Uvamizi wa Nchi kwa Ajili ya Kujinu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uvamizi wa Nchi kwa Ajili ya Kujinufaisha na Vitu Wanavyoshirikiana Watu.

Question

Tumesikia kwamba kuna Hadithi moja ya Mtume S.A.W. yenye maana ya kuwa watu wote wanashirikiana katika maji na moto na mimea. Je, Hadithi hii ni dalili ya inauhalalisha utawala wa nchi nyingine zinazovamiwa au kufunguliwa kiuchumi kwa ajili ya kujinufaisha na vitu wanavyoshirikiana watu, na maliasili zingine zinazohitajiwa na watu wote kama maji ya mito na mbao, na kila kitu kilichomo ndani ya milima, misitu na mabahari na kila kitu chenye manufaa katika maliasili na rasilimali zake zisizotokana na juhudu ya mtu yeyote? 

Answer

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa Viumbe vyote, na Rehma na Amani zimfikie Mtume wetu, yeye na jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata mpaka siku ya Malipo. Baada ya hayo:
Uislamu umeweka Uuwiano kati ya umiliki wa mtu binafsi na umiliki wa wote, na ukayapangilia mahusiano kati yao, na kuyalinda mahusiano, kwa misingi inayoihakikishia Jamii ya Kiislamu usalama, utulivu, kuleana, maendeleo yao, uzalishaji na ustawi wa jamii. Na kutokana na maana hii, Uislamu unatofautisha kati ya vitu vinavyoweza kumilikiwa na mtu binafsi na vitu vingine ambavyo haviwezi kumilikiwa na mtu binafsi bali vinakuwa ni vya umma. Na Abu-Dawud amesimulia katika Kitabu chake cha: [Sunanu Abii Dawud] na Ahmad katika Kitabu chake cha: [Sunanu Ahmad], kutoka katika Hadithi ya Abu Kheddash kutoka kwa mtu mmoja miongoni mwa Muhajiriina, katika Maswahaba wa Mtume S.A.W. amesema: Nilikuwa na Mtume S.A.W. Katika jihadi mara tatu nikamsikia anasema: "Waaisilamu wanashirikiana katika vitu vitatu: Vyakula, maji na moto".
Na katika simulizi nyingine kutoka kwa Harith Ibn Aby Usama anasema: "Watu wanashirikiana katika vitu vitatu…..". Lakini katika simulizi yake mapokezi mmoja hajulikani [Bughyatul-Baheth kutoka kwa Zawaed Musnad Al-Hareth 1\805, Ch. Markaz Khedmat Al-Sunnah wa Al-Serah Al-Nabaweyyah-Al-Madenah Al-Munawarah]”.
Na kutajwa kwa Waisilamu katika kustahiki haki hii ya maliasili hakumaanishi kuwanyima haki raia wengine Wafuasi wa dini zingine, yaani Wanaoishi na Waislamu kama vile Mayahudi na wakristo, na wengine waliowekeana mikataba ya usalama na Waislamu, bali wote hao wana haki kamili sawa na Waislamu, na pia kutajwa kwa Waisilamu hapa, kumetokana na wao kuwa ndio wengi zaidi kuliko Wafuasi wa Dini zingine, katika jamii ya Kiislamu, au kwa sababu wao ndio wanaoambiwa kwa wakati huo, kutokana na Hadithi hiyo ulipokelewa wakati wa vita; na wanajeshi wakati ule walikuwa waisilamu tu, na wala haimaanishi kwamba wengine wananyimwa haki hiyo, kwani haki hii ni haki ya kimaumbile anayoihitaji kila mtu, na Hadithi hii inaithibitisha ya kwamba haki hii ya vitu hivi vitatu vilivyotajwa hapo juu haizuiliwi kwa mtu yeyote, kama ilivyokuja katika Hadithi ya Abu Hurairah R.A, kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Vitu vitatu havizuiwi kwa mtu yeyote: Maji, Chakula na Moto". Ilisimuliwa na Ibn Majah na Usahihisha matini yake Al-Hafedh Ibn Hajar katika kitabu cha: [Al-Talkhes Al-Haber 3\153, Ch. Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] au yanayoitwa kwa maji ya Iddi. Na maana ya Maji hapa ni: Maji ya mvua, maji ya mito na maji ya visima ni yale yasiyomilikiwa na mtu yeyote.
Na mwanazuoni Al-Jamal amesema katika maelezo ya kitabu chake: [Sharhu Manhaj Al-Tollab 3/568, Ch. Dar Al-Fikr] Kauli yake:”Maji ya Idi yana maana ya maji yasiyokatalia kama maji ya kisima. Na katika kamusi ya [Al-Mesbah] maana ya Al-Iddi ni: Maji yasiyokataliwa kama maji ya kisima” Na Al-Seyutiy alisema katika maelezo ya Abu-Dawud: Ni uwingi wa daima usiokataliwa na hayahitaji kufanya kazi yoyote, na asili yake haikuja katika wakati maalumu ni kama mali. Ni kutoka katika maelezo ya Al-Sandy juu ya Kitabu cha: [Sunna cha Ibn Majah 2\93, Ch. Dar Al-Jel]. Na maana ya Al-Kalaa ni: Ardhi ya mimea na nyanyasa zisizomiliki mtu yeyote.
Ama makusudio ya Moto hapa ni kuni zinazokusanywa na watu kutoka katika miti inayoruhusiwa kutumiwa na watu wote kwa ajili ya kuwasha moto, au ni mawe yanayozunguka moto hususan katika ardhi isiyofaa kupanda mimea. [Faydhi Al-Qadeer kwa Al-Menawey 6\271, Ch. Al-Maktabah Al-Tojariyah Al-Kubra] na [Jamea Al-Usul katika Hadithi za Mtume S.A.W. kwa Ibn Al-Athiir 1/485, Ch. Maktabet Dar Al-Bayan].
Na kutokana na maana ya Hadithi za Mtume S.A.W. na maana ya istilahi tatu zote ambazo ni maji, chakula na moto ni ile inazoashiriwa kuhusu vitu visivyomilikiwa na mtu yeyote au kikundi chochote maalumu, lakini ni milki ya wananchi wote. Imekuja katika kitabu cha: [Al-Amwal cha Abu-Ebed Uk. 375, Ch. Dar Al-Fikr]: Mimi ni Abu Ubayd, alisema: Mambo haya na Sunna yalikuja kwa ujumla, na yana maana mbali mbali na hukumu tofauti: Kwanza: ni vile vinavyoruhusiwa na Mtume S.A.W. kwa watu wote kwa usawa; kama vile maji, vyakula na moto, na hasa hasa, wakati wa safari za watu na katika mazingira yao ya jangwaya katika ardhi yenye mimea iliyooteshwa na Mwenyezi Mungu kwa wanyama, na isiyopandwa na binadamu. Na anasema: Mimea hii ni kwa wale wanaoikuta na hawaruhusiwa kuwazuia watu wengine katika kuitumia na kunufaika nayo, lakini wakawalisha wanyama wao pamoja, na kadhalika maji yanayokuta katika ardhi hii kwa wote na hii ni kauli yake pia: (Watu wote wanashirikiana katika maji na vyakula) na kadhalika kauli yake: "Mwislamu ni ndugu wa mwislamu wanashirikiana katika maji na miti" kwa hivyo Mtume S.A.W. alikataza kinyume cha amri hii”.
Na vitu vinavyotajwa katika hadithi za Mtume S.A.W. kama maji, moto na vyakula, na vinavyopimiwa kutoka kwa vipengile vya nishati ni kipawa kutoka kwa Mwenyezi Mungu bila juhudi yo yote kutoka kwa binadamu kama vile, jua, hewa, kivule na nyesha mvua, kwa hivyo Mwenyezi Mungu amejaalia vitu hivi vyote vinapatikana na watu wote, utawala wake chini ya mkono wake peke yake,hakuna mtu yeyote wa binadamu ana uwezo au utawala wowote juu ya vitu kama hivi bali Mwenyezi Mungu alivitawala vitu hivi chini ya mkono wake na amevijaalia vitu hivi huru kwa manufaa ya watu wote ,mbali na utawala wa mtu yeyote ;kwani lau utawala huu chini ya mtu yeyote utasababisha ukatili miongoni mwa watu wote,kwa hivyo haijuzu kwa mtawala wa nchi yoyote aviwazuia vitu hivi .Na asili ya mambo kama haya ni halali kwa watu wote wanaweza kuyatumia haya wakati wowote wanaoyataka. Na kwa upande mwengine mtu yeyote akifanya kazi yake mwenyewe itakuwa milki yake,Ibn Majah alisimulia katika kitabu chake Sunani yake kutoka kwa Ibn Hammal kwamba aliomba kuchukua eneo laitwa ‘Melh Sadda” katika eneo la Maareb,akalimpa kwake,na baadaye Al-Aqraa Ibn Habes Al-Tamimiy alikujia Mtume S.A.W., akasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika nilikuja eneo la Melhi (chumvi) wakati wa Jahilia na ilikuwa katika eneo halina maji, na mtu yeyote anayekwenda kwake aliweza kuichukua, na hii ni kama Maji Al-Iddi, Mtume S.A.W. akamstaafu Abyadh Ibn Hammal katika eneo lake la Melhi akasema: Nikulistaafu eneo hili lakini kwa sharti moja, sharti hii umelijaalia eneo hili ni Sadaqah kutoka mimi, Mtume S.A.W.: "Yeye kutoka kwako ni Sadaqah, na yeye ni kama Maji anayekujia kuyachukua".
Al-Sanadiy alisema katika maelezo yake kutoka kwa Ibn Majah [2\93, Ch. Dar Al-JIL]:”Akampa kwake”kwa maana akampa eneo hili, ilisemwa: ilidhaniwa kulipatia madini kutoka kwake kwa kazi ya bidii, lakini baada ya kulidhihirisha kinyume chake alirejelea (akastaafu) .Al-Seyutiy alisema kutoka kwa Al-Sobkiy: Ni dhahiri kwamba aliiacha kwa ukarimu wake Mtume S.A.W., na kauli yake Mtume S.A.W.: "Yeye ni Sadaqa kutoka kwako": ni mubalaghah kutoka kwa maadili ya tabia yake,na ilisemwa pia: ni dalili juu ya kwamba kuipa maadini ni juzu halali sharti ya kuipata yanayokuwa ndani yak chini kwa kazi na taabu, lakini ikiwa ni kitu dhahiri na kuipata vitu vyake kwa urahisi bila ya kazi au taabu basi haijuzu kuichukua au kuiipa kwa mtu yeyote, bali watu wote katika amri hii ni sawa kama maji na mimea,na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi.
Kwa upande mwingine vitu vinavyokuwa katika ardhi ya mtu maalumu anayeimiliki hiyo ardhi ni miliki yake mwenyewe na haijuzu kwa mtu yeyote kuchukua chochote bila ya idhini ya mmiliki huyo wa ardhi hiyo. Imamu Khattabiy amesema katika kitabu chake:“[Maalimu Sunan 3/129, Ch. Al-Matbaah Al-Elmiyah]: Maana ya maneno hayo ni mimea inayotoka katika ardhi maiti -yaani mimea kuitoka ardhini bila ya taabu au kazi yoyote ya binadamu-na watu wanaihimizia kwake basi manufaa na mimea ya ardhi hii siyo kwa mtu yeyote binafsi bali ni mali ya watu wote na haiwezikani kuizuia mtu yeyote kutoka kwake, na watu wa Jahiliyah, mtu yeyote akiichukuwa ardhi yoyote kwa nguvu kwa wanyama wake ili walikula, mtu huyu alikuwa akiwazuia watu wengine, lakini Mtume S.A.W. amebatilisha jambo hili na akawajaalia watu wote ni sawa kwa kuitumia ardhi hii kwa sheria miongoni mwa watu wote, lakini lau mimea inatoa katika ardhi ya mtu yeyote mwenyewe basi mimea na ardhi ni milki ya mtu huyu mwenyewe, na haiwezi mtu yeyote kuishirikiana naye ila kwa idhini yake. Lakini pamoja na kuthibiti ya umilki wa binafsi kwa mtu basi yapasa asiwazuia watu katika yanayoyazidishia kwake juu ya haja yake na hakuuzwi kwao, kwani katika hadithi ya Mtume S.A.W. kutoka kwa Abu Hurairah alisema kwamba Mtume S.A.W. Amesema: "Haizuia fadhili ziada ya maji ili kuizuia fadhili ziada ya mimea".
Al-Imam Al-Nawawiyy alisema katika maelezo ya Muslim [10\229, Ch. Dar Ihyaa Al-Turath Al-Arabiy]:”Masahaba zetu walisema: Kutumia maji jangwani kwa sharti kama tulizotajwa: Sharti ya kwanza ni: Hayakuwa maji mengine ya kutumia badala ya maji haya. Na ya pili ni: Ni kutumia maji kwa kunyiwa wanyama siyo kwa mimea.Na ya tatu ni: Lau mwenyi maji hakuyahitaji maji haya.Na lau maji yatoka katika milki mtu mmoja,basi maji haya ni kwake mwenyewe na hii ni madhehebu sahihi, na baadhi ya masahaba walisema: Hayamiliki. Ama akichukuwa maji katika kitu chochote ni halali na ni kuwa milki yake na hii ni sahihi, na baadhi yao walisema kwa ijimaa ya wanazuoni,na baadhi yao walisema hayamiliki bali yakuwa ni kuyahusu kwake. Na hii ni makosa dhahiri. Ama kuhusu kauli yake: Hayauzi maji kwa kuiuza mimea, kwa maana lau yakuwa baki maji kwa jangwa kama tulivyotajwa na kuna mimea yahitaji maji na wakati huu huu lazima kuiweka maji kwa wanyama na akiyauza maji ni kama kwamba kuiuza mimea inayohalali kwa watu wote na yasiyokuwa milki ya mwuzaji, na sababu ya haya ni kwamba wenye wanyama hawafanya juhudi au kuzipa bei ya maji haya na ni kama kwamba kuiuza mimea. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi.
Al-Imam Ahmad alitaja katika kitabu chake kutoka kwa Imran Ibn Umaiyr alisema: Nilishtaki kwa Ubaiyd Allah Ibn Abdullah kaumu moja walikataa kunipa maji, akasema: Nilisikia Abu Hurayrah, na Al-Masudy kwamba Mtume S.A.W. alisema: "Hayazuia maji yanayozidishia haja yake wala mimea".
Na katika kitabu cha“Al-Amwal”kwa Al-Qasem Ibn Salam [Uk. 377, Ch. Dar Al-Fikr]:”Ama kauli yake: Hayazuii maji yanayozidishia haja yake wala mimea ni ghairi ya hayo, na maana yake kwangu ni katika ardhi inayomilikiwa na mtu maalumu, na ardhi hii ina maji kama tulivyosifiwa, na ina mimea inayotoka ardhini bila ya taabu au gharama ya kisima ya maji au kulima mimea yoyote. Kwa hivyo Mtume S.A.W. alimruhusia kwa kupata kwa dharura, na alikataa nyingine, na walau hakumiliki kwake asingetaja neno la ziada hapa, na watu wote watakuwa ni usawa kisheria katika uchache na unyingi wake.
Kwa upande mwengine lau kuwa kuna maji,mimea na moto katika ardhi maiti yaani haina maliki au sahibu kwake, na baadhi ya watu waliitangulia kwake na walikaa karibu naye, basi watu hawa wanafaidika kwanza na hawazuia wengine kutoka kwa kuitumia vitu hivi. Kwani asili ya vitu hivi ni halali kwa watu wote vya kuvitumia; kwani watu wote ni wanashirikiana katika utumiaji wake kwa usawa lakini baadhi yao yaweza kuchukuwa kitangulia cha kutumia. Na dalili ya hayo katika hadithi ya Mtume S.A.W. kutoka kwa Ubada Ibn Al-Samet alisema "kwamba Mtume S.A.W. alihukumu katika kinywaji cha mitende kutoka kwa maji ya mtiririko wa mvua ya juu kasha ya juu baadaye, kwa maana ya juu kunywa kabla ya chini, na kuyaacha maji mpaka miguu ya chini, halafu kuyapeleka maji kwa chini moja kwa moja, mpaka kwisha maji". Imesimuliwa na Ibn Majah.
Na kutoka kwa Abdullah Ibn Al-Zubayr R.A. kwamba mtu mmoja kutoka Al-Answar alishtakiwa Al-Zubayr kwa Mtume S.A.W. katika kitu cha kutumia kwa kucuta maji kwa mtende, mtu wa Al-Answariy alisema acha maji yapita, lakini alikataa, kwa hivyo walihasimiana na walishtakiwa mbele ya Mtume S.A.W., na Mtume S.A.W., akasema kwa Al-Zubayr "Ewe Al-Zubayr mwagilia, halafu acha maji kwa jirani yako", Al-Answariy akakasirika, akasema: ni kwa sababu yeye ni Ibn ya Shangazi yako? Wakati huu huu uso wa Mtume S.A.W. alichagua rangi yake. halafu akasema: "Ewe Zubayr mwangilia, halafu funga maji mpaka rejea kwa mzizi", Al-Zubayr alisema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu nadhani Aya hii iliteremsha katika jambo hili:{La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana} [AN NISAA 65].
Imamu An-Nawawiy anaema katika maelezo ya Hadithi kutoka katika kitabu cha: [Sharhu Sahihil Muslim 15/108]: Na maana ya kurejea katika ukuta ni kuelekea huko, na maana ya ukuta huo ni asili ya ukuta na inasemekana pia kwamba ni mizizi ya miti, na maana iliyo sahihi ni ya kwanza na Wanachuo ni wamekadiria Kiwango chake ambacho ni kupanda kwa maji ardhini mpaka yakalowanisha mguu wa mtu, na kwa hivyo Mtu wa ardhi ya kwanza yenye maji hayo, ana haki yeye ya kuyafungia maji ardhini kwa Kiwango hicho kisha ayafungulie yaende kwa jirani yake aliye nyuma yake, na Zubaiyr alikuwa mmiliki wa ardhi ya kwanza, na Mtume S.A.W. akamwelekeza na akasema: Mwangilia kisha uyaelekeze maji kwa jirani yako) kwa maana kwamba: mwangilia kwa kiasi kidogo zaidi ya kiasi chako kisha utaelekea maji hayo kwa jirani yako. Na haya ni maelekezo kwa Zubaiyr na kumfahamisha aliridhike na kiasi hicho cha maji na mapendeleo zaidi jirani yake. Na jirani yake aliposema aliyoyasema, Mtume S.A.W. alimwamuru achukue haki zake zote.
Na kwa msingi huu, mikataba na makubaliano ya kimataifa yanafanya kazi ya kuweka mipaka ya kijiografia ya nchi zote Duniani na huifanya kila nchi iwe na haki ya kila maliasili inayopatikana ndani ya mipaka ya nchi hiyo, na haijuzi kwa nchi nyingine kuishambulia kwa kuivamia au kuitishia au vyovyote iwavyo miongoni mwao aina za mabavu na ushambuliaji ili tu kunufaika na maliasili zake kwa nguvu na kwa kulazimisha, hakika mambo yalivyo, uhalali wa kunufaika na mali za nchi unakuwepo kwa Misingi ya Kisheria na desturi za kimataifa na kwa kuomba idhini na kukubaliana na kwa Kiwango kilichowekwa na nchi yenye maliasili husika. Na hapo ni pale ambapo sababu ya dharura haikuingia katika suala hili, na kama nchi nyingine itakuwa inahitaji kunufaika na maliasili hizo kwa dharura ya kutaka kuiokoa isiangamie na kuporomoka, basi ni wajibu wa nchi jirani na nchi hiyo kuipa mkono wa msaada na kuisaidia bure inachokihitaji, kutoka katika ongezeko la ziada la malighafi hizo kutokana na ukubwa wa dharura ya nchi hizo ya kuhitaji vile wanavyoshirikiana watu, na kama sio hivyo, kiasili nchi yenye kustahhak zaidi fadhila na nyongeza ni ile iliyo karibu zaidi na maliasili hizo, uwe ni mto, msitu au majani ya aliyojiotea yenyewe.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia, haijuzu kutoa dalili katika Hadithi ya Mtume S.A.W. katika swali lililoulizwa, juu ya uhalali wa kuanzisha vita na kuzivamia nchi nyingine kwa ajili ya kujinufaisha na maliasili zilizomo ndani ya mipaka yake ya kijiografia na chini ya utawala wake, -ambapo wananchi wake wanahitaji mno uwepo wa kutosha wa maliasili hizo- na kisha kuzihalalisha kwa watu wote, kama vile maji, moto, ndishe na chumvi, na ambavyo vimetajwa katika Hadithi za Mtume S.A.W, na kila kinachoingia katika maana hiyo kwa namna ambayo haihitaji juhudi nyingi zaidi na kazi nzito kabla ya kunufaika navyo, ili vipatikane. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi. 
 

Share this:

Related Fatwas