Haki za Msahafu wa Swala ya Tahajud...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Msahafu wa Swala ya Tahajud

Question

Swali kuhusu kampuni ambayo imetumia wakati, bidii, na pesa ili kuutaarisha na kuandaa Msahafu (Qur'ani) wa Swala ya Tahajjud (Swala ya usiku) na imefanywa katika mfumo ambao unawezesha Swala za Sunna kwa wanaoswali, bila ya kufungua kwa kugeuza kurasa hizo; Kwa sababu kila robo iko kwenye ukurasa mmoja, na umeongezewa alama za rangi kwa ajili ya kufafanua hukumu za kusoma. Je, inaruhusiwa kwa kampuni hii kuhifadhi haki ya kutumia njia hii mpya ya kutengenezea msahafu, halafu ikatumia sheria ya haki miliki ya fikra kwa ajili ya kuulinda dhidi ya wale wanaotaka kuiga Msahafu huu? 

Answer

Sifa zote njema ni za Allah pekee, na sala na salamu ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya aali zake na Maswahaba zake, na juu ya wale wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo na baada ya huo:
Sheria imehimiza kufanya mashindano kwa vitendo vizuri. Mwenyezi Mungu amesema: {Na wa mbele watakuwa mbele (10) Hao ndio watakao karibishwa (11)} [AL WAQIA: 11:10], na Mwenyezi akasema pia: {Hawawi sawa miongoni mwenu wenye kutoa kabla ya Ushindi na wakapigana vita. Hao wana daraja kubwa zaidi kuliko wale ambao walio toa baadae na wakapigana. Na wote hao Mwenyezi Mungu amewaahidia wema.} [AL HADID: 10], na katika Hadithi Tukufu iliyopokelewa kutoka kwa Bukhari kutoka kwa Ibn Abbas R.A.: Kwenye Vita vya Badr wakati Muadh bin Afraa, na Muadh bin Amr bin Al-Jamouh- walipomvamia Abu Jahl wakamwua kwa panga zao mbili, wakampiga mpaka akafa, kisha wakaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., wakamwambia hivyo akasema: “Nani aliyemwua?” kila mmoja wao akasema: Ndiyo mimi niliyemwua, Mtume akasema, “Je! Ummefuta panga zenu mbili?" Wakasema: Hapana, na akatazama panga hizo mbili, akasema: "Nyinyi wawili mlimuua.
Imeonekana katika enzi hii na kuenea kile kinachojulikana kama haki miliki, ambayo ni: haki za yakinifu ambazo zina thamani ya kifedha, na zinaweza kumilikiwa na kufidiwa na kurithiwa, nazo ni haki zenye hali maalumu, ambazo zinathibitishwa kwa wamiliki wao kisheria na kidesturi, ni sawa tukisema: haki hizi ni kama pesa kwa mujibu wa maslahi ya umma kama walivyosema wanavyuoni waliotangulia miongoni mwa wafuasi wa madhehebu ya Imama Abu Hanifa. Na kwa mujibu wa maoni ya wanavyuoni wengi kuhusu (pesa) kwamba: Kitu kilicho na faida kati ya watu kwa sababu ya kuweza kufaidika nacho basi mwenye kukipoteza kitu hicho anatakiwa kulipa pesa zake, na wanavyuoni waliokuja baadaye miononi mwa wafuasi wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa walikubaliana rai hiyo.
Katika muktadha ulio wazi zaidi: haki miliki zinatafsiriwa kama: haki za mtu kumiliki kazi za ubunifu za mawazo; Hiyo ni, uvumbuzi, kazi za fasihi na kisanii, alama, majina, picha, miundo na ubunifu wa viwandani, aliyoandika au kutayarisha, na mchoro au mfano wa viwanda hufafanuliwa kama mapambo au uonekano wa mapambo ya bidhaa, na mchoro wa tasnia au mfano unaweza kuwa na vitu vya sehemu tatu kama vile umbo la bidhaa au uso wake au kutoka katika vitu 2D kama picha, fonti, au rangi.
Kuhusu kuiga: ni utengenezaji wa kitu cha uwongo kwa njia ya kuiga kitu sahihi, na si sharti kitu cha kuigwa kuwa sawa kabisa na kitu sahihi, ambapo mhakiki aweza kuhadaishwa nacho, lakini inatosha kufikia kufanana kwa kiwango ambacho kingedanganya umma, na somo la kukadiria kupatikana kwa kuiga liko katika njia nyingi kati ya kitu kilichoigwa na kitu sahihi.
Maudhui ya umiliki ni uzalishaji wote wa kiakili, ikiwa na aina yoyote, mtindo wowote, na thamani yoyote. [Rejea: Huquuq Al-Milkiyah Al-Fikriyah baina Al-Fiqh wal Qanuun, Utafiti, umetayarishwa na Muhammad Al-Shalash, uliochapishwa katika Jarida la Chuo Kikuu cha Utafiti cha Al-Nahh (Taaluma za ubinadamu), juzuu ya 21, Ukurasa wa 788, Al-Iitidaa ala Haq Al-Milkiyah Al-Fikriyah, uliotayarishwa na Zwani Nadia, tasnifu (uk. 11, 22)]
Kwa mujibu wa yaliyotangulia hapo juu, tunasema: hali ya kuiga kwa vitu vya biashara na vingine, vikiwa na madhara kwa yule aliyetangulia, ni kushambulia haki za kielimu za wengine. Pia hali hiyo ina udanganyifu, licha ya madhara kwa wengine kwa upande wa kifasihi na wa kifedha.
Na ikiwa uigaji huu haukuruhusiwa, na unamdhuru mmiliki wa uvumbuzi wa kwanza, basi uigaji huu hauruhusiwi; Kwa sababu una yale tuliyoyataja kutokana na makatazo ya kisheria, na dalili zake zinajulikana, miongoni mwa dalili hizi ni Hadithi ya Mtume, S.A.W., “Yeyote anayetudanganya, basi yeye sio miongini mwetu.” [Imepokelewa kutoka kwa Imamu Muslim]. Kuhusu udanganyifu huo, Mtume S.A.W. amesema: “Mwenye kushiba kwa kitu asichopewa ni kama mwenye kuvaa nguo za uwongo”, na kuhusu madhara Mtume, S.A.W. alisema: “Hakuna kujidhuru wala kudhuru wengine” [Imepokelewa kutoka kwa Imamu Malik katika Al-Muwatta]. Kuhusu suala la kuzisababishia madhara mali za wengine, Mtume, S.A.W. amasema: “Hairuhusiwi kwa mtu kuchukua pesa za ndugu yake, isipokuwa tu kwa ridha yake [Imepokelewa kutoka kwa Ahmad], na dalili kuhusu suala hilo ni maarufu.
Hali ya kulinda haki zote za kielimu inatakiwa kisheria. Kwa sababu ya kuhuhifadhi haki ya mmiliki wake, na mwishowe husababisha maendeleo ya mwanadamu.
Jambo la msingi: kwamba hakuna pingamizi yoyote ya uvumbuzi katika eneo la kuchapisha Msahafu Mtukufu kwa njia ambayo haipingani na hukumu zake za kisheria, nayo kwa ujumla ni: kwamba lazima iheshimiwe na kutakasishwa, na kampuni hiyo iliyotajwa hapo juu ina haki ya kutumia njia hii mpya ya kutengeneza Msahafu, na kuikinga na dhuluma na kuigwa chini ya Sheria ya Haki Miliki ya Fikra.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Sekretarieti ya Fatwa
 

Share this:

Related Fatwas