Benki ya Tishu.

Egypt's Dar Al-Ifta

Benki ya Tishu.

Question

Katika baadhi ya nyakati sehemu za tishu za uvimbe huondolewa kwa wagonjwa wa uvimbe, ama kwa madhumuni ya matibabu au kwa sababu za kitafiti. Je? Ni wakati gani ruhusa ya mgonjwa inahitajika kabla ya kuondolewa sehemu yake iliyoathirika? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya utangulizo huo:
Ikiwa sehemu yake iliyoathirika ina uvimbe kamili, ikiwa imeondolewa baada ya upasuaji, basi hakuna ubaya wowote wa matumizi yake kwa madhumuni ya utafiti wa kisayansi, na haitegemewi ruhusa ya mmiliki wake, kwa sababu vitu vya aina hiyo havihitaji ruhusa ya wamiliki wao. Sehemu iliyoathirika inafanana na takataka zilizomo ndani ya maduka ya vinyozi na kliniki za meno, jambo linalojulikana kama kawaida ni kama ni jambo lenye masharti ya kisheria. [Al-Ashabah wal Nadhair kwa Ibn Najim pamoja na Sharhul Hamwi 1/307, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah].
Ikiwa sampuli ilichukuliwa kutoka kwa tishu za uvimbe: ama ilichukuliwa kiasi kidogo cha kufanyia uchunguzi, au kilikuwa zaidi ya hivyo; ikiwa kitatumika kiasi kidogo cha uchunguzi ambao unasaidia kumtibu mgonjwa basi hatua hii inaruhusiwa na ni halali; kwa ajili ya kutaka kujua ukweli wa ugonjwa -kisha kuutibu- na kile kilichoamrishwa katika misingi ya sheria ni kwamba kila Jambo ambalo wajibu hautimii isipokuwa kwalo basi nalo huwa ni wajibu, na kwamba ruhusa katika kitu ni idhini katika sehemu za kitu hicho vilivyokusudiwa. [Rejea: Ihkam Al-Ahakaam kwa ibn daqiq Al-Idi 2/288, Ch. ya Matwabai' Assunnah Al- Muhammadiyah.]
Ikiwa imechukuliwa juu ya hitaji la uchambuzi, basi hali hii ina picha mbalimabali:
Ya kwanza: ni kwamba hali ile ni kwa ajili ya mgonjwa na haimsababishii madhara yoyote, kama kuchukua sampuli ya ziada za tishu kama tahadhari; kuepusha matatizo yanayotarajiwa ikiwa kuna haja ya kurudia kuchukua sampuli yake tena na kadhalika, na inapendekezwa kuuliza idhini yake na kwa hivyo, hailazimishwi.
Pili: Sababu ya kuchukua sampuli ni kuifanyia utafiti wa kisayansi bila kumdhuru mgonjwa kwa kuchukuliwa sampuli hiyo, na iwe ni kwa ruhusa yake, tunasema: Mwanadamu, ingawa hamiliki mwili wake, lakini ana uwezo wa kufanya maamuzi juu ya mwili wake huo, kwa sharti la kutokuwepo uwezekano mkubwa wa uharibifu na kufikia masilahi yanayozingatiwa, na kwa mujibu wa hayo: suala hili hakuna shida katika kuliruhusu, bali linapendeza; njia zina hukumu ya makusudio, na inathibitisha Aliposema Mwenyezi Mungu Mtukifu: {Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote} [AL MAIDAH: 32].
Al-Qadhi Al-Baydhawiy alisema katika tafsiri yake ya Aya hiyo Tukufu [2/124, Ch. ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy]: “Yaani: aliyesababishia kuendelea maisha yake kwa kusamehewa au kusitishwa kifo chake, au kuokolewa kutokana na sababu zingine za kifo, ni kama kwamba aliyefanya hivyo kwa watu wote. Imekusudiwa kuuheshimu uhai wa nafsi katika nyoyo; na ubora wa kuzilinda.
Ni lazima ikumbukwe kwamba ruhusa hapa ni ruhusa ya kweli, sio ruhusa tu ambayo wakati mwingine hutolewa kwa kufanyika udanganyifu katika vituo vingine vya matibabu au sehemu za utafiti; kwa mgonjwa kusaini kwenye karatasi ambayo hajui yaliyomo au marudio, kwa hivyo, tunapendekeza kwamba idhini iliyoandikwa ya mgonjwa iambatanishwe na idhini iliyoandikwa na daktari ambaye anakiri kwamba hali hiyo haitamdhuru mgonjwa.
Tatu: Sababu ya kuchukua sampuli ni kwa madhumuni ya utafiti wa kisayansi bila kusababisha madhara kwa mgonjwa kutokana na kuchukua sampuli hiyo, lakini bila ruhusa yake. Hali hii licha ya kuwa hairuhusiwi, sio ya busara pia; mwanadamu ingawa hamiliki tishu zake, lakini tishu hizo amejaaliwa yeye na ziko ndani ya uwezo wake, kwa maana ya uwezo wa mtu: hairuhusiwi kwa mtu mwengine kuzitumia tishu hizo isipokuwa kwa ruhusa ya mwenye tishu hizo, pindi anapokuwa nazo kiuhalisia au kisheria, na kama hatakuwa na tishu hizo basi hatakuwa na mamlaka yoyote juu yake; Al-Fayoumi amesema katika kitabu cha [Al-Misbah Al-Muniir” [uk. 71, Ch. ya Al-Maktabah Al-Elmiyah].
Kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu: hairuhusiwi kuchukua chochote kutoka kwake bila ya ruhusa ya mmiliki wake au bila ya sababu ya kisheria; na kuchukua kitu kutoka katika mwili wa mgonjwa na sehemu zake ni marufuku; na inaruhusiwa kwa ajili ya dharura tu [Rejea: Al-Ashbah wal Nadhair uk. 84, 88, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], na imepokelewa kutoka kwa Imamu Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah R.A. kwamba Mtume wa Allah S.A.W., alisema: "Muislamu ameharamishiwa kwa Muislamu mwenzake: damu yake, mali yake na heshima yake (Yaani haramu kuchukua mali ya mwenzako, kumuua na kumdhalilisha)".
Ikiwa sampuli iliyochukuliwa haimilikiwi, kana kwamba sampuli nyingi zilichukuliwa kutoka kwake kwa uangalifu, kama ilivyoyotangulia kuelezwa hapo awali, kisha akaponywa na kukataa uwezekano wa hitajio la majaribio zaidi au alikuwa amekufa, na sampuli hiyo ikawa imesalia kwa jina lake, basi inaweza kutumika kwa madhumuni ya utafiti wa kisayansi. Na haipaswi kuulizwa ruhusa ya mmiliki wake -katika kesi ya yoyote ya tiba- au familia yake -katika hali ya kifo- kwa sababu jambo hilo katika sampuli ambazo ziko kwenye uvumilivu wa kimila, kwa sababu hatima yake ni kupoteza au unyongaji.
Nne: Sababu ya kuchukua sampuli ni kuifanyia utafiti wa kisayansi, pamoja na uharibifu wa athari iliyochukuliwa kutoka kwake, hali hii ni marufuku, hata ikiwa mtu huyo aliyechukuliwa sampuli kutoka kwake ameruhusu, kwa sababu ya madhara atakayopata; imepokelewa kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Ibn Abbas, R.A. kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. amesema: "Hakuna kudhuriana wala kulipiza madhara".
Kama ikichukuliwa sampulia pasipo na idhini ya mmiliki wake, ingekuwa sababu mbili za kukataza jambo hili; Sababu ya kewanza ni: kupata uharibifu, na sababu ya pili ni: ukiukaji wa mamlaka ya mwengine.
Kutoa sababu kwamba kinayokusudiwa ni faida itokanayo na utafiti wa kisayansi, ambayo hatimaye inawanufaisha wanadamu, sababu hii haikubaliki kwani hii ni njia isiyozingatiwa ya kufikia kile kinachokusudiwa, ambapo kinachokusudiwa pengine kinaweza kutekelezwa kwake au kwa njia nyingine miongoni mwa njia halali, vile vile: madhara hayaondoshwi kwa madhara mengine.
Kinachosemwa katika tishu pia husemwa katika maji ya mwili, kama vile damu au ute wa mifupa, au uingizwaji wa seli ya mgongo au uingizwaji wa mgongo.
Ikumbukwe, hata hivyo, kwamba kuwepo kwa duka la tishu kunamaanisha kuwa dula hili ni kama shirika la kisayansi badala ya kuwa ni kama hifadhi ya kuhifadhi tishu za binadamu tu, kwa hivyo, hairuhusiwi kwa shirika lolote nje au ndani kutumia sampuli bila kufichua aina ya majaribio yaanayokusudiwa kufanywa.
Matumizi ya sampuli zilizohifadhiwa kwa faida ya shirika lolote lingine lazima yawe chini ya usimamizi wa pamoja wa pande hizo mbili, na sio kwa kuzingatia jinsi ya kunufaishana kwa faida tu, au la si hivyo, hali hii itasababisha maovu mengi, kama vile kuchukuliwa sampuli kwa ajili ya kupata fedha au kupata sampuli nyingine, ambayo ni kinyume na dhamira ya awali ya mradi huo, ambao ni kuongeza kiwango cha wafanyakazi wa kisayansi, na ushiriki halisi katika utafiti wa kisayansi unaofanikisha kusudio hili.
Na Mungu Mwenyezi Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas