Mkataba wa Kizamani wa Kukodisha.

Egypt's Dar Al-Ifta

Mkataba wa Kizamani wa Kukodisha.

Question

 Tumeona maombi yaliyowasilishwa, ambayo yanajumuisha swali la: Hukumu ya Sheria kuhusu kuongeza mkataba wa kukodisha kwa warithi wa wapangaji wa nyumba katika jengo lililokodishwa tangu zamani miaka ya 1960 na 1970, kwa kujua kwamba baadhi ya wapangaji wa nyumba walifariki na baadhi yao hawaishi tena katika nyumba hizo zilizokodishwa.

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na sifa njema ni zake, na rehema na amani zimshukie Bwana wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na Aali zake na Masahaba wake na wafuasi wake. Na baada ya hayo:
Upangishaji katika Sheria ni: Mkataba wa manufaa yanayokusudiwa, yanayoainishwa na yanayoweza kutolewa kwa malipo yanayoainishwa. [Ansa Al-Matwalib kwa Sheikh Zakaria Al-Ansariy 2/403, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islami]
Sheria ya Kiraia ya Kimisri imeeleza kukodisha katika mada yake namba (558) kwamba: “Ni mkataba ambao mmiliki anaahidi kumwezesha mpangaji kufaidika na kitu maalumu (nyumba) katika kipindi maalumu kwa malipo maalumu”.
Mkataba wa kukodisha una sheria zilizopangwa, na miongoni mwa sheria hizi: Sheria za kukodisha maeneo, ambazo zilikusudiwa kupambana na mgogoro wa makazi ulioibuka tangu mwanzo wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ambapo harakati za ujenzi katika Misri, zilisimama wakati ule hasa ujenzi wa makazi kutokana na kutokuwepo kwa vifaa vya awali vya ujenzi, hali hii ilioana na kuingia kwa wingi kwa majeshi na baadae wafanyakazi wa kiraia, pamoja na makundi ya wahamiaji yaliokuja kutoka nchi zilizovamiwa na majeshi ya adui, kisha kuondoka idadi kubwa ya watu wa vijijini na mijini kwa sababu ya wingi wa kazi ambazo huambatana na kuwepo kwa makundi ya watu hawa waliohamia, ambapo upatikanaji wa nyumba ni jambo gumu, wamiliki walianza kuwatahadharisha wapangaji kwa kuhama makazi yaliyokodishwa mwishoni mwa mikataba yao, au kwa kulipa kodi mara mbili ya makazi yaliyopo au kwa kuzidisha katika kodi kwa maeneo mapya, wakati huo Utawala wa kijeshi ukaogopa kuwa wamiliki wanaongeza mgogoro wa makazi zaidi. Wakatoa sheria ya kijeshi namba (151) kwa mwaka 1941 na wakafunga mikono ya wamiliki wa nyumba ili wasiongeze kodi isipokuwa katika mipaka finyu tu, na kuamua kuongeza muda wa mikataba ya sasa baada ya kumalizika moja kwa moja mpaka kutolewa kwa amri nyingine, na kisha watawala wa kijeshi wakairekebisha sheria hii kwa marekebisho kadhaa, kisha wakaibadilisha kwa sheria namba (315) ya mwaka 1942, kisha wakaibadilisha kwa sheria namba 598 iliyotolewa Julai 11, 1945, na kisha wakairekebisha kwa marekebisho machache kwa sheria namba (604) iliyotolewa Julai 31, 1945.
Wakati wa kukomesha sheria za kimila, ilitolewa sheria namba (97) kwa mwaka 1945 na kuamua muendelezo wa masharti yaliyomo kwenye sheria namba 598 iliyorekebishwa kwa sheria namba (604) kwa kipindi cha mwaka mmoja ili iweze kutolewa kwa sheria ya kupanga uhusiano kati ya wamiliki wa nyumba na wapangaji baada ya kumalizika kwa mwaka, sheria hii haikutekelezwa katika kipindi hicho, sheria ilitolewa chini ya namba (140) kwa mwaka 1946, ikiwa ni pamoja na hukumu zilizojumuishwa katika sheria, na ziliendelea kufuatiliwa mpaka kutolewa sheria namba 121 kwa mwaka 1947, na kufuatiwa na sheria namba (52) kwa mwaka 1969, ambayo ikabadilishwa na sheria namba. (49) kwa mwaka 1977, kisha ikarekebishwa kwa sheria namba 136 kwa mwaka 1981. Iliyokusudiwa kwa sheria za kodi ya maeneo ni sheria ya zamani, kila sheria katika kipindi cha utekelezaji wake.
Sheria za kodi ya maeneo za kisasa ni: Sheria namba 49 ya mwaka wa 1977, Sheria namba 136 ya mwaka wa 1981, na sheria hizi mbili ni sheria ambazo watu wanaziita sheria ya zamani.
Sheria hizi zilikuwa na baadhi hukumu maalumu zinazopelekea kutoka nje ya sheria ya jumla ya kukodisha zilizomo katika Sheria ya Kiraia, na sheria hizi ziliwekwa katika uhalisi ili kutoa makazi yenye kodi nafuu kwa upande mmoja, na kutoa utulivu katika makazi kwa kubaki mkataba mradi mpangaji anaendelea kulipa kodi kwa upande mwingine, Utawala wa kijeshi ukazichukua hukumu hizi ni kama hukumu zinazohusiana na matendo asili.
Kisha ilitolewa baada ya hapo Sheria namba (4) kwa mwaka 1996 na kuamua kupitia mikataba ya kodi ya maeneo kwa sheria ya kiraia siyo kwa hukumu za sheria za kukodisha maeneo chini ya namba (49) kwa mwaka 1977, na namba (136) kwa mwaka 1981, na hali hii kuhusiana na mikataba iliyofanyika kuanzia tarehe ya Sheria namba (4) kwa mwaka 1996, sheria hii ya mwisho ni sheria ambayo watu wanaiita sheria mpya, lakini mikataba ya kukodisha iliyofanyika kabla ya tarehe hiyo, ikawa chini ya sheria ya zamani kwa muda wa mikataba hiyo.
Na kuongeza kwa mkataba wa kukodisha ni miongoni mwa hukumu zilizowekwa na sheria ya zamani ya kimisri, na dhana ya kuongeza hapa ni kwamba mkataba wa kukodisha haumaliziki kwa kumalizika kwa muda wake wa mkataba, lakini unaongezwa moja kwa moja na kwa mujibu wa sheria kwa walengwa fulani walioainishwa katika Sheria.
Sheria ya kimisri imeweka kuongeza mikataba ya kodi kwa muda usiojulikana na bila ya haja ya kukubaliana kwa mkandarasi kwa matini maalumu zinazohusiana na matendo asili. Na haikuishia tu kwa mujibu wa masharti yaliyoelezwa katika sheria, hukumu hii inatumika kwa mikataba iliyofanyika kabla ya sheria ya mwaka wa 1996 inayotajwa hapo juu.
Kama mpangaji asili ni wa kwanza wa walengwa wa sheria ya kuongeza muda wa mkataba basi sheria iliainisha walengwa wengine kwa kuongeza mkataba wa kukodisha katika hali ya kifo cha mpangaji asili au kuiacha nyumba ya kodi, na kuhesabiwa katika idadi maalumu ya jamaa, kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 29 ya Sheria namba (49) ya mwaka wa 1977 kuhusu kodi ya maeneo kwamba: “Mkataba wa kukodisha makazi haumaliziki kwa kifo cha mpangaji au kwa kuiacha nyumba iliyokodishwa kama akikaa ndani yake mkewe au watoto wake au yeyote wa wazazi wake waliokuwa wakiishi naye hadi kifo au hadi wakati wa kuiacha nyumba ... katika hali zote, mmiliki anaahidi kubadilisha mkataba wa kukodisha kwa wale ambao wana haki ya kuendelea kumiliki nyumba, na wakazi hawa wanalazimika kufuata hukumu zote za mkataba”.
Inafahamika kupitia kifungu hicho, kwamba wanaofaidika kutokana na kuongeza muda wa mkataba wa kodi ni: Wanandoa, watoto wakiume na kike, na wazazi ambao walikuwa wanaishi pamoja na mpangaji katika tarehe ya kifo au kuiacha nyumba.
Hawa ni jamaa wote wanaofaidika na kuongeza kodi kisheria, na haikutajwa katika matini za kisheria yanayomaanisha kwamba sheria inasawazisha katika maisha yao, lakini inathibitisha kuongeza kodi kwa ajili yao wote, kama walivyokuwa walengwa wote kwa makazi kabla ya kifo au kuiacha nyumba, wanashirikiana wote baada ya kifo au kuiacha nyumba kamili. Kama Mmoja wao aliacha kukaa nyumbani basi wengine watapata haki yao hii.
Ni nia ya kukaa iliyotajwa katika makala iliyotangulia ni makazi ya imara ya kawaida yanayoendelea mpaka kifo au kuiacha nyumba, ambapo nia ya mkazi ni kuwezesha haya makazi ni makazi ya kwenda na kurudi kwake; basi hakuna makazi ya kudumu isipokuwa makazi haya tu.
Vile vile sheria haikuweka masharti kwa wanandoa, watoto na wazazi kuendelea kwa kukaa kipindi fulani katika makazi, lakini inatosha kukaa tu wakati wa kifo au wakati wa kuyaacha makazi.
Na pia inafahamika kwamba si muhimu kuwa mlengwa ni mrithi, kwani pengine ana haki ya kuongeza kodi na anazuiliwa kutoka urithi, vile vile si lazima kwamba kila mrithi atakuwa mlengwa, bali pengine mrithi hana haki ya kukaa kama masharti ya kifungu namba (29) hayakutekelezwa kwake.
sheria na taratibu hizi ni miongoni mwa masuala yanayofuata maslahi yanayochaguliwa na Watawala basi wanatunga sheria zinazofaa kwa maslahi ya umma, na maslahi hapa yanathabiti na ukweli kwamba nyumba ni ya familia mara nyingi; ambapo mpangaji anaikodisha ili kuishi ndani yake pamoja na familia yake, na wale jamaa wahusika ndio wanaoishi pamoja na mpangaji, nao mara nyingi ni familia yake.
Iliamuliwa katika sheria kwamba matendo ya Watawala yanakusudiwa maslahi, na kwamba mwenye mamlaka ana utawala wa kuzuia kwa yanayoruhusiwa, na yanayokusudiwa kwa kuzuia ni kwamba mwenye mamlaka ana haki ya kuchagua moja ya mambo mawili: Kitendo au kuacha kwa jambo moja linaloruhusiwa kutendwa au kuachwa, kisha kulazimisha watu kwa uchaguzi huu kulingana na mamlaka yaliotolewa na sheria.
Asili ya jambo hili ni kauli yake Mwenyezi Mungu: (Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.)[An-Nisaa: 59], Ibn Ashour alisema katika ufafanuzi wake «Al-Tahriir wal Tanwiir» [5/97, 98, Ch. Dar Tunisia lelnashr]: «Wenye madaraka katika sisi ni wahusika wanaotegemewa kusimamia mambo ya watu ya kimaisha, basi madaraka ni yao... wenye madaraka hapa ni wahusika wengine isipokuwa Mtume, Khalifa, Walii, viongozi wa majeshi, wanavyuoni wa fiqhi kutoka masahaba, wenye jitihada, wataalamu katika siku hizi za mwisho, na wenye madaraka ni watu wanaoitwa pia Ahlul Hal wal Aqd yaani watu wenye mamlaka».
Imepokelewa kutoka kwa Imam Muslim na Al-Bukhari kutoka kwa Abdullah Ibn Omar R.A., kwamba Mtume, S.A.W., alisema: “Inampasa Muislamu kusikia na kutii kwenye kitu anachokipenda au anachokichukia isipokuwa akiamrishwa Maasi kama akiamrishwa Maasi asisikilize wala kutii”.
Imepokelewa kutoka kwa At-Tirmidhiy -na asili yake katika Sahihi ya Imam Muslim- kutoka kwa Wael ibn Hajar, R.A., kwamba Mtume, S.A.W., aliulizwa na mtu kwamba: Je, kama tukiwa na wakuu wanaotuzuia haki yetu na wanatuombea haki yao? Mtume wa Allaah S.A.W., alisema: “Msikilizeni na mumtii; basi yaliyo juu yao ni yale waliyobebeshwa, na yaliyo juu yenu ni mliyobebshwa nyinyi”.
