Ushoga

Egypt's Dar Al-Ifta

Ushoga

Question

Ni upi ukweli wa Ushoga, na ni ipi Hukumu yake Katika Sheria ya Kiislamu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya utangulizo huo:
Ushoga ni istilahi mpya inayohusu matumizi yote yanayoambatana na matamanio ya utupu, yanayokwenda kinyume na umbile la kibinadamu, ambalo Mwenyezi Mungu aliwaumbia wanadamu.
Na matumizi haya ni kosa katika hukumu ya Sheria na ni dhambi ya wazi, na mwenye kufanya hivyo ni asi kwa Mwenyezi Mungu, kwa hiyo anastahiki adhabu hapa Dunia na huko Akhera, isipokuwa atakapotubu.
Na mwenyezi Mungu anasema: {Na ambao tupu zao wanazilinda. Isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, (kulia). Basi hao ndio wasiolaumiwa. (Lakini) anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka (ya Mwenyezi Mungu)} [AL MUMINUN: 5-7].
Na hii ni dalili ya kuwa: kila aina ya matumizi na matamanio ya kijinsia nje ya wigo wa mahusiano ya kisheria ambayo Mwenyezi Mungu ameyaruhusu, yote hayajuzu; kwa sababu yanazingatiwa kuwa ni uadui, dhulma, na kuchupa mipaka ya Mwenyezi Mungu.
Na kazi hii ni kuzuia umbile madhubuti ambao hupelekea mazoea ya kutokuwa na mvuto baina ya mwanamume na mwanamke kisha sharia inaweka mipaka na vigezo vinavyoruhusu na kupangilia Jambo hili.
Na kuzuia umbile madhubuti kuhusu uhusiano wa jinsia kunadhihirika katika kutoshelezeana baina ya jinsia mbili, yaani mwanamume anatosheka na mwenzake, na mwanamke anatosheka na mwenzake. Na huenda matumizi haya yakawa kwa jinsia ya Mnyama, yaani mwanadamu kwa mnyama, kama itakavyokuja. Na tutazungumzia kila aina moja ya matumizi haya.
Na kuhusu uhanithi, maana yake ya kilugha ni: viteno vya watu wa Lutwi. Na Al-Laith anasema: Lutwi alikuwa Nabii, na Mwenyazi Mungu alimtuma kwa watu wake, wakamkadhibisha, wakafanya walivyofanya, kwa hiyo watu jina lake likanasibishwa na vitendo vya watu wake. [Lisaan Al-Arab: 7/ 396, Ch. ya Dar Saadir]
Na katika istilahi ni: mtu kuingiza kichwa cha uume au kiasi kidogo cha kichwa hicho katika utupu wa nyuma wa mwanaume au mwanamke, hata kama ni mtumwa wake, [Al-Iqnaa’, pamoja na Al-Bijirmiy: 4/176, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Zinaa na uhanithi zimekusanywa kuwa zote ni kuingilia kulikoharamishwa, isipokuwa uhanithi ni kuingilia katika tupu ya nyuma, na zinaa ni kuingilia katika tupu ya mbele.
Na Ibn Qudamah anasema: “Wanazuoni wamekubaliana pamoja kuuharimisha uhanithi, na Mwenyezi Mungu ameulaani katika Kitabu chake, na kumfedhehesha mwenye kuufanya. Pia Mtume S.A.W., ameulaani. Na Mwenyezi Mungu anasema: {Na (tulimpelekea) Luti. Basi (wakumbushe watu wako) alipowaambia Watu wake: “Je! Mnafanya jambo chafu ambalo hajakutangulieni yoyote kwa (jambo chafu) hilo katika walimwengu”. “Nyinyi mnawaendea wanaume kwa kuwa ndio mnaowatamani badala ya wanawake! Ama nyinyi ni watu wafujaji”} [AL AARAF: 80-81], na Mtume S.A.W. anasema: “Mwenyezi Mungu anamlaani mtu anayefanya kitendo cha watu wa Luti, Mwenyezi Mungu anamlaani mtu anayefanya kitendo cha watu wa Luti, Mwenyezi Mungu anamlaani mtu anayefanya kitendo cha watu wa Luti”. [Al-Mughniy: 9/60, Ch. ya Maktabat Al-Qahirah].
Al-Mawardiy anasema: “Uhanithi ni miongoni mwa mambo machafu kabisa kiuharamu, na Mwenyezi Mungu anasema: {Na (tulimpelekea) Luti. Basi (wakumbushe watu wako) alipowaambia kaumu yake: “Je! Mnafanya jambo chafu ambalo hajakutangulieni yoyote kwa (jambo chafu) hilo katika walimwengu”. “Nyinyi mnawaendea wanaume kwa kuwa ndio mnaowatamani badala ya wanawake! Ama nyinyi ni watu wafujaji”} [AL AARAF: 80-81]. Basi ameujaalia miongoni mwa mambo machafu sana, kwa hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaadhibu watu wa Luti kwa kuwadidimiza ardhini, na akawashushia adhabu kali, Ili mwanaume asije kumuendea mwanaume mwenzake. Na imepokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W, kuwa alisema: “Mwenyezi Mungu anamlaani mtu anayefanya kitendo cha watu wa Luti, Mwenyezi Mungu anamlaani mtu anayefanya kitendo cha watu wa Luti”… na imethibitishwa kuwa uhanithi ni miongoni mwa mambo machafu kabisa, na unafungamana na adhabu kali kabisa”. [Al-Hawiy: 13/222, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]
Na miongoni mwa Hadithi zilizotajwa katika mlango huu: ni ile iliyopokelewa na Ibn Majah na At-Tirmidhiy ambaye alisema: ni Hadithi yenye hukumu ya Hassan Ghariib; na imesahihishwa na Al-Hakim, kutoka kwa Jaabir Ibn Abdillahi R.A, alisema: Mtume S.A.W. alisema: “Kilichonihofisha sana kuliko chochote katika umma wangu, ni kitendo cha watu wa Luti”.
Na An-Nasaaiy katika kitabu cha: [As-Sunanul-Kubra], Ibn Hibban katika kitabu chake, na Al-Baihaqiy walipokea kutoka kwa Ibn Abbas R.A,: “Mwenyezi Mungu Mtukufu anamlaani mtu anayefanya kitendo cha watu wa Luti, Mwenyezi Mungu anamlaani mtu aliyefanya kitendo cha watu wa Lutwi, Mwenyezi Mungu anamlaani mtu aliyefanya kitendo cha watu wa Lutwi”.
Na Al-Haitamiy alikihesabia kitendo hicho kuwa ni miongoni mwa dhambi kubwa, akisema: “Hakika Mwenyezi Mungu amekiita kitendo hicho kuwa ni kitendo kichafu, na kisichopendeza, kama itakavyokuja kuelezwa, na akataja adhabu ya watu wa taifa lililotangulia, na kitendo hicho kinazingatiwa kuwa ni uzinzi, kwa rai mashuhuri ya wafuasi wa Madhehebu ya Imamu Shafiy, kwa dalili ya Qiyasi ya lugha, na kitendo hicho kinawajibisha adhabu kwa mujibu wa rai ya wengi wa wanazuoni.
Na Mwenyezi Mungu hakulishushia adhabu taifa lo lote kama alivyolishushia adhabu taifa la watu wa Lutwi, hakika aliwapofua macho yao, akazipaka nyuso zao weusi, akamuamuru Jibrililu aving’oe vijiji vyao kutoka chini ya mizizi yake, kisha avipindue pindue juu chini, kisha awadidimize ardhini, kisha awanyeeshee mvua kubwa ya mawe ya Jahannamu kutoka mbinguni.
Na Maswahaba walikubaliana pamoja kuwa mwenye kufanya kitendo cha uhanithi auawe, na wakahitilafiana kuhusu namna ya kumuua.
Na umma wote umekubaliana pamoja kuwa aliyemfanyia mtumwa wake kitendo kulawiti cha watu wa Lutwi, anazingatiwa kuwa ni miongoni mwa watu wa Luti walio wachafu na wenye kulaaniwa, na kwa ajili hiyo, Mtu mwenye sifa hizi anastahiki laana ya Mwenyezi Mungu, na anastahiki laana ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na anastahiki laana ya Mwenyezi Mungu, na Malaika, na watu wote.
Na kitendo hicho kilienea kwa matajiri na wapenda anasa, ambao walijitafutia watumwa wao, wawe weusi au weupe, kwa ajili ya kitendo hicho, kwa hiyo wanastahiki laana kali ya kudumu na ya dhahiri, na fedheha kubwa kabisa, maangamizi, na adhabu hapa duniani na kesho Akhera, kwa kipindi cha wao kudumu katika kufanya mabaya, matusi, machafu, na maovu ambayo yanaletea ufakiri, uangamizi wa mali, kuondoka kwa baraka, pamoja na hiyana katika mtangamano na amana.
Kwa hiyo unawakuta wengi wao walifilisika, kutokana na waliyoyachuma, na kumfanyia matendo mabaya aliyewaneemesha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwapa, na hawajaribu kurejea kwake yeye aliye Mwanzilishi wake, Muumbaji wake, Mtengenezaji wake, na Mtoa riziki wake, na badala yake wakalifanya hili linaloundwa kwa kuvua kanzu ya hayaa na muruwa, na kuziepusha sifa za waungwana na mashujaa, na kuzipata sifa za wanyama.
Hakika alipata sana sifa mbaya na mbovu kuliko zote, ambapo hatukuti mnyama dume amwingilie mwenzake, na vipi sifa hii inayoipushwa na punda, na vipi anaikubali huyu mwenye sifa ya uongozi au ukubwa, hapana bali yeye ni wa chini kabisa kuliko uchafu wake, na mbaya sana kuliko habari yake, na mvundo sana kuliko mzoga, na anastahiki ubaya na fedheha, na ni mwenye ari na dharau, na haini kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu na amana aliyoipewa, basi aepushwe na afukuzwe kabisa, na aangamizwe ndani ya Moto na achomwe”. [Az-Zawajir: 2/231-235, Ch. ya Dar Al-Fikr]
Na Al-Manawiy kuhusu kazi ya watu wa Luti anasema: “Ni kazi mbaya sana kuliko zote, kwa sababu kila lilioumbwa na Mwenyezi Mungu katika ulimwengu, alilijaalia sawa na kitendo maalumu, kisichoendana na kingine, na akajaalia mwanaume mtendaji na mwanamke mtendewa, na akaweka ndani yao matamanio kwa ajili ya uzazi na kuwepo jinsi, kwa hiyo mwenye kugeuza hivyo basi ataondoa hekima ya Mola.
Na kitendo hichi kimelaaniwa kisheria, kiakili, na kitabia; ambapo kisheria ni katika Aya hii: {Na tukawamiminia mvua ya mawe ya udongo wa motoni}. [AL HIJR: 74]. Na imepokelewa Kuwa Jiburilu A.S, aliviinua vijiji vya watu wa Luti juu ya mbawa zake mpaka watu wa mbinguni wakasikia sauti ya mbwa zao na majogoo pia, kisha akavipindua pindua, na akavinyeshea mvua ya mawe juu yake. Na kiakili: kwa sababu Mwenyezi Mungu alimuumba binadamu kwa ubora zaidi kuliko kuliko viumbe vingine vyote, na akampulizia nafsi itamkayo na ambayo huitwa roho kwa kauli ya Sharia, na akaweka ndani yake pia nguvu ya mwili.
Hayo yote ni kwa ajili ya kumfanya amjue Mola wake na mambo ya juu ambayo miongoni mwayo ni kujua sababu na hekima zake, na kitendo hiki kinaondosha hekima yake, kama ilivyotajwa hapo juu. Na kitabia: ni kwa sababu kitendo hiki hakitimizwi isipokuwa kwa kuwapo mtendaji na mtendewa, na uovu wa tabia inayoyakiuka maumbile”. [Faidhul Qadiir: 2/420, Ch. Ya Al-Maktabah At-Tijariyah]
Wengi wa wanazuoni walikubaliana adhabu kali ya mlawiti, na wakahitilafiana katika namna yake. Imamu Abu Hanifa, mbali na wanafunzi wake wawili, anaona kuwa mlawiti lazima atukanwe na kukemewa, ambapo maneno makali na matusi ni adhabu ndogo mno kuliko adhabu kali anayostahili kuadhibiwa kwayo. Vile vile wanazuoni wamekubaliana juu ya uharamu wa kitengo hiki cha watu wa Lutwi, lakini wakahitilafiana juu ya adhabu ya mlawiti. Imamu Shafiy katika moja ya rai mbili na Abu Yusuf na Muhammad, wanaona kuwa muhusika wa kitendo hiki analazimika kuadhibiwa adhabu ya uzinifu; kwa maana ya kwamba; atapigwa mawe hadi kufa akiwa ameoa, na asiyeoa atapigwa viboko mia moja. Kuhusu mtendewa: Imamu Shafiy kwa rai yake hii, anasema kwamba: Mtu huyu atapigwa viboko mia moja na atapelekwa ugenini kwa muda wa mwaka mmoja, akiwa mwanamume aliyeoa au mwanamke aliyeolewa, au ambao bado hawajaingia katika ndoa.
Wanazuoni wengine walielekea kuwa mlawiti anapigwa mawe akiwa ni mwenye kuoa au siyo, na rai hii pia ni ya Imamu Malik na Imamu Ahmad, na kauli nyingine ya Imamu Shafiy wauwawe wote mtendaji na mtendewa, kwa kutegemea dhahiri ya Hadithi; na kuhusu namna ya kuwaua, imesemwa kuwa waporomoshewe jengo juu yao, na imesemwa pia watupwe kutoka mlimani kama ilivyofanywa kwa watu wa Luti. Na rai ya Imamu Abu Hanifa: mlawiti anateswa bila ya kupewa adhabu kali, kama ilivyotajwa katika: [Maa’alim As-Sunan, na Al-Khattabiy: 3/333, Ch. ya Al-Matbaa’ah Al-Ilmiyah; Sharh As-Sunnah, na Al-Baghawiy: 10/310, Ch. ya Al-Maktab Al-Islamiy].
Lakini kwa rai ya wafuasi wa madhehebu ya Hanafiy kuwa: aliyezoea kufanya hiyo, basi Imamu ana hiari juu yake, akitaka atamuua au atampiga au atamfunga, kama ilivyotajwa katika: [Hashiyat Ibn A’abidiin: 4/27, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Al-Haskafiy anasema: “Katika kitabu cha Al-Bahr: Uharamu wa kitendo hiki ni mbaya zaidi kuliko zinaa; kwa sababu uharamu wake ni wa kiakili, kisheria, na kimaumbile, na katika Al-Mujtabaa: mwenye kukihalalisha kitendo hiki ni kafiri, kwa rai ya wengi wa wanazuoni” [Ad-Durul Mukhtar: 4/28].
Na Ad-Dimishqiy Al-Uthmaniy anasema: “walikubaliana kuwa uhanithi ni haramu, na ni miongoni mwa dhambi chafu sana”. [Ramatul Ummah: Uk. 358, Ch. ya Qatar]
Al-U’umraniy anasema: “Uhanithi ni haramu, nao ni kuwaendea wanaume katika tupu zao za nyuma, na kitendo hicho ni miongoni mwa madhambi makubwa… na Waislamu wamekubaliana pamoja kuwa ni haramu”. [Al-Bayan: 12/264-366, Ch. ya Dar Al-Minhaaj]
Na miongoni mwa vitendo hivyo vya Haramu ni ushoga na usagaji na kusagana.
Na maana yake ni: Mwanamke anapomfanyia mwanamke mwenzake, kama wanavyofanya mwanamume na mwanamke.
Na hukumu yake: Hakuna hitilafu kati ya wanazuoni kuwa: Usagaji ni haramu; kwa kauli yake Mtume S.A.W.: “Kusagana kwa wanawake kunazingatia kuwa ni zinaa.baina”. [Hadithi hii imepokelewa na At-Tabaraniy katika Al-Mu’jam Al-Kabiir].
Na Ibn Hajar alikuhesabia Kusagana kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa, akasema: “Usagaji wa wanawake ni mwanamke anapomfanyia mwanamke mwenzake, kama mwanamume anavyomfanyia mwanamke, hivyo ndivyo ilivyotajwa na baadhi ya wanazuoni, wakitoa dalili ya kauli yake Mtume S.A.W.: “Usagaji ni zinaa ya wanawake baina yao”, na kauli yake: “Mwenyezi Mungu hakubali Shahada ya: Hakuna Aabudiwaye kwa haki isipokuwa Mwenuezi Mungu, kutoka kwa watu watatu: Mpandaji mwenzake wa kiume, na Mpandwaji; Mpandaji mwenzake wa kike, na Mpandiwa; na Imamu dhalimu”. [Az-Zawajir: 2/235].
Al-Manawiy anasema: “Kwa jumla: Adh-Dhahabiy na wengine waliuhesabia miongoni mwa dhambi kubwa, kwa mujibu wa Hadithi hii na nyingineyo”. [Faidhul Qadiir: 4/135].
Wanazuoni walikubaliana pamoja kuwa: hakuna adhabu kuhusu usagaji; kwa sababu sio zinaa, lakini inalazimika kuadabishwa; kwa sababu ni kosa.
Na Ibn Qudamah anasema: “wanawake wanaposagana, basi wao wanazigantiwa Kuwa ni wazinifu zinaa, na wanalaaniwa, kutokana na ilivyopokelewa na Mtume S.A.W., kuwa alisema: “Mwanamke akimwendea mwenzake, basi wao wote wawili ni wazinifu”, na haiwawajibikii adhabu; kwa sababu tendo hili sio la kuingiliana, na mfano wake kama ni wa kuingiliana nje ya tupu zao, lakini ni lazima waadabishwe; kwa sababu kitendo chao kinazingatia Kuwa ni zinaa isiyo na adhabu, na mfano wake ni kama kugusana mwanamume na mwanamke bila ya kuingiliana”. [Al-Mughniy: 9/58].
Na Al-Mawardiy anasema: “Maana halisi ya usagaji ni: mwanamke kumuendea mwanamke mwenzake, na kitendo hicho kukatazwa kama zinaa, na tofauti kati yake ni adhabu; kwa liivyopokelewa na Mtume S.A.W. kuwa alisema: “Usagaji ni zinaa kati ya wanawake” na unalazimika adabu bila ya adhabu, kwa sababu hakuna kuingiliana kati yao”. [Al-Hawiy Al-Kabiir: 13/224].
Na Al-U’umraniy anasema: “Inaharamishwa mwanamke kumwendea mwenzake; kwa kauli yake Mtume S.A.W.: “Mwanamke akimwendea mwenzake, basi wao ni wenye zinaa” kwa hiyo waadhibiwe, kwa sababu ni kosa lisilo na adhabu wala kafara. Na Imamu Malik anasema: kila mmoja kati yao analazimika adhabu ya kupigwa viboko mia”. [Al-Bayan: 12/369].
Na An-Nafarawiy mfuasi wa madhehebu ya Malik anasema: Mwanamke aadabishwe akisagiana na mwenzake”. [Al-Fawakih Ad-Dawaniy: 2/209, Ch. ya Dar Al-Fikr]
Na Sheikh U’ulaish anasema: “Usagaji yaani mwanamke kugusana na mwenzake mpaka wakapata hisia za ladha ya mapenzi, bila kuzini, kwa sababu hakuna kuingiliana kwa tupu zao, na adhabu ya kuwaadabisha inakadiriwa kwa jitihada ya Imamu. [Minahul Jaliil: 9/251, Ch. ya Dar Al-Fikr]
Na Al-Buhutiy anasema: “(lazima waadabishwe) yaani mfanyaji na mfanyiwa nje ya utupu, vile vile wale wanaosagana, na Jike dume wakiingiliana katika utupu; kwa sababu ya kufanyika kwa maasi haya”. [Kashful Qinaa’: 6/96, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Na Ibn Al-Humam anasema: “Mwanamke akimwendea mwanamke mwenzake, basi wao waadabishwe kwa ajili ya hayo”. [Fat-hul Qadiir: 5/262, Ch. ya Dar Al-Fikr]
Na miongoni mwa matumizi yasiyo ya kawaida ni: kuingiliana na mnyama:
Na wanazuoni wamekubaliana juu ya uharamu wa kuingiliana na mnyama, kwa sababu ya kukusanywa kwake katika kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na ambao tupu zao wanazilinda. Isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, (kulia). Basi hao ndio wasiolaumiwa, (lakini) anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka (ya Mwenyezi Mungu)}, pamoja na kupokelewa kuhusu hukumu hii katika baadhi ya Hadithi, lakini zote ni dhaifu.
Na Al-Fakhr Ar-Raziy anasema: “Umma wote umekubaliana pamoja juu ya uharamu wa kuingiliana na wanyama”. [Tafsiir Mafatiih Al-Ghaib: 23/305, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turaath Al-Arabiy]
Na kundi la wanazuoni walitaja kuwa ni miongoni mwa dhambi kubwa na vitendo vichafu, kama ilivyotajwa katika: [Az-zawajir: 2/139; na Tanbiih Al-Ghafiliin, na Ibn An-Nahaas, Uk. 287, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Kuhusu adhabu yake ya kidunia, wanazuoni wanahitilafiana: Je, adhabu ni lazima, au inatosha kuadabishwa? Kama ilivyotajwa katika: [An-Najmul Wahaaj: 9/ 108, ch. ya Dar Al-Minhaj; Maa’alim As-Sunan: 4/ 609; Rahmatul Ummah: Uk. 358].
Al-U’umraniy anasema: “Ni haramu kumwendea mnyama, kwa kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na ambao tupu zao wanazilinda. Isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, (kulia). Basi hao ndio wasiolaumiwa}. Kwa hiyo mtu mwenye hukumu ya adhabu ya zinaa akifanya hivyo, basi atawajibika nini? Kuna kauli tatu, Ya kwanza: lazima auawe, awe mtu huyo alimeoa au hajaoa. Na hii ni rai ya Abu Salama Ibn Abdur Rahman; Ya pili: ni kama zinaa, yaani atapigwa vipoko kama hajaoa, na atapigwa mawe mpaka afe kama atakuwa ameoa; na ya Tatu: hakuna uwajibu wa kumuadhibu bali ataadabishwa, na rai hii ni ya wanazuoni wengi”. [Al-Bayan: 12/370].
Na Al-Buhutiy anasema: “(Mwenye kumuendea mnyama yoyote ataadibiwa) kwa sababu hakuna andiko lolote sahihi kwake, na haiwezekani kukilinganisha kitendo hiki na uhanithi; kwa sababu mnyama si kama mwanadamu na pia ni kitendo kisichokubalika, na (ataadabishwa papo hapo) kwa sababu hakuna utatanishi, ni kama vile kumwingilia maiti”. [Kashaful Qinaa’: 6/95].
Na miongono mwa matumizi yasiyo ya kawaida ni: mwanamke kuingiliwa na mnyama:
Sura hii imetajwa katika vitabu vya wanazuoni, waliiunganisha na hukumu ya mwanaume aliyemwendea mnyama, sura iliyojadiliwa hapo juu.
Ad-Dumairiy anasema: “Mwanamke akiingiliwa na kima, hukumu yake ni mfano wa mwanaume kumwendea mnyama. Na haya yamenukuliwa na Al-Baghawiy pamoja na wanachuoni wengineo”. [An-Najm Al-wahaaj: 9/109].
Na Ibn A’abidiin anasema: “Mwanamke akiingiliwa na kima, hukumu yake ni mfano wa kuwaendea wanyama, yaani hana adhabu yoyote ila huadabishwa tu”. [Hashiyat Ibn A’abidiin: 3/155].
Na Al-Buhutiy anasema: “(Mwanamke akiingiliwa na kima, hukumu yake ni mfano wa kumwendea mnyama) kwa maana ya: kuadabishwa kiasi chake, kwa mujibu wa madhehebu, na kwa mujibu wa rai nyingine: auliwe”. [Mwisho, Kashaful Qinaa’: 6/95].
Na Ad-Disuqiy anasema: “Aliyefanya hivyo, aadabishwe”. [Ad-Disuqiy Ala Ash-Sharh Al-kabiir: 4/242, Ch. ya Dar Al-Fikr]
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia: Hakika ushoga ni kitendo kilicho kinyume cha maumbile ambayo Mwenyezi Mungu aliwaumbia watu: kwa hiyo Sharia inabainisha kuwa inahalalisha kuingiliana kwa njia ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaumbia watu, na namna ilivyohalalishwa katika Sharia, na kwamba inakuwa haramu na inapelekea kuadhibiwa kwa aliyejiepusha na uhalali mpana wa kimaumblie, kwa kuelekea katika eneo finyu la uharamu usio wa kawaida. Vile vile ni haramu kuweka sheria inayoruhusu matumizi yasiyo ya kawaida, na kuitangaza, kwa njia yoyote iwayo. Na mtu aliyeishi katika nchi ambayo inaruhusu kisheria matumizi yasiyo ya kawaida, basi haijuzu kwake kufanya hivyo; kwa sababu ni haramu kwa kauli ya pamoja ya wanazuoni wa Kiislamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

 

Share this:

Related Fatwas