Sijida ya Kisomo

Egypt's Dar Al-Ifta

Sijida ya Kisomo

Question

Kipi kinasemwa wakati wa kusoma au kusikia sehemu ya kuleta sujudu ya kisomo ndani ya Qurani Tukufu katika hali ya kutokuwa na uwezo wa kutekeleza kwa haraka?

Answer

Inapendeza kwa Muislamu kuleta utajo wakati anaposhindwa kuleta sijida ya kisomo.

Sijida ya kisomo ni Sunna iliyosisitizwa ndani ya swala na nje ya swala, kwa kauli ya Mtume S.A.W:

“Mwanadamu anaposoma sehemu ya kuleta sijida na akasujudu basi sheitani hulia na anasema: Majuto yaliyoje” Imepokewa na Muslimu.

Limewekwa sharti la kufaa kuleta sijida ya kisomo, ni mtu kuwa msafi kutokana na najisi, usafi wa mwili, nguo, sehemu, kuelekea Qibla na kustiri tupu, wala haifai kuleta sijida ya kisomo isipokuwa masharti haya yatakapo kamilika, ikiwa Muislamu hajakamilisha masharti ya sijida ya kisomo au imekuwa ngumu kwake kuileta basi inamtosha kusema mara nne:

“Subhana Allah, Wal-Hamdulillah, Walaa ilaaha illa Allah, Wallahu Akbar, Wala haula walaa kuwwata illa billahil-Adhiim”, na mfano wake miongoni mwa dhikri na nyiradi ambazo ndani yake kuna wasifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Share this:

Related Fatwas