Hukumu ya kuchukua Malipo Mbadala y...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kuchukua Malipo Mbadala ya Kujivua Upangaji.

Question

Ni ipi hukumu ya kisheria kwa mpangaji wa jengo la makazi kuchukua kiasi kikubwa cha fedha kama mbadala wa kujivua upangaji wake wa Makazi hayo na kuachia haki zake kwa kuyakabidhi masilahi yake ya muda wa mwisho wa upangaji kwa kumpa Mtu mwingine au mwenye nyumba, hali ya kuwa anajua kujivua kwa mpangaji huyo? 

Answer

Sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola Mlezi wa viumbe vyote. Na Rehema na Amani zimwendee Bwana Wetu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, yeye na Jamaa zake na Maswahaba wake na kila atakayewafuata. Na baada ya Utangulizi huu:
Maana ya Kujivua inayokusudiwa hapa ni kuacha au kutoka katika nyumba ya kupanga. Na katika Maana ya Istilahi ni mpangaji kuiacha haki ya kunufaika na jengo alilopanga, kwa kupewa Malipo ya fedha kama Mbadala wa kuliacha kwake jengo. Na Dkt. Wahba Zuhailiy ameelezea kitendo hicho cha kujivua kwa kuchukua mbadala wa fedha inayotolewa na Mtu kama malipo ya kuachiwa manufaa ya nyumba au ardhi au duka kubwa au dogo, kuachiwa haki yake ya kujinufaisha kwavyo. [Jarida la Baraza la Fiqhi ya Kiislamu, toleo la Nne, Maudhui ya kujivua manufaa kwa kulipwa fedha, [Dkt. Wahbah Zuhailiy]
Na sura iliyoenea ya Kujivua ni kufikia makubaliano baina ya mmiliki wa nyumba na mkodishaji wa Kwanza na mkodishaji wa pili, kwamba mkodishaji wa Kwanza amwachie haki ya kuitumia nyumba hiyo, mkodishaji wa pili, kwa kulipwa, Mpaka mwisho wa muda wa pango la nyumba hiyo, ili mkodishaji wa pili autumie muda huo uliobaki badala ya yule wa kwanza. Na huko kuachia haki kutasajiliwa kwa mkataba wa kwanza ambao una nakala ya Mkodishaji, au akaambatana nao, na hili litafanyika kwa ridhaa ya mwenye nyumba iwapo atashuritisha katika mkataba wa kwanza kwamba mpangaji asiwe na haki ya kuachia haki yake ya kunufaika na nyumba husika kwa Mtu mwingine isipokuwa kwa yeye kukubali hivyo. Na masharti ya aina hiyo yanazingatiwa kisheria.
Na mpangaji anamiliki manufaa ya alichopanga na anaweza kukitumia yeye au kumpa mtu mwingine akutumie, jambo ambalo linamaanisha kwamba kiasili inajuzu kukodisha kiundani kwa mujibu wa sheria, kinyume na yaliyomo katika kanuni hivi sasa ambapo uhalali huu unaweza kuwekewa masharti kwa masilahi maalumu. Amesema Al Bahuutiy katika kitabu cha: [Sharhu Muntahaal Iraadaat: 2/259, Ch. ya Aalamu Al Kutub]: Na "Mpangaji mwenye haki ya kutumia kikamilifu alichokipanga" ambaye ni Mwenye Mkataba mfano wa hayo pia madhara (kama watashurutisha wawili hawa) kwa maana ya Watu hawa wawili kwamba mkodishwaji wa manufaa anufaike kikamilifu yeye mwenyewe; kwa kubadilika kwa sharti kutokana na kukana kwake mazingira ya Mkataba nayo ni umiliki wa manufaa na kujiwekea uwezo yeye mwenyewe au anayemwakilisha”. Mwisho.
Na katika Kitabu cha; [Kashaaful Qinaai: 5/69, Ch. ya, Ad Dar Al Elmiiyah]: “Tofauti na manufaa ya Kitu kilichokodishwa, hicho ni cha Mkodishwaji na ana haki ya kukitumia na akampa malipo mbadala ya Kitu hicho”. Mwisho.
Mkodishawaji Ana haki ya kuhamisha umiliki wa Manufaa na kumpa Mtu mwingine, iwe kwa kulipwa au bila ya kulipwa; kwani Msingi katika hili ni kwamba Mtu yoyote atakayeyamiliki Manufaa basi ana haki ya kulipwa malipo badala na kuyachukua malipo atakayokuwa. [Kitabu cha Minahul Jaliil: 7/493, Ch. ya Dar Al Fikri] Na Kitabu cha Al-ashbaahu wa Nadhwaair, cha Asuyuutiy, uku, 326, Ch. ya Dar Al-kutub Al Elmiyah].
Na Jamhuri ya Wanazuoni imekubaliana kuwa inajuzu kwa Mpangaji kukodisha pango lake kwa mtu mwingine, na kulikamata ndani ya muda wa mkataba, kwa kuwa tu jengo hilo halitaathirika kwa kutumiwa na Mtu mwingine, na Wanachuoni wengi wa Fiqhi katika Salafi yaani wema waliotutangulia, wamejuzisha, iwe kwa Mfano au ziada ya malipo ya awali.
Na Kadhi Abu Yaaliy, ambaye ni katika wafuasi wa Madhehebu ya Imamu Hanbali, yeye anaona kwamba jambo hili linakatazwa moja kwa moja; kwani Mtume S.A.W. amekataza kujipatia faida kwa kitu ambacho hakijadhaminiwa, na Manufaa hayo hayajaingia katika dhamana yake, kwa hiyo haikujuzu, na ya kwanza ni sahihi zaidi; kwa kuwa makabidhiano ya nyumba yamechukua nafasi ya makabidhiano ya manufaa [Al Mughniy li- Ibni Quddaamah: 6/53, Ch. ya Dar Al Kitaab Arabiy].
Ama kuhusu kukodisha kwa Mpangaji kwa bei ya juu zaidi kuliko ile ya Mwenye nyumba: Wanachuoni wa Madhehebu ya Maliki na Shafiyy wanaona Kuwa inajuzu kufanya hivyo bila mipaka yoyote, yawe malipo hayo ya pili yanayolingana na aliotoa yeye au kwa kuzidisha au kwa kupunguza; kwani kupangisha ni kuuza, na yeye ana haki ya kuuza alichopangishwa kwa thamani ile ile aliyoitoa, au kwa kuongeza au kupunguza kama kuuza, na Ahmad ameafikiana nao kwa kauli Sahihi zitakazo kwake.
Na Wanachuoni wa Madhehebu ya Hanafiy wanaona kuwa ukodishaji wa pili unajuzu kama malipo yake hayatakuwa sawa na malipo ya awali, kwa maana iliyotangulia. Na ikiwa malipo ya ya ukodishaji wa kwanza na wa pili yatakapofanyika, basi nyongeza haitakuwa nzuri kwa mpangaji. Na atatakiwa aitoe Sadaka, na Upangaji wa pili utakuwa sahihi; kwa kuwa nyongeza yoyote ndani yake ina utata. Na ikiwa itazushwa nyongeza katika Pango linalokodishwa, basi ziada itakuwa nzur; kwani ziada hiyo ni mbadala wa ziada mpya, na kama atakarabati Jengo kwa kukarabati baadhi ya kasoro au akaboresha kwan namna ambayo inaleta tofauti ya bei ya Jengo, kwa kutokana na ukarabati huo, basi katika hali hiyo itakuwa inajuzu kuchukua nyongeza ya malipo hata kama nyongeza hiyo itakuwa maradufu ya malipo ya awali kwa Mujibu wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa. Na Wanachuoni wa Madhehebu ya Hanbali wao wanaifuata kauli ya pili ambayo; ikiwa mpangaji wa kwanza ataongeza kitu katika Jengo basi inajuzu kwake kufanya hivyo katika malipo bila ya kuwapo sharti lolote la kulingana na kiwango cha malipo au kutofautiana kwake, iwe ni kwa idhini ya mkodishaji au bila idhini yake. Na Imamu Ahmad ana kauli ya tatu kwamba iwapo mkodishaji ataidhinisha ongezeko la nyongeza basi itajuzu, na kama hakuidhinisha basi haisihi.
Na Khatwiib As Sherbiiniy amesema katika kitabu cha: [Mughniyl Muhtaaj: 3/474, Ch. ya Ad Daar Al Elmiiyah]. "Na Mpangaji ana haki ya kujinufaisha kikamilifu yeye mwenyewe au kumnufaisha mtu mwingine) kama ambavyo inajuzu kwake kumpangisha Mtu mwingine lakini kwa sharti la uaminifu kwa aliyekabidhiwa, na kama alimshurutisha kuitumia nyumba na kunufaika nayo yeye mwenyewe binafsi basi haitasihi kumpangisha mwingine na ni kama vile kumuuzia kitu na akamshurutisha kutokukiuza kitu hicho”. Mwisho.
Na katika Kitabu cha: [Al Muhadhabu cha Shiraziy: 1/403, Ch. ya Isal Halabiy]: “Na mkodishwaji ana haki ya kupangisha nyumba aliyopanga.
Na katika Kitabu cha [Mughniy cha Ibnu Quddaamah, 6/53-55, Ch. ya Dar Al Kitaab Al Arabiy] inajuzu kwa mkodishwaji kukodisha alichokodishiwa ikiwa atakipokea. Na Ahmad amelizungumzia Jambo hili. Na pia Saiid bin Musiibu, na Ibnu Siiriin, na Kukashifu, na Ikramah, na Abuu salamu Ibnu Abdulrahman, na Nukhaiiyu, na Shuubaa, na Thauriy, na Shafiy na Wanachuoni wenye maoni. Na Kadhi ametaja ndani yake rai nyingine kwamba haijuzu; kwa kuwa Mtume S.A.W. amezuia kunufaika na kisichoingia katika dhamana yake; na kwamba yeye ameingia mkataba katika kitu ambacho hakiingii katika dhamana yake, na kwa ajili hiyo hakijuzu. Ni kama vile kuuza kitu kilichokwishapimwa kabla ya kupewa. Na ya kwanza ni sahihi zaidi; kwa kuwa kupokea Kitu kumechukua nafasi ya kupokea Manufaa, kwa dalili kwamba inajuzu kukitumia kitu hicho utakavyo, na kwa ajili hiyo ikawa inajuzu kuingia mkataba katika kitu hicho, kama vile kuuza matunda yaliyo mtini. Na kinabatilika kuipima Riwaya nyingine kwa asili hii hii… na inajuzu kwa mpangaji kukodisha pango lake kwa Malipo yanayofanana na aliyoyatoa yeye au kwa kuzidisha. Ahmad ameyasema hayo. Na amepokea hivyo kutoka kwa atwaau, Hassan, Azahriy na pia Shafiy amesema hivyo hivyo na Abu Thaur na Ibnul Mundhir. Na kutoka kwa Ahmad kwamba yeye anaona kuwa iwapo kutaongwzwa nyongeza yoyote katika Kinachokodishwa itajuzu kwake kurejesha kwa ziada hiyo na kama sio hivyo haitajuzu, na ikiwa atafanya hivyo, basi hiyo ziada ataitoa sadaka, na Shuabiy amepokea hivyo. Na hivyo ndivyo walivyosema: Thauriy na Abu Hanifa; kwa sababu yeye anapata faida kwa kitu ambacho hana dhamana nacho na Mtume S.A.W, amekataza kujichumia faida katika kitu kisichokuwa na dhamana; na kwamba yeye ananufaika na kitu ambacho hakupewa dhamana yake na kwa ajili hiyo haijuzu. Kama vile mtu angelipata faida katika chakula kabla ya kukabidhiwa. Na hili linaenda kinyume kabisa na hali ambayo kama mtu angelilifanyia kazi jambo; kwani kwa kawaida kazi hufanywa kwa malipo ya kazi hiyo. Na kutoka kwa Ahmad Kuna Mapokezi ya tatu: Ikiwa mmiliki wa nyumba atamruhusu aongeze bei pango, basi kwa hali hiyo itajuzu yeye kuongeza bei, na kama mmiliki wa nyumba hajamruhusu basi haitajuzu yeye kuongeza bei ya pango. Na Ibnu Musib anaona kuwa inachukiza kufanya hivyo, na pia Abuu Salamu, Mujaahid, Ikrimah, Shuabiy, na Nakh-iyu. Wao wanaona Kuwa nyongeza ya aina yoyote ile inachukiza; kwa kuingia kwake katika faida fulani ambayo hakijadhaminiwa, na sisi tunaona kuwa ni Mkataba unaojuzu kwa mtaji wa fedha, na kwa ajili hiyo ikawa inajuzu kuongeza bei ya pango baada ya kukabidhiwa, ni sawa na kuuza kitu baada ya kukitia mkononi kitu hicho, na ni kama vile mtu aliliboresha jengo bila kupata sehemu ya ujira wake, na kwa mujibu wa Hadithi ni kwamba kama Manufaa hayo yangelipita bila ya kuyatumia ipasavyo yangelikuwa chini ya dhamana yake. Na wala hakisihi Kipimo cha kuuza chakula kabla ya kukipokea; hakika mauzo hayo hayaruhusiwi kabisa kwa ujumla wake, awe amepata faida au hajapata faida, na hapa ndipo panapojuzu katika Jumla hii, na kuweka kwao sababu kwamba kupata faida kwa mbadala wa kazi yake kumefutwa kwa namna ambayo kama angelifagia nyumba na kuisafisha, hakika hatua hiyo kwa kawaida inaongeza malipo yake”. Mwisho.
Na Ibnu Haazim wa Madhehebu ya Dhwaahiriyah anasema katika kitabu chake cha [Al Muhallaa: 7/23, Ch. ya Dar Al Fikr] “Na Mtu yoyote atakayekodishwa nyumba, Mtumwa, mnyama au kitu chochote, kisha na yeye akakikodisha kwa fedha zaidi ya alivyolipa yeye, au kwa kiasi cha chini kuliko alivyolipa yeye, au mfano wa alivyolipa yeye, ni halali na inajuzu kwake kufanya hivyo. Na vilevile fundi aliyepewa kazi ya kutengeneza kitu kisha na yeye akamwajiri Mtu mwingine amfanyie kazi hiyo kwa Kiwango cha chini cha fedha au cha juu au kilicho sawa na alichopewa yeye, basi kufanya hivyo, na nyongeza inajuzu kwa wote wawili ni halali, isipokuwa ikiwa walisaini Mkataba wa yeye mwenyewe kuishi katika nyumba hiyo, au kama ni mnyama amtumie yeye mwenyewe au aifanye kazi husika yeye mwenyewe, basi katika hali hiyo haijuzu kinyume na mkataba wa kukodisha; kwani hakika mambo yalivyo haikuja amri yoyote kutoka kwa Mtume S.A.W, inayokataza kufanya hivyo, na huku ni kukodishiana ambako Mtume S.A.W, alikuamrisha kama ni kukodishiana”. Mwisho.
Na kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia: hakika kinachochukuliwa leo hii katika kile kinachoitwa “Mtu kujivua au kuuondosha mkono wake”, hakuna kizuizi chochote cha hilo kisheria, anachokichukua mkodishaji kama malipo mbadala ya kujivua kwake hiyo haki yake ya kunufaika na nyumba ya iliyokodishwa kwa mtu mwingine, kunachukua nafasi yake na inajuzu ikiwa muda wa pango bado upo; kwa sababu yeye anaingia Mkataba wa kumilikisha Manufaa ya Jengo, kwa hivyo yeye ana haki ya kummilikisha mtu mwingine na kulipwa malipo kwa kufanya hivyo. Mtu atakaemiliki manufaa atamikiki haki ya kulipwa kwa kuimilikisha kwa mwingine kama ilivyotangulia kutajwa katika Msingi wa Fiqhi ya Kiislamu ulio mashuhuri.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas