Mke Kuwa Mjamzito Pamoja na Kutokuw...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mke Kuwa Mjamzito Pamoja na Kutokuwepo Uwezekano wa Kupewa Mimba Hiyo na Mume Wake.

Question

Je! Mke ataadhibiwa anapobeba ujamzito kama haukuwepo uwezekano wa kuupata ujauzito huo, kama vile aliyeolewa na mvulana au mume aliyekatwa uume wake? 

Answer

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu, na rehema na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu na Jamaa zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya utangulizi huu:
Mke aliyeolewa kama atakuwa mjamzito na uwezekano wa kuupata ujauzito huo haukuwapo kwa kuolewa na mvulana asiyebaleghe au na aliyekatwa uume wake, au mumewe hakuwepo kwa muda mrefu, je, kuwepo kwa ujauzito huo ni sababu ya kuadhibiwa kwake, au kwamba suala hili linaingia ndani ya msingi unaosema kuwa adhabu zinaondoshwa katika mambo yenye shaka?
Suala hili linaweza kutokea bila ya mke kufanya uzinzi; pengine kutokea kwa kulazimishwa au kwa usingizi mzito au tendo la ngono la shaka, au kufikiwa na manii ya mtu kupitia njia ya maji ya kuoga, na kadhalika. Suala hili limetajwa na wanavyuoni katika vitabu vyao, nao walisema hivyo na baadhi ya aina mbalimbali za suala hili, kwa hali inayomwezesha mwanachuoni wa Faqih kupima hali za sasa juu ya suala hilo.
Hukumu katika suala hili ni kwamba: Ikiwa hakuna uwezekano wa kupewa ujauzito huo na mume wake, basi haadhibiwi kama atadai kuwa kuna shaka shaka. Na vile vile wanavyuoni wameitaja hukumu hiyo hiyo kwa mwanmke aliye bikira.
Miongoni mwa dalili za suala hili iliyopokelewa kutoka kwa Bi. Aisha R.A, kutoka kwa Mtume S.A.W.,: "Waondosheeni adhabu Waislamu kadiri mnavyoweza, kama mkipata njia yoyote kwa Muislamu basi mwacheni huru, kwa sababu Imamu anapokosea katika msamaha ni bora zaidi kuliko kukosea katika adhabu". Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhi na wengine na Hadithi hii ina ushahidi.
Al-Manaawi anasema: "(waondosheeni) (adhabu) ni wingi wa adhabu, nazo ni aina ya mateso maalumu anayopewa mtu kwa kufanya kosa (kwa Waislamu) (kadiri mnavyoweza) yaani muda wowote wa uwezo wenu kama mtapata njia yoyote ya halali, (kama mkipata njia kwa Muislamu basi mwacheni huru) yaani msimwadhibu hata kama shaka itakuwa na nguvu zaidi na ikitawala dhana kwa dai liliodaiwa kuwa akilala na mwanamke asiye Halali kwake (Hakika Imam) yaani mwenye mamlaka (kama atakosea) kosa lolote (msamaha ni bora zaidi kuliko kukosea adhabu), yaani kosa lake katika msamaha ni bora zaidi kuliko kosa lake katika adhabu. Na usemi huu ni kwa ajili ya wenye mamlaka na manaibu wao, ambapo adhabu zinaondoshwa kwa mambo yenye shaka kama Shaka hiyo ikiwa kwa mtendaji kama vile aliyejamiiana na mwanamke akidhani kuwa ni halali kwake. [At-Taysiir Bisharhil Jamii As-Saghiir 1/53, I. Maktaba ya Imam Shafiy – Riyad].
Wanavyuoni wanasema kuwa kama Mwanamke bikira atakuwa mjamzito na kukawepo shaka yoyote basi haadhibiwi, inajulikana kwamba mwanamke aliyeolewa ni sawa Mwanamke huyo awe bikira kihukumu, bali hukumu hii inahusiana na mwanamke aliyeolewa zaidi kuliko bikira; kwa sababu adhabu yake ni kupigwa kwa mawe. Vile vile maneno ya wanavyuoni katika sehemu hii ni ya kiujumla, kwa hivyo suala letu hili linaingia katika hali hii, na anayekwenda tofauti analazimishwa kutoa dalili yake.
Ibn Qudaamah alisema: “Kama mwanamke akiwa mjamzito na hana mume wala hana bwana basi haadhibiwi, na anaulizwa, kama akidai kuwa alilazimishwa, au alijamiiana kwa tuhuma, au hakutambua uzinzi, basi haadhibiwi. Haya ni maoni ya Abu Hanifa na Shafi. Imamu Malik anasema: anaadhibiwa kama akiwa mwenyeji si mgeni, isipokuwa kama dalili za kutumia nguvu zitadhihirika, na alikuwa mwenye kuomba msaada au mwenye kulia. Kwa mujibu wa kauli ya Omar R.A.: kupigwa kwa mawe ni wajibu juu ya kila aliyezini miongoni mwa wanaume na wanawake kama akiwa ameoa au ameolewa, kama ikiwepo dalili, au ilikuwepo kwa kukiri. Imepokelewa kutoka kwa Othman alijiwa na mwanamke ambaye alijifungua kiasi cha miezi sita, Othman R.A. aliamuru kupigwa mawe, Ali R.A. akasema: Huna njia juu yake, Mwenyezi Mungu anasema: {Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini.}. Hii inaonesha kuwa walikuwa wakipigwa kwa mawe kwa mujibu wa hali zao, na imepokelewa kutoka kwa Omar kwa tamko lile lile la Hadithi, na imepokelewa kutoka kwa Ali R.A. kuwa akasema: Enyi watu hakika uzinzi ni wa aina mbili: uzinzi wa siri na uzinzi hadharani. Uzinzi wa siri ni ule unaoshuhudiwa na mashahidi, na mashahidi hao ndio wa kwanza kumpiga kwa mawe mzinifu, na uzinzi wa hadharani ni kwa kukiri mzinifu yeye mwenyewe, hivyo mwenye mamlaka ni wa kwanza wa kumpiga mzinizi kwa mawe, na haya ni maoni ya Masahaba R.A., na hakukuwepo mpinzani wao katika zama zao, kwa hivyo maoni haya ni kwa makubaliano. Kwetu sisi ni kuwa kuna uwezekano kwamba ni kutokana na kujamiiana kwa nguvu au shaka, na adhabu zinaondoshwa katika mazingira tatanishi. Inasemekana kwamba mwanamke anaweza kuwa mjamzito pasipo na kujamiiana ikiwa manii ya mtu yatakuwa yameingia ndani ya uke wake ama kwa kufanya kitendo hicho cha kuingiza manii mwenyewe au kafanyiwa na mwingine. Kwa hivyo, hali ile ile kwa ujauzito wa bikira. Kuhusu maoni ya Maswahaba: Hadithi zimetofautiana nao, Imepokelewa kutoka kwa Said: Tumeambiwa na Khalaf Ibn Khalifa, kwamba Hashim alituambia kuwa, mwanamke aliletwa kwa Omar ibn Al-Khattab, akiwa hana mume, na ni mjamzito, aliulizwa na Omar kuhusu ujauzito huo, akasema: Mimi ni mwanamke ambaye ninaposhikwa na usingizi wa fofofo huwa sihisi chochote, mtu mmoja aliniingilia nilipokuwa katika usingizi mzito, sikuamka isipokuwa baada ya yeye kumaliza, Basi Omar akamwoondolea adhabu. Imepokelewa Hadithi hii kutoka kwa Al-Baraa ibn Sabra kutoka kwa Omar kuwa mwanamke mjamzito alipelekwa kwake na akadai kwamba alilazimishwa kuzini kwa nguvu. Omar akasema mwacheni huru; na akaandika kwa wakuu wa majeshi, kwamba haruhisiwi yoyote kumwua mtu yeyote ila kwa idhini yake tu. Imepokelewa kutoka kwa Ali na Ibn Abbas, Kwamba walisema kuwa: Kama yakiwepo katika adhabu maneno kama labda au pengine, basi adhabu hii inaondoshwa. Imepokelewa kutoka kwa Ad-Daraqutni kutoka kwa Abdullah Ibn Masuud na Muadh Ibn Jabal na Oqbah Bin Amer, walisema: Adhabu inapotolewa katika Mazingira tatanishi inaondoshwa kadiri inavyoweza. Hakuna shaka yoyote kwamba adhabu inaondoshwa kwa mazingira tatanishi, ambayo ni hali inayotokea hapa”. [Al-Mughni kwa Ibn Qudaamah 9/79, Maktabat Al-Kahira].
Al-Bajayrami anasema: “Uzinizi hauthibitishwi kwa kiapo (kinachoombwa kutoka kwa mdai) wala kwa ujauzito wa mwanamke ambaye hana mume, hali ambayo ni kinyume na mtazamo wa Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Malik. Ash-Sha'rani anasema katika kitabu cha Al-Mizan: Kama mwanamke aliye huru atakuwa na ujauzito wakati ambapo hana mume pia kijakazi ambaye mume wake hajulikani na anasema kuwa: amelazimishwa, au amejamiiana katika mazingira tatanishi, basi haadhibiwi kama walivyosema Abu Hanifa, As-Shafiy na Ahmad katika mapokezi yao. Imamu Malik anasema: mwanamke huyo anaadhibiwa kama atakuwa mwenyeji na sio mgeni, Haikubaliki kauli yake kuhusu suala la utatanishi na uzinzi, isipokuwa ikiwepo athari ya hali hiyo, kama akija akiomba msaada nk. Hali ambayo inaonesha ukweli wa kauli yake, na mtazamo mwingine unategemea kuwa hakuna uthibitisho wa ukweli wa kauli yake, hali ambayo inalazimisha kuadhibiwa kwa sababu inawezekana akijamiiana katika hali ya usingizi wake au katika hali ya kuzirai kwake akawa mjamzito kutokana na hivyo. (Hashiyatul Bajirmi ala Al-Khatib 4/175, Dar Al-Fikr).
Sheikh Ad-Dardeer anasema katika kitabu cha “Ash-Sharhul Saghiir”: “Uzinzi (unathibitika) (kwa kukiri) hata kwa mara moja (kama mtu hakujirudi) kwa kukiri kwake ... (na kwa ushahidi) wa haki wa watu wanne ... (au kwa ujauzito): yaani uzinzi unathibitika pia kwa kuibuka kwa ujauzito wa Mwanamke (asiye na mume) ambaye mtoto ataunganishwa naye, kwa hiyo mwanamke akiwa hana mume au ameolewa na mvulana au na aliyekatwa uume wake au akazaa mimba kwa miezi sita baada ya kuolewa kwake tu. (na) hana (bwana anayekiri) kwa kujamiiana naye, bali alikanusha yaliyotokea, hali hii ni kinyume na mwanamke aliyeolewa na mume ambaye mimba atamuunganisha au na bwana aliyekiri kwa kujamiiana naye. (Wito wake Haukubaliki) yaani wito wa mjamzito (aliyelazimishwa kujamiiana kwa nguvu basipo na dalili) inayoonesha ukweli wa kauli yake lakini anaadhibiwa, kinyume na anahusika na mshtakiwa, na kuomba msaada katika hali ya shida basi haadhibiwi.”
Imamu Swaawi amelieleza suala hili akasema: “Kwa kauli yake: (Madai yake hayakubaliki): yaani madai yake kuwa ujauzito huu ni kutokana na manii yaliyoingia ndani ya uke wake bila ya kujamiiana, lakini madai yake kuwa kujaniiana kwa shaka au kimakosa katika hali kuwa kwake usingizini, basi madai haya yanakubalika; kwa sababu mambo haya huwa yanatokea mara nyingi mno.” (Haashiyatul Sawi ala Ash-Sharul Saghiir 4/454, Dar Al-Maarif).
Ndani ya Maneno haya kuna maelezo ya asili ya suala hilo, kama inavyoeleweka kutokana na maneno yaliyotangulia kwamba Wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Malik hawaadhibu kabisa katika hali hii, kwa mujibu wa Mapokezi yao kwa makubaliano, lakini wana mitazamo tofauti katika suala hili kama ilivyotangulia, pengine walizuia kuondoa adhabu kutokana na mambo yenye shaka katika baadhi ya hali kwa ajili ya kuondoa kisingizio, na wakaruhusu kulingana na msingi wa kuondoa adhabu kutokana na mambo yenye shaka.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia: Kama mwanamke akiwa mjamzito naye ameolewa na mvulana au na mwanamume aliyekatwa uume wake au haukuwepo uwezekano wa kupata ujauzito kutokana na mume huyo, hairuhusiwi kuadhibiwi kwa sababu ya shaka iliyotokea.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
 

Share this:

Related Fatwas