Kuwatumia wasio Waislamu katika vit...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwatumia wasio Waislamu katika vita.

Question

  Je, inaruhusiwa kuwatumia wasio Waislamu katika vita?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu ameumba wema na uovu, na kila kimoja kati ya viwili hivi kina watu na wafuasi wanaojaribu kukitangaza. Watu wema wanapaswa wajiepushe na uovu huo, au la si hivyo utaenea kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: {Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawapambanishi watu kwa watu basi dunia ingeli haribika.} [AL BAQARAH: 251 ]. Yeye anautoa uovu kutoka duniani na kila kitu ndani yake, lakini kwa mikono ya waja wake, kama alivyosema: {Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini} [AT TAWBAH: 14]. Hii ni miongoni mwa sababu za kutunga sheria ya jihadi. Tangu zama zlizopita mtu alijua vita, na wala Uislamu haukuanzisha, na pengine upo uovu, Waislamu na wengine wanakubaliana kujiepusha, na pengine jambo hilo ni maslahi kwa baadhi yao au kwa sababu iliyo ya siri au ya wazi.
Inawezekana kwa Waislamu kusaidiwa na wengine katika vita kwa ajili ya uchache wa Waislamu, ikiwemo katika idadi au silaha au vinginevyo.
Hali hii wanavyuoni wameizungumzia katika zama za kale, ambapo imegawanywa katika kuwatumia wao katika kupambana na wasiokuwa Waislamu, na katika kupambana na madhalimu miongoni mwa Waislamu.
Mtazamo sahihi zaidi katika jambo hili ni kuruhusiwa kwa hali ya kwanza, nayo ni kusaidiwa nao katika kupambana na wasiokuwa Waislamu ikiwa utakuwepo uhakika wa kusalimika na usaliti wao. Ama kuhusu kusaidiwa nao katika kupambana na madhalimu miongoni mwa Waislamu; basi asili ya suala hilo ni kutoruhusiwa isipokuwa katika hali ya uwepo wa dharura kwa sharti lililotangulia hapo juu.
Ushahidi wa hilo ni kwamba kama ikiwa vita hiyo inaruhusiwa, basi hukumu ya vyombo vyake ni kama hukumu ya malengo yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na saidianeni katika wema na uchamngu} [AL MAIDAH :2], na hali hiyo kwa ujumla, inagusia kusaidiana kwa Waislamu na wengine katika nyanja zote, hufanyika hivyo ikiwa si dhambi wala uadui .
Zimepokelewa Hadithi kutoka kwa Mtume S.A.W., zinazoruhusu hivyo, na imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W., kwamba wasio Waislamu wanaoabudu masanamu, na watu wa kitabu walishirikiana na Mtume, S.A.W., katika vita, na Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah R.A.: "Hakika Mwenyezi Mungu anaiimarisha dini kwa mtu mwovu". [Maimamu wawili Al-Bukhari na Muslim Wamekubaliana na Hadithi hiyo].
Kauli Hiyo ni ya kiujumla nayo ni pamoja na Muislamu na wengine, nayo inachukua nguvu kupitia Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa An-Nasaaiy katika Sunani yake kutoka kwa Anas amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu anaiimarisha dini hii kwa taifa la watu amabo hawatakuwa na sehemu ya kheri yoyote katika akhera".
Al-Haythami alisema katika mlango huo Hadithi kadhaa, miongoni mwao ni: imepokelewa kutoka kwa Omar Ibn Al-Khatwab alisema: nilisikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., anasema: "Mwenyezi Mungu ataipa nguvu dini hii kwa Manasara kutoka ukoo wa Rabia juu ya ufukwe wa mto wa Al-Frati". [Imepokelewa kutoka kwa Al-Bazzar na watu wake ni watu wa As-Sahih isipokuwa Abdullah Ibn Omar Al-Qurashiy, naye ni mwaminifu kujiamini. Rejea: Mujamaa Az-Zawaid 5/302, Ch. Maktabat Al-Qudsiy].
Na imepokelewa kutoka kwa Ibn Shihab akisema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. amevamia vita ya Al-Fathu, Fathu Makkah, na kisha akatoka nje pamoja na Waislamu waliokuwa naye, wakapigana katika eneo la Hunain, basi Mwenyezi Mungu ameinusuru dini yake na Waislamu na siku hiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alimpa Swafwan Ibn Umaiya ng’ombe mia moja kisha mia moja nyingine". Ibn Shihab alisema: Saeid Bin Al-Musayyib ameniambia kwamba Swafwan alisema: Haki ya Mungu! (Wallahi!) Mtume wa Mwenyezi Mungu amenipa aliyonipa, nikawa ninamchukia sana kuliko watu wote, kisha akaendelea kunipa mpaka nikawa ninampenda zaidi kuliko watu wote. [Hadithi hii Imepokelewa na Imam Muslim]. Basi Swafwan alitoka katika vita akiwa ni mshirikina na hakuingia katika Uislamu mpaka baada ya vita. Na hii inaonesha kuwa kumtumia kulichelewa kiwakati.
Na Abu Dawud kwa Al-Zahriy, kwamba Mtume, S.A.W. alisadiwa na watu miongoni mwa Wayahudi katika vita, akawapa sehemu kutoka nyara. [Al-Marasiil 1/224, Ch. Muassasit Al-Risala].
Imepokelewa kutoka kwa Ibn Abi Shaybah: Tuliambiwa na Hafs Ibn Ghiath kutoka kwa Ibn Juraij kwa Az-Zohariy kwamba: "Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., alivamia vita pamoja na Wayahudi, akawapa sehemu kutoka katika nyara.". Tuliambiwa na Wakii akasema: imepokelewa kutoka kwa Ametusimulia Sufian kutoka kwa Ibn Juraij kutoka kwa Az-Zohari kwamba: "Mtume S.A.W. alikuwa akivamia pamoja na Wayahudi, akawapa sehemu kutoka katika nyara kama sehemu ya Waislamu". Tuliambiwa na Wakii alisema: Ametusimulia Al-Hassan bin Salehe kutoka kwa Al-Shaibani alisema: kwamba Saad bin Malik alipigana vita pamoja na watu miongoni mwa Wayahudi akashindwa kwao. Tuliambiwa na Wakii akisema: Ametusimulia Sufian kutoka kwa Jaber alisema: nimemwuliza Amer kuhusu Waislamu wanaovamia vita pamoja na watu wa Dhima wakawatoa wao sehemu kutoka nyara, na hawachukui kodi kutoka wao, basi ni Sunna nzuri kwao. Tuliambiwa na Wakii alisema: Ametusimulia Israeli kwa Jaber kwa Amer alisema: Niliwahi maimamu, na kisha alisema kama hivyo. Tuliambiwa na Abdul Rahim bin Suleiman kwa Al-Hajjaj, alisema: Niliambiwa na aliyemsikia Al-Qasim akitaja kuhusu Salman Bin Rabia Al-Baahili: kwamba alivamia vita Balenjar na alisaidiwa na watu miongoni mwa washirikina dhidi ya washirikina na akasema: maadui wa Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya maadui wa Mwenyezi Mungu. [Kitabu cha Ibn Abi Shaybah 6/488, Ch. Maktabat Al-Rushd].
Imepokelewa kutoka kwa Abdul Razzaq kutoka kwa ibn Juraij alisema: nikasikia Ibn Shihab alisema: "Wayahudi walikuwa wakivamia pamoja na Mtume, S.A.W. akawapa sehemu kutoka katika nyara kama sehemu ya Waislamu". Imepokelewa kutoka kwa At-Thawriy akasema: Yazid Bin Yazid Bin Jaber ameniambia, kutoka kwa Al-Aahriy, kutoka kwa Al-Thawriy, kutoka kwa Jabir, kutoka kwa As-Shabiy alisema: Nilimwuliza kuhusu makafiri wanaovamia pamoja na Waislamu watachukua nini? Akasema watachukua waliyoafikiana nayo. [Kitabu cha Abdul Razzaq 5/188, Ch. Baraza la Kielimu - India].
Ibn Hazm alisema: "Tuliisimulia kupitia Wakii, na Sufian At-Thawriy kutoka kwa ibn Juraij, kutoka kwa Az-Zahriy kwamba "Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. alikuwa akivamia kwa usaidizi wa Wayahudi na alikuwa akiwapa kwao sehemu kama alivyowapa Waislamu). Tuliisimulia kutoka kwa Az-Zahriy kupitia njia zote zilizo sahihi, kupitia Wakii, Al-Hasan bin Hai kutoka kwa As-Shaibani ambaye ni Abu Ishaq kwamba Saad bin Malik naye ni ibn Abi Waqas alipigana vita kwa usaidizi wa watu miongoni mwa Wayahudi akashindwa. Na kwa njia ya Wakii, Sufian kutoka kwa Jaber alisema: Nilimwuliza As-Shabiy kuhusu Waislamu wanaovamia kwa usaidizi wa watu miongoni mwa wa watu kitabu, As-Shabiy akasema: niliwawahi maimamu wajuzi wa Fiqhi na wasio wajuzi wa Fiqhi wakipigana vita kwa usaidizi wa watu wa Dhima na wanawapatia sehemu ya ngawira walioipata, na hawachukui chochote katika kodi. Al-Shabiy alizaliwa siku moja na Ali, akawawahi Masahaba waliokuwa baada yake R.A. Nayo ni kauli ya Al-Awzaaiy na Sufian At-Thawriy. Kwamba anawapa ngawira washirikina walioshiriki vita kama anavyowapa waislamu". [Al-Muhala 5/398, Ch. Dar Al-Fikr].
Na kufuatana na tuliyoyasema wengi wa wanavyuoni wameyafuata, wanavyuoni wa madhehebu ya Ashafiy na Al-Hanbali wamesema kwamba Imamu Hassan analazimika kujua maoni yao kuhusu Waislamu, na kuamini uhaini wao, wanavyuoni wa madhehebu ya Shafiy wakasema kwamba ni jambo la lazima Waislamu wawe wengi ili iwapo wasaidizi wakifanya uhaini na wakajiunga na wale ambao wanawapiga vita waislamu, waweze wote kupambana nao, na Al-Mawardi ameweka sharti la kwenda kinyume na itikadi ya adui.
Ibn Al-Humam alisema: "Je, inawezekana kusaidiwa na kafiri? Kwetu: kama ina haja, basi inawezikana, na huu ni mtazamo wa Imam Shafi. Anasema Imamu Shafi: kuwajibu kwake Mtume S.A.W, washirikina kulikuwa katika vita ya Badr, kisha yeye S.A.W. walisaidiwa na Mayahudi wa Bani Qainuqaa katika vita ya Khaibar, na alisaidiwa na Watu wa Swafwan Ibn Umaiah amabye aliyekuwa miongoni mwa washirikina katika miaka nane, katika vita ya Hunain, kujibu kulikuwa kama akiwa na hiari ya kwamba anaweza kusaidiwa naye au la kama alivyofanya na Mwislamu, basi hakuna upinzani kati ya Hadithi hizo mbili, na kama akiwa ni mshirikina, basi akafutwa kwa hali yake ya baadaye, na hakuna kitu kibaya, kwamba kusaidiwa na washirikina kupambana washirikina kama wakitoka nje kwa hiari na kushindwa kwao na hawakuchangia na hawakuwa na bendera yao wenyewe, haikuthibitishwa kwamba Mtume, S.A.W. aliwapa sehemu ya ngawira iliyopatikana vitani, na labda majibu yake katika vita ya Badri ni kwa ajili ya kuwa na matumaini ya kuingia katika Uislamu. "[Sharhu Fahul Qadir ala Al-Hidaya 5/242 Ch. Ihyaa Al-Turath].
Khatib Al-Sherbini alisema: "(Ana-yaani Al-Imam- asaidiwe) juu ya makafiri (kwa kafiri) miongoni mwa watu wa Dhima na wengine, lakini inaruhusiwa kusaidiwa nao katika hali mbili: moja yao ni aliyoyataja kuwa (Kuamini usaliti wao) alisema katika kitabu cha: [Al-Rawdha]: Kwamba kujua maoni yao mazuri kuhusu Waislamu. Ar-Rafii alifanya kujua maoni yao mazuri na kusalimika na uhaini wao ni sharti moja. Na ya pili yao ni kile alichokisema kwamba: (na wawe kama walioungana nao majeshi ya makafiri, tupambane nao) yaani kama wao walijiunga na kikosi kingine basi kuna uwezekano kuwashinikiza, na kama wakiongezeka kwa mara mbili haikuruhusiwa kusaidiwa nao, na sharti ya wanavyuoni wa Iraq ni uchache wa Waislamu, Ar-Rafiy alisema: sharti hiyo na iliyo kabla yake, ambayo ni kuwapambana na bendi ni kama zinapingana, kwa sababu kama walikuwa wachache mpaka wanahitaji kupinga bendi ya kusaidiwa na nyingine jinsi ya kuweza kupinga pamoja?
Mtungaji alisema: hakuna kupinga; kwa sababu inakusudiwa kuwa bendi iliyo ni wasaidizi wawe wachache hawazidishi idadi yao kwa uzushi mara kwa mara. Al-Balqini alisema: akajibu kuwa makafiri kama wakikuwa mia mbili, kwa mfano, na Waislamu walikuwa mia moja na hamsini Miongoni mwao ni uchache kwa ajili ya usawa wa idadi hizo, na kama wakisaidiwa kwa makafiri hamsini, basi idadi hizo mbili zilikuwa sawa, hata wale wa hamsini walikuwa katika upande mmoja pamoja na adui, wakawa mia mbili na hamsini Waislamu wanaweza kupinga nao kwa ajili ya kutozidisha idadi yao kwa mara mbili. alisema: pia katika vitabu vya wanavyuoni wengi kutoka Iraq wanazingatia haja pasipo na kutajwa uchache, na haja inawezakana ikawa hali ya huduma, basi masharti hayo mawili hayapingani. Mwisho.
Al-Mawardi ametia sharti lingine ambalo ni kukiuka itikadi ya adui kama Mayahudi na Wakristo, na alilipitisha katika Hashiyat Al-Rawdha. "[Mughni Al-Muhtaaj 27/6, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya].
Ibn Qudaamah alisema: "Haiwezekani kusaidiwa na mshirikina. Ibn Al-Mundhir na Al-Jawzajani na kundi la wanavyuoni walisema hivyo. Na umepokelewa ushahidi kutoka kwa Ahmed kwamba inaruhusiwa kusaidiwa naye. Na kauli ya Al-Khuraqi pia inaonesha hivyo wakati inapohitajika, nayo ni maoni ya madhehebu ya Imamu Shafiy; kwa Hadithi ya Al-Zahriy tuliyoitaja, na habari ya Swafwan Bin Umayya, na inapaswa kuwa wanaosaidiwa nao wawe na maoni mazuri kuhusu Waislamu, lakini kama hakuna Uhakika wa kusalimika nao, basi haifai kusaidiwa nao; kwa sababu tukikataza kusaidiwa na ambao hawaamini miongoni mwa Waislamu, kama vile mvunja moyo na anayetisha, basi kafiri huzingatiwa tangu mwanzoni". [Al-Mughniy kwa Ibn Qudamah 9/207, Ch. Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy.
Baadhi ya wanavyuoni wameenda kinyume na hivyo, wanavyuoni wa madhehebu ya Maalik wamezuia waislamu kusaidiwa na washirikina, lakini hawazuiwi kama wanatoka nje mwenyewe. Maoni mengine ni ya wanavyuoni wa Madhehebu ya Maalik –nayo ni uchaguzi wa Asbagh- kwamba Mwislamu anazuiliwa kabisa.
