Kupiga Chuku (Hijama).

Egypt's Dar Al-Ifta

Kupiga Chuku (Hijama).

Question

Siku hizi watu wengi wanazungumzia – hasa madaktari – kupiga chuku (Hijama), baadhi yao wanaunga mkono na wengine wao wanapinga, ingawa kupiga chuku kunatambuliwa na baadhi ya Vyuo Vikuu nchini Marekani na baadhi ya nchi zilizoendelea, lakini pia wapo wale wanaoyashuku matokeo ya tiba hii. 

Answer

Kupiga chuku (Hijama) ni miongoni mwa njia za matibabu ziliyopitishwa na Sheria na ziliyotokea katika enzi ya Mtume S.A.W., na yeye hakulikana jambo hili, lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., mwenyewe alipigwa chuku, nayo ni aina ya matibabu yaliyokuwa yakifanyika hadi hivi karibuni. Ofisi ya Kutoa Fatwa inashauri kuwaelekea madaktari waaminifu ili kupata ushauri wao na kuuzingatia kwa kiwango cha usawa na kupiga chuku kama ni aina ya matibabu kwa ugonjwa unaolalamikiwa na mgonjwa, na ikiwa dawa hii itamsaidia au la.
Vile vile Ofisi ya Kutoa Fatwa inashauri kwamba madaktari hao wawe bobezi katika kupiga chuku na wasiwaachie jukumu hilo wengine ili kuzuia matatizo yasitokee kutokana na uchafuzi na kutozingatia kuchemsha na kuvitwaharisha vifaa kwa njia inayotakiwa.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, katika hali halisi ya swali hilo: Hakika kupiga chuku ni aina ya matibabu ambayo ni halali na dawa hii imethibitishwa kwa mujibu wa yaliyotajwa katika Hadithi sahihi za Mtume S.A.W., na haizui kuwa aina hii ya matibabu ni halali na ni maendeleo ambayo yametokea katika sayansi ya matibabu, kwa sharti kuwa anayetibu kwa kutumia aina hii ya matibabu ni lazima awe daktari mwenye ujuzi na bobezi katika nyanja hii na anaruhusiwa kufanya hivyo na idara ya huduma za matibabu inayotambuliwa na wenye mamlaka.
Kama mganga hakufuata njia za kisharia na sheria za kisasa zinazopanga aina hii ya matibabu ni haki ya mamlaka husika kuingilia kati na kuwadhibiti wanaofanya kazi ya kupiga chuku, kwa ajili ya kuhifadhi afya za wananchi, iwe nchi zao ni za Kiislamu au zisizo za Kiislamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas