Dini ndio suluhisho.
Question
Katika malumbano ya Kitamaduni, Kistaarabu na fikra za kisasa, Je, Dini bado ni suluhisho?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hakika miongoni mwa Matatizo makubwa katika Historia ya Fikra ya Kiislamu ni mzunguko wa Fikra hii mbaya katika safari ya kusaka maamuzi, na katikati mwanga wa mzunguko huu wa Kifikra wenye Mgongano, mwanadamu katika zama zilizopita aliishi na anaendelea kuishi katika zama hizi katika maisha magumu kabisa kufikirika.
Tuchukulie mfano wa hali hiyo kutoka kwa mmoja miongoni mwa Wanafikra wa zama hizi, naye ni Alber Camy, unapozisoma tafiti zake, Simulizi na Maigizo yake hakika mambo yalivyo, utashangazwa kwa utajiri wake mkubwa wa kisanii unaopendeza, na jinsi anavyobobea kwa undani zaidi, lakini mwishowe yeye atakupeleka katika hisia zilizokumbwa na kukata tamaa na uzembe na kutokuwa na uyakinifu. Kila anachokiandika kinazama katika kiza hiki na wahusika wake wakuu mwishoni hawana la kufanya isipokuwa kujinyonga kama ni matokeo ya kawaida na ya kiakili ya Imani zao za mvurugiko wa Uadilifu, na Uadilifu wa mvurugiko. Mwandishi huyu, Alber Camy, si lolote bali ni alama ya makumi ya mamia ya Wanafikra wa zama hizi ambao wamepoteza imani ya kitu maalumu kilicho juu ya mwanadamu, na kilicho ongofu kuliko maada, na wakapoteza mtazamo ulio wazi unaohitajika kwa kila mwenye kujitengenezea njia yake katika Maisha.
Hakika Imani yao ilituama katika Akili ya Kibinadamu peke yake, lakini akili hiyo, vyovyote ikuavyo, haina uwezo wa kufanya kazi peke yake kuona na kuleta suluhisho au aina mbalimbali tatuzi za kiakili za suala hili la maisha lililo gumu na lenye mkanganyiko, kwa kuwa akili imekuwa ikikinzana na sehemu ya suala hili la maisha, na mara nyingi akili imekuwa daima ikigonga kingo za ufinyu wake na kujikuta inashindwa kuelea angani na kupaa.
Na hapo ndipo Dini inapojitokeza kama suluhisho la Mwenyezi Mungu Mtukufu linalokusanya kila kitu na lililo bobezi ili kuleta katika Suala la maisha tafsiri yake inayoingia akilini ambayo haitetereki katika wimbi la apammbano na mzunguko wake unaofedhehesha.
Dini kama suluhisho, inaanzia katika Imani ya Kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu anaeupangilia Ulimwengu wote kwa kuangazia Imani hiyo, Ulimwengu huo ambao unaonesha kwa Ujumla wake na kila kitu kimoja kimoja, Kumwamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambapo Athari inaonesha Muathiri, na kwa mfano: kama hakuna mti basi hakuna matunda.
Uhusiano baina ya mtu na Muumba wake lazima uainishwe daima na uhusiano kushindwa na kuweza, au uhusiano wa upungufu na ukamilifu, na si katika nguvu za mwanadamu kuzifikia Nguvu za Muumba wake, kwani kutangulia kwa nguvu za Mwenyezi Mungu hakutokani na mchupo wa kukua kwake, bali ni ni nguvu zisizo na kikomo kwa kila maana ya kutokuwa na kikomo cha uwezo na Siri.
Kwa hiyo, Imani ni jambo la kiutendaji zaidi la kuimarisha hali ya mwanadamu katika Dunia hii badala ya kuiacha ikitapatapa hovyo bila mwelekeo. Ingawa baadhi ya falsafa za vitu zinamfikishia Mwanadamu lengo lake, hakika Dini imelitangulia jambo hili, kwa kuivuka mipaka ya maisha ya Dunia Kuelekea katika maisha ya Akhera, kwa kufungamanisha baina ya lengo la mwanadamu hapa duniani na huko Akhera, maingiliano yenye nguvu na mahusiano ya kina, wakati ambapo juhudi za falsafa za vitu zimefungika katika kipindi kifupi cha uhai ambacho haziwezi kukivuka na kuelekea maisha mengine.
Na ili utu uweze kufanikisha uwepo wake ulio bora zaidi unatakiwa uvuke baadhi ya peo za maisha, na kuamini ya kwamba, nyuma ya peo zote hizi za Kimaisha, kuna peo zingine za juu zaidi ya hizo na ambazo zinastahili kuziendea kwa kujitolea kwa ajili yake kwa uwezo wake wote wa Kiimani. Na hapo ndipo unaapodhihiri mchango wa Dini
Kama utu hautakuwa na Imani ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isipokuwa malengo ya kidunia, basi hakika mambo yalivyo, unaweza ukayasambaratisha hata matumaini yake ya Duniani yakakatika katika, na hapo ndipo unaapodhihiri wazi wazi upungufu wa vitu.
Dini kama suluhisho huwa na Imani Kamili na hutoa lengo la Uwepo wa Ulimwengu, na hutia nguvu ya kuvuka kwa mchupo ulio na uwazi,. Na Dini peke yake ndiyo inayoyapa maisha uhai wake, na kuupa utu pumzi ya maisha yake yenye matarajio makubwa zaidi, ya kudumu yaliyo kamili, na kuelekea katika umilele. Na huu ndio ujumbe wa Dini. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Katika Fikra ya Kiislamu kwa upande wa mtazamo wa kifasihi, Dr Muhammad Ahmad Al – Arab, Cairo: Baraza Kuu la Utamaduni, 1983, (uk: 71-76)