Sijda ya kisomo

Egypt's Dar Al-Ifta

Sijda ya kisomo

Question

Ni nini cha kusemwa wakati wa kusoma au kusikia Aya ya sijda katika Qur’ani Tukufu katika hali ambayo mtu hawezi kuitekeleza mara moja?

Answer

Inapendeza kwa Muislamu kusema baadhi ya uradi na dua wakati haiwezekani kusujudu sijda ya kisomo.

Kusujudu sijda ya kisomo ni Sunna iliyotiliwa mkazo katika Swala, na wakati wowote; Kwa mujibu wa kauli yake Mtume (S.A.W): “Anaposoma mwanadamu (Aya) ya kusujudu kisha akasujudu, shetani atajitenga na kulia, kisha husema (kujiambia): “Ole wake” imepokelewa kutoka kwa Imamu Muslim. Ili sijda ya kisomo iwe sahihi, inatakiwa awe ametwaharika kutokana na  hadathi, utwahara mwili na nguo na mahali pa kusujudu, kuelekea kibla na kufunika sehemu za siri. Sijda ya kisomo haijuzu isipokuwa yatimizwe masharti haya. Iwapo Muislamu hatatimiza masharti ya sijda ya kisomo au haiwezekani kwake kuyatekeleza, basi inaweza kumtosheleza kusema mara nne: “Subhanallah, Walhamdulillah Walaa ilaha illallah Wallahu akbar Walaa haula Wala Quwwata illa billahi” na uradi na dua zinazofanana na ambazo ndani yake mna sifa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.”

Share this:

Related Fatwas