Usahaulifu wa Mgonjwa wa (Al-Zahaym...

Egypt's Dar Al-Ifta

Usahaulifu wa Mgonjwa wa (Al-Zahaymar) na Athari yake Juu ya Saumu.

Question

Ni ipi hukumu ya saumu ya mgonjwa wa “Al-Zahaymar” anajiyesahau kwa kula chakula au kunywa vinywaji na ilhali ameghafilika na kufanya hivyo mchana wa Mwezi wa Ramadhai? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu, na sala na salamu zimfikie Mtume wetu S.A.W, na Aali yake na masahaba zake na wanamofuata yeye. Ama baada ya utangulizi huu:
Ugonjwa wa “Al-Zahaymar” ni ugonjwa unaotokea katika akili, na una alama na viwango vyake, na huwa unaanza kwa kusahau na upungufu wa kumbukumbu, na huishia kwa kupotea yake yote. Na kwa hakika jambo hilo lilitajwa katika matini ya kisheria; kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni; kisha anakufisheni. Na miongoni mwenu wapo wanao rudishwa kwenye umri mbaya kabisa, hata akawa asijue kitu baada ya ujuzi alio kuwa nao. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi na Mweza}. [AN NAHL 70]
Al-Imam Fakhr Al-Diin Al-Raziy alitaja katika tafsiri yake [Mafateh Al-Ghaibu 20/239, Ch. Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy] kwamba katika aya hii ya Qurani iliyotajwa hapo juu: [Ishara juu ya viwango vya umri wa binadamu. Na wanazuoni wanasema kwamba umri wa binadamu una viwango vinne: Cha kwanza ni: umri wa mwanzo na kukua kwa binadamu. Na cha pili ni: Umri wa nguvu, yaani umri wa ujanani. Na cha tatu ni: Umri wa upungufu wa uchache, na cha nne ni: Umri wa upungufu mkubwa wa nguvu yaani umri wa uzee].
Na Al-Imam Al-Baydhawiy anabainisha katika tafsiri yake [Anwar Al-Tanzel wa Asraru Al-Taaweel 3/233, Ch. Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy], maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: {Hata akawa asijue kitu baada ya ujuzi alio kuwa nao}. Yaani: [atabadilika kutoka katika hali na kuelekea katika hali nyingine inayofanana na hali ya utotoni, tena kwa kusahau na kuwa na ubaya wa ufahamu].
Na Mtume S.A.W., alimwomba Mwenyezi Mungu amkinge na asije kurejea katika umri wa unyonge kabisa; na katika jambo hili Imamu Al-Bukhariy alisimulia katika Sahihi yake kutoka kwa Abdu-AlmalekIbn Ameer, alisema: Nilimsikia Amru Ibn Maimun Al-Udiyy akisema: Saad alikuwa akiwafundisha wanawake maneno haya ya dua ya Mtume S.A.W., kama mwalimu anayewafundisha vijana namna ya kuandika, na anasema: Kwa hakika Mtume S.A.W, alikuwa akijikinga kwa dua na mambo haya katika mwisho wa kila Sala: "Ewe Mola wangu ninajikinga kwako kutoka na khofu, na ninajikinga kwako kutokana na kurejea katika umri wa unyonge kabisa, na ninajikinga kwako kutokana na fitina ya dunia, na ninajikinga kwako kutokana na adhabu ya kaburini". Na alimzungumzia na Musaab akamsadiki.
Al-Badr Al-Ainy alisema katika maelezo ya [Sahihi ya Al-Bukhariy] [Umdat Al-Qarea 14/119, Cha: Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy]: (Umri wa unyonge kabisa), maana yake ni uzee, kwa maana: Alirejea katika umbo lake la awali, la utotoni kitoto, unyonge wa mwili wake, udhaifu, upungufu wa akili, na vile vile inasemwa: Unyonge mkubwa kabisa wa umri: ni ubaya wake, yaani hali yake ya uzeeni, na unyonge na udhaifu wa kutimiza fardhi zake, na pia kushindwa kujihudumia yeye mwenyewe, wakati ambapo atakuwa mzigo mkubwa kwa ndugu zake, mpaka wakatamani umauti umfikie. Na kama asingelikuwa na watu au ndugu, basi msiba wake ungelikuwa mkubwa sana].
Al-munawy alisema katika kitabu cha: [Faydhu Al-Qader 2/124, Cha. Al-Maktaba Al-Tugariyah Al-Kubra]); (Umri wa unyonge mkubwa): maana yake ni mwisho wa umri wa mwanadamu katika hali ya uzee, unyonge, kushidwa, udhaifu na kutoweka kwa akili, na mwisho wa kila kitu ni ubaya wake].
Maana ya hayo ni kwamba mwisho wa umri ni uzee na khofu, na tofauti kati ya khofu na uwendawazimu ni kama anavyosema Imamu Al-Subkiy kwa kunukulu kutoka kwa Imamu Al-Seyuty katika kitabu cha: [Al-Ashbah na Al-Nadhaer Ku. 212-213, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah] - kwamba uzee sana ni kuchanganyika kati ya akili na uzee, na hakuitwi uwendawazimu; kwani uwendawazimu unapatikana kwa sababu ya ugonjwa wa akili na unaweza kupona, lakini uzee ni kinyume cha hayo, na inabainika kwamba uzee ni daraja kati ya kutofahamu na uwendawazimu na maana yake ni karibu na kutofahamu zaidi.
Na fatwa sahihi na uchaguzi hapa ni kwamba anayekula au kunywa katika mchana wa Ramadhani na hali ya kuwa amesahau, basi saumu yake ni sahihi na hataifunga siku hii kwa sababu ya kula kwa kusahau; na hii ni kutokana na Hadithi iliyosimuliwa katika Sahihi mbili kutoka kwa Abu-Huraira R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W, alisema: "Pindi mtu aliyefunga akisahau na akala na akanywa, basi atimize saumu yake kwani hakika Mwenyezi Mungu amemlisha na akamnywesha".
Na katika riwaya nyingine uliyopo katika Al-Bukhary kutoka kwa Abu-Huraira R.A., kwamba Mtume S.A.W., alisema: "Mtu yoyote aliyefunga akasahau na akala na kunywa, basi akamilishe saumu yake, kwani hakika Mwenyezi Mungu amemlisha na amemnywesha". Na Ibn Khuzaymah na Ibn Habban walisema katika Sahihi zao mbili na Al-Dar Qatwniy katika Sunanu zake kutoka kwa Abu Hurairah, kutoka kwa Mtume S.A.W., alisema: "Anayekula ndani ya mwezi wa Ramadhani akiwa amesahau, basi haifunga siku hii kwa kuilipia kwa kusahau na haina kafara". Na Al-Imam Al-Nawawiy alisema katika kitabu cha: [Al-Majmuu 6/324, Ch. Dar Al-Fekr] kutoka kwa musnadi ya hadithi hii: [Sahihi na Hasan].
Na hii ni kauli ya jamhuri ya wanazuoni wa fiqhi kutoka kwa Hanafiah na Shafiiyah na Hanabilah, na katika matini ya kitabu cha: [Al-Kanziy] na maelezo yake kwa Zaylaey kutoka katika vitabu vya Al-Hanafiyah [Tabyeen Al-Haqaeq katika sharh Kanz Al-Hdaqaeq 1/223, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy]: (Mfungaji akila au akanywa au akilala na mke na hali ya kuwa amesahau atakuwa hakufuturu). Na kauli hii ya akila au akanywa au akilala na mke wake, hali ya kuwa amesahau; inaafikiana na kauli ya Abu hurairah kutoka katika kauli ya Mtume S.A.W.: "Mfungaji mwenye kusahau akila na akanywa basi atimize saumu yake kwani hakika Mwenyezi Mungu amemlisha na akamnywesha"; na kwa sababu ya usahaulifu ni alama ya wanadamu wengi, na kama mfungaji akifuturu kwa sababu hali ya hewa ya joto kali na akiwa amejisahau basi atimize saumu yake. Na hii ni kwa mujibu wa Hadithi ya Mtume S.A.W, - kama tulivyoitaja hapo juu -: "Mfungaji anayesahau akila na akanywa basi atimize saumu yake kwani hakika Mwenyezi Mungu amemlisha na akamnywesha na hakuna haja tena ya ya kuilipa siku hii". Imesimuliwa na Al-Dar Qatny, na alisema katika Kitabu chake cha: [Musnadi kuwa Hadithi hiyo ni sahihi na wasimulizi wote ni wakweli].
Na jambo hilo lilitajwa pia katika kitabu cha “Mughny Al-Muhtaj” kwa mwanazuoni [Al-Khateeb Al-Sherbiny (2/158, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah), na hiki ni miongoni mwa vitabu vya Wafuasi wa Madhehebu ya Shafi. Na pia katika kitabu cha: [Kashaaf Al-Qenaa” cha mwanazuoni Al-Bahuti Al-Hanbaly 92/320, Ch. Dar Al-Fekr], na wote wameafikiana juu ya jambo moja tu kutokana na Hadithi ya Mtume S.A.W., ya kuwa: anayesahau akala na akanywa basi atimize saumu yake kwani hakika Mwenyezi Mungu amemlisha na akamnywesha na hakuna haja ya kuilipa siku hiyo.
Na dalili ya wanazuoni ya kisheria hapa ni kuwa, mwanasheria hakubatilisha saumu ya mtu mzima alipokula na kunywa wakati wa kusahau, kwa hivyo tunaweza kusema kwamba hukumu ya mgonjwa wa “Al-Zahaymar” ni sawa na ya mfungaji mwenyekusahau, na pia hakuna haja ya kuilipa siku siku hiyo, hata kama akiwa mgonjwa wa “Al-Zahaymar” ni hali yenye sura ya nadra katika jamii, [Nashr Al-Bunuud cha Bwana Abdullahi Ibn Al-Haj Al-Alawiy Al-Malikiy 1/208, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]; kwani sura ya nadra inaweza kuingia katika mambo ya kiujumla, na rai hii pia ilichaguliwa na Ibn Al-Subkiy katika kitabu cha “Jaami Al-Jawamii” (pamoja na maelezo ya kitabu cha: [Sharhi Al-Muhala na Hashiyat Al-Attar, 1/507, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Kutokana na maelezo hayo yote ya hapo juu kuhusu usahaulifu wa mgonjwa wa “Al-Zahaymar”, tunaweza kusema kwamba: Mgonjwa wa “Al-Zahaymar”, akila au akanywa, mchana wa Ramadhani katika hali ya kuwa anasahau, basi atimize saumu yake, na saumu yake hiyo ni sahihi, na wala halazimiki kuilipa siku hiyo na pia hakuna kafara yoyote juu yake,
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas