Kubadili Mwelekeo.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kubadili Mwelekeo.

Question

Kijana mmoja alimkinaisha msichana ili aoane nae ndoa isiyo rasmi bila ya familia yake kujua lolote juu ya ndoa hiyo, kwa maana ya ndoa ya siri, na msichana alikubali kutokana na msisitizo wa kijana huyo na maneno yake matamu, wakazungumza mazungumzo yao na wakafikia maridhiano, mbele ya mashahidi wawili Waislamu, miongoni mwa wafanyakazi wenzake. Na baada ya muda kupita, kijana huyu alimchukia mke wake na akaamua kumwacha. Na sasa hivi kijana mwingine anataka kumposa kwa njia ya jamaa zake na kufunga nae ndoa rasmi. Je, inajuzu kwa msichana kuolewa na huyo kijana mwingine aliyemposa kwao, au kijana wa kwanza aliyemuoa kwa njia isiyo rasmi analazimika kumpa talaka kwanza? Pamoja na kujua kuwa msichana hajui mahali alipo kijana huyo wa kwanza kwa sasa? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa R.A., yanaona ya kuwa haishurutishwi walii kwa ajili ya usahihi wa ndoa; na mwanamke mwenyewe akipitisha mkataba wa ndoa yake basi inasihi kufungwa ndoa hiyo. Na sababu yake inatokana na maoni ya wafuasi wa madhehebu hayo kuwa: mwanamke alipitisha haki yake, wakati yeye ni mwenye jukumu la kufanya, mwenye akili na busara. Na kwa hiyo ana haki ya kuitumia mali yake na kumchagua mume kwa maridhiano, na mambo yote hayo yanajuzu. [Taz. Al-I’inayah na Al-Babertiy: 3/257, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Katika kitabu cha [Multaqa Al-Abhur na Sharh yake: Majmaa Al-Anhur na Mwanachuoni Damaad, ni miongoni mwa vitabu vya wafuasi wa Madhehebu ya Hanafiy: [1/332, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy] anasema: “Inasihi kwa mwanamke aliye huru, mwenye kukalifishwa, bikira au asiye bikira, kujiozesha yeye mwenyewe bila ya walii, yaani bila ya idhini ya walii wake au kuwepo kwa walii huyo, na haya ni maoni ya Maimamu Abu Hanifa na Abu Yusuf- kutokana na uwazi wa mapokezi; kwa sababu mwanamke huyo anatumia haki yake, ambapo anabeba jukumu lake kikamilifu, na kwa sababu hiyo ana haki ya kuzitumia mali zake. Na asili ya suala hili ni kwamba: mtu ye yote mwenye haki ya kuzitumia mali zake kwa kulibeba jukumu lake binafsi, yeye mwenyewe, hivyo ana haki ya kujiozesha, na ye yote asipoweza kufanya hapana”.
Na wanazuoni wengine wa Madhehebu ya Maliki, Shafiy, na Hanbali walikinzana na wafuasi wa Madhehebu ya Hanafi wakisema: Walii ni sharti la kusihi ndoa, na wakatoa daili ya Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mtakapowapa wanawake talaka nao wakamaliza eda yao, basi msiwazuie kuolewa na waume zao endapo baina yao wamepatana kwa wema}. [AL BAQARAH: 232].
Na upande wa dalili hii ni kwamba: Walii asipohitajika basi zuio lake halitakuwa na maana. Na pia walitoa dalili za mapokezi ya wapokeaji wanne, isipokuwa An Nasaiy, kutoka kwa Abu Musa Al-Asha’riy, walipokea kuwa Mtume S.A.W. alisema: “Hakuna ndoa isipokuwa kwa walii”. Na ilivyopokelewa kutoka kwa Ummul Muuminin Aisha R.A, kuwa Mtume S.A.W., alisema: “Mwanamke ye yote anapoolewa bila ya idhini ya walii wake, basi ndoa yake ni batili, ndoa yake ni batili, ndoa yake ni batili”, na ilivyopokelewa na Ibn Majah kutoka kwa Abu Huraira R.A, kuwa Mtume S.A.W., alisema: “Mwanamke hamuozi mwanamke wala hajiozeshi nafsi yake”. [Taz. Sharh Al-Kharashiy Ala Mukhtasar Khalil: 3/172, Ch. ya Dar Al-Fikr; Mughniy Al-Muhtaj: 4/242, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah; Sharh Muntaha Al-Iradaat: 2/673, Ch. ya Aaalam Al-Kutub].
Ikiwa inafahamika hivi, na kutokana na madhehebu ya wengi wa wanazuoni: hakika aliyeolewa bila ya walii, ikiwa kusudio lake ni kuifuata rai ya Imamu Abu Hanifa, au alifanya hivi bila ya kusudio hili hata kidogo.
Na kama akifanya hivi kwa nia ya kuifuata rai ya Imamu Abu hanifa, basi mkataba wa ndoa yake ni sahihi, kwa njia ya hukumu na siyo kwa hakika; yaani: haihukumiwi kuwa ni mwenye dhambi, kutokana na kumwacha walii; na kwa sababu yeye alifanya hivi kwa mujibu wa hoja, nayo ni kumfuata Imamu mwenye jitihada.
Na kama akifanya hivi bila ya kusudio kumfuata Imamu Abu Hanifa, pia inahukumiwa kuwa ndoa yake ni sahihi, kwa njia ya hukumu na maana iliyotangulia. Kwa sababu kazi ya mtu wa kawaida inaunganishwa na kauli ya mmoja wa wenye kujitahidi; na uunganishaji huu unajengwa kwa ilivyoamuliwa katika misingi ya Fiqhi kuwa: Mtu wa kawaida halazimiki kufuata madhehebu maalumu.
Kwa hiyo akifanya kitu ambacho ni sahihi kwa mujibu wa kauli ya baadhi ya Maimamu, basi kazi yake hii ni sahihi, ingawa wanazuoni wengine wanasema: siyo sahihi.
Na maana hii inaamuliwa na Bwana As-Samhudiy katika kitabu chake cha: [Al-I’iqd Al-Farid Fi Lijtihad wat-Taqlid], na inaegemezwa pia kwa ilivyonukuliwa na Bwana Suleiman Ibn Yahya katika Fatwa zake, kutoka kwa Imamu Al-Husain Ibn Abdur-Rahman Al-Ahdal kuwa alisema: “Kazi zote za watu wa kawaida kuhusu ibada na mauziano na mengineyo, ambayo hayapingani na kauli ya pamoja ni sahihi na S.A.W., iwapo watamfuata Imamu mwaminifu, na haya ni kutokana na rai sahihi”. [Mwisho; na Mukhtasar Al-Fawaid Al-Makkiyah, na pia kwa mujibu wa Mufti wa Madhehebu ya Shafiy Makkah Takatifu, Karne ya Kumi na tatu Hijriyah, Sheikh U’ulwiy As-Saqqaf: Uk. 47, Ch. ya Dar Al-Bashayir Al-Islamiyah].
Na Imamu Abul Fat-h Al-Harawiy anasema: “Madhehebu ya wanazuoni wetu wote – yaani wafuasi wa madhehebu ya Shafiy – ni kuwa: Mtu wa kawaida hana madhehebu”. [Mwisho: Al-Bahr Al-Muhiit, na Az-Zarkashiy: 8/375, Ch. ya Dar Al-Kutbiy].
Na kwa mtu wa kawaida hana madhehebu, basi halazimiki kufuata madhehebu yoyote maalumu, na ana haki ya kuchagua katika kufuata madhehebu yo yote miongoni mwa madhehebu yanayotambulika na kuzingatiwa, hivyo hivyo mtu huyo ana haki ya kuacha madhehebu moja na kuelekea madhehebu mengine.
Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha [Ar-Rawdha: 11/117, Ch. ya Al-Maktab Al-Islamiy] anasema: “Linaloashiria dalili kuwa: Mtu wa kawaida halazimiki kufuata madhehebu maalumu, na anaomba fatwa kutoka kwa anayemtaka, au anayemkuta, bila ya kutaka ruhusa kwa yoyote”. [Mwisho].
Na Mtaalamu Ibn Hajar Al-Haitamiy katika [Fatwa za Fiqhi: 4/315, Ch. ya Al-Maktabah Al-Islamiyah] anasema: “Ni sahihi zaidi kuwa: Mtu wa kawaida ana hiari ya kumfuata aliyemtaka hata pamoja na kuwepo aliye bora zaidi kwake, na hali ya kutofuata madhehebu maalumu ni ruhusa, na anaweza pia kufuata ruhusa, kutokana na kauli za baadhi ya wanazuoni, ambazo zilikubaliwa na Sheikh I’izziddin Ibn Abd Assalaam; pamoja na maelezo marefu”. [Mwisho].
Lakini kama hakimu au kadhi alihukumu usahihi wa mkataba huu wa ndoa, basi mkataba ni sahihi na unazingatiwa, na haijuzu kuubatilisha. Na sababu ya hayo ni kuwa: hukumu ya hakimu kuhusu ndoa utekelezaji wake ni wa nje na ndani yake. Na Mwanachuoni Mkubwa Akmal Addin Al-Babirtiy katika kitabu cha [Al-I’inayah: 3/252, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “Maana ya utekelezaji wake kwa nje ni: utekelezaji wa mkataba kivitendo kama vile: kukutana kimwili baina ya mume na mke, kutoa matumizi, yamini, na mengineyo; na maana ya utekelezaji wake kwa ndani ni: kuleta uhalali mbele ya Mwenyezi Mungu”. [Mwisho].
Na kama mkataba huu wa ndoa utapelekwa kwa mfuasi mmoja wa madhehebu ya Shafiy, kwa mfano, kwa ajili ya kuutolea fatwa yake, wakati mkataba huu haukukusanya masharti na nguzo zake, kutokana na kanuni za madhehebu yake, na bado kadhi akawa hajahukumu usahihi wake, kisha Mufti huyu akataka kuyapitisha madhehebu yake juu ya mkataba huo, basi hana budi kutoa hukumu ya ubatili wa mkatabu, kutokana na kanuni za madhehebu yake.
Na Imamu Ibn Hajar Al-Haitamiy katika kitabu cha [Tuhfat Al-Muhtaj: 10/109, Ch. ya Dar Ihiyaa At-Turath Al-Arabiy] kwenye maneno yake kuhusu: masharti anayotakiwa Kadhi mwenye kujitahidi ayafuate, anasema kuwa: kadhi asipokuwa mwenye jitihada kwa uwazi, basi atakuwa mfuasi wa Imamu maalumu, na ikiwa hivyo basi: “halazimiki isipokuwa kufahamu kanuni za Imamu wake, na analazimika kuziangalia kanuni wazi kabisa katika Sharia; kwa hiyo yeye mbele ya mwenye jitihada ni mfano wa mwenye jitihada mbele ya Andiko la Sharia”. [Mwisho].
Na suala hili limejengwa na suala lingine la msingi, nalo ni: Hukumu za Sharia za Fiqhi zilizoambatana na jitihada: usahihi wake ni mmoja kwenye kauli moja miongoni mwa kauli zote, na hata isipotambuliwi nasi, lakini ni inatambuliwa mbele ya Mwenyezi Mungu, na mwenye usahihi ni mmoja pia hata asipotambuliwa, na wengine wana kosa isipokuwa yule mmoja, na kwa vyo vyote iwavyo, wote ni wenye thawabu.
Na hii ni kauli ya wengi wa wanzuoni, na Al-Mawardiy aliinukulu kama ilivyotajwa katika kitabu cha [Al-Bahr Al-Muhiit, na Az-Zarkashiy: 8/283, Ch.ya Dar Al-Kutbiy], kutoka kwa Maimamu: Shafi, Abu Hanifa, Maliki, na wengi wa wanazuoni.
Na Sheikh Abu Is-haq Ash-Shiraziy katika kitabu cha [Sharh Al-Lumaa’: 2/1046, Ch. ya Dar Al-Gharb Al-Islamiy] anasema: “Haya ni maandishi ya Imamu Shafi, katika madhehebu yake mawili: ya zamani na ya sasa, na hana kauli nyingine isipokuwa hii, na simjui yoyote miongoni mwa wafuasi wake aliyeyapinga madhehebu yake”. [Mwisho].
Katika kitabu hicho [2/1048] alinukulu pia kutoka kwa Abu Aliy At-Tabariy kuwa alisema: “Al-Muzaniy alimaliza maneno hayo kaitka kitabu cha At-Targhiib Fil Ilm, na akasisitiza kuwa usahihi ni kauli moja, na akatoa dalili ya hayo, nayo ni madhehebu ya Imamu Maliki, Al-Laith, na pia ni madhehebu ya waandishi wote wafuasi wa Imamu Shafi, wa zamani na waliokuja baada yao, na rai hii pia ni ya wafuasi wa Al-Asha’ariy, miongoni mwao ni: Abu Bakr Ibn Mujahid, Abu Bakr Ibn Furak, na Abu Is-haq Al-Isfrayiniy”. [Mwisho].
Na hivi ndivyo ilivyosahihishwa na Ibn As-Subkiy katika kitabu cha [Jamu’u Al-Jawamii’] ambapo ilitajwa ndani yake, pamoja na Sharh yake na Mwanachuoni Al-Mahaliy [2/428-429; pamoja na Hashiyat Ala’attar, Ch. ya Dar Al-kutub Al-Ilimiyah]: “Kuhusu suala ambalo halina dalili thabiti miongoni mwa masuala ya Fiqhi… rai sahihi, kutokana na maoni ya wengi wa wanazuoni, ni kuwa: mwenye usahihi juu yake ni mmoja tu; na hukumu yake ni ya Mwenyezi Mungu kabla ya kufanya jitihada. Na imesemwa kuwa: haina dalili, bali ni kama Masuala yaliyofichikana ardhini, na Mungu akipenda mmojawapo atayafichua. Lakini rai sahihi ni kuwa: kuna alama, na mwenye kujitahidi anawajibika kuikuta hukumu yake, kwa sababu anaweza kuikuta. Pia mwenye kukosea hana dhambi, bali ana thawabu, kwa sababu yeye alifanya bidii katika kuitafuta”. [Mwisho].
Na dalili ya usahihi wa hayo ni kuwa: ikiwa kuna hukumu nyingi katika suala moja, basi inalazimika kuwepo vinyume pamoja; kwa sababu hukumu mbili zikiwa mfano wa wajibu na haramu, au kutakiwa na kuchukiwa, huwa ni hukumu za kugongana, na kukukutana vinyume ni muhali, na kwa hiyo hukumu nyingi katika suala moja ni muhali, hivyo ni lazima hukumu iwe moja, na huu ndio ukweli unaotakiwa.
Hivyo hivyo, Maimamu Bukhari na Muslim wamepokea kutoka kwa Amr Ibn Al-Aas R.A, kuwa Mtume S.A.W, alisema: “Hakimu anapohukumu na akajitahidi kisha akapatia, atapata ujira mara mbili, na akihukumu na akajitahidi, akakosea, atapata ujira mara moja”.
Na upande wa dalili ya Hadithi ni wazi; kwa sababu kauli ya Mtume S.A.W, inaonesha kuwa: mmoja wa wenye jitihada amepatia na mwingine amekosea, na hii inamaanisha kuwa haki ni moja, lakini haki zinapokuwa nyingi, basi mwenye jitihada ye yote atakuwa S.A.W. katika jitihada zake, na hii ni kinyume cha maana ya Hadithi.
Na Masahaba wa Mtume S.A.W, walihojiana masuala mengi, na kila mmoja kati yao alitoa kauli ya hoja yake, na wakakosoana wenyewe kwa wenyewe, na maana ya hayo ni kuwa: kila mmoja anataka kupata haki.
Na dalili yake pia ni kauli ya pamoja ya umma kuwa: inawajibika kuchunguza, kufanya jitihada, kuzipanga dalili, na kuzijenga zenyewe kwa zenyewe, na lau wote wangekuwa S.A.W., basi uchunguzi na jitihada zisingekuwa na maana. [Rejea: Sharh Al-Lumaa’ na Ash-Shiraziy: 2/1045; Al-Bahr Al-Muhiit na Az-Zarkashiy: 8/283-284; Usuul Al-Fiqh na Sheikh Zuhair: 4/266-267, Ch. ya Dar Al-Basair].
Na kwa mujibu wa hayo: Mkataba wa ndoa uliofungwa bila ya walii na yule anayemfuata Imamu Abu Hanifa, ni mkataba batili kwa rai ya Imamu Shafiy, kutokana na jitihada yake yeye mwenyewe, ambapo yeye anaona kuwa rai yake ni sahihi, na kutokana na rai yake hiyo mkataba si sahihi kwa kweli, lakini kwa kuchukulia hivyo, na sababu yake ni uwezekano wa kuwa madhehebu nyingine ni sahihi pia.
Na ikiwa mkataba usiokusanya masharti yake si batili, basi hakuna faida ya masharti yaliyowekwa na mwenye jitihada ambayo hupingana na madhehbu mengine; kama haisihi kauli yao kwa mfano: hii ni sahihi katika madhehebu ya Imamu Shafi, au batili katika madhehebu ya Hanafiy.
Hivyo hivyo kuuita usahihi wa kweli wa uwazi juu ya mkataba huu wa ndoa uliofungwa kati ya pande mbili – ingawa sharti moja limeondolewa, miongoni mwa masharti au nguzo zake, kwa rai ya kulizingatia hili lililoondolewa – hayo yanapingana na ufafanuzi wa Wanachuoni wa Misingi ya Fiqhi, kuhusu usahihi. Maana usahihi ni: “kukubaliwa tendo lenye sura mbili katika Sharia”. [Taz. Al-Mahsuul na Ar-Raziy: 1/112, Ch. ya Muassasat Ar-Risalah; Al-Ihkaam na Al-Amidiy: 1/130, Ch. ya Al-Maktab Al-islamiy; Jamu’u Al-jawamii’ Bisharh Al-Mahaliy: 1/99, pamoja na Hashiyat Al-bannaniy, Ch. ya Dar Al-Fikr].
Kwa hiyo tendo linalotendwa mara kwa hali ya kukubaliwa Kisharia, kutokana na kukamilisha yanayozingatiwa kisheria katika masharti na nguzo, na mara nyingine hupingana nayo, kutokana na ukosefu wa hayo – na ikiwa tendo hili ni ibada au mkataba – hakika usahihi wake ni kukubaliwa na Sharia. Na kama mwenye jitihada au mfano wake, akiona kuwa kuna ukosefu wa aliyoizingatia nguzo katika mkataba, basi hawezi kuuzingatia usahihi; hayo ni kutokana na ufafanuzi uliotajwa wa usahihi huo.
Pia wanazuoni wa madhehebu ya Shafiy matawi mengi yanayotakiwa/yanayopendeza au yanachukiwa, na wakaelezea hayo kuwa kuepusha hitilafu. Na kanuni hapa ni kuepusha hitilafu na kutakiwa. [Taz. Al-Ashbah Wan-Nadhair na As-Sayutiy: Uk. 136, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]; na kuwa kuepusha hitilafu ni kutakiwa na kunamaanisha: mwenye kukalifishwa anapofanya ibada au kufunga mkataba kwa njia waliyoikubali wenye jitihada wote, ni bora zaidi kuliko kukubaliwa na baadhi yao na kukataliwa na wengine. Na hii ni wazi kuwa hawazingatii kauli zote za wenye jitihada kuwa ni sahihi, na kinyume cha hayo, hakuna maana ya kanuni hii wala maelezo haya.
Kutokana na hayo maandishi ya vitabu vilivyotambuliwa vya madhehebu ya Shafiy, iliamulia kuwa: anayeoa bila walii kwa kumfuata Imamu Abu Hanifa, basi mkataba wake ni batili, kutokana na nadhari ya jitihada ya Imamu Shafi; ambapo mkataba huu haukusanyi masharti yake yote, na kama mkataba kama huu utapopelekwa kwa mfuasi wa Madhehebu ya Shafiy atauhukumu kuwa batili; vile vile maandishi ya madhehebu ya Hanafi yanaainisha kuwa: mkataba wowote ambao haukutimizwa masharti yake kwa nadhari ya Imamu Abu Hanifa ni batili kwa nadhari ya Imamu Shafiy; na Maimamu wawili wanasema: mkataba wowote ambao utapungua sharti moja, miongoni mwa masharti ya usahihi wake, basi mkataba huo hauna athari yoyote, kama vile: kutoa talaka, au kuwepo mwenye kuhalalisha wakati wa kumwacha mke mara tatu.
Na lililotajwa katika vitabu vya madhehebu ya Hanafiy, miongoni mwake kuna yalilotajwa na Mwandishi wa kitabu cha [Badaii’ As-Sanaii’: 2/335, Ch. ya Dar Al-kutub Al-Ilmiyah] kuwa: “Upweke katika ndoa batili hauwajibishi eda; maana hiyo kiuhalisia siyo ndoa”. [Mwisho].
Na Imamu Burhan Ad-Din Ibn Maza katika kitabu cha [Al-Muhit Al-burhaniy: 3/122, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] alinukulu kutoka katika [Majmuu’ An-Nawazil] miongoni mwa vitabu vyao kuwa: “Talaka katika ndoa batili kiuhalisia siyo talaka, bali ni kuachana, kwa hiyo haiathiri idadi ya mara za talaka”. [Mwisho].
Na mwandishi wa kitabu cha [Ad-Durul Mukhtar] kutoka katika [Al-Jawharah] miongoni mwa vitabu vyao anasema kuwa: mtu anapomwacha mkewe aliyemwoa kwa ndoa ya batili mara tatu, ana haki ya kumuoa tena bila ya mhalalishaji ambaye ni mume mwingine atakayemwoa na kumwacha pale atakapotaka kumwacha. Na alisema pia: “hakutaja hitilafu”. [Mwisho].
Na Mtaalamu At-Tahtawiy katika [Hashiya yake: 2/127, Ch. ya Bulaq, 1282] alinukulu kwenye maelezo yake (ana haki ya kumuoa bila mhalalishaji), kutoka kwa Al-Burhan Al-Halabiy, mwandishi wa [Tuhfat Al-Akhyar Ala Ad-Duru Al-Mukhtar] anaeleza: “Maana talaka inaambatana na yule aliyeolewa ndoa sahihi, au mwenye eda ya talaka, au mwenye kuvunjiwa mkataba wa ndoa kwa sababu ya kutoka katika Uislamu, au kutoukubali Uislamu”. [Mwisho]. Kisha At-Tahtawiy alisema: “ Aliyeolewa ndoa batili sio miongoni mwa waliotajwa”. [Mwisho].
Na Mwanachuoni Ibn Abidin katika [Hashiya yake: 3/284, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah] alielezea kauli hii akisema: “Haipatikani talaka katika hali ya ndoa iliyo batili, na wala idadi ya talaka haipungui kwa ndoa batili, maana huko ni kuachana, kama tulivyotaja hapo juu kutoka katika Al-Bahr na Al-Bazaziyah, Mlango wa Mahari, kwenye maelezo ya ndoa batili. Na kwa kuwa katika ndoa iliyo batili ni kutengana na siyo talaka kwa kiuhalisia wake, mtu ana haki ya kumuoa Mwanamke aliyetengana naye katika ndoa batili, kwa mkataba mwingine sahihi wa ndia, bila ya mhalalishaji ambaye ni mwoaji mwingine atakapomwacha mke kwa muda anaoutaka mwenyewe, pamoja na haki ya idadi ya talaka tatu”. [Mwisho].
Na mwandishi wa [Ad-Duru] alisema pia: “mtu huyo atamuoa mke wake aliyetengana naye, mara mbili kupitia eda, na baada ya kumaliza eda haruhusiwi. Na hamuoi mtalaka wa ndoa sahihi na kweli baada talaka ya mara ya tatu, akiwa mwanamke huru, na mara mbili akiwa mjakazi, hata kama atakuwa amemwacha kabla ya kumwingilia, mpaka aingiliwe na mume mwingine, kwa njia ndoa iliyo sahihi, na siyo batili wala ya muda. Na kama mwanamke atakuwa ameolewa na mtumwa lakini bila ya idhini ya bwana wake, na kumwingilia kabla ya kupata idhini hiyo, basi hajiuzu, mpaka awe amemwingilia baada ya kupata idhini ya kumwoa”. [Mwisho kwa maelezo machache].
Na Ibn Abidin alisema akielezea [3/409] kuwa: “kauli yake: ndoa sahihi na ya kweli, kwa ajili ya kuepusha ndoa batili, nayo ni ile isiyokuwa na baadhi ya masharti ya usahihi wake; kwa mfano ndoa bila mashahidi, hii haina hukumu kabla ya mume kumwingilia mke wake. Na baada ya kumwingilia inawajibika mahari inayofanana na ya wenzie, na talaka ya ndoa hii haipunguzi idadi ya talaka tatu; maana huko ni kuachana, na hata kama atamwacha mke wake mara tatu hakuna kitakachohesabika, na ana haki ya kumwoa bila ya kuolewa na mume mwingine kisha kuachwa kihalali na kuolewa nae. [Mwisho].
Kuhusu madhehebu ya Imamu Shafiy: Ilitajwa katika kitabu cha [Al-Umm na Imamu Shafi: 5/266, Ch. ya Dar Al-Maarifah] kwenye maneno yake juu ya kuingilia ambapo mwanamke awe halali kwa mumewe: “Kama mtu ameoa ndoa batili kwa njia yoyote, kisha akamwingila, basi mwanamke hatakuwa halali kwa mumewe; mfano wake: ndoa ya muda, ndoa katika hali ya kuhirimia Hija, ndoa mbadala, ndoa bila idhini ya walii, au ndoa ambayo kuna kasoro ya mkataba wake, mwanamke hatakuwa halali kwa kumwingila; kwa sababu mwanamume huyu sio mume wake, na talaka yake haimsibu mwanamke”. [Mwisho].
Na ndani yake pia [5/268]: “Ndoa batili yo yote haina talaka yoyote, kwa sababu hawa wawili sio mtu na mkewe. Na kutokana na yote tuliyoyasema ndoa yake ni batili katika ndoa ya mwanamke bila kuwepo walii wala hakimu, au kuozeshwa na walii lakini bila yeye mwanamke kuridhia ndoa hiyo, akiwa bado amekubali au siyo, na kwa ujumla mkataba wa ndoa hiyo ni batili ambapo hakuna ndoa kati yao”. [Mwisho].
Na ndani yake pia anasema [5/128] kuwa: miongoni mwa yanayowatenga mume na mke ni: “kila ndoa inayofungwa kibatili, kwa mfano: ndoa bila walii, ndoa ya mtumwa bila idhini ya bwana wake, ndoa ya mjakazi bila ya idhini ya bwana wake:, kisha akasema: “aina hizi zote za ndoa ni batili, na hupelekea kufungua mkataba huo, siyo kwa maana ya talaka lakini kuvunja mkataba”. [Mwisho].
Na Imamu Abu Said Al-Istakhriy miongoni mwa wenye mtazamo wa madhehbu ya Shafi anasema: “Mume anapotoa talaka katika ndoa iliyofungwa bila ya walii basi haitatekelezwa, na hahitaji mhalishaji, hata kama atatoa talaka mara tatu”. [Mwisho]. [Na Ash-Sharh Al-Kabiir, na Ar-Rafiiy:7/533, Ch.ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah].
Na Imamu Al-Baghawiy katika kitabu cha [At-Tahdhib] anasema: “Kama mwanaune atafunga ndoa bila walii, na akampa talaka mke wake mara tatu, inajuzu kumuoa baadaye bila ya haja ya mume mwingine; kwa sababu ndoa isipokuwa sahihi talaka haitekelezwi”. [Mwisho, na Al-Kaul As-Sadiid, na Al-Inbabiy].
Na Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha [Ar-Raudha:7/51] anasema: “Kumwingilia Mke katika ndoa iliyofungwa bila walii kunawajibisha mahari inayofanana na Wanawake wenzie, na hakuna adhabu yoyote, na ikiwa mtendaji anafahamu kuwa kufanya hivyo ni haramu au halali, kwa jitihada au kwa kufuata, au kwa dhana halisi, kutokana na utata wa hitilafu kati ya wanazuoni. Lakini anayefahamu kuwa ni haramu anaadibiwa… na akimpa talaka mke wake talaka haitekelezwi; vilevile akimtaliki mara tatu hatahitaji mhalalishaji (mume mwingine wa kumuoa na kumuacha kwa hiari yake)”. [Mwisho].
Abul Abbas Al-Qamuliy katika kitabu cha [Sharh Al-Wasit] anasema: “Na iwapo mume atampa talaka mke wake aliyemwoa bila ya walii, kuhusu kutekelezwa talaka na kuhitajia mhalalishaji, kwa kuwapo talaka tatu, kuna rai mbili: na sahihi zaidi, kwa rai ya Ar-Rafiy: hapana; kwa sababu hiyo ni ndoa batili, kwa hiyo haichukui hukumu ya ndoa sahihi”. [Mwisho, na Al-Hukm Al-Mubram, na Al-Halawaniy, Uk. 56].
Na Imamu Shihabuddin Al-Adhriiy anasema: “iwapo mume atampa talaka tatu katika ndoa iliyofungwa bila ya walii, basi talaka hiyo haitekelezeki na hahitajiki mhalalishaji”. [Mwisho, na An-Nusus Ash-Shariyah, na Ash-Shanawaniy, Uk. 23, Ch. ya Matbaat As-Saadah, 1338 H.].
Na katika kitabu cha [Asna Al-Matalib, na Sheikh wa Uislamu Zakariya Al-Ansariy: 3/125-126, Ch. ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy] ilitajwa kuwa: “Kama mwanamke ataingiliwa katika ndoa iliyofungwa bila ya walii, hali ya kuwa mwanamke huyo amejiozesha yeye mwenyewe, na kukakosekana hukumu ya hakimu kuwa ndoa hii ni sahihi au batili, basi analazimika kupewa mahari wapewayo wanawake wenzie, mbali na ile iliyoainishwa, kutokana na ubatili wa ndoa, na kwa Hadithi ya: “Mwanamke yeyote aliyejiozesha yeye mwenyewe bila idhini ya idhini ya walii wake, hakika ndoa yake ni batili – kasema mara tatu – na iwapo mume atamwingilia mke wake, basi mke huyo atakuwa ana haki ya mahari kutokana na uhalali wa tupu yake, na kama wakigombana, basi hakimu ni walii wa asiyekuwa na walii wake”. [At-Tirmidhiy ameipokea, na Kauli ni kwamba hukumu yake ni: Hasan; na Ibn Hibban na Al-Hakim, wao walisema kwamba Hukumu ni Sahihi.
Na katika hali hii, hakuna adhabu yoyote, ikiwa mtendanji anafahamu kuwa ni haramu au hafahamu hivyo; kutokana na utata wa hitilafu kati ya wanazuoni kuhusu usahihi wa ndoa hii. Lakini atakanywa katika hali ya kuwa kwake anafahamu ni haramu, kutokana na kuifanya haramu isiyoambatana na adhabu au kafara yoyote.
Na kama mume hatamwingilia mke wake aliyemwoa kwa ndoa hii ya bila walii wake, na mwanamke ameolewa kwa idhini ya walii na kabla kuwatenganisha, kuna rai mbili: kwanza: ndoa hiyo ni batili, na pili: ndoa hiyo ni sahihi, kama itakavyokuja mwanzo wa mlango wa nne, pamoja na nyongeza ya sharti, ambalo ni: iwapo atampa Mkewe talaka tatu, hana haja ya kuwapo mhalalishaji, yaani hakuna haja ya Mwanamke kuolewa na mtu mwingine ili awe halali kwake; kutokana na kutotuka talaka; kwa sababu talaka inatekelezwa kutokana na ndoa sahihi.
Na ikitolewa hukumu na hakimu kuwa ndoa hii ni sahihi au batili, basi hukumu hii haitenguliwi, kama vile mengi ya masuala yenye hitilafu ndani yake. [Mwisho].
Sheikh wa Uislamu Mtaalamu Abdur-Rahman Ash-Shirbiniy alinukulu katika Hashiya yake ya [Sharh Al-Bahjah Al-Wardiyah, na Sheikhwa Uislamu Zakariah: 4/109, Ch. ya Al-Maimaniyah] kuwa: Ash-Shams Ar-Ramliy na Az-zayadiy na Ash-Shabramalisiy na Al-Qalyubiy wote walisisitiza ubatili wa ndoa iliyofungwa bila ya walii, na kutokuwa kwake na talaka.
Na miongoni mwa hoja zinazotegemewa ni njia ya wafuasi wa Imamu Shafi: Kama ilivyonukuliwa na Imamu An-Nawawiy katika kitabu cha [Al-Majmuu’: 1/255-256, Ch. ya Al-Muniriyah] kuwa: “watu wawili mmoja wao ni Mfuasi wa Madhehebu ya Shafi na mwingine ni Mfuasi wa Madhehebu ya Hanafi, waliukuta mvinyo sehemu fulani, wakati hakuna maji, Mfuasi wa Madhehebu ya Hanafi akatawadha kwa mvinyo, na Mfuasi wa Madhehebu ya Shafi akatayammamu, kisha wakasali pamoja, basi sala ya maamuma ni batili; kwa sababu kila mmoja kati yao anaona kuwa sala ya mwingine ni batili; mfano wa watu wawili waliosikia sauti ya kinachotengua udhu, itakua ni batili”. [Mwisho]
Vile vile wakazingatia kuwa: Mfuasi wa Madhehebu ya Shafi anaposwali nyuma ya mwingine wa madhehebu ya Hanafi, kisha akaona kuwa imamu wake alifanya kitu cha kuvunja Swala, kutokana na dhana ya mfuasi wa Shafi, basi haisihi kuufuata Uimamu wake. Kama ilivyokuja katika vitabu vikuu vya madhehebu ya Shafiy. [Al-Minhaj na Sharh yake Mughniy Al-Muhtaj, na Mtaalamu Al-Khatib Ash-shirbiniy: 1/478-479, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah]: “Kama mfuasi wa Madhehebu ya Shafi ataswali nyuma ya mfuasi wa Madhehebu ya Hanafi, na huyu Mfuasi wa Hanafiy akalifanya jambo linalovunja swala, kwa mfano: kama vile kuigusa tupu, kuacha unyenyekevu, kuacha Bismillaahi, Suratul Fatiha, au baadhi ya Aya zake, au kujitoa damu damu; basi hapo rai mbili:
Ya kwanza: hukumu yake ni usahihi wa kuswali nyuma yake, katika hali ya kutokwa na damu tu, isipokuwa kugusa tupu na mwingineyo, kwa kuzingatia nia ya maamuma, maana imamu atakuwa ametengukwa na udhu katika hali ya kuigusa tupu yake, kinyume cha utoaji wa damu.
Ya Pili: kinyume cha ya kwanza, kwa kuzingatia imani ya imamu, ambapo maamuma anaona kuwa imamu anachezea hali ya utoaji damu, kwa hiyo nia yake siyo sahihi, na hapo ndipo maamuma anaposhindwa kuitambua nia. Na mwenye kupinga katika matawi ya Fiqhi kwa mfano mfuasi wa Hanafi, akihifadhi wajibu wa Tahara na Swala kama ilivyo kwa Shafiy, basi kumfuata Uimamu wake katika Swala ni sahihi; hivyo hivyo ikiwa kuna mashaka ya kuwa mfuasi wa Madhehebu ya Hanafiy amekwisha yatekeleza mambo yote ya wajibu, kwa ajili ya dhana njema kuwa anaangalia hitilafu; na haidhuru kutoamini uwajibikaji wake, bali kinachodhuru ni imani ya imamu kuwa ni batili kama anavyoamini maamuma”. [Mwisho]
Na Mtaalamu Ibn Hajar katika kitabu cha: [Tuhfat Al-Muhtaj: 2/282 kwenye maelezo yake ya maandiko ya [Al-Minhaj] hapo juu, baada ya kuyataja maneno ya Sheikh Al-Khatib, anasema: “Ukisema kuwa: Maneno yaliyotajwa yanasisitiza kilichojulikana kama: anayemfuata mwingine kiusahihi, basi Swala yake ni sahihi hata kwa upande wa mpingaji wake. Nasema: maana ya kuwa sahihi kwa mpingaji wake ni kuwa: Swala inaliachilia jukumu la mfanyaji asije akaulizwa kwalo, na wala hatuunganishi Swala yetu na swala yake; kwa sababu uunganishaji huo unapelekea ubaya mwingine, nao ni: imani yetu kuwa yeye hafahamu nia yetu, na kwa sababu hii tumekataza kuunganisha, na siyo kwa ubatili wa swala yake kutokana na imani yake yenyewe.
Hivyo kwa njia ya uunganishaji huo hauleti faida yoyote, na kwa njia ya kumwachilia jukumu la mfanyaji hufaidika kwa nje na kwa ndani: sala yetu na sala yake zinatazamiwa kuwa sahihi au batili; kwa sababu kuhusu matawi mwenye usahihi ni mmoja tu, lakini kila mwenye kufuata, anafuata kutokana na kuwajibika kuifuata rai yenye nguvu zaidi kwake, aamini kuwa alivyosema imamu wake ni karibu zaidi na makubaliano ya jambo hili kuliko alivyosema mwingine, pamoja na uwezekano wa ukaribu wa kauli ya mwingine kwa hali yake, basi iangalie zaidi”. [Mwisho]
Na maneno haya ya Mwanachuoni aliyotajwa hapo juu ni muhimu sana; kwa sababu anaamua kuwa: usahihi wa Swala ya mpingaji aliyefanya ubaya ni kwa mujibu wa nadharia ya Imamu Shafi, na wala sio kwa mujibu wa imani yake yenyewe, maana yake ni kuwa: huachilia jukumu lake mbele ya Mwenyezi Mungu, asije akaulizwa juu ya jambo hilo, na bila kukanushwa na ye yote, kwa hiyo ni sahihi kihukumu kwa rai ya Imamu Shafi, na sahihi kiukweli kwenye nafsi yake, yaani mpingaji .
Bora kutanabahisha kuwa ndani ya madhehebu kuna rai yenye nguvu ndogo, nayo ni: ya yule aliyeoa bila walii, kisha akampa talaka tatu mke wake, analazimika kuhalilisha, na hii ni rai ya Imamu Abu Is-haq Al-Maruziy. [Taz. Ash-Sharh Al-Kabiir, na Ar-Rafiy: 7/533], na Ibn Hajar Mwandishi wa [At-Tuhfa: 7/240] aliifuata rai hiyo. Lakini fikra ya rai hii – ingawa ina nguvu ndogo – kuwa: kuweka kinga kwa mambo ya ndoa, kama alivyoeleza hivyo Abu Is-haq; au kutokea katika sura ya kukatazwa, nao ni: uzushi uliopo wa kufuata suala moja – kama alivyosema Ibn Hajar-; na siyo fikra ya usahihi wa mkataba wa ndoa kwa Imamu Shafiy.
Wanazuoni wengi walitaja kuwa rai hii ni dhaifu, na miongoni mwao ni: Abu Is-haq Ash-Shiraziy; ambapo alisema katika kitabu cha [Al-Muhadhab: 2/426-427, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah] “Haisihi ndoa isipokuwa kwa walii, na kama mwanamke atakuwa amefunga ndoa basi haitakuwa ni yenye kusihi… na kama mwanamume aliyempa talaka mke wake huyo talaka hiyo haitekelezwi. Na Abu Is-Haq anasema: talaka hiyo inatekelezwa; maana ni ndoa yenye hitilafu za Wanachuoni katika usahihi wake, na kwa hivyo talaka itekelezwe; mfano wake ni kama ule wa kumuoa mwanamke katika muda wa eda ya dada yake, na madhehebu ni ya kwanza, maana ni talaka nje ya miliki yake, basi haisihi, kama vile alimpa talaka mwanamke asiye ndugu wa karibu”. [Mwisho]
Ikiamuliwa hivyo, na ndoa ikafungwa bila ya walii, na washiriki wakawa wametanabahi kumfuata Imamu Abu Hanifa au siyo, kisha yakajitokeza masilahi ambayo yanatakiwa kupatikana, au madhara ya kuepushwa, kama vile mwanamume aliyemaliza Idadi ya talaka zake tatu kwa mke wake, au kijana kumdanganya msichana asiye na uzoefu, na akafunga naye ndoa bila ya walii, kisha akamwacha kama mtu aliyeanguka hewani, kama ilivyokuja katika uhalisia wa swali, kisha mwenye tatizo hili akataka kuyafuata Madhehebu ya Imamu Shafi, yaani kwa kuzingatia nguzo ya walii katika kuufunga mkataba wa ndoa, na kama hakuna walii basi mkataba huo hausihi.
Na kwa mujibu wa maelezo hayo: Talaka tatu katika mfano wa kwanza, hazizingatiwi, na mtu ana haki ya kufunga ndoa upya, pamoja na kupitisha athari za ndoa, kama vile: ithibati ya ndoa, nasaba ya watoto kupitia muda uliyopita, pamoja na kutokuwepo dhambi. Vilevile, katika mfano wa pili: Kuhusu msichana huyu ana haki ya kuolewa na mtu mwingine, bila ya kujali kungoja kuachwa na mume wa kwanza, baada ya kumaliza eda, hali ya kuwa mume huyo wa kwanza alimwingilia; kwa kuzingatia kwamba hakuna mkataba wowote wa ndoa uliofungwa baina yao; pamoja na sharti ya: kutokuwepo hukumu ya kadhi ili kuamua usahihi wa ndoa ya kwanza, ambapo haijuzu hali hii kuondoka na kufuata sura iliyotajwa hapo juu.
Na wanazuoni wa madhehebu ya Shafiy walitaja kuwa hii inajuzu, na kabla ya kutajwa maandishi yao, ni bora kutanabahisha kuwa: kauli ya hii inajuzu imejengwa kwa suala lingine la msingi, nalo ni: suala la kumfuata Imamu baada ya kutenda tendo. Na Wenye Misingi ya Fiqhi walichunguza suala hili, na wafuasi wa madhehebu mengi, ambayo Ibn As-Subkiy alizifikisha Madhehebu sita, katika kitabu cha [Jama’ Al-Jawamii’, pamoja na Sharh Al-Mahalliy, na Hashiyat Al-Bannaniy: 2/399-400].
Na Hukumu iliyotajwa na wengi wa wanazuoni wa madhehebu ya Shafi ni kuwa: inajuzu. Na Mwanachuoni Al-Bijirmiy katika Hashiya yake juu ya kitabu cha [Al-Iqnaa’ na Al-Khatib Ash-Shirbiniy katika Matawi ya Madhehebu ya Shafi: 1/58, Ch. ya Dar Al-Fikr] anasema: “Inajuzu kuyahama madhehebu na kuyafuata mengine, hata baada ya kutekeleza kazi”. [mwisho].
Na katika kitabu cha [Ia’anat At-Talibiin Ala Hall AlFadh Fat-hu Al-Mui’in, na Shaeikh Abu Bakr Ibn Muhammad Shata Al-Bakriy Ad-Dimyatiy: 4/ 250, Ch. ya Dar Al-Fikr]: “Ibn Al-Jammal anasema: Jua kuwa rai sahihi zaidi ya maneno ya wanazuoni kama vile Ibn Hajar na wengineo ni kuwa: Inajuzu kuyahama madhehebu na kwenda madhehebu mengine yaliyoandikwa, hata ikiwa kwa njia ya kutamani tu, na ikiwa mtu atafanya hivyo siku zote au katika baadhi ya maamuzi yake, hata kama itatolewa fatwa au hukumu au itatekelezwa kinyume na hivyo, kama haitakuwa na uzushi wowote”. [Mwisho]
Na Mwanachuoni Bwana Abdur-Rahman Ibn Ubadillahi As-Saqqaf Al-Hadhramiy, anasema katika kitabu chake [Saubu Ar-Rukam Fi Tahqiq Al-Akkam ] ambaye alikijaalia kama Hashiya ya kitabu cha Ukadhi wa kitabu cha [Tuhfat Al-Muhtaj, na Mwanachuoni Ibn Hajar Al-haitamiy: 1/49, ambacho kilichapishwa sura ya muswada wake, Jeddah, 1412 H., na kunukuliwa kwa Hashiyat Al-jamal kuwa: Mwisho wa Wahakiki Mwanachuoni Ibn Qasim Al-Abbadiy alielekeza maneno yake kuwa: Inajuzu kumfuata Imamu Abu Hanifa baada ya kuitekeleza kazi kwa uwazi; na Sheikh As-Saqqaf alielezea akisema: “Huenda Imamu Abu Hanifa anaona kuwa: Inajuzu kumfuata Imamu baada ya kuitekeleza kazi, au Mtaalamu Ibn Qasim halizingatii hilo kuwa ni sharti; na hoja hii inatosha, na katika jambo hili kuna kiasi kikubwa cha faraja na shida pia huondoshwa”. [Mwisho]
Na mwanafunzi wake Sheikh Mansur A-Tablawiy alinukulu kuwa: Aliulizwa juu ya mwanamke mfuasi wa madhehebu ya Shafiy aliefanya Tawafu ya Ifadhwa bila ya mavazi ya kujisitiri kutokana na kutoelewa au kwa kusahau, kisha akaenda Mji wa Yemeni, akaolewa, kisha akaelewa kuwa Tawafu yake ni batili, akataka kuyafuata Madhehebu ya Abu Hanifa kwa ajili ya kusihi kwake, ili awe halali, na kuelewa usahihi wa ndoa. Je, hii inasihi ingawa ni kumfuata baada ya kulitekeleza Jambo hili?
Ibn Qasim alitoa Fatwa kuwa: ni sahihi, na hakuna kosa lo lote. Na At-Tablawiy alisema: “baadhi ya wanazuoni walitoa Fatwa kumfuata yeye, na suala hili ni muhimu, na linatokea mara nyingi, na lina mifano mingi”. [Mwisho] Hapo Mtaalamu Ash-Shabramalisiy alielezea baada ya kunukulu hivyo katika Hashiya yake ya [Nihayat Al-Muhtaj na Ar-Ramliy: 3/318, Ch. ya Dar Al-Fikr] akisema: “Muradi wa (mifano yake) anamaanisha kuwa: Kila jambo linalopingana na Madhehebu ya Imamu Shafi, na likawa sahihi kwa Madhehebu mengine yanayozingatiwa na kutambulika. Na kama mtu atafanya jambo lililo batili kwa rai ya Shafi, lakini ni sahihi kwa rai ya mwingine, kisha akaelewa hivyo baada ya muda mfupi, basi inajuzu kwake kumfuata aliyejuzisha kwa wakati uliopita na ujao, na hukumu zake zitatekelezwa, kwa hiyo kuwa macho katika hilo kwani, kwa hakika ni muhimu mno”. [Mwisho]
Kuhusu matini: hakika ni kinyume cha ililotangulia kuwa: rai sahihi ya Madhehebu ni kuwa: Mtu anapooa bila ya walii, kisha akampa talaka tatu mkewe, talaka hizo tatu hazitambuliki kisheria na hazizingatiwi kuwa zimetokea, na halazimiki kuwa na mhalalishaji. Kwa sababu Jamuhuri ya wanazuoni wa madhehebu hayo walieleza kuwa: hii ni sahihi, hata mtendaji akinuia kwanza kumfuata Imamu Abu Hanifa, kisha baadaye akabadili kwenye kumfuata Imamu Shafi. Na hii huitwa (Kubadili mwelekeo). Na miongoni mwa matini hizo ni:
Kauli ya Ash-Shihab Ar-Ramliy kuwa: “Mtu anapofunga ndoa na mwanamke kulingana na Madhehebu ya Hanafiy; hali ya kuwa mwanamke anaipitisha ndoa hiyo moja kwa moja au kwa kuwakilishwa na mtu baki pamoja na kuwa walii wake yupo, pamoja na mashahidi; kisha akamwingilia, akamfuata Imamu Abu Hanifa, kisha akampa talaka tatu. Kwa uwazi huu, ndoa hiyo ni batili kwa mujibu wa madhehebu ya Imamu Shafiy, lakini ni sahihi kwa mujibu wa Madhehebu ya Hanafi, na kwa sababu ya kumfuata yeye basi hayo yanakuwa ndio madhehebu yake. Kwa hiyo ana haki ya kuyabadili Madhehebu ya Imamu Shafi kuwa ndoa ni batili, kisha akafunga ndoa nyingine upya na kwa sahihi, bila ya haja ya Uwepo wa mhalalishaji, hata kama mwanamume ni mfuasi wa madhehebu ya Hanafiy. [Mwisho na: Kashful Qinaa’ An shawarid At-Talaq wal Ikhtilaa’, na Sheikh Muhammad Shuhba Al-Hassaniy Al-Manfalutiy Ash-Shadhliy Ash-Shafiy [T: 1163 H., Muswada wa Al-Maktabah Al-Azhariyah].
Pia imenukuliwa na Al-jamal Al-Isnawiy katika [Al-Muhimmat] na Ibn Qasim Al-A’abbadiy na Ash-Shihab Ar-Ramliy kuwa: kama ndoa itakuwa imefungwa katika hali ya kuhitilafiana kati ya Maimamu, inajuzu kwa mwenye kumfuata Imamu anayesema kuwa ni sahihi kwake kutomfuata Imamu anayesema kuwa kufanya hivyo ni batili, katika mazingira ya kutolewa talaka tatu, na pia uahalilishaji unatoweka, wakati huo atakuwa na haki ya kufunga ndoa mpya kwa masharti kamili yanayozingatiwa kisheria kwa Madhehebu yanayosema kuwa ndoa ya kwanza ni batili.
Na Mtaalamu Ibn Hajar- aliyeifuata katika Sharh Al-Mihaj njia ya Abu Is-haq Al-Maruziy, ambayo ina nguvu ndogo ya Madhehebu – katika kitabu cha [Tuhfat Al-Muhtaj: 7/240] anasema: “Mtu aliyeoa ndoa yenye hitilafu ya kimadhehebu, hali ya kuwa alimfuata Imamu mwenye rai ya kuwa ndoa hiyo ni sahihi, au kwa mujibu wa hukumu yake, kisha akampa talaka tatu mkewe, analazimika kuwa na uhalilishaji, na hana haki ya kumfuata Imamu anayeona kuwa ni batili; kwa sababu huu ni uzushi wa kufuata ndani ya suala moja ambao kwa hakika unakatazwa, na katika hali ya mtu kutojali kumfuata Imamu na hukumu hiyo, basi halazimiki kuwa na Mhalalishaji”.
Hapo, Mtaalamu Ibn Qasim Al-A’abbadiy alielezea akisema: “(Kauli yake: na hana haki ya kumfuata anayeona kuwa kufanya hivyo ni batili) hii inakatazwa, bali ana haki ya kumfuata; kwa sababu hili ni suala lingine, kwa hiyo hakuna uzushi”. [Mwisho], kisha akainasibisha kauli hii kwa Ash-Shams Ar-Ramliy.
Na Mtaalamu Shamsuddin As-Saginiy, mfuasi wa madhehebu ya Shafi katika kitabu chake [Fat-hu Al-jalil] anasema kwenye maneno yake ya kinachoutengua uhalilishaji: “Kama ndoa itakuwa imefungwa kwa njia batili; kama vile kwa uwepo wa walii au mashahidi wasiokuwa waaminifu, na mwanamume na mwanamke walikuwa wanaijua kasoro ya masharti hayo wakati wa kufunga ndoa, au wakajua hivyo baada ya kufunga ndoa, hata ikiwa baada ya talaka tatu; basi inajuzu kwa mujibu wa Madhehebu yetu kufungwa upya ndoa pamoja na kukamilisha masharti, bila ya uwepo wa mhalilishaji; kwa sababu mume na mke wanajua kuwa mkataba wa kwanza ni batili. Lakini kufungwa upya kwa ndoa ni kwa njia ndani na siyo kidhahiri; na kadhi peke yake na siyo mtu mwingine akijua hivyo atalazimika kutoa hukumu ya wanandoa kuachana, na asipofanya hivyo: ndoa ya pili itabakia kama ilivyo kwa usahihi wake na haigeuzwi na kuwa batili, na hapo, kadhi atapata dhambi kutokana na kunyamaza kwake”. Kisha Mwanachuoni huyo alitaja kuwa: Ash-Shihab Ar-Ramliy na Mtaalamu Al-Halabiy walikuwa wakitoa fatwa ya hivyo”. [Mwisho, na: Kashful Qinaa’, na Al-Manfalutiy].
Lakini mtungaji wa kitabu cha [Kashful Qinaa’] alinukulu kutoka kwa Imamu Abu Muhammad Mudhhiruddin Al-Khuwarizmiy, Mtumgaji wa kitabu cha: [Al-Kafiy Fil Fiqhi], naye mwanazuoni wa Madhehebu ya Shafiy (Alikufa: 568) kuwa alisema: haijuzu kabisa kuwapinga mume na mke waliofunga upya ndoa yao, wala kuwaachanisha, maana hiyo inajuzu kwao kiundani na kidhahiri, na kadhi au mtu mwingine yoyote hana haki ya kuwapinga wala kuwasumbua. Na akataja kuwa Ibn Hajar amekwisha lisahihisha hilo katika kitabu cha [Sharhul U’ubaab]. Na hiyo inamaanisha kuwa Ibn Hajar ana maneno mengine ambayo hayajatajwa katika [Sharhul Minhaj] na Ibn Is-haq aliyafuata; na kuwa: Sheikh Shamsuddin Al-I’inaniy, mfuasi wa madhehebu ya Shafi, mwenye Hashiya ya [Sharhu At-Tahriir] na Sheikh wa Uislamu Zachariya, naye ni miongoni mwa watoaji wa Fatwa ya Madhehebu, aliyataja hayo hayo pia; na akasema: “Mahali pake hali ya kutoelewa kabla kutekelezwa na kutolewa Fatwa, lakini akielewa hali yake mwanzoni mwanzoni, na akampa idhini yake ya kutekeleza, hapo haijuzu kumpinga tena kwa kauli ya pamoja, na kama ikichukulia kuwa ni dhaifu, lakini ikiimarishwa kwa idhini ya kadhi na kuiruhusu, basi iweje ije kupingwa baada ya kuimarisha? Hasa ikijulikana kwa uwazi wa kutopinga, na hiyo ni bora zaidi”. [Mwisho]
Pia Sheikh Muhammad Ibn Ibrahim Al-Ghayatiy, mwanafunzi wa Ash-Shams Al-Inbabiy, alinukulu katika risala yake inayokusanya kuwa: Mama wa mwanamke aliyeolewa kwa mujibu wa madhehebu ya Abu Hanifa ni mtu baki. [Muwada katika Maktabat Al-Azhar Ash-Sharif], kutoka kwa Mwanachuoni Al-Qalyubiy kuwa alisema: Haijuzu kwa mtu ye yote kuwapinga mume na mkewe waliofunga upya ndoa yao – yaani kwa njia iliyotajwa – wala kuwaachanisha. Kisha Al-Ghayatiy akataja kuwa: hiyo ni rai yenye nguvu zaidi, iliyotolewa Fatwa katika Madhehebu haya.
Na Mwanachuoni, Sheikh Muhammad Ibn Abdul Muta’al Al-Buhutiy, mfuasi wa madhehbu ya Shafi, naye ni miongoni mwa wanafunzi wa Sheikh wa Uislamu Shamsuddin Al-Inbabiy – katika kitabu chake [Fat-hul Ighlaq Fi Ahkaam At-Talaaq: Uk. 67-68, Ch. ya Al-Matba’ah Al-a’amirah Ash-Sharqiyah, Mwaka 1321 H.] anasema: “Mtu anapofunga ndoa na mwanamke kwa kufuata Madhehebu ya Hanafiy; hali ya kuwa mwanamke huyo anafunga ndoa hiyo yeye mwenyewe au akiwa anamwakilisha mtu asiye ndugu ingawa walii wake yupo, pamoja na mashahidi; kisha akamwingilia, akamfuata Imamu Abu Hanifa, kisha akampa talaka tatu. Kwa uwazi huu ni batili kwa mujibu wa Madhehebu ya Imamu Shafiy, lakini ni sahihi kwa mujibu wa Madhehebu ya Hanafiy, na kwa sababu ya kumfuata yeye basi yakawa ni Madhehebu yake. Kwa hiyo ana haki ya kubadilisha Madhehebu ya Imamu Shafiy yaonayo kuwa ndoa hiyo ni batili, kisha akafunga ndoa sahihi upya, bila ya haja ya mhalalishaji, hata kama mume huyo atakuwa ni mfuasi wa madhehebu ya Hanafiy.
Na muhtasari wake ni: Ndoa imefungwa katika hali ya kuhitilafiana kati ya Maimamu, mmoja wao anaihalalisha, na mwingie anaibatilisha, na mwenye ndoa hiyo alikuwa akimfuata huyu anayeihalalisha, kisha talaka tatu zikatekelezwa, basi ana haki ya kuibadili kutoka katika usahihi na kuielekeza kwenye ubatili, na akafunga ndoa kwa kuyakamilisha masharti yanayozingatiwa kisheria kwa rai ya anayeona kuwa ndoa ya kwanza ni batili, na hapo uhalilishaji utaanguka moja kwa moja”. [Mwisho]
Na rai hii pia imenukuliwa na Sheikh Muhammad Hussein A’aql Az-Zaa’baliy mfuasi wa madhehebu ya Shafi katika risala yake: [Futuh Al-Khallaq Fima Lam Yaqaa’ Wama Waqa’ Min Ahkaam At-Talaaq Ala Madhhab Al-Imamu Ashafiy RA: Uk. 26-27, Ch. ya Al-Matba’ah Al-Husainiyah Al-Misriyah, Mwaka 1326 H.], ambapo hakuzidisha isipokuwa maneno machache kwa ajili ya kuielezea Kauli ya wa Al-Buhutiy, kwa hiyo hakuna haja ya kuyataja tena.
Na Sheikh wa Uislamu, Mwanachuoni Mkubwa Sheikh Abdur-Rahman Ash-Shirbiniy katika Hashiya zake Ala Sharh Al-Bahjah [1/18] anasema: “Kuhusu maji aliyoyatawadha mfuasi wa Madhehebu ya Hanafi, hata asiponuia, hukumu yake ya kutambuliwa ni maji ya kutumiwa; kwa sababu hakuna upingaji wa mfuasi wa madhehebu mengine, kutokana na maelezo ya Ar-Ramliy. Na mfano wake ni kufunga ndoa bila walii ambapo pia hauna upingaji wa mwingine, na kwa hivyo rai inayotambuliwa ni kuwa: Iwapo mtu atamfuata Imamu Shafi basi hahitaji mhalalishaji; na ndoa yake ya kwanza haithibitishi uharamu kati yake na Mama wa Mkewe au Binti yake wala kuwaharamishiwa kwao, isipokuwa hali ya kumwingilia, hapo uharamu upo, yaani; uharamu wa kuwaoa, na sio uharamu wa udungu wa karibu”. [Mwisho]
Mtaalamu Sheikh Ahmad At-Talawiy mfuasi wa Madhehebu ya Shafi katika maelezo yake ya [Al-Manhaj] na Shaeikh wa Uislamu Zakaria anasema: Mtu aliyeoa bila walii kisha akampa mke wake talaka tatu, tutamtolea Fatwa, hali ya kuwa anamfuata yule anayesema kuwa ndoa hiyo ni sahihi, kuwa: talaka haitekelezwi; kwa sababu ndoa hiyo sio sahihi katika Madhehebu yetu; na ana haki ya kufunga ndoa nyingine na mwanamke huyo bila ya ya kuhitaji Mhalalishaji, kwa mujibu wa Madhehebu ya Imamu Shafi; hali ya kuwa mwenye masharti kamili kwa rai ya Imamu”. [Mwisho, na An-Nusus Ash-Shariyah na Ash-Shanawaniy: Uk. 53].
Na mwanafunzi wake Mtaalamu Sheikh Muhammad Abdul Fattah Ash-Shanawaniy mfuasi wa madhehebu ya Shafi – Sheikh wa Riwaaq Ash-Shanawaniyah hapa Al-Azhar Ash-Sharif, katika karne iliyopita – aliandika risala iitwayo: [An-Nusus Ash-Shariyah Ala Anna Man Tazawajat Bila Walii Au Bishuhuud Fasaqah A’aqduha Baatil Inda Assadah Ashafiiyah], na akaipitisha hukumu hii ndani ya risala hiyo. [Uk.13-14] anasema: “Mmoja wa Waislamu akimfuata Imamu Abu Hanifa kwa kuoa bila ya walii au kwa kuwapo mashahidi waovu, kisha akampa mke wake talaka tatu, ana haki ya kurejea kutoka katika Abu Hanifa na kumfuata Shafiy, akafunga ndoa upya kwa masharti kamili ya Madhehebu ya Imamu Shafi, akamwingilia mke wake bila ya kuwapo mhalalishaji; pasipo hukumu kutolewa na hakimu kwa usahihi wa mkataba wa kwanza, na hakuna kosa lolote kwa kufanya hivyo; kwa sababu kufunga ndoa bila walii au kwa mashahidi waovu ni batili kutokana na nadharia ya Imamu Shafiy, hata kama mwenye ndoa hiyo akiamua kumfuata Imamu Abu Hanifa; maana Imamu Shafi aliweka masharti ya kuwapo kwa walii na mashahidi waaminifu ili ndoa iwe sahihi, kwa hiyo ndoa yoyote isiyoyatimiza masharti haya yote au sharti moja kati ya masharti haya inazingatiwa kuwa ni batili kwa maoni yake; kutokana na dalili zake thabiti… Na kama ndoa haitakuwa na masharti kamili ya Imamu Shafiy, na hakuna hukumu ya hakimu itakayouleta usahihi wake, ukionyeshwa kwa Imamu Shafi hakuna uwezekano wa kuhukumiwa isipokuwa kuwa kwake batili, na hata akihukumu kinyume cha hivyo, basi atachuma dhambi na itakuwa batili”. [Mwisho]
Na sababu ya kuandika risala hii ya Mtaalamu aliyetajwa hapo juu ni kuwa: wakati huo risala mbili ziliandikwa na mwandishi aitwaye: Sheikh Muhammad Mansur; Ya kwanza ni: [Al-Qaulul Fasl Fi Bayan Sihat U’uquud Abu Hanifa Inda Ash-Shafiy], na ya pili ni: [Nuur Al-Hidayah], na mwandishi huyu aliziandika risala hizi mbili baada ya kujua kuwa karibu yake mtu mmoja alimpa talaka tatu mke wake, wakaachana kwa njia isiyo rasmi, kisha mume akamwingilia mke wake, baada ya kupeleka shitaka lake Sheikh Abdul Wahhab Al-Khudariy mfuasi wa madhehebu ya Shafi, na Sheikh Suleiman Al-Abd Mkuu wa wafuasi wa madhehebu ya Shafi wakati huo, walitoa Fatwa ifuatayo: Ndoa iliyofungwa kwa madhehebu ya Abu Hanifa ni batili, kisha ndoa hiyo ikafungwa upya kwa madhehebu ya Shafiy.
Muhammad Mansur alielekea mwelekeo usio mwema, akamshutumu Sheikh Suleiman Al-Abd na Sheikh Al-Kuhdariy, akawatendea vibaya na akawahusisha na upingaji wa Madhehebu ya Shafiy, na madhehebu zote, na hakutosha hivyo, bali akamtaja Sheikh wa Al-Azhar wakati huo akiwapo Sheikh Muhammad Abul Fadhl Al-Jizawiy kwa njia mbaya isiyokubalika.
Na Sheikh Ash-Shanawaniy alipambana naye, akabainisha kuwa yeye ni mzushi dhidi ya madhehebu hayo, mwongo, mjanja wa maneno, pamoja na kasoro ya ufahamu wa matini na kuyaelekeza atakavyo yasiyomaanishwa, na yeye ni mdai wa asiyoyafahamu, na amewahi kutengwa na Al-Azhar, kwa sababu ya kufeli kwake katika Mtihani wa Shahada ya (Al-A’alimiyah).
Kisha Sheikh alifuata uhakiki wa risala zake mbili ibara hadi ibara, akabainisha kuwa yeye alizichukua Ibara hizo kutoka katika kitabu cha Sheikh Ahmad Al-Halawaniy mfuasi wa Madhehebu ya Shafi, naye ni mwanafunzi wa Mtaalamu Ash-Shams Al-Inbabiy, kitabu kiitwacho: [Al-Hukm Al-Mubram Fi Anna Umm Allatiy Tazawajat Bila Walii Bitaqliid Abi Hanifa Muharram], baada ya kukiharibu, na bila ya kukiashiria kwake hata kidogo.
Na Sheikh Al-Halawaniy alikuwa akimfuata Sheikh wake Al-Inbabiy, ambaye aliandika risala ya maudhui hii iitwayo: [Al-Qaul Assadiid Fi Sihat Nikah Al-Mara’ah Bila Walii Maa’a At-Taqliid], nao ni muswada ndani ya Al-Maktabah Al-Azhariyah.
Na Ash-shanawaniy alitaja kuwa: Wengi wa wanazuoni walijibu kitabu cha Al-Halawaniy kupitia wakati wake- na Al-Inbabiy aliwapinga wengi wa wanafunzi wake.
Na wanazuoni wafuasi wa madhehebu ya Shafiy wa Al-Azhar Ash-Sharif katika wakati huo walikubali kitabu cha Sheikh Ash-Shanawaniy, wakashuhudia kuwa hukumu yake ndiyo iliyotajwa katika madhehebu na kutambuliwa, na kusifiwa na zaidi ya wanazuoni thelathini miongoni mwa Wakubwa wa wafuasi wa madhehebu ya Shafi. Miongoni mwao ni: Sheikh Muhammad Ibn Salim An-Najdiy Ash-Sharqawiy, Mkuu wa wafuasi wa madhehebu ya Shafiy katika wakati huo, na mwanachama wa Baraza kuu la Taasisi za Dini; Sheikh Abdul Muu’tiy Ash-Sharshimiy; Sheikh Muhammad Qindil Al-Hilaliy; Sheikh Yunus Al-U’utafiy; Sheikh Muhammad Ali Al-Barad As-Sakandariy, na hawa ni wa Jumuiya ya Wanazuoni Wakubwa; Sheikh Muhammad Imam As-Saqqa; Sheikh Muhammad Al-Halabiy; Sheikh Abdul Muu’tiy As-Saqqa; Sheikh Mahmud Ad-Dinariy; Sheikh Muhammad Abdus-Salaam Al-Qabbaniy; Sheikh Yusuf Al-Marsafiy; Sheikh Salamah Al-A’azamiy; Sheikh Mustafa Al-Hihyawiy; Sheikh Suleiman Al-Abd, Mkuu wa Wafuasi wa Madhehebu ya Shafiy, kabla ya Sheikh An-Najdiy.
Kuhusu ubatili wa ndoa iliyofungwa bila idhini ya walii, pamoja na kuwa mama wa mke hathibitiki kuwa ndugu wa karibu, makundi ya wanazuoni wafuasi wa Madhehebu ya Shafiy wa Dimyat, Misri, wakati wa Sheikh wa Uislamu Al-Inbabiy, walimfuata Sheikh Ash-Shanawaniy, na wakahojiana na Mtaalamu Al-Halawaniy kuhusu suala aliloliashiria katika kitabu chake [Al-Hukm Al-Mubram]; na pia rai alioitaja Sheikh Iwadh katika maelezo yake ya [Al-Iqnaa’ na Al-Khatib Ash-Shirbiniy: 2/81, Ch. ya Mostafa Al-Halabiy], vile vile Sheikh wa Uislamu Ash-Shirbiniy katika Hashiya zake za [Sharh Al-Bahjah Al-Wardiyah: 4/109-110] kuwa: ni rai inayotambuliwa. Na imeungwa mkono pia na Sheikh Muhammad Ibrahim Al-Ghayatiy katika risala yake iliyotajwa hapo juu; na hukumu ya kuwa: Mama wa Mwanamke aliyeolewa kutokana na madhehebu ya Abu Hanifa siye miongoni mwa ndugu wa karibu.
Kwa Mujibu wa hayo:
Katika hali hii ya maudhui ya swali: Tunatoa Fatwa kwa rai ya madhehebu ya Imamu Shafi anayeona kuwa ndoa hii ni batili; kwa sababu ya kutokuwapo nguzo ya walii. Na kwa hiyo, inajuzu kwa msichana huyu kuolewa tena, pamoja na imani yake kuwa mkataba wa Ndoa ya kwanza ni batili; na hapo ni baada ya kuimaliza eda yake, hali ya kukutana kimwili na mvulana aliyetajwa, na na kama haikuwa hivyo, basi hatakuwa na eda, na inajuzu kuolewa wakati wowote autakao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.


 

Share this:

Related Fatwas