Hukumu ya Twalaka kwa Walii

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Twalaka kwa Walii

Question

Je! Inaruhusiwa kwa walii wa mtu ambaye ni mwendawazimu kumwachisha mke mtu huyo ikiwa talaka hiyo ina maslahi au inamwondolea madhara mwendawazimu huyo? 

Answer

Sifa zote njema ni za Allah pekee, na sala na salaam ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya jamaa zake na maswahaba zake, na juu ya wale wanaowafuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Imeamuliwa kwa mujibu wa Fiqhi kwamba vitendo vya wanadamu huzingatiwa kwa sharti la kuwa na akili timamu na kukubalika na kadhalika; Kwa sababu tabia ya vitendo hivi hutegemea dhamira sahihi, na hali hii iko tu pamoja na akili timamu.
Wataalamu waliobobea taaluma ya Usuulu (Misingi Mikuu ya Sheria) walisema katika vitabu vyao juu ya kinachojulikana kama “maafa ya akili”, ambayo ni: sababu zinazoathiri utimamu wa akili ya mtu, na walisema kwamba kati ya maafa hayo ni ya mbinguni - Hayo ni maafa ambayo mtu hana chaguo nayo:- kama vile wazimu, ambao ni: kutoweza kutofautisha kati ya vitu vizuri na vibaya ambavyo matokeo yake yanayojulikana hayaoneshi athari zake na vitendo vyake vina utata, kwa hivyo vitendo vyake havina athari za kisheria. [Sharh Al-Talwiih ala Al-Tawdhiih kwa Saad Eddin Al-Taftazani 2/331, Subih].
Kwa sababu ya kukosekana usawa, Sharia imethibitisha mamlaka ya uwalii juu ya mwendawazimu kwa mwingine; kwa ajili ya kuufanikisha ulinzi wake, na chini ya mamlaka haya, walii anabeba jukumu kamili la maswala yanayomuhusu mtu ambaye yuko chini ya uwalii huo.
Kati ya vitendo ambavyo walii anaweza kufanya ni: kumwozesha mwendawazimu ambaye yuko chini ya mamlaka yake; kwa maslahi ya hali ya usafi, au malazi, na hifadhi yake.
Imam An-Nawawiy alisema katika Ar-Rawdha [5/435, Dar Alam Al-Kutub]: “Ikiwa umri wa mwendawazimu ni mkubwa, hakuozeshwa sio kwa haja, na anaozeshwa kwa haja ya kuonesha hamu yake kwa wanawake, au kwamba anahitaji mtu anayemhudumia na hampati kati ya maharimu wake ambaye anaweza kufanya hivyo... au kwa kutarajiwa kupona kwake kwa ndoa, na ikiwa inaruhusiwa kumuozesha, atachukuliwa na baba, kisha babu, halafu sultani tu, kwa uwalii wa mali.
Kuhusu talaka, kanuni ya msingi ni kwamba talaka ni haki inayomilikiwa na mume peke yake. Kwa mujibu wa Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Majah kutoka kwa Ibn Abbas, R.A., kwamba Mtume S.A.W., alisema: “Talaka imepewa kwa mume peke yake tu.” Hakuna yeyote isipokuwa mume ambaye ndiye ana haki ya kumpa mkewe talaka isipokuwa akimpa ruhusa ya kufanya hivyo kwa mwingine, basi inaruhusiwa; Kwa sababu kanuni ya msingi ni kwamba mtu anafanya hivyo mwenyewe, lakini kanuni hii iko kwa watu wenye akili timamu tu. Kwa hivyo, mwendawazimu hawezi kumpa talaka ikiwa ana wazimu, na hali hii inaruhusiwa kama akipona; Na imepokelewa kutoka kwa Ali na Aisha, R.A. kwamba Mtume, S.A.W., alisema: “Wamesamehewa (watu wa aina) tatu aliyelala mpaka aamke, mtoto mdogo mpaka abaleghe, na aliyepungukiwa na akili mpaka zirudi.”
Wataaluma wa Fiqhi walitofautiana kuhusu: Je! Walii anaweza kumpa talaka mke wa mwendawazimu ambaye yuko chini ya mamlaka yake? Maoni ya wanavyuoni wa umma ni kwamba Walii hana haki hiyo, ambayo ni maoni ya Abu Hanifa, Imam Ash-Shafi na Imam Ahmad bin Hanbal pia.
Imam Al-Sarkhasi Al-Hanafi anasema katika kitabu chake cha: [Al-Mabsut 24/25, Dar Al-Marefa - Beirut]: “Kama mvulana atakuwa na mke, na baba yake au mtu baki akamwachisha kwa kumvua ndoa, au akamwachisha mke au akmwachia huru mtumwa wake, kisha mvulana huyo akajakutoa idhini ya kukubali hayo baada ya kuwa mkubwa na Mtu mzima, basi ni batili; kwa sababu hakuna wa Kujuzisha kitendo hicho wakati kinatokea, kwa hivyo talaka na kuacha huru ni madhara matupu kwake, kwa hivyo akili yake au uwalii wa walii wake havizingatiwi; Kwa sababu kuthibiti kwa uwalii juu yake ni kwa ajili ya kumtoshelezea faida yake tu na sio kwa ajili ya kumdhuru”.
Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Abu Hanifa walisema kwamba hukumu ya mwendawazimu wakati wa wazimu wake ni kama hukumu ya mvulana [kama inavyopatikana faida katikakitabu cha: [Radul Muhtaar kwa mwanachuoni Ibn Abdin 3/25, Dar Al-Kutub Al-Elmiyah]; Hii ni kwa sababu ya ushiriki wao tu katika kukosekana kwa akili, wazimu na utoto ni kati ya sababu zanazolazimisha kumzuia mali yake.
Sheikh Al-Islam Zakariya Al-Ansariy alisema katika kitabu cha: [Asna Al-Matalib] kutoka vitabu vya wanavyuoni wa madhehebu ya Imamu Shafiy [2/212, Darul Kitab Al-Islami]: “(Tawi: Mtoto hachukuliwi kama mlezi) ... na jaji na mdhamini wake ni kama mlezi, na mwendawazimu na mpumbavu ni kama mtoto ... (wala mkewe hatalikiwi); Kwa sababu talaka ni haki ya mume peke yake tu.
Al-Bhoutiy alisema katika kitabu cha: [Sharh Muntaha Al-Iradat] kutoka vitabu vya wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Ahmad Bin Hanbal [3/59, Alam Al-Kutub]: “(Na sio haki ya baba wa mdogo kumzuia) mumewe (kutokana na mali zake) kama wengine miongoni mwa mawalii; Kwa sababu hana haki ndani yake (vile vile baba wa mume mchanga au wazimu au (bwana wao), yaani kijana na mwendawazimu ( hana haki ya kuwataliki wao), maana: kijana na mwendawazimu; kufuatana na Hadithi inayosema: “Talaka amepewa mume peke yake tu.”.
Dalili ya usemi: kanuni ya msingi ni kwamba talaka iko mikononi mwa yule mume peke yake tu - kama inavyooneshwa na Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Majah - na kwa sababu walii hana haki ya kuondoa haki ya mwendawazimu; kama kusamehe kwa deni, na kuondoa ulipaji wa kisasi, na kwa sababu njia yake ni matamanio, kwa hivyo haikuingia katika suala la uwalii. [Al-Mughni 7/270, Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabi]
Baadhi ya wanavyuoni waliotangulia wamesema kuwa inaruhusiwa kwa walii kumtaliki mke wa mwendawazimu ambaye yuko chini ya mamlaka yake, ikiwa hiyo ni kwa manufa yake. Ataa alisema: “Walii wa mwendawazimu anaruhusiwa kumtaliki mkewe, na aangalie mpaka kupona.” Saeed Bin Al-Musayyib alisema: “Talaka ya mwendawazimu asiye na akili sio jambo, walii wake ndiye anaye haki ya kutaliki kwake” [Musanaf Ibn Abi Shaybah 4/27].
Pia ni maoni ya wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Malik; imetajwa katika mukhtasar Khalil wa Sharhih kwa mwanachuoni Al-Kharashi [17/17]. Dar Al-Fikr]: “Ni haki ya mume pekee yake kutaliki mkewe lakini mvulana na mwendawazimu hawana haki hii”.
Kuachana na mke ni talaka kwa mujibu wa maoni ya wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Maalik kama inavyojulikana. [Rejea; Mawahib Al-Jalil kwa Al-Hattab 4/19, Dar Al-Fikr, Sharhu As-Saghiir kwa Bw. Ahmed Al-Dardeer 51/2/2, na Hashiat Al-Sawy- Dar Al-Maaref].
Wanavyuoni wa madhehebu ya Imam Ahmad bin Hanbal wanaona kwamba inaruhusiwa kwa walii wa mwendawazimu kumpa talaka, lakini hukumu hii siyo kwa mawalii wote, lakini kwao hukumu hii inahusiana na baba na sio mwingine ambaye ana haki ya kuozesha; Kama walii wa baba na mtawala; Kwa sababu ni hali inayomnufaisha mwendawazimu ambaye ni mume tu, na inaruhusiwa kumiliki haki hii ili kuiondoa. [Al-Mughni 7/41, Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabiy, Matalib Uli An-Nuha Sharhu Ghayatil Muntaha kwa Al-Rahibani Al-Hanbali 5/164, Al-Maktab Al-Islami].
Lakini dalili hii inajibiwa kuwa ni kipimo badala ya matini - ambayo ni Hadith ya Ibn Majah iliyotajwa hapo juu – nacho ni kipimo kibofu.
Sheria ya kimisri haikutangaza katika vifungu vyake hukumu ya talaka ya walii wa mwendawazimu wa wale walio chini ya mamlaka yake, isipokuwa kwamba Fiqhi ya kisheria ilifuata rai ya wanavyuoni wa umma [Rejea: Mausuat Al-Fiq wal Qadhaa Fil Ahwal Al-Shakhasiyah kwa Muhammad Azmi Al-Bakri 4/20, Dar Mahmoud]; Katika muhtasari wa maelezo kuhusu marekebisho ya Sheria ya kifamilia Na. (100) kwa mwaka 1985, vifungu vya kisheria vinavyohusu Sheria ya kifamilia, ikiwa havijkutajwa, vitahukumiwa na maoni ambayo ni sahihi zaidi ya wanavyuoni wa madhehebu ya Abu Hanifa, isipokuwa kwa yale ambayo yametengwa kwa hilo.
Hii ndio iliyotajwa na Dar A-Iftaa (Ofisi ya kutoa Fatwa) nchini Misri hapo awali. Katika Fatwa iliyotolewa na Mufti wa zamani wa Misri na mkuu wa mabwana wa madhehebu ya Imam abu Hanifa kwa wakati wake Sheikh Bakri Al-Sadafiy Ijumaa ya kwanza ya 1328 AH ilisema kuwa: “Aliye na haki ya kutaliki ni: mume ambaye ni mtu mzima mwenye akili timamu aliyebaleghe aliyeamka, kwa hivyo hairuhusiwi kwa baba wa mtoto, au kwa mwendawazimu, au kwa mtu aliyelala. Au kwa mvulana kutaliki, hata kama akiwa kijana, na ikatajwa rai hii katika Fatwa nyingine ya Sheikh Hassan Mamoun, Mufti wa zamani, katika tarehe ya kwanza ya Ramadhani 1378 AH, na 10 Machi, 1959AD.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotangulia hapo juu: Walii hana haki ya kumtaliki mke wa aliyezuiliwa mali yake kwa sababu ya wendawazimu, na akiona hivyo, anaweza kupeleka jambo hili kwa jaji kwa kuzingatiwa, kwa sababu jaji pekee ndiye aliyepata haki ya talaka katika hali kama hiyo kama akihakikisha kile kinacholazimisha talaka kufuatana na Sheria.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Sekretarieti ya Fatwa


 

Share this:

Related Fatwas