Nadhiri Halisi na Nadhiri Inayotege...

Egypt's Dar Al-Ifta

Nadhiri Halisi na Nadhiri Inayotegemea Sharti.

Question

Mimi niliweka Nadhiri ya kuchinja mnyama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama jambo langu nililolikusudia litafanikiwa, na kwa bahati nzuri, jambo hilo likatimia. Na dada yangu pia alikuwa anataka kuchinja mnyama. Je inajuzu mimi kushirikiana naye katika ng'ombe dume mdogo au lazima nichinje peke yangu tu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, maswahaba wake na watakaowafuata mpaka siku ya Malipo. Na baada ya hayo:
Watu wengi huweka Nadhiri inayofungamana na kutokea kwa kitu. Na kinachowekewa Nadhiri huwa kinaainishwa na wakati mwingine mtu huwa hakiainishi kinachowekewa Nadhiri bali hukiacha huru kitokee kama ilivyokuwa katika swahi hilo.
Na Nadhiri ni kitu anachokitanguliza mtu kwa Mola wetu Mlezi au anakiwajibishia katika nafsi yake kama vile Sadaka, Ibada nyingine, na wingi wa Nadhiri ni (Nudhuur) katika lugha ya Kiarabu. [Tazama: Al Mu'jam Al Wasiitw Uk. 912, kidahizo cha (na-dha-ra), Ch. Dar Ad Da'uwa]
Na miongoni mwa maana zake katika Fiqhi ni: kutoa kitu ambacho bado hakijaainishwa. [Tazama: Mughniy Al Muhataaj kwa Al Khatwiib As Shirbiniy 231/6, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah].
Na kuna tofauti baina ya Nadhiri isiyojulikana na Nadhiri halisi, na Nadhiri isiyojulikana ni ile ambayo mtoa Nadhiri haainishi ndani yake ibada maalumu. Ibn Qudamah alisema: "Nadhiri isiyojulikana; ni pale mtu anaposema: nina Nadhiri juu yangu, na hii inawajibisha kafara kwa kauli ya wengi wa wanazuoni. Na ilipokelewa hivyo kutoka kwa Ibn Masu'od, Ibn Abbas, Jaaber na Aisha. Na kwa kauli hiyo wakasema Al Hassan, Atwaa', Twawuus, Al Qasem, Salem, As Sha'biy, An Nakha'iy, Ikrimah, Sai'ed Bin Jubair, Malik, At Thauriy na Muhammad Bin Al Hassan na simjui aliyeenda kinyume na kauli hiyo isipokuwa Shafi; akasema: "Nadhiri yake haikamiliki; kwani kuna Nadhiri zisizokuwa na kafara ndani yake".
Na tuna yaliyopokelewa na Uqbah Bin Amer anasema: Mtume S.A.W. anasema: "Kafara ya Nadhiri isiyotajwa ni kafara ya kiapo". Imepokelewa na At Tirmidhiy na akasema Hadithi hii ni Hasana, Sahihi na Gharibu. Kwani hayo ni Maandiko, na hii ni kauli ya wale tuliowataja katika Maswahaba wa Mtume S.A.W, na Taabiina (waliokuja baada ya Maswahaba R.A, na hatumjui yoyote miongoni mwao aliyeenda kinyume na hivyo, kwa hiyo inakuwa ni Ijmaau (Wote wamepitisha hivyo). [Al Mughniy kwa Ibn Qudamah 5/10, Ch. Maktabat Al Qaherah]
Ama kwa upande wa Nadhiri halisi ni ile ambayo mweka Nadhiri amenuia ndani yake ibada lakini bila ya kuweka kiwango cha ibada hiyo, na hiyo ndiyo Nadhiri inayoulizwa hapa.
Na hukumu ya Nadhiri huru ni ile ambayo mweka Nadhiri anakalifishwa kufanya jambo linavyotakiwa na sheria mfano wa Nadhiri iliyoainishwa na mweka Nadhiri, na ikiwa aliainisha kuwa ni saumu au Swala basi anatakiwa kufanya inavyokubalika katika Ibada hizo za Swala na Kufunga.
Lakini, Je atafanya ibada ya Wajibu au inayojuzu katika Nadhiri hizo? Kuna hitilafu baina ya wanazuoni wa madhehebu moja. Na juu yake, kinachotakiwa kwa mwenye swali ni kwamba achinje katika wanyama wanaotosheleza katika kichinjo cha Wajibu au katika vichinjo vya Sunna kwa tofauti zilizotajwa.
Na kwa kuwa kilichosuniwa - ukiongezea na Wajibu - kina masharti kama vile mwaka, basi lazima itekelezwe hivyo katika Kichinjo, na ikiwa Mweka Nadhiri atashirikiana na mtu mwingine katika Kichinjo kikubwa kama vile ng'ombe itawajibika kutopungua fungu la Mweka Nadhiri na kuwa chini ya Saba, kwani saba hutosheleza. Pamoja na kutimiza masharti yaliobakia, ama kwa upande wa kumchinja ng'ombe mdogo ambaye hajafikia umri unaokubalika katika kutoa Sadaka ya nyama basi hawezi kutosheleza katika utoaji wa sadaka ya nyama hata kama atachinjwa na mtu mmoja.
Na dalili ya hayo ni kwamba Mweka Nadhiri amefuata ibada kama alivyotakiwa katika kukabiliana na masharti na kwa hivyo inamlazimu kwa kuwapo kwake; na kwa kuwa Maandiko mengi yamepokelewa kwa Amri ya kutekeleza Nadhiri, na asili ya Amri ni Wajibu.
Na asili katika Nadhiri ni Qur'ani Tukufu na Sunna na makubaliano ya wanazuoni; ama katika Qur'ani Tukufu ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wanatekeleza ahadi zao (Nadhiri)". Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na waziondoe Nadhiri zao (kwa maana ya kuzitekeleza ipasavyo)".
Ama katika Sunna tukuza basi Bi Aisha alipokea na akasema: Mtume S.A.W. amesema: "Na mwenye kuweka Nadhiri ya kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu basi na amtii Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na atakaeweka Nadhiri ya kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu basi asithubutu kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Na kutoka kwa Imraan Bin Huswain kutoka kwa Mtume S.A.W. anasema: "Karne iliyo bora kwenu ni Karne yangu kisha ya wale wanaoifuatia, kisha wanaofuatia, kisha watakuja watu watakaokuwa wanaweka Nadhiri na hawazitekelezi, wanawafanyia hiana wanaowaamini na wala hawaaminiki tena, na wanashuhudia lakini hawatoi Ushahidi, na unawadhihirikia wao unene." Zilipokelewa na Al Bukhariy, na waislamu walikusanyika kwa usahihi wa Nadhiri kwa ujumla, na ulazima wa kuitimiza. [Tazama: Al Mughniy kwa Ibn Qudamah 3/10]
Kwa kuwa kila ibada ina masharti yake basi ni lazima kuyatekeleza masharti hayo; kwani Jambo ambalo Wajibu hauwezi kukamilika isipokuwa kwalo basi nalo pia ni wajibu.
Na kama tulivyosema, kundi la wanazuoni walitaja:
Al Kassaniy akasema: "Kama mtu alinuia Saumu katika Nadhiri isiyojulikana na hakunuia idadi ya siku; basi atalazimika kufunga siku tatu katika hali ya wazi, na katika Nadhiri iliyoning'inia, iwapo sharti litapatikana, na anaponuwia chakula bila idadi; analazimika kuwalisha masikini kumi kila mmoja atampa nusu ya pishi moja ya ngano; kwani kama yeye angelikuwa hana nia basi angelazimika kutoa kafara ya kuapa, kuutokana na tuliyoitaja kwamba Nadhiri isiyojulikana ni kiapo, na kafara yake ni kama kafara ya kiapo kwa mujibu wa Maandiko.
Aliponuia kwa Nadhiri hiyo, Saumu alikuwa ameelekea kwenye Saumu ya Kafara, nayo ni kufunga siku tatu, na akaelekea katika kulisha chakula cha Kafara, nacho ni chakula cha kuwalisha masikini kumi, na kama angesema: Yeye ana nafasi ya kutoa sadaka basi atalazimika kutoa nusu ya pishi moja Na kama angelisema: Mwenyezi Mungu Mtukufu ana Saumu juu yangu basi atalazimika kufunga siku moja; na kama angelisema: Mwenyezi Mungu Mtukufu ana Swala juu yangu basi analazimika kusali rakaa mbili; kwani hicho ndicho kiwango cha chini kilichopokelewa, cha Swala iliyoamrishwa, na Nadhiri inazingatiwa kuwa ni Amri. iwapo atakuwa hakunuia kitu chochote kinachoelekea kuwa katika Kiwango cha chini kilichopokelewa kwa kuamrishwa na Sheria ya Uislamu". [Bada'i As Swana'i 92/5, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
An Nawawiy akasema: "Tawi: Je ni wajibu kulala na Nia ya kufunga Saumu ya Nadhiri au inatosha kutia nia yake kabla ya kupetuka kwa jua? Hiyo inajengeka juu ya kwamba inapofuata ibada ya Nadhiri na akaiacha huru, je Nadhiri yake anaiteremshia kitu gani?
Katika jambo hilo ni kauli mbili zikachukuliwa kutoka maana ya kauli ya Ashafi –Rehema ya Mwenyezi Mungu juu yake- La kwanza: Anateremka katika Wajibu ulio chini yake unaofanana na ule wenyewe unakuwa wajibu kwa asili ya Kisheria; kwa sababu kinachowekewa Nadhiri ni Wajibu. Na kwa hivyo kimefanywa kuwa kama wajibu katika sharia. Na la Pili: Atashuka kiasi cha chini cha kinachosihi mfano wake, na kuna uwezekano mkubwa ikasemwa: kwa uchache inajuzu Kisheri; kwani tamko la mwenye Nadhiri halihukumii Uwajibikaji wa ongezeko juu yake.
Na kauli ya pili ni sahihi zaidi kutokana na maoni ya Imamu Ghazaliy. Na kauli ya kwanza ni sahihi zaidi kwani wanazuoni wa Iraq waliisahihishia na vile vile Ruyaniy na wengineo. Na tukiisema kauli ya Kwanza, tutalazimika kuilaza nia na kama sio hivyo tutakuwa tumejuzisha kwa nia ya kunuia Mchana, na hii ni pindi anapoacha kuainisha Nadhiri ya Saumu. [Raudhat At Twalbiin kwa An Nawawiy 306/3, Ch. Al Maktab Al Islamiy]
Zarkashiy amesema: "Nadhiri isiyoainishwa, je hii Nadhiri inaifuata njia ya Wajibu Kisheria au hukumu yake ni kwamba inajuzu? Zipo kauli mbili: Rafi'iy amesema katika mlango wa Kutayamamu: Na kauli yao; Inaifuata njia ya kujuzu Kisheria, yaani katika hukumu pamoja na kuwajibika kiasili. Na walikusudia kujuzu Kisheria hapa ni vichinjo vya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ambavyo imejuzushwa kuviacha. (Mwisho wa kunukulu). Na kinachopatikana hapo ni kwamba hakuna tofauti katika kuwajibika kwa Nadhiri isipokuwa tofauti ipo katika hukumu yake kama vile kujuzu katika vichinjo vya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu au kama vile Wajibu katika Asili yake.
Nilisema: Na iliyo sahihi zaidi ni kuiweka kama Wajibu, na kwa ajili hiyo, Faradhi na Nadhiri havikusanywi pamoja kwa Tayamamu moja, na wala Swala iliyowekewa Nadhiri haiswaliwi juu ya Mnyama wala na Mtu aliyekaa huku akiwa na uwezo wa kusimama, kwa usahihi wake. Na anapoweka Nadhiri ya Swala yoyote ile bila kuiainisha, basi atalazimika kuswali rakaa mbili, na ikiwa ataweka Nadhiri ya Kichinjo cha mmoja wa wanyama basi atafuata masharti ya Kuchinja mnyama, na wala haijuzu kula kichinjo cha Nadhiri kama kiliwavyo Kichinjo cha Wajibu tangu mwanzoni bila ya kufuata utaratibu wake kama vile kuchinja kwa ajili ya Tamatui (Ukusanyaji wa Ibada ya Hija na Umra kwa Wakati mmoja), na mfano wake...na kuna baadhi ya sura zinazotengeka katika hili". [Al Manthuur fi Al Qawaid Al Fiqhiyah 271/3, Ch. Wizara ya Waqfu ya Kwait]
Ibn Qudamah akasema: "Na anaweka Nadhiri ya kufunga Saumu bila ya kutaja idadi ya siku za kufunga, atalazimika mtu kuifunga siku moja; kwani siku moja ndio kiasi cha chini cha kufunga kinachosihi Kisheria. Na mwenye kutia Nadhiri ya Swala, kuna mapokezi mawili: la kwanza ni Kwamba rakaa moja hutosheleza; kwa sababu Witri ni rakaa inayokubalika Kisheria. Na ya pili: Hakutoshelezi isipikuwa kuswali rakaa mbili; kwani rakaa moja haitoshelezi katika Faradhi. Katika Nadhiri, kitu kama kusujudu hakiwezi kutosheleza Kafara ya Swala. Na anapoweka Nadhiri ya kumwacha huru Mtumwa, basi huyo ndio anaetosheleza katika Wajibu; kwani Uwazi huchukuliwa kutokana na ilivyozoeleka Kisheria, na huo ndio Wajibu katika Kafara ya Nadhiri. Na mtu anapoweka Nadhiri ya kuchinja Mnyama, basi haitatoshelezeka isipokuwa kwa kichinjo kinachotolewa katika ibada hiyo kwa kawaida Na analazimika kuipeleka nyama kwa mafukara wa Makka, Eneo Takatifu. Kwani uwazi wa Kichinjo unapelekea hivyo. [Al Kafiy fi Fiqh Al Imam Ahmad 216/4, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Ibn Rajab Al Hambaliy amesema: "(Msingi wa Mia moja): Wajibu kwa Nadhiri: Je huambatana na Wajibu kisheria au na iliyo Suniwa? Ndani yake kuna hitilafu na yanajitokeza Masuala mengi mno" [Al Qawaid Uk. 229, Ch. Dar Al Kutub Ak Elmiyah]
As Syutwiy anasema: "(Msingi wa nne) Je? Nadhiri. Inapita njia ya Wajibu au ya Kujuzu? Kuna kauli mbili. Na uteuaji wa kauli sahihi unatofautiana katika Matawi. Miongoni mwake: Nadhiri ya Swala. Na iliyo sahihi zaidi katika hizo ni ya Kwanza; na analazimika kuswali rakaa mbili. Na miongoni mwake ni: Nadhiri za kuchinja vichinjo, na kauli Sahihi ndani yake ni. Ya kwanza: inashurutishwa ndani yake mwaka na kusalimika na kasoro yoyote. Miongoni mwake ni Nadhiri ya kuchinja Mnyama. Na akawa hakutaja jina la kitu chochote Na iliyo sahihi ndani yake: Ya kwanza: Haitoshelezi isipikuwa kwa kinachotosheleza katika kuchinja Mnyama Kisheria Na ni lazima kumfikisha katika eneo la Haram, Eneo tukufu. [Al Ashbaah wa An Nadha'er Uk. 165, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na haya yote yatatokea ikiwa mtu hataiainisha Nadhiri yake. Na mtu akiiainisha Nadhiri yake kwa chochote, kwa mfano akiwa ameainisha kichinjo au mwaka au ukubwa basi halazimiki na chochote isipokuwa alichokiainisha.
Na Ibn Qudamah akasema: "Na ikiwa ataweka Nadhiri ya Mnyama bila kuainisha Mnyama huyo, basi kiwango kidogo cha chini kinachoweza kutosheleza ni mbuzi au kondoo, au mbuzi saba walionenepa au ng'ombe; kwani kutoainisha kichinjo huchukuliwa katika Sheria asili yake, na hakitoshelezi isipokuwa kile kinachotosheleza katika vichinjo kiasili. Na zinazuilika ndani yake kasoro zinazozuilika ndani yake. Na ikiwa ataibainisha Nadhiri tangu mwanzoni, kitakuwa kimetosheleza kile kilichoanishwa mapema, kiwe kidogo au kikubwa au kingine chochote, kwa kauli ya Mtume S.A.W.: "Ni kama kwa mfano akimtoa kuku kama kafara au akatoa yai". [Al Kafiy 541/1]
Na kutokana na maelezo hayo yaliyotangulia: Hakika yako wewe unapokuwa umetoa Nadhiri iliyo huru bila ya kuainisha kitu chochote kinachowekewa Nadhiri kwa kukichinjia kichinjo, kauli iliyo sahihi zaidi hapo miongoni mwa kauli za Wanachuoni inakulazimu wewe kuchunga Masharti yaliyotajwa katika kuchinja ambako ni wajibu kama vile Mnyama wa Tamatui wakati wa Hija. Na Damu ya Wajibu kwa kukiuka vilivyoharamishwa, na kichinjo kwa kauli ya aliyekiwajibisha, na hakuna ubaya wowote kumshirikisha mtu mwingine katika kichinjo hicho kimoja kama kinaweza kutosheleza katika chinjo la wajibu na ilitegemewa kushirikiana ndani yake kama vile ng'ombe mkubwa, ama kwa ndama mdogo aliyetajwa kwenye swali, kimsingi hawezi kutosheleza katika uchinjaji wa Wajibu kwa mtu mmoja sembuse kumshirikisha mtu mwingine.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas