Haki za Ujirani Mwema.
Question
Mimi nina kipande cha Ardhi na nimejenga nyumba na ninazumgukwa na nyumba za majirani zangu kwa pande zote nne. Na mmoja wa Majirani hao anaitumia nyumba yake kama karakana ya uhunzi, pamoja na kwamba eneo hili ni la makazi. Jambo ambalo linaniudhi sana na kuwaudhi majirani wengine pia kutokana na kelele kali na harufu mbaya zitokazo katika karakana hiyo. Je sisi tuna haki ya kumzuia Jirani yetu huyo kuendelea na kazi yake ya Uhunzi na kuandaa mashitaka kwa ajili ya kuyapeleka Polisi, ili Karakana hiyo ifungwe?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni zake Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Maimamu wawili wamepokea kutoka kwa Ibnu Omar kwamba amesema: Amesema Mtume S.A.W.: Jiburili aliendelea kuniusia mimi juu ya jirani mpaka nikadhani kuwa atanirithisha. Na anasema S.A.W.: Mtu yoyote anaemwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake, basi amkirimu Jirani yake. [Hadithi hii ni Mutafaqun alaihi], na anamsema Mtume S.A.W.: Hataingia peponi yule ambaye jirani yake hasalimiki na shari zake zote. [Imepokelewa na Muslim]. Na Hadithi zote zinathibisha jinsi ya kumuheshimu jirani na kumfanyia wema. Na zinambainishia kuwa ana haki kwa jirani yake, hatakiwi kumuudhi au kumdhuru, na haki hizi pamoja na wajibu sio kwa muislamu tu peke yake bali zinavuka na kuwaelekea wasio waislamu pia. Na Uislamu umempangilia jirani jinsi ya kumtendea jirani yake katika pande mbali mbali. Na katika vilivyopangwa na Uislamu ni suala la haki ya jirani kunufaika na baadhi ya manufaa yaliyo katika miliki yake kama kunapatikana kutokana na kujinufaisha kwake na anavyovimiliki yeye, madhara kwa jirani yake. Na wanachuoni wa Fiqhi katika masuala haya wana kauli mbili:
Kauli ya kwanza: Ni kwamba yeye hapewi haki ya kunufaika kwake na kinachokimilikiwa na mwingine kama vile nyumba, ikiwa kuwa na haki hiyo kutapelekea madhara kwa jirani yake, na jirani ana haki ya kumzuia jirani yake kuyapata manufaa hayo. Na iwapo atakataa basi jambo lake litapelekwa kwa hakimu, na ikiwa halina madhara yoyote basi hakatazwi kulifanya, na huu ndio mtazamo wa Fatwa ya Wanazuoni wa Madhehebu ya Hanafi. Na pia ni mtazamo wa Fatwa wa madhehebu ya Maliki. Na ni sahihi zaidi kwa wafuasi wa madhehebu ya Shafi na Sahihi kwa wafuasi wa madhehebu ya Hambali, lakini tofauti iliyopo baina yao ni katika kuyatafsiri madhara anayozuiwa mtu kuwa na haki ya manufaa ya kinachomilikiwa na mtu. Mwanachuoni Ibnu l-Mahaami mfuasi wa madhehebu ya Hanafi baada ya kutaja kwake jumla ya sura za suala hili kwa Kipimo katika Umbo la Masuala haya ni kwamba afanye mmiliki kile anachokiona yeye vyovyote atakavyo; kwani yeye anafanya kutokana na utashi wake wa kile anachokimiliki mwenyewe, hata kama kinaleta madhara kwa wengine, lakini Kipimo kinaachwa katika sehemu ambayo inapindukia madhara yake kwa mwingine na kumsababishia madhara makubwa zaidi, na hili ndilo kusudio la Uwazi katika yale yaliyotolewa na Swadru Shahiid, nayo ni katika yanayokuwa sababu za maangamizi na kuzorotesha nguvu za jengo kwa sababu hiyo, au inatoka katika unufaishaji kwa ujumla wake nalo ni katika yanayozuia mahitaji muhimu kama vile kuzuia mwanga kikamilifu juu ya waliyoyachagua kuyatolea Fatwa. Ama kwa upande wa kupanua zaidi katika kuzuia kila kinacholeta madhara fulani huzuia mlango wa kunufaika na anachokimiliki mtu. [Fathul Qadiir, 7/326, Ch. Dar Al Fikr].
Na anasema Mhakiki Ibnu Abidiin baada ya kuyapokea yaliyosemwa na Ibnul Allaamah bin Mahaami: Angalia jinsi alivyokifanya kilichotolewa Fatwa kama kipimo ambacho kinakuwa na madhara ya wazi ndani yake sio yasiyokuwa na mipaka, na kama sio hivyo ingelazimika kama ingelikuwa ana mti unaomilikiwa ambao jirani yake anajipatia kivuli na akataka kuukata ili kuzuia madhara kwa jirani yake, kama alivyoamua yeye katika Alfathi kabla yake. Mimi nikasema: Na Maula Abuu Suudi alitoa fatwa ya kwamba kuuzuia mwanga kiukamilifu kwa namna ambayo inazuia kuandika, na kwa ajili ya hili, kama sehemu hiyo ingelikuwa ina madirisha mawili kwa mfano, na jirani akauzuia mwanga wa mmoja wao kiukamilifu, haizuiliwi ikiwa kuna uwezekano wa mtu kuandika kwa kutumia mwanga mwingine.
Na Uwazi ni kwamba mwanga wa mlango hauzingatiwi; kwa kuwa mwanga huo unahitaji kufungwa kwa kufungwa mlango kwa ajili ya baridi na mfano wake kama alivyo eleza katika Tanqiihil Haamidiyah. Na katika Albahru: Ametaja Raziy katika kitabu cha Iatihsaan, kama mtu angelitaka kujenga nyumba yake kama tanuri la kuokea mikate tena la kudumu kama yanavyokuwa maduka au visagio vya nafaka au Kiwanda cha kutia rangi nyeupe kwenye nguo, basi haijuzu; kwani kufanya hivyo kunamdhuru jirani madhara makubwa hakuwezi kukawa katika masoko au katika visagio vya nafaka au katika Kiwanda cha watia rangi nyeupe kwenye nguo basi haijuzu; kwani hiyo inawadhuru majirani kwa madhara makubwa sana ambayo hayaepukiki, kwani hutoa moshi mwingi, na kisagio cha nafaka na sauti za kugonga zinazodhoofisha jengo, kinyume na bafu; ambalo halina madhara yoyote isipokuwa kwa unyevu na kuna uwezekano wa kuepuka kwa kuwa bafu hujengwa ukuta baina yake na jirani, kinyume na tanuri lililozoeleka katika nyumba za makazi. (Mwisho)
Na Nasafiy amesahihisha katika bafu kwa kusema kwamba madhara kama yatakuwa makubwa sana yatazuiliwa na kama hayatakuwa makubwa sana hayazuiliwi. [Radul Muhtaari, 5/448. Ch. Dar Al Fikr].
Kilicho wazi ni kwamba Wafuasi wa Madhehebu ya Imamu Hanafi wanayazingatia madhara ya wazi kila kinachodhuru miliki ya watu kinyume na mmiliki mwenyewe, na mfano wao ni wafuasi wa Madhehebu ya Imamu Shafi. Katika Sherehe ya Almanhaj, kitabu cha Sheikh Zakariyal Answaary: kwa kawaida mmiliki anafanya atakavyo katika anachokimiliki hata kama kufanya hivyo kutapelekea madhara kwa jirani yake au uharibifu wa mali yake, kama vile mtu aliyechimba kisima au pakawa na majani yakasababisha ukuta wa jirani yake ukapata ufa au majani yaliyomo yakabadilisha maji ya kisima, na ikiwa atapindukia hali ya kawaida kama ilivyotajwa kama sehemu ya kilichopindukiwa kama vile akawa anagonga gonga kwa nguvu sana na kusababisha usumbufu kwa majengo mengine au kuyazuia maji katika miliki yake, mpaka unyevunyevu ukasambaa katika kuta za jirani yake, na ana yeye haki ya kutumia miliki yake hata kwa vibanda vya kibishara au mabafu na zizi la farasi, au kisagio cha vyakula au chumba cha muhunzi kama anaweza kuzijenga kuta zake vyema, kwa maana kila kilichomo kwa namna inayofaa kwa kusudio; kwani kufanya hivyo hakuwezi kuudhuru umiliki hata kama kitamdhuru mmiliki kwa mfano wa harufu mbaya. [3/565, Ch. Dar Al Fikr].
Na mfano unaofanana na huu ni katika kitabu cha Iqnaau cha Khatwiibu Sharbiiniy. Na wafuasi wa Imamu Maliki na Imamu Hambali wameenda tofauti na rai hii. Sura walizozitaja wao ni za wazi ya kwamba kinachomdhuru Mmiliki kinazuiwa pia kama kile kinachoudhuru umiliki, yamekuja haya katika Sharhu Swaghiir, cha Dardiir Mfuasi wa Madhehebu ya Malik; na yakapitishwa maamuzi ya kuzuia moshi kama kuzia bafu, jiko la kuokea mikate, jiko la kawaida na tanuri la kuokea matofali, pamoja na kuzuia harufu mbaya, kama vile ya tumbaku na harufu zingine za machinjio au eneo la utumbo. Na muradi wake ni sasa na sio zamani, na yanazuiliwa yanayoudhuru ukuta kama vile mirindimo ya kugongwa kwa nguvu, masagio ya chakula, kisima, na kupanda miti, na kuzuia ujenzi wa zizi la farasi; kutokana na kuwemo madhara ya harufu mbaya ya uchafu kwa ukuta na sauti za wanyama, na kuzuia duka lililo mbele ya mlango hata kama kwa kuwepo njia iliyokatisha, kwa uzuri; kwa kuwa duka lina madhara makubwa zaidi ya kufunguliwa kwa mlango kwa ajili ya kwenda sambamba na ukaaji ndani yake, na sehemu inayozuiliwa hapo ni kama ilivyotajwa kwamba imetokea na wala sio iliyokuwepo tangu zamani…
Na wala haipelekei kukataza sauti kama vile kuvuta kitambaa kwa ajili ya kukiboresha na mfano wake kama vile mhunzi na seremala pamoja na mtia rangi kwenye vitambaa kutokana na uchache wake; na kwa ajili hiyo, baadhi yao wamesema: haya ikiwa hayakuzidi na kuendelea, na ikiwa yatazidi na kuendelea yatazuiliwa. [3/485, Ch. Dar Al Maarif]
Anasema Swaawiy akisisitizia yaliyotangulia miongoni mwa maneno ya Sheikh Dardiir: Kauli yake: ya kuzuuia moshi ni kama kuzuia bafu kwa maana ya: kuzuia moshi huo kusababisha madhara kwa jirani kwa sababu yake. Na kauli yake: na kuzuia harufu mbaya, kwa maana na ikipelekea kuzuia kutokea kwa vyenye harufu mbaya. Kauli yake: kama kuwamba, kwa maana ya kiwanda cha kuwamba ngozi, machinjio yaliyoandaliwa kwa ajili ya kuchinjia, na eneo la utumbo: nalo ni sehemu ya kusafishia utumbo kwa ajili ya kuondosha uchafu wa kwenye utumbo. Na mtu anazuiliwa kukung'uta jamvi na mfano wake mbele ya mlango wa nyumba yake ikiwa vumbi litawadhuru wapiti njia, na hana hoja yoyote kwamba yeye amefanya hivyo katika mlango wa nyumba yake, Ameisema kauli hii Ibnu Habiib. Na mfano wa maneno kama haya imetajwa katika Sherehe za Mukhtaswar Khaliil.
Na katika Kashaaful Qinaai cha Bahuutiy Mhambali: Inaharamika kwa jirani kusababisha katika milki yake madhara kwa jirani yake kama vile kuchimba shimo karibu na ukuta wa jirani yake, kunamdhuru, na kujenga bafu ambalo linamdhuru na kujenga tanuri linalomuudhi jirani yake kwa kuendelea kutoa kwake moshi wake na kujenga duka la shaba au eneo la uhunzi vinavyomdhuru jirani kutokana na wingi wa kugongagonga na kuta zinaathirika kwa mitikisiko isiyokwisha na kisagio cha nafaka kinachomuudhi na kuchimba kisima kinachoyakata maji ya kisima cha jirani yake, na kunywesheleza, na kuwasha moto unaovuka mipaka ya ukali wake nakuingia kwa jirani na mfano wa hayo wa kila kinachodhuru… na ikiwa hichi ndicho kilishosababisha madhara kwa jirani hapo kabla katika miliki ya jirani kutokana na kujenga bafu au kisagio cha nafaka na vyakula na mfano wake, kwa mfano mwenye kiwanda cha kusafishia ngozi au mfano wake, kama vile kisagio cha vyakula kilichotengenezwa kwa mawe na tanuri la kuokea mikate, na pembezoni mwake, mtu akalima ardhi au akajenga, kwa maana ya kujenga pembezoni mwa jirani yake nyumba, nikasema: au alinunua nyumba pembezoni mwake kwa namna ambayo anadhurika mwenye miliki yake anayesababisha hayo yaliyotajwa kama vile kiwanda cha ngozi na mfano wake hawajibiki mtu huyo mwenye kiwanda hicho, kuondosha madhara; kwa kuwa yeye hakusababisha kutokana na kile anachokimiliki, madhara kwa jirani, na wala hana jirani huyo haki ya kumzuia jirani yake kunyanyua nyumba yake hata kama atazidisha kipimo hadi kiwango cha juu cha kuezeka zaidi yake au atapunguza kiwango hicho, kwa maana kwamba jirani kwa jirani yake hana haki ya kumzuia kurefusha jengo lake hata kama atachelea kupungua kwa malipo ya kodi ya nyumba yake. [3/408, Ch. Dar Al kutub Al Elmiyah]
Na hoja ya Jamhuri ya wanazuoni katika kuzuia kwao kumsababishia jirani madhara ni ujumla wa maana ya kauli yake S.A.W: Hakuna kujidhuru au kumdhuru mtu mwingine.[Hadithi hii Imepokelwa na Ahmad na Ibnu Maajah, na Hakim na wengine wengi] na Maandiko yanayoamrisha uzuri wa kuishi na jirani na kumtendea wema na kutomdhuru ni mengi.
Kauli ya pili: hakuna mtu yoyote anayekatazwa kujinufaisha na anachokimiliki hata kama kufanya hivyo kunasababisha madhara kwa mwingine, mtu hana uwezo wa kumzuia jirani yake kujinufaisha na miliki yake hata kama kufanya hivyo kuna madhara, na hii ndio rai ya Wafuasi waliotangulia wa Madhehebu ya Hanafi, na hii ni kwa mujibu wa hukumu. Ama kwa upande wa sharia wao wanasema kwamba ni wajibu kwao kujizuia na kila kitu kinacholeta madhara kwa jirani yake.
Anasema Kasaniy: Mmiliki ana haki ya kufanya atakavyo kwa kile anachokimiliki, iwe ni kwa kuwasababishia madhara wengine au kutowasababishia madhara wengine, na anatakiwa ajijengee sehemu anayoimiliki choo au bafu au kisagio cha mawe au tanuri la moto, na ana haki ya kukaa katika jengo lake, liwe ni jengo la uhunzi au Jengo la starehe, na ana haki ya kujichimbia kisima ndani ya jengo analolimiliki au kujenga shimo la maji machafu au bafu hata kama ujenzi wake huo unawaudhi majirani zake au unawaletea madhara, na jirani yake hana haki ya kumzuia hata kama jirani huyo atamtaka jirani yake abadilishe kufanya hivyo hawezi kumlazimisha; kwani umiliki usio na mipaka alionao ndio asili yake katika anachokimiliki, Na kumzuia kwake ni kwa lengo linalohusiana na haki ya mwingine, na kama hakuna mfungamano wowote basi hakuna kizuizi isipokuwa ya kwamba kukataa yanayopelekea kumuudhi jirani ni jambo la kidini kwa Hadithi ya Mtume S.A.W.: Muumini ni yule ambaye jirani yake amesalimika na maudhi yake. Na iwapo atafanya kitu chochote katika hilo, hata kujenga nyumba dhaifu katikati ya ukuta wa Jirani haipatikani uhakika; kwani mambo yalivyo hatakiwi mtu kujenga katika miliki ya mtu mwingine. [6/264, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Wale wanaoikubali rai hii wamemili zaidi upande wa kuwa na haki ya kujiamulia kuko mikononi mwa mtu hata kama hatua hiyo italeta madhara kwa mwingine. Na inaweza ikasemwa kwamba: Hakika haki hii inafungamanishwa na kutoleta madhara yoyote; na hii ni kwa kuyajumuisha matukio yote yanayozuia madhara – kama Jamhuri ilivyotoa dalili – na hiyo, rai iliyo sahihi zaidi ni ile ya walioisema kauli ya mwanzo ya kwamba Ujirani kwa manufaa ya nyumba unajuzu kama hautaleta madhara yoyote kwa jirani.
Na katika zama zetu hizi pamezoeleka kuweka vibao maalumu vya kupangilia masuala ya mazingira ambavyo vimewekewa masharti maalumu na sifa maalumu kwa ajili ya maeneo ya viwanda na wafanyaji wa kazi za mikono na kazi za kiviwanda, kama ambapo sifa maamulu za kazi za viwanda ambavyo lazima viwekwe mbali na maeneno ya makazi kwa kuangalia hatari yake na kwa sababu ya madhara yanayoletwa na kuondosha raha ya wananchi. Na ufupisho wa yale yaliyofikiwa na Mashirika na Sheria zinazofundishwa na mashirika haya na sheria zinazopokea bila kujali mtazamo wa Wakuu wa Madhehebu ya Maliki na Hanbaliya.
Na kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia na katika uhalisia wa Swali liloulizwa: ni haki ya muulizaji kumzuia jirani yake asiendelee na kazi yake ya uhunzi nyumbani kwake – kwa maana nyumba ya kupanga – ikiwa kufanya hivyo kunamuudhi yeye na kunawaudhi Majirani zake kutokana na makelele makali na hewa chafu zinayotoka katika nyumba ya jirani mwenye kazi za uhunzi na hasa kwa kuwa eneo hilo ni la makazi kama ilivyokuja katika swali la muulizaji, jambo ambalo linalazimisha kazi za aina hiyo kuwa mbali na maeneo ya makazi ya watu lakini katazo hili linakuwa kwa njia ya upande maalumu nazo ni pande za idara zilizopelekewa malalamiko hayo kisha zichukue hatua zake zenyewe baada ya kuyapokea malalamiko hayo. Na wala haiwi haki yake yeye mwenyewe kujichukulia hatua ya kuzuia shughuli hizo za uhunzi; kutokana na kuwa kwake ni jukumu la pande maalumu, nalo ni jambo lisilojuzu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.