Kupangusa kwa Maji Kwenye Soksi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kupangusa kwa Maji Kwenye Soksi

Question

 Baadhi ya watu hupangusa kwa maji kwenye soksi wakati mwingine soksi hizo huwa ni nyepesi ambapo hazizuii maji kupita na kufika mguuni, wanatoa hoja kuwa miongoni mwa wanachuoni wapo waliopitisha hukumu ya kupangusa kwa maji kwenye soksi, je maneno haya ni sahihi?

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, swala na salamu ziwe kwa Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W. pamoja na Maswahaba wake na wale wenye kumfuata kwa wema mpaka siku ya mwisho, na baada ya hayo:.
Ulazima katika kutawadha ni kuosha miguu miwili kwa kufanyia kazi maandiko ya Qur`ani kwenye Surat Al-Maidah, lakini sharia imeacha ulazima huu ili kuondoa uzito kwa waja, ikahalalisha kupangusa kwa maji juu ya khofu mbili, ambapo hitajio kubwa ni baridi kuwa kali sana au mfano wa safari au mambo ya kazi, ni ruhusa kupangusa.
Wanachuoni wamekubaliana kuwa miongoni mwa masharti ya kupangusa kwenye khofu ni kuzivaa baada ya kuwa umeshajisafisha na hadathi mbili kubwa na ndogo, na kuwa ni zenye kufunika sehemu za miguuni za lazima kuoshwa, kuzuia maji kutoingia ndani, na ziwe zenye kina kikubwa cha kufumwa na ngumu zenye kuwezekana kutembea nazo.
Kutokana na hayo, sharti la kina kikubwa cha kufumwa kwa kitu ni kufikia kusitiri kilicho ndani yake, anasema Imamu shaafi katika kitabu cha: [Ummu 1/49 Ch. ya Dar Al-Maarifa]: “Ikiwa khofu mbili zimetengenezwa kwa manyoya au kitambaa haziwi katika maana ya khofu mpaka ziwe sehemu za kutawadhwa kuwa zimefunikwa na kitu kigumu kisichoonesha”.
Masuala ya kupangusa juu ya kile kinachoitwa katika zama zetu “soksi” zimezungumziwa na wanachuoni kwa anuwani: Kupangusa kwa maji juu ya kile kinachochukuwa nafasi ya khofu, na kuzungumzia katika jumla ya hivyo ni pamoja na soksi, baadhi ya wanachuoni wamepitisha kufaa kufuta juu ya soksi, na baadhi wakaweka kigezo, na wengine wakazuia kwa maana wameona haifai, na sababu ya tofauti hii inarejea kwenye sababu mbili:
Ya Kwanza: Ni tofauti katika kuthibiti Hadithi zilizopokelewa toka kwa Mtume S.A.W. za kufaa kufuta juu ya soksi.
Ya Pili: Ni tofauti kuwa je inafaa kuleta kipimo katika mambo ya ibada au hapana, miongoni mwao wapo waliopitisha Hadithi ya kufuta juu ya soksi, au wameielezea lakini haijathibiti kwao Hadithi na wala hawaoni uwepo wa ulinganisho na khofu, na kuhusisha kufuta au kupungusa kwenye khofu, wala hawajasema kufaa kufuta juu ya soksi, na wenye kuthibiti kufaa kwa Hadithi kufuta juu ya soksi, au wakapitisha uwiano wa kisichokuwa khofu kwa khofu basi wamepitisha kufaa kufuta juu ya soksi.
Kupitia mitazamo ya wanachuoni ni kuwa soksi haina sifa moja, bali imekuwa na sifa nyingi ambapo haiwezekani kuzikusanya kati ya sifa hizi, kama vile tofauti ya kuifanya soksi ni aina ya khofu au tofauti yenye kufanana, baadhi wameielezea kuwa ni khofu lakini ni katika aina maalumu, na baadhi wameifananisha na khofu lakini imekuwa na sifa tofauti na khofu kwa upande wa urefu na aina.
Anasema Al-Adhiim Aabady akitoa sababu ya tofauti hii katika wasifu: “...amefahamu kutokana na kauli hizi kuwa soksi ni aina ya khofu isipokuwa yenyewe ni kubwa kidogo, baadhi ya wanachuoni wanasema yenyewe inafika kwenye ugoko wa mguu, na baadhi yao wanasema: Yenyewe ni khofu huvaliwa juu ya khofu mpaka kwenye kaabu mbili, kisha wakatahitalifiana: je yenyewe hutengenezwa kwa ngozi au manyoya na pamba, akaifasiri mwenye kamusi kuwa ni kivaliwa cha mguuni, na tafasiri hii kwa ujumla wake inaonesha juu ya kufunika mguu inayotokana na ngozi manyoya na pamba. Ama kwa upande wa Tweiiby na Shaukaniy wameweka kigezo cha kuwa ya ngozi, na hii pia ni maelezo ya Sheikh Dahlawiy. Ama Imamu Abubakr Ibn Al-Arabiy kisha mwanachuoni Al-Ainiy wamesema inatengenezwa kwa manyoya.
Ama mwanga wa Umma Al-Halawaniy akaigawa katika aina tano, basi tofauti hii Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kujua zaidi, ama kwa sababu watu wa lugha wametofautiana katika tafasiri ya soksi, au kwa kuwa kwake soksi ni yenye umbile tofauti na kutengenezwa nchi mbalimbali, baadhi ya maeneo ilikuwa inatengenezwa kwa ngozi, na baadhi yake zipo kila aina, kila mmoja ameifasiri tafasiri ya umbile linalopatikana nchini kwake, wengine wameifasiri aina zote zinazopatikana nchi mbalimbali kwa aina yeyote ile iliyopo” kitabu cha: [Ain Al-Maaboud 1/270].
Jambo ambalo linatupa uyakini ni kuwa soksi – ni sawa sawa ikiwa ni aina ya khofu au inafanana na khofu – ni yenye sifa tofauti na khofu, na ipo tofauti na kila kinachoitwa kwenye zama zetu “soksi”, wala hazifanani isipokuwa ni kwa upande wa jina, na kufanana jina hakulazimishi kufanana kitu chenyewe, hivyo haifai kuondoa tofauti katika kufuta juu ya soksi kwa kufuta juu ya soksi, wala dalili haikamiliki kwa kufaa kufuta juu ya soksi kwa kusema: soksi haikuwa isipokuwa ni aina maalumu ya soksi.
Baadhi ya wanachuoni wamepitisha kupangusa kwa maji juu ya soksi nyembaba, hivyo inafaa kufuta juu ya soksi, kwa sababu hata kama kutakuwa na mjadala kuwa soksi ni aina maalumu ya soksi, kuleta dalili kwa baadhi ya wanachuoni juu ya kufaa kufuta juu ya soksi nyembamba hilo limejibiwa, ni kuwa jopo la wanachuoni wanaona kuwa haifai kufuta juu ya soksi isipokuwa ikiwa itachukuwa nafasi ya khofu kwa sababu kwa kuwa kwake nzito au ngumu inazuia maji kuingia na kufikia mguuni, na iwe inawezekana kutembea nayo, na akaongeza Imamu Abu Hanifa sharti la kuwa ya ngozi au kuwa kama kiatu, akaikubali rai hii Imamu Maliki katika utengenezaji wake maalumu, na kuifanya kiatu kwa kuweka ngozi kwa chini, tofauti na kuifuma kwa kuweka ngozi juu yake na chini yake, angalia kitabu cha: [Sharhul kabiir 1/141 Ch. ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Araby].
Ama kwa sura ya nje wamepitisha kufuta kwa kila kinachovaliwa kwenye miguu miwili ikiwa kinachokuwa nafasi ya kuvaliwa kwa khofu, na kinafika juu ya kaabu mbili, ikiwa itakosekana sharti ya ugumu na uwezo wa kutembea nayo ndipo inapoingia soksi nyepesi, rejea kitabu Cha: [Al-Mahally cha Ibn Hazm, 1/321 Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya], na wakaleta dalili ya hilo kama ifuatavyo:
Dalili ya Kwanza: Hadithi ya Mughirah Ibn Shu’ba: “Kuwa Mtume S.A.W. alifuta kwenye soksi mbili na viatu viwili” Hadithi hii imetokana na Ahmad na Abu Daudi kutoka kwa Uthman Ibn Aby Shaibah, pamoja na Tirmidhy kutoka kwa Hannad na Mahmoud Ibn Ghailaan, na An-Nisaaiy kutoka kwa Is’haq Ibn Ibrahimu, na Ibn Maja kutoka kwa Ally Ibn Muhammad, wote hawa wamepokea kutoka kwa Wakii kutoka kwa Sufyani kutoka kwa Abi Qais kutoka kwa Huzeil Ibn Sharhabeel.
Dalili ya Pili: Ni Hadithi ya Abi Musa Al-Ash’ary: “Kuwa Mtume S.A.W. alitawadha na kufuta juu ya soksi mbili na viatu viwili”. Ni Hadithi inayotokana na Ibn Majah kutoka kwa Muhammad Ibn Yahya, kutoka kwa Muallaa Ibn Mansour na Bashar Ibn Adam, kutoka kwa Issa Ibn Yunus, kutoka kwa Issa Ibn Sinan, kutoka kwa Dhihaak Ibn Abdulrahman Ibn Azrab.
Dalili ya Tatu: Hadithi ya Thuuban amesema: “Mtume S.A.W. alituma wajumbe wakiwa njiani walipatwa na baridi, pindi walipofika kwa Mtume S.A.W. walifikisha malalamiko ya yale yaliyowakuta ikiwa ni pamoja na baridi, Mtume S.A.W. akawaamrishi kufuta juu ya khofu”. Imepokelewa na Ahmad kutoka kwa Yahya Ibn Said kutoka kwa Thaur kutoka kwa Rashid Ibn Saad.
Sura ya dalili katika Hadithi mbili za kwanza: Ni kuwa soksi moja kwa moja kwenye Hadithi hizo mbili, inaonesha kuwa kila kinachotokea ni jina la soksi kufuta juu yake ni jambo lenye kufaa, kama kitu cha kuleta joto kilichoelezewa katika Hadithi ya tatu ni kila kitu chenye kuleta joto mguuni ikiwa ni miongoni mwa khofu soksi na mfano wa hivyo.
Jibu la dalili za Hadithi mbili kwa upande wa mapokezi na dalili: Ama kwa upande wa mapokezi ni Hadithi ya Mughirah na Abi Mussa Al-Ash’ariy kwa wapokezi hao kuna maelezo, kwani wanachuoni wakubwa wa umma na wahifadhi wa Hadithi wamewadhoofisha, katika Hadithi ya Mughirah amezungumza Abu Daud: “Alikuwa Abdurahman Ibn Mahdy hazungumzi kwa Hadithi hii, kwa sababu kinachofahamika kwa Mughirah ni kuwa Mtume S.A.W. alifuta juu ya khofu mbili”, na anasema An-Nisaa katika kitabu Al-Kubraa: “Hatumfahamu yeyote akiwa na Aba Qais kwenye upokezi huu, na usahihi kuhusu Mughirah ni kuwa Mtume S.A.W. alifuta juu ya khofu mbili”, ametaja Baihaqy Hadithi hii na akasema: “Ni Hadithi inayopingwa. Sufyan Thauriy ameidhoofisha na Abdulrahman Ibn Mahdiy na Ahmad na wengineo, kinachofahamika kutoka kwa Mughirah ni Hadithi ya kufuta juu ya khofu mbili, amesema Abu Muhammad Yahya Ibn Mansour: Nimemuona Muslim Ibn Hajaj ameidhoofisha Hadithi hii, na akasema Abu Qais na Huzeil Ibn Sharhabil hawaizingatii, hii ni pamoja na kupingana kwao na wasomi wa dini waliopokea habari hii kutoka kwa Mughirah na wakasema: Kufuta juu ya khofu mbili, na wakasema: Hatuwezi kuacha uwazi wa Qur`ani kwa mfano wa Abi Qis na Huzail.
Kisa hiki kikatajwa na Muslimu kwa Abi Abbas Muhammad Ibn Abdurahman, nimemsikia akisema nimemsikia Ally Ibn Mukhallad Ibn Shaiban anasema nimemsikia Aba Qudama Sarkhasy anasema: Amesema Abdulrahman Ibn Mahdy nikamwambia Sufyan Thaury: Lau atanizungumzisha Hadithi Abi Qais kutoka kwa Huzail sitokukubali. Akasema Sufyan: Hadithi ni dhaifu au akasema wahaa (si ya kuzingatiwa) au neno la mfano wake”. Akasema pia: Nilimuuliza Aba Zakaria - yaani Yahya Ibn Mueen - kuhusu Hadithi hii, akasema: Watu wote wameipokea kwa maana ya juu ya khofu mbili tofauti na Abi Qais”. Na amesema mfano wa hivyo katika kitabu cha: [Al-Maarifa].
Amesema An-Nawawiy katika cha: [Majmuu 1/527]: “Hadithi ya Mughirah ni dhaifu wameidhoofisha wahifadhi wa Hadithi, ameidhoofisha pia Baihaqiy na amenukuu udhaifishaji wake toka kwa Sufyan Thauriy na Abdurahman Ibn Mahdiy na Ahmad Ibn Hanbal na wengineo ambao ni wasomi wa Hadithi, pamoja na Tirmidhy amesema: Hadithi ni hasan.
Ni Imamu mmoja tu ametoa hukumu kwenye Hadithi hii ya Mughirah kuwa ni Hadithi inayochukiza, na mtazamo wake: Ni kuwa ndani yake kuna mpokezi Aba Qais, naye ni Abdurahman Ibn Tharwan, amesema An-Nisaai kuwa ndani yake hakuna ubaya, na amesema Abu Hatim: Si Hadithi yenye nguvu sana nayo ni katika Hadithi chache, aliulizwa Hafidh ni namna gani Hadithi yake? akasema: Ni hasan ni Hadithi laini, na akasema Dar Kutuniy katika kitabu cha: [Al-Ilal 7/112 Ch. ya Dar Tiba] kuhusu maelezo ya Hadithi hii: Hakuna aliyeipokea zaidi ya Abi Qais, nayo ni katika inayoashiriwa, kwa sababu kinachofahamika kutoka kwa Mughirah ni kufuta juu ya khofu mbili.
Na akasema Abdillah Ibn Ahmad katika kile alichonukuu Uqaily: Nilimuuliza baba yangu kuhusu Abi Qais Abdurahman Ibn Tharwan, akasema: Yeye yupo hivi na hivi – huku akitikisa mikono yake – naye anakwenda kinyume na Hadithi alizo zizoofisha [Al-Uqail 2/327 Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiya]. Na akasema Hafidh Ibn Hajar katika kitabu cha: [Taqreeb 2/337 Ch. ya Dar Rasheed]: Ni ukweli lakini huenda alikwenda kinyume”.
Kwa kuongezea ni kuwa Hadithi ya kupangusa kwa maji juu ya khofu mbili imepokelewa kwa Mughirah kiasi cha njia sitini hakuna katika njia hizo kupangusa kwa maji juu ya soksi isipokuwa ni mapokezi ya Abi Qais, kwa sababu hiyo ndio imehukumiwa kuwa ni Hadithi inayopingwa, na Hadithi inayopingwa: Ni ile iliyopokelewa na watu dhaifu wanaokwenda kinyume na wale wanao aminika, kwa mfano kukubalika Abi Qais Hadithi inakuwa isiyo na wapokezi wengi, kwa sababu amekwenda kinyume na anaye kubalika kwa aliye bora zaidi kukubalika.
Ama usahihi wa Hadithi wa Tirmidhy na Ibn Habban hauna faida, kwa sababu ya kukubali kwake hakanushi Hadithi isiyo na wapokezi wengi wala inayochukiza, kwa kusahihisha kunakuwa kwa upokezi tu, kwa kuongezea hili ni sharti la Tirmidhy katika Hadithi baada ya kupokea kwake, ambapo amesema baada ya kuitaja, hakika kufuta juu ya soksi mbili si kauli moja ya wanachuoni: “Wakasema: Hufutwa juu ya soksi mbili pindi zikiwa nzito”, nayo ni kauli pia iliyopitishwa na jopo la wanachuoni, vilevile ameweka kigezo Ibn Habban kufaa kufuta kwa kuwepo kiatu pamoja na soksi, ambapo amesema katika kitabu Tabwib: “Ametaja uhalali wa mtu kufuta juu ya soksi mbili ikiwa zipo pamoja na viatu viwili”, nayo ni kauli aliyoikubali Abu Hanifa.
Na Hadithi ya Abi Mussa amesema Abu Daud: “Hadithi ya Abi Mussa Al-Ash’ary si yenye kuungana wala yenye nguvu”, na akasema Baihaqiy:
Si yenye kuungana kwa sababu ni katika Hadithi zilizopokelewa na Sahaak Ibn Abdirahman kutoka kwa Abi Mussa, wala haijathibiti kumsikia yeye, na wala si Hadithi yenye nguvu, kwa sababu ni katika mapokezi ya Issa Ibn Sinan kutoka kwa Dhihaak na ameifanya kuwa ni dhaifu Ahmad na Ibn Mueen pamoja na Abu Zaraa na An-Nisaai na wengine”, amesema Twabrany katika kitabu cha: [Al-Ausatiy 2/24 Ch. ya Dar Al-Haramain]: “Haipokelewi Hadithi hii kutoka kwa Abi Mussa isipokuwa kwa upokezi huu, amekuwa peke yake Issa Ibn Sinan”. Pamoja na kauli za baadhi zimethubutu kuwa Dhihaaq amesikia, Hadithi imetiwa ila kwa kuchanganyika kwake Issa Ibn Sinan.
Ama kwa upande wa mjadala wa dalili, anasema Ibn Hajar katika kitabu cha: [Diraya uk 71 Ch. ya Dar Al-Maarifa]: “Imepokelewa na Ahmad Abu Dawud na Haakim, na upokezi wake umekatika na kudhoofishwa na Al Baihaqiy, amesema Al Bukhariy: haifai”.
Ama maelezo ya kukatika kwake ni kuwa Rashid Ibn Saad aliyepokea kwa Thauban hakusikia toka kwake kama ilivyonukuliwa hivyo na Abu Haatim kutoka kwa Imamu Ahmad, lakini Bukhary katika historia yake [3/292 iliyochapwa na Dar al-Kutub Al-Elmiyah], amesema: Kuwa yeye amesikia kwake, na katika yote ni kuwa hakuna dalili kabisa ya kufaa kufuta juu ya soksi ima ziwe soksi nyembamba au nzito, kwa sababu maana ya khofu kuwa na joto si soksi, limeelezewa hilo na Khalil katika kitabu cha Al-Ain na mwenye kitabu cha Muhitw na Ibn Sidah katika kitabu cha: Al-Mukhassas, na Ibn Mandhuur katika kitabu cha: Al-Lisaan, na Zaidy katika kitabu cha Taaj, na Ibn al-Athiieer katika kitabu cha: [An-Nihaayah].
Kutokana na maelezo hayo: Dalili ya wazi haijanyooka kwa yale waliyoyapitisha, ikiwa dalili yao itaondoka basi haifai kupangusa kwa maji zaidi ya kwenye khofu mbili isipokuwa kwa kufikiwa masharti ya khofu pamoja na kuwepo tofauti kati ya jopo la wanachuoni lakini hata hivyo wamekubaliana kuwa ugumu na uwezo wa kutembea nayo ni yenye kuzingatiwa bila ya tofauti yeyote, nayo ni hali isiyofikiwa katika kitu chenye kuvaliwa ndani ya zama zetu kwa maana ya soksi, hivyo haifai kupangusa kwa maji juu ya soksi. Na rai hii pamoja na kuwa ni dalili nzuri zaidi lakini masuala yanabakia na tofauti yasiyo kusanywa kwenye kauli moja, na katika Fiqhi tofauti ni kutopinga kile chenye tofauti, mwenye kuwa katika hali ya kulazimika na wala hakupata nafasi isipokuwa ni kufuta juu ya soksi basi hakuna ubaya wa kufuta kwenye soksi akiwa ni mwenye kunuiya kufuata wale waliopitisha, wala haifai kumpinga.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas