Urithi wa Kiislamu na Mitazamo yake...

Egypt's Dar Al-Ifta

Urithi wa Kiislamu na Mitazamo yake ya Hekima

Question

Ni ipi mitazamo ya hekima ya urithi wa Kiislamu ambayo inasaidia kuwa na ufahamu sahihi? 

Answer

Sifa zote njema ni za Allah pekee, na swala na salaam ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya aali zake na maswahaba zake, na juu ya wale wanaowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Malipo
Katika matini ya kiurithi ambayo tumeitaja katika maudhui ya “Urithi wa Kiislamu – tangulizi za kimifumo na jabirio la utendaji” ambazo zimezungumzia kadhia ya kuuza, na uuzaji ni aina katika aina za makubaliano, katika hilo tunaelezea mtazamo wa “Makubaliano” wa wanachuoni wa Fiqhi, mtazamo wa “Mali” na mtazamo wa “Umiliki” na mitazamo hii kwa duru yake inazalisha mitazamo mingine, kama vile nadharia ya “dhima” nadharia ya “Uhalali wa Majukumu” nadharia ya “Niyaba”. Ikiwa kama nafasi itatosha kuzungumzia mitazamo yote hiyo, isipokuwa muundo huu katika uchambuzi unaweza kutoa mfano uliobora na wakuigwa katika majaribio ya kueleza neno la urithi kwa hali yeyote ile.
Katika ufafanuzi wetu tutajikita zaidi kwenye mtazamo wa makubaliano au mkataba pamoja na kuelezea kwa uchache mitazamo hii mingine.
Mwanzo kabisa, neno “Mtazamo” ni neno ambalo limeingia kwenye matumizi ya Waislamu hivi karibuni, na hiyo ni baada ya Waislamu kuelekezea mtazamo wa Kimagharibi, kwa sababu uelewa huu umeanza huko Magharibi na kuwa ni kipimo kingine cha mwenendo wa mwanadamu cha kupinga masuala ya Ufunuo au Wahyi, ambapo kanisa limegongana na fikra mpaka fikra hii ikatoka kwenye nafasi yake kama kipimo cha tathmini, halijazingatiwa kanisa kuwa ni marejeo ambayo watu wanayo kwenye fikra zao, hapa ndio uelewa wa “Nadharia” - kama msingi wa fikra na mwenendo – ukawa na matokeo ya uzoefu wa Kimagharibi wa kutoka kwenye mamlaka ya Ufunuo.
Lakini wanachuoni Waislamu pindi walipotumia – kwa maana ya neno la nadharia – katika vitabu vyao hawakulitumia kwa maana hii inayobeba maadili ya Kimagharibi, lakini walitumia katika mfumo wa wamtumizi ya wanachuoni wa mwanzo “Kanuni za Kifiqih” lakini - kwa upande mwingine – tunakuta kuwa ufahamu wa “Nadharia” unatofautiana na ufahamu wa “Kanuni” nadharia ni yenye kutumika sana kuliko kanuni. “Kanuni ya kifiqih” kwa mfano inasema: Hakika ya mambo ni kwa makusudio yake, madhara huondolewa na uyakini hauondolewi kwa shaka….n.k, - kama nadharia ya “Mkataba” imechukua nafasi kubwa katika sharia ya Kiislamu kama vile nadharia ya kuuza kununua riba biashara ya salamu kutoa zawadi uwakala ndoa….n.k, na katika sehemu hizo imeweza kugundulika na kueleweka na kupitisha mambo jumla, mambo haya jumla ndio ambayo yameitwa “Nadharia”. Na kutokana na haya na baada ya mijadala mingi kufanyika kati ya wanasharia wa Kiislamu na watafiti wake kuhusu matumizi ya uelewa wa nadharia, imekubalika kutumika ufahamu huu kwa maana hii.
Makubaliano: Ni nini makubaliano? Mtazamo jumla unazungumzia uelewa wa makubaliano, nayo – kwa maana yake nyepesi – ni makubaliano kati ya matakwa mawili, kwa maana kuwepo utashi au matakwa na ari kwa kila upande, pindi panapofikiwa makubaliano na kukutana matakwa ya pande mbili kwenye kitu maalumu, basi makubaliano haya ndio ambayo huitwa “Makubaliano”, lakini utashi unazingatiwa ni jambo la ndani kwa maana haiwezekani kuonekana, kama vile hauko wazi ni ngumu kuupima, na kutokana na hilo haiwezekani kwa yeyote kuuona, kwani kuona hakuji isipokuwa kwenye mambo yaliyowazi yenye kudhibitika, vilevile ridhaa – ni kama utashi – ni yenye kujificha haiwezi kuonekana, na haupo wazi wakati mwingine hufanyika upande mmoja na usifanyike upande mwingine, bali hutofautiana viwango vyake wakati mmoja na mwingine, na kama hivyo hakuna hali ya udhibiti na kuonekana katika uuzaji isipokuwa maneno na muundo wenye kuelezea jambo ambalo linatokea, kwa mfano “Nimekuuzia hiki kitu”.
Na kutokana na hayo, nguzo muhimu kwenye kadhia ya makubaliano – bali ni nguzo pekee kwa mtazamo wa Abu Hanifa – ni muundo. Lakini makubaliano kwa jopo la wanachuoni yana nguzo tatu kwa ujumla, nguzo sita kwa ufafanuzi nazo:
Nguzo ya kwanza –Wakubalianao wawili: Nguzo ya pili– Muundo “kukubali na kuitikia” Nguzo ya tatu– Cha kukubaliana “pesa thamani bidhaa kitu chenye thamani”. Hizi tatu ndio nguzo za makubaliano ambazo makubaliano hayawezi kukubalika mpaka zikamilike nguzo hizi, ama kwa upande wa Abu Hanifa wanaona kuwa – hata kama watapatikana wakubalianao wawili na kupatikana kitu cha kukubaliana – basi hakuna makubaliano ya kuuziana mpaka pawepo muundo wa makubaliano “Nimekuuzia nimenunua” na jopo la Wanachuoni wanaona kuwa tofauti haivuki kuwa ni tofauti ya kineno na wala sio tofauti ya kweli.
Sura hizi zenye nguzo tatu kwa wanachuoni zinatengeneza mtazamo wa makubalino, ambao unakusanya ufahamu mbalimbali na nguzo nyingi lakini pia sharti nyingi.
Katika Fiqih ya Kiislamu huitwa neno “Makubaliano” kwa makusudio ya aina mbili, kusudio jumla na kusudio maalumu, kusudio jumla linakusanya hatua zote ni sawa sawa makubaliano yametimia kwa jina la mtu mmoja au watu wawili, wameona kuita moja kwa moja makubaliano na kuwepo makubaliano yaliyo haribika, vilevile wakaita usimamizi wa kadhi “kwa maana kiongozi anasimamia” makubaliano, na kuyagawa katika sehemu ya makubaliano huru, lakini anapokosekana kiongozi au kadhi huzingatiwa kwao ni makubaliano wanayaweka katika kitengo cha makubaliano yasio huru, na kuitwa makubaliano maalumu ambayo yapo kwenye mabadilishano kama vile makubaliano ya kuuza na kununua, hivyo vitengo vya makubaliano vimekuwa sita ambavyo ni: Makubaliano ya kujitolea mfano kama vile uwakala, makubaliano ya mabadilishano, makubaliano yanaanza kwenye kujitolea na kumalizikia kwenye mabadilishano mfano wa usimamizi na mkopo, makubaliano ya kuvunjika mfano wa talaka, makubaliano huru mfano wa wakala na mfano wa usimamizi wa kadhi, makubaliano yasio huru mfano wa kutokuwepo wakala na kadhi.
Hivi ndio huonekana uelewa mpya – hatukufahamu wakati wa kuanza kuzungumza – imekuwa ni lazima kuuweka wazi kwa sura huru ikiwa ni kama utangulizi ili iwezekane kufahamu pande zote za tamko na ufahamu wake kikamilifu, pindi tunaposema nguzo za makubaliano au mkataba kwa sura ya jumla ni tatu, hapo katika nadharia ya makubaliano tunakutana na nadharia ya mkataba kile kinachoitwa “sharti za makubaliano”. Na hapa ni lazima kutenganisha kati ya nguzo na sharti na kuelezea uhusiano uliopo kati yake, na namna yamepokelewa mambo haya katika muundo wa waandishi Waislamu wa zamani. Hilo litatuweka wazi mfumo uliopo katika mitazamo yenye hekima na mitazamo ya jumla ambayo tumeizungumzia hapo juu vilevile inatuonesha viwango mbalimbali vya uchambuzi.
Kwa kuanzia tu wanachuoni wameelezea nguzo kuwa ni sehemu ya kitu kwa ndani uwepo wake unawezesha uwepo wa kitu chenyewe, ama uwepo ni kitu kinachokuwepo akilini, ama kitu chenyewe ni kile kinachokuwa kwa nje, tumeona katika mtazamo jumla ni namna gani imetenganishwa kati ya kinachokua akilini na kinachoonekana, kisha nguzo za Swala ni sehemu ya ndani ya Swala, ambazo zenyewe zinaanza kwa Takbira, kusoma Surat Al-Fatihah, Kurukuu, Kusujudu…..na sehemu hizi zinafikiwa kwa ukamilifu wa Swala na kwa sura yake ya kiakili, ama kwenye uhalisia ikiwa mimi nitataka kuonesha Swala halisi basi nitatekeleza zile nguzo nilizojifunza.
Ama sharti, yenyewe ni kama nguzo kwani kitu hakitimii isipokuwa kwa kukamilika sharti, isipokuwa yenyewe inakuwa nje ya umbo la kitu, mfano wa sharti katika ibada ya Swala ni kama vile kutawadha, kuelekea Qibla, kusitiri tupu kuingia wakati wa Swala, vitu vyote hivi vipo nje ya Swala, na ni vitu vyingine tofauti na Swala.
Ama katika hali ya mkataba au makubaliano nguzo zake kwa upande wa Imamu Abu Hanifa ni moja tu nayo ni muundo, na kwa upande jopo la wanachuoni kuna nguzo tatu za ujumla, ama sita ni za ufafanuzi zaidi, ama sharti zake wanazigawa waandishi – kwa mujibu wa jopo la wanachuoni – sehemu tatu:
Sharti ya Kwanza: Ni akili, pindi makubaliano yanapohitaji utashi basi huu utashi unahitaji kwa mwenyewe kuwa ni mwenye akili, na kutokana na hilo ikatakiwa kueleweka akili ni nini, na kujibiwa kuhusu: akili ni nini? Na vipi viwango vya akili? Na upi uhusiano wa hii akili na matendo? Tunakuta wanachuoni wetu hawakuacha mambo yakijiendea tu, utaona wanazungumzia yote haya kwa kile walichokiita uhalali wa majukumu, na kupambanua kwa kiwango ambacho kinatengeneza mtazamo kamili.
Wamesema: Hakika uhalali huu unagawanyika sehemu mbili: Uhalali wa wajibu, na uhalali wa kutenda, ama uhalali wa wajibu unagawanyika kwenye uhalali wa wajibu pungufu na uhalali wa wajibu kamili, ama wa kwanza unakuwa kwa watoto wadogo, pindi anapozaliwa mtoto kwa kutoka tu tumboni kwa mama yake na kuwa mwanadamu mwenye harakati na kuanza kutoa sauti, kwa maana zimeanza kuonekana alama za uhai, basi anakuwa ni mwenye uhalali wa wajibu kamili, wakati ambapo hawezi – akiwa katika hali hii bado mtoto – kutekeleza mambo au kufanya jambo lolote, wanachuoni wanauliza: hivi ni mpaka wakati gani atakuwa hivyo?
Wamekuta kuwa mwanadamu katika ukweli anapitia hatua tatu: Mpaka anapotimiza miaka saba ya umri wake anakuwa mwanadamu mtoto mdogo asiyeweza kupambanua kati ya vitu, na kutoka umri wa miaka saba mpaka umri wa kubaleghe anakuwa ni mtoto mwenye kupambanua, baada ya umri huo ndio anakuwa mwenye kubaleghe na kuwa mtambuzi kamili wa mambo, kutokana hayo wanachuoni wakaelezea uhalali wa kutekeleza au –uthibiti wa ubinadamu– umegawanyika sehemu tatu kwa mujibu wa hatua za makuzi ya mwanadamu na uwezo wake wa kufahamu na kupambanua kama walivyotambua, wakatenganisha kati ya mwanadamu asiye na uhalali, mwenye uhalali pungufu na mwenye uhalali kamili, anakuwa si mwenye uhalali kuanzia pale anapozaliwa mpaka anapofikia umri wa miaka saba, na anakuwa ni mwenye uhalali pungufu kuanzia umri wa miaka sababu mpaka umri wa kubaleghe, ni mwenye uhalali kamili pale anapokuwa ni mtambuzi, katika hatua ya mwisho mwanadamu anaweza kufanya matumizi sahihi ya mali, na kujifanyia mwenyewe yale anayoyataka ikiwa ni pamoja na kufanya mikataba na makubaliano, na hii ndio ramani ya uhalali kwa wanachuoni.
Lakini ni vipi ikiwa huyu asiye na uhalali akifanya mauzo na manunuzi? Hapa wameona kuwa vitendo vyake hivyo ni batili kwa hali yeyote mfano wa vile inavyokuwa kwa mtu mwenye uhalali kamili, lakini hata hivyo wametenganisha haya matumizi ni kuwa na aina nyingi: Aina ya kwanza –kuna matumizi yenye manufaa moja kwa moja, aina ya pili– matumizi yenye madhara moja kwa moja, aina ya tatu– matumizi yanakusanya kati ya madhara na manufaa, na wakatenganisha matumizi ya mwanadamu sawa na kutokea kwake kwa mujibu wa hali yake ya uhalali wa kutenda, wakasema: Mwenye uhalali kamili anafanya atakacho, yakiwa yenye madhara moja kwa moja kama vile kujitolea, au yenye manufaa moja kwa moja mfano wa kupokea kilichotolewa sadaka au kupewa zawadi, au yenye kukusanya manufaa na madhara kama vile mabadilishano, mmoja wao anauza kitu kwa sarafu tano na huenda kesho bei yake ikapanda na kuwa sarafu kumi au ishirini na kuwa ni manufaa kwake kwa leo lakini ni madhara kwa kesho.
Lau litafanyika lolote katika hayo kwa huyu mtoto asiye na uhalali wa kufanya hayo basi inakuwa ni batili, ama lau huyu mwenye uhalali pungufu akafanya maamuzi kama haya basi anakuwa ni mwenye kusimamishwa, kwa maana ikiwa ni matumizi yenye madhara moja kwa moja inakuwa ni batili kufanya matumizi hayo, lakini yakiwa ni yenye manufaa moja kwa moja basi matumizi yake yanakuwa ni sahihi, ama ikiwa atafanya matumizi yenye kujumuisha kati ya mawili, anakuwa ni mwenye kusimamishwa mpaka pale atakapopata muongozo au kuacha kabisa, kwa mujibu wa itakavyoonekana uwepo wa manufaa kwenye matumizi haya.
Hivi ndivyo inavyokuwa uhalali, ambapo ni sharti la kwanza ambalo linapaswa kukamilika kwenye kuingia makubaliano au mkataba ili makubaliano hayo yawe sahihi, kwa sababu nguzo ya kwanza ya makubaliano ni wana makubaliano wawili, na katika sharti zake wanatakiwa kuwa ni wenye uhalali kamili, au uhalali pungufu katika manufaa tu, ya moja kwa moja.
Sharti ya Pili: Ni kuwa mwenye kuingia mkataba au makubaliano ni mwenye mamlaka juu ya kinachoingiwa mkataba au makubaliano, kwa maana kuwa ni mmiliki, au kaimu wa mmiliki, ima kwa kumuwakilisha na anakuwa ni wakala, au usimamizi wa kawaida kama kuwa ni baba au kuwa ni wasia kwake kama vile kupendekezwa na baba yake kabla hajafariki, au kupendekezwa na hakimu au kadhi pindi inapoonekana kuwa mtoto atapoteza ikiwa hatokuwa na mtu wa kumsimami kwenye mambo yake, ndio hivi wakati msimamizi na mwenye kuusiwa wote hawa wanasimama badala ya mmiliki, kwa sababu mmiliki ameshindwa kushiriki mwenyewe, ima kwa sababu ni mtoto mdogo au ni mtu asiyejitambua kwa maana mjinga au ni mgonjwa wa akili kwa maana ya mwendawazimu au yasiyokuwa hayo, lakini kwa ujumla watu hawa pamoja mmiliki ni watu wenye mamlaka ya kutumia kitu au kukifanyia makubaliano.
Hivyo mwanadamu anapokuwa si katika hawa basi huyo anakuwa si mwenye uwezo wa kuingia makubaliano ya kitu, lakini kwa upande wa Imamu Abu Hanifa amepitisha kile alichokiita “Mauzo ya asiye miliki” ni mtu ambaye hamiliki kitu wala mamlaka ya kitu isipokuwa ametumia, na wamesema uuzaji aina hii unategemea na kuidhinishwa na mmiliki, kwa mfano ikiwa mmoja miongoni mwetu anaendesha gari kwa kasi mwisho akagonda ng’ombe kwa mfano lakini hakumpata mwenye ng’ombe na akaona huyu ng’ombe atakufa hivyo akaamua kumuuza kwa mmoja wa wanabucha ili kumuhifadhi huyu mnyama lakini pia kulinda thamani yake kwa mwenye ng’ombe badala ya kufa na akishakufa maana yake hana thamani tena, basi uuzaji wake huu unakuwa ni wenye kutegemea maamuzi ya mwenye ng’ombe: Ima aruhusu atatekeleza au asiruhusu.
Ama nguzo ya pili – nayo ni sehemu ya makubaliano – miongoni mwa sharti zake ni kuwa safi chenye manufaa na kutokuwa na kizuizi, hivyo hawaruhusu kuuza vilivyo najisi, wala hajajuzisha kwa maana ya kuruhusu kuuza kitu kisicho na manufaa kisharia au hata kimazoea pia, mfano kuuza wadudu wadogo wadogo kama vile mende, hawajapitisha kuwauza kwa sababu ya kutokuwa na manufaa, vilevile vitu ambavyo havipo kwenye kawaida, hivyo wanachuoni hawajapitisha kama vile kukodi mti ili kuanikia nguo zilizofuliwa, na hilo ni kwa sababu si jambo la kawaida kufanyika hivyo wala watu hawajasikia likafanyika hilo.
Kama vile haipaswi kwenye hiki cha kukubaliana kuwa na kizuizi cha kuuzwa kwake, mfano mzuia kuuza silaha kwa kafiri wa vita, au kuzuia kuuza Msahafu kwa kafiri, na mfano wa kuuza silaha wakati wa fitina kama kuwa kwa muuzaji kukuta watu wawili wanagombana na mmoja wao akaelekea kwangu na kuniomba nimuuzie kisu, hapa haifai kwangu kumuuzia kisu kwa wakati huu, au ikawa kuzuia ni kutokana na sababu katika bidhaa kama vile madawa ya kulevya, au ikawa sababu ni kwa upande wa haki kwa muuzaji, au mwenye kitu cha makubaliano, mfano wa rehani, rehani ni kizuizi cha kutumika kitu, ambapo katika hali hii inakuwa ni haki.
Nguzo ya tatu – Ni sura ya makubaliano – yenyewe ina masharti, miongoni mwake ni pande mbili kukubaliana kikamilifu, kwa mfano ikiwa atasema muuzaji kumwambia mteja au mnunuzi “Nimekuuzia hiko kwa sarafu kumi” mnunuzi akajibu kwa kusema: “Nakinunua kwa sarafu tisa” makubaliano hapa hayajafikiwa au bado hayajatimia, hakuna kuitikia na kukubali, vilevile ni lazima yawepo makubaliano, kwa maana kukubaliana na kile anachotaka muuzaji kuuza pamoja na kukubaliana na mnunuzi anayetaka kununua, kwa upande wa Imamu Shafi ni lazima iwe cha kuuzwa au kukubaliana chenye kuonekana au kwa sifa iliyokamilika.
Jambo muhimu ni kuwa mtazamo maana yake ni kuainisha uelewa wa kitu, kisha nguzo zake, vigawanyo vyake kisha sharti zake, kwa maana ya kuzungukwa kwa sura ya jumla ikiwa inafungamana undani wake kwa sura ya jumla, lakini hasa kwa namna tunavyoshughulikia nayo ni kadhia ya Mkataba.
Hapa sura nyingine inakuwa wazi ya namna gani Waislamu wa zamani waliweza kuandika vitabu vyao kwa uhusiano mkubwa na wakina na fikra za Kimagharibi (falsafa ya Kigiriki wakati huo) hawaikatai moja kwa wala kuikubali moja kwa moja bali wameidurusu falsafa hiyo kisha wakaikubali kile kinachokubaliana na Qur`ani na Sunna na kuvikataa vinavyopingana na miongozo ya Kitabu na Sunna.
Arosto pindi alipozungumza kuhusu sababu (mfano wa meza ni nini sababu ya uwepo wake?) akasema sababu yake ni nne: Sababu kamili nayo ni ambayo inakamilisha sababu nne, na kukamilisha uwepo wa kitu. Sababu ya kwanza ni sababu ya kimatirio, nayo katika meza ni mbao. Sababu ya pili ambayo imeitwa ni sababu ya sura ambayo katika meza ni sura yake, kwa sababu ubao unawezekana kutengeneza kiti au meza au visivyokuwa hivyo, lakini kilichotokea ni kuwa sisi tumeipa sura ya meza. Ama Sababu ya tatu ambayo imeitwa “sababu ya ufanisi” nayo ni inayotengeneza kitu, kwa maana seramala ambaye ametengeneza meza hii ni kwa sababu bila ya kuwepo kwake huyu fundi haikuwa inawezekana kuwepo meza hii, kisha akaongeza Sababu ya nne na kuiita “Sababu isiyokuwepo” nayo ndio lengo la kutengenezwa meza hii, lau kusingekuwepo matirio sura ufanisi na lengo basi kitu hiki kisingekuwepo.
Pindi tunapozingatia sababu hizi nne tutakuta kuwa sababu mbili katika hizo zinaingia ndani ya kitu na sababu mbili zingine zipo nje ya kitu (sababu ya kimatirio sababu ya sura zimeingia kwenye kitu chenyewe, ubao ni katika vinavyotengeneza meza vile vile sura ya meza)… kwa hivyo mazingatio ya wanachuoni yalikuwa kwenye kile kilichokuwa ndani ya kitu na wakaita “Nguzo” na kile kilichokuwa nje ya kitu wakaita “Sharti”. Basi mwenye kuangalia sura ya jumla atakuta kuwa imejengwa kwa nguzo hizo na kupitia nguzo hizo imezaliwa vitu vinavyofungamana na mfano huu, kisha pindi tunapoingia kwenye urithi tunafahamu ibara ambazo zimeundiwa vitabu vyake kwa ufahamu mwepesi na wakina, na hilo pindi tunapounganisha kati ya mitazamo ya hekima na sura za ujumla.
Mtazamo huu ambao unawezekana kuuita nadharia ya mkataba, ambayo maana yake ni sehemu katika sehemu zake leo hii nayo ni mauzo, ikikamilisha nadharia ya fedha, kwa sababu moja ya nguzo ya nadharia ya kuuza ni “kitu cha kuuzwa” na kwa sababu kitu cha kuuzwa kinatengeneza thamani na kuwa na kuthaminishwa, ikiwa thamani kwa mtazama wa jopo la wanachuoni ni lazima iwe imekemilika ndani yake sharti mbili ambazo ni uhalali na kunufaisha, kila kilicho haramu kisharia sio thamani au sio mali, vile vile kisicho nufaisha.
Nao katika hilo wanatenganisha kati ya kitu na manufaa ya kitu na hukumu ya kitu katika uhalali na kutokuwa halali, ambapo vinapatikana vitu ambavyo wanaviita wazungumzaji kitu chenyewe, na kunapatikana manufaa na kupatikana hukumu ya kisharia ya kitu hiki, kwa mfano gari manufaa yake ni kuipanda, hivyo kitu kinakuwa ni gari na kupande ndio manufaa yake, kuimiliki na manufaa yake vyote hivyo ni halali.
Imamu Abu Hanifa wameweka masharti mawili katika kitu mpaka kiweze kuitwa mali au thamani: Sharti la kwanza – kiwe ni katika jinsi ya kitu, sharti ya pili – kubadilika bilai ya kuweka sharti la uhalali ni sawa sawa kimekuwa halali au sio halali, wakatengeneza mtazamo au nadharia nyingine ya kadhia ya thamani au mali ambayo ni manufaa, ama kwa upande wa jopo la wanachuoni wanazingatia mali au thamani ni kile chenye thamani kinalipiwa au kutumika, wakaweka sharti la kuwa halali, kwa maana jopo la wanachuoni wameweka sharti la uhalali na kubadilika kwa maana ya kuwa na manufaa bila ya kuweka sharti ya kitu.
Hivi ndio tunakuta wamegawa “Mali” kwa viwango mbalimbali, wakagawa baadhi kwenye: Mali ya majengo au yenye kuhamishika na inayofanana na hivyo au yenye thamani, na mali inayokubali kufanyiwa thamani au isiyokubali hivyo, wakachora ramani ya mali ni lazima kufahamika ili tufahamu ibara zao kwa kina zaidi, ramani hii ndio ambayo inawezekana kuitwa “Nadharia ya mali”.
Wameanza kugawa mali kati ya mfano na kuthaminika, wakasema wanachuoni pindi tunapozingatia mali tunakuta kuwa baadhi yake ni ya mfano yenye kufanana yenyewe kwa yenyewe, kama vile hali ya uzalishaji bidhaa iliyo rehani, ambayo imekuwa ni mfano, kiwanda kizalisha bidhaa fulani kwa yenye alama ya biashara na nambari maalumu ambapo mteja anaweza kuipata kwa rejareja kwenye bidhaa hiyo hiyo ambayo ameipata mteja mwingine sokoni, bidhaa hii inaitwa thamani ya mfano, thamani ya mfano ni ile yenye kuwa na mfano wake. Ama mali ya kuthaminika ni mali isiyo na mfano wake, kwa mfano siwezi kupata sokoni bidhaa kisha ikatengenezwa kwa mtumiaji kwa maana ya mteja sawa na kuwa na sifa ambazo ameziainisha mteja, na sababu hii hurejewa kufanyiwa tathmini ya thamani ya mfano kwa kuuoanishwa, ama mali ya kuthaminika marejeo katika kutathmini yanarejea kwenye thamani yake.
Wameona kuwa thamani ya mfano inawezekana kufanyiwa mchakato wa kukopwa, ama ya kuthaminika haiwezekani kufanyiwa hivyo, na hiyo ni kwa sababu thamani ya mfano inathibiti katika dhima ya deni, ambapo inawezekana kwa mkopaji kulipa mfano wake bila ya kudhurika chochote mwenye bidhaa, pindi anapokopa mtu mmoja kwa mwenzake chombo cha kurekodia kama vile kaseti kwa alama ya biashara maalumu na kuwa na sifa maalumu, basi mkopaji anaweza – katika hali ya kuharibika – chombo hiki kwenda sokoni na kununua chombo cha kurekodia chenye alama ya biashara na sifa na kumfidia mwenye chombo chake kilicho haribika, lakini chenye kukubali thamani hakifai kuazimwa au kukirudisha tena kwa thamani yake hiyo hiyo, na wala sio yeye anaeweka thamani yake kwenye jukumu hilo, kwa sababu hiyo pindi mkopaji anapoharibu mali yenye thamani inakuwa kwake ni kuweka dhamana, kwa maana kulipa thamani yake ambayo imewekwa na mwenye kitu chake katika dhamana.
Ama kwa upande wa mgawanyo “Mali isiyo hamishika/ mali yenye kuhamishika”, tunakuta wanachuoni wametofautiana kuhusu mali isiyohamishika na mali inayohamishika. Imamu Abu Hanifa amesema: Mali isiyohamishika ni mali isiyohama kabisa, na kwa sura hii mali isiyohamishika itakuwa ni ardhi, ambapo haina uwezekano wa kuhama kabisa, ama jengo kwa mtazamo wao ni kuwa inawezekana kuhamishwa kwa kubomolewa au kuvunjwa na kurudiwa kujengwa tena sehemu nyingine, kisha nyumba za chini na zile za ghorofa – kwao wao – ni katika mali zisizo hamishika, kwa sababu haiwezekani kuihamisha – katika hali ya kawaida – kama ilivyo.
Kwa upande wa mali “Inayo thaminika / isiyo thaminika” unaonekana kwenye mtazamo wa Abu Hanifa ambao wamesema kuwa, mali ni kitu tu ni sawa sawa kimekuwa halali au haramu, hivyo basi pombe kwa watu wa Kitabu ni mali, lakini mali isiyo kubalika thamani, kwa sababu hiyo wamelazimika kugawa mali kwenye mali yenye kuthaminika kwa maana yenye thamani nayo ni halali kisharia, na ile isiyo thaminika kwa maana isiyo na thamani nayo ambayo si halali. Ama jopo la wanachuoni – wao hawajizingatia – kisharia isiyokuwa halali kuwa ni mali – hivyo wao hawakulazimika kugawa huku, kisha kunatofauti maana ya mali inayo thaminika na ile isiyo thaminika kwa jopo la wanachuoni tofauti na Imamu Abu Hanifa.
Mali ya kuthaminika kwa upande wa jopo la wanachuoni ni mali yenye thamani kwa watu mfano wa bidhaa, na ile isiyothaminika ni mali isiyo na thamani kwa watu mfano wa punje ya ngano mbichi ambayo imedondoka kwenye shuke la ngano, haina thamani kwa mchukuaji, mgawanyo huu unaelimisha uelewa wa jopo la wanachuoni – sio watu wa Abu Hanifa – kadhia ya dhamana, lau mimi nitaingia kwenye nyumba ya asiyekuwa Muislamu na kukuta chupa ya pombe kisha nikaichukua na kuitupa nje kupitia dirishani au nikaimwaga pombe yenyewe basi hiyo pombe haitozingatiwa kuwa ni mali kwa sababu yenyewe ni haramu, kisha hakutakuwa na fidia kwa upande wangu kwa mwenye ile pombe, isipokuwa ni vitu ambavyo inafaa kukorofishana kwa ajili ya hivyo.
Katika maelezo ya haraka kuhusu nadhari ya mmiliki, inawezekana kusema kuwa mmiliki au umiliki kwa wanachuoni wa sharia wamegawa sehemu tatu, ambayo ni: Miliki ya wote, miliki ya nchi na miliki ya mtu binafsi, na umiliki ni uhusiano kati ya mwanadamu na kitu, pamoja na kuwa maelezo haya yanazingatiwa ni matamshi ya kisasa hayajapatikana katika fiqih lakini yapo karibu sana na kile kinacho maanishwa na wanachuoni wa Fiqih. Umiliki binafsi ni umiliki wa mtu kitu, ama umiliki wa wote ni umiliki wa kitu kinachomilikiwa na Waislamu wote au wananchi wote, wote wanakimiliki kwa ujumla wao, katika umiliki wa wote haiwezekani kumzuia yeyote kunufaika nacho kitu hiko, kwa mfano inafaa kwa wote kuvua samaki baharini mtoni au ziwani, inafaa kwa watu wote kukata miti misituni….n.k. na kuna miliki ya dola au nchi, kwa maana kama dola – ikiwa kama taasisi iliyopo – inamiliki vitu hivi, kisha inafaa kwa nchi au dola kuuza au kununua, mfano kama vile vituo vya kuzalishia umeme au vituo vya radio na mfano wa hivyo.
Lengo linalokusudiwa kuweka wazi haya ni kusisitiza kuwa kufahamu nadharia za hekima na kuzieleza kwa kina na kuzivumbua inazingatiwa ni sharti muhimu sana ya kile tunachojifunza, nacho ni urithi, ni sawa sawa kuufahamu urithi wenyewe au kufahamu mahusiano yake na mitazamo ya jumla.
Tunarejea kwenye tamko ambalo tunalo na kuzingatia yaliyomo, na tunajaribu kufahamu ni namna gani unadhibiti nadharia hizi katika kuzifahamu kwa kina zaidi, anasema mtunzi:
Kitabu cha mambo ya mauzo, mwisho wake ni ibada, kwa sababu ni katika matendo yaliyo bora kabisa, na pia kulazimika kwenye hilo ni zaidi na kuwa na wafanyaji wachache, tamko lake kwa asili ni chanzo, kwa sababu hiyo limekuja kwa muundo wa umoja, pamoja na kuwa chini yake kuna aina nyingi, kisha likawa jina lenye ndani yake mabadilishano kama maelezo yake yatakavyo kuja: kisha ikiwa itatakiwa upande mmoja wa makubaliano ambao anaitwa kwa anayekuja kutoka upande huo kuwa ni muuzaji, itafahamika kuwa ni umiliki wa mabadilishano kwa sura maalumu, ikikabiliana na ununuzi ambao ni upande mwingine ambao anaitwa yule anayetokea huko ni mnunuzi, na kufahamika kuwa ni umiliki wa mabadilishano pia, inafaa kuita jina la muuzaji kuwa mnunuzi na kinyume chake, na maana ya kumiliki na kumilikishwa kwa kuangalia upande wa maana ya kisharia kama maelezo yatakavyo kuja:
“Ikiwa itakusudiwa pande mbili kwa pamoja ambazo kupitisha mabadilishano na kuvunjika kunarejeshwa kwao….”
Wanachuoni wameangalia nguzo za makubaliano ziwepo kati ya hawa wawili wanao kubaliana, na maakubali haya yawe kwa utashi kamili wakati wa kukamilishwa kwake.
Hapa inapaswa kwetu – tukiwa tunazungumzia nadharia ya mkataba – kuzungumzia hatua za makubaliano, kwani mkataba au makubaliano yana hatua Nne: Hatua ya kufanyika, Hatua ya kufaa, Hatua ya utekelezaji na Hatua ya lazima.
Ama hatua ya kufanyika: Kwa upande wa madhehebu ya Abu Hanifa yanaweza kufanyika makubaliano hali ya kuwa yameharibika, na yanaweza kufanyika makubaliano hali yakiwa sahihi, ikiwa kitu cha makubaliano si cha kisharia kwa asili yake au kwa sifa yake basi makubaliano yanakuwa ni batili, ama kikiwa cha kisharia kwa mmoja kwa asili tu hiko kitu au kwa sifa zake tu basi makubaliano yanakuwa yameharibika, ikiwa ni kitu cha kisharia kwa asili yake na sifa zake basi hiko kinakuwa ni sahihi, kwa sababu hiyo kufanyika makubaliano chini ya hali hizo yanafaa na yana haribika, na huenda yakafanyika makubaliano yakiwa hayafai au yameharibika, hivyo kupitishwa makubaliano au mikataba ni hatua inayotanguliwa na hatua ya hukumu yake ya kuwa ni sahihi au batili, vilevile wanachuoni wamechukuwa kwa njia nyingine lakini sio sehemu ya kuisherehesha.
Kwa mfano ukweli wa riba, ni sehemu ya mauzo, na hili ndilo washirikina wanavyosema: Hakika mauzo ni kama riba. Hapa wao wanasema kwa ukweli wao, lakini ni ipi tofauti kati ya kuuza bidhaa na kuuza sarafu mia kwa sarafu mia na kumi? Jibu ni kuwa pindi kilichokuwa kwenye makubaliano ni pesa au sarafu, nayo ndio kitu cha mbadilishano kwa watu, sharia imeharamisha katikati ya mabadilishano haya kuwepo ongezeko wakati wa kuchukua na kutoa, makubaliano haya yanakuwa ni haramu kwa sifa iliyothibiti na wala sio kwa kukosekana kwa nguzo zake na masharti yake, hivyo inakuwa imeharibika na batili, lakini kwa upande wa Imamu Abu Hanifa – kutokana na mitazamo yao iliyopita – inakuwa imeharibika hata kama sio batili.
Kwa sababu hiyo; wanamfanya mtu anamiliki kiwango hiki cha ongezeko nayo ndio riba, ikiwa atatoa au kumuuzia mtu mwingine kisha akaitumia basi hatotakiwa kurejesha pesa hii ya ongezeko. Ama upande wa Jamhuri ya wanachuoni wanaona kuwa ni makubaliano kwa muda, na huu muda ndio unaopelekea kuchukuwa kiwango cha riba – ziada – ni mwenye kutakiwa kurejesha kiwango hiki cha fedha cha ziada, kana kwamba kiwango cha ziada cha riba – ambacho kimechukuliwa kwa ubaya – hakimilikiwa na mtu yeyote na kuwa katika jukumu lake.
Kwa upande wa watu wa Abu Hanifa wanasema uharamu unaokuwa kwao ni kwa watu waliofanya muamala wa kwanza, ama ikiwa wale waliofanya muamala wa kwanza wakatoa na kumpa mtu mwingine hapo uharamu unaondoka, ama kwa upande wa Jamhuri ya wanachuoni ni kuwa ongezeko hili lenyewe ni haramu na litaendelea kuwa haramu na haliwezi kuingia kwenye miliki ya mtu yeyote, bali ni haramu kwa yeyote yule anayebeba jukumu hili.
Duru ya kufanyika makubaliano yaliyo sahihi na yaliyo haribika, ikiwa patakosekana chenye kuharibu basi makubaliano yanakuwa ni sahihi, na usahihi huu una nafsi mbili au duru muhimu mbili: Kutekelezwa na kusimamishwa. Huenda makubaliano yakawa sahihi lakini yakawa yamesimamishwa mpaka yapitishwe na kiongozi au mmiliki, yanakuwa ni yenye kusimamishwa mpaka yapitishwe na mwenye mamlaka kamili ya kinachofanyiwa makubaliano, mfano wa uhalali wa kufanya matumizi mtoto mdogo ambaye si mtuambuzi.
Ama mtekelezaji chini yake kuna aina mbili: Lazima na isiyo lazima, na yana ainishwa haya kutokana na hiyari: Sharti la hiyari, mtazamo wa hiyari na hiyari yenye kasoro, kama muuzaji kumwambia mteja au mnunuzi nimekuuzia hiki kitu kwa sharti la kunipa fursa siku tatu, hapa makubaliano ni sahihi na yenye kutekelezwa isipokuwa hakuna ulazima mpaka kupita siku tatu, baada ya siku hizo tatu yanabadilika na kuwa ni lazima, hivi ndivyo inakuwa lazima kwa sharti la kutokea jambo au hiyari fulani. Ama hiyari ya aibu ni kama mmoja wao anunue kitabu kutoka kwa mwenye duka la vitabu na kumwambia: Kama nitapata kitabu kingine sehemu nyingine basi hiki nitakirudisha, hapa mauzo au makubaliano yanakuwa yamefanyika na ni sahihi, lakini hakuna ulazima isipokuwa ni baada ya kupita muda wa kuchunguza kosoro, hapo ndio kunakuwepo na ulazima kwake, hapa anasema mtunzi wa urithi kuwa:
“Ikiwa itatakiwa kwa pande mbili kwa pamoja ambazo kupitisha mabadilishano na kuvunjika kunarejeshwa kwao”
Uhusiano huu baada ya kufanyika makubaliano yanaweza kuvunjwa kwa sababu ni makubaliano yaliyoharibika, na inawezekana kupitishwa na kuhama kutoka nafasi ya kufaa na kwenda kwenye nafasi ya utekelezaji, mfano wa tuliyosema kuwa makubaliano haya ni yenye kusimamishwa, kisha atakuja mwenye mamlaka na kupitisha au kutopitisha.
Hivyo neno kufaa na kuvunjwa hufahamika kwa uelewa wa kina pindi tukifahamu hatua nne za mkataba ambazo ni: Kufanyika makubaliano, Kufaa makubaliano, Kutekeleza makubaliano na Kulazimika kwenye makubaliano.
“Husemwa kwa upande wa kilugha: Kukutana kitu kwa kitu kwa sura ya mabadilishano, huingia ndani yake yasiyofaa kumilikiwa”.
Hapa hutokea nadhari nyingine nayo ni nadhari ya mkono nayo ni moja ya vinavyotengeneza nadhari ya umiliki, na ufupi wake ni kuwa mpaka vitu viwe ni miliki yangu ni lazima viwe halali visafi vyenye manufaa, lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kuwa ni maalumu kwa mwanadamu lakini havija kamilika masharti haya mfano uchafu wa mnyama, ni najisi kwani uchafu kwa mtazamo wa Imamu Shaafi hivyo hauingii katika umiliki, kisha haifai kuuza wala kununua, lakini mnyama huyu huenda akawa ni mnyama maalumu kwa mwanadamu na kumilikiwa, na uchafu wake unachukuliwa kwa manufaa, ambapo hutumika uchafu huo au kinyesi hiko cha mnyama kama mbolea shambani, na hutumika kama nishati, uchafu huu umekuwa na manufaa na thamani, na watu wapo tayari kugharamia kwa maana ya kufanya malipo kwa pesa, hivyo tunafanyaje? Ikiwa huu uchafu au hiki kinyesi sio miliki yangu ni namna gani naweza kukitumia? Na ni uhusiano upi unaokuwepo kati yangu na yeye mpaka matumizi haya yafanyike?
Hapa wamesema wanachuoni: Uhusiano uliopo ni “Umaalumu” wakasema kinyesi hiki ni maalumu kwa mwenyewe, hivyo imekuja kuwa mkono kwenye kitu huenda ukawa ni mkono wa umiliki lakini pia unaweza kuwa ni mkono maalumu, ikiwa ni kwa upande wa umiliki kwa maana ya kukamiliki masharti ya umiliki hapa mkono unakuwa ni mkono wa umiliki, ama ikiwa si katika umiliki mkono unakuwa ni mkono maalumu na wala sio mkono wa umiliki, na wakati mwingine kitu kinakuwa si umiliki wa maalumu, hapa ndipo hutokea nadharia ya mkono usiofungamana kokote, na kwa hali hiyo mkono umegawanyika: Mkono miliki, mkono maalumu, mkono usio wa upande wowote.
Kisha umegawanywa mkono kwa mgawanyo mwingine nao ni mkono wa dhamana na mkono wa uaminifu, ama mkono wa dhamana unakuwa kwa mfano mmoja wao akiazima kitabu kwa mwenzake ili asome, kitabu – hapa – ni cha mtu wa kwanza lakini hakipo mikononi mwake, na wala sio miliki yake, lakini kipo chini ya mamlaka yake, ikiwa kitapotea au kuharibika basi aliyeazima anakuwa ni mdhamini kwa maana atamlipa mwenye kitabu thamani ya kitabu, kwa maana anakuwa dhamana wakati kikiharibika. Ama uaminifu ni kana kwamba mtu kuweka kitabu kwa mwenzake kama amana, anakilinda na kukihifadhi bila ya mapungufu isipokuwa pindi kikiibiwa kuungua moto, hapa sio yule aliyepewa kitabu kukitunza anapaswa kumlipa kama fidia mwenye kitabu, kwa sababu mkono wake kwenye ile amana au kitu kilichowekwa ni mkono wa uaminifu na wala sio upande wa dhamana. Uchafu huu pindi mtu anapotaka kunufaika nao na kuupata kwa kulipia thamani, wanachuoni wanasema kuwa muamala huu haufanyiki kwa upande wa kuuziana, lakini unafanyika kwa upande wa kuondoa mkono na ule umaalumu, mfano mfanyakazi aliyekuwepo hapo mwanzo anaweza kumuachia kazi mwenzake asiye na kazi kwa kumuuzia, yeye hapa anakuwa hamiliki kazi hii, na pana makubaliano haya yanawekwa kwenye sura ya kuondoa mkono kwenye umaalumu, wanasema: “Kisichofaa kumilikiwa kama kitu maalumu na kisichokuwa na sura kama kupewa na kutolewa kwa sura ya mabadilishano mfano wa kama vile kutoa salamu, kujibu adhana kumuombea dua mwenye kupiga chafya na kadhalika.
Kwa upande wa sharia: Makubaliano ya mabadilishano ya thamani yanaonesha umiliki wa kitu au manufaa ya moja kwa moja na wala sio kwa sura ya kujenga ukaribu.
Hapa wamesema kuwa miongoni mwa masharti ya makubaliano ni kutoshurutishwa wala kuwa na muda maalumu, ama yaliyofungwa ni kama kusema muuzaji kumwambia mnunuzi, nitakuuzia hiki kitu pindi ndugu yangu aliyesafiri atakaporejea, makubaliano haya sio sahihi. Ama muda maalumu ni kama vile Mnunuzi anaposema: Nimenunua kwa muda wa mwezi moja, kwani makubaliano ya kuuziana lazima yawe ni ya kudumu na wala sio kwa muda. Wala haikuwa kutotaja sharti hili katika nadharia ya makubaliano isipokuwa ni kwa sababu masharti mengine yanakuwapo katika baadhi ya mikataba tu, mfano: Makubaliaano ya uwakala yanafaa ambapo miongoni mwa masharti yake ni kuwa kwa muda tu, hilo ni sharti la makubaliano maalumu.
Anasema: “Nguzo zake ni tatu: Mwenye kufanya makubaliano, kinachoingiwa makubaliano, muundo wa makubaliano, lakini kwa ukweli kuna nguzo sita kama zitakavyoelezwa. Makubaliano – katika ueleweka wake – ni aina ya jumla ya makubaliano. Hivyo wamesema: Kinyume cha mkataba ni kutoa, kinyume na mabadilishano ni kutoa bure, na kwa mali mfano wa ndoa, kunufaika mmiliki wa kitu ni kukodisha, kinyume na ukaribu ni mkopo. Na kusudio la manufaa ya kuuza mfano wa haki ya kupita, na kuweka kigezo cha hali ya kudumu ndani yake ni kutolewa kukodisha pia, kutolewa kitu kimoja kwa vigezo viwili ni kutokuwa na kasoro.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Chanzo Kitabu: Njia ya kuelekea katika Kuufahamu urithi, cha Fadhilatu Mufti wa Misri. Dr. Ally Juma.


 

Share this:

Related Fatwas