Athari ya Kukosekana Mahali pa Kute...

Egypt's Dar Al-Ifta

Athari ya Kukosekana Mahali pa Kutekelezwa Hukumu ya Kisheria.

Question

Tunasikia toka kwa baadhi ya wanachuoni kuwa baadhi ya maandiko ya kisheria yanakosa sehemu yake, na wanatoa mfano kwa hilo kwa mtu aliyekatwa mkono au kukatwa mguu, watu hao wamepoteza sehemu ya kuosha kwenye kutawadha, je hukumu inaondoka katika masuala hayo na mfano wake kwa kukosekana sehemu yake au hapana? 

Answer

Shukrani zote za Mwenyezi Mungu, Swala na salamu ziwe kwa Nabii wa mwisho pamoja na Masahaba wake na jamaa zake na wale wote wenye kumfuata kwa wema mpaka siku ya mwisho, na baada ya utangulizi huo:
Miongoni mwa tafiti ambazo zinatajwa kama utangulizi wa maelezo ya msingi wa sheria: “Hukumu ya kisheria” wasomi wa mambo ya Usuul dini wameelezea “Hukumu ya kisheria” ni “Maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu yanayofungamana na vitendo vya watu waliopewa amri ya kutekeleza au kuwa na hiyari, wakaweka wazi wanachuoni wa sheria kuwa hukumu ya sheria ni lazima iwe na sehemu ya kutekelezwa, wakazungumza katika hali ya kuondoka kwa sehemu hii na kuelezea kuondoka huku kwa maelezo tofauti, miongoni mwake: “Kuondoka sehemu husika” angalia kitabu cha: [Bidayat Al-Mujtahid, 2/185, chapa ya Dar Al-Fikr]. Maelezo mengine: “Kukosekana sehemu husika” angalia kitabu cha: [Al-Mabsut cha Sarkhasiy, 2/100 chapa ya Dar Al-Maarifa], pia wameeleza: “Kutokuwepo sehemu” angalia kitabu cha: [Radd Al-Mukhtar cha Ibn Aabideen, 3/354 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah], maelezo mengine: “Kutoweka sehemu: Angalia kitabu cha: [Mawahib Al-Jalil, 1/192, chapa ya Dar Al-Fikr, na kitabu cha Ibn Qassim Al-Abbady, 2/102, 103, chapa ya Dar Ihyaa- At-Turath Al-Arabiy].
Pia: “Kukosekana sehemu” angalia kitabu cha: [Al-Inaayat cha Al-Babartiy, 3/107 chapa ya Dar Al-Fikr, na kitabu cha: Badaai As Swanaai cha Kaasaty 3/137 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]. Maelezo mengine: “Kutosheleza sehemu” angalia kitabu cha: [Fat-h Al-Qadeer cha Ibn Al-Humam 3/208 na 4/444 chapa ya Dar Al-Fikr]. Pia: “Kutosheleza maudhui” angalia kitabu cha: [Al-Inayat 6/424]. Maelezo mengine: “Kukosekana maudhui” angalia kitabu cha: [Bariqat Mahamoudiyah cha Khadamy 2/46 chapa ya Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah].
Miongoni mwake pia: Kutoweka maudhui” na “Kuondoka maudhui” na “Kubadilika maudhui” maelezo haya matatu utayakuta katika kitabu cha: [Shiiat Al-Mudawana fi Uluum Al-Usuul, angalia kitabu Al-Fusul Al-Gharwiyah fi Al-Usuul Al-Fiqhiya cha Haairy, uk. 399, chapa ya Dar Ihyaa Al-Uluum Al-Islamiyah] na pia kwenye ripoti ya utafiti wa alama kubwa za Mwenyezi Mungu cha Aafa Hussein Al-Burujardiy uk. 109, chapa ya Taasisi ya uchapishaji wa vitabu vya Kiislamu, pia kitabu cha: [Manaahij Al-Ahkaam cha Mirzaa Al-Qummiy uk. 329 chapa ya Taasisi ya uchapishaji wa vitabu vya Kiislamu]. Pia maelezo mengine: “Kuangamia sehemu” na “Kubatilika sehemu” lakini maelezo haya mawili ndiyo yamepokelewa kwa wingi pamoja na kile kinachoitwa (Sehemu ya makubaliano) ambayo inazingatiwa ni moja ya nguzo za miamala ya kifedha, kwa maana: kinachofanyiwa makubaliano na kuonekana hukumu zake na athari zake, nayo inatofauti kwa kutofautiana makubaliano, wakati mwigine kitu cha kukubaliana kinakuwa ni chenye thamani kama kwenye kuuza kutoa zawadi na rehani, lakini inaweza kuwa ni kazi miongoni mwa kazi, kama vile kazi ya kukodisha kazi ya kulima kazi ya uwakala na wakati mwingine huwa ni manufaa ya kitu, kama vile manufaa ya kilichokodishwa katika makubaliano ya kukodisha, na manufaa ya kitu cha kuazimisha katika makubaliano ya kuazima, na huenda ikawa tofauti na hivyo, kama vile makubaliano ya ndoa ulezi na yasiyokuwa hayo. Angalia kitabu cha: [Badaai As Swanaai 7/379 na Al-Mughniy cha Ibn Qudamah 5/290 chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Kwa ufupi: Maneno yanayotumika katika kuelezea maana ya kukosekana sehemu hupelekea maana moja au iliyokaribiana, lakini pamoja na kutumia wanachuoni wa Sheria msamiati wa kuondoka sehemu na unayofanana na msamiati huo lakini bado hawajabainisha kusudio la sehemu ya hukumu, mwenye kuzingatia katika ibara zao atakuta kuwa wanatumia kwa maana nyingi hutofautiana kwa kutofautiana sehemu iliyopokelewa, huenda ikawa: Mtendaji mwenye kuaelezewa kuhusika na kitendo, au kuwa: Anayetokewa na kitendo, au kuwa: Anayetokewa na kitendo hiki (Sehemu na muda) au inakuwa: Sifa ambayo imeainishwa na Sheria ya kuhusika na kitendo.
Mfano wa sehemu kwa maana ya mtendewa ni pamoja na yaliyokuja kwenye kitabu cha [Badaai Sanaai miongoni mwa vitabu vya Imamu Abu Hanifa 1/3] kuwa: “Maana ya neno usafi kwa upande wa lugha na upande wa Sheria ni: Usafi na Utwahara. Usafi ni: Kuthibitisha usafi wa sehemu.
Amesema Al-Khatwib As-Shirbiny katika kitabu cha: [Mughniy Al-Muhtaj, 5/442 chapa ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]: Kufanana kuna aina tatu: Kufanana mtendaji, kama vile kuwa mjinga, kufanana sehemu, kama vile kudhania kuwa ni mke wake, kufanana pande, kama vile ndoa pasina walii.
Na katika maana hiyo pia kauli yao: “Sehemu ya tofauti” na “Sehemu ya mvutano” kwa maana: sehemu yenye tofauti na kitovu cha mvutano, isipokuwa sehemu hapa ni kwa upande wa maana haikusudiwi sehemu halisi.
Na mfano wa sehemu kwa maana ya mtendewa (muda) ni ule aliosema As Sarkhasiy katika kitabu cha: [Al-Mabsuut 7/210]: “Ikiwa makubaliano ya mali yatakuja kabla ya muda na akakataa muhusika kukubali basi atalazimishwa kuchukua”.
Amesema mwanachuoni Ad Dardeer katika namna ya kusali Sala za Eid mbili kwenye kitabu cha sherhe Al-Sagheer, 1/525 chapa ya Dar Al-Maarif: “Sehemu ya takbira ni kabla ya kusoma” kwa maana ya muda wake.
Mfano wa sehemu kwa maana ya mtendewa (yule anayetokewa na kitendo) kauli yao: “Sehemu ya makubaliano” kwa maana mwenye haki ya kutumia.
Amesema Ibn Qudamah katika kitabu cha: [Al-Mughniy 4/113]: “Chenye kuuzwa hakika kimekuwa ni sehemu ya makubaliano kwa kuzingatia ni sifa ya mali, chenye kupelekea upungufu basi kinakuwa na kasoro”.
Miongoni mwa mifano ya sehemu kwa maana ya mtendaji: Ni pamoja na aliyosema As-Sabakiy katika [Fatwa yake 1/201 chapa ya Dar Al-Maarif], ikiwa utasema: Kila mmoja ni lazima awe na sehemu basi ni ipi sehemu ya wajibu wa zaka? Nikasema: Kwa upande wa Imamu Shafi sehemu yake ni mali, na kwa upande wa Imamu Abu Hanifa sehemu yake ni katika mwili wa mmiliki, kwa sababu jukumu la utekelezaji kwa upande wake ni dalili tu, na ibada za mwili sehemu yake ni mwilini kwa mtazamo wetu na upande wao, kama vile ibada ya Swala na funga, na kwa sababu hii ikiwa huyu mtu atakuwa amefariki basi anakuwa hana wajibu wa ibada kwa sababu ya kuondoka sehemu ya kutekelezea ibada.
Na mfano wa hilo pia ni yale yaliyosemwa kwenye maneno yanayoelekezwa kwa mtu mwenye kughafilika mwenye kulala na mwenye kusahau pamoja na maneno yanayohusiana na kiongozi wa Waislamu au mambo ya nambari, mtumwa na Khalifa, kwa mfano ni sehemu ya maneno yanayoelekezwa kwao, mfano wa maneno yanayohusu nambari ni pamoja na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wajizuilie na machafu wale wasio pata cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu awatajirishe kwa fadhila yake. Na wanao taka kuandikiwa uhuru katika wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki, basi waandikieni kama mkiona wema kwao. Na wapeni katika mali ya Mwenyezi Mungu aliyo kupeni. Wala msiwashurutishe vijakazi vyenu kufanya zina kwa ajili ya kutafuta pato la maisha ya dunia, ilhali wao wanataka kujihishimu. Na atakaye walazimisha basi Mwenyezi Mungu baada ya kulazimishwa kwao huko, atawasamehe, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu} [AN-NUUR: 33]. Sehemu ya kusudio hapa ni kwa maana ya mtendaji – naye ni bwana – ambaye hayupo ndani ya zama zetu, na kwa maana ya mtendewa – naye ni mtumwa – pia hayupo ndani ya zama zetu, vilevile maneno yanayoelekezwa kwa Kiongozi wa Waislamu baada ya kudondoka kwa Uongozi mkubwa na kupoteza sehemu yake, ambapo hakuna Khalifa au Kiongozi kwa maana inayofahamika kwa Waislamu, kwani Khalifa au Kiongozi ni sehemu kwa maana ya mtendaji katika maelezo yanayoelekezwa kwake, na kwa maana ya mtendewa yule anayefanyiwa kitendo ikiwa maelekezo ni yenye kuelekezwa kwa raia kama vile ulazima wa utiifu kwa mfano.
Katika uelewa wa neno sehemu kunaingia ndani ya masharti na nguzo, kwa mfano sharti la Swala ni usafi kujua kuingia kwa wakati kuvaa nguo yenye kusitiri tupu kuelekea Qibla......n.k, masharti haya ni sifa zilizowekwa na Sheria kufanyiwa kazi, inafaa kuyafanya ni sehemu yake, kwa upande mwingine inawezekana kurudisha masharti hayo katika dalili miongoni mwa dalili za sehemu iliyopita, kwani usafi wa viungo ni jambo la kimaana linapangiliwa na dalili ya sehemu kwa maana ya mtendaji, vilevile kuelekea Qibla, pia kusitiri tupu, kufahamu kuingia kwa wakati ni mambo ya maana yanawekewa dalili ya sehemu kwa maana ya mtendaji na kwa maana ya mtendewa pia kwa maana ya mwenye kufanyiwa kitendo, usafi wa sehemu ni sehemu kwa maana inayofanyiwa kitendo, vilevile husemwa hivyo kwenye nguzo zingine zilizobakia.
Kwa maelezo hayo: Kutokuwepo sehemu maana yake: Ni hali ya hukumu ya Sheria kukosa muda wake au sehemu yake au sifa yake iliyowekwa kisheria.
Na kuondoka sehemu si chenye kufutwa, hata ikiwa vimeshirikiana vyote viwili kuondoa hukumu, isipokuwa kufutwa kunakuwa ni kwa sababu aliyoitaka Mwenyezi Mungu, ni sawa sawa hekima ya hilo imefahamika kwetu au haijafahamika, tofauti na kuondoka kwa sehemu, kuondoa hukumu katika hali hii sababu yake ni kukosekana kwa sehemu, vilevile kuondoa hukumu kwa kufuta ukweli wake upo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na huitwa kwa kitu kingine ni upanuzi, anasema Zarkashy: “Nguzo za kufuta ni tatu: Mfutaji. Chenye kufutwa. Kifutio. Ama kwa upande wa mfutaji kwa ukweli ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuitwa neno lake linaloonesha kufuta ni mfutaji” angalia kitabu cha: [Al-Bahr Al-Muhiit 4/69 chapa ya Wizara ya Waqfu na Mambo ya Kiislamu nchini Kuweit], tofauti na hali ya kuondoka sehemu, ambaye anahukumu kuondolewa hukumu ukweli ni mwanasheria kutokana na dhana yake ya hukumu kukosa sehemu yake, sambamba na hilo anatoa hukumu ya kurejesha hukumu kutokana na dhana yake ya kufikiwa uwepo wa sehemu, na mfano wa hilo: Ni yaliyopokelewa kwa Omar Ibn Khatwabu kusimamisha utoaji adhabu ya mwizi ndani ya mwaka wa njaa, haisemwi kuwa Umar alifuta hukumu ya adhabu ya mwizi, bali aliisimamisha kutekelezwa kwa kukosa sababu, kwani masharti ya kutekelezwa adhabu ni kutokuwepo kwa yanayoleta shaka, na sharti hili ni katika jumla ya sehemu ya hukumu, pindi iliposhindikana kufikiwa sharti hili ndipo Umar aliposimamisha utekelezaji wa adhabu hii ya mwizi kuwa aliwahi tekeleza adhabu hii kwa kufikiwa sharti zake kama vile inavyofahamika.
Katika yanayofungamana hapa na kile tunachosema: Ni masuala ya kuwa je kukosekana sehemu inafuta hukumu ki akili au hapana? Amezungumza Imamu Ar-Razy kuwa kukosekana sehemu ni aina katika aina za kufuta, ametoa dalili ya kufaa kufuta katika hali ya kuondoka kwa sehemu, nayo ni kudondoka hukumu ya kuosha kwa mtu asiye na mguu, na akaelezea pia Siraj Al-Armawy katika kitabu cha: [Tahseer 1/386 chapa ya Taasisi ya Risalah]. Amesema katika kitabu cha: [Al-Mahsuul 3/133 chapa ya Chuo Kikuu cha Imamu]: kama patasemwa: Ikiwa itafaa kuhusisha kwa kutumia akili basi hilo linapelekea kufaa kufutwa? Tumesema: Ndiyo, kwa sababu mwenye kuondokewa miguu unaondoka kwake ulazima wa kuosha miguu yake, na hilo linafahamika kiakili tu”.
Lakini jopo la Wanachuoni wa Sheria hawaoni kufutwa kiakili, bali amesema Al-Aamady: “Ama kujizuia na kufuta kwa akili kwa hakika kunakuwa kwa upande wa mfutaji mwenye kufahamu uwazi wa muda wa hukumu inayokusudiwa katika mtazamo wa mwanasheria, na hilo halina njia ya kuliangalia kwa kauli yao tu ya akili, tofauti na uelewa wa kutowezekana kuwa Mola Mtukufu ni kiumbe mwenye kukadiriwa” kitabu cha Hukumu 2/387 chapa ya Dar Sameei pamoja na kitabu cha Muntaha Al-Suul uk. 145.
Ama mifano ambayo ameitaja Imamu Ar-Razy haikubaliki kuwa ni upande wa ufutaji wa kiakili, kwa sababu mwenye kukosa miguu miwili haijafutwa kwake kuosha miguu hiyo bali ulazima ndio umeondoka kwa sababu ya kutokuwa na uwezo na si vinginevyo.
Amesema mwanachuoni Al-Qurafiy wakati akisherehesha maelezo ya Imamu Ar-Razy katika kitabu cha: [Nafaisu Al-Usuul 5/2073, 2074 chapa ya Nizaar Mustafa Al-Baaz]: “Hatukubali kuwa hii ni yenye kufuta, kwa sababu ulazima ni ule uliothibiti mwanzo wa amri isipokuwa kwa sharti la uwezo na kubakia sehemu pamoja na kuendelea maisha, kukosekana hukumu wakati wa kukosekana sharti haisemwi hiyo ni kufutwa, na wala hiyo sio kujifuta yenyewe, kwani mwenye kusafiri ndani ya mwezi wa Ramadhani haijafutwa kwake ibada ya funga wala Swala, bali amelazimishwa kwa sharti, ikiwa mwanamke atakuwa katika hali ya hedhi haisemwi: Imeondolewa kwake ibada ya funga na Swala, hili halina njia ya kulielekea bali hufikiwa katika hukumu yenye sharti pasina kubakia na mpangilio wa sharti hilo, au katika sehemu pasina sharti na kutobakia sehemu hiyo, na jibu lake ni kuwa imeondolewa hukumu baada ya kuthibiti kwake, na hukumu hizi ndizo zilizothibiti katika msingi wa Sheria isipokuwa kwa sharti hizi za hali hii, hakibadiliki kitu mpaka ikasemwa kuwa kimefutwa”.
Tofauti kati ya Imamu Ar-Razy na wengine katika hili ni tamko tu ambapo hakuoneshi uzito wowote, kudondoka kuosha miguu miwili kwa mfano kwa mtu aliyekatwa ni jambo lililokubalika ni sawa sawa ikiwa tutasema: Kuondoka kwa sehemu au kufutwa kiakili au kuondoka kitu kwa kuondoka sharti zake au sababu zake.
Miongoni mwa yanayofanana na kukosekana sehemu: Ni kushindikana, nako ni kubadilisha kitu katika uhalisia wake na sifa zake na kuwa kwenye hali na sifa nyingine tofauti, miongoni mwa mifano yake: Pombe haiwezekani kuwa siki, damu haiwezekani kuwa kinywaji, chakula hakiwezekani kuwa matapishi, kutowezekana ni mabadiliko ya sifa pamoja na kubakia kitu kama kilivyo, yenyewe katika ukweli wake ni sawa na hali katika hali za kukosekana sehemu, hukumu ya pombe kwa mfano ni uharamu wa kuitumia, ikiwa itageuka basi hukumu hii inaondoka kwa kuondoka sehemu husika yenyewe hapa ni sifa ambayo imebadilika na kuchukua sifa nyingine ambayo ni siki, na inalazimisha kauli kuwa sehemu ya uharamu – kwa maana ya sehemu ya hukumu – katika pombe ni sifa na wala sio jina lake, na kinyume na hivyo lau ingekuwa ni jina ndiyo sehemu basi ingeendelea kubakia hata baada ya kufikiwa na hali isiyowezekana, pamoja na hayo umeondoka uharamu, hivyo husemwa: Hakika uharamu umeondoka kwa kuondoka sifa inayohusiana nayo.
Miongoni mwa yanayofanana na kukosekana sehemu: Kukosa uhalali: Na uhalali unachukua maana katika msamiati kwa maana ya kufaa, anasema Al-Bazdawy: “Ama uhalali wa lazima unagawanyika matawi yake, na asili yake ni moja nayo ni kufaa kwa hukumu” kitabu cha: [Usuul Al-Bazdawy pamoja na sherehe yake kitabu Kashful asraar 4/237 chapa ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy], na maana nyingine: Uhalali ni kufaa mwanadamu kwenye wajibu wake, na kufaa matumizi yake na kufungamana na kutekeleza maamrisho.
Nayo inagawika sehemu zifuatazo: Uhalali wa lazima, na uhalali wa utekelezaji, ama uhalali wa lazima: Ni kufaa mtu ulazima wa haki halali kwake pamoja na wajibu juu yake, hii inaitwa uhalali wa mtu kwenye haki na wajibu.
Ama uhalali wa kutekeleza: Ni mtu kufaa yale yanayoamriwa kwake kuzingatiwa ni Sheria, nayo ni sifa inayomfanya mtu kuwa na haki ya kujibu kukubali kuanzisha na mengineyo katika matendo ambayo Sheria imeweka sharti ya kuzingatiwa ni mtu kuwa na akili timamu, na hufanya kazi uhalali huo kwa kuzingatia matendo ni sawa sawa yakiwa ni ya kauli au vitendo.
Na uhalali wa kutekeleza wakati mwingine hutokewa na yale yenye kuathiri kwa mapungufu au kutokuwepo kitu husika, ambapo hali hii huitwa “Ukosefu wa uhalali” miongoni mwake ni pamoja na hali ya: Uendawazimu, usahaulifu, usingizi, kupoteza fahamu, maradhi, utumwa, hedhi, ujinga, ulevi, kukosea na kutenzwa nguvu.
Hali hizi ndizo miongoni mwa hali za kukosekana sehemu, kwani yule mwenye kutokewa kwenye akili yake chenye kuathiri kwenye ufahamu wake kwa kuwa na hali ya upungufu au kuondokewa kabisa pindi anapofikiwa na tamko la kisheria anakuwa hana sehemu halali ya utekelezaji wa hakumu zilizokuja kwenye tamko, hivyo basi wanachuoni wa Sheria wamemvua au kumuondoa mtu mwenye hali kama hiyo kwenye amri ya utekelezaji wa kisheria, hivyo katika hali hii inafaa kusema: Sehemu ya tamko la kisheria linalopasa utekelezaji wa kitu au kuacha kutekeleza katika hali hii sehemu hiyo haipo, kwa kuongezea na hayo ni kuwa baadhi ya hali hizi huzingatiwa kwenye ukweli wake ni miongoni mwa masharti au nguzo za kufikiwa utekelezaji wa hukumu za kisheria, imefahamika uelewa wa sehemu unaendana na masharti na nguzo za kitendo, kwani hukumu ya kisheria inamtaka mwanadamu kuwa na sifa ya kutekeleza amri, nayo sifa hiyo imepungua au haipo kwa yule aliyetokewa na hali ya ukosefu wa akili, na miongoni mwa masharti ya kutakiwa kutekeleza maamrisho ni mtu kutokuwa na udhuru unaozingatiwa ni wenye kuzuia kutekelezwa kwa amri halali ya kisheria.
Ukweli ni kuwa: Kauli ya kuwa hukumu inaondoka kwa kuondoka kigezo chake tu sio sahihi, kwani zimekutwa baadhi ya matawi ya Sheria kutokosekana kwa sehemu, lakini kumetokea tofauti kati ya mwenye kusema hukumu inaondoka na mwenye kusema bado inabakia.
Katika masuala haya: Masuala ya kukosekana sehemu mbili za kusafishwa: Wakati mwingine hutokea kuwa mtu mwenye kutaka kuswali hukosa cha kujisafishia, kama vile mtu kufungwa au kuzuiwa sehemu isiyo na maji na ardhi yake ni yenye uchafu, je anaweza kuswali mwenye hali hii pasina kutawadha? Au Swala yake ataichelewesha mpaka pale atakapokuwa na uwezo wa kujisafisha? Na akiwa ataswali kwa hali hiyo hiyo je Swala yake itapaswa kurudiwa tena baada ya kuwa na uwezo wa kujisafisha au hapana?
Katika hali hii wanachuoni wa Sheria wana kauli Nne:
Kauli ya Kwanza: Hapaswi mtu huyo kuswali, isipokuwa inapendezeshwa tu, na atapaswa kulipa Swala ni sawa sawa ameswali au hakuswali, hii ni kauli ya Imamu Shafi na Imamu Ahmad Ibn Hanbal. Kitabu cha: [Al-Majmuu An-Nawawy 2/322 chapa ya Maktabatuh Al-Irshaad, na kitabu cha: [Al-Insafu cha Mardawy 1/281 chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy].
Kauli ya Pili: Hana ulazima wa kuswali, na wala hapaswi kulipa Swala yake, nayo ni kauli iliyopitishwa kwa watu wa Imamu Malik. Kitabu cha: [Haashiyat Ad-Dusuuqy kwenye Sharh Al-Kabiir 1/163 chapa ya Dar Ihyaa Al-Kutub Al-Arabiyah].
Kauli ya Tatu: Ni haramu kwake kuswali na anapaswa kulipa, ni kauli ya Abu Hanifa na Zufur, ni kauli isiyopitishwa na watu wa Imamu Malik na Imamu Shafi pamoja na kauli ya At-Thaury na Al-Auzaai, angalia kitabu cha: [Badaaii Sanaaii 1/50, na kitabu Mawaahib Al-Jalil 1/360 na Al-Majmuui 2/322 pamoja na kitabu Al-Insaf 1/281 na Fat-h Al-Bary cha Ibn Hajar 1/440 chapa ya Dar Al-Maraif].
Kauli ya Nne: Ni lazima kwake kuswali katika hali hii – lakini katika kurudia hiyo Swala kuna kauli mbili katika kila madhehebu – kauli ya watu wa Malik si yenye kutegemea, jambo jipya ni kwa watu wa Imamu shafi na madhehebu ya Imamu Abi Hanifa, na kwa kauli hiyo amesema Abu Yusuof na Muhammad Ibn Al-Hassan ni katika watu wa Abu Hanifah, isipokuwa wao wamesema: Anafananishwa na wenye kuswali, na hiyo ndiyo Fatwa kwa watu wa Abu Hanifah. Kitabu ni [Sharhu Al-Mahally ala Al-Manhaj 1/109, 110 chapa ya Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy], na kitabu cha: Al-Inswaf 1/282, 283].
Tofauti katika masuala haya imejengeka katika msingi wa kutokuwepo dalili ya wazi katika hili, kama vile kumekuwa na mvutano katika mambo mawili:
Jambo la Kwanza: Ni kuwa Swala ni nguzo muhimu katika Uislamu, Sheria ya Kiislamu imewajibisha pamoja na hali za mtu kushughulishwa, kama vile hali ya vita vya jihadi.
Jambo la Pili: Ni kuwa sharti la kisheria linalazimisha kukosekana kwake ni kukosekana cha kuwekewa sharti, ni sahihi kuwa usafi ni sharti la kisheria katika Swala.
Maelezo yaliyotangulia yanaonesha kuwa, kauli katika masuala haya chanzo chake ni kauli mbili: Kauli ya kwanza ya mwenye kusema wajibu wa Swala utaondoka, na kauli ya pili ya mwenye kusema wajibu wa Swala hautaondoka, kwa upande wa watu wa Imamu Malik ambao ndio wenye kusema wajibu wa Swala utaondoka kwa mtu aliyepoteza viungo viwili vya kutawadhwa wamefanya kati ya hoja ya kuondoka kwa sehemu, na hii ni kauli pekee katika masuala ya kufanyia kazi kukosekana kwa sehemu, na kauli iliyokaribu na hii ni kauli ya Abi Yousuf kuwa inalazimika kufanana, na kufanana kwa hakika sio Swala.
Ukweli ni kuwa kupima kunapelekea mwelekeo walioenda nao watu wa Malik, ambapo ufuasi ni sehemu katika Swala, imekuwa ni lazima kuondoka wajibu wa Swala katika hali ya kukosekana sehemu yake, lakini kumekuwa na maelekezo mengine yenye nguvu zaidi ya mazingatio ya kukosekana sehemu, nayo ndiyo ambayo yamefanya tabu wanachuoni kuona wajibu wa Swala hauwezi kuondoka katika hali hii, miongoni mwa kauli hizo ni Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhary na Muslim kuwa Mama wa Waumini Bibi Aisha R.A. pindi alipomuazima Bibi Asmaa R.A. pambo na likapotea, Mtume S.A.W. aliwatuma baadhi ya Masahaba zake kulitafuta, ukawakuta wakati wa Swala wakaswali pasina kutawadha, pindi waliporudi kwa Mtume S.A.W. wakamuelezea hilo, ndipo ikateremka Aya ya kutayammamu. Hadithi hii inaonesha kuwa Masahaba waliswali Swala kamili pasina kutawadha wakati wa dharura ya kukosekana sehemu, hivyo kauli ya kusema wajibu wa Swala unaondoka katika hali ya kukosekana cha kujisafishia inapingana na andiko hili la Hadithi.
Na katika masuala mengine pia: Ni masuala ya kutofautiana kwa nchi mbili:
Kusudio la nchi mbili: Ni sehemu au nchi au taifa ambalo wanaishi watu wengi wakiwa chini ya uongozi maalumu, anasema Ibn Aabideen: Kusudio la nchi: Ni sehemu maalumu inayotawaliwa na utawala wa Kiislamu au utawala wa Kikafiri”. Kitabu cha: [Haashiyatu Ibn Aabideen 4/166].
Jopo la wanachuoni wa Sheria wamegawa nchi kwa maana hii sehemu mbili: Sehemu ya kwanza: Nchi ya Waislamu, nayo ni nchi ambayo inaongozwa na kiongozi Mwislamu, na kutekelezwa humo hukumu za Uislamu. Sehemu ya pili: Nchi isiyokuwa ya Kiislamu, nayo ni nchi ambayo hazitekelezwi humo hukumu za Uislamu, wala kiongozi wake mkuu si katika Waislamu, na inaweza kuwa ni nchi ya ahadi au nchi ya vita.
Na kugawa nchi kuwa ni nchi ya Kiislamu na isiyo ya Kiislamu inaendana na zama zetu, ambapo wanachuoni wametumia kwenye vitabu vyao neno “Nchi ya vita” ni matumizi yanayochunga muda au zama, ambapo nchi hizo zilikuwa zikiwaingiza Waislamu kwenye Ukristo kwa uadui, na kushambulia nchi zao au kuwafukuza kwenye nchi zao, ama hivi sasa tunaona ulimwengu haukatai wala kupinga kuwepo kuishi Waislamu wala kupinga mahubiri ya Uislamu, na wala hakuna vita vilivyotangazwa kati ya nchi fulani na nchi za Waislamu.
Kutokana na tofauti ya ipi hiyo nchi ya Waislamu na isiyokuwa ya Waislamu, wanachuoni wameweka hukumu inayofungamana na kutekelezwa kwake kwenye nchi ambayo zimo hukumu hizo, na milango ya Sheria imejaa ushahidi wa hilo, katika milango ya kisasi ulipaji dia kafara adhabu mirathi wasia ndoa vilevile makubaliano maovu na yenye kukusanya kati ya matawi hayo yote – pasina kuingia kwenye maelezo ya kina – kuwa inafaa kuifanya nchi ni sehemu ya hukumu, na sehemu hapa kwa maana ya eneo, na imefahamika kuwa maana ya sehemu ni eneo, kwa mfano: Masuala ya riba ndani ya nchi isiyokuwa ya Kiislamu madhehebu ya Imamu Malik yamezuia riba, lakini Imamu Shafi na Hanbal ni sahihi, Abu Yousuf ni katika watu wa Abu Hanifa, nayo ni kauli ya Ishaka na Al-Auzaii, na kupitishwa na Abu Hanifah na Muhammad, tofauti ya masuala inajengeka kwenye tofauti ya nchi na athari zake kwenye hukumu ya kisheria, maana yake ni kuifanya nchi ni sehemu ya hukumu, katika hilo hutolewa masuala yote yanayofungamana na nchi ya vita na nchi ya Kiislamu.
Mifano hii miwili na mingineyo ni katika mifano ya kuondoka sehemu, inatufanya kutorudiarudia ibara ya kuwa hukumu inaondoka kwa kukosekana tu sehemu yake, haikutuwezesha kuwa kigezo katika hili, nayo ni kuwa: Asili ya hukumu ni kuondoka kwa kukosekana sehamu yake, hii ndiyo hukumu asili ya hali za kukosekana kwa sehemu, na huondolewa katika hilo baadhi ya hali, miongoni mwazo: Ni hukumu kuwa ni muhimu zaidi ya sehemu ambayo imekosekana, na miongoni mwazo pia: Ni kupatikana kwa kitu mbadala cha sehemu kinachochukua sehemu yake katika kupatikana hukumu, nayo inafanana kwa sehemu kubwa na wajibu unaofungamana kwenye kafara, wajibu wa kumuacha huru mtumwa ikiwa atashindwa basi afunge ikiwa atashindwa basi alishe chakula, na kushindwa huku ni kukubwa zaidi kuliko kumpata mtumwa, kwa mfano akawa hawezi kuhimili thamani yake, bali inakusanya pia: Ikiwa ataweza kuhimili thamani yake lakini hawezi kuipata kwa kukosa kiungo kwa mfano, ndiyo masuala ya kukosekana sehemu.
Kwa maelezo hayo: Hakika asili ni kuwa hukumu inaondoka kwa kukosekana sehemu yake, lakini hili si jambo muhimu sana katika sura zote, katika baadhi ya sura hukosekana sehemu na kubakia hukumu, lakini kwa maelezo yenye nguvu zaidi kuliko kukosekana sehemu, wala haibadilishwi akili kufanyia kazi hukumu ikiwa sehemu yake haipo, lakini inabakia kuanisha kusudio kwa sehemu ya hukumu na kuangalia dalili zake ni katika jambo muhimu ili kuwezesha kufahamika athari ya kukosekana kwake kwenye hukumu, tofauti katika masuala ya utekelezaji wa kukosekana sehemu inarejea kwenye kuainisha dalili ya sehemu na kuyaendea masuala kwa kuwa kwake yanakusanya sehemu isiyokuwepo, au kisichokuwepo sio sehemu ya kufanyika hukumu, na hii ndiyo kazi ya mwanachuoni katika hali itakayotokea mbele yake, ili asije jichanganya na maana nyingine yoyote kwenye masuala ya kukosekana sehemu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi


 

Share this:

Related Fatwas