Kusafisha Mali Haramu kwa Njia ya ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusafisha Mali Haramu kwa Njia ya Urithi.

Question

 Mmoja katika ndugu zangu amefariki na kwa mujibu wa mgao wa kisharia wa mirathi mimi nina fungu katika mali ya marehemu, lakini ninachokifahamu mimi na warithi wengine kuhusu marehemu ni kuwa kuna sehemu ya mali aliyotuachia sisi kurithi aliichuma kwa njia iliyo haramishwa na Dini, je ni halali kwetu kurithi mali iliyo haramu na hali ya kuwa sisi ni wenye kuihiitajia sana mali hii na wala hatuwafahamu wenye mali zao, au ni haramu kwetu kuichukuwa?

Answer

  Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Suala la kujipatia mali kwa njia za haramu katika hali zote linazingatiwa ni kula mali ya watu kwa njia batili, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe} [AN NISAA: 29].
Anasema tena: {Wala msiliane mali zenu kwa batili nakuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua} [AL BAQARAH: 188].
Ukweli ni kuwa mali zote ambazo mkono wa mwanadamu umezimiliki ni miliki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, isipokuwa kuongezwa umiliki wa mwanadamu ni kwa njia ya kujinufaisha nazo lakini hakuwa huyo mwanadamu bali ni mja katika waja wa Mwenyezi Mungu amepewa jukumu la usimamizi na umiliki wa mali ambaye ni ya Mwenyezi Mungu kwa njia ya kumpa mtihani na majaribu, kwani Mola Mtukufu anasema: {Kisha tukakufanyeni nyiye ndio wenye kushika mahala pao baada yao katika ardhi ili tuone jinsi mtakavyo tenda} [YUNUS: 14].
Na akasema tena: {Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyo kupeni} [AN NUUR 33].
Akasema tena: {Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na toeni katika alivyo kufanyeni nyinyi kuwa ni waangalizi wake} [AL HADEED: 07].
Anasema Imam Al-Qurtwubiy katika tafasiri yake [17/238, Ch. Dar Al-Kutub Al-Misriya]: “katika alivyo kufanyeni nyinyi kuwa ni waangalizi wake” ni dalili kuwa asili ya umiliki ni Mola Ambaye Utukufu ni Wake, na mja hana katika mali isipokuwa ni kufanya matumizi ambayo yanaridhiwa na Mwenyezi Mungu”.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ametoa ruhusa kwa mwanadamu kuchuma mali na kunufaika nayo lakini pia kuitoa mali hiyo kwa njia ya halali na maalumu, ama aliyoichuma kinyume na uhalali haimiliki mali hiyo wala haiwi haki kwake kuitumia hata kwenye matumizi ya mambo mema, ikiwa atatoa sadaka kwa mali aliyopora kwa njia ya dhuluma pamoja na kuwa na uwezekano wa kuirejesha kwa mwenyewe basi anapata dhambi kwa kupora na matumizi ya hiyo mali na wala hatapata thawabu za sadaka bali thawabu hizo zitaandikwa kwa mwenye mali.
Amesema Imam Abu Abbas Al-Qurtwubiy katika kitabu kinachofahamika kutokana na kufanya ufupisho wa kitabu cha: [Imam Muslim 3/59, Ch. Dar Ibn Katheer, na Dar al-Kalam At-Twayib]: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu hakubali sadaka ya mali haramu, kwa sababu si yenye kumilikiwa na mwenye kutoa sadaka, na mali hiyo haifai kutumiwa na yeye.
Ikiwa mali iliyopo mkononi mwa Muislamu si mali iliyochumwa kwa njia halali haiwi miliki kwake na wala haifai kwa mwenye kujua hili kushirikiana naye na kupokea mali hii isipokuwa ni kwa njia ya kuirejesha kwa mmiliki asili ikiwa ni mwenye kufahamika au kuitoa sadaka kwa niaba ya mwenye mali, kinyume na hivyo basi huko ni kusaidia kwenye mambo yenye dhambi na kula mali za watu kwa njia batili.
Anasema Ibn Rajab Al-Hambaliy katika kitabu cha: [Jaamii Al-Uluumi wal Hikam 1/210, Ch. Dar As-Salaam: “Wakati wowote itakapofahamika kuwa mali ni ya haramu, iliyopatikana kwa njia haramu, basi ni haramu kuchukua mali hiyo”.
Wanachuoni waliotangulia wamezingatia kufaa kwa mirathi kuna masharti, miongoni mwa masharti hayo: Ni iwe mali ya kurithiwa ni miliki halali ya marehemu wakati wa uhai wake, kila kilichokuwa kwenye umiliki halali wa Muislamu kabla ya kifo chake kinahamia baada ya kifo chake kwa njia ya mirathi kwenda kwa warithi wake baada ya kuthibiti umiliki wake hali yakuwa ni chini ya mikono yake.
Amesema Al-Khatwib katika kitabu cha: [Mughniy Al- Muhtaaj 6/50, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Hakirithiwi isipokuwa kile kilichokuwa kina milikiwa na maiti”.
Mali haramu zipo aina mbili: Mali inaweza kuwa haramu yenyewe kama vile pombe au ulevi, na huenda mali ikawa halali yenyewe lakini ikawa haramu kwa sababu za njia ya upatikanaji wake, kama vile mali iliyopatikana kwa njia ya uporaji kutoka kwa mwenye mali au kwa njia ya wizi au iliyochumwa kwa kufanya michezo ya kamari na biashara haramu.
Anasema Ibn Taimia katika kitabu cha: [Al Fatawa Al-Kubraa 4/210, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah: “Yaliyo haramu yana sehemu mbili: Kuna chenyewe kuwa ni haramu kama vile najisi ya damu na mzoga, na kilicho haramu kwa haki ya mwingine, ambacho chenyewe ni katika vilivyo halali miongoni mwa vyakula, makazi, mavazi, vipando, fedha na vyinginevyo. Na uharamu wa hivi vyote unarejea kwenye dhuluma, hivyo huharamishwa kwa sababu mbili: Ya kwanza: Kupatikana kwake kinyume na ridhaa ya mwenyewe wala ruhusa ya kisharia, na hii inazingatiwa ndio dhuluma halisi: kama vile kuiba, kufanya udanganyifu, uporaji wa wazi, na hii ni katika aina maarufu za haramu.
Sababu ya pili: Kupata kinyume na ruhusa ya sharia, hata kama mwenyewe ataruhusu kama vile makubaliano na kukabidhiana mali haramu kama ile inayotokana na riba, kamari na mfano wa hivyo”.
Na mali haramu yenyewe haiingii katika miliki ya Muislamu kwa sura yeyote, na kwa hili ni bora zaidi kutohama mali hiyo kwenye kwenye umiliki wa warithi wake pindi akifariki, kwa sababu kumiliki kwao kwa mirathi ni sehemu ya kuwamilikisha warithi wao, ikiwa asili imebatilika basi tawi nalo limebatilika.
Ama mali halali yenyewe lakini haramu kwa sababu ya njia ya kuipata kwake marehemu, basi warithi ima wanafahamu wenye asili ya mali au watakuwa hawawafahamu, ikiwa wanawafahamu ni lazima kuirudisha mali kwao, na kama hawatairudisha basi wanakuwa ni wenye kula mali za watu kwa njia ya dhuluma, inakuwa ni haramu kwa warithi kuichukua mali hii, na ni lazima kwao kuirudisha kwa wenyewe, kufa kwa aliyeiiba au kupora hakupelekei kile kilichoibwa au kuporwa kuwa ni mali halali kwa warithi.
Ama ikiwa warithi hawawafahamu wenye mali, wanachuoni wametofautiana katika hali hii na kupatikana kauli mbili, kauli ya kwanza: Ni lazima kwa warithi kuitoa sadaka na wala si vyema kwao kuirithi, nayo ni madhehebu ya Jamhuri ya wanachuoni.
Amesema Ibn Abideen katika kitabu cha: [Raddu Al-Muhtaar 5/99, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah: “Ikiwa mmiliki amefahamika basi hakuna shaka katika uharamu wake ulazima wa kuirudisha kwa mwenyewe… vile vile si halali ikiwa amefahamu ni mali ya kupora hata kama hatofahamika mmiliki wake, kwani ni katika mali inayorithiwa na warithi iliyopatikana kwa njia ya rushwa au dhuluma, ikiwa mrithi atafahamu hilo basi si halali kuichukua, na kama hajui basi anaweza kuichukua, na kama itakuwa ni mali yenye deni basi ataitoa sadaka kwa nia ya kuwaridhisha wenye mvutano….la kufahamika ni kuwa ikiwa amefahamu ni mali inayotokana na mambo ya riba ni lazima irudishwe, na kama sio hivyo ikiwa atafahamu ni mali ya haramu si halali kwake na ataitoa sadaka kwa nia ya mwenye mali”.
Na katika kitabu cha: [Miiyaar Al-Muurab cha Wanshareesiy 6/147, Ch. Wizara ya Waqfu na mambo ya Kiislamu nchini Morocco]: “Aliulizwa Yahya Ibn Ibrahim kuhusu mali haramu je ni halali kurithiwa au hapana? Akajibu: Si halali kurithi mali ya haramu kwa kauli ya Imam Maliki, na wanachuoni wengi wa Madina, pamoja na Hassan na Ibn Shihaab wanaihalalisha kwa mirathi”.
Amesema Imam An-Nawawiy: “Mwenye kurithi mali bila kujua anayemrithi ameichuma wapi, je ni katika mali halali au haramu, na wala hapakuwa na alama basi mali hiyo ni halali kwa kauli za wanachuoni wote, ikiwa atafahamu kuwa ndani yake kuna haramu na kuwa na shaka na kiwango cha haramu basi atakiondoa kiwango cha haramu kwa kufanya jitihada”. [Kitabu Al-Majmuu 9/428].
Amesema Abu Haamed Al-Ghazaaliy katika watu wa Imam Shafiy ndani ya kitabu cha: [Aal-Ihyaa 2/130, Ch. Dar al-Maarifa]: “Ikiwa atafahamu kuwa sehemu ya mali yake ilikuwa ni mali ya dhuluma basi analazimika kutoa kiwango hicho kwa kufanya jitihada, na wakasema baadhi ya wanachuoni: Halazimiki na dhambi zitakuwa kwa marehemu”.
Amesema Imam Mardawiy katika kitabu cha: Al-Inswaaf 8/322, Ch. Dar Ihyaau At-Turaath Al-Arabiy: “Faida: katika kufaa kula mali iliyo kuwa na uharamu ndani yake kuna kauli nyingi: Ya kwanza: Ni haramu moja kwa moja, ameelezea hivyo mtoto wa Sheeraziy katika kitabu cha: [Al-Muntakhab] kabla ya mlango wa mambo ya kuwinda. Amesema Al-Azjiy mwishoni mwake: Hiki ni kipimo cha madhehebu, kama tulivyosema katika mfanano wa vyombo safi na vile vyenye najisi, ni kwa uchambuzi wa kadhi, na kuelezea Abu Khatwab katika kitabu: [Al-Intiswaar], amesema Ibn Aqeel katika masuala ya kufanana kwa vyombo: Na amesema Imam Ahmad: Hainishangazi kula kutokana na mali hiyo, na akaulizwa Al-Muruuziy kuhusu yule anayefanya miamala ya riba na kula mali hiyo? Amesema: Hapana. Akasema kwenye kitabu kingine: Wala asile mali iliyochanganyika na haramu isipokuwa kwa dharura. Na kauli ya pili: Ikiwa haramu imezidi theluthi ya mali, ni haramu kula, na kama chini ya hapo hapana inafaa, ameyasema hayo kwenye kitabu cha Riaaya, kwa sababu theluthi inaweza kudhibitiwa kwenye sehemu nyingi. Kauli ya tatu: Ikiwa haramu ndio nyingi basi ni haramu kula mali hiyo, kinyume na hivyo hakuna urahamu, kauli hii imeelezewa pia na Ibn Al-Jauziy katika kitabu cha: [Al-Minhaaj], kauli imenukuliwa na Athrum na Maimamu wengine wafuasi wa Imamu Ahmad katika masuala ya yule mwenye kurithi mali ndani yake kuna haramu: Ikiwa atafahamu kitu kwenye mali yenyewe basi atarudisha, ikiwa sehemu kubwa ya mali yake ni mali ya ufisadi atajiepusha nayo, na imenukuliwa kuwa mtu akiwa anamiliki mali ikiwa mali hiyo sehemu kubwa ni mali ya uporaji au riba basi inapaswa kwa warithi kuachana na mali hiyo, isipokuwa ikiwa mali haramu ni sehemu ndogo isiyofahamika, na imenukuliwa pia kutoka kwake: Je mtu anaweza kuomba kwa mrithi mali akaitumia kwenye kazi za mudharaba wakanufaika wote wawili na kunufaika na yeye? Akasema: Ikiwa sehemu kubwa ya mali ni haramu basi haifai.
Kauli ya nne: Kutokuwa haramu moja kwa moja, ikiwa haramu ni chache au nyingi, lakini inachukiza na inachukiza zaidi kutokana na uwingi wa haramu na uchache wake, imeelezewa hivyo kwenye kitabu cha: [Al-Mughniy] na kushereheshwa, na amesema Ibn Aqeel katika kitabu cha: Al-Furuui]: Na inajengeka kwa tofauti hii: Hukumu ya mashirikiano yake na kukubali sadaka yake na zawadi yake pamoja na kujibiwa maombi yake na mfano wa hayo, ikiwa hafahamu kuwa ndani ya mali kuna haramu, basi asili ni halali, kwani hakuna haramu kwa matarajio, na ikiwepo kuacha ni bora zaidi ili kuondoa shaka.
Ikiwa sababu ya uharamu ndio yenye nguvu dhana yake inaelekea kama vile kwenye chombo cha watu wa kitabu na chakula chao, nikasema: Sahihi ni kuacha. Na katika hilo kunajengeka ikiwa kuna mgongano na kile asili, kumekuwa na mitazamo mingi”.
Kauli ya pili: Ni kuwa ni halali kwao kurithi, nayo ni maelezo ya Imam Abu Hanifa, na baadhi ya Maimam wa Imam Malik, amenukuu Ghazaliy kutoka kwa baadhi ya wanachuoni bila ya kuwataja, na amenukuu kwa Hassan Al-Baswariy, na Ibn Shihaab pamoja na Ibn Qassim, na kunukuu toka Imamu Malik kuwa, mali haramu ikiwa haijafahamika kwa warithi wake basi hakupelekei kwao kuitolea sadaka mali hiyo lakini inapaswa kwao kufanya hivyo, hii inapelekea kuwa inafaa kwao kihukumu kuirithi mali hiyo, na inapendeza kwao mali ya deni kuitolea sadaka.
Amesema Ibn Abideen katika kitabu cha: [Raddu Al-Muhtaar 5/99]: “Amefariki mtu na mrithi anafahamu kuwa marehemu baba yake alikuwa akijipatia mali kwa sura isiyo halali lakini hafahamu huyu mrithi kiwango cha kuweza kukirudisha, basi ni halali kurithi na kilicho bora ni kuitolea sadaka kwa nia ya kumuondoa baba yake kwenye utata huo”.
Amesema Ibn Abideen: “Kauli yake: Na tutahakiki uwingi kwa maana ndani ya kitabu cha: [Tahadhari na Uhalali], amesema: Amefariki mtu na mali yake ni ya haramu kurithi mali hiyo ni halali, kisha akaashiria na kusema: Hatuyafanyii kazi mapokezi haya, nayo ni haramu moja kwa moja kwa warithi, na haramu hata kama haifahamiki milango yake hivyo inapaswa kuwekewa sharti la ikiwa kitu chenyewe ni haramu ili kikubaliane na yale tuliyonukuu, ambapo ikiwa imechanganyika kwa kiwango ambacho haiwezekani kutofautisha, anaimiliki kwa umiliki mchafu, lakini si halali kwake kuitumia ikiwa hakutopelekea kitu mbadala”.
Amesema Imam Ibn Najiim katika kitabu cha: [Al-Ashbaah wa An-Nadhaair]: “Uharamu unavuka katika mali pamoja na kufahamu haramu hiyo isipokuwa kwa upande wa haki ya mrithi, mali kwa mrithi wake ni halali hata kama atafahamu uharamu wa mali hiyo, lakini akaweka sharti la kutofahamika milango ya upatikanaji wa mali”.
Amesema Al-Hamawiy katika kitabu cha: [Ghamru Al-Uyuun Al-baswaair 3/234 – 235, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Akaweka sharti katika kitabu cha Dhaahiriya na kuendelea. Kwa maana ya kuvua kilichotajwa, na matokeo yake ni kuwa halali kwa mrithi kwa sharti la kutojua milango ya upatikanaji wa mali, ikiwa amefahamu basi ni lazima kurudisha kila kitu kwa mwenyewe”.
Na ananukuu Imam Abu Hamed Al-Ghazaliy katika kitabu cha: [Al-Ihyaa 2/130] baadhi ya wanachuoni na madhehebu yao kuwa, katika urithi husafisha mali haramu, kisha anajadili madhehebu haya kwa kusema: Wamesema baadhi ya wanachuoni: Halazimiki mrithi na dhambi ni kwa mrithiwa, na kuchukuwa dalili ya yale yaliyopokelewa kuwa kuna mtu alitawalishwa kazi za Sultan alifariki huyu mtu, akasema Sahaba: Hivi sasa mali yake imekuwa safi kwa maana kwa warithi wake, mapokezi haya ni dhaifu….Ni vipi kifo cha mtu kinapelekea uhalali wa kitu na kauli hii inachukuliwa kutoka wapi?”
Amesema Al-Muwaaq katiba cha: Taaj wa Ikiliil 6/591]: “Aliulizwa sheikh Abu Muhammad Ibn Abi Zaid kuhusu mtu aliyefariki na kuacha mali haramu akasema: Ibn Shihaab amehalalisha kwa warithi wake, na kuhalalishwa na Hassan Al-Baswariy na Abu Qaasim pamoja na wengine, akatengenisha Imamu Malik kati ya kufahamika watu wake kisha kurudishiwa, na ikiwa hawafahamiki hakupelekei kwa warithi kuitolea sadaka lakini inapaswa kwao kuwa hivyo”.
Amesema Ibn Rushd katika wafuasi wa Imamu Malik kwenye tangulizi zilizoandaliwa [1/159, Ch. Dar Al-Gharbi Al-Islaamiy]: “Ama mirathi: Haiwi nzuri kwa mali ya haramu, hii ni kauli sahihi ambayo inapaswa kuangaliwa, imepokelewa na baadhi ya waliosema kuwa mirathi humsafisha mrithi, hilo si sahihi”.
Imepokelewa kutoka kwa Hassan Al-Baswariy kuwa siku moja aliingia nyumbani kwa mtu aliyekuwa akimtembelea kwa vile alikuwa anaumwa, akawa yule mwenyeji anaangalia sanduku ndani ya nyumba yake kisha akasema kumwambia Hassan Al-Baswariy: Ewe Aba Said hizi ni laki moja lakini bado sijazitolea zaka, na wala sijazitumia kwa kuunganisha undugu. Akasema Hassan Al-Baswary kumwambia mtoto wa yule mgonjwa baada ya kifo chake: Imekufikia hii mali halali, basi hakuna ubaya kwako, imekujia mali kutoka kwa yule aliyekuwa na kundi likazuiliwa kwa ubatili wa ukusanyaji wake, na wenye haki walinyimwa” imepokelewa kutoka kwa Ibn Shihaab kuwa amesema kwa yule aliyekuwa na kazi akawa anachukuwa rushwa pamoja na kufanya ulaghai, na yule aliyekuwa biashara yake imejaa riba: “Hakika mali ya urithi aliyoiacha ni chafu kwa warithi wake kuirithi ambavyo amelazimisha Mwenyezi Mungu kwao, wamefahamu uchafu wa uchumaji wake au kutofahamu kwao, dhambi na dhuluma ipo pembezoni mwake” kitabu cha: [Fatawa Ibn Rushd 1/640, Ch. Dar Al-Magharibiy].
Dhambi ya mali iliyochumwa kwa njia ya haramu – kwenye kauli ya pili – haiwi isipokuwa kwa mwenye kuzama kwenye dhambi na kuchuma kwake, mrithi urithi umehamia kwake kwa njia halali basi ni safi kwake kurithi, kwa sababu hakuna anayebeba dhambi za mwingine, lakini kuhamia kwenye haki ya mrithi kwanza ni baada ya kuthibiti hiyo mali kwa mrithiwa.
Na amechukuwa dalili ya kauli hii kwa kipimo cha mali haramu ya kupora ikiwa ni mali yenyewe na kuitumia mporaji kwa kuuza au kuitoa zawadi. Mali hiyo inakuwa ni halali kwa mnunuzi au kwa yule aliyepewa zawadi, anapimwa mrithi sawa na yule aliyepewa zawadi na kuwa ni mali safi kwa mrithi. Kitabu cha: [An-Nawaazili lil Elmiy 2/133, Ch. Wizara ya Waqfu na mambo ya Kiislamu nchini Morocco].
Lakini uuwiano huu unajadiliwa: Kuwa ni kipimo tofauti, kwa sababu vitendo vya mporaji katika kitu alichopora kinampita mwenye kitu chake na kulazimika mporaji kulipia kitu cha mfano wake ikiwa ni kitu chenye mfano au thamani yake ikiwa ni kitu chenye kuthaminika, na kubakia mporaji kuwa na dhamana kwa kile alichopora wala hapitwi na haki ya mmiliki, hapa kuhusu urithi kwao mali haramu inakuwa ni mali safi pasi ya kulazimika kurudisha mali kwa wenyewe, hivyo hakuna sura ya dalili hapa, kama matumizi katika mali ya kupora ikiwa kwa yule anayefahamu kuwa ni mali ya kupora haifai kwa mnunuzi au mwenye kupewa zawadi kuichukua wala kuikubali.
Kauli hii inapewa nguvu baada ya kuelezewa kauli za wanachuoni ikiwa ni pamoja na yale aliyofikiwa na jopo la wanachuoni, ambayo ni kauli ambayo inasimama kwa dalili na misingi ya kisharia ambayo inaharamisha kufanya uadui juu ya mali za wengine na kula mali chafu, ikiwa utafunguliwa mlango wa kula mali za watu kwa ubatilifu kwa njia ya rushwa kamari biashara isiyo halali na warithi wakafahamu kuwa mali itakuwa safi kwao baada ya kufariki kwa mrithiwa wao, hilo litahamasisha kwa warithi juu ya hilo na wengi kufanya makosa kwa mali haramu kwa sababu urithi wao, kuufanga mlango huo ni lazima.
Kauli yenye nguvu ni kauli ya kwanza, pamoja na hayo hakika warithi wakiwa ni watu masikini basi wanaweza kuchukua katika mali hii kiasi cha mahitaji muhimu, ikiwa mmiliki halali hafahamiki, kwa njia ya kuchukuwa sadaka upande wao, na wala sio kwa njia ya urithi, na kitakachozidia hapo ni lazima kitolewa sadaka.
Amesema ndani ya kitabu cha: Al-Mujmuui 9/428 – 429, Ch. Al Maktabah Al-Muniiriya: “amesema Al-Ghazaliy: ikiwa ana mali haramu na akataka kuleta toba na kujivua na mali hiyo, ikiwa mali hiyo ina mmiliki halali basi ni lazima kurudiswa kwake au anaye muwakilisha, akiwa mwenye mali halali ameshafariki ni lazima mali hiyo ilipelekwe kwa warithi wake, ikiwa mmili halali hafahamiki na ni ngumu kufahamika basi inapaswa kutumika mali hiyo kwa masilahi ya Waislamu wote…. Na anaweza kujipa sadaka yeye mwenyewe na watoto wake ikiwa ni masikini, kwa sababu watoto wake wakiwa ni masikini basi sifa ya kupewa sadaka wanakuwa nayo, bali wao ni bora zaidi kupewa sadaka, na yeye anaweza kuchukuwa kiasi cha mahitaji yake, kwa sababu na yeye pia ni masikini. Haya ni katika aliyoyasema Ghazaliy na kuelezewa na Maimamu wengine, nayo ni kama walivyosema, na Ghazaliy naye ameyanukuu toka wa Muawiya Ibn Abi Sufian na wengine katika waja wema waliotangulia, kutoka kwa Ahmad Ibn Hambal na Haarith Al-Muhaasibiy na wasio kuwa hao wawili wawili katika waja wema, kuwa haifai kuiharibu mali hii na kuitupia baharini, hakuna kinachobakia isipokuwa ni kuitumia katika masilahi ya Waislamu. Mwenyezi Mungu ndiye Anayejua zaidi.
Na amesema Ibn Al-Qiyyim katika kitabu cha: [Zad Al-Miaad 5/691]: “Ikiwa ni mwenye kuhitaji basi anaweza kuchukua kiasi cha mahitaji yake, na kinachobaki atakitolea sadaka, hii ni hukumu ya kila kinachochumwa kwa njia ya haramu kwa haramu wa mbadala wake ikiwa ni kitu au manufaa”.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia na uhalisia wa swali: Ni kuwa inafaa kwenu kuchukuwa mali ya haramu ambayo mmeachiwa na warithi wenu kwa njia ya sadaka na wala sio kwa njia ya urithi, na kwa kiwango cha kukidhi mahitaji yenu na dharura zenu na kinachozida hapo ni lazima mkitoa sadaka, na hii ni kwa mujibu wa rai iliyopitishwa katika rai za wanachuoni na madhehebu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

 

 

Share this:

Related Fatwas