Ukweli wa Uislamu na Mchango wake k...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ukweli wa Uislamu na Mchango wake katika Jamii ya Kisasa.

Question

Anwani hiyo ni anwani ya mkutano wa Kiislamu wa Kimataifa ambao uliandaliwa na Taasisi ya "Aali Al Bait" kwa mawazo ya Kiislamu katika Nchi ya Kifalme Jodani, ndani ya mji wake mkuu, Ammaan, kuanzia tarehe nne mpaka tarehe sita, mwezi wa Julai, mwaka wa elfu mbili na tano, chini ya Ulezi wa Mfalme wa Jodani, Abdallah wa Pili. Mfalme huyo alihudhuria sherehe ya ufunguzi wa mkutano huo, na alihutubia kwa hotuba yenye ufasaha mkubwa kuhusu maana halisi ya anuani ya mkutano, na kuhusu risala ya Ammaan ambayo aliitoa katika mwezi wa Ramadhani ya Mwaka uliotangulia mkutano huo. Akifupisha kwayo uhakika (ukweli) wa Uislamu na vizuizi ambavyo anakabiliana navyo Muislamu, na namuna ya kusahihisha sura ya Uislamu Ulimwenguni.
Hayo ni mazungumzo ya mkutano huo, ambao ulihudhuriwa na Samaahat Mufti wa Misri Dkt. Ali Juma, Mheshimiwa Waziri wa Wakfu wa Misri Dkt. Mahmoud Hamdi Zaqzouq, Samaahat Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar Dkt. Ahmad At Twaib, Dkt. Ahmad Kamal Abu Al Majd Mkuu wa Chombo cha Haki za Binadamu cha Misri na kundi kubwa kutoka wanavyuoni wa Kimisri, na kundi la wanavyuoni kutoka mataifa yote duniani, na kutoka madhehebu yote ya kifiqhi.
Tafiti muhimi zaidi ni tafiti hamsini zilizotangulizwa katika mkutano huo, na idara ya mkutano ilikuwa ikiomba Fatwa kadhaa kutoka kwa wanavyuoni wakuu wa kidini; wa kisunna, wa kishia na wa kiibadhi kutoka mahali mbali mbali duniani kuhusu maswali kadhaa. Majibu yote yaliafikiana na maana moja, rai moja; kwani majibu hayo ni kitambulisho cha Uislamu, ambacho haitokei hitilafu kwa hayo baina ya mtu mmoja miongoni mwa wenye akili katika zama zote zilizopita, na ambayo yalikuwa kwa baadhi yao ni mahali pa kuangalia kutokana na umbali mkumbwa kwa upande wa watu hao kutoka kundi la kielimu.
Swali: 1
Fatwa hizo zilikuwa na maswali matatu; Swali la Kwanza: Je, Inajuzu kwa Muislamu kufuata mtu yeyote anayefuata madhehebu yoyote miongoni mwa madhehebu manane ya Kiislamu; Kihanafi, Kimaliki, Kishafi, Kihanbali, Kijafari, Kizaidia, Kiibadhia na Kidhahiria?
 

Answer

Jibu lake ni kama ifuatavyo: Uislamu ni Mpana zaidi kuliko matokeo ya akili za wenye kujitahidi, kwani hakika Uislamu unafaa kwa zama zote, sehemu yoyote na kwa walimwengu wote. Kwa hiyo, Basi Umma wa Kiislamu unazungumza na watu wote katika hali zote. Kwa hivyo atakayemwamini Mtume Mteule S.A.W. basi yeye ni katika Umma wa Majibu, na asiyemwamini basi yeye atakuwa ni katika Umma wa walioanganizwa. Na Waislamu wote wa Mashariki na Magharibi, waliotangulia na waliokuja baada yao, wamekubaliana ya kwamba Mujtahidu (Mwanazuoni Mwenye kujitahidi) ni yule anayefuata maneno yake katika Kulingania Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hiyo ni baada ya kutimiza Masharti yote ya kujitahidi yaliyobainishwa katika Elimu ya Misingi ya Fiqhi, na awe ni Katika Wanachuoni wenye ukumbusho (vitabu vya Mwenyezi-Mungu vya kale) ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwataja katika kauli yake:
{Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui} [AN NAHL 43]. Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tuliowapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye elimu ikiwa nyinyi hamjui}. [AL ANBIYAA 7]
Na baadhi ya Maswahaba watukufu R.A. wamefikia cheo hicho, basi madhehebu yao yamenukuliwa kwa wakufunzi wao waliowafuatia, na madhehebu yenye wafuasi yamenukuliwa kwa wafuasi wao pia, na kwa waliokuja baada yao mpaka karne ya nne ya Hijria. Basi wenye kujitihadi wengi wamedhihiri mpaka idadi ya wenye kujitahidi imefikia Wanachuoni tisini.
Hakika madhehebu yao yamefuatwa na rai zao zikategemewa kisha madhehebu manane yakaenea na kutufikia kwa mnyororo wa mapokezi pamoja na Wanachuoni wa zama zote kuyatumikia kama vile kwa kutoa dalili zake, na kuzithibitisha nukulu zake, na kuchukua hatua za kusahihisha dalili zilizotumiwa na kila madhehebu kutoka katika Hadithi za Mtume S.A.W., au Athari zilizopokewa kutoka katika machimbuko ya Hadithi, na kutafiti katika maana ya matamshi yaliyomo kwenye vitabu vya madhehebu hayo kwa upande wa lugha na kwa upande wa Sheria, Madhehebu hayo yakawa ndio yaliyoenea zaidi kuliko mengine mengi. Madhehebu hayo ni: ya Hanafiy, ya Malikiy, Shafiy na Hanbaliy, - na yanaitwa madhehebu ya kisunna- na ya kijafaria, ya kizaidia, ya kiibadhia na ya kidhahiria – na hayo ni madhehebu yasiyo ya kisunna – na hitilafu baina ya Madhehebu haya hakika inapatikana katika wigo wa kinachodhaniwa na haijawahi kutokea hitilafu katika kile chenye dalili ya wazi ambayo hukufurishwa mwenye kuikana.
Na kutokana na hayo; hakika mtu yeyote anayefuata madhehebu yoyote miongoni mwa madhehebu ya Kiislamu au anatumia katika maisha yake sehemu ya madhehebu hayo, basi yeye ni muislamu mwenye Uislamu sahihi, na hayo huafikiana na amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwetu kwa mshikamano anaoutaka Mwenyezi Mungu kwetu sisi kama pamoja, na tuwe Umma mmoja, na tusihitilafiane kwani kufanya hivyo kutapelekea nyoyo zetu pua kusihitilafiane.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwaneema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimola Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka} [AALI IMRAAN 103].
Na Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungelitoa vyote viliomo duniani usingeli weza kuziunga nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye waunganisha. Hakika Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.} [AL ANFAL 63].
Na kauli ya Mwenyzi Mungu Mtukufu: {Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.} [AL ANBIYAA 92]
Swali la Pili:
Ni ni ipi Mipaka ya kukafirisha katika Uislamu? Na je, inajuzu kuwakafirishia wafuasi wa madhehebu ya Kijafariya ua Kisufiya?
Jibu:
Hakika Muislamu anayeshuhudia kwa Ulimi wake shahada mbili hatoki katika Dini ya Uislamu isipokuwa atakapofanya kitu miongoni mwa vyenye kukufurisha, tena kwa kukusudia, akijua na akichagua kufanya hivyo, kama vile kusema waziwazi kwamba yeye ni Kafiri, au akakanusha Uwepo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au ukweli wa Risala ya Mtume Muhammad au ukweli wa Qura’ni Tukufu, na kwamba hayo sio maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, au akalisujudia sanamu, au akahalalisha madhambi makubwa kama vile kunywa pombe, na kuzini na ndugu wa karibu na uzinzi kwa ujumla wake, au mabalaa mengine yasiyokuwa hayo yaliyotajwa, ambayo Muislamu ambaye ni miongoni mwa watu wa Kibla kitakatifu, hawezi kuyasema hayo.
Na Mabwana wa kijafaria R.A. wote, ni jamhuri ya wanavyuoni miongoni mwa Umma. Nao ni wale waliozuia shubha mbalimbali mbele ya wapagani na wengineo, nao ni wale waliofuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Sunna ya Mtume S.A.W, katika zama zote za historia, na atakayewakufurisha au kuwataja vibaya basi Dini yake itatiliwa shaka.
Al Haafidh Bin Asaakir amesema katika Kitabu chake cha: [Tabyiinu Kadhbil Muftarii]: “Tambua – Mwenyezi Mungu Mtukufu aniwafikishe mimi na nyinyi katika radhi zake na atujaalie sisi tuwe miongoni mwa wamchao ukweli wa kumcha – kwamba nyama za Wanachuoni zina sumu, na ni kawaida kabisa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wenye kufichua pazia la wale wenye kuwatia kasoro linajulikana. Na kwamba mtu yeyote atakayeutumia ulimi wake katika kuwatia kasoro basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atampa mtihani wa kufa moyo wake kabla ya Umauti wa Mwili wake”.
Na kutokana na hayo, basi mwenye kujiingiza katika Ashaaira, na Usufi, yuko katika hatari kubwa sana na panahofiwa asije akawa miongoni mwa Khawaarij na Murjifuuna ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwatajia katika kauli yake: {Kama wanaafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao,na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwayakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu}. [AL AHZAAB 60]
Ama Swali la Tatu:
Ni nani anayejuzu kuzingatiwa kuwa Mufti katika Uislamu na ni yepi masharti yake?
Jibu:
Ni kwamba Mufti ni mtu anayejitahidi ambaye Wanachuoni wa Elimu ya Misingi wanamzungumzia, na Mujtahidi ni yule anayetekeleza mchakato mzima wa kujitahidi katika Dini, nao ni kutumia nguvu zote katika kugundua Hukumu ya Kisheria kutoka katika dalili zinazozingatiwa. Al Khatwib alisimulia katika kitabu chake cha: [Al Faqiih wa Al Mutafqeh] kutoka kwa Imamu Shafi kauli yake: “Si Halali kwa Mtu yeyote kujitolea Fatwa katika Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isipokuwa awe mtu mwenye kukijua Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu: kwa kujua Naasikh na Mansuukh (Aya inayofuta hukumu na Aya yenye Hukumu iliyofutwa), Aya za Hukumu, Aya zenye mshabihiano wa maana, na jinsi ya kutafsiri na kuteremka kwake, na ajue ipi ya Makkah na ipi ya Madina, na imekusudiwa nini, na baada ya hapo atakuwa ni mwenye kuona (mtambuzi wa) kwa Hadithi za Mtume S.A.W, na azijue Hadithi kama alivyoijua Qur`ani, na awe mtambuzi wa Lugha, mtambuzi wa mashairi, na anayoyahitajia katika Sunna na katika Qur’ani Tukufu, na atumie hivyo kwa Uadilifu, na awe msimamizi wa hitilafu za Watu wa miji mbalimbali, na awe ni mwenye elimu na uwezo wa kugundua baada ya hapo na pindi atakapokuwa hivyo basi ana haki ya kuzungumza na kufutu Masuala ya Halali na Haramu, na kama hatakuwa hivi basi hana haki ya kutoa Fatwa”. [Al Khatwib Al Baghdadiy kitabu chake cha: Al Faqiih wa Al Mutafqeh 33-331/2].
Na inamlazimu kila mwanachuoni kujua Qur`ani na elimu zake, Sunna ya Mtume na elimu zake na lugha ya Kiarabu na elimu zake afuate mfumo mmoja katika kutoa Fatwa kwa kutegemea utaratibu wa dalili, na anapoulizwa swali lolote atafute hukumu yake katika Qur`ani, na ikiwa hakupata basi katika Sunna, Ikiwa hakupata basi atatumia Kipimo, mpaka afanikiwe kugundua hukumu ambayo moyo wake utaridhika nayo. Na inashurutishwa katika hukumu hiyo itakayotolewa isije ikahitilafiana na Ijmaai ya Wanachuoni. Na kwa upande wa dalili zenye hitilafu za Wanachuoni ndani yake kama vile Istihsaan, na Sheria za walio kabla yetu iwapo jitihada zake zitapelekea kusihi kwa kitu ndani yake basi atakitumia katika kutolea Fatwa. Na iwapo dalili kwake yeye zitakinzana basi analazimika kutoa Fatwa kwa dalili iliyo sahihi zaidi.
Hilo ndilo lengo la majibu yetu, na tumeafikiana nayo – wanavyuoni wa Sunna na Samaaha Imamu Mkuu wa Al Azhar, na wanavyuoni wa madhehebu ya Shia na miongoni mwao Samaaha Sheikh Muhammad Saiyed Al Hakiim, Sheikh Ishaaq Al Fayaadh, Sheikh Bisher An Najafiy, na mwanachuoni, Ayatullahi Muhammad Ali At Taskhiriy, Imamu ya madhehebu ya Al Ibadhiy Sheikh Ahmad Bin Hamad Al Khalili Mufti wa Omani, Sheikh Ibrahim Al Waziri Imamu ya madhehebu ya Az Zaidiy wa Yemeni, Baraza Kuu la Fiqhi ya Kiislamu na wengi wengineo.
Tunatarajia Mwenyezi Mungu Mtukufu awaongoze wavulana katika Dini ya Haki, ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu amemteremshia Bwana wetu Mtume Muhammad S.A.W. na awasaidie waitumie katika maisha yao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Rejea: Kitabu cha: Simaatul Al Aswer, cha Samaahat Mufti wa Misri, Dkt. Ali Jumah.


 

Share this:

Related Fatwas