambao unajuzu kufunuliwa? Tunatarajia kuibainishiwa hukumu hiyo, katika Swala na nje ya Swala. 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na Sifa Njema za Mwenyezi Mungu, na Rehema na Amani zimshukie Bwana wetu, Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake, na waliomfuata, na baada ya hayo:
Uso katika lugha ya Kiarabu ni: Mkabala wa kila kitu, na inasemwa: (Wajahtuhu) yaani nimemkabili uso kwa uso. [Al-Qamuus Al-Muhiit, na Al-Fayruz Abadiy, Uk. 1255, kidahizo; HA-WA, Ch. ya Muassasat Ar-Risalah; na Al-Misbaah Al-Muniir Fi Ghriib Ash-Sharh Al-Kabiir, na Al-Fayumiy, Uk. 649, Kidahizo; WAJAHA, Ch. ya Al-Maktabah Al-Ilmiyah].
Na mipaka ya uso katika Sharia: kwa urefu, ni mwanzo wa nywele za kichwa, yaani mahali pa kawaida kuota nywele, mpaka chini ya taya mbili, nayo ni mifupa miwili ya kuota meno ya chini, na mifupa miwili hiyo inaingia katika mipaka ya uso, na kwa upana kati ya masikio mawili; kwa sababu hii ni sehemu ya mkabala. [Taz. Hashiyat Al-Adawiy Ala Kifayat At-Talib Ar-Rabbaniy: 1/187, Ch. ya dar Al-Fikr; Sharh Al-Manhaj, na Sheikh Zacharia Al-Ansariy Bi-Hashiyat Al-Bijirmiy: 1/67-68, Ch. ya dar Al-Fikr Al-Arabiy; Sharh Al-Muntaha, na Al-Bahuutiy, mfuasi wa madhehebu ya Hanbal: 1/56, Ch. ya A’alam Al-Kutub].
Al-Kasaniy mfuasi wa madhehebu ya Hanafiy katika kitabu cha: [Badaiu’ As-Sanaii’: 1/3, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah] anasema: “Hakuitaja mipaka ya uso kwa uwazi wa mapokezi, lakini ametaja katika mapokezi yasiyo ya Mzizi kuwa ni: kuanzia sehemu ya maoteo ya nywele mpaka chini ya kidevu, na mpaka wa ndewe za masikio, na uainishaji huu ni sahihi; kwa sababu uainishaji wa kitu umechukuliwa kwa maana yake ya kilugha; kwa kuwa uso ni sehemu ya mkabala wa mtu, au mkabala katika hali ya kawaida, na hii imeletwa kwa uainishaji kama huo”. [Mwisho].
Kwa mujibu wa hayo, sehemu hii inayopakana kati ya kidevu na shingo haiingii katika mipaka ya uso si kwa njia ya kilugha au kisharia.
Na wengi wa wanazuoni miongoni mwa wafuasi wa madhehebu ya Hanafi, Malik, na Shafi wanakubaliana kuwa: Tupu ambayo lazima mwanamke kuisitiri ndani ya Swala na nje ya Swala ni mwili wake wote, isipokuwa uso wake na vitanga vyake viwili vya mikono. Na haya pia ni madhehebu ya Al-Awzai’i na Abu Thawr, miongoni mwa wenye jitihada wa Salaf, na kauli moja katika madhehebu ya Ahmad. [Taz. Tabiyin Al-Haqaaiq Sharh Kanz Ad-Daqaaiq, na Az-Zailai’iy: 1/96, Ch. ya Dar Al-Kitaab Al-Islamiy; Kifayat At-Twaalib Ar-Rabbaniy Ala Risalat Abi Zaid Al-Qairawaniy, na Ali Ibn Khalaf Al-Minuufiy; 1/313, Ch. ya Dar Al-Fikr; Nihayat Al-Muhtaaj Sharh Al-Minhaaj, na Ash-Shams Ar-Ramliy; 2/7-8, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Wafuasi wa madhehebu ya Hanbal wamesema kuwa uchi wa mwanamke huru mwenye kuvunja ungo ndani ya Swala ni mwili wake wote, isipokuwa uso wake. Na makundi ya wanazuoni walisema: Pamoja na vitanga vyake, na rai hii iliyochuguliwa na Al-Majd Ibn Taimiyah, na uso na vitanga vya mwanamke huru mwenye kuvunja ungo ni uchi nje ya Swala, kwa kuzingatia mtazamo, kama ilivyo katika mwili wake wote. [Kashful Qinaa’ A’an Matn Al-Iqnaa’, na Al-Bahuutiy: 1/266, Ch. ya dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Kuhusu miguu kuna rai mbili kwa wafuasi wa madhehebu ya Hanafi, na iliyo sahihi kuwa: Siyo uchi ndani ya Swala, lakini ni uchi nje ya Swala. [Al-Ikhtiyar Li Ta’lili Al-Mukhtaar, na Ibn Mawduud Al-Mawsiliy: 1/46, Ch. ya Al-Halabiy].
Na Abu Yusuf mfuasi wa Abu Hanifa amesema kuwa mikono siyo tupu. [Hashiyat Ash-Shalabiy Ala Tabyiin Al-Haqaiq Sharh Kanz Ad-Daqaaiq: 1/96, Ch. ya Dar Al-Kitaab Al-Islamiy]
Kufuatana na kauli ya wengi wa wanazuoni: Haijuzu kufunua sehemu iliyoulizwa, ndani na nje ya Swala, na baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Hanbal [kama iliyotajwa katika kitabu cha Al-Furuu’, na Ibn Muflih: 2/39, Ch. ya Muassasat Ar-Risalah] walisema kuwa: “Swala haibatiliki kwa kufunua sehemu chache, ambayo haizingatiwi vibaya, kwa kawaida katika kuitazama kwayo hata lau kwa makusudi, kama vile kutembea hali ya kuitekeleza swala”.
Na Al-Mardawiy mfuasi wa madhehebu ya Hanbal katika kitabu cha: [Al-Inswaaf Fi Maa’riat Ar-Rajih Min Al-Khilaaf: 1/457, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy] alitaja faida mbili muhimu: “kwanza: Kadiri ya uchache ni le inayozingatiwa hivyo kwa halia ya kawaida, kwa rai sahihi ya madhehebu. Na baadhi ya wanazuoni walisema kuwa: Kadiri ya uchache wa uchi ni kadiri ya ncha ya kidole, kama ilivyotiliwa mkazo mtungaji wa kitabu cha Al-Mubhij, na Ibn Tamiim anasema kuwa: Haina dalili, na rai ndiyo aliyoisema. Pili: Kufunua sehemu kubwa ya uchi ndani ya wakati mfupi ni sawa na kufunua sehemu ndogo ndani ya wakati mrefu, kama ilivyotangulia kuwa sahihi kwa madhehebu”. [Mwisho].
Na sehemu hiyo haizingatiwi vibaya kuitazama kwa kawaida, hakika mazoeo ya nchi zetu ni kuifunua bila ya kukanusha, kwa hivyo mwanamke aliyeswali hali ya kufunuka, basi swala yake ni sahihi, na hana dhambi; kutokana na kanuni inayosema: “Anayetatizika na kitu kama hicho, afuate aliyejuzisha hivyo, kwa kujiepusha kuingia katika haramu”. [Taz. Hashiyat Imamu Al-Baijuriy Ala Sharh Ibn Qaasim Al-Ghuzziy Ala Matn Abi Shujaa’ katika Fiqhi ya wafuasi wa madhehebu ya Shafiy: 1/41, Ch. ya Mustafa Al-Halabiy].
Na matokeo ya kanuni hii ni: “Fiqhi iliyojengeka kwa dhana na siyo kwa yakini, na inaongezeka nguvu kwa kuwa: Kusahihisha matendo ya watu ni bora zaidi kuliko kuyabatilisha, hasa katika hali ya kukubaliwa kwa kauli za baadhi ya wanazuoni, na hali ya kuwa hayakuwa mbali na mipaka ya Sharia”.
Na karibu na maelezo hayo anasema Abu Yusuf mfuasi wa madhehebu ya Hanafi kuwa: Mikono siyo uchi. Na Ibn Mawduud Al-Mawsiliy katika kitabu cha [Al-Ikhtiyaar Bi-Taa’lili Al-Mukhtaar: 1/46, Ch. ya Al-Halabiy] anasema: “kama ingefunuka mikono ya mwanamke, basi swala yake ingelikuwa sahihi, kwa sababu hiyo ni miongoni mwa urembo dhahiri, nao ni bangili, naye anahitaji kuacha wazi anapokuwa katika kazi zake, kwa mfano kupika chakula, mikate, n.k., lakini kuisitiri ni bora zaidi”. [Mwisho].
Kuhusu kuifunua nje ya swala, hii ni miongoni mwa njia za kueneza balaa zilizo enea na kuna uzito wa kuisitiri, na kanuni hapa ni: Shida hupelekea wepesi. [Al-Ashbah Wan-Nadhair, na As-Sayutiy, Uk. 7, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah], Na Mwenyezi Mungu amesema: {Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika dini}. [AL HAJJ: 78].
Na kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia: Inajuzu kwa mwanamke kufunua sehemu ambayo inaanza chini ya kidevu mpaka katika shingo yake, ndani na nje ya Swala, bila ya kupata dhambi, na ni bora zaidi na afadhali kuisitiri, kwa kujiepusha na hitilafu, lakini katika hali ya kutokuwapo uzito au tabu, basi hapo hakuna kosa, hali ya kutokuwepo fitina.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


 

Share this:

Related Fatwas