Utiifu wa Afisa wa Polisi kwa Wakuu Wake Wakimwamuru Anyoe Ndevu Zake
Question
Nini haki ya Idara za Serikali, kwa mfano Polisi, kumlazimisha afisa au mfanyakazi ndani ya Idara hiyo aache kufuga ndevu zake, kutokana na upingaji wa kufanya hivyo na Kanuni za Serikali, na kumlazimisha kwa amri rasmi alizozipata kutoka kwa wakuu wake, kwa ajili ya kuitekeleza Sheria?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ndevu ni: jina la nywele zilizopo katika mashavu mawili na kidevu. [Al-Mhkam, na Ibn Sidah: 3/444, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Na hii ni miongoni mwa ibada ya kidini inayotakiwa kisheria kwa wanaume, kwa ilivyopokelewa na Maimamu Bukhari na Muslim, kwa mujibu wa tamko la Muslim, kutoka kwa Ibn Umar R.A., kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Punguzeni masharubu na fugeni ndevu”.
Na amri ya kufuga ndevu imetajwa kwa tamko mbali mbali, ambapo Imamu An-Nawawiy aliyafuatilia katika Sharh yake ya Sahihi Muslim [3/151, Ch. Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy] akayaainisha na kuwa mapokezi matano, nayo ni; (punguzeni), (zidisheni), (refusheni), (shikilieni), na (acheni).
Na Imamu Muslim pia amepokea kutoka kwa Ummul Muuminiin Aisha R.A., kuwa alisema: Mtume S.A.W., amesema: “Mambo kumi ni katika Maumbile: kukata masharubu, kufuga ndevu, kupiga mswaki, kuvuta maji puani, kukata kucha, kuosha maungio ya vidole, kunyonyoa nywele za kwapani, kunyoa nywele za tupu, na kustanji kwa maji”. Musa’ab Ibn Abi Shaibah, mmoja wa wapokeaji wa Isnadi ya Hadithi alisema: “Jambo la kumi nimelisahau, nadhani kuwa ni kusukutua”.
Na madhehebu manne ya kufuatwa yamekubali kuwa asili ya kufuga ndevu ndiyo inatakiwa kisheria, lakini yametofautisha katika ngazi ya amri hiyo: Je, ni jambo la lazima? Kwa hivyo basi kufuga ndevu ni wajibu, na kwa hiyo mwenye kufuga ndevu ana thawabu na mwenyekuacha kufuga ana adhabu; au ni jambo lisilo lazima? Basi kufuga ni jambo linalosuniwa, kwa hiyo mwenye kufuga ana thawabu na mwenyekuacha kufuga hana adhabu, na katika hali hii kunyoa ndevu ni jambo linalochukiza, yaani mwenye kuacha kufuga hana adhabu na mwenye kufuga ana thawabu kwa kukusudia.
Wengi wa wanazuoni wa madhehebu ya Hanafi, Malik, na Hanbal walielekea katika mazingatio ya madhehebu zao, uwajibu wa kufuga ndevu, na uharamu wa kuzinyoa.
Na Mtaalamu Al-Haskafiy mfuasi wa madhehebu ya Hanafi katika kitabu cha: [Ad-durul Mukhtaar 6/407, na Hashiyat Ibn A’abidiin, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] alisema: “Ni haramu kwa mtu kuzikata ndevu zake”. [Mwisho]
Lakini pia walisema kuwa: mtu anapokuwa na nywele chache kidevuni mwake (huitwa katika istilahi ya kifiqhi: Kausaj); na kama mtu mwingine akizinyoa nywele chache hizi bila ya idhini ya mhusika, basi hana kosa; na inafahamika kuwa kuzinyoa nywele chache hizi katika hali hii hakuna uharamu; na katika kitabu cha Al-Hidayah na Sharh yake [Al-I’inayah na Mtaalamu Al-Babirtiy 10/281, Ch. Dar Al-Fikr]; “Ndevu za Kausaj akiwa na nywele chache kidevuni mwake, akizinyoa basi hakuna kosa; kwa sababu nywele chache hizi hazina uzuri’. [Mwisho]
Al-Mutariziy katika kitabu cha Al-Mughrib Uk. 407, Ch. Dar Al-Kitab Al-Arabiy] anasema: “Kausaj: ni neno la kuazimwa, maana yake ni mtu mwenye nywele chache kidevuni mwake tu, na hazipo pande mbili za uso”. [Mwisho]
Kuhusu madhehebu ya Malik: Mtaalamu Sheikh Muhammad Uleish mfuasi wa madhehebu ya Malik katika kitabu cha: [Minah Al-Jalil 1/82, Ch. Dar Al-Fikr] anasema; “inaharamishwa kwa mtu kuzinyoa ndevu”. [Mwisho]
Na mfano wa hayo katika kitabu cha: [Hashiyat Mtaalamu Ad-Desuoqiy Ala Ashrah Al-Kabiir, na Saiydiy Ahmad Ad-Dardiir 1/90, Ch Dar Ihiyaa Al-Kutub Al-Arabiyah].
Na Sheikh Al-Buhutiy katika kitabu cha: [Sharh Muntaha Al-Iradaat, miongoni mwa vitabu vya madhehebu ya Hanbal [1/44, Ch. A’alam Al-Kutub] anasema: “Kufuga ndevu zake na kuharamishwa kuzinyoa’. [Mwisho]
Na hii ni hoja iliyochaguliwa na baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Imamu Shafi, miongoni mwao ni; Al-Qafal Ash-Shashiy, na mwanafunzi wake Al-Hulaimiy, Ibn Ar-Rifa’ah, ambaye ameinukuu kutoka katika andiko la Al-Umm, Al-Adhrii’iy, Az-Zarkashiy, pamoja na Mtaalamu Ibn Ziyad Al-Yamaniy katika fatwa zake, Sheikh Zain Ad-Diin Al-Millibariy mtungaji wa kitabu cha: [Fat-h Al-Mui’ii] Tazama: [Hashiyat Ibn Qasim Al-A’abbadiy Ala Tuhfat Al-Muhtaj, na Ibn Hajar: 99/376-377, Ch. Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy; Mukhtasar Al-muhimat, na Az-Zarkashiy, L/36, Muswada wa Maktabat A’atif Afandiy, Isanbul, nambari: 1050; Ghayat Talkhis Al-Murad Min Fatawa Ibn Ziyad, Uk. 81, Bihamish Bughiat Al-Mustarshidin Fi Talkhis Fatawa Ba’dh Al-Aimmah Minal Ulamaa Al-Mutaakhiriin, na Saiyd Abdur-Rahman Ibn Muhammad Ibn Umar Ba’alawiy, Mufti wa Miji ya Hadhramiyah; Fat-h Al-Mui’iin na Sharh yake: Ia’anat At-Twalibiin na Dimyatiy: 2/386, Ch. Dar Al-Fikr].
Na dalili yao ni Hadithi sahihi, kutoka kwa Ibn Omar R.A., kuwa Mtume S.A.W, amesema: “Wapingeni washirikina, fugeni ndevu, na punguzeni masharubu”. Na Hadithi hii ndiyo dalili ya uwajibu, kwa maoni ya wanazuoni hawa, kutokana na sababu mbili: Kwanza: kuhusu amri, kwa sababu asili ya maana ya amri ni kuonesha uwajibu. Pili: sababu ya amri hii ni kuwapinga washirikina, na kwamba kulinga nao ni haramu, na kuwapinga ni wajibu; kwa ilivyopokelewa na Abu Dawud, kutoka kwa Ibn Omar R.A., kuwa Mtume S.A.W., amesema: “Mwenye kujifafanisha na wengine, basi yeye ni miongoni mwao”.
Kuhusu madhehebu ya Shafiy jambo linalotambuliwa liwe Fatwa ni kuwa kufuga ndevu ni jambo linalopendeza, na kuzinyoa ni jambo linalochukiza; Imamu Siraju-Diin Ibn Al-Mulaqin katika kitabu chake: [Al-Ii’laam Bi Fawaid Umdat Al-Ahkaam 1/712, Ch. Dar Al-A’asimah] anasema: “Jambo linalojulikana katika madhehebu ni kuchukiza”. [Mwisho]
Na rai hii ndiyo iliyotambuliwa na wanazuoni wawili wa madhehebu, nao ni Imamu Abul Qasim Al-Rafii’iy na Imamu Muhiy Diin An-Nawawiy, kisha wanazuoni wawili wa sasa ambao ni Imamu Shamsu Diin Muhammad Ar-Ramliy na Imamu Shihabu Diin Ahmad Ibn hajar Al-Haitamiy, na wengi wengine wa wanazuoni wa madhehebu, ambao wana jukumu la kuteua hoja yenye nguvu na utambulisho, na kujuzisha kwa rai yenye nguvu zaidi na rai yenye nguvu ndogo na rai inayotegemewa katika Fatwa ndio inayonasibishwa nao na kutegemewa kwao.
Na Mtaalamu Ibn Hajar katika kitabu cha: [Sharh Al-U’ubaab] anasema: “Wanazuoni wawili Al-Rafii’iy na An-Nawawiy walisema: kuzinyoa ndevu ni jambo linalochukiza”. [mwisho] [Hashiyat Ibn Qasim Al-A’abbadiy Ala Tuhfat Al-Muhtaj na Ibn Hajar: 9/376, Bihamish na Hashiyat Ash-Sharwaniy, Ch. Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy].
Na hii ni ibara ya wazi ya Imamu An-Nawawiy katika kitabu chake [At-Tahqiiq L/7, mswada wa Maktabat Al-Azhar Ash-Sharif: 2820/104501, Fiqh Aam] ambapo anasema: “inachukiza kuziondoa mvi, kupunguza nywele za nyusi, ndevu, nywele za mdomo wa chini, kuzitia rangi nywele, kuchana ndevu, (kwa safu) kuzisokota, kuzinyoa, kuzinyonyoa, na hasa zinapokuwa changa, na kuzikata”. [Mwisho]
Na mfano wa hayo unapatikana katika kitabu cha: [Sharh Muslim 3/149, Ch. Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy], ambapo alizingatia kuzinyoa ndevu ni miongoni mwa mambo yanayochukiza.
Na kabla ya wanachuoni hawa wote, alikuwapo Hojat Al-Islam Al-Ghazaliy, kama inavyobainika kwa maneno yake katika kitabu cha: [Ihiyaa Uluum Ad-Din: 1/143, Ch. Dar Al-Maa’rifah, Bairut] ambapo alitaja kuwa kuna mambo kumi ya kuchukiza kuhusu ndevu, na miongoni mwayo ni kuzinyonyoa, na kuzinyonyoa na kuzinyoa ni sawa, isipokuwa kuzinyonyoa kuna athari kubwa zaidi, kwa sababu kunyoa kunabaki mizizi ya nywele, lakini kunyonyoa ni kuzing’oa nywele mizizini yake.
Sheikh wa Uislamu Zakariya Al-Ansariy katika kitabu cha: [Asna Al-Matalib 1/551, Ch. Dar Al-Kitab Al-Islamiy] anasema: “Inachukiza kuzinyonyoa ndevu, zinapokuwa changa kwa ajili ya kupata kupendeza na sura nzuri”. [Mwisho]
Na Imamu Shihabudin Ahmad Ar-Ramliy katika Hashiya yake ameeleza: “kauli yake; inachukiza kuzinyonyoa ndevu… n.k, na mfano wake kuzinyoa, na kauli ya Al-Hulaimiy katika Minhaj yake: Hairuhusiwi kwa mtu kuzinyoa ndevu zake na nyusi zake ni kauli dhaifu’. [Mwisho]
Na katika kitabu cha: [Fatwa za Ash-Shihab Ar-Ramliy [4/69, Ch. Al-Maktabah Al-Islamiyah] pia imetajwa kuwa aliwahi kuulizwa: Je, inaharamishwa kuzinyoa ndevu na kuzinyonyoa au la? Akajibu kuwa: “Kuzinyoa ndevu na kuzinyonyoa ni jambo linalochukiza na siyo haramu. Na kauli ya Al-Hulaimiy katika Minhaj yake kwamba: hairuhusiwi kwa mtu yoyote kuzinyoa ndevu na nyusi zake ni kauli dhaifu”. [Mwisho]
Na anasema Mwanae Mtaalamu Mhakiki, ambaye ni Shamsudin Muhammad Ar-Ramliy katika kitabu cha: [Nihayat Al-Muhtaj 8/149, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Inatakiwa kuzigawa nywele, kuzichana ndevu, na inachukiza kuzinyonyoa na kuzinyoa”. [Mwisho]
Na Imamu Ibn Hajar katika kitabu cha: [Tuhfat Al-Muhtaj 9/376, Ch. Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy] alitaja kuwa: kauli ya kuharamisha kuzinyonyoa ndevu na kuzinyoa ni kinyume cha rai inayotambuliwa, na maelezo yake yatatolewa baadaye inshaallah.
Na Mtaalamu Al-Khatib Ash-Shirbiniy katika kitabu cha: [Al-Iqnaa' 4/346, na Hashiyat Al-Bijirmiy, Ch. Dar Al-Fikr] anasema: “Inachukiza kuzinyoa ndevu hali ya kuwa changa, kwa ajili ya kupata uzuri’. [Mwisho]
Na mwenye Hasiyat Al-Bijirmiy anasema: “Kauli yake: hali ya kuwa kwake bado changa, hilo silo sharti, kwa kuwa mtu mzima ni mfano wake, kwa maana: kuzinyoa ndevu ni jambo linalochukiza hata kwa mtu mzima, na siyo haramu, na huenda aliainisha hivyo kwa kauli yake: kwa ajili ya kupata uzuri’. [Mwisho]
Na Mtaalamu Shihabudin Al-Qalyubiy katika Hashiyat zake kwa [Sharh Al-Mahalliy ya Al-Minhaj 4/205, Bi Hamish Al-Mahalliy na Hashiyat Amirah, Ch.Mustafa Al-Halabiy] anasema: “Kauli sahihi zaidi ni kuwa: inachukiza kuzinyoa ndevu kwa nafsi yake mwenyewe”. [Mwisho]
Na haikatazwi kuwa hukumu hii ni ya kutambuliwa kwa namna ilivyosemwa kuwa Imamu Shafiy alisema maneno katika kitabu cha: [Al-Ummu] ambapo inafahamika kwacho uharamu wa kunyoa, au kwa ilivyotangulia kuwa uteuzi wa baadhi ya wanazuoni wa madhehebu ya Shafiy, kwa sababu wanazuoni hawa wa sasa ima wawe watangulizi wa wanazuoni wawili hawa, au miongoni mwa wafuatao baada yao; kuhusu watangulizi wa wanazuoni wawili kwa mfano Al-Qaffal na Al-Hulaimiy, kutoa Fatwa kwa kutegemea vitabu vya watangulizi wake na kuyazingatia haya kama ni madhehebu, ni jambo linalokanushwa.
Na Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha: [Al-Majmuu’ 1/81, Ch. Al-Muniriyah] anasema: “Haijuzu kwa Mufti anayefuata madhehebu ya Imamu Shafi wakati anapotegemea kunukulu achague kitabu kimoja au vitabu viwili miongoni mwa vitabu vya wanazuoni wa zamani, au wengi wa sasa; kwa sababu kuna mabadiliko mengi kati yao kuhusu uamuzi halisi na kuteua hoja yenye nguvu; kwa sababu Mufti huyo hakika ananukulu madhehebu ya Imamu Shafiy, lakini anakuwa hana yakini kuwa vinapatikana katika vitabu viwili hivyo na vinginevyo ndiyo ya madhehebu ya Imamu Shafiy au hoja yenye nguvu ndani yake, kutokana na mabadiliko yaliyomo katika vitabu hivyo.
Na hii haina shaka yoyote kwa yule anayeambatana na madhehebu hata ikiwa ni kidogo, kwa hiyo pengine kuna watunzi kumi wanaoihakiki hukumu moja na hakika yake siyo ya kawaida kutokana na ilivyoamuliwa katika madhehebu, na pia inapinga rai ya wengi wa wanazuoni, na huenda ikawa inapinga rai ya Imamu Shafiy au maneno yake”. [Mwisho]
Kuhusu maneno ya Al-Qaffal na Al-Hulaimiy yanaweza kulinganishwa na maana ya jambo linalochukiza, ikiwa tamko lake ni (hairuhusiwi), na kulinganishwa na maana ya (kutoruhusu) inayokusanya pia (jambo linalochukiza), kwa kuwa jambo linalochukiza siyo halali, yaani siyo mubaha. Na Mhakiki Ibn Hajar ameashiria hivyo, ambapo alisema katika kitabu cha: At-Tuhfah 9/375-376]: “Walitaja kuhusu ndevu, mambo yanayochukiza, miongoni mwake ni: kuzinyonyoa, kuzinyoa, na pia kunyoa nyusi, na haipingwi na kauli ya Al-Hulaimiy: (haijuzu hivyo); kwa kuweza kuelewa muradi wake na kukanusha uhalali wa uwiano wa pande mbili".
Na kuchagua maana inayofaa, ikiwa tamko ni (hairuhusiwi) basi maana ni ile ile, au (inaharamishwa) basi ni kinyume cha rai inayotambuliwa. [Mwisho]
Na kuhusu wanazuoni wanaofuata Mashekhe hawa wawili, maneno yao hayakupewa kipaumbele na maneno ya Mashekhe wawili, na hii ni rai inayojulikana katika madhehebu; kama ilivyotajwa katika kitabu cha: [Al-Fawaid Al-Makkiyah Fiimaa Yahtajuhu Talabat Ash-Shafiiyah] na Bwana Ulwiy As-Saqaaf Mufti wa madhehebu ya Shafiy, Makkah Takatifu, karne iliyopita [Uk. 36, kati ya vitabu saba vizuri]:
“Sheikh Ibn Hajar na wengineo, miongoni mwa wanazuoni wa sasa, wanasema: wahakiki walikubaliana kwa pamoja kuwa vitabu vilivyowatangulia Mashekhe wawili: Ar-Rafii’iy na An-Nawawiy, havizingatiwi isipokuwa baada ya uchunguzi kamili na ukaguzi, mpaka kufahamika kuwa rai yenye nguvu zaidi katika madhehebu ya Imamu Shafiy. Kisha wakasema; hii inahusu hukumu ambayo haikujadiliwa na Mashekhe wawili, lakini wakiijadili; kauli ya pamoja ya Wahakiki kuwa: walikubaliana kuwa ni ya kuzingatiwa”. [Mwisho]
Mhakiki Sheikh Muhammad Ibn Suleiman Al-Kurdiy mfuasi wa madhehebu ya Shafiy katika kitabu chake: [Al-Fawaid Al-Madaniyah Fiman Yufta Bi Qaulihi Min Aimmat Ash-Shafiiyah Uk. 36, Ch. Dar Al-Faruuq] anasema: “Ilivyokubaliwa na Wahakiki wa sasa, na Mashekhe wetu hawaachi kuwanasihi na wangaliinukulu kwa Mashekhe wao na waliokuwa kabla yao kuwa: rai ya kutambuliwa ni ile wanayo kubaliana Ar-Rafii’iy na An-Nawawiy; na kutokuwepo kauli ya pamoja ya wasomaji wa maneno yao kuwa kuna kusahau, na iweje?!”. [Mwisho]
Na inavyoainisha kauli ya kuwa jambo linalochukiza ni ya kutambuliwa kwenye madhehebu ya wafuasi wa Shafiy kuwa hoja inayokubaliwa na Sheikh wa Uislamu Zakariya Al-Ansariy na wataalamu wa sasa Ibn Hajar, Ash-Shams Ar-Ramliy, na Al-Khatwib Ash-Shirbiniy, kama tulivyonukulu hapo juu. Na Mtalamu Abu Bakr Muhammad Shata Al-Bakriy Ad-Dimyatiy katika kitabu cha: [Ia’anat At-Talibin Ala Hall Alfadh Fat-h Al-Mui’in 2/386, Ch. Dar Al-Fikr], kwenye kauli ya Al-Millibariy “Inaharamishwa kuzinyoa ndevu” alisema: “kauli ya kutambuliwa ya Al-Ghazaliy, Sheikh wa Uislamu, Ibn Hajar katika kitabu cha: [At-Tuhfah, Ar-Ramliy, Al-Khatwib], na wengineo ni: jambo linalochukiza’. [Mwisho]
Na Mtaalamu Al-kurdiy katika kitabu cha: [Al-Fawaid Al-madaniyah Uk. 56] anasema: “Wanapokutana Sheikh wa Uislamu, Ibn Hajar, Ash-Shams Ar-Ramliy, na Ash-Shirbiniy, basi kauli yao ni ya kuzingatiwa na kupewa uzito; kwa sababu Zakariya, Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa na ngazi ya juu katika kuzisoma matini, na Ibn Hajar ni mjuzi wa mapokezi na kuhakiki njia za Mashekhe wawili, na Al-Jamal Ar-Ramliy anajulikana kwa ukaguzi wa kunukuu na vitabu vyake vimekubaliwa na wanazuoni wa ngazi ya juu wa Misri, na mfano wake ni Ash-Shirbiniy… na mfano wake ni Ash-Shihab Ar-Ramliy”. [Mwisho]
Katika kitabu cha: [Al-Fawaid Al-Makkiyah Uk. 37] kunukulu na Al-Kurdiy kuwa alisema: “Wanazuoni wa Zamzamu (yaani wanazuoni wa Msikiti Mtakatifu) walifuata maneno yao, wakakuta ndani yake asili ya madhehebu ya Imamu Shafiy R.A., na kwa maoni yangu hasa haijuzu kutoa Fatwa kwa inavyowapinga hawa: Ar-Ramliy na Ibn Hajar, na pia At-Tuhfah na An-Nihayah, isipokuwa wasiyoyajadili hapo kutoa Fatwa kwa maneno ya Sheikh wa Uislamu, kisha kwa maneno ya Al-Khatib… n.k.”. [Mwisho]
Na sababu muhimu ya kuweka mbele maneno ya Ibn hajar na Ar-Ramliy katika vitabu vyao: (At-Tuhfah na An-Nihayah) na kuzingatia waliyoyasema kuwa: vitabu hivyo vimekwisha somwa na wanazuoni wa madhehebu ya Imamu Shafiy, kisha wamevirekebisha na wakayakubali masuala na hukumu yaliyomo ndani yake.
Mtaalamu As-Saqaaf katika kitabu cha: [Al-Fawaid Al-Makkiyah Uk. 37]: anasema: “Wanazuoni wa Misri au wengi wao walielekea kuyatambua aliyoyasema Sheikh Muhammad Ar-Ramliy katika vitabu vyake, hasa katika mwisho wake, kwa sababu vitabu hivi vimesomwa kikamilifu mbele ya mtungaji, na wanazuoni mia nne, na wao wakavikosoa na kuvirekebisha, na usahihi wake wamefikia ngazi ya uhakiki zaidi.
Na wanazuoni wa Hadhramaut na Sham, Wakurdi, Daghistan, na wengi wa Yemen, Hijaz walielekea kuwa: yaliyotambuliwa ni aliyoyasema Sheikh Ibn Hajar katika vitabu vyake, hasa [At-Tuhfah], kwa yaliyomo ndani yake ya mkusanyiko wa matini ya Imamu, pamoja na ukaguzi zaidi wa mtungaji, na kusoma kwa wahakiki wa vitabu hivyo mbele yake, na idadi yao haiwezekani kuhesabiwa”. [Mwisho]
Kuhusu ilivyonukuliwa na baadhi ya wanazuoni wa sasa kutoka kwa Imamu Najmudin Ibn Ar-Rifa’ah kuwa alitaja katika Hawashiy Al-Kifayah kuwa: Imamu Shafiy alitaja katika kitabu cha Al-Ummu: uharamu wa kunyoa, hapa haisihi kuwa dalili ya kupinga yaliyotambuliwa katika madhehebu; kwa sababu matini ni: tamko lenye maana pekee, na haichanganyiki na mengine [Jamu’ul Jawamii’ Bisharh Al-Mahaliy na Hashiyat Al-A’attar: 1/308], na Ibn Ar-Rifa’ah alidai kuwa Imamu Shafiy amekwisha taja uharamu wa kunyoa, kisha hakutuonesha matini hiyo, ili tuweze kuona kuwa matini hii ni ya wazi kuhusu uharamu, au ni ibara ya kawaida yenye maana mbali mbali?
Jambo muhimu hapa kuwa matini hii ingelikuwa wazi basi angeliitaja, kisha ingelikuwa mashuhuri kati ya watu na ndani ya vitabu, hasa hilo ni suala ambalo wahariri wa madhehebu inafikiriwa kuwa wameipinga matini inayoandikwa. Na sisi hatukukuta, baada ya ukaguzi, matini wazi inayoonesha maana hiyo ndani ya nakala tuliyo nayo ya kitabu cha Al-Ummu, nayo ni nakala ya kuchapishwa, kupitiwa, kuhaririwa, kurekebishwa na mwenye kueleza ambaye alieleza robo ya ibada ya kitabu hicho, katika juzuu ishirini na tano, yangali miswada katika Jumba kuu la Vitabu, naye ni Mtaalamu Mhakiki Sheikh Ahmad Bik Al-Huseiniy, mwanafunzi wa Sheikh wa Uislamu Shamsudin Al-Inbabiy, baada ya kuzikusanya nakala zake mbali mbali kutoka kwa miji kadhaa, kisha alikichapisha katika Kampuni ya Serikali ya Misri, Mwaka 1326 H.
Alisema, Mungu amrehemu, akizungumzia ailvyofanya kwa ajili ya kuirekebisha matini ya kitabu cha Al-Ummu katika utangulizi wa maelezo yake yaitwayo: Murshidul Anaam Ila Brri Ummil Imam [Juzuu la kwanza ya utangulizi – L/10, mswada wa Jumba la Vitabu la Misri, Nambari: 1522- Fiqhi Shafiy]: “Nilikitafuta kitabu hiki (Al-Ummu) kutoka mahali pake, nikafunga nia halisi kusafiri mahali pa kuwepo kwake, kwa ajili ya kupata johari na uzuri wake, na kueleza hakika za kweli za ulimi wake, lakini sikukuta miji ya Misri, ingawa kuwepo mengi ya majumba ya vitabu ndani yake, isipokuwa juzuu kadhaa zenye mabadiliko na taratibu mbaya, ambapo hatuwezi kuelewa ibara zake wala nidhamu yake, kwa hiyo nilielekea safari upande wa miji isiyo ya Misri kutafuta maktaba zenye vitabu, mpaka upole wa Mwenyezi Mungu na Rehema yake zimenifikisha lengo kuu na shabaha njema, nayo ni; kupata nakala kamili ya kitabu.
Na sikusikia habari ya kuwepo nakala au sehemu ya kitabu hiki mahali popote, isipokuwa kufanya juhudi kukipata, mpaka Mwenyezi Mungu amerahisisha kupata nakala nyingi, ambazo nimezitegemea kuitoa nakala moja yenye usahihi kabisa, hivyo matumaini yapo, kwa hiyo nimesujudu kumshukuru Mwenyezi Mungu, na moyo wangu umejaa kwa sifa zake njema na shukuru… n.k.,” [Mwisho]
Kuhusu ilivyodaiwa kuwa dalili ya Imamu Shafiy ya uharamu ni kauli yake katika kitabu cha: [Al-Ummu 6/88]: “Kama mtu mshari akinyoa nywele za mwingine, kisha nywele zikakua tena kama ilivyokuwa au bora zaidi ya ilivyokuwa hapo kabla, basi hatakuwa na malipo ya fidia, kwa sababu kunyoa nywele bila ya idhini ya muhusika siyo kosa la jinai, kwa sababu kunyoa nywele kunaambatana na ibada ya Hija, na hakuna kuumia, hata ikiwa unyoaji huo haujuzu kwa ndevu, lakini hauumizi wala kupoteza nywele, kwa sababu zinakua upya”. [Mwisho]; kuzingatia maneno haya kama dalili ya uharamu ni kosa, kwa sababu maneno haya siyo matini inayomaanisha uharamu; na kama ilivyotajwa hapo juu kuwa matini ni: tamko lenye maana pekee, na halichanganyiki na mengine, na ufafanuzi huu haupatikani katika maneno haya, kwa sababu kauli yake “hata ikiwa unyoaji huo haujuzu kwa ndevu” inaweza kumaanisha: kuzinyoa nywele bila ya idhini au kumaanisha kunyoa kwa kawaida. Vile vile kauli yake “Haijuzu” haimaanishi uharamu weyewe, kwa sababu “Jambo linalochukiza” pia inaweza kuelezwa kwa (haijuzu).
Mfano wa hayo kauli ya Imamu As-Shafiy katika kitabu cha: [Al-Ummu 1/281]: “Haijuzu, kwa rai yangu, kuacha Swala ya kupatwa Jua kwa msafiri na mkazi na mtu yeyote anayeweza kutekeleza swala kwa vyovyote’. [Mwisho]
Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha: [Al-Majmuu’ 5/60, Ch. Al-Muniriyah] baada ya kunukulu ibara iliyotajwa hapo juu ya (Al-Umm): “kauli yake (haijuzu kuacha Swala ya kupatwa Jua) huenda kutatanisha, na inajuliakana kuwa ni Sunna bila ya kupinga.
Na jibu lake kuwa muradi wake ni kwamba: inachukiza kuziacha, kwa sababu ya kutilia mkazo. Na Hadithi nyingi zilizoamuru kutekeleza, kama vile kauli yake Mtume S.A.W.: “Hakika Jua na Mwezi ni alama mbili miongoni mwa alama za Mwenyezi Mungu, na hazipatwi kwa ajili ya maisha ya mtu ye yote wala kufa kwake, lakini mkiona hivyo, basi ombeni Mwenyezi Mungu na semeni takbira na swalini na toeni sadaka”, na katika mapokezi mengine: “nendeni haraka kwa ajili ya Swala” au “Swalini mpaka kuishe”, au “Swalini mpaka vikapambazuka”, na tamko ni kuwa hayo yote yametajwa katika Vitabu viwili sahihi, na Imamu Shafiy alitaka kuwa inachukiza kuiacha; kwa sababu huenda jambo linalochukiza linaelezwa kuwa kutojuzu, ambapo linajuzu linaitwa kwa pande zinazolingana, lakini jambo linalochukiza si hivyo”. [Mwisho]
Na katika sehemu nyingine ya kitabu chenyewe, aliinukulu kwa wana misingi ya Fiqhi kwa uwazi, akisema [5/287]: “Jambo linalochukiza ni kutojuzu kwa wana misingi ya Fiqhi”. [Mwisho]
Na kama matini hiyo inayodaiwa ikikubalika kuwa ni wazi iwe dalili ya suala hili, lakini haizingatiwi iwe kauli ya Imamu Shafiy R.A., na haizingatiwi kuwa madhehebu yake wala kuionesha kwa njia ya wanazuoni waliotangulia, na hivyo haizingatiwi kuwa kuweka kauli ya wafuasi kipaumbele cha kauli ya Imamu, kama wanavyodhani baadhi ya wasioelewa; lakini kwa sababu, hii ni aina ya kupingana katika madhehebu, na misingi ya madhehebu na masuala yake hakika zimenukuliwa kwa njia ya midomo na usikilizaji tabaka baada ya tabaka.
Na kuhusu ilivyotajwa katika kitabu kimoja ama ni nakala madhubuti na Isnad yake ni sahihi kwa mtungaji wake, au ni nakala isiyotambuliwa kabisa; kama ikiwa moja ya hayo ni sahihi, basi haiwezekani kupingana na madhehebu iliyonukuliwa kundi kwa kundi, kwa hiyo wanazuoni walitaja kuwa: haijuzu kuwapinga Mashekhe wawili hawa kwa kutegemea matini ya (A-Ummu), si kwa kuwa maneno yao yanatangulizwa mbele ya maneno ya Imamu Shafiy, lakini kwa sababu iliyotajwa hapo juu, na Mashekhe wawili waliyasoma matini ya Imamu, wakazidhibiti kauli zake, wakavipata vitabu vyake kutoka kwa nakala zake zilizotambuliwa, ambapo haisihi kuzipinga kwa matini iliyokutwa katika kitabu kimoja au nakala moja.
Mhakiki Ibn Hajar katika kitabu cha: [Sharh Al-U’ubaab na Al-Fawaid Al-Madaniyah, na Al-Kurdiy: Uk. 37] anasema: “Wahakiki walikubali kwa pamoja kuwa rai inayotolewa Fatwa ni ile iliyotajwa na An-Nawawiy na Ar-Rafii’iy, ambapo haitolewi Fatwa kwa rai ya wale waliowapinga kwa mujibu wa matini ya Al-Ummu au maneno ya wengi wa wanazuoni au wengineo; kwa sababu Mashekhe wawili hawa ni wenye elimu zaidi ya matini na maneno ya wanazuoni kuliko wale wanaowapinga, na Mashekhe hawakumpinga Imamu Shafiy isipokuwa kuwepo hoja ambayo baadhi ya wanazuoni waliielewa, na wengine hawakuielewa.
Na dalili ya usahihi wa hayo kuwa: Mashekhe walieleza kuwa ni jambo linalochukiza kwa anayeongozwa na Imamu wa Swala anainuka juu yake mahali popote, bila ya kuainisha ikiwa msikiti au penginepo, lakini baadhi ya wanazuoni wa sasa walipinga kuwa Imamu alitaja katika kitabu cha: [Al-Ummu] kuwa ni jambo linalochukiza, hayo yanaambatana na kitu kingine, na wengi wa wanazuoni waliifuata, hata mimi mwenyewe niliwafuata kwa muda mrefu, mpaka niliona matini nyingine ya Imamu Shafiy R.A, inayoonesha kuwa jambo linalochukiza la kuwa katika muinukoni ndani ya msikiti; kwa hiyo alichukia Swala ya Imamu ndani ya Kaaba wakati anayeongozwa yuko nje yake, na akaeleza hivyo kwa kuinuka juu yake.
Basi tazama vipi walijua kuwa Imamu Shafiy ana matini mbili lakini walichagua moja tu? Kwa sababu kuinuka mmoja juu ya mwingine kunaharibu ufuatano kamili unaotakiwa kati ya Imamu wa Swala na Maamuma, wakati waliiacha matini nyingine, kwa kupinga Qiyasi kilichotajwa, siyo bure lakini kwa ajili ya shime ya uchunguzi wa mambo ya dini zimewapelekea hivyo, na ingelitiliwa mkazo wa kukagua vitabu vya Imamu Shafiy na wanazuoni wa madhehebu ingelionekana kuwa wao hawaipingi matini yake isipokuwa kwa ajili ya iliyo na nguvu zaidi kuliko hiyo”. [Mwisho]
Katika Fatwa za Imamu Shihabu Ar-Ramliy [4/262-263, Ch. Al-Maktabah Al-Islamiyah]: “Aliulizwa ikiwa matini mpya ya Imamu Shafiy itaipinga rai ya Mashekhe wawili, basi ipi itekelezwe? Mkisema: ni matini, basi vipi wanazuoni wa wakati wetu wanakana rai ya wale wanaopinga maneno ya Mashekhe wawili au mwelekeo wao? Walieleza kuwa matini ya Imamu inayoambatana na mfuasi ni kama dalili yenye nguvu zaidi, basi vipi wanaiacha wakati wanataja maneno ya wanafunzi? Akajibu kuwa; inajulikana kuwa Mashekhe, Mungu awarehemu, wamejitihadi sana kwa ajili ya kudhibiti madhehebu, kwa hiyo uangalifu wa wanazuoni watendaji na ishara za waliotutangulia miongoni mwa Maimamu wenye uhakiki zikielekea ukubalifu wanayoyaona Mashekhe, na kuchukua waliyoyarekebisha kwa ukubalifu na ridhaa, wakategemeza hayo yote kwa dalili na hoja.
Katika hali ya upweke wa mmoja wao mbali na mwingine, inachukuliwa kwa rai ya Imamu An-Nawawiy, kwa kuangali nia nzuri na dhamiri halisi. Kuna upinzani dhidi ya Mashekhe wawili na wengineo kuwa wao wameipinga matini ya Imamu Shafiy, na hayo hutokea mengi, hata ikisemwa kuwa: wanafunzi mbele ya Imamu Shafiy ni mfano wa Imamu Shafiy na wenye jitihada wengine mbele ya matini ya Mwenye sheria, kwa hiyo haisihi kujitahidi pamoja ya uwezo wa kupata matini. Ikajibiwa kuwa: hii ni rai dhaifu, kwa sababu hii ni ngazi ya watu wa kawaida, lakini waliogobea katika madhehebu basi wana ngazi ya jitihada maalumu, na hii ni njia ya wakuu wenye uwezo wa kueleza na kuleta dalili yenye nguvu zaidi. Na suala la kuwa Mashekhe wawili waliacha kutaja matini iliyoashiriwa hapo juu kwa sababu kuwa dhaifu, au inaambatana na dhaifu, wakati wanafunzi waliacha matini zake wazi, kwa sababu ya kuzipinga kanuni zake, kwa hiyo wakazieleza… basi haikubaliki kuwakanusha wanafunzi wakizipinga matini.
Na haisemwi kuwa: hawakuzisoma; na hii ni ushahidi wa kukanusha, bali ni wazi kuwa wao walizisoma, na wakazigeuza asili yake kwa kutumia dalili, na kwa hivyo hawakuwa mbali na ufuasi wa Imamu Shafiy, na kuwa mwenye jitihada anaugeuza udhahiri wa matini ya Mwenye sheria kwa sababu kama hiyo, wakati hakuwa mbali na ufuasi wake, na hii inatosha kwa mwenye insafu”. [Mwisho]
Imamu Ibn Ar-Rifa’ah mwenyewe hakunukulu maneno haya katika msingi wa maelezo yake ya kitabu cha At-Tanbiih kiitwacho (Kifayat An-Nabiih), lakini aliyataja chini ya ukurasa na Hashiyah, kwa mujibu wa kunukulu kutoka kwake, na yaliyotajwa katika msingi na asili ya kitabu cha: [Al-Kifayah 1/253, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] ni:
Kunukulu kutoka kwa An-Nawawiy katika kitabu cha: [Ar-Rawdhah] kuwa inachukiza kunyonyoa ndevu hali zikiwa changa; kwa ajili ya uzuri na sura nzuri, hapa Ibn Ar-Rifa’ah hakujibu, kama kwamba anaikiri, ama kwa matini ya [Al-Ummu], wala nyingine, na vilevile Al-Jamal Al-Isnawiy hakujibia kwa kitu katika kitabu chake kiitwacho [Al-Hidayah], ambaye alikitunga hasa kwa kumjibu Ibn Ar-Rifa’ah katika kitabu chake [Kifayat An-Nabiih].
Hakika tumerefusha majadiliano katika taarifa ya madhehebu ya wafuasi wa Imamu Shafiy, kwa sababu wengi ambao walijaribu kuandika katika suala la hukumu ya ndevu hawaleti usahihi wake, kisha wakaendelea haraka kuunganisha uharamu kwa madhehebu na wanaujasiri wa kosoa Maimamu wa madhehebu wanaosema kuwa rai inayotambuliwa ni jambo linalochukiza.
Kundi la wanazuoni miongoni mwa madhehebu mengine wamekubali rai ya wafuasi wa madhehebu ya Imamu Shafiy, ambapo matini zao huashiria uharamu; miongoni mwa wanazuoni hawa: Kadhi I’iyadh mfuasi wa madhehebu ya Malik katika kitabu cha: [Ikmalul Mu’lim 2/63, Ch. Dar Al-Wafaa] ambapo anasema: “Inachukiza kuzinyoa, kuzikata, yaani ndevu”. [Mwisho], na Mtaalamu Al-Ubiy mfuasi wa madhehebu ya Malik ameinukulu kutoka kwake katika kitabu cha: [Sharh Muslim 2/39, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], na hakumjibu.
Katika kueleza Hadithi ya Abdullahi Ibn Omar R.A., kuwa: Mtume S.A.W, aliamuru kuyanyoa masharubu na kuzifuga ndevu, Sheikh Muhammad Ibn Abdil Baqiy Az-Zurqaniy Al-Misriy mfuasi wa madhehebu ya Malik katika kitabu cha: [Saharh Al-Muwatwa' 4/529, Ch. Maktabat Ath-Thaqafah Ad-Diniyah] anasema: "(aliamuru) kwa njia ya kutakiwa, na kusemwa: kwa njia ya uwajibu”. [Mwisho]
Na Imamu Ibn Qudamah katika kitabu cha: [Al-Mughniy 1/66, Ch. Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy] anasema: “Kuhusu kuondosha nywele za uso, akasema Muhanna: nilimuuliza Abu Abdillahi, yaani Imamu Ahmad kuhusu kuondosha nywele za uso, akasema: hakuna ubaya kwa wanawake, na mimi nachukia kwa wanaume”. [Mwisho] Na maana ya kuondosha ni: kuziondosha nywele kwa wembe. [Tazama: Lisaan Al-Arab, na Ibn Mandhuur: 9/50, Ch. Dar Saadir].
Kutumia tamko la jambo linalochukiza au jambo linalochukiza kwa uwazi, ambapo baadhi ya Salaf wanalitumia kwa maana ya uharamu, lakini pasipo na dalili ya kuonesha hiyo, basi maana yake inabakia hiyo hiyo ya istilahi, ambapo mtendaji wake haadhibiwi.
Kwa hiyo baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Hanbal walieleza kuwa: kufuga ndevu ni amri ya kutakiwa kufanya hivyo, na hawakuonesha uwajibu wake au ukubwa wa kufuga; Ibn Muflih mfuasi wa madhehebu ya Hanbal katika kitabu cha: [Al-Adaab Ash-Shari’iyah: 3/329, Ch. A’alam Al-Kutub] anasema: “Mwanamume kufuga ndevu zake ni Sunna”. [Mwisho], na Sunna huenda inakusanya sehemu ya wajibu, kwa maana ya kuwa ni mapokezi ya Mtume S.A.W., lakini asili yake ni kuonyesha tendo linalotakiwa. Na mfano wa hayo walieleza wanazuoni wengine; Imamu Shamsu Diin Al-Maqdisiy katika kitabu cha: [Ash-Sharh Al-Kabiir Ala Matn Al-Muqni’ 1/105, Ch. Dar Al-Kitaab Al-Arabiy] anasema: “Inatakiwa ndevu zifugwe”. [Mwisho]
Sheikh Ibn Abdil Qawiy katika Kasida yake [I’iqdul Faraid wakanzul Fawaid 1/15] anasema:
Inachukiza kwa wanaume kuondosha nywele za uso
Vile vile kunyoa kichogo kwa ajili ya matini
Na inatakiwa kuzifuga ndevu, kwa kiasi cha
Chini ya koo na ziada ya ngumi.
Katika kitabu cha: [Fathul Malik Al-Aziz Bisharh Al-Wajiiz, na Ibn Al-Bahaa Al-Baghdadiy mfuasi wa madhehebu ya Hanbal 1/223, Ch. Dar Khidr, Bairut]: “Inatakiwa kuzifuga ndevu… na inachukiza kuzikata kiasi kisicho chini ya ngumi, alitaja hivyo, kwa sababu Sunna ni kuzifuga ndevu, na sisi hatukuchukia kuzikata zinazozidi ngumi kwa ajili ya tendo la Ibn Umar; kwa sababu yeye ni mpokeaji wa Hadithi na mjuzi sana kwa kusudio lake, na kinyume cha hivyo ni kinyume cha maumbile”. [Mwisho]
Wanazuoni wawili wa Moroko walitunga katika kunusuru kauli ya jambo linalochukiza pamoja na dalili na sababu, wao ni: Bwana Abdulhai Ibn As-Siddiq Al-Ghimariy katika kitabu chake: [Al-Hujatu Ad-Damighah Ala Butlan Daa’wa Man Zaa’ama Anna Haaliqa Allihiyati Malu’unun wa Salatuhu Batilah], na ndugu yake Bwana Abdulaziz, Mungu awarehemu, katika kitabu chake: [Ifadatu Dhawiy Al-Afham Bianna Halqa Al-Lihiyati Makruhun Walaisa Biharam] Na utoaji dalili utatajwa baadaye.
Na baadhi ya wanazuoni wa sasa walielekea kuwa kuzifuga ndevu ni aina ya mazoea, na siyo ya mambo ya ibada, na amri inayoambatana nayo ni kwa ajili ya kuongoza na siyo ya uwajibu au inayotakiwa, na hiyo inatajwa na Sheikh Muhammad Rashid Ridha katika Fatwa yake ya Gazeti la Al-Manaar [22/429] ambapo anasema: “Jawabu la suala la kuzinyoa ndevu: suala hili na mifano yake itakayotajwa baadaye silo la mambo ya dini ambayo anayoabudiwa Mungu kwa kutenda au kuacha, lakini ni mambo ya kawaida yanayoambatana na urembo, uzuri, na usafi, yaitwayo katika Hadithi zinazoambatana nayo: Sunna za Kimaumbile, yaani: mazoeo yanayoambatana na uzuri wa hulka.
Na amri ya mambo hayo siyo kwa ajili ya uwajibu wa dini, na katazo siyo kwa kuharamisha, kama alivyosema Imamu At-Twabariy. Ni dhahiri kuwa amri hapa ni ya kuongoza, inayoambatana na manufaa ya maisha na masilahi yake.
Ama maelezo ya kuwa ni Sunna za Kimaumbile, hakika lengo lake kuwa mambo hayo ya kimaumbile yatakuwa katika hali nzuri kabisa katika uzuri wa umbo, usafi, na afya.
Kuhusu ilivyotajwa kuwa hayo kwa ajili ya kutofautiana na watu wa dini nyingine, hakika lengo lake ni waislamu watakuwa na sura na mazoeo mazuri yanayowahusu, kwani wao ni Umma Mpya, na dini yao itawajaalia kama kiongozi na kigezo kwa watu wa dini zote kwa kurekebisha mambo ya dini na dunia, na ufisadi wa kidini na wa kijamii ulikuwa wa kawaida katika mataifa yote, kwa kauli ya pamoja ya wanahistoria.
Na kuzifuga ndevu ni miongoni mwa Sunna za Kimaumbile, maana yake ni: urembo unaohusu mwanamume ambaye uumbwaji wake ni kamili kuliko mwanamke, na hii ni alama ya tofauti kati yao, kama tunavyoona tofauti hii kati ya wanyama wa kiume na wa kike.
Basi suala hili ni la mazoea ya kimaisha na sio la kidini, na lengo lake ni kutakasa nafsi, ili kustahiki ujirani wa Mungu na thawabu yake katika Akhera, kama tulivyosema.
Na kama kuzifuga ndevu ni kwa nia ya ufuasi na kuimarisha muungano wa Umma, mfano wa yanayoleta thawabu, kama vile mazoeo yote na mambo ya halali yanayoambatana na nia nzuri, na kwa kuwa masuala hayo siyo ya dini, basi Waislamu hawakuangalia mambo kama kuzitia rangi nywele, na wakaangalia kuzifuga ndevu, pamoja na usahihi wa Hadithi zinazoamuru kuzifanya hivyo, kwa kuwa ni urembo na kutofautiana na Watu wa Kitabu. Pia baadhi ya wanazuoni walichukia kuzitia rangi nywele, na wengine waliharamisha kuzipaka kwa rangi weusi.
Kuhusu kauli ya mwenye swali: ikiwa Hadithi ni sahihi, basi hoja nini kwa anayeinyoa ndevu zake miongoni mwa Waislamu, na kati yao wabebaji wa Sharia? Jawabu lake ni watu hutenda walivyozoea na kufungamana kutokana na Sunna hizi, hata baadhi ya Salaf waliziacha baadhi yake”. [Mwisho kwa muhtasari]
Kwa hivyo Sheikh Ridha alijipinga katika mahali pengine, akaeleza kuwa ni jambo linalochukiza kuzinyoa ndevu, na mara akasema; haisihi kusemwa; hayo ni miongoni mwa mambo ya mazoeo wala siyo ya dini. [Gazeti la Al-Manaar: 7/733; 14/29; 31/442].
Imamu Mkuu Sheikh Mahmud Shaltut katika kitabu chake: [Al-Fatawa Uk. 229, Ch. Dar Ash-Shuruq] anasema: “Kwa hakika suala la mavazi na sura ya mwanadamu, miongoni mwake kuzinyoa ndevu, hayo yote ni mambo ya mazoea ambayo mtu lazima akubali mwelekeo wa mazingira yanayomuhusu, na kama mazingira yakiamua kuwa kitu fulani ni kizuri, basi mtu ataendana na mazingira yake, na kupinga kwake kuzingatiwe kama kazi isiyo ya kawaida ya desturi”. [Mwisho]
Mfano wake Sheikh Muhammad Abu Zahrah katika kitabu chake: [Usulul Fiqhi Uk. 115, Ch. Dar Al-Fikr] ambapo alichagua kuwa kuzifuga ndevu ni miongoni mwa mazoea na siyo ya mambo ya Sheria.
Inawezekana kuchukuliwa katika rai hii walivyoelekea wengi wa Maulamaa wa Al-Azhar kwa njia ya kiutendaji zaidi; kwa sababu tunawaachia kufuatana na kazi ya uchunguzi kuwa ni jambo linalochukiza, na pamoja na kusudio la kuutekeleza uharamu na kuung’ang’ania; na wao ni warithi wa Unabii na nyota za kuongoza Ulimwengu.
Na inategemewa kwa rai hii aliyoyataja Al-Hafidh Ibn Hajar Al-A’sqlaniy katika kitabu cha: [Fat-h Al-Bariy 10/355, Ch.Dar Al-Ma’rifah] kuwa kuacha rangi ya nywele inayoamrishwa ni bora ikiwa mazoeo ya watu wa mahali wataacha hivyo, ambapo alisema: “kuna tofauti kuhusu kutumia au kutotumia rangi ya nywele; Abu Bakr na Umar na wengineo waliitumia, kama ilivyotajwa hapo juu, lakini Ali, Ubay Ibn Kaa’b, Salamah Ibn Al Akwaa’, Anas na wengine hawakuitumia.
At-Twabariy alieleza hivyo kuwa: wao waliotia rangi nywele walikuwa na haja ya kufanya hivyo, kutokana na ubaya wa mvi zao, na hao walioiacha hawakuwa na haja nayo, kutokana na mvi huonekana za kawaida, kwa maana hiyo ilielezwa kauli yake Mtume S.A.W., katika Hadithi ya Jabir, iliyopokelewa na Imamu Muslim kuhusu habari ya Abu Quhafah, ambapo Mtume S.A.W., alipoona kichwa chake kimekuwa cheupe kabisa alisema: “Geuzeni hivyo bila ya weusi; na mfano wa hayo Hadithi ya Anas iliyooneshwa hapo juu mwanzoni mwa mlango wa (inavyotajwa kuhusu mvi), na At-Twabariy, Ibn Abi A’asim wameongeza kwa njia nyingine, kutoka kwa Jabir akisema: “Walikwenda kuzitia nywele zao rangi nyekundu”, akasema: anayekuwa katika hali hii ya Abu Quhafah inatakiwa kwake kutia rangi, kwa sababu haipelekei kiburi kwa wengine, lakini ambaye hakuwa na hali hiyo basi hatakiwi kufanya hivyo. Na kutia rangi kwa uwazi ni bora kwa sababu ni kuitikia amri ya kuwapinga Watu wa Kitabu, pia kuzihifadhi nywele kutokana na vumbi na sababu nyinginezo, lakini ikiwa mazoea ya watu wa mahali ni kuacha kutia rangi, na kufanya hivyo hupelekea hali ya umashuhuri, basi kuacha kwake ni bora zaidi. [Mwisho]
Tuemkwisha taja kauli za madhehebu kuhusu suala hili, na kuhusu utambulisho na uchaguzi: rai tunayoitambua kwa kutoa Fatwa ni: ile walioielekea wafuasi wa madhehebu ya Shafiy kuwa ni: kuzifuga ndevu ni Sunna, na inachukiza kuzinyoa, na hivyo kwa mambo mawili: Kwanza: kauli hii ni yenye nguvu zaidi kuhusu dalili. Pili: kueneza kutahiniwa kwa suala la kuzinyoa ndevu.
Na maelezo ya hayo ni kama yafuatayo:
Kuhusu kauli ya kuwa: inatakiwa kuzifuga ndevu na inachukiza kuzinyoa ni rai yenye nguvu zaidi, hayo kwa ajili ya dalili zifuatazo:
Kwanza: kauli yake Mtume S.A.W: “Wapingeni washirikina, fugeni ndevu, na punguzeni masharubu” siyo amri kwa uwazi, bali ni ya kusababishwa kwa sababu ya kupingana na washirikina na kutolingana nao, na sababu hii inaonesha kutowajibika, kwa kuwa kuwapinga makafiri si wajibu isipokuwa katika mambo yanayohusu imani zao na mambo yanayohusu dini.
Kuna dalili nyingi za hizo, miongoni mwake: kukata sharubu pamoja na kuzifuga ndevu ambazo zilipokelewa katika Hadithi pamoja na sababu yake yenyewe, hakuna mmoja aliyesema kuwa ni wajibu, bali Omar Ibn Al-Khtwab R.A., alikuwa akiliacha sharubu yake, na kulisuka kwenye hasira; na Imamu Malik alikuwa akikata sehemu ya sharubu lake bila ya kulinyoa, pia alikuwa akiliacha kwake ncha mbili, na kutoa hoja yake kuwa Umar alikuwa akifanya hivyo. [Tartiib Al-Madarik, na Kadhi I’iyadh: 1/121, Ch. Matbaa’at Fadhalah, Moroko].
Na miongoni mwake ni kuwa: Mtume S.A.W., aliamuru kuzigeuza mvi, akisema katika Hadithi ilivyopokelewa na Imamu Tirmidhi na wengineo, kutoka kwa Abu Hurairah R.A.: “Zigeuzeni mvi zenu, na wala msifanane na Mayahudi”, na idadi kubwa ya Masahaba hawakuwa wakizitia rangi nywele zao, na haikupokelewa kuwa wanaotia rangi waliwalaumu wengine kuwa wamefanya mambo la kuacha rangi, ambapo huleta mfanano unaokatazawa.
Imamu At-Twabariy alinukulu kauli ya pamoja ya kuwa amri hiyo ya kuzigeuza mvi na kukataza mfanano hapa maana yake ni jambo linalochukiza na siyo uharamu; alisema hivyo katika kitabu cha: [(Tahdhibul Aathaar Uk. 518, Ch. Dar Al-Maamuun Litturath]:
“Mtu aliyekuwa na nywele nyeusi za kichwa na ndevu ana hiari ya kuacha kuzigeuza kwa kutumia rangi, vile vile aliyekuwa na nywele nyeupe za kichwa na ndevu ana hiari ya kuacha kuzigeuza bila ya kupata dhambi kwa kuacha kutia rangi, kwa sababu amri hiyo ya Mtume S.A.W., ilikuwa kwa njia ya hiari na siyo kwa njia ya faradhi, na kwa kuongoza na siyo wajibu; vile vile sioni kama kuna ubaya kwa aliyekuwa na mvi chache kuzigeuza, kwa sababu kukataza kwa Mtume S.A.W., kulikuwa kwa njia ya jambo linalochukiza siyo kwa njia ya uharamu; kutokana na kauli ya pamoja ya Salaf na wafuasi wao ya hivyo; na kuwa katazo kwa Mtume S.A.W., kufanya hivyo lingelikuwa kwa njia ya uharamu, au amri yake ingelikuwa kwa njia ya uwajibu, basi wasiotumia rangi wangelikuwa wakiwalaumu watumiaji, au watumiaji wangelikuwa wakiwalaumu wasiotumia, lakini jambo la suala hili lilikuwa kama nilivyoeleza, na kwa ajili ya hayo, wote waliacha kulaumiana wenyewe kwa wenyewe”. [Mwisho]
Na miongoni mwake ni: Hadithi iliyopokelewa na Abu Dawuud, kutoka kwa Shaddad Ibn Aus R.A., kuwa Mtume S.A.W., alisema: “wapingeni Mayahudi, wao hawaswali wakivaa viatu vyao”, wakati haikupelekea mmoja wa wanazuoni kauli yake ya uwajibu wa kuswali kwa kuvaliwa viatu, bali walitofautiana kuhusu: je ni ile inayokokotezwa, mubaha, au jambo linalochukiza? [Faidhul Qadiir; 4/67, Ch. Al-Maktabah At-Tijariyah Al-Kubra], na Imamu Ibn Daqiiq Al-I’id anasema: “Mtu kusali akiwa amevaa viatu ni miongoni mwa mambo yaliyoruhusiwa na siyo miongoni mwa mambo yanayotakiwa; kwa sababu hayo hayaingii katika maana ya yanayotakiwa katika Swala”. [Mwisho] [na Umdatul Qariy, na Al-Badr Al-A’iniy: 4/119, Ch. Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy].
Na miongini mwake ni: Hadithi iliyopokelewa na Imamu Ahmad katika Musnad yake, kutoka kwa Amr Ibn Al-Aas R.A., Kuwa Mtume S.A.W., anasema: “Hakika tofauti kati ya Funga yetu na Funga ya Watu wa Kitabu ni chakula cha Daku”.
Na chakula cha Daku ni jambo linalotakiwa, na Imamu Ibn Al-Mundhir alinukulu kauli ya pamoja ya hayo katika kitabu chake cha: [Al-Ijmaa’ Uk. 49, Ch. Dar Al-Muslim] akisema: “Walikubali kwa pamoja kuwa chakula cha Daku ni kilichotakiwa”. [Mwisho]
Na miongoni mwake: ilivyopokelewa na Ibn Saad katika kitabu cha: [At-Tabaqaat 1/159-160, Ch. Dar Saadir], kutoka kwa Ibn Abbas R.A., kuwa Mtume S.A.W., alipomwambia Jaa’far Ibn Abi Taalib R.A., akisema: “Ewe Jaa’far, wewe ni mfano wangu kiumbo na kitabia” hapo Jaa’far aliendele kumzunguka Mtume S.A.W., akasema Mtume S.A.W., unafanya nini Jaa’far? Na Jaa’far akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: An-Najashiy alikuwa akitaka kumpendeza mtu, huendelea kumzunguka”. Na hili lilikubaliwa na Mtume S.A.W., kwa sababu hakumkanusha alivyochukua Jaa’far kutoka kwa Manasara wa Wahabeshi, na hii ni matini ya wazi kuwa kupingana si wajibu.
Na miongoni mwake: ilivyopokelewa na Al-Baihaqiy kuwa; Ummul Muuminiin Bibi Zainab Binti Jahshi R.A., alikuwa mwanamke wa kwanza aliyechukuliwa kwa jeneza, lililotayarishwa na Asmaa binti U’mais Al-Khtha’miyah R.A, alipokuwa huko nchi ya Uhabeshi, nayo ni nchi ya Manasara R.A., aliwaona wakitengeneza majeneza, nae akalitengeneza kwa ajili ya Zainab katika siku ya kifo chake.
Na mfano wake ni kama ilivyopokelewa na Al-Haakim katika Al-Mustadrak, kutoka kwa Ibnu Abbas R.A., alisema: Fatimah aliugua sana, akamwambia Asmaa binti U’mais: je ninaweza kubebwa kwa kitanda hadharani? Akasema Asmaa: ndio inawezekana, lakini ninakutengenezea jeneza kwa ajili yako, kama nilivyoona likitengenezwa huko katika nchi ya Uhabeshi. Akasema: nataka kuliona, na Asmaa akamletea matawi laini ya mitende, yaliyokatwa katwa katika Mtaa wa Al-Swaaf, na yakawekwa juu ya kitanda kama jeneza. Na hili lilikuwa ni jeneza la kwanza, hapo Fatimah akatabasamu, na mimi sikumuona akitabasamu baada ya kifo cha Baba yake, isipokuwa katika siku hiyo, kisha tukamchukua, tukamzika usiku. Na hili limetokea wakati wa Masahaba watukufu R.A., wakiwepo, na hakunukuliwa yoyote katika wao kuwa alikataza kazi ya Fatimah R.A., kuwa ni kulingana na Manasara wa Uhabeshi, na hii ni kauli ya pamoja kwa njia ya kunyamaza, nayo ni hoja.
Katika kitabu cha: [Jamu’ul Jawamii’ na Sharh yake, na Mtaalamu Al-Mahalliy 2/221, na Hashiyat Al-A’attar, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah] alisema: “Rai sahihi kuwa: kauli ya pamoja ni hoja kwa uwazi”. [Mwisho]
Na miongoni mwa wanazuoni walioashiria kuwa mfanano na wasio waislamu hauharamishwi kwa ajili yake tu; Al-Hafidh Ibn Hajar katika kitabu cha: [Fat-h Al-Bariy 10/98, Ch. Dar Al-Maa’rifah] kwenye maneno yake ya sababu zinazopolekea uharamu wa kutumia vyombo vya dhahabu na fedha; ambapo alisema: “Imesemwa kuwa: sababu ya kukataza ni kufanana na Waajemi, na kauli hii ina mtazamo wake, kwa sababu ya kuwa kuna kuchelea adhabu kwa anayeifanya hivyo, na mfanano peke yake haufikii kiwango cha kuchelea adhabu hiyo”. [Mwisho]
Licha ya hayo kuwa: tukikubali kuwa mfanano na wasio waislamu hukanushwa katika kila njia, kukitekeleza kinachofanana na kazi ya Watu wa Kitabu hakuitwi mfanano, isipokuwa mtendaji hukusudia mfanano, kwa sababu mfanano humaanisha kushirikiana katika kukitekeleza kitu, ambapo huonesha kufunga nia na kuelekea kuitekeleza kazi kwa bidii. Na miongoni mwa misingi ya Sharia ni kuzingatia kusudio la mwenye kukalifishwa, na dalili ya hayo ilivyopokelewa na Imamu Muslim, kutoka kwa Jaabir R.A., alisema: Mtume S.A.W., aliugua, na tukaswali nyuma yake hali ya kuwa yeye ameketi, akatazama nyuma akatuona tukisimama, akatuashiria tukaketi, na alipotoa salamu akasema: “Mlikaribia kulifanya tendo la Waajemi na Warumi, wanasimama wakati wafalme wao wakiwa wameketi, basi msifanye hivyo, na wafuateni Maimamu wenu, na Imamu anaposwali hali ya kuwa amesimama, swalini kwa kusimama, na kama atakuwa ameketi, swalini mkiwa mmeketi”.
Na kazi ya Waajemi na Warumi imekwisha fanywa, lakini kwa kuwa Masahaba pale ambapo hawakukusudia kufanana, basi sifa hii haikuambatana nao kisheria. Kwa hiyo, Mwislamu anayenyoa ndevu zake hafikiri kuwa kufanya hivyo ni kufanana na wasio waislamu, licha ya kusudio lake.
Imamu Ibn Nujaim katika kitabu cha: [Al-Bahr Ar-Raaiq 2/11, Ch. Dar Al-Kitaab Al-Islaamiy]: Anasema: “Elewa kuwa mfanano na Watu wa Kitabu hauchukizi katika kila kitu, na sisi tunakula na kunywa kama wanavyofanya, lakini uharamu ni kulingana nao katika maovu, na ndivyo inavyokusudiwa mfanano huo, na kwa hiyo isipokusudiwa mfanano, basi haichukizi’. [Mwisho]
Ibn A’abidiin katika kitabu cha: [Rad Al-Muhtaar 1/624, Ch. Dar Al-Fikr] alisema akieleza kauli ya mtungaji wa kitabu cha: [Ad-Durul Mukhtaar]: “Mmfanano nao, yaani Watu wa Kitabu, hauchukizi katika kila kitu”, kwa sababu tunakula na kunywa kama wanavyofanya… na inayotegemewa ni yaliyotajwa katika Adh-Dhakhirah na kitabu cha [At-Taharriy].
Na Hishamu anasema: “Nilimuona Abu Yusuf akivaa viatu vinavyotengenezwa kwa misumari, nikasema: hivi kuna ubaya wowote wa kutumia chuma hiki? Akasema: hapana, nikasema; Sufyan na Thaur Ibn Yazid walichukizwa na kufanya hivyo, kwa sababu kunafanana na kazi za mapadri, anasema: Mtume S.A.W., alikuwa akivaa viatu vyenye nywele, na hakika hivi ni miongoni mwa mavazi ya mapadri. Hapa aliashiria kuwa mfanano wa mambo yanayoambatana na masilahi ya watu haudhuru, na kwa sababu kutembea umbali mkubwa hakuwezekani isipokuwa kwa kutumia aina hii ya viatu. {Mwisho]
Na kuna ishara kuwa muradi wa mfanano ni kazi yenyewe, yaani sura ya mfanano bila ya kusudio’. [Mwisho]
Kwa hiyo amri ya kuzifuga ndevu inaambatana na sababu yenyewe inayoelezwa katika Hadithi hizi na kila kinachochukuwa maana yake, na amri hizi zote zinajengwa kwa linalotakiwa, kwa hiyo amri ya kuzifuga ndevu ni mfano wake, kwa kuwa sababu ni moja, na hukumu ikijengwa kwa sababu moja, basi inapaswa kuifuata kwa kuwepo na kutokuwepo.
Katika jambo hilo Imamu Abu Suleiman Al-Khatwabiy katika kitabu cha: [Maa’alim As-Sunan 1/31, Ch. Al-Matbaa’ah Al-Ilmiyah, Halab] anasema: “Kuzifuga ndevu ni kuzirefusha na kuzihifadhi, na inachukiza kwetu kuzikata, mfano wa kazi ya Waajemi, na sura ya Watu wa Kisra ilikuwa kuzikata ndevu na kufuga masharubu, kwa hiyo Mtume S.A.W., aliwaomba umma wake kuwapinga katika mavazi na sura”. [Mwisho]
Pili: Hadithi ya mambo kumi ya kimaumbile, iliyotajwa hapo juu kwa tamko lake, na ndani yake ni kutaja ndevu kati ya mambo hayo kumi, na mabaki ya mambo hayo kumi siyo wajibu kwa jumla, na kuiunganisha ndevu kwa hayo kumi huonesha kuwa siyo wajibu mfano wake; na haisemwi kuwa; dalili ya kuunganisha ni dhaifu kwa rai ya Wenye Misingi ya Fiqhi, kwa sababu udhaifu huu unaainishwa kuwa mambo hayo kumi yasipotajwa kwa tamko moja linaloyakusanya yote pamoja, lakini tamko la kimaumbile linayakusanya yote yaliyotajwa.
Imamu Ibn Daqiiq Al-I’iid katika kitabu cha: [Ihkaam Al-Ahkaam 1/126-127, Ch. As-Sunnah Al-Muhammadiyah] anasema: “Kutoa dalili kuwa uunganisho kwa jumla ni dhaifu, lakini hapa ni nguvu, kwa sababu (maumbile) ni tamko moja lililotumiwa kuonesha mambo haya matano, lakini yakitengana katika hukumu, yaani baadhi yake huonesha uwajibu, na mengine huonesha inayotakiwa, hapo inapaswa kulitumia neno kwa maana mbali mbali kama ilivyofahamika katika Elimu ya Misingi, na udhaifu wa uunganisho unapatikana katika hali ya kuwa kila sentensi inaundwa peke yake, na neno moja halikutumiwa katika maana mbali mbali”. [Mwisho]
Tatu: Ndevu kwa Waarabu kabla ya kuja Uislamu ilikuwa katika desturi ya wanaume na alama ya pambo lao kwa uwazi, na wao walikua wakichukia kunyoa ndevu zao, na kuzingatia kuzinyonyoa na kuzikata ni aina ya aibu na ubaya. Na ilivyoamuliwa kuwa jambo likiambatana na desturi na adabu linageuka kutoka katika uwajibu na kuwa linalotakiwa kufanywa; na maana ya adabu ni: mambo yanayoambatana na uzuri wa maadili na kuyarekibisha mazoea [kama alivyoyataja Mtaalamu Saa’d Ad-Diin At-Taftazaniy katika kitabu cha: [Sharh At-Talwiih: 1/293, Ch. Subeih].
Na imetajwa katika kitabu cha: [Fat-h Al-Bariy 9/523,] kwenye maelezo ya Hadithi ya Amr Ibn Salamah kuhusu kula kwa mkono wa kulia: “Al-Qurtubiy anasema: Amri hii ni kwa njia inayotakiwa; na kwa njia ya kutukuza sana mkono wa kulia kuliko mkono wa kushoto, kwa sababu ni mwenye nguvu zaidi na kipaumbele kuhusu kazi, na wenye uimara kwa shughuli, na maana yake inachukuliwa kwa (Yumn) yaani baraka, na Mwenyezi Mungu aliwatukuza watu wa Pepo, ambapo aliwanasibisha katika kulia, na akageuza hivyo kwa wenye kushoto. Akasema: kwa jumla, upande wa kulia na linalonasibishwa kwake na linalochukuliwa kwake unasifiwa kilugha, kisheria, na kidini, lakini upande wa kushoto ni kinyume cha hivyo.
Ikiwa hivyo ikiamuliwa, basi kati ya adabu zinazonasibishwa tabia njema na wasifu mzuri kwa waungwana ni upande wa kulia unahusika na kazi tukufu na hali safi. Na akasema pia: amri kama hizo ni kati ya mazuri kamili na tabia zinazopendeza, na asili ya hayo yote ni kupendeza na inayotakiwa”. [Mwisho]
Kutokana na dalili hizi ni wazi kuwa kauli ya inatakiwa kuzifuga ndevu na inachukiza kuzinyoa, hiyo imekusanya kati ya dalili mbali mbali, na haikutekeleza baadhi ya dalili na kuziacha nyingine, kwa hiyo kauli hii ni ya mwisho na yenye nguvu zaidi; kwa sababu mkusanyo kati ya dalili mbili au dalili nyingi na kuzitekeleza pamoja, hata kwa kiasi fulani, ni afadhali kuliko kuziacha au kuitekeleza moja kati yake na kuiacha nyingine. Kuacha na kuzembea kwa jumla ni kinyume cha msingi, kwa hiyo haitegemewi kwake isipokuwa kwenye kupingana na dalili, na kutoweza kukusanya kati ya dalili mbili au dalili zote.
Hapa tunajibu baadhi ya hoja zingine za wanaosema kuwa ni dalili ya kuharamisha, na ni dalili za madai yao:
Miongoni mwake ni: kuzinyoa ndevu ni kugeuza uumbaji wa Mwenyezi Mungu, ambapo Mwenyezi Mungu alitaja kauli ya Shetani aliyefukuzwa: {Na nitawaamrisha, basi watabadili aliyoumba Mwenyezi Mungu}. [AN NISAA; 119], walisema: kuzinyoa ndevu ni kati ya kubadilisha uumbaji wa Mwenyezi Mungu, basi itakuwa miongoni mwa utiifu wa Shetani, na itakuwa haramu.
Haifai Kutoa dalili ya Aya hii, kwa sababu tunadai kuwa ibara ya (uumbaji wa Mwenyezi Mungu) ina maana ya: dini ya Mwenyezi Mungu, na hapo kama kwamba Shetani anasema: atawaamuru watu wabadilishe dini ya Mwenyezi Mungu, kwa kufuru, na kubadilisha umbile la Kiislamu, ambalo mwenyezi Mungu aliwaumbia.
Tamko la (uumbaji wa mwenyezi Mungu) lilitumiwa katika sehemu nyingine ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwa maana ya (dini ya Mwenyezi Mungu) katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi uelekeze uso wako katika dini iliyo sawasawa – ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu: (yaani dini hii ya Kiislamu inawafikiana barabara na umbo la binadamu), Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini iliyo haki, lakini watu wengi hawajui} [AR RUUM; 30], yaani: msibadilike, kwa kufuru, umbile la Mwenyezi Mungu ambalo aliwaumbieni. [Tazama: Adwaaul Bayan, na Ash-Shanqitiy; 1/308-309, Ch. Dar Al-Fikr]
Tamko la (uumbaji wa Mwenyezi Mungu) katika sehemu hii linaimarisha maana iliyotajwa katika Suratun Nisaa iwe (dini ya Mwenyezi Mungu); kwa kuwa Qur`ani inajitafsiri yenyewe kwa yenyewe.
Na tafsiri hii inasemwa na wafasiri wengi wa Salaf, miongoni mwao ni: Ibnu Abbas, Adh-Dhahaak, An-Nakhi’iy, Said Ibn Jubair, Mujaahid, Qatadah, As-Suddiy, na wengineo, na miongoni mwao anayeeleza sababu ya hii iliyotajwa; kutoka kwa Adh-Dhahaak katika kauli yake Mwenyezi Mungu: {basi watabadili aliyoumba Mwenyezi Mungu} anasema: dini ya Mwenyezi Mungu, na hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu: {ndilo umbile Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu; Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu}, anasema: yaani dini ya Mwenyezi Mungu.
Na Mujaahid anasema: {basi watabadili aliyoumba Mwenyezi Mungu} yaani: dini ya Mwenyezi Mungu, kisha alisoma: {Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini iliyo haki}, na rai hii aliyoichagua Imamu Ibn Jariir At-Twabariy katika Tafsiri yake [Tazama. Jamiu’ul Bayan, na At-Twabariy; 9/218-220, Ch.Muassasat Ar-Risalah; Ad-Durul Manthuur, na As-Sayutiy; 2/690, Ch. Dar Al-Fikr].
Kuitafsiri Aya hii kwa maana ya kubadili uumbaji wa Mwenyezi Mungu kwa uwazi, inapelekea kuwa ni: mabadiliko yoyote ya kitu chochote cha asili ya uumbaji wake ni kukatazwa, lakini hii ni kinyume cha kauli ya pamoja ya hayo.
Miongoni mwa dalili zao pia: kuzinyoa ndevu ni kufanana kwa wanaume na wanawake, jambo ambao ni haramu; kwa Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhariy, kutoka kwa Ibn Abbas R.A., kuwa alisema: Mtume S.A.W., amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na hali kadhalika wanawake wanaojifananisha na wanaume.
Lakini dalili hii imekataliwa; kwa sababu mfanano kati ya mambo mawili unapelekea kuwepo jambo la kushirikiana kati yake, ambalo halikuwepo hapa; kwa kuwa mwanamke hana ndevu za kuzinyoa, ili pasemwe kuwa mwanamume anaezinyoa ndevu zake anafanana na mwanamke, lakini uso wa mwanamke ni laini, kinyume na uso wa mwanamume, hata baada ya kuzinyoa ndevu zake, athari ya nywele ingali ikidhihirika, na uso wa mwanamke usio na nywele na hauelezwi kuwa umenyolewa kwa njia ya lugha au mazoea, kinyume cha uso wa mwanamume unaonyolewa; kwa hivyo basi tofauti kati yao ipo, kihisia, kilugha, na kimazoea, na kama tofauti ipo, basi hakuna mnasaba wala mfanano kati yao.
Ikiwa maelezo haya ni sahihi, basi kunyoa sharubu kunazingatiwa kuwa ni kujifananisha na wanawake, vile vile kuzifuga nywele za kichwa, na itakukwa wajibu kwa mwanamume kuzinyoa, na hayo yote ni kosa na ni batili. Na itazingatiwa kuwa anayenyoa ndevu zake na kufuga sharubu hana mfanano wowote na wanawake; kwa sababu uso wake katika hali hii haufanani na uso wa wanawake, kutokana na dalili hii, na wao hawasemi hivyo.
Tuzingatie hapa ilivyotajwa hapo juu kwa dalili kuwa sharti la kuzingatia mfanano kuwa mwenye kulingana anakusudia mfanano, kwa sababu kulitekeleza jambo linaloshirikiana bila ya kuwepo nia na kusudio, haliitwi mfanano.
Miongoni mwa dalili zao ni dai lao kuwa kuna kauli ya pamoja kuwa kunyoa ni haramu, kwa kutegemea kauli ya Abu Muhammad Ibn Hazm katika kitabu cha: [Maratib Al-Ijmaa’ Uk. 157, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Wamekubaliana kuwa kuzinyoa ndevu yote ni aina ya adhabu, na haijuzu kufanywa hivyo, vile vile: haijuzu kufanywa na Khalifa, muungwana, na mwanazuoni”. [Mwisho]
Na hayo yaliyotajwa hayaelezi hukumu ya kuzinyoa ndevu kwa uwazi, lakini yanaelezea hukumu ya kuzinyoa kwa njia ya kuadhibu katika hali ya uhalifu, yaani kuzinyoa kwa ajili ya hayo haijuzu. Na kuzinyoa kwa lengo la kuadhibisha au kusababisha adha mwilini, hayo yote yanakatazwa kisheria, na huu ni muradi ulio wazi.
Na inayotegemeza maelezo hayo ni kauli yake baadaye: “vile vile: haijuzu kufanywa na Khalifa, muungwana, na mwanazuoni”, yaani kama haijuzu kuzinyoa kwa njia ya kusababisha adha mwilini, hali kadhalika kuhusu waliofuatwa katika hali zao na kazi zao, pia haijuzu. Na ikiwa kusudio kwa mwanzo wa ibara ni kuwepo kauli ya pamoja kuwa kuzinyoa ndevu ni haramu, basi haina faida ya kuwataja Khalifa, muungwana, na mwanazuoni mwishoni mwake, kwa sababu wao ni miongoni mwa waliowahi kutajwa.
Na Ibn Hazm alitaja katika mwisho wa kitabu chake: [Uk. 177] kuwa: hakuweka ndani ya kitabu neno lolote isipokuwa kwa maana mahsusi, ambapo bila ya mahsusi maana itaharibika, akisema; “tunataka yule aliyesoma kitabu chetu hiki kuangalia masharti mawili: Kwanza: asitunasibishie haya hatukuyasema kwa njia ya uzushi au makusudio…
Pili: ayazingatie maneno yetu yote katika kitabu hiki, kwa sababu hatukutaja neno kwa mtindo wa kauli ya pamoja isipokuwa kwa ajili ya maana mahsusi, na maana itaharibika bila ya kutaja neno hilo, basi msomaji atanabahi, ili apate faida kubwa ya hayo, apate elimu, achemshe bongo, ajifunze maana ya tamko , na ayaunde maneno katika maana”. [Mwisho]
Na Tukichukulia kuwa ibara hii ilitajwa kuonesha hukumu ya kunyoa, hatukuchukulia kuwa inaonesha kuwepo kauli ya pamoja, kwa sababu yeye alisema (wamekubaliana) na hakusema (wamekubaliana pamoja); na ilitajwa mwishoni mwa kitabu chake: [Uk. 178] maneno mafupi, huenda yakaeleweka kutoka kwake kuwa anatumia neno (kukubaliana) kwa maana yasiyo ya (kukubaliana pamoja), akisema: “Msomaji wa maneno yetu inapasa kuelewa kuwa kuna tofauti kubwa kati ya kauli yetu (hawakubaliana pamoja) na kauli yetu (hawakubaliana) tu”. [Mwisho]
Na tukichukulia kuwa ibara hii inaonesha hukumu ya kunyoa, na kuwa haijuzu kwa kauli ya pamoja, basi hatuchukulii kuwa ibara ni dalili ya kuwepo kauli ya pamoja inayoonesha uharamu, kwa sababu kauli yake (haijuzu) huonesha ziada ya uharamu, na jambo linalochukiza linaelezwa kuwa (haijuzu), kama tulivyotaja hapo juu, kwa hiyo kuichukulia kauli yake hiyo kuumaanisha uharamu ni ushupavu bila ya dalili, na kuteua rai ya nguvu zaidi bila ya hoja, na hayo yote ni batili.
Na tukichukulia kuwa ibara hii inaonesha hukumu ya kunyoa, na kuwa ni kuharamishwa kwa kauli ya pamoja, basi lazima tuukataze usahihi wa kauli hiyo ya pamoja, kwa sababu yupo mpingaji, vilevile kuna shida ya kuwepo kauli ya pamoja kuhusu suala hili, wakati ikifichwa na wanazuoni wakuu wanaosema kuwa jambo linalochukiza, na kila mmoja kati yao ni mtaalamu mkubwa kati ya wanazuoni, na hakuna mmoja kati yao isipokuwa yupo katika ngazi ya juu kabisa ya maarifa na kuvisoma vitabu.
Na mengi ya kauli za pamoja zilizotajwa na Ibn Hazmi katika kitabu chake hazikukubalika, na aliposema ndani yake [Uk. 16]: “Hakika tunaingiza ndani ya kitabu hiki kauli ya pamoja iliyo kamili ambayo kamwe haipingwi, lakini inayojulikanwa kama inavyojulikanwa kuwa swala ya Asubuhi katika hali ya usalama na hofu ni rakaa mbili, na kuwa Mwezi wa Ramadhani ndio uliyo kati ya Shawaal na shaaban, na kuwa yaliyo ndani ya Misahafu ndiyo aliyoyaleta Muhammad S.A.W., na akatuambia kuwa ni Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa Zaka ya ngamia watano ni kondoo mmoja, n.k. Na hili ni jambo la lazima linaloambatana na nafsi ya mchunguzi wa habari, msimamizi wa hali za kunukulu, ambapo mtu akizifuata yeye mwenyewe kupitia aliyoyajaribu ya hali za dunia, atayakuta thabiti na tulivu ndani ya nafsi yake”. [Mwisho]
Ingawa hayo, aliyafuata Sheikh Taqiy Ad-Diin Ibn Taimiyah katika kitabu chake [Naqd Maratib Al-Ijmaa’ Uk. 287, Ch. Dar Ibn Hazm] akisema: “Yeye alishurutisha kuhusu kauli ya pamoja wanavyoshurutisha wengi wa wanazuoni wa elimu ya Kalaam, na Fiqhi, kama ilivyotajwa hapo juu, nayo ni: kuelewa kuwa kutokuwepo upinzani, na kuelewa kuwa kauli ya pamoja ilipokelewa kwa mlolongo wa uhakika. Na akajaalia kuelewa kwa kauli ya pamoja ni miongoni mwa elimu za lazima, kama vile kuelewa elimu za habari zenye uhakika zaidi, kwa rai ya wengi wa wanazuoni.
Na inajulikana kuwa mengi ya kauli za pamoja alizozitaja si karibu na maelezo hayo, wala kuwa ndani yake, ikuwaje hivyo na tofauti inajulikana, na miongoni mwake ambayo yeye mwenyewe anakanusha kuali ya pamoja ndani yeke, na akachagua kinyume chake, bila ya kuwepo mpingaji?”. [Mwisho] Kwa hiyo inabainika kwa ilivyotangulia: ubaya wa kutegemeza ibara hii ili kuonesha kauli ya pamoja iliyodaiwa.
Kuhusu jambo la pili lililotujaalia kuteua kuwa kuzinyoa ndevu ni jambo linalochukiza, na kwa kuitoa Fatwa kwake, nalo ni: kujaribiwa kwa kuzinyoa ndevu; na inajulikana katika kanuni za Fiqhi na msingi wa Sharia kuwa jambo likiwa na dhiki litapanuka, na kutahiniwa kwa kitu kunapelekea kurahisishiwa wanaokalifishwa.
Na mwenye kufuata maneno ya wanazuoni atakuta hukumu nyingi za Fiqhi zina mwelekeo maalumu, kwa mujibu wa kanuni za fani ya Fiqhi, kisha wanazuoni waligeuza kwa hukumu nyingine, ambayo ni rahisi zaidi, kwa sababu ya kutahiniwa kwa hukumu ya kwanza.
Na wanazuoni walitaja kuwa: mwenye kukalifishwa akitahiniwa kwa kitu, basi atamfuata aliyekijuzisha kwa ajili ya kujiepusha na uharamu, na miongoni mwa hao walioashiria hivyo ni: Sheikh wa Uislamu Al-Burhan Al-Baijuriy katika Hashiya yake ya Fiqhi ya [Fat-h Al-qariib Al-Mujiib 1/41, Ch. Al-Halabiy], kwenye kauli yake Mtaalamu Ibn Qasim Al-Ghazziy: (na haijuzu katika hali isiyo ya dharura kwa mwanamume wala mwanamke kuvitumia vyombo vya dahabu wala fedha) ambapo alisema: “Al-Balqiniy na Ad-Dumairiy walivizingatia miongoni mwa dhambi kubwa, na Al-Adhrii’iy alinukulu kwa wengi wa wanazuoni kuwa ni miongoni mwa dhambi ndogo, na hii ni ya kutambuliwa, na Dawud Adh-Dhahiriy anasema: kuvitumia vyombo vya dhahabu na fedha ni jambo linalochukiza, na hii ni kauli ya Imamu Shafiy katika madhehebu yake ya zamani.
Na imesemwa kuwa uharamu unaambatana na kula na kunywa tu, kwa kuchukua uwazi wa Hadithi, nayo ni: “Msinywe katika chombo cha dhahabu wala cha fedha, na msile katika sahani zake”. Kuna rai ya wafuasi wa madhahebu ya Hanafiy kuwa: inajuzu kuvitumia vikombe vya kahawa, lakini kwao rai ya kutambuliwa ni uharamu wa kufanya hivyo, kwa hiyo inatakiwa kwa mwenye kujaribiwa na kitu hicho, kama inavyotokea mara nyingi, azifuate rai zilizotangulia, kwa ajili ya kujiepusha na uharamu”. [Mwisho]
Na wanazuoni pia walitaja kuwa anayepewa Fatwa ana haki ya kuichagua kauli inayopinga madhehebu yake kwa sababu ya kutahiniwa, na miongoni mwa hao:
Imamu Abu Hanifa anasema: hakuna yamini katika mambo haya yafuatayo: Ndoa, Talaka rejea, Kutofanya tendo la ndoa, Utumwa, Mtoto, Nasabu, Walii’, na Hukumu. Na wanafunzi wake wawili wanasema; kuna yamini katika hayo isipokuwa Hukumu (adhabu Maalumu) na Lia’an (Laana).
Na Mtaalamu Majd Ad-Diin Al-Muwsiliy katika kitabu cha: [Al-Ikhtiyar 2/113, Ch. Al-Halabiy] anasema: “Mwanazuoni Abul Laith alichagua kutoa Fatwa kwa rai ya wanafunzi wawili, kwa sababu ya kujaribiwa [Mwisho]
Na katika kitabu cha: [Ad-Durul Mukhtar, na Al-Haskafiy 6/63, na Hashiyat Ibn Abidiin, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Inajuzu kukodisha mfereji na mto, pamoja na maji, na kwa rai hii inatolewa Fatwa, kwa sababu ya kujaribiwa”. [Mwisho]
Na Abu Hanifa alielekea kuwa: viatu vikipata unajisi wenye ukubwa, kama vile kinyesi na mavi, na kama vikikauka, kisha akavisugua ardhini, basi inatosha kuwa safi, lakini vikiwa vya majimaji au haina ukubwa, kama vile pombe na mkojo, haifai isipokuwa kuoshwa, na Abu Yusuf anasema: inatosha kufuta kwa maji isipokuwa mkojo na pombe, na Muhammad anasema: haijuzu isipokuwa kuoshwa, kama vile nguo.
Na wanazuoni wa madhehebu ya Hanafiy walitaja kuwa: kauli ya Abu Yusuf ndiyo inayochaguliwa, kwa sababu ya kujaribiwa. [1/234-235, Ch. Dar Al-kitab Al-Islamiy]
Kuhusu ndevu, kuna kutahiniwa kwa kuzinyoa; ambapo wengi wa Waislamu wanaifanya, kama inavyochunguzwa katika kila upande, na baadhi ya wanazuoni wa sasa waliangalia hivyo kuhusu suala la kuzinyoa ndevu, na wakaelewa kuwa kazi hizi za wengi wa watu inalazimu kurahisishwa kwa kutoa Fatwa, hata ingelikuwa kauli sahihi kwa mtazamo wa Mufti ni uharamu.
Na Mtaalamu Sheikh Muhammad Habibullahi Ash-Shanqitiy, Mfuasi wa Madhehebu ya Malik, katika kitabu chake: [Fathul Muni’im Bibayan Mahtija Libayanihi Min Zad Al-Muslim 1/179, Ch. Al-Halabiy] anasema: “Kutokana na kujaribiwa kwa kuzinyoa ndevu katika nchi za Mashariki, hata kwa wengi wa Waislamu wafuate wengine, kwa kuogopa kuwa watamdhihaki, kwa kuwa mazoea ni kuzinyoa, kwa hiyo nimejitahidi kuchunguza asili inayojuzisha kuzinyoa, ili iwe ufumbuzi wa kutoutekeleza uharamu kwa makubaliano. Nimeitumia kanuni ya Msingi ya Fiqhi, nayo ni: kitenzi (Fanya) katika kauli ya wengi wa wanazuoni huonesha uwajibu, na imesemwa: kwa inayotakiwa, na imesemwa: kwa kiasi ya kushirikiana kati ya inayotakiwa na uwajibu, na imesemwa kuna maelezo zaidi: ikiwa ni kauli ya Mwenyezi Mungu katika Qur`ani, basi huonesha uwajibu, na ikiwa ni kauli ya Mtume S.A.W., kama ilivyotajwa katika Hadithi hii kwa mujibu wa mapokezi yake mawili, nayo ni: (fugeni) na (acheni), basi huonesha: inayotakiwa… Na kauli ya mwisho hii ndiyo ni bora zaidi kuitekelezwa; kutokana na kujaribiwa”. [Mwisho kwa muhtasari].
Yaliyotangulia yanahusu hukumu ya ndevu kisheria, na kuhusu hukumu ya sheria kuwa Idara ya Serikali, kwa mfano Polisi, kumlazimu afisa au mfanya kazi asifuge ndevu zake, inajulikana kuwa mazoeo ya kazi za askari wa polisi na Jeshi, tangu mamia ya miaka, kuwa wanazinyoa ndevu zao, na hatukusikia kuwa suala kama hili lilichochea mgogoro kwa njia ya hukumu ya utiifu au kwenda kinyume na maamrisho, lakini kutokana na rai tofauti za wanazuoni, kama ilivyotajwa hapo juu, suala hili linaingia chini ya kanuni ya Fiqhi iliyotajwa na Imamu As-Sayutiy na wengineo kuwa: “Halikanushwi lililo tofauti, lakini linakanushwa lililokubalika”. [Al-Ashbaah Wan-Nadhair, na As-Sayutiy, Uk. 158, Ch. dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Kwa hiyo sisi tuko mbele ya pande mbili, upande wa kwanza ni Idara ya Serikali, na upande wa pili ni wahusika wanaofanya kazi ndani ya Idara.
Kuhusu wafanya kazi: hakuna ubaya kwao kuyasikiliza maamrisho ya wakuu wao, wanapowaamuru wanyoe ndevu zao, bali hii ni wajibu wa kisheria kwao.
Na hayo ama yanaambatana na kuwepo Sheria au Mwongozo maalumu unaodhibiti jambo hilo, na kuwalazimisha wafanya kazi wa Idara ya Serikali wanyoe ndevu zao, au kutowepo Sheria, na katika hali ya kutowepo Sheria basi jambo hili litaingia chini ya misingi na miongozo mikuu inayopelekea kuwa maamrisho ya wakuu wa Idara ni wajibu.
Na miogoni mwa hayo, kanuni ya (41) ya Sheria nambari (109), Mwaka 1971, kuhusu Asasi ya Polisi kuwa: “Afisa wa Polisi analazimika kuyatekeleza maagizo yanayotolewa kwake kwa makini na uaminifu, na hayo kwa wigo wa Sheria, Miongozo, na Nidhamu zinazotendeka”. [Mwisho]
Na katika kanuni (47) ya sheria hiyo kuwa: “Afisa yeyote anayehalifu wajibu wake ulioandikiwa katika Sheria hii, Maamuzi yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, au anaenda kinyume na wajibu wa kazi zake, anaenda mwenendo, au anaonekana katika sura inayopelekea kasoro ya heshima ya kazi zake, ataadhibiwa kisheria”. [Mwisho]
Na mfano wake katika Sheria ya Maamuzi ya Kijeshi, iliyopo katika kanuni (153) ya Sheria hii kuwa: “Mtu yeyote anayehusika na Maamuzi ya Sheria hii, akitenda jinai hizi: kuupinga usikivu wa amri za kijeshi, amri za kikosi chake, au amri zozote zingine zikiwa za maandiko au mdomo ataadhibiwa; akiwa afisa: atafukuzwa kazini, au atapewa adhabu ya chini ya hii iliyondikwa katika Sheria; na akiwa askari: adhabu yake itakuwa kufungwa au adhabu ya chini ya hii”.
Kwa vyovyote vile, usikivu wa maamrisho katika hali hii ni wajibu wa kisheria, kwa sababu kuzihifadhi Miongozo na Sheria ni miongoni mwa utiifu unaotakiwa kisheria kwa Mwenye Mamlaka; yaani Kiongozi naye ni Khalifa wa zamani au Rais wa nchi katika Nidhamu ya Kisasa ya Utawala; na pia Kiongozi ni Mwenye Mamlaka Kuu, kama vile: Makamanda wa Majeshi n.k,
Na tunatanabahisha kuwa Kiongozi sio mtu anayeonekana au mtu binafsi, lakini ni Mwakilishi wa Sheria na Miongozo, kwa lengo la kuzilazimu na uwajibu wa kuzitekeleza na kuzihifadhi, kwa sababu makusudio ya mwisho ni kuweka Nidhamu Kuu na kuzima fitina ya uasi, na kuondoa vurugu katika jamii.
Na asili ya uwajibu wa utiifu wa Kiongozi ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu, walio katika nyie (Waislamu wenzenu)}. [AN NISAA: 59].
Mtaalamu Ibn A’ashuur katika Tafsiir yake [At-Tahriir wa At-Tanwiir 5/ 97-98, Ch. Ad-Dar At-Tunusiyah Linnashr] anasema: “Wenye Mamlaka ya Umma ni wao ambao watu wanawapa jukumu la kupanga mambo yao, na wakawategemea hivyo, na amri inakuwa kama kazi yao … na wao ni wale wanaomfuata Mtume S.A.W., kama vile: Khalifa, Msimamizi wa nidhamu (Waziri), Makamanda wa Majeshi, Wanazuoni wa Masahaba na Wenye kujitahidi, Wanazuoni wa sasa kwa ujumla, pia wale wenye Mamlaka. [Mwisho]
Maimamu Bukhari na Muslim walipokea kutoka kwa Abdillahi Ibn Omar R.A., kuwa Mtume S.A.W., alisema: “Ni wajibu kwa kila mtu Mwislamu kusikia na kutii kila amri, aipende au asiipende, isipokuwa akiamrishwa kufanya maasi, hapo sio wajibu kwake kuipokea hiyo amri wala kuitii”.
Imamu At-Tirmidhiy aliipokea, na asili yake ipo katika Sahihi Muslim, kutoka kwa Wail Ibn Hajar R.A., kuwa Mtume S.A.W., aliulizwa na mtu: Unaonaje kama viongozi wetu wawe wanatutaka haki zao na wasitoe haki zenu, unatuamuru nini? Mtume S.A.W., akasema: Sikilizeni na tiini amri zao, wao watahesabiwa juu ya wajibu wao na ninyi mtahesabiwa juu ya wajibu wenu.
Utiifu wa Mwenye Mamlaka ni wajibu katika anayoyaamuru, na kuwa anayoyaamuru kwa njia ya lazima, kuyatekeleza pia ni wajibu, hata ikiwa asili yake ni ile inayotakiwa au halali au jambo linalochukiza. Imamu Ibn Hajar Al-Haitamiy katika kitabu cha: [Al-Fatawa Al-Fiqhiyah 1/278, Ch.Al-Maktabah Al-Islamiyah] anasema:
“Kauli zao: Inawajibika kumtii Imamu katika anayoyaamuru na anayoyakataza, isipokuwa yanayopinga hukumu ya Sharia, na inaonekana kuwa muradi wa yanayopinga hukumu ya Sharia kuwa: anaamuru kufanya madhambi au anakataza kutekelezwa wajibu, na hii haikusanyi jambo linalochukiza, ambapo akiamuru jambo linalochukiza, inakuwa ni wajibu kulitekeleza, na hapo hakuna kupinga”. [Mwisho]
Ndani yake pia: [2/235-236]: “Kuna uwazi wa maneno yao katika Mlango wa Uimamu kuwa: “Imamu akiamrisha jambo linalochukiza, ni wajibu kulitekeleza, na hapo kitendo kitageuzwa kiwe wajibu, na hii si mbali ya muradi”. [Mwisho]
Miongoni mwa kanuni za Sharia zinazotambuliwa ni: kazi ya Mwenye Mamlaka juu ya raia inaungana na masilahi. [Al-Ashbaah Wan-Nadhair, na As-Sayutiy; Uk. 121, Ch. Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Na Sheria hizi na mifumo ni kati ya masuala yanayoambatana na maoni ya Mwenye Mamlaka kuhusu masilahi yenye nguvu zaidi, basi anatunga sheria inayoidhibiti, kutokana na masilahi makuu, na ana haki ya kuchagua kati ya kauli za wenye jitihada ambazo anaziona kuleta masilahi yanayotakiwa. Huenda masilahi ni: kwa wigo wa mataifa ya kisasa yenye makundi ya watu mbali mbali, msimamo wa Idara za Kazi lazima uko katikati hata inayohusu sura ya wafanya kazi na wawakilishi wake, kwa hiyo huepushwa aina zote za kutofautisha za kidini, ambazo haziingii katika wigo wa wajibu wa kisheria.
Kwa hiyo inajulikana kuwa: haisihi kutotii Miongozo na Sheria kwa Hadithi ya Mtume: “Hakuna utiifu wa kiumbe ye yote katika kumuasi Mwenyezi Mungu Muumba. [Imepokelewa na At-Twabaraniy katika Al-Kabiir], kwa sababu asili ya fikra hizi mbili siyo moja.
Kwa kuwa kwa uwazi kuzinyoa ndevu si miongoni mwa dhambi, kama tuvyotaja kuwa ni jambo linalochukiza. Na hakika ya jambo linalochukiza ni kwamba: hakuna adhabu yoyote kwa mwenye kuacha kufanya, na kuna thawabu kwa mwenye kufanya kwa makusudi, (nia yakupata dhawabu) na hakika ya dhambi ni kwamba: kuna adhabu kwa kuifanya, na kuna thawabu kwa kuiacha kwa makusudi. Kwa hiyo kila moja kati ya aina hizi mbili ina uhakika tofauti na nyingine, bali maana ya Hadithi hii inaonesha utiifu wa Mwenye Mamlaka pindi anapoamrisha jambo la kuchukiza, kama alivyoashiria: An-Nafarawiy, mfuasi wa madhehebu ya Malik katika kitabu cha: [Sharhu Risalat Abi Zaid Al-Qairawaniy 1/211, Ch. Dar Al-Fikr].
Na wanazuoni walitaja kuwa jambo linalochukiza halichukizi tena ikiwa kuna haja ya kulifanya, kwa sababu kuchukiza kwa jambo kunaondoshwa kwa kulihitaji, na hayo yamesemwa na Mtaalamu As-Safariniy, mfuasi wa madhehebu ya Hanbal katika kitabu chake: [Ghidhaaul Al-Baab 1/323; 1/420; 2/18; 2/64, Ch. Muassasat Qurtubah], na akataja kuwa ni msingi wa madhehebu yao, na maelezo ya wanazuoni wa madhehebu ya Shafiy huonesha maana hii, na mfano wake: kauli zao katika kukausha maji ya udhu na kuoga kuwa: ikiwa kuna haja kwake kama kuogopa baridi, kuwepo unajisi n.k, basi hakuna jambo linalochukiza kwa uwazi. [Al-Majmuu; 1/486, Ch. Al-Muniriyah]
Na kauli zao kwa aliyetaka kuchinja udh-hiya, kuanzia siku kumi za Mfungo tatu, ni jambo linalochukiza kwake kukata kitu cha mwili wake, nywele zake mpaka kuchinja, na kuwa jambo linalochukiza linaambatana na kutokuwepo haja ya kufanya hivyo, na hii ilitajwa na kundi la wanazuoni, miongoni mwao Az-Zarkashiy [Asna Al-Matwaalib; 1/542, Ch. Dar Al-Kitaab Al-Islamiy].
Na kauli zao: ni jambo linalochukiza kwa kadhi kutoa hukumu akiwa hali ya kubadilika tabia yake, kama hasira, njaa kali, hofu kubwa, kuwa na haja, na kila linalotesa, lakini chukizo la jambo linaondoshwa hali ya kuwepo ulazima wa kutoa hukumu upesi, na huenda ikawa mara nyingi inatakiwa kutoa hukumu upesi. [Asna Al-Matwaalib: 4/298].
Na rai hiyo ilielezwa na Mtaalamu Ash-Shihaab Ar-Ramliy katika Hashiya yake ya [Asna Al-Matwaalib] miongoni mwa vitabu vya Madhehebu ya Shafiy [1/186], kwenye maneno yake ya chukizo la jambo kwa kuingia watoto msikitini, na kuwa jambo hilo silo kwa uwazi, lakini linaainishwa kwa watoto wasio na akili kamili, na kuwa kuingia kwao hakuambatani na Swala wala haja maalumu.
Na akasema: “Hali ya lazima huenda kuondosha jambo linalochukiza, kwa mfano kutumia kipande kidogo cha dhahabu kuvipamba vyombo. [Mwisho]
Hali kadhalika kwa watu hawa wanapojiunga na Taasisi za Polisi na Jeshi, wao wamekwisha kubali usikivu wa mambo yanayodhibiti kazi ndani ya Taasisi hizi, na kuendesha kazi zao baadaye.
Na kanuni ya kisheria ni kwamba: Mambo yanayojulikana kimazoea, ni sawa na Masharti yanayoshurutishwa. [Ghmzu U’uyuun Al-Basair, na Al-Hamawiy: 4/206, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], vile vile maridhiano ya kitu, ni sawa na maridhiano ya matokeo yake. [Al-Manthuur, na Az-Zarkashiy: 2/176, Ch. Wizara ya Wakfu ya Kuwait]
Na kwa hayo yote tunaongeza kuwa: Mtu yeyote kati ya watu hawa akiwa ana imani ndani ya moyo wake juu ya uwajibu wa kuzifuga ndevu, kufuatana na waliosema hivyo kati ya wanazuoni, basi katika hali hii analazimika kuwafuata hao waliosema kuwa kuzinyoa ni jambo linalochukiza; kwa ajili ya kuepusha hisia ya ndani ya dhambi; na kwa ilivyoamuliwa kabla ya hapo ni kuwa: anaejaribiwa kwa kitu kilicho tofauti basi atamfuata aliyejuzisha kati ya wanazuoni, kwa kujiepusha na uharamu, na akikataa hivyo, basi atageuza kwenda upande mwingine au Idara isiyo ya Polisi ambamo ndani yake hakuna sharti la kuzinyoa ndevu.
Na maneno yetu haya kuwa inajuzu kumfuata aliyejuzisha hayamaanishi kuwaruhusu watu waende kinyume na hukumu ya Sharia, bali kusudio ni kuyarekebisha matendo ya watu iwezekanavyo; kwa sababu mtu akifanya kitu kwa kutegemea rai inayojuzisha kisheria ni bora kuliko kukuta milango yote imefungwa, kisha hatakuta njia isipokuwa kuufanya uharamu, wakati alikuwa na ruhusa ya kumfuata aliyejuzisha.
Na kuhusu Viongozi wa Serikali, tunawanasihi kuyakagua maagizo haya, na kuyachunguza upya kwa lengo la kuelewa uwezekano wa kuwaruhusu wafanya kazi wazifuge ndevu zao, kwa kuzingatia kuwa jambo hili linaruhusiwa katika Taasisi kama hizi za nchi nyingine; na kuwa kuruhusu kuzifuga ndevu, kwa kutokuwepo kizuizi ni kuitekeleza Sunna na kuepusha kumpinga aliyewajibisha kufanywa.
Na inajulikana kuwa: kuitekeleza Sunna hata ikiwa kati ya mambo mazuri yanayotakiwa ni: sababu kubwa ya kuimarisha uongofu na kuleta ushindi, vile vile: kuepusha upingaji ni jambo linalotakiwa kwa kuzingatia kanuni ya kinga, nayo ni kanuni ya kishera kwa uwazi.
Imamu Taqiy Ad-Diin As-Subkiy katika kitabu cha: [Al Qawai’id 1/111, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] Anasema: “Kuna kauli mashuhuri katika maneno ya Maimamu, na huenda yanahesabiwa kama kauli ya pamoja… ni: kuepusha upingaji ni bora zaidi”.
Na wafanyakazi hawa wanalazimika kuyasikiliza maagizo, mpaka yatokee mabadiliko haya kwa utashi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.