Sunna za Mtume – Kuhusu Misingi ya ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Sunna za Mtume – Kuhusu Misingi ya Kuzifanyia Kazi.

Question

 Ni misingi ipi ambayo tunapaswa kuifanyia kazi kwa Sunna Takatifu za Mtume?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Sunna ni kitu kinachonasibishwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. na kuletwa kwetu na Maswahaba wa Mtume S.A.W., kisha wakafuata watu wa Taabiin ambao ni watu waliokuja baada ya Maswahaba wa Mtume kisha waliofuata baada yao, na sisi tunawafahamu kwa majina yao kwani kila mmoja wao kuna faili kamili ndani ya elimu inayoitwa “Ilmu Arjaal” na ndani ya elimu inayoitwa “Elimu ya “Ajarhu wa Ataadiil” inayokusanya kanuni za hukumu za wasomi hawa kwa upande wa maadili na tabia na huitwa “Al-Al-Adaala” huwekwa sharti kwa mpokezi wa Hadithi sahihi kuwa ni “Mwadilifu”, na kwa upande wa kiakili huitwa “Udhibiti” huwekwa sharti kwa mpokeaji wa Hadithi kuwa ni mwenye kudhibiti kwa maana ya kutosha katika upokezi.
Sunna imepewa umuhimu mkubwa na wanachuoni pamoja na wanafunzi wa elimu na kufanya uhakiki wa kina na wa ndani zaidi kwa upande wa upokezi na matini ya Sunna yenyewe, hawakuhusisha tu kukubalika kwa Hadithi sahihi kwa kuangalia kilichopokelewa na wapokezi lakini pia wanachuoni wa Hadithi na wachambuzi wake wameangazia upande wa “Uelewa” nao ni umakini kwenye matini na uzito wake kwenye vithibiti vya Sharia na misingi yake, kuna vitabu vingi vinavyohudumia Sunna kati ya vitabu vya historia, vitabu vya mapokezi, vitabu vya usahihi wa Hadithi, vitabu vya Hadithi dhaifu na vinginevyo vilivyo husishwa kufuatilia “Maudhui”, kwa maana ya Hadithi za uzushi kwa Nabii wa Mwenyezi Mungu S.A.W..
Kutokana na hayo inatuwia wazi kadhia ya kwanza kwa mtafiti wa kijamii pale anapoikaribia Sunna, nayo ni kadhia ya kukubalika kwa Hadithi, tumeelezea hili kwa ufupi hapo nyuma.
Mtafiti anaanza kuangalia katika “Upokezi” ili kuthibitisha unasibishwaji wa kauli au kitendo au sifa au kukiri kuliopo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., kinyume na hivyo basi hakuna maana kwa kazi zingine za kiutafiti ambazo zinategemea Hadithi zisizokubalika, huenda maneno yakawa ni mazuri lakini wakati huo huo yakawa si maneno ya Mtume S.A.W., na miongoni mwa makosa ya wazi ni pamoja na kufumbia macho jambo hili ambapo Mtume S.A.W. amesisitiza juu ya kosa la jinai na adhabu kali kunasibisha kitu kwake kwa uongo, ndipo ikaja Hadithi yenye wapokezi wengi inayosema: “Hakika kunisemea uongo mimi sio kama kumsemea uongo yeyote, kwani mwenye kunisemea mimi uongo kwa makusudi basi na ajiandae makazi motoni” ( ).
Kuangalia katika upokezi haijaacha kuwa ni muhimu kwa wanafunzi wa elimu na watafiti wa leo, namna ya kurejea kwenye vitabu vinavyozingatiwa ni kazi za watu wa elimu ya Haidhti wenye weledi, na mtafiti anavirejea vitabu hivyo katika kutafuta usahihi wa upokezi na uzuri wake au udhaifu uliopo, nao ni wenye kutafautiana katika misimamo yao ndani ya baadhi ya Hadithi, na wanakubaliana katika misimamo mingine, lakini kwa ujumla kuna ashiriwa baadhi ya ukweli:
- Maswahaba wote ni wenye kuaminika pasina tofauti yeyote ile kati ya watu wa Sunna pamoja na tabaka tatu za Tabiina: Tabiina wakubwa: Nao ni wale waliokutana na Maswahaba: Kwa maana ni wenye kuaminika. Tabiina wa kati: Asili kwao ni watu wa kuaminika maadamu hakuna kauli ya Imamu miongoni mwa Maimamu wa Hadithi na kujeruhi kwa kumdhoofisha au kumjeruhi. Tabiina wadogo: Si wenye kuaminika isipokuwa kwa ushahidi wa Imamu wa Hadithi.
- Hadithi yenye nguvu sana ya usahihi ni ile iliyokubalika na Masheikh wawili nao ni (Imamu Bukhary na Imamu Muslimu) ikifuatiwa na ile iliyothibitishwa peke yake na Imamu Bukhary kisha iliyothibitishwa peke yake na Imamu Muslimu.
- Baada ya vitabu hivi viwili vinakuja vitabu vinne vya kwanza vya Hadithi, na huitwa Hadithi zilizopokelewa humo kwa pamoja (Zimepokelewa na watu wa Sunna) ni Sunna ya Abi Daud, Sunna ya Ibn Majah, Sunna ya An-Nisaay pamoja na Sunna Tirmidhy, na kuna mapokezi yaliyo dhaifu lakini ni mengi sana miongoni mwake yana mwelekeo sahihi na hasan, na kujumuika vitabu hivi vinne pamoja na vile vitabu viwili vilivyopita na kufanya jumla vyote kuwa ni vitabu sita vya Hadithi (Husemwa: Hadithi imepokelewa na Maimamu sita kwa maana ya wale Masheikh wawili na hawa wa nne).
- Inafuata baada ya hawa ni mapokezi ya Imamu Ahmad na kitabu cha Al-Muwatwaa cha Imamu Maliki, kisha kinafuata baada ya hapo kitabu cha Sunna ya Ad-Daaramiy na Ad-Daaraqutwniy, sahihi ya Ibn Habbaan, kitabu cha Ibn Aby Shaibah na wengineo….vitabu vya mwisho pamoja na kuwa na mapokezi yaliyo sahihi na muhimu pamoja na kufahamika sana lakini hata hivyo ndani yake kuna Hadithi nyingi dhaifu.
Kisha mtafiti anapaswa baada ya hapo – kama hatua ya pili – kukamilisha hilo kwa kuangalia kwenye matini ya Hadithi ili kuthibitisha hatua ya kwanza, na hatua hizo zote mbili zinakuwa ni katika jumla ya kadhia za kuaminika.
Kadhia ya Pili: Ni kadhia ya kufahamu matini ya Hadithi – baada ya kuikubali – kabla ya kuichambua madhumuni na muundo wa tafiti ya sayansi ya kijamii, na husaidia katika kufahamu matini kwa kurejea kwenye vitabu muhimu vilivyosherehesha Hadithi na kufahamika na ambavyo leo vimekuwa vinapatikana kwa wingi mfano kama vile vitabu vya tafasiri ya fiqh na vitabu vyote vya urithi kwa njia ya mtandao wa maelezo. Wala haimaanishi kufuata miongozo ya vitabu hivi vilivyo sherehesha Hadithi kuwa ni marejeo ya mwisho vyenye utajiri wa kuzingatiwa, uelewa bado ni wenye kuhitaji ukina zaidi, bado na utaendelea mlango kuwa wazi ili kuelewa Hadithi zaidi na zaidi yale ambayo hayakuwa yameelezewa hapo nyuma, haswa pamoja na kuongezeka “Kiwango cha maarifa” na kuendelea kwa maarifa ya ulimwengu na maisha kwa kila siku.
Kadhia ya Tatu: Ni kadhia inayohusu ufafanuzi na kunufaika na maarifa na utafiti wa Sunna, nayo inahitaji umiliki muhimu unaowezekana kuupata, na ni muhimu kuupata nao ni: Umiliki wa “Ufahamu jumla wa Sharia ya Kiislamu”.
Ufahamu huu huenda ukawa ni wenye kufahamika zaidi kwa baadhi kuliko wengine, na uwazi wake unaongezeka kwa kuongezeka maarifa ya kina ya Sharia, na mahusiano ya wazi katika mifumo yake, na kwa kiwango gani ufahamu wa mtafiti au mwenye kufanya jitihada wa athari zinazofungamana na mtazamo huu jumla, kila anapokuwa mtafiti mwenye kusoma zaidi Sharia ndio kila unapokuwa mtazamo huu wa kina zaidi kama vile nadharia inayotawala akili na elimu ya tafiti.
Ufahamu huu unapelekea kwenye Fiqih ya “Kauli vitendo na Fatwa” Na Fiqih ya “Makusudio ya Sharia” pamoja na Fiqih ya “Sababu” nayo kwa ujumla wake ni sehemu inayosaidia kufahamu na uchambuzi mzuri, na hii inakuwa ni “Muundo wa kinadharia” kwenye Hadithi, ni sababu katika tofauti za kifiqih mpaka Maimamu wakabainisha kama vile Imamu Maliki na Shafi ( ). Bali jambo la tofauti lilikuwepo wakati wa Mtume S.A.W. kwa Maswahaba wake, na Hadithi “Asiswali yeyote miongoni mwenu Swala ya Alasiri isipokuwa mpaka mtakapofika eneo la bani kuraidhah ( ) kinachofahamika kulikuwa na mitazamo miwili ambayo Mtume aliikubali mitazamo yote hiyo miwili, kuanzia mtazamo wa kuwajibika na tamko lenyewe, na mtazamo wa kuangalia sababu malengo na makusudio, hakuna tatizo ikiwa tamko litakubaliana na sababu ya jambo pamoja na makusudio yake, lakini pindi akili ya mtafiti inapohisi mgongano basi uwezo wa akili huelekea kwenye upande wenye nguvu ya hoja au nguvu ya sababu.
Tofauti kati ya mitazamo miwili na kati ya kile kinachowezekana kuonekana miongoni mwa akili mbalimbali ni kina cha mtazamo wa jumla na undani wa kuangalia ukina wa masuala na kuwajibika na msingi thabiti pasin kuibatilisha kwa njia ya moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kufanyia kazi kwa ajili ya kutengeneza mtazamo huu jumla wenye kukubalika, na kunufaika na Sunna mtafiti anahitaji hatua zifuatazo:
a- Ufuatiliaji Dini: Kwa maana ya kufuatilia Qur`ani na Hadithi pasina kujitosheleza na kimoja bila kingine.
b- Mtazamo: Kwa maana kujenga mtazamo katika kila masuala (Tutatoa mifano).
c- Ufanisi: Kwa maana ya kujaribu kuleta ufanisi wa mtazamo huu katika tatizo linalofanyiwa utafiti, ikiwa ni lenye mfungamano.
Wakati mtafiti anapotoa hukumu ya kitu katika kuzaa kwake fikra zinazotokana na uhalisia basi ni lazima kuchunga mtazamo au mitazamo ambayo ameitengeneza hapo mwanzo wakati wa kufuatilia Qur`ani na Hadithi, kwani jambo – ikiwa tunafahamu – mwanzo wake ni kuamini Kitabu na Sunna na kuzipenda pamoja na kuwajibika nazo katika jambo lote.
Hatua hizi Tatu (Kufuata Dini Mtazamo na Ufanisi) ni hatua zinazotakiwa kwa ajili ya kuzifanyia kazi Sunna, ufanisi wenye uelewa unao hudumia mwenendo mzuri, na kwa hatua hizi tunachukua mifumo ya waja wema waliotangulia pasina kusimama kwenye masuala yao, na huu ni ulazima wa mtafiti na mtafuta elimu wa leo ili kupambana na matatizo ya muda wote.
Hatua hizi tatu ni katika njia ya kutengeneza mtazamo jumla unaofaa kufanyia kazi Sharia zote za Kiislamu Qur`ani na Sunna, kwa sura ambayo inapaswa kuchunga tofauti kati ya kuifanyia kazi Qur`ani na kufanyia kazi Hadithi kwa sura tofauti muhimu yake ni kuwa:
1- Hakika Qur`ani ni yenye kuhifadhiwa kuanzia herufi na kuendelea, wakati ambapo Hadithi ni zenye kuhifadhiwa kwa upande wa maana.
2- Qur`ani ni muujiza, na Sunna si muujiza, kwa sababu Sunna ndani yake yameingia maelezo ya wapokezi, hivyo Qur`ani inatoa hukumu kwenye tatizo la Hadithi.
3- Qur`ani ni ibada kwa kuisoma wakati wote na katika hali zote pamoja na kukamilika kwa masharti ya usafi uelewa na utakasifu…..Sunna si ibada kwa kuzisoma kwake lakini ni ibada kwenye kuzitekeleza.
4- Qur`ani ni Kitabu cha muongozo hivyo yenyewe ipo karibu zaidi – mara nyingi- kuelewa misingi mikuu na mwenendo wa Mungu misingi na kanuni kuu, ama Hadithi au Sunna zenyewe ni utekelezaji wa kanuni hizi na misingi hii hivyo inawezekana kusema kuwa Qur`ani ni huru kwa maana imekomboka na vifungo vya wakati sehemu hali watu na mazingira, ama Hadithi ni sehemu kwa maana ya uhalisia ni sehemu kwenye Qur`ani, kutokana na hivyo inapaswa kufanyia kazi Sunna wakati wa kuangalia (Kutoa mtazamo baada ya ufuatiliaji) kwa mtazamo wenye uhalisia ili uwe pia ni chanzo kingine.
Mifano ya kiutendaji ya kufanyia kazi misingi hii miwili:
Hatua tatu za kufanyia kazi misingi hii miwili (Kitabu na Sunna) tunatoa mfano wa kadhia ya “mwanamke” mwenye kuibua hisia hivi sasa, ili mtafiti Muislamu aweze kuleta ufumbuzi kutokana na mtazamo wa Kiislamu basi ni juu yake kukusanya kati ya misingi miwili asili, atafuatilia Aya na Hadithi kama hatua ya kwanza, anazikusanya na kuzingatia na kuzirejea kwa wanachuoni waliotangulia na waliopo kwa uthibitisho ufahamu na ukina zaidi.
Kisha inakuja hatua ya pili (Ufafanuzi), nayo ni hatua muhimu ambayo inahitaji jitihada za kiakili na kufanyia kazi fikra pamoja na kuunganisha sehemu ndogo ndogo na kurejea misingi jumla, na kuleta uwiano kati ya vilivyoachana, na kuvipa nguvu kati ya vilivyotofautiana.
Aya ya kwanza ya Surat An-Nisaa inaonesha kuwa mwanamme na mwanamke wameumbwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini pia pale Mungu aliposema: {kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanya mwenziwe katika nafsi ile ile} Azzumar: 6. Asili ni moja na kila mmoja kati ya wawili hao ni mume na mke kwa mwenzake, na hii inaana kuwa wote wawili “Wanakamilishana” kila mmoja anamkamilishia mwenzake, mtafiti katika hili atatoa fikra ya “Mashirikiano” inayokanusha “Kukubaliana kunako gongana”.
Vile vile Amesema Mola Mtukufu {Na mwanamume si sawa na mwanamke.} Surati Al-Imraan: 36, ukanushaji wenye “Kufanana” haina maana ya umuhimu wa kupambana au kupigana vita, kwani pia Amesema: {Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke, kwani ni nyinyi kwa nyinyi} Al-Imraan: 195. Na akasema Mola Mtukufu: {Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema} [AN NAHL: 97] ……hakuna tofauti, kwani Qur`ani imekanusha “mfanano” na vilevile imekanusha “tofauti” basi ipi ni jumla? Na ipi ni maalumu? Au ipi ni asili moja kwa moja? Na ipi ni dharura? Au kuna sifa nyingine inayokutanisha mambo mawili, au kuyabadilisha kinyume? (Kukusanya dalili mbili – ikiwa itawezekana – ni bora kuliko kupuuza moja wapo) – Kanuni.
Tunakamilisha nukta ya kufuatilia, tunakuta kauli ya Mwenyezi Mungu: {Wala musitamani alicho wafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wana fungu katika walio vichuma, na wanawake wana fungu katika walio vichuma. Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu} [AN NISAA: 32]. Aya imeashiria kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amewafadhilisha wanaume kwa wanawake kama vile alivyowafadhilisha wanawake kwa wanawaume, wote ni wanafungu katika yale waliyochuma, na kukataza kila upande kutamani yale waliyonayo upande mwingine, na kuwataka wamuombe Yeye Mola Mtukufu fadhila zake na kuwabainishia kuwa Mola Mtukufu Anafahamu yale wasiyoyajua: {Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu} [AN NISAA: 32].
Katika Aya mbili zingine amebainisha kitu ambacho amewafadhilishia wanaume akasema Mola Mtukufu: {Nawanaume wana daraja zaidi kuliko wao} [AL BAQARAH: 228], na akasema tena Mola Mtukufu: {Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde} [AN NISAA: 34].
Kwa kuzingatia zaidi tunakuta kuwa kuna usawa”: {Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao} [AL BAQARAH: 228]. {Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke, kwani ni nyinyi kwa nyinyi} [AAL IMRAAN: 195], wala hatukuti kuna “Uwiano” kwani tunatofautisha kati ya usawa na uwiano kwa kauli yake Mola Mtukufu: {Wala msitamani alicho wafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko wengine} [AN NISAA: 32], haya yanayowezekana kuyafafanua katika kufuatilia Qur`ani, kisha tunakuta kuwa Hadithi inasisitiza.
Hadithi inasema: “Mtume S.A.W. amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha na wanaume” ( ).
Kwa maana Mtume anaharamisha kuyahama maumbile na kufanya utashi wa kuyahama maumbile hayo kutoka kwenye wigo wa aina ya maumbile na kwenda wigo mwingine, ni lazima kwa mwanaume kutofanya juhudi za kutaka kuwa mwanamke au kama mwanamke, wala mwanamke kufanya juhudi za kutaka kufanana na mwanaume, na huitwa mwanamke wa aina hii ni jike dume.
Usawa ni tofauti na uwiano” inaonesha kuwa mwanamme na mwanamke ni wenye kutofautiana, wakiwa ni wanandoa wawili wenye kukamilishiana, basi ni nani mwenye tamko “wakati wa kutofautiana?” amri na tamko ni kwa mwenye kupewa uwezo na Mwenyezi Mungu Mtukufu wa kuongoza na kuwa na tamko la mwisho, katika maswala ya wanawake huchukuliwa ushahidi wa mwanamke na huenda ushahidi wa mwanamme usikubalike, katika maswala ya nyumbani Mwenyezi Mungu Mtukufu amempa mwanamme jukumu la usimamizi kwa mwanamke.
Na zingatia tofauti kati yao, tukuta kuwa mwanamke ni kiumbe “dhaifu”, wote wanaume na wanawake, watu wa zamani na hata wa sasa – isipokuwa baadhi ya walinganiaji wa “Jandar” – wamekubaliana kuwa mwanamke ni dhaifu zaidi kuliko mwanamme, tofauti kati ya watu wa fikra na ndani ya makundi ya harakati za wanawake wanaojihusisha na mambo ya wanawake hivi sasa si katika ukweli huu bali ni katika athari zake, na “yanayopaswa” kufungamana na mwanamke, hapa inaonekana tofauti ya msimamo wa Kiislamu katika kadhia ya mwanamke.
Katika ufuatiliaji wa Qur`ani na Hadithi – tunakuta kuwa Uislamu haujawataja vibaya wanawake katika andiko lolote, pamoja na kuwepo kwa uzushi mwingi, lakini Uislamu unatengeneza nadharia ya “udhaifu wenye kuheshimika”, wakati ambapo walinganiaji wengine wanalingania kumfanya mwanamke ima ni mtu wa mwisho, kwa maana ulinganiaji wa kuwa mwanamke ni mtu wa mwisho na kumtoa katika asili yake ambayo ameumbiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kulingania “kutoheshimu udhaifu wake”, na hali hii si ngeni bali hutekelezwa pia kwa vitendo vya kurithiwa ndani ya jamii nyingi za Waislamu, wakati ambapo matamko ya Qur`ani na maneno ya Mtume S.A.W. na vitendo vyake vyote havihusiki kwa ukaribu wowote wa mfano wa vitendo hivyo.
Ndani ya Kitabu Mwenyezi Mungu Anasema: {Enyi mlio amini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu. Wala msiwadhikishe ili muwapokonye baadhi ya mulivyo wapa - isipokuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake} An-Nisaa: 19.
Na anasema tena: {Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa nikipawa. Lakini wakikutunukieni kitu katika mahari, kwa radhi yao, basi kileni kiwashuke kwa raha}: An-Nisaa: 04.
Kauli nyingine: {Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri. Wala si halali kwenu kuchukua chochote mulicho wapa wake zenu, ila ikiwa wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kushikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu} [AL BAQARAH: 229].
Na kauli yake: {Na mtakapo wapa wanawake talaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema. Wala msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakaye fanya hivyo, amejidhulumu nafsi yake. Wala msizichukulie Aya za Mwenyezi Mungu kwa maskhara. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, na aliyo kuteremshieni katika Kitabu na hekima anacho kuonyeni kwacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu} [AL BAQARAH: 231].
Qur`ani inasema tena: {Na mtakapo wapa wanawake talaka nao wakamaliza eda yao, basi msiwazuie kuolewa na waume zao endapo baina yao wamepatana kwa wema. Hayo anaonywa nayo yule miongoni mwenu anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ni bora zaidi kwenu na safi kabisa. Na Mwenyezi Mungu anajua, lakini nyinyi hamjui} [AL BAQARAH: 232].
Aya nyingine ya Qur`ani: {Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo} [AL BAQARAH: 233].
Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hesabu ya eda. Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake} [AT TWALAAQ: 01].
Na kauli nyingine: {Wawekeni humo humo mnamo kaa nyinyi kwa kadiri ya pato lenu, wala msiwaletee madhara kwa kuwadhiki. Na wakiwa wana mimba, wagharamieni mpaka wajifungue. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao, na shaurianeni kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwingine} [AT TWALAAQ: 06].
Udhaifu wenye kuheshimika na usimamizi wa mwanamme hapa maana yake ni mpangilio shirikishi ambao utaukuta mfano wake kati ya wanaume wenyewe, na kati ya wanawake wenyewe, kati ya wanaume kuna kiongozi anayeongoza ni baba au mtoto, kwa upande wa wanawake ni mtoto na binti, dada mkubwa na dada mdogo….na mfano wa hivyo, huu wote ni utaratibu shirikishi.
Nadharia ya usawa bila ya uwiano, nadharia ya udhaifu wenye heshima, nadharia ya utaratibu shirikishi, kushirikiana pasina mivutano, nadharia ya sifa maalumu na majukumu (Kwa maana ya kila pande mbili za mume na mke kuna sifa zake ambazo zimewekwa kwake mume au kwa maana anajukumu maalumu) nadharia zote hizi shirikishi na zenye kufafanuliwa kutokana na ufuatiliaji wa Dini (Qur`ani na Hadithi) zinakuwa ndio asili au msingi.
Hatua ya tatu ni ufanisi, miongoni mwake ni pamoja na kujibu sehemu na matukio ya kinyume na kuyabatilisha, inakusudiwa ni kutokubali fikra au kutumia maelezo ndani yake kuna kubatilisha msingi huu, na hasa fikra zilizokuja kutokana na mitazamo mbalimbali, na fikra zilizo ganda katika mzingiro wa urithi katika yale Mwenyezi Mungu hakuteremsha mamlaka, kama vile kauli yao: Washaurini na nendeni nao kinyume, na kauli yao: Mwanamke ameumbwa mwenye upungufu….na mfano wa hayo.
Ama kauli ya kwanza Mwenyezi Mungu Anasema: {Na shaurianeni kwa wema. Na mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee mwanamke mwingine} [AT TWALAAQ: 06].
Na Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao. Na mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha basi hapana ubaya kwenu mkitoa mlicho ahidi kwa mujibu wa ada. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo yatenda} [AL BAQARAH: 233].
Ama kauli ya pili Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. anaweka wazi maana ya upungufu wa akili ya mwanamke ni katika usahaulifu wa ushahidi, na upungufu wa dini yake ni katika yale yanayokosekana kutokana na hali yake ya hedhi na nifasi ikiwa ni pamoja na kukosekana ibada za Swala na Funga, basi ni vipi nadharia inaenezwa kwenye mambo yote wakati Mtume S.A.W. amehusisha vitu maalumu badala ya vitu vyote? Ni vipi hayaenezwi yale yaliyoenezwa na kauli yake Mtume S.A.W. inayosema: “Mbora wenu ni mbora wenu kwa familia yake” ( ). Na katika Hadithi ya Umu Zaraa ni kauli yake Mtume S.A.W. kwa Bibi Aisha RA: “Nimekuwa kwako ni kama baba wa Zarii kwa mama Zarii” ( ), wamekubaliana Maimamu wa Hadithi, ni vipi wakati nusu ya mafundisho ya Dini tumechukuwa kutoka kwa Bibi Aisha R.A?
Hii ni kiasi cha mifano ya vitendo ya utekelezaji wa hatua tatu katika kuifanyia kazi kadhia za Qur`ani na Hadithi, ambazo ndio chanzo katika Sharia ya Kiislamu, na kuna vyanzo vyingine vya kufanyia kazi na kunufaika navyo pembezoni mwa mwanzo hivi viwili, kama vile vitabu vya tafasiri vitabu vya Fiqih vitabu vya sherehe na vitabu vya sira, ni vyenye manufaa katika kuelewa vyanzo hivi viwili na kuongoka navyo, na mifano sio jiwe kwenye kufuata au kuwa na mitazamo tofauti, lengo ni kuweka wazi na kubainisha “Uwezekano” wa kufanyia kazi urithi wetu pamoja na Qur`ani na Hadithi ufanisi ulio chanya katika viwanja vya elimu ya kijamii na kibinadamu ili kufikia malengo kadhaa:-
- Kufikia mawasiliano kati ya Muislamu na Dini yake, mawasiliano ya kielimu na mawaisiliano ya kivitendo, na haya ndio makusudio ya kazi za ulinganiaji kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwenye haya.
- Kufikia mawasiliano kati ya Dini na urithi kwa upande mmoja na kati ya uhalisia na fikra za Muislamu kwa upande mwingine, kupitia usomaji tena wa urithi na kuboresha (na wala sio kurekebisha kwani wenyewe si wenye kuharibika) na jaribio la kuboresha katika masomo na silabasi ya sasa.
- Kujenga kizazi kipya cha Kiislamu kinachofikiri Uislamu katika mambo yote ya maisha na elimu, na kuboresha maendeleo ya kielimu pamoja na kufikia kusudio la Mwenyezi Mungu Mtukufu kwenye nchi na kwa waja, na Mwenyezi Mungu ndio mtawala wa hayo Naye ni mwenye uwezo wa hayo.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Chanzo: Kitabu “Njia ya kuelekea kwenye ufahamu wa urithi” cha Fadhilatuh Mufti wa Misri Dr. Ally Juma.

 

 

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas