Udhibiti wa Uzingatio wa Kutokubali...

Egypt's Dar Al-Ifta

Udhibiti wa Uzingatio wa Kutokubaliana.

Question

Kulikuwa na maoni mengi kati ya kikundi cha wanaoswali na Imamu wa msikiti ambao ninaswali, kwa sababu ya kusoma dua ya qunuti ya Imamu katika Swala ya Alfajiri, ambapo Imamu anaona kwamba dua ya qunuti ni Sunna, wakati ambapo kikundi cha wanaoswali hawakubaliani naye katika hili, na jambo hilo lilizidi hadi kutokea mgawanyiko kwa wanao swali baada ya kundi hilo kuamua kutoswali nyuma ya Imamu huyo katika Swala ya Alfajiri baada ya kuamua Imamu kuendelea kuomba dua ya qunuti, na jambo hilo halikuishia hapo tu, bali baadhi ya wanaoswali walijaribu kuvuta idadi kubwa zaidi ya wanaoswali msikitini kwao na kuwashawishi wasiswali nyuma ya Imamu huyo.
Swali:
Je! Msimamo wa Imamu anayeshikilia kusoma dua ya qunuti ni sahihi ingawa mgawanyiko huu katika safu ya wanaoswali haswa kwa kuwa jambo hilo - yaani kusoma dua ya qunuti - ni Sunna tu ambayo haibatilishi Swala kwa kuiacha, na kudumisha umoja na kutokuwepo kwa mfarakano ni miongoni mwa mambo ya wajibu?
 

Answer

Sifa zote njema ni za Allah pekee, na swala na salaam ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu, na pia juu ya jamaa zake na maswahaba zake, na juu ya wale wanaomfuata kwa kwa wema mpaka Siku ya Malipo:
Wanachuoni wa Fiqhi hugawanya masuala ya Fiqhi katika masuala waliokubaliana na masuala `waliotofautiana, na dua ya qunuti katika Swala ya Alfajiri ni miongoni mwa masuala waliotofautiana na ambayo kuna maoni mengi juu yake, kama masuala mengine katika enzi hii, hadi ulipoondolewa kwenye mifumo yake utata ambao wanachuoni waliujadili, na labda miongoni mwa sababu muhimu zaidi ni kutokuwepo vidhibiti – na ukweli ni kwamba kutokuwepo kwa vidhibiti ni tabia miongoni mwa tabia za enzi hii – na kinachosababisha ukosefu huu ni kwamba baadhi ya vidhibiti hivyo viko katika nafsi ya mwenye jitihada ambaye maneno yake hayakuelezea kutokuwepo kwa vidhibiti hivi, na hali hii inabainisha kuwa hatukupata kitabu kamili kinachojumuisha mada hii, lakini ni dondoo, ambazo zingine zinahitaji juhudi nyingi, haswa kwani vidhibiti hivi ni nguzo ambayo Fatwa huizungukia katika kila enzi, au angalau ni moja ya vifaa vyake.
Vidhibiti hivi, kwa kweli, inawezekana kuvifanya misingi au adabu za kutofautiana, na moja ya sifa muhimu zaidi za vidhibiti hivi ni kwamba baadhi ya vidhibiti hivi vinaeleweka kwa kuzingatia vingine.
Miongoni mwa misingi au adabu hizi ni yaliyosemwa na wanachuoni wa Fiqhi kama vile wanachuoni wa madhehebu ya Imam Maliki, Shafiy, Hanafi na Hanbali kwa kusema kwamba ni bora zaidi kuzingatia hali ya kutofautiana. Kwa kweli, baadhi ya wanachuoni wa madhehebu ya Imam Maliki wamefanya msingi huu kutokana na dalili ambazo wanachuoni wa madhehebu ya Imam wanazitegemea katika kushughulikia hali halisi, vile vile msingi huu unaelezewa kama (misingi ya madhehebu), hadi Ibn Arafah alichukulia kama moja ya faida za madhehebu hii.
Wanachuoni wengi wa Fiqhi na wenye jitihada wengi walisisitizia msingi huu na waliufanyia kazi kwenye masuala mengi yenye utata, kuonesha kwamba maana hii ilikuwa imejikita katika akili zao. Kutoka kwa wanachuoni wa madhehebu ya Imam Abu Hanifa ni: Imam Ibn Nujaim, Ibn Al-Humam, Ibn Abidin, na kutoka kwa wanachuoni wa madhehebu ya Imam Shafiy ni:
Imam Al-Zarkashiy, Al-Ezz Bin Abd Al-Salam, na Al-Taj As-Subkiy, Al-Suyutiy, na kutoka kwa wanachuoni wa madhehebu ya Imam Ahmad ibn Hanbal ni: Al-Muwaffaq Ibn Qudamah na Al-Bhoutiy, na wengine – [Rejea: Al-Bahr Al-Raeeq 1/52, Ch. ya Dar Al-Kitab Al-Islamiy, na Fatah Al-Qadeer 3/151, Ch. ya Dar Al-Fikr, Al-Dur Al-Mukhtar (1/147) (3/8), Ch. ya Dar Al-Fikr, Al-Dur Al-Manthur kwa Al-Zarkashi 2 / 127-128), Ch. ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Nchini Kuwait, Al-Qwaid Al-Kubra kwa Al-Ezz Ibn Abdul Salam 1/370, Ch. ya Dar Al-Qalam, na Al-Ashbah wal-Nadhaer kwa Al-Suyutiy uk. 136, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyah, na Al-Ashbah wal-Nadhaer kwa Al-Subki 1 / 110-111, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Almiyyah, na Al-Mughni 1/135) (2/11), Ch. ya Dar Al-Fikr, na Sharhul Muntaha 1/16, Ch. ya Alam Al-Kutub]-. lakini, wanaweza kuelezea msingi huu kwa kusema kuwa: Kutoka kwenye kutofautiana, kwa kuwa ni miundo miwili ya maana moja, tofauti na ile inayoweza kuwa ya kawaida kuhusu tofauti kati ya misimgi hii miwili
na uhusiano wao na Wanachuoni wa madhehebu ya Imam Malik, na labda sababu ya tuhuma hii ni kile ambacho baadhi ya Wanachuoni wa madhehebu ya Imam Maliki walichotaja, kama Ibn Arafa na Al-Shatibiy, kuhusu ufafanuzi wa kuzingatia kutofautiana, kama Ibn Arafa anavyosema katika ufafanuzi wake: “Utekelezaji wa dalili katika maana yake ambayo dalili nyingine iilitekelezwa”- [Hudud ya Ibn Arafa na ufafanuzi wake kwa Ar-Rasaa (uk. 177), Al-Maktaba Al-Ilmiyah nchini Tunisia] -.
Al-Shatibiy anasema katika ufafanuzi wake pia: "Kuipatia kila moja, yaani dalili za kauli mbili kile kinachohitaji dalili nyingine au baadhi ya kile kinachohitaji ni maana ya kuzingatia kutofautiana.” – [Al-Mwafaqaat 5/107, Ch. ya Dar Ibn Affan] - na kulingana na maana ya fafanuzi hizi mbili, maoni ya Wanachuoni wa madhehebu ya Imam Malik waliotangulia, kama vile Imam Al-Qibab – [Al-Miyar Al-Muarab kwa Al-Wanshrisi 6/388, Ch. ya Wizara ya Wakfu ya Moroko] - na maana yake ni kwamba mwanafiqhi anatekeleza dalili ya asiyekubaliana naye kwa maana ya dalili ya asiyekubaliana naye, kama vile kusema, kwa mfano: kuthibitisha urithi kati ya wanandoa wa Shighaar (Ni aina ya ndoa iliyoharimishwa nayo ni kumuozesha mtu binti yake mtu mwingine kwa sharti kwamba mtu huyo naye amuozeshe yeye binti yake, na hakuna mahari baina yao) wakati mmoja wao anapofariki, ingawa anasema kutoruhusiwa kwa ndoa hii ikifanyika, kwa hivyo hii ilikuwa sababu ya kusema kuwa wanachuoni wa madhehebu ya Imam Malik hawatazingatia kutofautiana ila baada ya kutokea - ambayo ni, baada ya kutokea kwa suala linalobishaniwa - isipokuwa kwamba kwa maelezo mafupi ya matawi yaliyotajwa na wanafiqhi wa madhehebu ya Imam Malik, inadhihirika vinginevyo, na kwamba wanachuoni wa madhehebu ya Imam Malik, kama wanafiqhi wengine wa madhehebu matatu, huzingatia kutofautiana kabla na baada ya tokeo hilo.
Wanafiqhi na wanachuoni wanakubaliana kwamba inapendekezwa kushughulikia maswala yenye utata, lakini pendekezo hili linaweza kupunguzwa au kudhibitishwa kulingana na pingamizi la suala linalozungumziwa, na matini juu ya hayo ni mengi, na kati ya hayo ni yale yaliyotajwa na Al-Zarkashi aliposema: “kutofautiana kunahusiana na majadiliano: Kwanza: Inastahili kutoka kwake.”. – [Al-Mathnour 12/7] - na Al-Ezz Ibn Abd Al-Salam anasema: “Ikiwa dalili zimefanana katika kutofautiana kote ambapo kauli ya yule ambaye ametofautiana iko mbali nayo, basi inashauriwa kutoka kwenye hali hii ya kutofautiana.” – [Al-Qaweed Al-Kubra (1/370)] - Ibn Abdin anasema: “Na hali ya kuzingatia kwa kutofautiana inahitajika kwetu.” – [Radul Muhtaar (1/131)] - Ibn Abdin ananukuu kutoka kwa mwenye kitabu cha [Al-Nahr Al-Faiq] akisema: “viwango vya kusisitiza (An-Nadbu) vinatofautiana kulingana na nguvu na udhaifu wa dalili ya asiyekubaliana.” – [Radul Muhtaar (1/147)] - .
Na mafunzo yanayopatikana kutokana na maelezo ya wanafiqhi na wanachuoni ni kwamba maana ya kuzingatia katika kutofautiana au kutoka ni: kufuata muktadha wa kutofautiana, au kutekeleza dalili ya mpinzani wake, na maana yake ni: kupanga athari za kutenda pamoja na hukumu juu yake kwa kutoruhusiwa kwake, au kwamba yeyote anayefikiria kwamba jambo hili ni halali anaacha kulifanya ikiwa mtu mwingine anafikiria kwamba ni marufuku.
Vivyo hivyo, kwa upande wa uwajibu, inapendekezwa kwa yule anayefikiria kwamba kitu kinaruhusiwa kukifanya ikiwa kuna mmoja kati ya maimamu ambaye anafikiria kwamba kitu hicho ni wajibu. Dalili inayothibitisha ukweli wa kauli hii ni Hadithi ya Aisha, R.A., aliposema: "Utba Bin Abi Waqqaas alimuusia ndugu yake Sa`ad Bin Abi Waqqaas akamwambia, “Mtoto aliyezaa naye Waliydah (mjakazi) wa Zam`ah ni mwanangu, muweke kwako umuangalie”.
Ulipofika mwaka wa ufunguzi (wa Makka) Sa`ad bin Abi Waqqaas akamchukua (mtoto) akasema, "Mtoto wa ndugu yangu, naye aliniusia mimi nimuwangalie”. Abdu bin Zam`ah akasema, "Huyu ni ndugu yangu ni mtoto wa Waliydah (ni mtoto wa mjakazi wa) baba yangu amezaliwa juu ya kitanda chake”. Wakaongozana kwenda kushtakiana kwa Mtume S.A.W. Sa`ad akatoa hoja zake, na Abdu bin Zam`ah akatoa hoja zake. Mtume S.A.W. akasema: “Yeye ni wako ewe Abdu bin Zam`ah! Mtoto ni wa mwenye kitanda alichozaliwa (yaani wa mwanaume), na kwa mzinifu mwanamke ni (kupigwa) mawe”.
Kisha akamwambia mkewe Sawdah Bint Zam`ah. Kisha akamwambia Sawda binti Zam’ah, mke wa Mtume, S.A.W.: “Jifunike asikuone ewe Sawdah” Alipomuona alikuwa amefanana na Utba”.
Bibi Aisha R.A. akasema, "Tokea hapo yule mtoto hakumuona tena (Sawdah) mpaka kufa”. (Hadithi hii Mutafaq alayhi).
Nabii Muhammad S.A.W., alijali na kuzingatia hukumu zote mbili, hukumu ya kitanda na hukumu ya kufanana, kwa hivyo kwa kumunganisha mtoto huyo na rafiki yake - ambaye ni Zam’ah - alizingatia hukumu ya kitanda, na kwa amri yake kwa Sawdah R.A., kujifunika na mtoto aliyeambatanishwa na baba yake, alizingatia hukumu ya kufanana.
Imam Al-Nawawiy anasema kuhusu hali ya kutahadhari: “Kwa hivyo alimwamuru - yaani, kujifunika – kwa upande wa uwajibu na kutahadhari. Kwa sababu mtoto huyo kwa upande wa Sheria, ni ndugu yake; Kwa sababu aliambatanishwa na baba yake, lakini alipoona kufanana kwake kabisa na Utbah Ibn Abi Waqqas, aliogopa kwamba atakuwa ni katika maji yake (Manii), na kuwa simaharimu kwake, kwa hivyo akamwamuru ajifunike naye kwa kutahadhari. [Sharh Muslim 10/39, Ch. ya Dar Ihyaa At-Turaath Al-Arabi, Beirut]
Na katika Hadithi ya Aisha R.A., kwamba Mtume wa Mungu S.A.W., alisema: “Mwanamke yeyote aliyeolewa bila ya idhini ya Walii wake, ndoa yake ni batili, ndoa yake ni batili, ndoa yake ni batili, na ikiwa ataingiliwa, basi ana mahari ambayo inaruhusiwa kutokana na uke wake." – (Imepokelewa kutoka kwa Ahmad), At-Termedhiy, Ibn Majah, na wengine. Mtume S.A.W., aliamua kwamba mkataba huo ulikuwa batili na batili, na hali ilikuwa kutozingatia matokeo yake, lakini matokeo yake kwa njia ambayo ililazimu kuzingatiwa baada ya kutokea, hali ambayo ni uthibitisho wa mahari, Kwa maneno mengine, Mtume S.A.W., alitoa kila moja miongoni mwa dalili hizi mbili baadhi ya iliyohitaji nyingine.
Na Hadithi ya An-Nu'man Ibn Bashir, R.A., inathibitisha msingi huu aliposema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, S.A.W., alisema: “Halali iko wazi na haramu iko wazi, baina yao ni vitu vyenye shaka ambavyo watu wengi hawajui.
Kwa hivyo, yule anayeepuka vyenye shaka anajisafisha nafsi yake kwenye dini yake na heshima yake, lakini yule anayetumbukia katika mambo yenye shaka, huanguka katika haramu, kama mchunga anayechunga pembezoni mwa mpaka, anashukiwa kuingia ndani (ya shamba la mtu).
Hakika kila mfalme ana mipaka yake, na mipaka ya Allaah ni makatazo Yake ... ”- (Hadithi hii Mutafaq alayh) -. Miongoni mwa mambo yenye shaka ni mambo ambayo wanachuoni wanatofautiana katika uchambuzi na marufuku yake.
Miongoni mwa dalili zinazothibitisha msingi huu pia ni ile iliyopokelewa kutoka kwa Ibn Masoud kuhusu kuacha kufupisha Swala huko Mina, na kuikamilisha pamoja na Othman, hadi alipoambiwa:
Je, Unafanya jambo lile ulilokanusha? Alisema: “kutofautiana ni shari” – (ilipokelewa kutoka kwa Abu Dawud na Al-Bayhaqiy, na asili yake ni kwa Ahmad huko Al-Musnad, na Muslim huko Al-Sahih) -. Ibn Masoud aliacha jambo aliloamini kuwa ni sawa kwa mujibu wa dhana yake, kwa ajili ya maslahi muhimu zaidi kuliko hayo, ambayo ni hofu ya kugawanyika na kutengana, na tendo lake Ibn Masoud ni sahihi kulifanya liwe kutekeleza rai isiyokubaliwa na wanachuoni wengi au rai ambayo ni dhaifu kwa sababu ya kutokea kwa dharura, au kuleta maslahi iliyokubaliwa na wanachuoni wengi, na hii inaonesha kile tulichotaka kwamba tabia ya utunzi ni mojawapo ya sifa muhimu za misingi au adabu za kutofautiana. Lakini kutofautiana tu sio dalili ya kutosha kwa kusema kwamba kunazingatiwa, vinginevyo hali ile ingepelekea mtu kufuata makubaliano yaliyokatazwa, na wakati huo huo madhehebu za kifiqhi hazikuanzishwa.
Kwa kuwa hakuna suala ambalo halikosi kutofautiana ndani yake, hata suala linalokubaliwa na wanachuoni pia, kuna baadhi ya wanachuoni hawakulikubali.
Al-Zarkashiy katika kitabu cha: [Al-Bahr Al-Muhiit anasema - (8/311), Ch. ya Dar Al-Kutubi]: “Jua kwamba hali ya kutofautiana haionekani kuwa na shaka na haizingatiwi, lakini inaangaliwa chanzo na nguvu yake. Al-Ruyani alisema katika sehemu ya ushuhuda kutoka kwa [Al-Bahr]: Ikiwa hali ya kutofautiana yenyewe hunaleta tuhuma, basi masuala mawili yangelikuwa sawa, ikimaanisha suala la kuhitaji adhabu kwa mujibu wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa kwa kunywa pombe na ushuhuda wake, lakini tuhuma iko katika dalili”, na kutokana na hivyo yanabebwa maneno ya wale ambao hawakuona dalili ya kutofautiana. Kwa sababu hii, wanachuoni wameweka masharti ambayo lazima yatimizwe ili kutekeleza msingi huu: Mojawapo ya masharti hayo ni kwamba chanzo cha kutofautia ni chenye nguvu, na ikiwa ni dhaifu basi hakijaliwi. Al-Suyuti alielezea hali hii akisema: “Kuimarisha mtazamo wake ili isichukuliwe kuwa ni kosa.” – [Al-Shabah wa Al-Nadha'ir (uk. 137)] –
Kwa hivyo mnywaji wa pombe anaadhibiwa, na haizingatiwi hali ya kutofautiana kwa madhehebu ya Abu Hanifa, kwa sababu dalili za kutoharimisha pombe ni dhaifu – [Mughni Al-Muhtaj 6/11, Ch. ya Dar Al-Kutub Al-Elmiyyah], pia haikuzingatiwa hali ya kutofautiana kwa Ataa Ibn Abi Rabah kuhusu kuruhusiwa kwa kujamiiana na watumwa wa kike na uchi, kwa sababu maoni haya hayana dalili inayozingatiwa na sahihi, kwa hivyo mwenye kufanya hivyo anaadhibiwa. Na udhaifu wa suala hili unaweza kuwa ni kwa sababu ya kupingana kwake na matini au Kiasi au Ijmaa, na ukweli ni kwamba hali hii ni ngumu kufikia. Kwa hivyo, At-Taj Al-Subki anasema katika kitabu cha [Ashbah (1/113)] -: “Nguvu na udhaifu wa suala hili ndio haiishii kuzungukwa na watu peke yao.” Masuala mengi yasiyokubaliwa wanachuoni wanayaangalia kama ni yenye nguvu au dhaifu, ikimaanisha kuwa ni miongoni mwa mambo ya kiuwiano, lakini suala linaloonekana kuwa udhaifu wake halizingatiwi hata kidogo”- kitabu cha: [Al-Ashbah wa Al-Nadhair kwa Ibn Al-Subki (1/112, 113)].
Miongoni mwao ni: hali ya kuzingatia kwa kutofautiana haisababishi kukiuka makubaliano, au uzushi wa marufuku, na kwa hivyo ndoa ya mtu aliyeoa bila walii au mashahidi haifai. Kwa sababu ndoa bila walii, hata ikiwa iliruhusiwa na Abu Hanifa, na bila mashahidi, ikiwa Malik aliiruhusu, lakini hali hii ya pamoja hakuna hata mwanachuoni mmoja wa madhehebu yoyote anaikubali.
Vile vile miongoni mwao ni: hali ya kuzingatia kutofautiana haisababishi kutofautiana kwingine, kwa hivyo tunahitaji kutoka nje ya hali hii ya kutofautiana, na mfano wake: kutenganisha Swala ya Witri ni bora zaidi kuliko kuisali pamoja, na hali ya kutofautiana kwa Abu Hanifa haikuzingatiwa kuhusu kuiswali Witri pamoja ni bora zaidi. Kwa sababu wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Malik wanaosema kuwa inachukiza, yaani kuswali Swala ya Witri pamoja.
Baadhi ya wanachuoni wameongeza sharti la kwamba hali ya kuchanganya kati ya madhehebu lazima iwezekane, vinginevyo, haiachwi itikadi zake kwa ajili ya kuzingatia rai iliyokubaliwa na baadhi ya wanachuoni. Kwa sababu hali hii inasababisha kugeuza kile kinachohitajika kwake kufuatwa na kinachofikiriwa kuwa kina uwezekano mkubwa, na hali hii hairuhusiwi kabisa.
Al-Zarkashiy alitaja hivyo katika kitabu chake Al-Manthur, na ilinukuliwa kutoka kwa Abu Ishaq Al-Isfraini – [Al-Manthur (2/131)] - na akataja mifano mitatu ya hiyo, Wa kwanza wake, lakini kuhusu kutoruhusiwa kabisa kwa kuzingatia: Kwa sababu kuzingatia kutofautiana sio kitu zaidi ya kuiachia rai inayokubaliwa na wanachuoni wengi na hatima ya rai iliyokubaliwa na baadhi ya wanachuoni mara moja au baadaye kutimizwa kwa masharti yaliyotajwa hapo awali, kwa hivyo rai ilikubaliwa na baadhi ya wanachuoni tu maana yake ni rai dhaifu kabisa, kwa sababu ikiwa ilikuwa dhaifu, haingezingatiwa kama ilivyokuwa hapo awali, lakini jambo hilo linazunguka kati ya msimamo wa dhana na dhana inayowezekana zaidi, na msimamo wa dhana inayowezekana zaidi haujadili upande mwingine ambo ni msimamo wa dhana tu.
Imamu Al-Qibab Al-Malikiy anasema: “Dalili za kisheria, zikiwemo zinazodhihirisha nguvu yake, kwa hali inayolazimisha mwenye kuiangalia kukubali usahihi wa dalili moja miongoni mwao na kuifuata. katika hali hii hakuna kuzingatia kutofautiana. Miongoni mwa dalili ni ile inayopata nguvu kwa dalili nyingine, katika hali hii ni bora zaidi kuzingatia kutofautiana, kwa hivyo Imamu anasema na kufuata dalili iliyokubaliwa na wanachuoni wengi. Kama ukifanyika mkataba au ibada kufuatana na dalili nyingine hakutabatilisha mkataba na vile vile ibada hiyo kwa sababu ya ukweli kwamba hii imetokea kulingana na dalili yake, na sio kwa sababu kuwa moyo umefurahishwa tu.”- [Al-Miaar Al-Muarab (6/388)] - Kwa kuongezea hayo kwamba ile rai inayokubaliwa na baadhi ya wanachuoni tu inawezekana kuwa rai inayokubaliwa na wanachuoni wengi, kwa sababu njia hii katika kushughulikia kutofautiana ni pamoja na kazi ya nafsi na Fatwa.
Na inaweza kuongezwa kwa kila rai miongoni mwao hali ambayo huamua hatima ya inayotarajiwa, bila shaka, na uhusiano huu wa kuingiliana ulielezewa na Al-Ezz Bin Abd Al-Salam katika kitabu cha [Al-Qawaid Al-Kubra (1/369)] - Ambapo alisema: “Kuna sehemu kwa kutofautiana: Sehemu ya kwanza: kutofautiana kuwa katika hali ya kuharamisha na kuruhusiwa, basi ni bora kutoka kwenye kutofautiana kwa kukuzuia. Sehemu ya pili: kutofautiana kuwa katika hali ya kupendekeza au kulazimisha, basi kuitekeleza ni bora zaidi. Sehemu ya tatu: kutofautiana kuwa katika hali ya uhalali, kwa hivyo kutekeleza ni bora zaidi”. Kwa mujibu wa utaratibu huu, mifano iliyotajwa na Az-Zarkashiy inayohusu kutofautiana katika masharti ya kuswali Swala ya Ijumaa. Inawezakana kuzingatia kutofautiana huku kwa kusema kwamba Swala ya Ijumaa inalazimishwa, na huu ni mfano wa kwanza uliotajwa na ambao tulisema kuwa ulikuwa wenye nguvu zaidi, basi ilitajwa mifano mingine miwili, ambayo ni: Imamu aliyetangulia katika kusoma Al-Fatihah, na mwanzo wa wakati wa Al-Asiri. ikajibiwa kuhusu suala la kwanza kwa uwezekano wa kuainisha kauli ya yule anayesema kwa kubatilisha Swala ya yule anayesoma Al-Fatihah kuwa hana kisingizio, na kuhusu suala la pili kwamba kauli ya Al-Astakhari kwamba mwisho wa wakati wa Al-Asiri ni hatima ya kivuli cha kila kitu ambacho ni mfano wake, na kwamba atakayeswali baada yake ameswali baada ya kumalizika wakati wake, rai hii inahukumiwa kuwa ni dhaifu, kwa hivyo hali ya kutofautiana haizingatiwi.
Kwa kutumia kile tulichotaja juu ya suala la Qunuti katika Swala ya Al-Fajiri, hali ile iliyofanywa na Imamu ni sahihi na hakuna lawama kwake, lakini kuzingatia kutofautiana katika hali hii, ni kuacha dua ya Qunuti kwa hofu ya mfarakano, na tabia hii inaendelea kulingana na misingi ya kisheria kama tulivyotaja, na tunatoa wito kwa Waislamu katika kila mahali wasitawanyike na wasiwe maadui kwa sababu ya maswala haya madogo ambayo hutofautiana, haswa kwa kuwa hayawakilishi utambulisho wa Uislamu, kwa hivyo yeyote anayefanya hivyo, hakuna lawama na yeyote ambaye hafanyi hivyo, halaumiwi pia.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
Sekretarieti ya Fatwa

 

Share this:

Related Fatwas