Mawazo ya urithi, Vipengele vyake n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mawazo ya urithi, Vipengele vyake na Sehemu zake

Question

Je! Ni vipi vipengele vya mawazo ya urithi na zipi sehemu zake? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ili kuelewa urithi wetu mkubwa wa Kiislamu vizuri, ni lazima - mwanzoni - tuelewe "maono kamili" ya watengenezaji wa urithi huu, kwa sababu maono haya yaliondolewa katika falsafa ya Magharibi wakati wa karne nne zilizopita, mpaka wanafalsafa wa Magharibi na wafuasi wao Mashariki walipoitoa kutoka katika hali ya kawaida ijulikanayo na watu kwa umaalumu, sio tena - kama ilivyokuwa – katika hali ya kawaida kati ya watu. Hapo zamani, tulikuwa tukiona daktari, mwanariadha, mwanasiasa, na mifano yao wakiwa na maono maalumu kuhusu ulimwengu. Maono haya ni pamoja na maono ya falsafa, maono ya habari, utamaduni au ya uadilifu... Suala hilo lilikuwa na mshikamano mkubwa na lililounganishwa, maono ya ulimwengu hayakutenganishwa kwa duru nyembamba kwa jina la utaalamu au kitu kingine chochote. Katika muktadha wetu wa sasa, tunahitaji kutambua mifano ya maono haya, kutafuta vyanzo vyao, na kuelezea ni vipi vinaathiri akili ya umma, na nyuma yake akili ya kisayansi iliyozalisha urithi kama huo.
Miongoni mwa mifano ya maono haya ni kwamba Waarabu - kwa mfano - walikuwa wakifikiria ulimwengu kama ndege, mdomo wake au kichwa chake kwenye Mashariki (China, ...), na kuna mrengo wa Sham na Uturuki, mrengo wa Yemen na nchi nyingine kama visiwa vya Bahari ya waarabu na Bahari ya Hindi, na mkia huko Marrakesh (Moroko) na nyuma yake Bahari ya Giza (Bahari ya Atlantiki). Haya ni maono ya habari ambayo yalikuwa yameenea katika vivuli vya dari zingine za utambuzi katika masomo ya jiografia na demografia. Hata waliita "Sham" kwa jina hili linalomaanisha "upande wa kushoto", na waliita "Yemen" kwa jina hili kumaanisha upande wa kulia, hivyo kwa mdomo wa ndege waliomfikiria. Hivi karibu ni vitu vyote ambavyo havikuandikwa kwenye vitabu au havikuwa wazi ndani yake, lakini vilikuwa vya kawaida kabisa na vilitawala akili za watu wote katika nyakati hizo.
Ndege huyu - aliyedhaniwa na Waarabu - aligawanywa katika mikoa saba, na wakaiita "mikoa saba." Na nambari "saba" - kwa wazee hawa - ilikuwa na maana kama "maana ya kimfumo." Maana ya kimfumo ni imani kwamba Mwenyezi Mungu amejenga ulimwengu huu kwa mifumo. Miongoni mwa mifumo hii, Mwenyezi Mungu ameumba vitu vingi idadi yake ni saba: kama mbingu, dunia, bahari, mikoa, siku za wiki, n.k., hata kwenye hesabu wanazingatia idadi "saba" ni idadi kamili. Kwa sababu ni kukamilika kwa mzunguko wa nambari... Na kumekuwa na maandishi ya zamani juu ya nambari katika Qur'ani, Sunnah na zingine. Kama vile (Al-Isaad katika Hesabu) na Ibn Hajar Al-Asqalani, ambapo hadithi zilizotaja nambari na umuhimu wake zimeorodheshwa, na vile vile vitabu vya kisasa kama vile maandishi ya Ali Basha Mubarak.
Tantawi Jouhari ana kitabu kiitwacho [Bahjat Al-Ulum] ambacho kinajaribu kuweka wazi sehemu za mawazo haya. Kulingana na dhana kwamba kuna malezi ya kihistoria na kitamaduni ambayo yalisababisha urithi huu mkubwa, inazungumzia muziki, nambari, alama ... nk, kama viashiria vya tabia na sehemu za mawazo haya.
Kwa mfano, aliweka wazi kuwa asili ya muziki katika watu wa zamani ilikuwa kuzunguka kwake kati ya utulivu na mwendo, na utulivu na mwendo ni maelezo mawili ya hali mbili ambazo zinashiriki na kuelewa hali ya kuishi. Viumbe ni vya kutulia au vya mwendo, na muziki unatokana na uwepo huu. Halafu waliona kuwa muziki ni njia ya kujieleza, kama lugha au hotuba, na lugha hiyo ina herufi zinazochanganya kuunda maneno na sentensi.
Kuanzia hapa muziki ulipimwa na kujengwa katika ustaarabu wa Kiislamu. Ilisemekana kwamba sehemu zake za kimsingi zinaundwa na herufi mbili (konsonanti na irabu), "tin, tin...". Na herufi hizi mbili kwa kuchanganyika kwao kuunda vikundi au sentensi au kitu kama hicho. Na jambo hilo linaendelea na mlolongo wa nambari, mlolongo wa kijiometri na kila kitu kina muziki wake .. Halafu walianzisha uwiano wa usanisi kwa kuingiza mlolongo wa hesabu na jiometri, na idadi ya muziki ilionekana na kadhalika... Na juu ya hii muziki wa Waarabu na ustaarabu wa Kiislamu ulijengwa.
Muziki kwa Waislamu - na kwa kufumbia macho hukumu yake katika Sheria - una "mfumo" na una maana ya kimfumo. Kama unapopanda, hushuka: hupanda kwa kile kinachoitwa (Al-Jawab: sauti ya juu zaidi), kisha hushuka kwa kile kinachoitwa (Al-Qarar: hali ya chini kabisa ya sauti). Kuna uthabiti, na uthabiti unamaanisha “Uthabiti mutlaki”, na unamaanisha kwamba aliyezalisha hali hii alikuwa akiamini kwa mutlaki, na akahusisha sheria za kimsingi ambazo alizitegemea ujenzi wake kwa “Mutlaki”; Hiyo ni, misingi iliyo nje ya nafsi yake na nje ya tabia ya jamii yake nyembamba.
Kwa hivyo, huyu ndiye mtu anayeweza kuelewa maana ya uadilifu mutlaki, ukweli mutlaki, na haki mutlaki... tofauti na mtindo wa Magharibi ambao unadai kwamba vitu vyote ni vya kiasi. Hii ndio tofauti kuu kati ya ustaarabu wetu na ustaarabu wa Magharibi: mzee wetu anasema umuhimu wa uwepo na ulazima wa kutambua “mutlaki” ambayo maisha yake yanapaswa kupimwa, na huko Magharibi wanasema kwamba “mutlaki” labda haipo au haina maana. Na haya yote hufanyika katika ulimwengu unaokaa katika roho na akili: ulimwengu wa maono kamili ambayo huathiri mambo yote ya ustaarabu halisi.
Wengine wanaweza kuulizana: Je! Ni yupi iliyoleta maisha (ustaarabu halisi) au maadili na maono ya jumla? Na sisi - kwa kweli - hatujui mwanzo wa mada kutokana na mwisho wake. Je, dhana hizi na maono ndiyo ambayo yalileta ustaarabu, au ustaarabu ulioleta dhana hizo? Au ni mduara kama vile wataalamu wa mantiki wanaoita “zamu”, kama swali la yai na kuku?
Ili kufafanua zaidi maono haya, vyanzo vyake, na sifa zake zilizo wazi, tunawasilisha mifano ya maingiliono ya mawazo ya urithi yanayoshughulikia mutlaki na maswala yake kadhaa:
Wamesimama - katika urithi - juu ya matukio kadhaa ambayo ni sawa na masuala ya zamu na masuala ya kiasi na mutlaki, ambayo ni pamoja na jozi ya kiakili, na upili wa kiitikadi ambayo yanaonekana kupingana, kama masuala ya mwazo na mwisho, kutokuwepo na uwepo, dhati na sifa, mwisho na isiyo na mwisho, ambayo mara nyingi hupendekezwa na mwingine ambaye aliyaona mapema, na majibu yao kwa masuala haya yalikuwa dalili wazi za maono yao kwa kuwepo.
Mwingine alisema: Mtazamo wa kitu ni tawi la maoni yake (na hii ni sahihi), lakini (yule mwingine) alitaka kwa maneno yake kumfanya Mungu anamwili... Hiki ni chanzo cha upagani [Kwa sababu hii walimtengeneza mungu wao kwa mawe au mti (au hata kutokana na tende, na hata akiwa na njaa anamla), au kwa picha ya Bwana (maana yake: Nabii Issa, amani iwe juu yake) ... au kusema kwamba alikuwa akiishi ndani ya Buddha au Confucius .. au kusema: Hakika ulimwengu huu na nyenzo zake ni mola wetu, kwa hivyo wanaabudu mizimu n.k...] Kwa sababu hiyo akasema kwamba imani ya kitu na uwepo wake ni tawi la mtazamo wake.. Kwa hivyo je! kwako -Muislamu- unaweza kuamini kwa ambaye hapana kitu kama mfano wake, ambaye macho hayamfikilii, na Wala hana anaye fanana naye hata mmoja?
Muislamu mwenye urithi akajibu kupitia uhakika wake kwamba uwepo ni kielelezo cha uwepo wa mwumbaji, Mwenyezi Mungu, na kwamba akili iliyo wazi hailingani na ukweli wa uwepo wala hailingani na matini sahihi. Ikiwa haufikirii hapo mwanzo au mwisho, au katika hali zote mbili. Mtu anapobisha hodi mlangoni.. unaamini kuwa kuna mtu mwenye akili timamu amesimama mlangoni .. unaamini uwepo wake na hukufikiria dhati yake. Vivyo hivyo, ulimwengu uliumbwa na Muumba mzuri, anayeshuhudiwa na uumbaji wake. Ninamwamini bila kumfikiria mwenyewe.
Na watu wa urithi wetu waliongeza kuwa: Mwenyezi Mungu amepiga mifano katika kuwapo au ukweli ulioshuhudiwa kwa ajili ya kuelewa vitu ambavyo ni ngumu kwa akili kujitenga, na mifano hii inawajibu wale wanaokataa uwepo wa Mungu au sifa zake za juu. Mifano hii iliyopo na ya kiakili ambayo waligundua zana za kutatua shida za kifalsafa na za kiitikadi, ikiwa ni ukweli kutokana na maisha halisi au ukweli wa hesabu (na ukweli wa hesabu kwa wote wana hadhi ya vitu vinavyoaminiwa kwa akili) .. Majibu haya yalifanywa kupitia mchakato wa vikundi vya maingiliano kwa muda. Madhumuni ya mifano hii, au yeneye ya kufikiriwa kutoka kwao, ilikuwa kukadiria dhana kamili kutoka kwa uthibitisho wa kiasi na kuonyesha jumla ya akili kwa kutumia sehemu iliyogunduliwa ... Tunapitisha baadhi ya mifano hii kama "mduara", "mshumaa", "nukta", na "kioo", kwa ajili ya kuonyesha vyanzo vya akili ya kiislamu, na ilitumiaje vyanzo vyake vyote - chini ya mwavuli wa ufunuo na maono ya jumla yanayotokana nayo - katika kujenga maoni yake na mitaala ya sayansi yake.
Mduara, suala la nafsi moja, na maoni mengi: Wanachuoni wa elimu ya Tawhiyd walipiga mfano huu wa uwepo ulioshuhudiwa ili kuthibitisha ukweli wa “Mambo ya ghaibu”: kwamba Mwenyezi Mungu Mwenyewe ni mmoja na sifa zake ni nyingi, kwa hivyo waliulizana mbele ya wapinzani wao: Wapi mwanzo wa mduara? Mwanzo wake ni mwisho wake! Mahali pa kuanzia ni mahali pale pale pa mwisho; Hiyo nukta ambayo ilileta sifa mbili zinazoonekana kupingana (kama ile ya mwanzo na ya mwisho) .. Wazee walisema: "Ni nafsi moja, tofauti kwa kuzingatia: maana, kwa kuzingatia mwelekeo wa harakati kwenye mzunguko wa mduara kulia au kushoto", na suluhisho hili hili la tatizo katika hesabu ya kisasa na jiometri ya uchambuzi na wazo la "mwelekeo.": Hasi na chanya. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye sifa Tukufu. Anaye - Ametakasika - nafsi moja (Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee), na sifa na majina - ambayo ni mazuri kabisa - ni nyingi.
Nukta na suala la kutokuwepo na kuwepo: Wanachuoni wa elimu ya Tawhiyd walipiga mfano huu wa uwepo wa kushuhudiwa pia, ili kuonesha “jinsi Mwenyezi Mungu alivyoumba vitu vilivyopo kutokana na visivyo kuwepo” kwa hivyo wakasema: “Nukta” ina sifa za kushangaza sana; Haina mwelekeo, na ikienda, inaunda maumbo tofauti, inaweza kutengeneza mstari (mstari ni kuendelea kwa nukta) na inaweza kutengeneza mistari ya maumbo ya aina. Nukta - kwa ukweli - ni kama “kisichokuwepo”. Kwa sababu hakuna kitu kidogo kuliko hicho, namna gani kisiwepo hii inabadilika au karibu na kutokuwepo kwa uwepo na viumbe? Kwa hili, tunaweza kusema kwamba ulimwengu haukuwa kitu na kisha ukabadilishwa na kuwepo kwa uwezo wa juu, kwa sababu kitu ambacho sio chochote kinaweza kuwa ngumu kuwepo. Mfano wake ni “Nukta”.
Mshumaa na mwendelezo wa suala la kuumba kutokana na kutokuwepo bila kuwa na athari kwa mwumbaji: Walisema: Ikiwa tunachukua sehemu yake, ni kati ya vitu viwili: ama hupungua kwa kuchukua kutoka kwake, na hii ni hali kwa ujumla, au inaongezeka kwa kuchukua kutoka kwake kama shimo, kwa hivyo namna gani inachukuliwa kutoka kwa kitu bila mabadiliko ya ongezeko au kupungua kwa kuchukuliwa kutoka kwake? Au ni vipi Mwenyezi Mungu alituumba na sisi hatukutoka kwake na yeye hakutokana na nasi? Je! Mungu hakubadilika? Hapa ulikuja mfano wa mshumaa (ambao ni mfano kutokana na uwepo wa dhahiri) kujibu hali ya kitu ambacho kinaweza kuchukuliwa kutoka kwake, kwa hivyo hakuna ongezeko au kupungua.. Tunapokaribia utambi wa mshumaa usiowashwa kwa utambi mwingine uliowashwa, wa kwanza unawasha bila kupungua au kuongezeka kwa uzito, saizi au umbo la pili.
Hii pia ilikuja kuwajibu wale waliouliza, wakisema: Mungu yuko wapi? Je! Yuko nje ya ulimwengu? Kwa hivyo Mungu amewekewa mipaka ya ulimwengu na ana mwisho? Au ni ndani ya ulimwengu? Au ni ulimwengu unaokaa kwa Mungu? Kati ya madai ya suluhisho na madai ya shirikisho, n.k.
Kioo na suala la aliye na mwisho na asiye na mwisho: Walisema: Hakuna kitu katika uwepo huu wa kweli (mtazamo) ambacho hakina mwisho kwa ukweli, kwa hivyo kila kitu kilichopo kinahesabiwa, kupimwa, kwa chombo chochote cha kupimia .. Kwa hivyo tunawezaje kuamini kwa asiye na mwisho kabisa ambaye ni wa kwanza na hakuna kabla yake kitu chochote, naye ni mwisho, kwa hivyo hakuna kitu baada yake, naye amekizunguka kila kitu? Watu wenye urithi walijibu kwa swali: Je! Ikiwa tutaweka kioo katika makabiliano mengine? Katika hali hii, tunapata picha “zisizo na mwisho” hata jicho limechoka kufuata picha hizi. Ikiwa hii ni moja ya sifa za kioo kilichotengenezwa, basi hali ikoje katika sifa za Mungu Muumba, utukufu uwe kwake?
Kwa hivyo, Yule Muislamu mwenye urithi alisimama katika hali ya kushangaza, wakati akijaribu kujibu maswali haya na mengine ambayo yalitokana na msuguano wa kitamaduni na mwingiliano na yule mwingine. Akasema, kwa mfano: Ninaona sifa zangu mwenyewe, na maarifa yangu ninajifunza kila siku: (Hakika elimu inapatikana kwa njia ya kujifunza tu) (1). Je! Mungu hufanya hivyo? Je! Anaangalia matokeo - kama ilivyo kawaida katika ngano za kigiriki, ambazo zinaonesha miungu wanaofuata mchezo mzuri... na hufanya Jupiter – ambaye ni mungu wao mkuu - kwa mfano anajifunza kama wanadamu wanavyofanya..? Muislamu huyu anayefikiri alisema: Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua kila kitu {naapa kwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinacho fichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi; ila vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha.}[SABAA': 3] { Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi} [AL HADID: 22]. Ikasemekana: Hiyo inamaanisha kuwa ujuzi wake usio na mwisho! Je! Katika ulimwengu kuna ukweli “usio na mwisho”? “Usio na mwisho” ni maoni tu ya kiakili... yaani kukadiriwa, kwa hivyo jambo linalokadiriwa kama “lisilo na mwisho” linaweza kutimizwa? Na linalokadiriwa halina mwisho, linalotimizwa linalokuwepo lenye mwisho!
Mifano hii imependekezwa kutatua shida za kifalsafa na za kiitikadi; na kumlazimisha mpinzani anayejadiliana na hoja kutokana na chanzo chake cha maarifa (uwepo ulioshuhudiwa), pamoja na ile inavyooneshwa na mifano hii ya ukuaji wa mawazo ya urithi.
Ili kuwa na uelewa wa kina wa elimu iliyorithiwa, ni muhimu kutambua sehemu za malezi ya akili yaliyosababisha matokeo haya au elimu hii! Tunapendelea neno la “Sehemu za malezi ya akili” kuliko neno la “maono ya jumla”. La mwisho ni moja ya sehemu hizo kwa kuongeza sehemu zingine za mawazo ya urithi. Vipengele hivi havimo katika kitabu maalumu, lakini watu wote walikuwa navyo. Kwa hivyo, haviwakilishi elimu ya fiqhi, au elimu yenyewe kutoka kwa elimu za urithi, bali ni usuli ambayo ilikuwa nyuma ya akili zao na elimu zao. Ninaamini kuwa kuelewa vipengele hivi kunachangia kutufikishia mabadiliko ya dhana katika kuelewa urithi wetu, katika kujielewa sisi wenyewe, na pia kuelewa mwingine.
Ingawa inamaanisha kufuata vipengele vya kiutaratibu katika mawazo ya urithi bila kushughulikia maelezo, inaweza kusemwa - vile vile - kwamba sehemu nyingi za urithi huu bado ni muhimu kwetu na sasa ziko mezani, na zinahitajika katika kujenga mtindo wetu wa utambuzi, ingawa madai yaliyopo ya kwamba enzi yetu hii haiwezi tena kuvumilia! Je! Ni yapi maoni yetu kuhusu suala la “Uumbaji wa Qur'ani” ambalo lilifufuliwa katika robo ya pili ya Karne ya tatu A.H na bado linaendelea kuwasilishwa kwa nguvu kamili, lakini kwa maneno na vichwa vipya. Tuna njia ya kisasa iliyopitishwa na watu kama Nasr Hamed Abu Zayd, Saeed Ashmawi, Muhammad Arkoun... ambao wanaona kuwa Qur'ani ni ya kiwakati na ya kihistoria! Je! Hali hii sio sawa na kusema Qur’ani imeumbwa? Kauli kuwa “Qur'ani imeumbwa” inamaanisha kuwa ni kiumbe, na kiumbe kimeumbwa baada ya kutokuwepo duniani. Kwa hivyo, kilikuwa na mahali, na ikiwa mahali pangeondoka... Qur'ani ilibaki kihistoria, na wanasema: “Historia ya Matini” ... hadithi hiyo hiyo ina kichwa au kibwagizo kingine, kana kwamba maswala hayakuwepo kabisa…, na majina na viingilio vilibadilika tu.
Na tunasema: Hakika Qur'ani Tukufu haina kikomo cha muda, sio ya muda wala ya kihistoria... Qur'ani ni nyumbulishi, kana kwamba iliteremka sasa hivi, inapindukia wakati, mahali, watu, matokeo na hali pia.
Kwa hivyo, tunaweza kufaidika - kwa mfano - kutoka kwa elimu ya Tawhiyd - kama ilivyoanzishwa hapo awali - kutoka kwa sehemu zake zote, kama vile hatuwezi kupuuza maelezo yake katika maswala yetu ya sasa. Badala yake, inaweza kudaiwa kuwa huduma zote za siku hizi zinaweza kushughulikiwa kupitia “elimu ya Tawhyid” ya kijadi... Lakini kile tunachohitaji sana ni “kudhibiti uundaji unaofaa”, basi mtindo wa utambuzi, njia na shida... majina yao na muundo wao wote umetofautiana !!
Swali sasa ni: Je! Akili ya Muislamu mwenye urithi ilitoka wapi kutokana na majibu haya na hukumu ambazo zilitawala juu ya uwepo na hata kutokuwepo kwake?
Hii ni pamoja na kile tunachojua leo kama “vyanzo vya maarifa” au kile kinachoitwa "epistemology." Vyanzo vya ujuzi tulivyonavyo ni ufunuo na uwepo. Hakika Muislamu alikuwa akija kwenye somo la elimu na kukubali kushughulikia kwa mada yoyote... pamoja na majibu yake ya binafsi juu ya maswala ya elimu hii... kwa kutegemea kwamba kwenye kumbukumbu yake na kutumia sheria za akili ambazo zinaambatana na mfumo wake, kwa hivyo yeye huondoa hukumu zake juu ya maswala kutoka kwa vyanzo vingi
Kuna hukumu ambazo urithi huu ulizitolea kutokana na matini (ufunuo), nyingine kutokakana na akili, na nyingine kutokana na kawaida, kutokana na tabia au hisia, kutokana na maumbile, n.k., na sehemu hizi zote na vyanzo vilivyotajwa - isipokuwa kwa matini au Sheria - huitwa “kuwepo”. Kwa hivyo “Sala ni wajibu”: kufuatana na hukumu, sheria na matini, na “moto huchemsha”: kufuatana na hukumu, sheria, hisia au uzoefu, na [moja kujumulisha moja sawa sawa na mbili]: kufuatana na hukumu ya kiakili, na vile vile “"kutokutana kwa pande mbili” nayo ni hukumu ya kiakili, .. na kadhalika.
Na kukoma kwa mchakato wa kuchanganya na kuunganisha vyanzo viwili nzuri (ufunuo na uwepo) katika wakati wa sasa hali hii ambayo imetujengea maradufu ya mawazo, elimu na utamaduni. Ukosefu wetu wa ufahamu wa vitu vya mtazamo wa kiakili kati ya watengenezaji hawa wa elimu hizi za urithi (yaani, waliundaje maoni yao? Je! Waliandikaje kile walichofikiria ...?) Ndio tunaoona kati ya wamiliki wa elimu ya jamii ya sasa hivi, na tunatafuta kuishinda hali hii.
Hali ya kwamba wanachuoni wa urithi wa Kiislamu walitengeneza akili kati ya vyanzo vyao vya maarifa na hukumu juu ya mambo inaibua swali la kile kinachosemwa juu ya kuletwa kwao kwa mantiki ya Aristoteli kwa elimu za Kiislamu, na hali hii inahitaji kuzingatia kidogo.
Katika kitabu cha [Al-Muqabasat] Abu Hayyan Al-Tawhiydi alitaja mijadala kati ya Abu Suleiman mtaalamu wa mantiki na watu wa sarufi na isimu (ambao walitofautishwa na kuanzisha kwao kwa elimu zao za lugha juu ya elimu fulani ya kiakili, lakini kutoka kwa duara la Kiisilamu, lisiloingizwa kutoka kwa Aristoteli au mtu mwingine yeyote). Hoja ilitokea katika majadiliano haya, na Waarabu walishinda zaidi. Katika kutafakari, tunaona kwamba kile walichosema watu wa Kiarabu, hii ndio “mantiki” ambayo tulichukua baada ya hapo, na kwamba mantiki ya Aristoteli iliingiliana naye katika nafasi ambayo ni “kawaida ya akili ya mwanadamu,” na kwamba iliyobaki kutoka kwa mantiki ya Aristoteli ilikataliwa, na kwamba iliyobaki kutoka kwa wanachuoni wa Kiarabu ilitulia.. Na jina hilo Kilichotumiwa kwa sheria hizi ni jina ambalo lilinukuliwa kutoka kwa Aristoteli: "mantiki"... Kilichobaki kutoka kwa sheria za Aristoteli ni jina tu.
Tumeacha hili kuwa na mkanganyiko uliopo hadi sasa, kwani neno "mantiki" lilikuja kutolewa na kukusudiwa kumaanisha mantiki ya Aristoteli, na kutumiwa kumaanisha mantiki ya Kiarabu, pia inatumika kumaanisha hali ya kawaida kati ya wataalamu wa aina hizi mbili ya mantiki ... na kadhalika. Kama kwamba majina yalipunguzwa kwetu, hatukupata kwa sarufi ya kiakili ya Kiarabu jina lingine isipokuwa neno la “mantiki.” Wanachuoni wengine waligundua hili, kwa hivyo Sheikh Al-Akhdari alifupisha jambo hilo katika kitabu kiitwacho “As-Sulam” - na alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja - kwa hivyo akasema, kwa mfano:
Ibn Al-Salah na Al-Nawawi wamekataza
Na wengine walisema: Wanapaswa kuarifiwa
Na msemo maarufu na sahihi
Inaruhusiwa kwa mwenye akili kamili
Mtaalamu wa Sunna na Kitabu
Kumwongoza kwenye haki
Sheikh Al-Akhdari huyo alitofautisha kati ya maneno matupu yaliyoingizwa, na sheria hizi zilizowekwa na zilizoshirikishwa na watu wenye busara, ambazo zinapaswa kudhibitiwa na Qur’an na Sunna, sheria za Kiarabu na akili timamu.
Na wakati hali ilipotulia baada ya Abu Hayyan na wengine, ilitulia kwa Masuni kufuata mantiki hii, na wakaingia katika miundo mingi ya kanuni na elimu za Kiislamu baada ya karne ya saba kwa maana hii, na maneno ya waliopinga, kama Ibn Taymiyyah na wengine, yalibebwa dhidi ya mantiki ya Aristoto, na maneno ya wafuasi wengine yalibebwa dhidi ya mantiki ya Kiarabu, na iliitwa “mantiki”; Kwa sababu iliongelea mada sawa na mantiki ya Aristoto. Yaani marekebisho ya uelewa: mawazo sahihi na yaliyo ya moja kwa moja:
Uwiano wa mantiki moyoni ni Kama uwiano wa sarufi na ulimi.
Mantiki huzuia kutokuelewana kama inavyofanya sarufi katika mantiki ya maneno. Aristoto alileta wazo; Kuweka chombo cha kisheria kinacholinda akili kutokana na makosa - kisha kuweke mikononi mwa Muislamu na kutoka katika lugha yake, wakati anapofuata Sunna na Qur’ani ili zimuongoze kwenye usahihi . Jihadharini! Unashughulika na wakati mpana, na mfululizo wa mabadiliko, na shule nyingi, na istilahi ambazo zinaweza kupingana. Jihadharini jihadharini na misemo, jihadharini na maana tu, kwa sababu wao wanasema: (Yeyote anayetafuta ukweli kutoka katika maneno ataangamia) Hivi ndivyo alivyosema Al-Ghazali. Uangalie maana ya mantiki: ipi ni sahihi? Na ipi ni batili?
Kwa muhtasari, kuelewa urithi wa kitamaduni wa Kiislamu kunahitaji kutambua sehemu za kuunda mawazo ya urithi kwanza, na hatua hii inahitaji juhudi na uvumilivu! Halafu hatua za kufaidika na: ufuatiliaji na kufahamu, kisha kutolewa na uanzishaji, kwa mlolongo kulingana na hivyo tunaweza kufaidika na maisha yetu ya kisasa. Baada ya hapo, ukweli lazima utambuliwe na matini iliyofahimiwa iunganishwe nayo, kwa hivyo ni operesheni au matumizi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Marejeo: Al-Tariiq Ila Fahm At-Turath (njia ya Kuelewa Urithi), kwa Mufti Mkuu wa Misri, Dk Ali Jomaa.


 

Share this:

Related Fatwas