Upanuzi wa Rawdha Tukufu.

Egypt's Dar Al-Ifta

Upanuzi wa Rawdha Tukufu.

Question

Je, inajuzu kupanua Rawdha ya Mtume S.A.W. 

Answer

Sifa zote njema ni za Allah pekee, na sala na salamu ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya aali zake na maswahaba zake, na juu ya wale wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo
Kwenye Sunna iliyotakaswa imetajwa Hadithi inayohusiana na fadhila za Rawdha Tukufu (Bustani ya Peponi). Imepokelewa kutoka kwa Maimamu wawili: Bukhari na Muslam katika Sahihi zao, kutoka kwa Abdullah bin Zaid Al-Mazeni, R.A. kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., amesema: “Baina ya nyumba yangu na mimbari yangu kuna bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi” Hadithi hii imepokelewa kutoka kwa Abu Huraira, na katika sura hiyo kutoka kwa kikundi cha Masahaba.
Maneno ya Hadithi yaliyotangulia ni sahihi zaidi kuliko yale yaliyotajwa, na Hadithi hiyo ilitajwa kwa maneno mengine. Hadithi hiyo ilipokelewa kwa neno la “Kaburi langu” badala ya “Nyumba yangu” kutoka kwa mapokezi ya Imam Ahmad katika Musnad yake, Al-Baihaqiy katika Sunan yake, na imepokelewa kutoka kwa At-Twabraniy kwa isnaad nzuri kuwa: “Baina ya mimbari na nyumba ya Aisha ni bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi”, Kuhusu Hadithi ya kwanza imepokelewa kwa maana yake. Na Hadithi hiyo ya pili, imeonesha kuwa nyumba inayokusudiwa ni nyumba ya Aisha, kwa hivyo hakuna upinzani.
Imam Abu Ishaq Al-Harbiy alisema katika kitabu chake: "Gharib Al-Hadith" [3/1013, Ch. Ya Jaamiatu Umm Al-Qura]: alisema: “Kati ya kaburi langu na mimbari yangu ni bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi”. Wakati kaburi lake lilikuwa baada ya nyumba yake iliruhusiwa kusemwa: Kati ya kaburi langu na mimbari yangu, kama nyumba ilivyohamishwa kaburini.
Imam Al-Twahawiy alisema katika kitabu chake “Biyan Mushkil Al-Athar” [7/324]: “Hadithi hii ina maana ambayo lazima tuisimamie, ambayo ni kauli yake, Mtume S.A.W.: “Kati ya kaburi langu na mimbari yangu ni bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi” kulingana na yale yaliyomo ndani yake, pamoja na kauli yake: “Kati ya nyumba yangu na mimbari yangu ni bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi”, kwa hivyo marekebisho ni lazima iwe nyumba yake ni kaburi lake, na hiyo itakuwa ishara kubwa ya Unabii, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameficha kila mtu mahali atakapokufa isipokuwa yeye, Mtume S.A.W., kama alivyosema: “Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani.” Basi, Mwenyezi Mungu amemwambia Mtume wake mahali atakapokufa na mahali palipo na kaburi, hata Mtume amefahamu hivyo katika maisha yake, na hali hiyo ni heshima nzuri kwake yeye tu”.
Kuhusiana na maana ya kauli yake, “Bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi”, Al-Hafidh Ibn Hajar alisema katika "Fath Al-Bari 4/100, Ch. ya Dar Al-Marefah]: Hiyo ni, kama bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi katika huruma na furaha kupitia kile kinachotokana na kikao cha kumkumbuka Allah, haswa katika enzi yake, Mtume S.A.W., kwa hivyo itakuwa mfano bila kilinganishi, au kwa maana kwamba: ibada ndani ya mahali pa Rawdha inapelekea Peponi, kwa hivyo Hadithi hii ni kama maana tu, au ni kweli, na kwamba inamaanisha kwamba ni bustani ya kweli, na kwamba mahali hapa pa Rawdha patahamishiwa Peponi Siku ya Kiama. Hii ni matokeo ya maoni ya wanavyuoni katika Hadithi hii.
Maana hii ya mwisho ya Rawadha kwa kweli ni mahali hapa pa Rawdha patahamishiwa Peponi katika Akhera, na kwamba mahali hapa hapaangamizwi kabisa, hayo ni maoni ya Imam Malik na yamechaguliwa na Ibn An-Najjar na Al-Darwardiy, na Ibn Al-Hajj akaisahihisha katika kitabu chake Al-Madkhal, kwa sababu wanavyuoni walielewa kutoka kwa Hadithi hii faida kubwa kwa mahali pa Rawdha. [Rejea: Wafaa Al-Wafa kwa Al-Samhudi 2/429, 430]
Al-Hafiz Ibn Hajar pia amechagua hivyo ambapo alisema katika kitabu cha: [Al-Fath 11/475]: “Inamaanisha kwa kupaita mahali pale ni Rawdha: kwamba mahali hapo patahamishiwa Peponi, kwa hivyo huwa ni bustani miongoni mwa mabustani yake, au ni jazanda, kwa sababu ibada iliyo ndani ya Rawdha inamwongoza mwenye ibada kwa kuingia bustani ya Peponi, na mtazamo huu unawezekana, kwani hakuna uhusiano kwa mahali hapo, na Hadithi hii imepokelewa kwa heshima kubwa ya mahali hapo zaidi ya mahali pengine.
Al-Aref Ibn Abi Jamarah alisema katika kitabu cha: [Bahjatul Nufuus 2/91: 93, Ch. ya Matbaatu Sidq Al-Khairiyah karibu na Msikiti wa Al-Azhar huko Egypt]: “Misingi ya sharia imetuonesha mahali palipobarikiwa na baraka zake kwa ajili ya kupaimarisha kwa utii, kwa sababu thawabu ziko zaidi ndani yake, na vile vile siku zilizobarikiwa pia, na inawezekana ... kwamba miongoni mwa mahali hapa ni bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi, Kama ilivyo baraka ya Jiwe Jeusi “Al-Hajar Al-Aswad” Peponi... patakuwa mahali hapa ni bustani miongoni mwa mabustani Peponi, na patarudi Peponi kama palivyokuwa mahali pake, na mwenye kuabudu ndani yake atakuwa na bustani Peponi, na mtazamo huu ndio unaoonekana zaidi; labda kwa ajili ya hadhi yake Mtume S.A.W. ambayo iko juu, na kati yake na baba yake Ibrahimu katika hali hii kuna mfanano. Nao ni kwamba wakati Ibrahimu alipohusishwa kwa jiwe Peponi, vile vile Mtume wetu amehusishwa kwa Rawdha ambayo ni bustani miongoni mwa mabustani Peponi”
Sheikh Nour Al-Din Al-Samhudiy alisema katika kitabu chake cha: [Wafa Al-Wafa Fi Akhbar Dar Al-Mustafa 2/431, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] baada ya kunukuu maneno ya Ibn Abi Jamrah: “Ni kutokana na thamani, ambapo ni kufahamu maneno ya Hadithi ile kwa ukweli wake, kwani haihitajiki kuiondoa kwake, na hakuna aibu kwa hali hii, kwa sababu inathibitisha sehemu ya fadhili za ulimwengu, kwa sababu kwa muda mrefu kama mwanadamu yupo katika ulimwengu huu hajafunua ukweli wa ulimwengu huo, kwa sababu ya kuwepo mawingu mazito, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi, na kuhusishwa kwa Mtume kwa hali hii iliyotajwa hapo awali: kwa ajili ya kuabudu kwake, au kwa sababu ya kwenda kwake S.A.W., mara kwa mara, kati ya nyumba na mimbari yake, na karibu na kaburi lake tukufu ambalo ni bustani kubwa.
Kuhusu kuainisha mahali pa Rawdha, wanavyuoni wametofautiana kuhusu yafuatayo:
Kauli ya Kwanza: Ni pale palipolingana na ncha zote mbili za mimbari kutoka mbele ya Msikiti upande wa kuelekea Qiblah, na kulingana na chumba, pamoja na mahali palipolingana na chumba kutoka kaskazini, na kwa hivyo ni eneo la mraba.
Mwanachuoni Al-Sayyid Jaafar Al-Barzanji alisema katika kitabu chake cha: [Nuzahtul Nadhiriin fi Masjidi Sayyid Al-Awlain Wal-Akhiriin Uk. 15, Sabihi katika Al-Azhar]: “Mtazamo huu ni ule unaotegemewa, nao ni mtazamo wa wanavyuoni wengi na umma wa watu”
Mwanachuoni Ibn Al-Hammam alisema katika kitabu cha: [Fateh al-Qadeer 3/180, Ch. ya Dar Al-Fikr]: “Rawdha Takatifu, ambapo ni kati ya mimbari na kaburi Tukufu.”
Ibn Al-Hajj alisema katika kitabu cha: [Al-Madkhal 1/262, Ch. ya Maktaba ya Dar Al-Turath]: “Rawdha Takatifu, ambapo ni kati ya mimbari na Kaburi.”
Imam An-Nawawiy alisema katika Al-Majmuu [8/254, Ch. ya Al-Muniriyah]: “Rawdha Takatifu, ambapo ni kati ya mimbari na kaburi Tukufu.”
Al-Samhudi alisema katika kitabu chakecha: [Wafa Al-Wafa 2/437]: “Na kwamba inayokusudiwa ni Msikiti uliokamilishwa kwa upande mmoja ni nyuma ya chumba cha heshima kwa mahali ambapo Mtume, S.A.W., alipozoea kukaa kwa wajumbe wa Kiarabu karibu na- karibu na dirisha la chumba cha heshima.
Mtazamo wa Pili: Rawdha ni Msikiti ambao ulikuwepo wakati wake, S.A.W.
Mtazamo huu ndio alioudai Al-Samaani; akisema katika kitabu chake cha: [Al-Amali]: “Wakati Mungu alipopendelea Msikiti wa Mtume wa Allah, S.A.W., na akautukuza na kuibariki ibada ndani yake na kuidhoofisha, kwa hivyo, Mtume wa Allah, S.A.W., alipoita mahali pale Rawdha yaani bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi. Abu Jaafar Ibn Nasr alimwuliza Adawdi Al-Maliki, kuhusu kauli yake Mtume S.A.W.: “Kati ya nyumba yangu na mimbari yangu ni Rawdha,” alisema: “Mahali hapa pote ni Rawdha”. Hivi ndivyo alivyosema Sheikh Zain Al-Din Al-Maraghiy Al-Shafi'y, Jaji wa Al-Madinah Al-Munawwarah (mji ung'aao), wakati wake mwaka 859 kutoka Hijra; alisema: “Inapaswa kuamini kwamba Rawdha Tukufu haiainishwi kama inavyojulikana sasa, lakini badala yake inapanuka kwa kiwango cha nyumba zake, S.A.W., kutoka upande wa Sham. Nao ni mwisho wa Msikiti katika wakati wake, S.A.W., na kutokana na hivyo: mpaka wa Rawdha ni kutoka upande wa Magharibi kutoka kwenye mimbari kulingana na mwisho wa nyumba kutoka kwa Sham, kwa hivyo itakuwa mraba.” Al-Raymi alinukuu kauli hii pia juu ya wakati wake Al-Khatwib Ibn Jumlah As-Salihi As-Shafiy. (Rejea: Wafa Al-Wafa 2/435, Nuzhat An-Nadhiriin, uk. 15)
Na ushahidi wao juu ya haya ni:
1- Mapokezi mengine ya Hadithi yameonesha kuwa kile kinachokusudiwa na nyumba hiyo ni nyumba ya Aisha. Kama tutagundua kuwa neno lililotajwa linahusu jambo kwa ujumla.
Mwanachuoni Badr Al-Din Al-Aini alisema katika “Umdatul Qari” [10/355, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: “Inakusudiwa kwa kauli yake: “Nyumba yangu”: moja ya nyumba zake, sio zote, ambayo ni nyumba ya Aisha tu, ambayo alizikwa ndani yake na kaburi lake likawa ndani yake, na imepokelewa Katika Hadithi moja kuwa: “Kati ya mimbari na nyumba ya Aisha bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi” Al-Tabarani aliyaleta mapokezi hayo katika Kitabu chake Al-Mujam Al-Awsat.
2 - Iliyopokelewa katika Musnad ya Imam Ahmad kutoka kwa Hadithi ya Abdullah bin Zaid Al-Ansari, kwamba Mtume wa Allah, S.A.W., alisema: “Kati ya nyumba hizi – maana: nyumba zake - hadi mimbari yangu ni bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi, na mimbari iko kwenye mfereji miongoni mwa mifereji ya Peponi.”
Mwanachuoni Ibn Hajar Al-Haytami alisema katika kitabu chake cha: “Al-Jawhar Al-Munadham Fi Ziarat Al-Kabril Shariif An-Nabawiy Al-Mukaram [Uk. 176, Ch. ya Dar Jawamii Al-Kalam kule Kairo]: “Haya ni kama mapokezi ya: “Nyumba yangu”, maana yake Msikiti wake wote ni Rawdha, kwa sababu nyumba zake, Mtume S.A.W., zilizozunguka na Msikiti kutoka Qiblah, Mashariki, Sham, na mimbari ya Magharibi.”
Jibu ni kwamba neno hili katika mapokezi hayo halifahamiki. Mapokezi mengine yaliyopokelewa kutoka kwa Sufyan bin Uyaynah, Malik bin Anas, Yazid bin Abdullah bin Osama bin Al-Hadi kutoka kwa Abdullah bin Abi Bakr, kutoka kwa Abdullah Bin Tamim, kutoka kwa Abdullah bin Yazid Al-Ansari kwa maneno haya: “Kati ya nyumba yangu na mimbari yangu”- Kama ilivyotajwa katika Tuhfat Al-Ashraf 4/339, Al-Maktab Al-Islami Ad-Dar Al-Qiymah - na kuhusu Mapokezi ya Ahmad, imepokelewa kutoka kwa Fulaih bin Sulaiman. Abu Hatim Al-Raziy alisema: Hadithi hiyo haina nguvu, Ibn Main alisema: Hadithi hiyo haina nguvu, Al-Nasai alisema: Hadithi hiyo ni dhaifu, Murah alisema pia: “Hadithi hiyo haina nguvu”. Tahdhib Al-Tahdhiib 8/273, Ch. ya Dar Al-Fikr]
Al-Hafiz Ibn Hajar alisema katika kitabu chake cha: [An-Nukat Ala Ibn As-Salah 2/157, Adhwaa As-Salaf]: “Yeyote anayetafakari maneno ya mababu miongoni mwa wanavyuoni wa Hadithi anaona kwamba, wanakanusha Hadithi ambayo inapingana na Hadithi ya wapokezi wanaohifadhi, Muislam alisema katika utangulizi wa kitabu chake: (Na ishara ya kukanusha kwa Hadithi ikiwa Hadithi yake ikitolewa kwa Hadithi ya watu wengine wanaohifadhi, basi mapokezi yake yanapingana na mapokezi yao. Au yanakaribia hayakukubaliana nayo)
3 - Iliyopokelewa katika mapokezi ya Abu Bakr, Saad Bin Abi Waqqas, na Anas, R.A., kwa kusema: “Kati ya nyumba yangu na mahali pa kusali kwangu” au “Chumba changu na mahali pa kusali kwangu”, Al-Samudi alisema katika kitabu cha: Wafa Al-Wafa 2/428]: “Kundi la wanavyuoni walisema: Inamaanisha mahali pa kuswali Swala ya Eid, na wengine wakasema: Mahali pa kuswali ambamo anaswali Msikitini, kama vile Al-Khatwabiy alisema. Nilisema: Mapokezi ya kwanza yanaunga mkono mapokezi yaliyopokelewa kutoka kwa At-Taher Bin Yahya kutoka kwa baba yake Yahya baada ya Hadithi yaliyotajwa ilisemayo: (Baba yangu alisema: Nilisikia zaidi ya moja wakisema: Wakati Saad aliposikia Hadithi hii kutoka kwa Mtume, S.A.W., akaijenga nyumba yake kati ya msikiti na mahali pa Kusali kwa Mtume S.A.W., na vile vile itakayotajwa katika mahali pa kuswali Swala ya Eid kutoka mapokezi ya Ibn Shabba kutoka kwa Aisha Bint Saad Bin Abi Waqas, nikasema: Na Hadithi hii ni dalili kwa kile kinachotokea kutoka kwa Rawdha kwa Msikiti wote wa Mtume S.A.W., na kile kilichoongezwa kutoka kando ya Magharibi.
Jibu: Hakika Hadithi ya Saad hiyo ilipokelewa kutoka kwa At-Tabarani katika kitabu chake cha: [Al-Mujam Al-Kabeer 1/147, Ch. ya Maktabat Al-Uluum wal-Hikam huko Mausil], na miongoni mwa wapokezi ni Ishaq Bin Muhammad Al-Farawiy; Al-Nasaiy alisema: Hajaaminiwa, na Abu Dawud alisema: ni dhaifu, na Al-Darqutwni alisema: Wanavyuoni walizungumzia udhaifu wake [Al-Mughni fi Ad-Duhuafaa 1/121, Idara Ihyaa At-Turath Al-Islamiy katika Qatar], na kuhusu Hadithi ya Anas imepokelewa kutoka kwa At-Twabarani katika kitabu chake cha: [Mujam Al-Awsat 5/252, Dar Al-Haramain huko Kairo], na mapokezi hayo miongoni mwa wapokezi wake ni Adiy Bin Al-Fadl At-Taymi, naye ameachwa, [Taqriib At-Tahdheeb 1/388, Ch. ya Dar Al-Rasheed, Syria], na kuhusu Hadithi ya Abu Bakr, imepokelewa kutoka kwa Al-Bazzar katika Musnad yake [1/145, Muasastul Qur'ani wa Ulumuh] na amesema mapokezi hayo yana aibu.
4 – Kutoa dalili kwa maana ambayo kwa ajili yake mahali hapa palikuwa bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi, kwa sababu ya kwenda kwake S.A.W., mara kwa mara kwake na Swala zake na ibada yake huko, na hii ilikuwa nyuma ya msikiti kabla ya kugeuza Qiblah. [Rejea: Wafa Al-Wafa 2/437]
Jibu: Sababu ya hii haijatambuliwa, na kikundi cha wanavyuoni wamesema sababu zingine kama kuchukua baadhi yao kwa maana dhahiri ya Hadithi hii. Na wakisema kuwa: fadhila ya Rwadha Peponi ni kama fadhila za Rukn na Maqam ya Kaaba, na fadhila za maeneo hupelekwa kwenye hukumu, sio kwa sababu, na kile kinachotajwa kwake uwezekano hakiruhusiwi kukitoa kama hoja.
Mtazamo wa Tatu: Unazunguka Msikiti wote kwa wakati wake, S.A.W., na baada yake.
Mtazamo huu ulichaguliwa na Sheikh Jamal Al-Din Al-Rimi Al-Shafi'y na aliandika kuhusu suala hili kitabu kinachoitwa: [Dilaltul Mustarshid Ala Ana Ar-Rawdha Hiya Al-Masjid]. Al-Samhudi alisema katika kitabu chake: [Wafa Al-Wafa 2/432]: “Sheikh Swafiy Ad-Din Al-Kazruni Al-Madani aliandika kitabu chake kuhusu suala hilo na nilitoa muhtasari katika kitabu changu kilichoitwa “Dafuul Taarudh wal Inkaar Libast Rawdat Al-Mukhtar”.
Dalili yake ni kwamba: Msikiti mzima ni Rawdha, na kwamba ikiwa hukumu ya kurudisha thawabu ya Swala mara mbili imewekwa kwa kile kilichoongezeka ndani yake, basi maelezo ya Rawdha yanaongeza kwa kuongezeka vile vile, na msingi ni kwamba ongezeko linalohusiana linafuata asili yake, na kwamba kile kilicho karibu na kitu fulani kilichukua hukumu yake.
Tumeelezea msingi ambao Al-Rimiy alijenga kauli yake, ambayo ni kwamba Msikiti mzima ni Rawdha, kwa hivyo hatuna neno baada ya hapo kuelezea kuongezeka.
Mtazamo wa Nne: Rawdha inalingana na mimbari na chumba tu, kwa hivyo inapanuka kutoka upande wa chumba na nyembamba kutoka upande wa mimbari, na pande zimeshikwa; kupitisha mimbari kwa mwelekeo wa Qiblah na kucheleweshwa kwa chumba katika mwelekeo wa Sham, ili iwe kama sura ya pembe tatu ambayo hulingana na mimbari.
Dalili ya kauli hii ni: Kuzingatia maana dhahiri ya wazo la kweli kutokana na maneno yake Mtume S.A.W., kuwa: “Kati ya Nyumba yangu na mimbari yangu ni Rawdah yaani bustani miongoni mwa mabustani ya Peponi.” Ndipo imefahamika kwamba Nyumba hiyo ni chumba cha Aisha, R.A., kama inavyojulikana. Sheikh Al-Barazinji katika kitabu chake [Nuzhat An-Nadhiriin Uk. 15]: “Mtazamo huu umethibitishwa kwa kauli yake Mtume S.A.W.: “Kati ya kaburi langu na mimbari yangu”, ambayo maana yake ni, kati ya nyumba yangu ambayo nimezikwa, kwa sababu kuainisha katika upana wa Kaburi Tukufu uko mbali zaidi, na msimamo wa safu ya kwanza inayofuata chumba sio miononi mwa Rawdha ... Na inaudhoofisha kwamba sehemu ya mbele ya zamani lazima iondokewe na jina la Rawdha wakati huo, kwa sababu iliondoka sambamba kati ya pande mbili za mimbari na chumba cha heshima, ingawa inaonekana kwamba sababu kubwa ya kuwa eneo hili ni Rawdha; kwa heshima yake paji lake Mtume la heshima, na hakuna mtu aliyesema chochote kutoka mahali pa kuswali kutoka Rawdha, lakini wanavyuoni walikubaliana kuyafanya maeneo hayo miongoni mwa Rawdha.
Muhtasari:
Mipaka ya Rawdha ni mada ya kutokukubaliana kati ya wanavyuoni, na maoni yenye kujulikana zaidi miongoni mwa maoni ya wanavyuoni ni kwamba Rawdha ni kati ya mimbari ya Mtume S.A.W., na Nyumba ya Aisha, R.A. Kutokana na yaliyotangulia hapo juu: anayetaka kuabudu katika Rawdha Tukufu anatakiwa kuabudu kati ya nyumba na mimbari yake Mtume S.A.W.
Kuhusu mitazamo miwili ambayo inapanua mipaka ya Rawdha na kuufanya Msikiti wote ambao ulikuwepo wakati wa Mtume ni ile iliyoongezewa, na ikiwa basi tukidhoofisha dalili zao basi wao mwishoni kila mmoja alisema mtazamo ulisemwa na Maimaamu wazingatiwe, na mitazamo yao ni miongoni mwa tofauti zinazozingatiwa.
Yeyote anayependelea mtazamo mmoja na ana uwezo wa kutazama, anaweza kuufuata mtazamo huu na kutoa Fatwa kwa wengine, lakini kwa wale ambao hawakuwa na uwezo huo na walitaka kuiga wanavyuoni ambao wamesema kwa mtazamo mmoja wao, basi hakuna kikwazo kwa hilo, na yeye atapata thawabu, Allah akipenda, na Allah ni Karimu na fadhila Zake ni kubwa na zisizo na ukomo, na inajulikana kuwa Msikiti wa Mtume uko wazi kwa wote ili aweze kuabudu ndani yake kwa ibada yoyote kama anavyotaka na hakuna kikwazo kwa nia yake ikiwa akikusudia kuabudu katika Rawdha, na hatutaji wakati huo kuomba upanuzi wa Rawdha Tukufu.
Na Mwenyzi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas