Kubadili sifa ya Salamu ya Mtume S....

Egypt's Dar Al-Ifta

Kubadili sifa ya Salamu ya Mtume S.A.W., Kupitia Tahiyyatu Baada ya Kifo Chake.

Question

Mlinganiaji mmoja alikuja msikitini kwa ajili ya kutoa somo kwa waumini, wakati alikuwa na kitabu cha: “Irshaad As-Salikiin Ilaa Akhtaa Al-Musalliin” na Sheikh Mahmud Al-Masriy, ambaye alisema katika kitabu hicho kuwa: Salamu ya Mtume S.A.W., kupitia Tahiyyatu baada ya kifo chake itakuwa kwa tamko la: Salamu iwe juu ya Mtume, na siyo: Salamu iwe juu yako Ewe Mtume. Na akasema kuwa: badiliko hili la salamu limefanywa na Bibi Aisha, kwa mujibu wa wasia wa Mtume S.A.W. Je, badiliko hili ni sahihi? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwenye kusoma kitabu kilichotajwa [Uk. 126, Ch. ya Dar At-Taqwaa] tulikuta matini ifuatayo: “kauli yao: Salamu iwe juu yako Ewe Mtume…”, na tamko hili lilikuwa likitamkwa wakati wa maisha ya Mtume, lakini baada ya kifo chake Masahaba R.A., walikuwa wakisema: “Salamu iwe juu ya Mtume S.A.W.”.
Na kutoka kwa Ibn Masu’ud R.A., alisema: “Mtume S.A.W., alinifundisha Tahiyyatu, wakati kiganja changu kipo kati ya viganja vyake viwili, kama alivyokuwa kanifundisha Sura ya Qur'ani: Maamkizi yote na Swala zote na mema yote ni kwa Allah. Salamu iwe juu yako Ewe mtume… hali wakati Mtume S.A.W., alikuwa hai kati yetu, lakini alipofariki tukasema: Salamu iwe juu ya Mtume”.
Sheikh Al-Albaniy alisema: Kauli ya Ibn Masu’ud: “Salamu iwe juu ya Mtume” maana yake kuwa Masahaba R.A., walikuwa wakisema: “Salamu iwe juu yako Ewe Mtume” katika Tahiyyatu, hali ya kuwa Mtume alikuwa hai, na alipofariki walibadili hivyo, wakasema: “Salamu iwe juu ya Mtume”, na inapaswa kuwa hivyo ni kutokana na mwongozo wake S.A.W., na dalili yake kuwa Aisha R.A., alikuwa akiwafundisha Tahiyyatu hivyo hivyo kupitia Swala: “Salamu iwe juu ya Mtume”. Imepokelewa na As-Saraj katika Musnad yake; na Al-Mukhalis Fil Fawaid kwa mapokezi mawili sahihi kutoka kwake (Aisha)”. [Mwisho].
Na kabla ya kubainisha hukumu ya suala hili tunaweza kusema kuwa: Hakika hitilafu katika masuala ya Fiqhi ni jambo la kweli na kuamuliwa; kwa sababu hukumu nyingi zaidi za Fiqhi zinathibitishwa kwa njia ya dalili zilizodhaniwa, na dhana hizi aghalabu zinapelekea kupingana.
Ikiwa ni wajibu wa mwanazuoni kufuata ilivyoishia dahana yake, basi haina budi ya kuwepo hitilafu kwa mujibu wa dhana ya dalili, na hivyo basi Umma wote umekubali kikamilifu Usuli wa Dini unaowakilisha kitambulisho cha Uislamu; na hivyo ni kutokana na ulinzi wa Mwenyezi Mungu na ulezi wake kwa Dini hii mpaka Yeye airithi ardhi na kila kilicho juu yake.
Kwa hiyo hakuna hitilafu katika mambo yaliyoundwa kwa nguvu zaidi kidalili na kimaana, yaani kuyakubali ni lazima. Zaidi ya hayo hitilafu katika mambo ya matawi ni kwa ajili ya kurahisisha tu, hivyo basi Umma hauna dhiki ya kuchukua madhehebu maalumu, na kama kuna shida ndani ya madhehebu moja ambayo hupelekea dhiki, basi unaweza kuibadili kwa nyingine, kwa mujibu wa vigezo maalumu.
Sheikh Mahmud Shaltut katika kitabu chake: [Al-Islam A’aqidah wa Sharia’ah: Uk.550, Ch. ya Dar Ash-Shuruq] anasema: “Hakika kuamuliwa haki ya jitihada ya mtu binafsi au jamaa ilivyofungua mlango mpana zaidi kwa wachunguzi na wenye nadhari miongoni mwa wanachuoni wa kiislamu kuchagua sheria ambayo mambo ya jamii za kiislamu kutokana na hali zake mbali mbali hupangwa nayo, wakati hawana pingamizi lolote kuhusu chaguo zao isipokuwa kitu kimoja nacho ni kutopingana na asili miongoni mwa asili yenye nguvu zaidi ya Sharia, pamoja na kujali aina za masilahi na njia ya uadilifu; hivyo ilikuwa msingi wa kudumu kwa Sharia ya kiislamu na kufaa kwake kwa kila wakati na mahali”.
Licha ya hayo, shime ya wanazuoni kuwa hitilafu yao isije kwa ajili ya matamanio na inadi, walikuwa wakihojiana na wanawakosoa wengine kwa wengine bila kukemea, kutia ujinga, ugomvi, au ukali wa madhehebu unaogawanywa; kwani hayo yote ni miongoni mwa sura za ujinga kwa Sharia na kanuni zake, na historia ya Maimamu na kauli zao, wakati hitilafu zao haikuwaondoa kamwe na kushika adabu kuhusu kujadiliana na mambo haya ya hitilafu.
Hakika wanazuoni wa zamani na wa kisasa waliandika katika adabu ya hitilafu; na Sheikh Abdul Fattah Abu Ghuddah alikusanya kitabu kizuri kiitwacho: [Namadhij Min Rasail Al-Aimmah As-Salaf Wa Adabuhum Al-Ilmiy] ambapo alikusanya ndani yake kauli, habari na hadithi za wengi wa Wanazuoni wakubwa hawa, kubainisha adabu mbele ya mpingaji.
Na matendo ya wanazuoni katika masuala ya hitilafu hayakuwa kwa msimamo hasi tu, bali yamekwenda mbele zaidi kwa kuweka msingi uitwao Fiqhi ya Hitilafu, ambapo walianzisha ndani yake kanuni na vigezo ambavyo ni lazima kuviangalia.
Na miongoni mwa kanuni hizi: kutokanusha jambo lenye hitilafu, na maana yake kumlaumu mwingine au kumkataza kuitekeleza rai yake, kwa sababu inapinga rai yake mwenyewe; au kuunga kauli ya mwingine na kukanusha, kwa kutumia mambo matatu ya kukanusha ambayo yalitajwa katika Hadithi: yaani mkono, ulimi, na moyo, kwa madhumuni ya kubadilisha; au kuipinga kazi ambayo imekubalika na rai ya mwenye jitihada mashuhuri katika mambo haya ya hitilafu. Kwani kila suala ambalo lina hitilafu kwa mujibu wa rai za Maimamu na masharti yao, hapo haisihi kumshutumu huyu aliyechukua rai ya mmoja wao, na kuchochea matatizo kwa kuwa mtu faulani haoni ubaya kuitekeleza rai hii, wakati mwingine anaona ubaya kuitekeleza.
Na suala la kubadili sifa ya Salamu ya Mtume S.A.W., katika Tahiyyatu kutoka katika nafsi ya pili iwe nafsi ya tatu ni miongoni mwa masuala ya jitihada ambayo maono ya wanazuoni yanahitilifiana, kutokana na hitilafu ya kukubali dalili na kuielewa kwake. Basi suala hili siyo miongoni mwa masuala ya Ijmaa ambapo inapelekea kumshutumu aliyelipinga. Kama inapasa kwa wanaoshughulika kwa Ulinganiaji wachunguze mambo haya ya Usuli Jumuishi hata wasije kuwawajibisha watu watekeleze rai maalumu kuhusu suala ambalo maono yanahitilafiana nalo, na wanakanusha wanaowapinga. Na hivyo hivyo ilivyosemwa na Sheikh Al-Albaniy katika utangulizi wa kitabu chake: [Sifat Salat An-Nabii S.A.W.: Uk. 24, Ch. ya Dar Al-Maa’arif, Riyadh] na baada ya kueleza sifa ya salamu ya Mtume S.A.W., katika Tahiyyatu, alisema: “Kwangu jambo hili ni pana, na kwa tamko lolote miongoni mwa matamko yote yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W., mwenye sala atalisoma katika Sala, basi atafuata Sunna”.
Na kuhusu suala hili tunasema kuwa: Tahiyyatu ya mwisho ni nguzo miongoni mwa nguzo zote za Sala, na bila ya Sala itabatilika, na katika Vitabu Viwili Sahihi vya Sunna, kutoka katika Hadithi ya Ibn Masu’ud aliema: “Tulikuwa tukiswali nyuma ya Mtume S.A.W., tukasema: Salamu iwe juu ya Jibrili, Mikaili, Salamu iwe juu ya fulani na fulani, na Mtume S.A.W., akageuka upande wetu, akasema: Hakika Mwenyezi Mungu ni salamu, na mtu yeyote kati yenu akiswali atasema: Maamkizi yote na Swala zote na mema yote ni kwa Allah. Salamu iwe juu yako Ewe Mtume na Rehema na Baraka za Allah. Salamu iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allah”. Na tamko la Ad-Daraqutniy na An-Nasaiy ni hivyo: “Tulikuwa tukisema katika swala kabla Tahiyyatu haijakuwa faradhi…”. Na isnad ya mapokezi mawili ni sahihi.
Pia matini ya Tahiyyatu ilipokelewa kutoka katika Hadithi ya Ibn Abbas, Ibn Omar, Aisha, Jabir Ibn Abdillahi, Abu Bakr, na wengineo, na baadhi ya mapokezi kuna hitilafu ya baadhi ya matamko. Na Imamu An-nawawiy katika kitabu cha [Al-Majmuu’: 3/437] baada ya kutaja Hadithi za Tahiyyatu, anasema: “Hadithi zote ni sahihi, na Imamu Shafi na wanazuoni wa madhehebu walisema: Tamko lolote lisomwe na mwenye sala litatosha, na wanazuoni walikubali pamoja kuwa: Inajuzu kusomwa kwa Tamko lolote kati ya matamko yote, na kunukuliwa Ijmaa na Kadhi Abu At-Tayib”.
Katika baadhi ya mapokezi ya Ibn masu’ud kuna ziada: “Wakati yeye yuko hai kati yetu, na alipofariki tukasema: Salamu, yaani iwe juu ya Mtume S.A.W. Na mapokezi ya Ahmad na Al-Baihaqiy katika kitabu cha:[ Al Fatawa Al-Kubra] na Ibn Abi Shaibah kwa tamko la: “Na apofariki tukasema: Salamu iwe juu ya Mtume” bila neno la (yaani); na ziada hii ilipokelewa, bila yaani, kutoka katika Hadithi ya Ibn Omar na Aisha, hivyo Hadithi ya Ibn Omar kama ilivyotajwa na Imamu Malik, Kitabu cha Sala, Mlango wa Tahiyyatu katika Sala, na Al-Baihaqiy katika [Al-maa’rifah]; na Hadithi ya Aisha iliyopokelewa na Ibn Abi Shaibah na Al-Baihaqiy katika kitabu cha:[ Al Fatawa Al-Kubra]
Na ilipokelewa na Abdur-Razzaq, kutoka kwa Ibn Juraij, kutoka kwa A’ataa, alisema: “Nilisikia Ibn Abbas, Ibn Az-Zubair wakisema katika Tahiyyatu ndani ya Sala: Maamkizi yenye Baraka ni ya Allah, Sala nzuri ni za Allah, Salamu iwe juu ya Mtume…”
Na Imamu Ibn Hajar baada ya kuitaja ziada hii anasema: “As-Subkiy katika Sahrh Al-Minhaj baada ya kutaja upokezi huu kutoka kwa Abu U’uwanah peke yake, anasema: “Ikiwa hii ni sahihi kutoka kwa Masahaba basi ni dalili ya kuwa kutumia nafsi ya pili katika Salamu, baada ya Mtume S.A.W., siyo wajibu, kwa kusemwa: Salamu iwe juu ya Mtume. Na mimi nasema: Hakika hii ni sahihi, na nimekuta dalili yenye nguvu. Abdur-Razzaq anasema: “Ibn Juraij alituambia, A’ataa aliniambia kuwa: masahaba walikuwa wakisema hali ya kuwa Mtume yupo hai: Salamu iwe juu yako Mtume, lakini alipofariki wakasema: Salamu iwe juu ya Mtume. Na Isnad hii ni sahihi”. [Fat-h Al-Bariy: 2/314, Ch. ya Dar Al-Maa’rifah].
Na ziada hii iliyotajwa inawajibisha kuwa salamu ya Mtume S.A.W., itakuwa kwa kutumia nafsi ya tatu, siyo nafsi ya pili, lakini hii siyo lazima. Na maelezo yake ni: ziada hii iliyotajwa na Al-Bukhariy siyo maneno ya Ibn Masu’ud, lakini ni maneno ya Al-Bukhariy kwa njia ya maelezo, na maneno yake haya siyo lazima kwa sababu inawezekana kuwa: makusudio ya maneno ya Ibn Masu’ud ni: “Tukasema: Salamu” yaani tukasalimia Mtume S.A.W., katika Tajiyyatu baada ya kifo chake mfano wa tulikuwa tukifanya hali ya uhai wake; na maana ya hayo kutoanguka salamu katika Tahiyyatu kutokana na kifo chake S.A.W.. Na ijapokuwa maelezo haya ni mbali kidogo lakini yangewezekana.
Zaidi ya hayo: Imamu Al-Bukhariy hakuweka upokezi huu katika mahali pake pa kufaa, kwa sababu Al-Bukhariy alipokea Hadithi ya Tahiyyatu katika mahali saba pa kitabu chake Sahihi; tatu miongoni mwake zinahusiana na sala [Nambari: 831-835-1202]; na mbili zinahusiana na kutaka idhini [Nambari: 6230-6265]; na moja inahusiana na Dua [Nambari: 3628]; na moja inahusiana na Upwekeshaji [Nambari: 7381].
Na upokezi huu wenye ziada ulitajwa katika Mlango wa Kutaka Idhini, Mlango wa kushikana mkono, kwa sababu ya kauli ya Ibn Masu’ud: “wakati kiganja changu kipo kati ya viganja vyake viwili. Na Kazi hii ya Imamu Al-Bukhariy siyo ya bahati tu, lakini ina zingatio maalumu, ambalo linaashiriwa mfano wake na Al-Hafidh katika kitabu cha [Al-Fat-h: 6/635] ambapo anasema: “Huenda Hadithi hii inaambatana na Sharti la Bukhariy, lakini inapingwa kwa lililopaswa kutendwa kutokana na Hadithi nyingine, kwa hiyo Imamu Al-Bukhariy hakupokea Hadithi hii katika Mlango wake hasa, bali ameipokea katika Mlango mwingine usiojulikana, ili kutanabahisha kuwa Hadithi ni Sahihi lakini madhumuni yake ya dhahiri hayakutekelezwa kwake. [Kwa muhtasari kutokana na maneno ya Mwalimu Muhammad A’awwamah katika uhakiki wake wa Mtunzi Ibn Abi Shaibah].
Kwa mujibu wa hayo tunasema kuwa: Imamu Al-Bukhariy haoni hitilafu ya kumswalia Mtume S.A.W., katika Tahiyyatu, hali ya uhai wake au kufariki kwake.
Kwa kuchukulia kuwa msemaji ni Ibn Masu’ud, kama ilivyo katika mapokezi yaliyotangulia nje ya Bukhariy, basi inapaswa kuwa amesema hivyo kwa njia ya jitihada, na siyo kwa njia ya dalili, hasa ziada hii haikusemwa ispokuwa kwa ulimi wa Masahaba watatu- Ibn Masu’ud, Ibn Omar na Aisha, pamoja na kuwepo hitilafu ya Hadithi ya Ibn Masu’ud kutoka katika Hadithi ya wawili wengine, kama itakavyokuja- ingawa Tahiyyatu ni sehemu ya Sala ambayo ni nguzo muhimu zaidi ya Dini baada ya Shahada Mbili. Na ikiwa jambo hili ni amri ya lazima, hapo hatusemi kushurutisha mapokezi yenye nguvu zaidi ya upande huu, lakini kwa ngazi ya chini haina budi ya kuwepo mengi, na matokeo yake Salamu kwa kutumia nafsi ya pili baada ya kifo cha Mtume S.A.W., sio wajibu.
Na Imamu Ibn Abdul Bar katika kitabu cha [Al-Istidhkar: 1/485, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyah] anasema: “Niliyoisema kuwa: hitilafu katika Tahiyyatu, Adhana, Iqama, idadi ya Takbira ya Jeneza na linalosomwa na kutolewa dua ndani yake, idadi ya Takbira ya Sala Mbili za Idi, kuinua mikono katika Rukuu ya Sala na Takbira ya Jeneza, Salamu ya Sala ni moja au mbili, kuweka mkono wa kulia juu ya kushoto katika Sala, kuacha mikoko huru, dua ya Kunuut au kuacha kwake, na hii yote ni mifano ya Hitilafu Mubaha, kama vile udhu mara moja, mbili, au tatu.
Lakini wanazuoni wa Hijaz na Iraq, ambao wao na wafuasi wao ni wahusika wa kutoa Fatwa, wanapinga ziada ya Takbira Nne kuhusu jeneza, na wakakanusha hivyo. Na hii haina dalili; kwa sababu Salaf walifanya Takbira saba, nane, sita, tano, nne, na tatu…
Na hilo nililoeleza hakika wanazuoni wote walilinukulu kutoka kwa waliotangulia mpaka waliowafuata, na wakalinukulu Tabiina kwa wema kutoka kwa waliowatangulia, kwa njia sahihi bila makosa wala usahaulifu; kwa sababu ni vitu dhahiri na vilitekelezwa ndani ya Miji ya Kiislamu zama hadi zama, na watu wote, wakiwa wanazuoni au wa kawaida hawana hitilafu juu ya vitu hivyo, kuanzia enzi ya Mtume wao S.A.W., hadi leo. Na hii inaonesha kuwa mambo haya yote ni mubaha kwa njia ya faraja na rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, walhamdulillahi”.
Hapo Ibn Abdul Bar anajaalia hitilafu kuhusu maneno ya Tahiyyatu iwe ya kukubalika, ambapo haijuzu kutilia mkazo wa baadhi yao na kukanusha wengine.
Na miongoni mwa linalotegemeza kuwa maneno ya Ibn Masu’ud yatolewe kutokana na rai na jitihada siyo na dalili nguvu kuwa: Omar Ibn Al-khatwab R.A, alikuwa akiwafundisha watu Tahiyyatu ya Sala, wakati alipokuwa juu ya membari na Masahaba wakihudhuria.
Imamu malik katika kitabu cha: [Al-Muwatta’] na Ibn Abi Shaibah katika kitabu cha:[Al-Muswanaf] walipokelea kwa Isnad yao, kutoka kwa Ibn Shihab Az-Zuhriy, kutoka kwa U’urwah Ibn Az-Zubair, kutoka kwa Abdur-Rhman Ibn Abdil Qariy kuwa: yeye alisikia Omar Ibn Al-Khatwab , akiwa juu ya membari, akiwafundisha watu Tahiyyatu, akisema: “Semeni: Maamkizi yote ni ya Allah, kazi nzuri zote ni za Allah, mema yote, Sala zote ni za Allah, Salamu iwe juu yako Ewe Mtume na Rehema na Baraka zake, Salamu iwe juu yetu Waumini na Waja wema wa Allah, Nashuhudia kuwa hakuna Mungu ila Yeye tu, nashuhudia kuwa Muhammad ni Mja wake na Mtume wake.
Ibn Al-Arabiy katika [Al-Qabas: 1/204, Ch. ya Dar Al-Gharb, Bairut, Ch. ya Kwanza, 1992] kupitia maelezo yake ya Hadith ya Omar anasema: “Malik RA, alitaja katika Mlango huu Tahiyyatu ya Omar Ibn Al-Khatwab RA, na akatilia nguvu zaidi kuliko ya Tahiyyatu ya Ibn Abbas na Tahiyyatu ya Abdillahi Ibn Masu’ud; kwa sababu Omar Ibn Al-Khatwab RA, alikuwa akiwafundisha watu Tahiyyatu hii, akiwa juu ya membari na kuifundisha kwa Waislamu hadharani, nao ni Masahaba, kati yao Ibn Abbas na Abdullahi ambao ni wapokeaji wa mwisho wa Tahiyyatu, na hakusikia upingaji na mtu yeyote, kwa hiyo hii ni Ijmaa yenye nguvu zaidi”.
Na Ibn Abdul bar katika [Al-Istidhkar: 1/484, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Ilmiyyah, 1421 H., 2000] anasema: kukubali kwao hivyo na Omar, pamoja na kuwepo hitilafu ya mapokezi yao kutoka kwa Mtume S.A.W., ni dalili ya kuwa mubaha na faraja kwa ilivyopokelewa naye S.A.W., pamoja na kuwa mapokezi yote ni karibu ya maana yenyewe kwa yenyewe, na huenda kuna neno ziada au neno pungufu”.
Dalili hapa kuwa: Omar alitaja Tahiyyatu wakati Masahaba wakihudhuria, na hakuna kutumia nafsi ya tatu katika salamu ya Mtume S.A.W., ya Tahiyyatu, na ikiwa tamko la nafsi ya tatu lina dalili ya nguvu basi Masahaba waliosikia maneno yake wangetanabahisha. Na Ibn Abi Shaibah katika [Al-Musanaf] na At-Tahawiy katika [Sharh Maany Al-Athaar] walipokea kwa Isnad Dhaifu, kutoka kwa Ibn Omar kuwa: Abu Bakr alikuwa akiwafundisha Tahiyyatu wakati aikwa juu ya membari, kama anavyowafundisha watoto shuleni: “Maamkizi yote, Sala zote, Mema yote ni ya Allah, Salamu iwe juu yako Ewe Mtume, na Rehema ya Allah na Baraka zake… n.k.”.
Inapaswa kutanabahisha kuwa: kuna tofauti kati ya ziada iliyotajwa katika Hadithi ya Ibn Masu’ud na ilivyopokelewa na Ibn Omar na Aisha; na Hadithi ya Ibn Omar na Aisha haina dai la tofauti kati ya maisha ya Mtume S.A.W., na kifo chake, bali ni Tahiyyatu ya hali mbili, kinyume cha Hadithi ya Ibn Masu’ud ambapo kuna dai la tofauti kati ya hali hizi mbili. Na kwa mujibu wa hayo, anayetegemea Hadithi ya Ibn Omar na Aisha kwamba kuna tofauti, basi analazimika kwanza kuthibitisha kuwa tofauti hii ndiyo inatakiwa.
Na kwa kuongeza kuwa imepokelewa na Ibn Omar na Aisha tamko la kutumia nafsi ya pili katika salamu ya Mtume S.A.W.; Al-Baihaqiy alipokea katika kitabu cha: [As-Sunan] kwa Isnad yake, kutoka kwa Abu Bishr alisema: “Nilisikia Mujahid akizungumzia kutoka kwa Abdillahi Ibn Omar, kutoka kwa Mtume S.A.W., katika Tahiyyatu: “Maamkizi yote ni ya Allah, Sala zote na Mema yote, Salamu iwe juu yako Ewe Mtume na Rehema ya Allah”. Na katika [Al-Musanaf] na Abdur Razzak, kutoka kwa Ibn Juraij alisema: Nilimwambia Nafii’: Vipi Ibn Omar alikuwa akisoma Tahiyyatu? Akasema: Alikuwa akisema: “Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Maamkizi yote ni ya Allah, Sala zote ni za Allah, Kazi nzuri zote ni za Allah, Salamu iwe juu yako Ewe Mtume na Rehema ya Allah na Baraka zake… n.k.”.
Na Imamu Malik alipokea kutoka kwa Abdur Rahman Ibn Al-Qasim, kutoka kwa Babake, kutoka kwa Aisha akisoma Tahiyyatu, alikuwa akisema: “Maamkizi yote, Mema yote, Sala zote, Kazi nzuri zote ni za Allah, Nashuhudia kuwa hakuna Mungu isipokuwa Allah, peke yake, bila mshiriki, na kuwa Muhammad ni Mja wake na Mtume wake, Salamu iwe juu yako Ewe Mtume, na Rehema ya Allah na Baraka zake… n.k.”. Na mfano wa pokezi hili ulitajwa na Al-Baihaqiy katika [Al-Maa’rifah] na [Al-Kubra].
Na kwa mujibu wa hayo ziada hii ya Ibn Masu’ud haifuatwi isipokuwa kupokelewa na Ibn Hajar kutoka njia ya Abdur Razzaq: Ibn juraij alituambia, A’ataa aliniambia kuwa: Masahaba walikuwa wakisema, hali ya Mtume S.A.W., yupo hai: Salamu iwe juu yako Ewe Mtume, na alipokufa wakasema: Salamu iwe juu ya Mtume. Alisema: “Hii ni Isnad Sahihi”. Na Isnad hii ilitajwa katika [Kanz Al-U’ummal], na akainasibisha kwa Abdur Razzaq, na bila shaka hii ni kauli wazi kutoka kwa Ibn Juraij kuwa ameisikia.
Na katika [Tahdhib At-Tahdhib, na Ibn Hajar: 2/617, Ch. ya Muassasat Ar-Risalah]: “Abu Bakr Ibn Khaithamah alisema: Ibrahim Ibn A’ara’arah alituambia kutoka kwa Yahya Ibn Said, kutoka kwa Ibn Juraij alisema: Nikisema: (A’ataa alisema) basi mimi niliisikia kutoka kwake, hata nisiposema: (Nilisikia)”.
Kwa hiyo haisihi kutia shaka katika Hadithi kwa dai la kukosoa Ibn Juraij, lakini lililotajwa katika [Al-musanaf] Nakala ya kuchapishwa: “Ibn Juraij kutoka kwa A’ataa” hivyo hivyo kwa kutumia tamko la (kutoka kwa).
Huenda huyu aliyekosoa Isnad alilitegemea upokezi wa Nakala ya kuchapishwa, na akasema haitegemewi tamko la (kutoka kwa) kuhusu mpokeaji mwongo, hata akiwa na kuwasiliana moja kwa moja na wapokeaji wengine; na aliyeisahihisha alitegemea kauli wazi ya kusikia ambayo ilitajwa katika upokezi wa Ibn Hajar katika [Al-Fat-h] pamoja ya kauli ya Ibn Juraij katika [Tahdhib At-Tahdhib].
Lakini ingawa Ibn Hajar alisahihisha Isnad- ambapo huimarisha upokezi wa Abu Maa’mar Abdullahi Ibn Sakhbarah- tunaona baadhi ya Wahifadhi kama vile At-Tahawiy katika [Sarh Al-Mushkil] alitoa hukumu kuwa ziada hii iliyopokelewa na Abu Maa’mar siyo ya kawaida.
Na wengi wa Marafiki za Ibn Masu’ud wamepokea Hadithi ya Tahiyyatu, na ziada hii haikutajwa katika Hadithi yo yote yao. Na miongoni mwao: Abu Wail Shaqiq Ibn Salamah, na Hadithi yake imepokelewa na Bukhariy, na njia yake ni nyingi ndani ya Sahihi na nyinginezo; na A’alqmah Ibn Qays, na Hadithi yake imepokelewa na Ibn Hibban, At-Tabaraniy katika [Al-Kabiir], na Al-Baihaqiy katika [Sunan], na Abdur Razzaq katika [Al-Musanaf] na wengineo; na Al-Aswad Ibn Yazid na Hadithi yake ni ya At-Tirmidhiy na mwingine; na Abul Ahwas Al-Jushamiy na Hadithi yake ni ya At-Tabaraniy katika [Al-Kabiir] na Abdur Razzaq katika [Al-Musanaf].
Pia Tahiyyatu imepokelewa na Ibrahim An-Nakhi’iy- naye ni miongoni mwa wanafunzi wa Ibn Masu’ud- bila ziada hii, vile vile At-Tahawiy aliipokea kwa Isnad Sahihi kuwa: Abullahi Ibn Masu’ud alimfundisha A’alqamah Tahiyyatu bila ziada ya upokeai wa Abu Maa’mar.
Kw mujibu wa hayo yote At-Tahawiy aliamua kuwa ziada hii ya upokezi wa Abi Maa’mar ni kukanushwa, pia At-Tahawiy alitoa dalili ya kutotambua matumizi ya nafsi ya tatu kwenye Salamu ya Tahiyyatu, akisema: “Vipi inajuzu Kutoa Salamu ya Mtume S.A.W., baada ya kifo chake mfano uleule wa kumsalimia hali yuko hai?
Akajibu kuwa: Abu U’ubaid alitaja kutoka kwa Ibn U’uyainah kuwa: Miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu alimtukuza Mtume wake S.A.W., akamjaalia neema ya kusaliwa baada ya kifo chake mfano uleule hali ya uhai wake, na hili ni jambo jema.
Na baadhi ya wanazuoni waolitoa maana kama hii kutoka katika maneno ya Mtume S.A.W., nayo ni: alivyotuambia Yunus alisema: Ibn Wahb alituambia kuwa: Malik alimwambia kutoka kwa Al-A’alaa Ibn Abdur Rahman, kutoka kwa Babake, kutoka kwa Abu Harairah RA, kuwa: Mtume S.A.W., alitoka kwenye Makaburini, na akasema: “Salamu iwe juu yenu Enyi watu waumini wa Nyumba, hakika sisi tutakutana nanyi. Natamani lau ningaliwaona Ndugu zetu”. Walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je, sisi si ndugu zako? Akasema: “Ninyi ni Masahaba zangu, na ndugu zangu ambao watakuja baadaye, na mimi nitawatangulia katika Hodhi.
Katika Hadithi hii, Mtume S.A.W., amewasalimia watu wa Makaburini wakiwa wafu, kama alivyokuwa akiwasalimia wakiwa hai, na ikiwa hivyo ni S.A.W. kuhusu watu wa Makaburini, itakuwa S.A.W. kabisa kuhusu Mtume S.A.W., na hii ni maana njema kabisa. [Sharh Mushkil Al-Athaar: 9/415, kwa maelezo machache, Ch. ya Muassasat Ar-Risalah, Ch. ya kwanza, Mwaka 1994].
Na muhtasari wa hayo ni kwamba: Tamko la Salamu ya Mtume S.A.W, kwa kutumia nafsi ya tatu katika Tahiyyatu ya Sala siyo wajibu, na anayeitumia hatakuwa na kosa, na anayeiacha pia hatakuwa na kosa.
Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Zaidi.

 

Share this:

Related Fatwas