Mume Kusafiri kwa Muda Mrefu na Kum...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mume Kusafiri kwa Muda Mrefu na Kumwacha Mke Wake.

Question

Ni ipi hukumu ya mume kusafiri safari ya halali lakini ni ya muda mrefu na kumwacha mke wake? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Safari ya halali inatokana na nia ya safari ya kukata masafa yatakayoruhusu kufupisha Swala na zaidi, ambapo kusudio la safari linakuwa ni jambo la Sunna kama vile kusafiri kwa lengo la kuwafanyia wema wazazi au kuunganisha undugu au kutafuta elimu, au safari iwe na lengo halali kama kusafiri kwa ajili ya biashara, au safari ya lazima kama kusafiri kwa ajili ya Jihadi, au safari iwe na lengo lenye kuchukiza (lenye hukumu ya makruhu). Na ndoa ni yenye kusimama kwa misingi ya upendo na huruma, na kwa wanandoa kuwa na utulivu kila mmoja kwa mwenzake, Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri} [AR RUUM, 21].
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amefanya ndoa kuwa ni utulivu, na Akajaalia kati ya wanandoa wawili upendo na huruma, bali Mwenyezi Mungu Akamfanya mwanamke awe sitara kwa mume wake, na mume ni awe vazi kwake. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao}[AL BAQARAH, 187].
Haijifichi nguvu ya kuelezea mfanano wa uhusiano wa mume na mke kuwa ni kama vazi, ambapo kitu kilicho karibu zaidi na mtu ni nguo zake na vazi lake.
Imamu Al-Qurtwubiy alisema: “Asili ya vazi ni katika kuvaa, kisha ikafananishwa kukaa wanandoa pamoja kila mmoja wao ni kama vazi kwa mwenzake, kwa kuungana mwili na kuchanganyika miili yao na kufanana na vazi, na baadhi wakasema: Inasemwa pindi kitu kinavyositirika kuwa ni vazi, basi inafaa kuwa kila mmoja kwa wawili hao ni sitara kwa mwenzake kwa kila kisichokuwa halali, kama ilivyopokelewa, na ikasemwa kuwa: Kila mmoja ni sitara kwa mwenzake katika yale yanayokuwa kati yao ikiwa ni pamoja na kitendo cha kuingiliana mbele ya macho ya watu. Na akasema Abu Abeed na wenzake: huitwa mwanamke kuwa ni vazi lako na tandiko lako na shuka yako. Na akasema Rabii: Wao ni tandiko kwenu na nyinyi ni shuka ya kujifunika kwao. Amesema Mujahid: Kwa maana ni utulivu kwenu, kwa maana hupeana utulivu nyinyi kwa nyinyi” [Tafsiri ya Qurtubiy, 3/191, Ch. Muassasat Ar-Risala].
Katika haki ya mke juu ya mumewe ni pamoja na kuwa naye na kukidhi mahitaji yake, lakini anaweza kuacha haki hii kwa ridhaa yake, kumekuwa na tofauti katika kuelezea huu muda ambao mke ana haki baada ya kupita muda huo kumtaka mume haki hiyo, hivyo kumekuwa na kauli nyingi, kwa kutofautiana hali na mazingira ya kila zama na mji, linaonesha hilo kwa Hadithi inayotokana na Imamu Bukhari na Muslim katika Hadithi zilizopokelewa na Abdillah Ibn Amr Ibn Al-Aas alisema: alisema Mtume S.A.W.: "Je sijakwambia kuwa funga mchana na simama usiku? Nikasema ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume akasema: Basi usifanye, isipokuwa funga na ufuturu, na simama usiku kisha ulale, kwani mwili wako ni wenye haki kwako, jicho lako ni lenye haki kwako, na mke wako ni mwenye haki kwako".
Pia inaonesha hivyo kupitia Hadithi inayotokana na Al-Baihaqiy kutoka kwa Abdillah Ibn Dinar kutoka kwa Ibn Umar: “Hakika Umar R.A. alimwuliza binti yake Hafsa: Ni kwa muda gani mwanamke anaweza kumsubiri mume wake? Akasema: Miezi mitano au miezi sita, basi Umar R.A. akafanya watu hawatoki kwa Jihadi kwa muda unaozidi miezi sita, wakitembea mwezi mmoja wakati wa kwenda na kukaa miezi minne na wakati wa kurudi huchukua mwezi mmoja”.
Ibn Qudamah alisema: “Aliulizwa Ahmad bin Hanbal: Ni muda gani mwanamume anaweza kuwa mbali na familia yake? akasema: Imepokelewa ni muda wa miezi sita”. Kitabu cha: [Al-Mughniy cha Ibn Qudama, 7/305, Ch. Maktabat Al-Kahera].
Al-Bahutiy Al-Hanbaliy alisema: “Ikiwa msafiri hana udhuru wenye kumzuia kurudi kisha akachelewa zaidi ya miezi sita kisha mke akataka arudi mume wake basi mume analazimika kufanya hivyo”. Kitabu cha: [Kashaf Al-Qinaa, 5/193, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Al-Kasaniy Al-Hanafiy alisema: "Mume ana haki ya kutaka kumwingilia mke wake wakati wowote autakao isipokuwa wakati wa kutokea sababu zinazozuia kuingiliana kama vile hali ya hedhi, nifasi kufanya dhihar. Kumwambia mke wewe ni sawa na mgongo wa mama yangu", kuhirimia ibada za Hija na sababu zengine, na kwa mke ana haki ya kutaka kukutana kimwili na mume wake kwani halali kwa mume ni haki kwa mke kama ilivyo halali kwa mke ni haki kwa mume, ikiwa mke atamtaka mume wake basi ni lazima kwa mume, na ulazima ni mara moja ama inapokuwa zaidi ya mara moja ni katika mlango wa kuishi kwa wema na kudumisha ndoa”. Kitabu cha: [Badaii' Al-Swanaii', 2/331, Ch. Al-Maktaba Al-Elmiya].
Ibn Al-Hamam Al-Hanafiy alisema: "Fahamu kuwa kuacha kumwingilia kabisa si jambo halali kwa mume, wameweka wazi watu wetu kuwa kumwingilia mke wakati mwengine ni lazima lakini haiingii chini ya hukumu ya ulazima isipokuwa uingiliaji wa kwanza, wala hawajakadiria muda, ni lazima kutofikia muda mrefu isipokuwa iwe kwa ridhaa yake na nafsi yake kuwa nzuri kwa hilo". kitabu cha: [Fat-h Al-Qadir, 3/302, Ch. Ihaya At-Turath].
Imamu Abu Hamid Al-Ghazaliy alisema: "Inapaswa kumwingilia mke kila ndani ya siku nne mara moja, huo ni wakati adilifu, ambapo idadi ya wake ni wanne, basi inafaa kuuchelewesha muda huu, ndiyo, inapaswa kuzidi au kupungua kwa mujibu wa haja zake za kumkinga mwanamke na uchafu, kwani kumkinga mwanamke na uchafu ni lazima kwa mume". Kitabu cha: Ihyaa Ulum Ad-din, 2/52, Ch. Mustafa Al-Halabiy].
Zarkany alisema katika sharhe yake ya kitabu cha: [Mukhtasar Khalil]: “Ni lazima kwa mume kumwingilia mke wake, na anahukumiwa akipata madhara ya kuacha kwake, na akishtaki uchache wa kukutana na mumewe, basi atakuwa naye usiku mmoja kwa kila siku nne”. Kitabu cha: [Sharh Al-Zarkaniy, 4/56, Ch. Dar Al-Fikr].
Ibn Taiymia alisema: "Ni lazima kwa mume kumwingilia mke wake kwa wema, kwa maana kwa kiasi cha kuhitaji kwake na uwezo wake mume - kama anavyomhudumia chakula na kumgharamia kwa kiasi cha mahitaji ya mke na uwezo wake mume - pasi na kuainisha mara ngapi ndani mwezi mmoja au ndani ya miezi minne au wiki au siku moja katika siku nne au tofauti na hivyo, na hilo ni kuwa dalili ya maandiko ya Qur`ani na Sunna ni kutokadiria hilo". Menyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao} [AL BAQARAH, 228].
Mtume S.A.W. amesema kumwambia Hindu mke wa Abu Sufian: "Chukua kile kinachokutosha wewe na mtoto wako kwa wema” ni Hadithi iliyopokelewa na Bukhari ni katika Hadithi iliyotokana na Bi. Aisha ikiwa wanandoa wamevutana katika kuingilia kunakostahiki, basi kiongozi atalazimisha kwa jitihada zake kwa mujibu wa mazoea na hali za wanandoa, kama atakavyolazimisha kugharamiwa mke mahitaji na makazi pamoja na haki zake zengine”. Kitabu cha: [Majmuu Fatawa Ibn Tayimia, 29/173, Ch. Riyadh].
Ibn Al-Qiyam alisema: "Ni lazima mume amwingilie mke wake kwa wema, kama vile anavyomgharamia kwa wema, kumvisha na kuishi naye kwa wema, bali hii ndiyo nguzo za kuishi na makusudio yake, hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameamrisha kuishi naye kwa wema, na kumwingilia ndani ya kuishi huku ni lazima, wakasema: Ni juu yake mume kumtosheleza kwenye kumwingilia kadiri itakavyowezekana, kama vile wajibu kwake kumtosheleza mahitaji ya chakula". Kitabu cha: [Raudat Al-Muhibbin, uk. 217, chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya].
Inapokosekana ridhaa ya mke katika hilo, basi wala haifai kwa mume kutoonekana kwa mke wake hata kwa safari halali ya muda mrefu, kutokana na haki yake ya kuingiliwa, na ikiwa safari yake ni kwa malengo haramu kutofaa ni bora zaidi, na kuainisha urefu wa muda kunatofautiana kwa tofauti ya hali na mazingira, na uainishwa muda wa sharia kwa kila nchi kutokana na mila yao na desturi zao.
Kutokana na maelezo yaliyotangulia: Ikiwa mke amemruhusu mume wake safari halali ya muda mrefu, basi ni ruhusa kwa mume kusafiri, ama ikiwa mke hajamruhusu mume wake, basi inakuwa haifai mume kufanya hivyo. Na uainishaji wa urefu wa muda kunakotegemea zaidi ruhusa ya mke, kunatofautiana kwa tofauti ya mazingira, muda, eneo na mazoea ya kijamii.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas