Jukumu la Kijinai la Mufti

Egypt's Dar Al-Ifta

Jukumu la Kijinai la Mufti

Question

Mufti anapojibu suala kwa kulitolea Fatwa, na Fatwa yake hiyo ikasababisha madhara kwa muulizaji au kwa mtu mwingine, je, Mufti huyo atakuwa na dhamana au hapana? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi wao. Na baada ya utangulizo huo:
Cheo cha kutoa Fatwa ni cheo kikubwa, na Mufti ana nafasi kubwa ya kumwakilisha Mwenyezi Mungu na ni Mrithi wa Mitumie A.S. wao wote, na anafanya kazi ya faradhi ya kutoshelezana, na anakaimu nafasi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, katika Uma wake na hasa Wanavyuoni ni Warithi wa Mitume.
Muhamad Bin Al Munkadir amesema: "Mjuzi yuko baina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Viumbe vyake, basi anatakiwa aangalie ni vipi anaingia baina yao". Na kutokana na hatari ya cheo cha Umufti, kwa hivyo hakimfai mtu isipokuwa yule ambaye masharti yote yamekamilika ya kumuwezesha kuichukua cheo hicho, na moja kati ya masharti hayo muhimu ni Kujitahidi. Basi asili kwa yule anayekwenda kuchukua cheo cha Umufti anatakiwa afikie hadhi ya kuwa Mwenye kujitahidi bila Mipaka, mfano wake awe sawa na Kadhi.
Al Kamal Bin Al Hamam wa kihanafi amesema katika kitabu cha [Fathu Al Qadiir]: Tambua ya kwamba yaliyotajwa kwa ajili ya Kadhi ndiyo hayo hayo yaliyotajwa kwa ajili ya Mufti, ya kwamba haruhusiwi kutoa Fatwa isipokuwa Mwenye kujitahidi, na raia ya Wanavyuoni wa Misingi imetulilzana hivyo, kwamba Mufti ni Mtu Mwenye kujitahidi, na kwa yule asiyekuwa Mwenye kujitahidi katika wale wanaozihifadhi kauli za Mwenye kujitahidi, yeye sio Mufti. Na ni wajibu wake pale anapoulizwa ataje kauli ya Mwenye kujitahidi – kama vile Abu Hanifa – kwa upande wa Simulizi zake. Kwa hiyo imejulikana kwamba kile kinachoonekana katika zama zetu kama Fatwa za waliopo, sio Fatwa, bali ni nukulu za maneno ya Mufti ili ayachukue muulizaji wa Fatwa. [256/7, Ch. Dar Al Fikr]
Na ikiwa wanachuoni wameshurutisha Jitihada halisi kwa mtoaji wa Fatwa, na wakatofautiana katika kutoa Fatwa ya Mwigaji, kwa hivyo wao pamoja na hivyo, wameharamisha kutoa Fatwa bila ya elimu, na wakamkosoa vikali yule ambaye uwezo wake wa kielimu wa kumfanya awe Mufti haujakamilika, na wakalikanusha jambo hilo. Na katika vitabu viwili sahihi kutoka katika Hadithi ya Abadullahi Bin Amru kutoka kwa Mtume S.A.W.,: "Hakika Mwenyezi Mungu haichukui elimu kwa kuitoa kutoka katika vifua vya Wanachuoni, bali anaichukua elimu kwa kuwachukua wanachuoni. Mpaka ikafikia wakati pakawa hakuna mwanachuoni hata mmoja na watu wakaongozwa na wajinga, basi wakawauliza na wakatofa Fatwa bila ya elimu, wakapotea na wakawapoteza watu".
Na Imamu Ahmad na Ibn Majah wakasimulia kutoka kwa Mtume S.A.W.,: "Aliyetoa Fatwa bila elimu basi dhambi ya Fatwa hiyo ni juu ya aliyetoa Fatwa".
Na katika Hadithi ya Jabir: "Tulitoka tukiwa safarini na mtu mmoja miongoni mwetu akaumizwa na jiwe lililompiga kichwani, kisha akaota (ndoto ya kujamiiana na mke wake) na akauliza wenzake akisema: Je mnaniruhusu nitayamamu? Wakasema: Hatuoni kama wewe unaruhusiwa kutayamamu wakati una uwezo wa kutumia maji! Yule mtu akatumia maji akaoga na kisha akafariki dunia. Na tulipofika kwa Mtume S.A.W, akaambiwa habari hiyo na akasema: Wamemuua na Mwenyezi Mungu awaue, kwanini wasiulize kama walikuwa hawajui? Hakika dawa ya ujinga ni kuuliza. Hakika mambo yalivyo ilikuwa inatosha kwa mtu huyo kutayamamu na kukamua kidonda chake kwa kitambaa kisha kulifuta jeraha lake hilo kwa maji na kuosha sehemu zingine za mwili wake". Imepokelwa na Abu Dawud kutoka kwa Jabir na Ahmad na Ibn Majah kutoka kwa Ibn Abbas R.A.
Basi kauli ya Mtume S.A.W. "Wamemuua na Mwenyezi Mungu awaue", ina nasaba ya kuua kwa waliotoa Fatwa ya hana ruhusa ya kutaimamu, basi wao wanasabaishia uharibifu wa roho, Na sababu ya uharibifu ni kosa lililojitokeza katika Fatwa, na wanachuoni wameuzingatia uharibifu huo kuwa ni sababu miongoni mwa sababu za Dhamana. Na kuanzia hapo, Wanachuoni wa Fiqhi wameweka maelezo yanayozungumzia jinsi ya kumdhamini mufti pale anapokosea katika kufutu masuala na Fatwa yake ikasababisha uharibifu wa mali au nafsi, kinyume na baina ya Wanachuoni wa Fiqhi katika masharti na vigezo vya Dhamana.
Na mifano ya masuala ambayo yanafuatwa kwa kosa katika Fatwa uharibifu mali au roho, ni mufti akifutu kwa mali kwa mtu mwingine asiye stahiki mali hayo, kama vili alifutu kuwa inajuzu kwa Kafiri kumrithi ndugu yake Mwislamu, na Kafiri akachukua Mali kwa mujibu wa Fatwa hiyo, au aalitoa Fatwa ya kuuawa kwa mtu mwenye kinga kwa kudhani kwake kuwa mtu huyo alibadili Dini kwa namna ambayo haipelekei kupewa adhabu ya kifo, na masuala mengine mengi kama hayo.
Na Suala la hakikisho la Mufti kwa upande wa kupokelewa kwake katika vitabu vya Wanachuoni wa Fiqhi, limetajwa kidogo mno isipokuwa kwa kuyachunguza yaliyoandikwa ndani ya vitabu hivyo tunasema: Hakika mambo yalivyo kwa upande wa Mtazamo wa Suala linalotolewa Fatwa linagawanyika katika Masuala ya kuhitilafiana na kutohitilafiana.
Na ikiwa Mufti atatoa Fatwa ya jambo la jitihada na ambalo ndani yake linahitilafu baina ya wanazuoni, basi hali hiyo haiambatani na dhamana, na hivyo ni kutokana na kuwa "Msingi ambao ni: Hakuna kukanusha katika jambo lenye hitilafu ndani yake. Na maana ya Msingi huu ni kwamba mtu asimzuie mtu mwingine kwa kumkanusha kwa sababu tu ya kufanya kazi yake katika suala la madhehebu ya kifiqhi yanayotofautiana na madhehebu yake, au ikanasibishwa kauli yake na kinachokanushwa kwa kutumia njia tatu za kukanusha zilizotajwa katika hadithi –mkono au ulimi au moyo- kama njia ya kubadilisha, Au ni kupinga tu kazi ya kukubali rai ya Mwenye kujitahidi inayozingatiwa katika masuala hayo yenye hitilafu. Na ikiwa haisihi kwa kuwa kwake tu ni kuchukiza katika Masuala ya hitilafu, dhamana hapo kwa kweli haipo hata kama kufanya hivyo kutapelekea uharibifu wa mali au nafsi, na tulitaja suala la kukanusha katika mambo yanayohitilifiana nayo katika Fatwa lililotanguliza lilitolewa kutoka kwa ofisi ya kutoa Fatwa, basi inaweza kulirejea.
Vile vile Mufti anapotoa Fatwa ya jambo la kujitahidi katika yanayohusiana na Nafsi au Mali na rai ya mwingine mwenye kujitahidi ikawa kinyume naye, basi jitihada ya kwanza haiwezi kuangamizwa na jitihada ya pili; kwani jitihada haiondoshwi na jitihada nyingine, na ikiwa jitihada yake haijaondoshwa basi yeye hana dhamana yoyote. Ongeza katika hayo kwamba masuala ya kujitahidi yako katika mzunguko wa dhana – kama ilivyoandikwa katika vitabu vya Misingi – na Jambo la Dhana linaweza kusadifu ukweli wa kitu au likaenda kombo na kitu, sasa vipi dhamana iwepo juu ya mzunguko wa Dhana!
Ama kwa upande wa kuwa suala ambalo Mufti ameenda tofauti kwa namna ambayo haipelekei Jitihada ndani yake, kwa mfano awe ameenda kinyume na andiko na Makubaliano ya Wanachuoni, au Kiasi kilicho wazi, na hilo ni katika yanayozingatiwa kuwa ni (unyonge uliodirikiwa), Mufti anaweza akawa na uwezo wa kutoa Fatwa na anaweza akawa hana uwezo wa kutoa fatwa.
Hali ya kwanza: Mufti anaweza kutoa fatwa.
Na iwapo Mufti atakuwa na uwezo wa kutoa fatwa – naye anajulikana zaidi kuliko Mufti aliyewekwa Madarakani na Kiongozi au kwa anayekaimu nafasi yake – basi hakika tamko la Wanachuoni wa Fiqhi limetofautiana katika uwajibu wa Dhamana kama yafuatayo:
Wanazuoni wa kimaliki wanaona kuwa haina dhamana juu ya mufti mwenye kujitihadi kama alikosa katika fatwa yake na kosa hilo lilifuatwa na uharibifu wa nafsi au mali.
Na Imamu Abu Ishaaq Al Esferaniy kwamba mufti mwenye kujitihadi ana dhama kama alikosa katika Fatwa yake na kosa hilo lilifuatwa na uharibifu wa nafsi au mali, na hayo ni yaliyoafikana na maoni ya imamu As Seyutwiy wa kishafi na Ibn An Najaar wa kihanbali.
Na Ad Desoqiy qmesema katika kitabu cha: [Hashiyat Ad Desoqiy juu ya Asharh Al Kabeer: "Katika Al Hatwaab: Kwamba mtu mwenye kuharibu kitu kutokana na Fatwa yake na kosa lake katika uharibifu huo likabainika, ikiwa mtu huyo ni mwenye kujitahidi basi hapatakuwapo dhamana, na ikiwa ni katika wenye kuwaiga wengine basi atakuwa na dhamana iwapo atachukua madaraka na akatawala kile kitendo alichokifanya cha kutoa fatwa, na kama sio hivyo basi fatwa yake itakuwa ni kwa ajili ya majivuno kwa kauli na hakuna dhamana ndani yake na atapewa adhabu ya kukemewa, na kama hakuwa na maendeleo ya matumizi ya Elimu basi ataadabishwa". [20/1, Ch. Dar Al Fikr]
Na An Nawaiy amesema katika kitabu cha: [Al Majmuu']; "Na ikiwa atafanya kazi kwa fatwa zake katika kuharibu na ikajulikana makosa yake na kwamba yeye ameenda kinyume moja kwa moja, basi kutoka kwa Abu Ishaaq ni kwamba yeye ana dhamana ikiwa ana uwezo wa kutoa fatwa, na wala hana dhamana iwapo hatakuwa na uwezo wa kutoa fatwa; kwani mwenye kuuliziwa fatwa atakuwa amesembea"
Na hivyo sheikh Abu Amru akaisimulia na hakusema yo yote juu yake, na hili ni tatizo na lazima atoke na dhamana kwa kauli ya kuhadaika iliyo maarufu katika milango miwili ya Ubakaji na Ndoa na mingine mingi, au akate kwa kutokuwa na dhamana kwani katika fatwa hakuna kuwajibika wala kimbilio. [45,46/1, Ch. Dar Al Fikr]
Az Zarkashiy amesema katika ufafanuzi wake wa vilivyotengwa katika Nguzo: "Ikiwa sababu itakutana na Kuhadaika na Kilicho cha moja kwa moja kimekitangulia cha moja kwa moja, amesema: Kama Mufti atamtolea Fatwa kwa kuharibu na akaharibu, kisha likabainika kosa lake, kama Mufti atakuwa na uwezo wa kutoa Fatwa basi yeye ana dhamana, na kama hana uwezo wa kutoa Fatwa basi hana hiyo dhamana; kwa kuwa mwomba fatwa amezembea yeye mwenyewe". [Al Manthuur 134/1, Ch. Wizara ya Waqfu ya Kuwait], na mafano wake katika kitabu cha: [Al Ashbaah wa An Nathaaer kwa As Seyutwiy Uk. 162, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na Ibn An Najaar alisema katika kitabu cha: [Al Kawkab Ak Muniir]: Na ikiwa muulizaji wa Fatwa atazifanyia kazi hizo Fatwa za Mufti (katika kuharibu) nafsi au mali ya mtu (na kisha kosa lake likaja kubainika), kwa maana ya kosa la Mufti katika Fatwa yake (wazi wazi), kwa maana kwa mujibu wa kwenda kwake kinyume na dalili moja kwa moja, (basi atakuwa na dhamana) kwa maana ya kwamba Mufti atakuwa na dhamana kwa kile alichokiharibu mwombaji wa Fatwa kwa mujibu wa hali ya Fatwa atakuwa na dhamana( ikiwa hatakuwa na uwezo) wa kutoa Fatwa sahihi. Kwa kuhitilifiana na Abi Ishaaq Al Isfrayiniy na alikusanya, bali ni bora zaidi kwake kuwa na dhamana kwa Yule mwenye uwezo wa kutoa Fatwa, amesema Barmaawiy na wengine: Ikiwa ataifanyia kazi Fatwa yake katika kuharibu, halafu ikabainika ya kwamba yeye alikosea, na kama hakwenda kinyume moja kwa moja basi hatakuwa na dhamana kwa kuwa yeye ni mwenye kuhadaika, na ikiwa atakwenda kinyume moja kwa moja basi atadhaminika". [514/4, Ch. Maktabat Al Ebaikan]
Na katika kitabu cha: [Al Bahjah kwa At Taswaliy]; "Al Borziliy akasema baada ya kauli ya Ibn Roshd: Na Muusiaji amekosea kaatika mali ya mayatima kwa maana ambapo ameiuza kwa madhara yanayompata mtu, kwa yale ambayo maandiko yake ni: Anakusudia baada ya jitihada, na hana dhamana juu yake, na atalipishwa fidia Yule atakayepata chini ya mkono wake pamoja na kupitwa, kama ambavyo atakapotoa urithi kwa mayatima halafu likadhihirika deni.
Na inasahihiswa kwa yaliyopo katika kitabu cha Ibn Al Mawaz kutoka kitabu cha: [Al Wasaya] Hakika mwenye kuachiwa wasia hapa atatozwa malipo na wala hatozwi malipo yule mweny kupata kwa mkono wake; kwani yeye amemfanya mwenye kuachiwa wasia atozwe malipo kwa kukosea na hii ni tofauti na Mwenye kujitahidi anapokosea, je yeye husamehewa kwa udhuru wake au hapana?" [177/2, Ch. ya Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na Sheikh Zakariyah Al Answariy amesema katika kitabu cha: [Esniy Al Matwalib]; "(Na iwapo ataharibu kwa Fatwa yake) katika kile alichoombwa kukitolea Fatwa, kisha ikabainika ya kwamba yeye alienda kinyume kabisa na dalili waziwazi au matini ya Imamu wake amenena hivyo (hakutozwa malipo kutokana na Fatwa yake) kutoka kwa yule aliyemtolea Fatwa hiyo na (hata kama angelikuwa na uwezo) wa kutoa Fatwa kwani hakuna uwajibikaji ndani yake". [286/4, Ch. Dar Al Kitaab Al Islamiy]
Na sababu ya uhitilifiano katika suala inarejea kwa kiwango cha ulazimo wa fatwa ya mufti, basi anayeona kwamba Fatwa ya mufti ikilazimisha basi analazimishwa na dhamana, na anaye haoni basi hana dhamana. Na kwa yule ambaye haimlazimu dhamana anaona kuwa Mtafuta Fatwa ana chaguo baina ya kuikubali fatwa na kuikataa, kwani hiyo fatwa haimlazimu kuitekeleza na pia Mufti anapokosea yeye ni mwajiriwa tu. Kwa kauli ya Mtume S.A.W.: "Pindi Kiongozi anapotoa maamuzi na akajitahidi na akapatia basi ana malipo ya aina mbili, na pindi anapotoa maamuzi na akakosea basi ana malipo ya aina moja tu". Sasa inakuwaje kwa yule aliyeajiriwa na ambaye anawajibika kuwa na dhamana!
Na hakika ametoa dalili yule asiyeiona dhamana kwa Hadithi ya Amru Bin Shuaib, kutoka kwa babake, kutoka kwa babu yake, kwamba Mtume S.A.W, akasema: "Mtu yeyote atakayejifanya mganga na akawa hajulikani kama ni mganga basi yeye ndiye mdhamini". [Imetolewa na Abu Dawud]
Na mwelekeo wa dalili ni kwamba Mtu mwenye kujifanya mganga wakati hajui kitu katika fani hiyo na akawa hakuhukumiwa isipokuwa kwa dhamana; basi mjuzi hodari wa kazi yake atakuwa hana dhamana juu yake kwa mweleweko kinyume, na anaingia ndani yake Mufti kwa Kiasi.
Na anayeona kwamba anamalimishwa kwa dhamana anaweka dalili ya kuwa Mufti aliyesababisha uharibifu ambao ni sababu miongoni mwa sababu za dhamana, na hasa kwa kuwa kosa limetokea kwa kwenda kinyume na Maandiko au kinyume na Ijmaai (Makubaliano ya wengi katika wanachuoni) hazingatiwi kuwa na udhuru ndani yake, na malipo yanapatikana katika Hadithi kwani hakika mambo yalivyo imemtokea kwa tabu yake katika kujitahidi, na wala haipingani hiyo na dhamana kama ambavyo pia haifichiki.
Na ambayo tunaiona kwamba kauli kwa dhamana ya mufti katika hali hiyo ni bora zaidi kwa sababu mbili:
Ya kwanza: Kuyatohoa masuala haya kwa msingi wa Kusababisha na Kuingia Moja kwa moja, na ufupisho wa maneno ya Wanachuoni wa Misingi, ni kwamba: Hakika Msababishaji ndiye mwenye kubeba dhamana iwapo sababu itazidi Uingiaji wa moja kwa moja, na kwamba Msababishaji haweki dhamana isipokuwa kwa kushambulia iwe alikusudia au hakukusudia, kwani washahidi bandia katika kumwua mwanadamu ni wenye dhamana katika hali hiyo kwanye maoni ya wanzuoni wa kihanafi, na wanalzimishwa kwa kisasi kwenye wengineo wasio wa kihanafi. Kwa sababu wao wamesababisha kifo cha aliyeshuhudiwa, hata kama kadhi ndiye aliyehusika na kifo hicho, na katika suala la Mufti hapana shaka yoyote katika kwamba Mufti ndiye aliyesababisha kifo cha mtu au uharibifu wa mali ya mtu kwa kosa la Fatwa yake aliyoitoa na hasa ikiwa Fatwa hiyo inatoka kwa yule ambaye alipewa na Kiongozi, cheo hicho cha kutoka Fatwa (mufti ya kirasimu kwa nchi) hakika Fatwa yake baadhi ya nyakati huwa ni wajibu kutekelezwa, na kosa lake ndani yake kwa yale yanayokwenda kinyume na Andiko au Ijamai ya Wanachuoni, iwapo itakuwa ndani yake na madhara kwa kuharibu mali au kusababisha kifo cha mtu basi dhamana iliyo juu yake inatokana na kusababisha uharibifu huo, kwani hali yake ni kama hali ya mwenyekukisukuma kifu kwa mtoto mdogo asiye na upambanuzi na mtoto huyo huyo akajiua kwa kisu hicho, basi dhamana itamlazimu jamaa ya mlipaji.
Ya Pili: Kiasi cha Mufti kwa Kiongozi iwapo kiongozi huyo atazembea kuangalia katika nyaraka za maamuzi yake, kwa mfano kama akitoa maamuzi ya mtu kuchapwa viboko au kumkata kiungo, au kumuua kwa kushuhudia mashahidi, kisha mtu huyo akachapwa, au akakatwa kiungo au akauawa, na ikabainika kuwa mashahidi hawa hawana sifa za kuwa mashahidi, basi hakimu atabeba jukumu la dhamana. [Rejea: Hashiyat Ad Desoqiy 355/4, na Al Mughniy kwa Ibn Qudamah 229/10, na Hashiyat Al Qaliyubiy 210/4, ] Au akazidisha kimakosa kipimo cha adhabu kilichowekwa, basi atabeba jukumu la dhamana, na vile vile Mufti katika suala letu hili iwapo atakosea katika Fatwa yake na kosa hilo likasababisha uharibifu wa Mali au Nafsi.
Hali ya Pili: Mufti alikuwa hana uwezo wa kutoa fatwa
Ni haramu kwa yule ambaye uwezo wake wa kufutu masuala haujakamilika, hata kama atapatia, kwa hiyo kufutu kwake masuala kutageuka uzushi halisi na kuizushia dini yasiyokuwamo ndani yake, na hili jambo limeharamishwa.
Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:. {Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafuya dhaahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila yahaki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asichokiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyoyajua}. [AL AARAF 33]
Na mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Na Siku ya Kiyama utawaona walio msingizia uwongo Mwenyezi Mungu nyuso zao zimesawijika. Je! Si katikaJahannamu makaazi ya wanao takabari?} [AZ ZUMUR 60]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akaseam: {Tazama vipi wanavyo mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na haya yatosha kuwa dhambi iliyo dhaahiri.} [AN NISAA 50]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali, na hichi haramu - mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa}. [AN NAHL 166]
Na katika vitabu viwili sahihi, kutoka kwa Abdullahi Bin Amru Bin Al Aaasw R.A. wote wawili, akasema: nilisikia Mtume S.A.W. anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu haondoshi elimu kwa kuindosha kutoka kwa waja, lakini yeye huiondosha elimu kwa kuwafisha Wanachuoni, mpaka ikawa hakubaki mwanachuoni hata mmoja kisha watu wakawapa uongozi na madaraka wajinga, na hao wajinga wakaulizwa na wakafutu masuala bila ya kuwa na elimu, wakapotea na wakapotosha".
Na Abu Dawud na Ibn Majah walipokelea kutoka kwa Abi Hurairah R.A., alisema: Mtume S.A.W. akasema: "Mtu yeyote atakayefutu Masuala bila ya kuwa elimu madhambi yake yatakuwa kwa ukubwa wa wale aliyowatolea fatwa hizo".
Ibn AS Swalah –rehema ya Mwenyezi Mungu juu yake- amesema katika kitabu cha: [Adabu Al Mufti] baada ya kuhisabishia vyeo vya mufti: "Na Mtu yeyote atakayechukua cheo cha kutoa Fatwa, na akapambana nacho na akawa yeye sio miongoni mwa watu wenye sifa hizi tano, basi atakuwa amejiingiza katika jambo zito, hivi hawafikiri hao kwamba wao watafufuliwa katika Siku Nzito! Mtu yeyote anayetaka kuingia katika kazi ya kufutu masuala akidhani kuwa ana uwezo basi aituhumu nafsi yake na amche Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wake Mlezi aliyetukuka, wala asijiwekee mpaka wa kujichukulia waraka yeye mwenyewe na kuuangalia. [Uk. 101, Ch. Dar Al Uluum Wal Hekam]
Na pamoja na uharamu wa kuingia katika kazi ya kutoa fatwa kwa mtu asiye kuwa na uwezo wa kufanya hivyo, lakini Wanachuoni wa Fiqhi wamehitilafiana katika kumbebesha dhamana kwa nafsi na mali anazozifisidi kwa sababu ya makosa yatokanayo na fatwa zake. Basi Ibn As Swalah na wengineo walinukuu kutoka kwa Abi Ishaaq Al Isfrayiiniy kwamba yeye hadhamini, na hiyo ni kauli moja miongoni mwa kauli mbili za Imamu An Nawawiy.
Na anaweka dalili juu ya hayo kwa yafuatayo:
Ya Kwanza: Hadithi ya Jaber iliyotangulia, na ndani yake: "Wamemuua na Mwenyezi Mungu awaue, kwanini wasiulize kama walikuwa hawajui? Hakika dawa ya ujinga ni kuuliza. Hakika mambo yalivyo ilikuwa inatosha kwa mtu huyo kutayamamu na kukamua kidonda chake kwa kitambaa kisha kulifuta jeraha lake hilo kwa maji na kuosha sehemu zingine za mwili wake".
Na Mwelekeo wa Dalili hapa ni kwamba: Mtume S.A.W, amekuthibitisha kukosea kwao, na akawaombea dua kali sana, lakini hakuwalazimisha wao kulipa fidia au kisasi.
Mala Ali Al Qari' amesema katika kitabu cha: [Murqaatu Al Mafatiih]; "Mwenyezi Mungu awaue" yaani Mwenyezi Mungu akawalaania, bali aliyasema hayo kwa ajili ya kukemea na kutishia, na ikachukuliwa kutoka kwake kwamba hakuna fidiya au malipo ya aina yoyote juu ya Mufti, na hata kama atafutu kinyume na haki. [484/2, Ch. Dar Al Fikr]
Ya Pili: Hakika Muulizaji wa Fatwa amezembea kwa kumuuliza mtu asiye kuwa na sifa za kuulziwa na kutoa fatwa, na kwa kutochunguza kwake na kuwajua wale wenye sifa ya kutoa fatwa, kwa hivyo uharibifu uliomtokea Muulizaji wa fatwa unatokana na yeye mwenyewe kujisababishia.
Na Ibn Mufleh na Ibn An Najaar wanavyuoni wawili wa kihanbali na wengineo wameona kwamba yeye katika hali kama hii, anabeba jukumu la dhamana, na inapatikana dalili ya rai hii kwamba dhamana ya siyekuwa na sifa ni bora zaidi kuliko dhamana ya mwenye sifa; kwa sababu yeye kuingia katika mambo asiyoyaweza ni uadui na kudanganyika, inakuwa kama vile amekusudia kumuudhi muulizaji na kumsababishia madhara, na kwa hivyo yeye ndiye anayemdhamini.
Na yanayodhihirika kama alivyonukuliwa na Ad Desoqiy Kuiweka dhamana kwa asiyekuwa na sifa ya kubeba dhamana akiwa mtu huyo aliwekwa kwenye cheo hicho cha kutoa Fatwa kama {Mufti rasmi} na akajiingiza yeye mwenyewe katika yale aliyoyatolea fatwa, kama vile akatoa maamuzi ya haki ya mali kwa Zaid dhidi ya Amru, na akajiingiza yeye mwenyewe katika jukumu la kuigawa mali hiyo na kumpa huyo Zaid kisha ikabainika ya kwamba yeye alikosea katika Fatwa yake, basi wakati huo atalazimika kubeba jukumu la dhamana.
Ama kwa yule ambaye hakuwekwa katika cheo hicho, bali akamsindikiza muulizaji huku akiwa naye, kama vile mtu anaeenda kwa fundi seremala kwa ajili ya kupatiwa dawa ya kutibu ugonjwa wa mwili wake, basi huyu ana haki ya kuwa na dhamana kutoka kwa fundi seremala ikiwa ataharibu kitu katika mwili wake, kwani kupona ugonjwa wa Muulizaji sharti lake awe na uwezo wa kuuliza swali sahihi, na kama sio hivyo basi kupona kwake hakutokei isipokuwa ugonjwa huongezeka.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia inabainika kwamba mambo yalivyo, Mufti anapofutu masuala ya kujitahidi ambayo yana hitilafu za wanachuoni ndani yake, kasha Fatwa zake hizo zikapelekea uharibifu wa mali au nafsi basi hakuna dhamana hapo juu yake, ila kama suala likiwa katika yale ambayo hayana ndani hitilafu zozote za wanachuoni au jitihada, basi yeye anaweza kuwa na uwezo wa kutoa Fatwa au anaweza kuwa hana uwezo wa kutoa Fatwa. Kama atakuwa na uwezo wa kutoa Fatwa basi kilicho sahihi ni kwamba yeye ana dhamana juu yake.
Na iwapo hatakuwa na uwezo wa kutoa Fatwa basi uwazi wake ni kwamba yeye ana dhamana kama atakuwa amepewa cheo hicho rasmi kwa ajili ya kutoa Fatwa nchini na akaanza kutoa Fatwa yeye mwenyewe, na kama sio hivyo ikiwa hakupewa cheo hicho rasmi kwa ajili ya kutoa Fatwa basi hana dhamana yoyote kwake bali ni juu ya aliyetakiwa kutoa Fatwa kwa kutolichunguza swali kwa wahusika wa kutoa Fatwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.


 

Share this:

Related Fatwas