Imepokelewa kutoka kwa Abu Dawud kutoka kwa Samrah Ibn Jandab R.A., kuwa alikuwa na baadhi ya mitende katika bustani la mtu wa Al-Ansaar, alisema, Samrah alikuwa akiingia mitende yake akamwudhisha mtu yule mwenye bustani, basi yule mtu akaomba kununua mitende hii lakini Samrah alikataa, akaomba kuihamishia mitende kwenye bustani nyingine, akakataa, basi alimjia Mtume S.A.W., akamwambia hivyo, Mtume S.A.W., akamwomba Samrah kuuza mitende hiyo kwa mtu yule lakini Samrah alikataa, akamwomba kuihamishia mitende hiyo kwenye bustani lingine, akakataa, Mtume S.A.W., alisema: «Basi mpe mitende hii kama zawadi, na utapata hivyo na hivyo» akimpendeza jambo hili, lakini Samrah alikataa, Mtume S.A.W., alisema: «Unataka kuwadhuru watu» Mtume S.A.W., alimwambia mtu yule wa Al-Ansaar: «Nenda na ng’oa mitende yake». Hadithi hii inathibitishia kwamba inaruhusiwa kwa mwenye mamlaka kuzuia uhuru wa mmiliki katika kutendea mali yake kama akiona kwamba kuna maslahi katika jambo hili.
Imepokelewa kutoka kwa Al-Hafidh Al-Baihaqi katika Sunan yake na Ibn Abi Shaybah katika tasnifu yake -kwa maneno yake- kwamba Hudhaifa Ibn Al-Yaman R.A., alimwoa mwanamke wa Kiyahudi, basi Umar alimwandikia kuwa mwache, akamwandikia: "Kama ni haramu nitamwacha", akamwandikia: "Sidai kuwa ni haramu, lakini ninaogopa kutendewa na wazinzi miongoni mwao".
Huyo ni Umar R.A., aliyezuia ndoa ya wanawake wa kitabu katika zama zake alipoogopa kwamba watu pengine hawachunguzi vizuri kuhusu kuwaoa wanawake mahashumu, kwa tendo hilo hakuharimisha jambo la halali, lakini alizuia yanayoruhusiwa kwa manufaa ya umma.
Na jambo ambalo ni sahihi zaidi ni lile lililopokelewa kutoka kwa Al-Azraqi [Akhbar Makka 2/69 Ch. Dar Al-Andalus - Beirut] kwamba Msikiti Mtukufu ulipokuwa finyu Umar ibn Al-Khatwab R.A., alinunua nyumba zinazouzunguka kutoka kwa wamiliki wake na kuzibomoa kwa ajili ya upanuzi wa msikiti, na wakati alipokataa baadhi yao kuchukua bei na alikataa uuzaji wa bei zao ziliwekwa katika kabati la Kaaba mpaka walipozichukua baadaye, Umar aliwaambia: «Mmekuja wakati Kaaba ilipojengwa basi hili ni ua lake, na wala Kaaba haikujengwa baada ya kuja kwenu», na tukio hili ni dalili inayothibitisha kuruhusiwa kwa kuingilia kwa mwenye mamlaka katika umiliki wa kibinafsi, bila shaka hali ya kumlazimisha mmiliki kwa kuongeza kodi ni nyepesi kuliko kumlazimisha kuiuza nyumba yake.
Wanvyuoni wamesema maana hii, kutoka hayo yaliyotajwa katika vitabu vya mabwana Al-Shaafi'iy kwamba kama mwenye mamlaka akiamuru kwa jambo linalopendekeza au linalochukiza au linaloruhusiwa inatakiwa litekelezwe; Imam Ibn Hajar katika fatwa yake ya kifiqhi alisema: [1/278, Al-Maktaba Al-Islamiya]: "Kauli yao: Ni lazima kumtii mwenye mamlaka wakati wa kuagiza kukataza isipokuwa kinyume na sheria ya Kiislamu tu. Inaonekana kuwa makusudi yao kwa kukiuka sheria ya Kiislamu ni: Kuagiza dhambi au kukataza wajibu, hali hii ni pamoja na mambo yanayochukiza, kama akiyaagiza, ni lazima yatekelezwe ambapo hakuna kukiuka wakati ule. Kisha maneno yao yana maana ya kwamba kutoa sadaka huwa ni wajibu kama mwenye mamlaka akiiagiza, lakini huwa ni wajibu pia kwa kila kinachoitwa sadaka".
Kuhusu yanayokumbushwa na baadhi ya watu kuwa kanuni hii ni kinyume na sheria, na kwamba mkataba unaofanyika chini yake mkataba batili; kwa madai ya kuwa mkataba wa kukodisha katika sheria hairuhusiwi kuendelea milele kwa mujibu wa maafikiano ya wanavyuoni, na ni muhimu kuainisha muda wake, kauli hii si sahihi, lakini kuhusu hali ya kutoendelea kwa mkataba wa kukodisha milele, basi ni sahihi, na rai hii inayochaguliwa na madhehebu manne yanayotumika kutolea Fatwa; basi kukodisha ni mauzo ya faida, na uuzaji si sahihi tu isipokuwa kwa kinachojulikana kiasi chake, makisio ya muda yalikuwa ni njia ya kujua ni kiasi cha faida kwa sababu hakitambui tu isipokuwa katika muda maalumu; kwa sababu ni pale kidogo kidogo. [Rejea: Al-Muhadhab kwa Al-Shirazi 2/246, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilamiya, Al-Mughni kwa Ibn Qudaamah 5/251, Ch. Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabi], lakini maana ya kuwa kitu ni cha milele ni: Kuendelea milele mpaka mwisho wa dunia [Rejea: Taj Al-Arous kwa Al-Zubaidi 7/371, 372 Ch. Dar Al-Hidayah,]. mkataba wa kukodisha ambao chini ya sheria ya zamani sio kama hivyo, kwa sababu kama kipindi chake ni kirefu mwishoni mkataba huu ni wa muda unaohusiana na wapangaji wanaopewa haki ya kuongeza muda wa mkataba kwa mujibu wa sheria na mmiliki basi ni bure kuondoa nyumba iliyokodishwa baada ya hapo.
Kusema kwamba ni lazima kuainisha muda wa mkataba wa kukodisha ni suala tata kati ya wanavyuoni, kwani baadhi ya vitabu vya fiqhi kutoka kwa Imam Al-Shafii vimetaja kwamba Imam Al-Shafii amesahihisha katika maneno yake kwamba mkataba wa kukodisha ni wa kudumu; akisema kuwa mauzo ya faida ni kama kuuza vitu vingine. [Rejea: Tibian Al-Haqaiq kwa Al-Zailai 5/106, Boulaq, Durar Al-Hukam Sharhu Majalatul Ahkaam kwa Ali Haidar 1/505, Daru Al-Jiil].
Inajulikana kwamba suala la makazi lililo chini ya sheria ya zamani ni suala lililosababisha shida, kwa sababi linahusiana na idadi kubwa sana ya watu na familia, na kusema kwa ubatili wa mikataba -ambayo ni sahihi kwa mujibu wa sheria- na kwamba maisha yao katika makazi haya ni kukaa kwa kunyakua na hairuhusiwi kwao – kauli hii ni hatari ambayo haisemwi na mwanachuoni wa Fiqhi yeyote, na mwanachuoni wa Fiqhi ni mtu ambaye anataka kusahihisha mikataba ya watu na shughuli zao kwa muda mrefu tu alipoupata upande wa kisheria.
Kwa hiyo, kuongeza muda ulioagizwa na sheria za kodi ya maeneo zinazofuatwa katika Misri kuhusiana na mikataba iliyoingiwa kabla ya tarehe ya Sheria namba (4) kwa mwaka 1996 sheria hii si kinyume na hukumu za sheria tukufu, bali ni suala lililo chini ya akaunti ya maslahi na maovu ambayo mwenye mamalaka anayaona, na haki yake ni kulipanga suala hili kwa kufuata sheria alizoziona kuwa zinafaa, na haki yake vile vile kulipitia mara nyingine na kulirekebisha kwa kufuata sheria inayofaa na maendeleo ya maisha ya watu ili kudumisha uuwiano unaohitajika na kutopoteza usalama wa kijamii.
Na Mwenyezi Mungu Mtukuf ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas