Urutubishaji wa Uzazi kwa Njia za Kisasa Nje ya Kizazi.
Question
Tumeangalia maombi yaliyotolewa na watu mbalimbali nayo ni pamoja na swali juu ya hukumu ya kisheria kuhusu mambo yafuatayo:
Suala la Kwanza: kugandisha viinitete vinavyotokana na kuchagua yai na manii katika maabara, na utumiaji wake ndani ya mfuko wa uzazi wa mke baada ya kupita muda mrefu.
Suala la Pili: Kufanya utafiti wa kimatibabu juu ya mayai, viinitete na manii ili kuboresha matibabu, sio kwa nia ya kubadilisha tabia ya maumbile.
Suala la Tatu: Msaada wa kimatibabu katika kuchagua aina ya kiinitete cha mtoto wa kiume au cha mtoto wa kike, kwa mujibu wa ombi la wazazi bila ya sababu za kimatibabu.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni zake Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wafuasi wake, na baada ya hayo:
Kuvigandisha viinitete ni aina moja ya maendeleo na uvumbuzi wa kisayansi katika nyanja za uzalishaji wa viwandani, na mchakato huu unafanywa katika maabara za kisasa na zenye ubora wa hali ya juu wa kisayansi zinazohusika na watoto katika hali za Urutubishaji kwa Njia za Kisasa nje ya Kizazi, ambapo kuna idadi kubwa ya mayai ambayo hayafai kuhamisha kwenda tumbo lingine baada ya kuhamisha moja ya yai lililo chaguliwa. inahitajika kuifungia idadi ya mayai ambayo ni zaidi – yaliyochaguliwa au yasiyochaguliwa - ili kuihifadhi, hali hii inaruhusu mke na mume siku zijazo kurudia mchakato wa kuchagua inapohitajika, kwa mfano, kukosekana kwa ujauzito katika mara ya kwanza katika ndoa, au ikiwa baadaye wanandoa wataamua kuwa na mtoto mwingine, bila ya haja ya kurejea upya mchakato wa kuhifadhi mayai kwa ajili ya kutoa mayai mengine.
Wazo la kugandisha kwa viinitete hutegemea kuweka seli chini ya joto la chini sana kwa kuziingiza kwenye nitrojeni, ambayo ina joto la nyuzi mia moja tisini na sita chini ya sifuri, na muda wa kuhifadhi unaweza kufikia miaka kadhaa bila ya kuathirika kwa mayai yaliyohifadhiwa.
Tunachokiona ni kwamba mchakato wa kugandisha uliotajwa haujakatazwa kisheria, kwa sababu ni ongezeko la mchakato wa mtoto ambaye ni katika urutubishaji uliopitishwa na mabaraza ya Fiqhi ya Kiislamu kati ya mume na mke kwa kuzingatia ukweli kwamba ni matibabu ya uzazi, na asili katika matibabu na dawa ni uhalali, na Maimamu wa Waislamu hawakutofautiana katika jambo hili, na ikiwa madawa yanaruhusiwa, basi ongezeko lake yaliruhusiwa pia, kwa sababu idhini ya kufanya jambo huruhusiwa kutokana na makusudi yake - kama alivyosema Imam Abu Al-Fath ibn Al-Fath ibn Daqiq Al-Idd katika Kitabu cha (Ihkaam Al-Ahkaam). Ruhusa hii inathibitishwa na hali ya kuelekea katika ungandishaji wa viinitete ambao unapunguza gharama kubwa za kifedha ambazo zinahitajika kutekeleza mchakato wa urutubishaji wakati wa kuchukua mayai kutoka kwa wanawake.
Lakini, ikumbukwe kwamba ruhusa hii imezuiliwa na udhibiti fulani, ambao ni:
1- Kukamilika kwa mchakato wa urutubishaji kati ya wanandoa, na kwamba Urutubishaji kwa njia ya nje ya Kizazi huingizwa katika mwanamke hali ya kuwa yuko katika ndoa kati yake na mwenye manii ambae ni mumewe, na hairuhusiwi baadaye kufutwa kwa mikataba ya ndoa kwa sababu ya kifo au talaka au kitu kingine chochote.
2 - Urutubishaji huu wa nje ya Kizazi na ulio salama kabisa huwekwa chini ya udhibiti mkali, ili kuzuia kutotokea mchanganyiko wowote kwa makusudi au kwa bahati mbaya na Urutubishaji mwingine wa aina hiyo uliohifadhiwa.
3 – Urutubishaji huo wa nje ya Kizazi usiwekwe ndani ya tumbo la mwanamke mwingine isipokuwa tumbo la mwanamke mwenye yai lililochaguliwa bila kuongezwa kitu kutoka kwa mwingine .
4 – Mchakato wa kugandisha viinitete hauna athari mbaya za pembezoni kwa viinitete hivyo kutokana na kuathirika kwa Urutubishaji huo kunakosababishwa na sababu mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza katika hali ya kuhifadhi, kama vile kujitokeza kasoro mbali mbali, au ulemavu wa akili ya mtoto hapo baadaye.
Kuhusiana na tafiti za kimatibabu juu ya viinitete vya binadamu kwa madhumuni ya matibabu safi, basi jambo hili limeelezwa, na lazima lizingatie maumbile ya jaribio la kisayansi katika suala la uwezekano wake wa kuwa hatari na pia uharibifu wa kiinitete, kwa hivyo, hairuhusiwi kufanya majaribio ya matibabu kwa kiinitete kikiwa ndani ya tumbo la uzazi, isipokuwa ikiwa madhumuni ya jaribio la kisayansi ni kuhifadhi afya yake, au kufuatilia kasoro za maumbile katika hatua za mwanzo, au kuongeza nafasi za kukiweka hai kiumbe hicho wakati kinapoonesha kuwa kinaweza kukumbwa na hatari fulani, kwa kuzingatia kwamba majaribio katika kesi za aina hizi na mifano yake inasababisha madhara makubwa; kama vile kusababisha kutoka kwa kiinitete au kukidhuru.
Ikiwa hakutakuwapo hatari yoyote, na maslahi ya utafiti yakawa yanaweza kupatikana, na pamoja na ruhusa ya wale ambao wana mamlaka kama walezi, hakuna chochote kibaya kwa kufanya utafiti huu; ili kufanikisha maslahi ya uma inayofaa kurudi faida yake kwa jamii nzima ya wanadamu.
Lakini, linalofanya tafiti kama hizi ni lazima liwe shirika la kisayansi ambalo huzingatiwa na kudhamini tafiti kama hizi kwa njia ya kitaaluma iliyopangwa, na kwa upande mwingine, lina jukumu la usimamizi juu ya maadili ya tafiti kama hizi.
Kuhusu viinitete vilivyotolewa vina kesi mbili, kesi ya kwanza: ikiwa kiinitete kimetolewa baada ya kupigwa roho ndani yake, kimefikia siku mia na ishirini tumboni mwa mama yake, na ishara ya uhai wake umeibuka baada ya kuzaliwa kwake. Basi ni marufuku kufanya utafiti na majaribio ya kisayansi juu yake kwani mwili wa binadamu umeheshimiwa, na Sheria mtukufu imeamuru kuuheshimu mwili wake, na wanavyuoni wa fiqhi walisema kwamba kama ikijuliwa uhai wake, basi ni kama mzima sawasawa; huoshwa, hutiwa katika sanda, husaliwa, na huzikwa.
Na kesi ya pili: kama kiinitete kimetolewa kabla ya kupuliziwa roho ndani yake, au baada ya kupuliziwa roho, lakini hakikuonesha ishara ya uhai wake baada ya kuzaliwa kwake, basi kama wenye mamlaka katika walezi wakiruhusu, na kama kuna masilahi yoyote yanayotokana na utafiti huo, basi inaruhusiwa kufanya hivyo.
Sheria Tukufu imeruhusu kukata sehemu ya mwili wa mfu wakati ambapo kuna masilahi ya uma, kama ilivyo katika adhabu ya wapiganaji vita waliotajwa katika Aya hii: {Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusulubiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchini. Huu ndiyo udhalili wao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa}. [AL MAIDAH: 33]
Inaruhusiwa kukata sehemu ya mwili wa mtu kwa ajili ya kuzuia udhalimu wa mtu kuwashambulia watu wengine, na haswa ikiwa tunasema kwamba sheria imekusudia adhabu kuwa kemeo kabla ya kuwa mabadiliko kwa ajili ya hali ya watu, na kwa hivyo kufanya majaribio ya kisayansi ambayo yana manufaa kwa watu ni muhimu zaidi.
Lakini tumeruhusu hivyo katika kesi ya pili kinyume na ya kwanza kwa sababu ruhusa hii ni kinyume na kawaida ambayo ni kuheshimu mwili wa binadamu, na kwamba dharura huwa inakadiriwa kwa kiasi chake.
Kuhusu matumizi ya mayai na manii katika utafiti wa kisayansi, asili yake ni kuruhusiwa kama hakuna jambo la haramu pamoja nayo, kama vile kurutubisha yai kwa manii ya mtu mgeni, au kupachisha viinitete katika mazingira ya viwanda ili kufaidi viungo vyake, au kuvitumia katika majaribio ya upachishaji wa wanadamu.
Kuhusu kuainisha jinsia ya viinitete, kuna njia zake tofauti, ikiwa ni pamoja na kuupangilia wakati wa kujamiiana kabla au wakati wa kurutubika kwa yai, na zingine ni zile zinazohusiana na kubadilisha asili ya uke kutoka katika kemikali mbili za urithi na kuelekea katika pande mbili za chini za uke na kinyume chake, na zingine kuhusu aina ya chakula, na zingine kupitia matibabu yanayotenganisha manii yanayobeba mbegu ya kiume na ya kike, ambayo hujulikana kama uchunguzi wa "Manii", au utenganishaji wa manii kwa kutegemeana na DNA.
Njia zote hizi zinaonekena kuwa aina mbili tofauti: ya kwanza ni kiwango cha mtu binafsi, na ya pili ni kiwango cha pamoja.
Tukiiangalia kwa kiwango cha mtu binafsi, tunasema: Kuwa asili yake ni kuruhusiwa; kwa msingi wa kwamba asili ya vitu ni kuruhusiwa, na kile anakichofanya mwanadamu katika hali hii hakitoki na sababu, na mwenye kuathiri kiuhalisia si mwingine bali ni Mwenyezi Mungu.
Ruhusa hii inathibitishwa ikiwa njia ya kuchagua jinsia ya kiinitete ina Sababu ya kushawishi; kama vile kuzuia magonjwa kadhaa ambayo yanaweza kuzuilika kwa kuchagua aina isiyobeba jeni ya ugonjwa wa kiume au wa kike. Vile vile ikiwa motisha ya kuchagua jinsia ya kiinitete ni kukidhi hitajio kubwa la wanandoa, kama kutamani kwao au kwa mmoja wao kuruzukiwa mtoto wa kiume lakini hawakuruzikiwa isipokuwa watoto wa kike tu, au mambo kama hayo miongoni mwa mambo ya halali.
Kwa kuchukua tahadhari ni kuwa hali hii imeainishwa kwa kutokuwa katika mbinu iliyotumiwa kwa kumuumiza na kumdhuru mzaliwa katika maisha yake yajayo, na hali hii inarejeshwa kwa waliobobea katika jambo hili. Haikubaliki mwanadamu awe katika nafasi ya kufanyiwa majaribio na kuchezewa.
Lakini tukiangalia jambo hilo na kulishughulikia kwa kiwango cha pamoja, ambapo linaonekana kuwai silo tabia ya mtu mmoja binafsi, lakini limekuwa mwenendo wa jumla kuelekea kuzaliwa kwa jinsia fulani, basi hali hii ni tofauti, na ni bora zaidi kuzuiliwa; kwa kuwapa uwezekano wa kusababisha usumbufu wa usawa wa asili, shida ya usawa wa idadi kati ya wanaume na wanawake jambo ambalo ni muhimu kwa mwendelezo wa uzazi wa mwanadamu.
Imejulikana kuwa kuna tofauti ya hukumu kati ya kuainisha jinsia ya kiinitete kwa kiwango cha binafsi na kwa kiwango cha pamoja; Fatwa hutofautiana kulingana na hukumu ya mtu huyo na ya umma, na tofauti hii ni ya kawaida katika Fiqhi ya Kiislamu, na ina mifano kadhaa; ukiwemo ule uliotajwa na wanavyuoni wa Fiqhi kwamba ikiwa watu wa mji fulani wawatakataa kutekeleza Sunnah ya Alfajri au kutoa adhana, wanapigwa vita, ingawa kuliacha jambo hili kunaruhusiwa kwa kiwango cha mtu binafsi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.