Al-kharshi anasema: "haiwezikani kusaidiwa na mshirikina isipokuwa kwa ajili ya kutoa huduma tu, kwa maana kwamba tunakatazwa kumtumia kafiri katika jihadi, isipokuwa awe mtumishi kwetu katika kubomoa au kuchimba visima au kutupa manati na kadhalika, [Sharhu Mukhtasar Khalil kwa Kharshi 3/114, Ch. Dar Al-Fikr].
Ushahidi wao ulio na nguvu kuliko wote ni ule uliohadithiwa na Bibi Aisha, mke wa Mtume, S.A.W, alisema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu akatoka nje kabla ya vita ya Badr, alipokuwa katika Hurratu Al-Wabarah mtu mmoja aliyetajwa kwa ujasiri wake na ushujaa wake, alimwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W. Masahaba walipomwona wakafurahi, na wakati alipomwendea akamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W.: nimekuja kwa ajili ya kukufuata Wewe, na kuwa pamoja nawe, Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia: unamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake? akasema: Hapana. Akasema, rudi nyuma, sitasaidiwa na mshirikina, Bi. Aisha alisema, kisha akaenda, tulipokuwa karibu na mti, mtu yule alimwahi Mtume, akamwambia, kama mara ya kwanza, na Mtume akamwambia pia kama alivyomwambia kwa mara ya kwanza, akamwambia, rudi nyuma, sitasaidiwa na mshirikina, akasema, kisha akarudi akamwahi tena msituni, akamwambia, kama alivyomwambia mara ya kwanza: unamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake? akasema: Ndiyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia: basi nenda". [Imepokelewa kutoka kwa Imam Muslim].
Lakini jambo hilo linabebwa juu ya ubora, au kama Waislamu wana nguvu na hawana haja ya watu wengine, au wanabahatisha kwamba huwenda mtu huyo ataingia katika Uislamu kama atalinganiwa, au jambo hilo limefutwa, kwa sababu lilikuwa katika vita ya Badr kama hadithi zilivyoonyesha, ama kuhusu Hadithi nyingine zinazotangulia zinazopigana, nazo ni wazi katika kuchelewa, baadhi yao katika vita ya Khyber na nyingine katika vita ya Hunain baada ya ushindi wa Makkah. Na maneno ya Imam As-Shafiy yalitangulia hapo juu.
Ama kuhusu suala la matumizi ya wasio Waislamu katika mapigano ya Waislamu wanao na dhuluma:
Asili ya hivyo ni kwamba hairuhusiwi. Askari waislamu wanakusudia kuwazuia siyo kuwaua, lakini askari wasio Waislamu, hawajui hivyo wala hawafanyi hivyo. Lakini kama iko haja ya kuwatumia wasio Waislamu, basi udhibiti wa jambo uwe kwa Waislamu, na wanadai kile wanachokiona miongoni mwa misingi ya sheria.
Ushahidi wa hayo ni umuhimu mkubwa wa kuwaua wanaostahili kuuawa, na dharura zinaruhusu makatazo, na dharura zinakadiriwa kwa kiasi chake, kama inavyojulikana kupitia misingi ya kifiqhi.
Wanavyuoni wengi wa madhehebu ya Malik, Shafiy na Hanbal wamefuata kama tulivyosema, na pia wanavyuoni wa Madhehebu ya Shafiy na Hanbal wamesema kuwa hairuhusiwi kuwatumia kwa ajili ya kupambana na wanaoonekana wenye haki; kwa kufuata maoni ya wanavyuoni wa Hanafiy wanaosema kuua wenye kudhulumu kwa nguvu wakati wanapokimbia katika vita.
Al-Bahutiy alisema: "(na inakatazwa kutumia) watu wa Haki (katika vita yao) yaani katika mapambano yao na wenye kudhullumu kwa nguvu (kwa makafiri) kwa sababu hatumiwi katika kupambana na makafiri, vile vile hatumiwi katika kupambana na Mwislamu, na kwa sababu inakusudiwa kuwazuia siyo kuwaua, ambapo hakusudii ila kuwaua tu (au ) yoyote na inakatazwa kusaidiwa katika vita yao (na anayeona kuwaua katika hali ya kukimbia kwao) kwa sababu anahimizwa kuua wale ambao hairuhusiwa kuwaua (isipokuwa kutokana na dharura) kama watu wa haki hawawezi kupigana nao, hivyo, basi inaruhusiwa kwa majibu yao. "[Kashaf Al-Qinaa 6/164, Ch. Dar Al-Fikr].
Khatib Al-Sherbini alisema: "(hairuhusiwa kutumiwa –ankusudia na wenye kudhullumu kwa nguvu-) katika mapambano (kwa makafiri) akiwa miongoni mwa watu wa dhima au wengine, kwa sababu inakatazwa kuhimizwa kumwua Mwislamu, kwa hivyo hairuhusiwa kwa Mwislamu anayestahili kulipiza kisasi kumwakilisha kafiri katika kulipiza kisasi hiyo, kama hairuhusiwi kwa imamu (mtawala) kuchukua kafiri kama mnyongaji anayetekeleza adhabu dhidi ya Waislamu. Tahadhari: Maana ya maneno yao, ni kwamba hairuhusiwa hivyo, lakini mwishoni, walisema kwamba inaruhusiwa kuwatumia makafiri wakati wa dharura, Al-Adhruiy na wengine walisema: (wala hawatumiwa) na wale (ambao wanaona kuwaua) katika hali ya (kukimbia kwao) kwa ajili ya uadui au itikadi kama ilhali kwa medhehebu ya Hanafi kwa ajili ya kukaa kwao... Al-Shaykhan walisema inaruhusiwa katika hali mbili, moja yao ni: kwamba wawe na ujasiri na ushujaa, ya pili ni: kwamba wanaweza kuzuiliwa nao kama wakiwafuatia baada ya kushindwa kwao. Al-Mawardi ameongezeka sharti ya Tatu: nayo ni kwamba wanapaswa wasimfuate anayekimbia wala wasiue anayejeruhiwa na kuamini kwamba watatekeleza hivyo. "[Mughni Al-Muhtaaj 5/407, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiya].
Abu Abdullah Al-Muaq Al-Maliki Alisema: “Katika kitabu cha Al-Nawadir: kama watu wa dhuluma wakiacha kufanya hivyo, basi mtawala anaweza kufanya pamoja nao kama anavyofanya na makafiri, wala haiwezikani kuwatupa kwa moto, na kwamba hawakwepo miongoni mwao wanawake na watoto. Sahnoun alisema kuhusu Al-Khawarij: Mtume S.A.W. amewaita waasi na hakuwaita makafiri, na Ali R.A. ametunga sheria ya kupambana nao, lakini hakusema kwamba wao ni makafiri wala hakuwatukana, wala hakuchukua fedha zao, urithi wao upo na wana hukumu za Uislamu katika hilo, lakini wameuawa kwa mujibu wa Sunna, na kwa sababu ya uzushi wao, na hivyo ni kama adhabu iliyotekelezwa juu yao, wala hawafuatiliwi kwa ajili ya kumwaga damu na kufanya uzinifu wala kwa ajili ya kulipiza kisasi, wala kwa ajili ya mahari wala adhabu (wala miti yao haikuchomwa wala hawakuuawa) matini ya Al-Quraafiy imetanguliwa hapo juu: nyumba zao hazikuchomwa na miti yao haikukatwa, na wala kuwatumwa mashirikina kwa ajili ya kuwapambana nao, na wala hawakupewa fedha (wala hawaulizwi fedha) matini ya Al-Quraafi imetanguliwa hapo juu: wala hawakupewa fedha”. [Al-Taji na Al-Iklil Sharhu Mukhtasar khalil 6/278, Ch. Dar Al-Fikr].
Abu Mohammad Bin Hazmi Alisema: “Swali: Je, inaruhusiwa kuwatumia watu wenyekudhulumu kwa nguvu katika kupambana na watu wa vita, au watu wa dhima, au watu wengine wa dhuluma? Abu Mohammed alisema: watu wanatofautiana katika jambo hili. Kundi katika watu hao linasema: Haijuzu kumtumia adui au mtu wa dhimma au wale ambao ni halali kuwaua katika hali ya kukimbia kwao. Na hii ni kauli ya Imama Shafii R.A... Abu Mohammad anasema: hivi ndivyo ilivyo kwetu sisi kama watu wa haki watakuwa na kizuizi chochote, lakini kama watu wa haki wako karibu na kuangamizwa, na wakalazimika kwa dharura na hawa wengine kwa hila, basi hakuna ubaya wowote baya kuwakimbilia maadui. Na wajilinde kwa watu wa dhima, mpaka watakapokuwa na yakini kwamba katika hali ya wao kushinda kivita hawatamdhuru mwislamu au mtu wa dhima kwa kuwaga damu yake au kwa mali yake, au uharamu katika visivyo halali. Na dalili ya hayo ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {naye amekwisha kubainishieni alivyo kuharimishieni, isipo kuwa vile mnavyo lazimishwa} na hiyo kwa ajili ya kila aliyelazimishwa kwake, isipokuwa kile kilichozuiliwa kwa matini ya Qur'ani au Sunna au kwa makubaliano ya wanavyuoni. Kama mwislamu akijua – akiwa ni mmoja au waislamu wengi- kwamba watu atakayewatumia miongoni mwa watu wa vita au watu wa dhima wanawaudhu waislamu au watu wa dhima katika kitu kinachoharimishwa, basi hairuhusiwi kuwatumia wao, hata akiuawa, lakini ni bora kusubiri kwa ajili ya amri ya Mwenyezi Mungu – hata akiangamizwa yeye mwenyewe na familia yake na mali yake - au anaweza kupambana nao mpaka afe katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ukarimu, kifo ni jambo la lazima kwa kila mtu na uthibitisho wa hivyo ni kwamba hairuhusiwi kwa yeyote kujiepusha dhulma kwa dhulma kwa mtu mwengine, wanavyuoni hawakutofautiana kuhusu jambo hilo. Ama kuhusu kuwatumia watu wenye kudhullumu kwa nguvu ili kupambana wengine wenye kudhullumu kwa nguvu pia, baadhi ya wanavyuoni wamekataza hivyo kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni wasaidizi}.
Na wengine wameruhusisha hivyo, na tunayafuata maoni yao hayo, kwa sababu hatukuwafanya wao ni kama wasaidizi, na Hasha, lakini tunawapambana nao kwa watu wengine kama wao kwa ajili ya kuwahifadhi watu wa haki kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu anaposema: {Ndio kama hivi tunawaelekeza madhaalimu wapendane wao kwa wao}... Abu Mohammed alisema: jambo hilo linaruhusisha kuwatumia watu wa vita kwa ajili ya kupambana na wengine wanaofanana nao, na kupambana na watu wa dhuluma kwa waengine wanaofanana nao miongoni mwa Waislamu ambao hawana sehemu ya kheri yoyote. Pia, mpotovu ni anapaswa kupigania dini, na kuwaepusha watu wa dhuluma, kama anavyopaswa Mwislamu mwema, hairuhusiwi kuwakataza wao, bali inapaswa kuwaita watu kwa ajili ya hivyo," [Al-Muhalla 11/355].
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia, inabainika kwamba inajuzu kusaidiwa na wasio Waislamu katika vita dhidi ya wasio Waislamu kama waislamu watasalimika na hatari yao. Ama kuhusu kusaidiwa na wasio kuwa waislamu katika vita dhidi ya majambaz Waislamu, asili ya jambo hili ni kutojuzu isipokuwepo dharura ya kufanya hivyo, na itajuzu kwa mashari yaliyotangulia kutajwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas