Kutumia Maziwa Yanayopatikana kwa K...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutumia Maziwa Yanayopatikana kwa Kuyakamua kwa Chombo cha Kunyonyeshea Kilichotengenezwa Badala ya Chuchu za Mama.

Question

Je inajuzu kunyonyesha kwa kutumia maziwa yanayopatikana kwa kuyakamua kwa chombo cha kunyonyeshea kilichotengenezwa ambacho kinapatikana katika baadhi ya Jamii, na chombo hicho kikachukua nafasi ya unyonyeshaji wa kawaida, katika kuthibiti uharamu wa undugu utokanao na kunyonya pamoja? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Chombo kilichotengenezwa kwa ajili ya kunyonyeshea ni chombo ambacho kazi yake ni kukamua maziwa ya Mwanamke. Na Mwanamke kutumia chombo hicho Inajuzu.
Chombo kilichotengenezwa kwa ajili ya kunyonyeshea ni chombo ambacho kazi yake ni kukamua maziwa ya Mwanamke. Na Mwanamke kutumia chombo hicho Inajuzu. Na uharamu wa kunyonya pamoja pia unapatikana kutokana na kunyonya maziwa yaliyokamuliwa kwa chombo hicho kwa masharti ya kunyonywa, kwa kuwa kwake milo mitano tofauti ya kunyonya maziwa hayo ndani ya miaka miwili, iwe mlezi husika yu katika ndoa au ameachwa au ni bikra; muhimu tu mnyonyeshaji awe katika umri wa kunyonyesha, nao ni miaka tisa ya mfumo wa mwezi, na kwa kuwa kinachoendelea kutoka matitini kinazingatiwa kuwa ni maziwa; kwani Jamhuri ya Wanachuoni haikushurutisha kuwa kwa mnyonyeshaji awe ameolewa au ameachika, na wakasema ya kwamba kama angelikuwa bikra au bila ya mume au akawa mtu mzima, basi kunyonyesha kwake ni Haramu kama masharti yote yatakuwa yamekamilika.
As Sarkhasiy alisema katika kitabu cha: [Al Mabsuotw 138-139/5, Ch. ya Dar Al Maarifah]; miongoni mwa vitabu vya Madhehebu ya Hanafi: "Na pindi maziwa yanaposhuka kwa Mwanamke hali ya kuwa Mwanamke huyo ni bikra na hajaolewa na akamnyonyesha mtoto mdogo basi huko kunazingatiwa kuwa ni kunyonyesha; kwani maana ya kuthibiti uharamu kwa kunyonya ni kupatikana kwa mshabihiano wa sehemu tu baina ya mnyonyeshaji na maziwa, na maziwa yaliyomtoka ni sehemu yake, iwe Mwanamke huyo alikuwa na mume au hakuwa na mume na maziwa yake yanamlisha mtoto anaenyonya basi huko ni kuthibiti kwa mfanano wa sehemu yake". (Mwisho)
Na Ibn Roshd Al Malikiy amesema: "Kuharamika kunatokea kwa maziwa ya Mwanamke bikra na mwanamke mzee ambaye hajawahi kujifungua, hata kama itakuwa bila ya kuingiliwa, ikiwa maziwa sio maji ya njano. [Tazama kitabu cha: Mawaheb Aj Jalili kwa Al Hatwaab 179/4, Ch. ya Dar Al Fikr Al Arabiy].
Na Imamu Abu Is-haq As Shiraziy miongoni mwa wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafi amesema katika kitabu cha: [Al Mohazab 157/2, Ch. ya Dar Al Fikr, Bairut]: "Na ikiwa Mwanamke bikira atatoa maziwa au Mwanamke aliyewahi kuolewa lakini hana mume akamnyonyesha mtoto kwa maziwa hayo basi kutathibiti kuharamika baina yao kwa kunyonya; kwani maziwa ya Mwanamke ni chakula cha Mtoto".
Na Mwenyzi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Ofisi ya Kutoa Fatwa.


 

Share this:

Related Fatwas