Elimu - Kuzizalisha Ni Wajibu kwa W...

Egypt's Dar Al-Ifta

Elimu - Kuzizalisha Ni Wajibu kwa Waislamu

Question

Je! Nini hukumu ya kuzalisha elimu, ambazo zimekuwa moja ya udhihirisho wa ustaarabu wa kisasa? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ustaarabu wa Waislamu ulitokana na elimu, na Waislamu waliotangulia walianzisha elimu ambazo hutumikia mhimili wa ustaarabu wao, ambayo ni matini tukufu. Walizingatia mhimili huu, wakautumikia, wakaenda nao, na wakaufanya uwe kiwango cha kukubalika, kujibu na kusahihisha, na Waislamu wakaanza kubuni elimu kama uvumbuzi, na wanahamisha kutoka kwa mataifa yaliyopita ambayo inawawezesha kuelewa ukweli, kugundua ukweli, na kuziainisha na kuziwasilisha kwa wale walio baada yao, na kwa wale walio karibu nao, na tuliona enzi ya tafsiri katika enzi ya Al-Ma'mun, na tulimwona Al-Biruni katika kitabu chake cha: [Tahkik ma Lelhind min Maqulah Mamduha fil Aql au Mardhulah]. Tulimwona Al-Khwarizmiy katika kitabu chake cha: [Muftah Al-Ulum], ambaye anatujengea mawazo ya kielimu katika historia ya Kiislamu na anaangalia utofauti huo kwa upande mmoja, na mwingiliano kwa upande mwingine. Hizi ndizo sifa mbili zilizokubaliwa kwa kila mtu ambaye ana ufikiaji wa urithi wa Kiislamu na matokeo yake ya kiakili.
1- Kuzalisha elimu kulikuwa tabia ya wenye dini hiyo hadi karne ya nne Hijiria, bali hali hii ya kuzalisha ilienea hadi karne ya sita. Adhud Ad-Din Al-Iji aliunda elimu mpya ambayo aliiita elimu ya (kuandika elimu) ambayo aliichukua kutoka kwa elimu ya isimu, sarufi, misingi na mantiki ambayo alizungumzia - muhimu zaidi ya yale aliyoshughulikia - suala la istilahi hii, ambalo linachukuliwa kuwa moja ya maswala muhimu zaidi ya kielimu hadi leo, kwani inachukuliwa kama udhibiti wa kielimu kuhifadhi lugha ya elimu na uelewa kati ya kikundi cha kielimu pamoja na mambo mawili muhimu; Kwanza ni uhamishaji wa maarifa kwa wale wanaotufuata, na ya pili ukuzaji wa maarifa kwa njia thabiti, endelevu na yenye nidhamu wakati huo huo, basi hali ya kuzalisha hii ilififia na wataalamu wa mambo ya Elimu walikuwa wakijishughulisha kurudia urithi na kuuhifadhi ili usipotee kama jibizo la kile kilichotokea katika karne ya saba ya uvamizi wa Watatari. na anguko la Baghdad 656 H.
2- Muhammad Rashid Reda aliita kwenye jarida la "Al-Manar" kwa uundaji wa elimu mpya ambayo inasoma Sunna za kimungu zilizotajwa katika Qur’ani Tukufu. Hali hii haikutokea hata baada ya kupita kwa zaidi ya miaka mia moja baada ya wito huo, kwa hivyo lazima tuelewe kuwa elimu zinazozalishwa ni aina ya dhihirisho la maisha ya mawazo, na kwamba hazikufa, nazo pia ni dhihirisho la mwingiliano pamoja na wakati tunaouishi, tatu nazo ni daraja kati ya sheria na ukweli unaotuzunguka, na watu wengi waaminifu huuliza juu ya jinsi ya kuzalisha elimu, na inahitaji uwezo wa kufikiria kwa ubunifu, ambako kunaweza kuwa hakupo kwa wengi wa wale waliofanya kazi ya kupeleka na kuhifadhi maarifa.
Mtazamo huu wa ubunifu ni lazima kwa mchakato wa jitihada, na watu wa kale waliuona kama jiwe la msingi. Kwa hivyo, kuipoteza pia kunaashiria kufifia kwa mchakato wa jitihada ambao hutoka kwa tabia iliyoanzishwa na mwanasheria huyo huyo, na kusisitizia maana hii, tunamwona Al-Suyuti katika kitabu chake cha: [Ar-Raru Ala Man Akhlada Ila Al-Ardh wa Jahl Anna Al-Ijtihad fi Kulli Asrin Fardh], anasema kwenye ukurasa wa 169 yale anayosoma: “Alisema Ibn Burhan: Makubaliano hayakuwa pamoja na kutokubaliana kwa mujtahid mmoja, tofauti na dhehebu moja, na dalili ya kimsingi kwa mpinzani anasema kwamba idadi ya wenye jitihada kama wakikubaliana juu ya suala moja, basi hali ya kutengwa kwa mmoja wao inahitaji udhaifu kwa maoni yake, tulisema: Sio sahihi; inavyowezekana kwamba yale ambayo kila mtu ameenda kuwa maoni wazi ambayo husababisha ufahamu, na kile alichoenda mmoja tu ni sahihi zaidi, na pengine yule anayeweza kuwa pekee yake huongezeka kwa nguvu ya maono na faida katika mawazo, na hii ndio sababu ya kuwa yule anatangulizwa katika elimu katika kila wakati, hugawanya maswala, na hugundua mambo ya kushangaza”.
Halafu ananukuu kauli yake Al-Ghazaliy kutoka kwa kitabu chake kinachoitwa [Haqiqatul Qaulini] kwenye ukurasa wa 181, anasema: Katika kitabu cha [Haqiqatul Qaulini], Al-Ghazali alisema: Kuweka hali za maswala haya sio jambo rahisi kwake. Badala yake, mtu mjanja anaweza kutoa Fatwa kwenye kila suala ikiwa hali yake imetajwa kwake, hata ikiwa ni gharama kubwa kuweka hali na kuonesha matawi na matokeo yote yanayowezekana katika kila tukio. Hakuweza kufanya, na hali hizo hazikutokea hata moyoni mwake, lakini hayo ni mambo ya wenye bidii.
3- Tutoe mfano ambao unawajibu kwa wale wanaotaka mfano wa kuzalisha elimu ili kufuata mfano wake, na ili kuwatuliza wale wanaotilia shaka mchakato huu na kile wanachofikiria kinaweza kujificha dhidi ya kushambulia misingi ya dini, au kutukana matusi utambulisho wa Uislamu, kwa hivyo tunajaribu kutoa mwanga juu ya mbegu za kuzalisha elimu na mifumo ya hiyo katika urithi wa Kiislamu, tukitumaini kwamba tunaweza kutambua njia waliyofuata katika kuhudumia ustaarabu wao.
Kwa hivyo, nadhani njia ni maono kamili ambayo taratibu hutoka, na maono haya kamili ni mfano wa utambuzi ambao tulizungumzia hapo awali, na kuhusu taratibu ndio njia ya utafiti wa kielimu ambao tunaona kati ya watu wenye msimamo mkali, ambapo Ar- Razi na shule yake wanafafanua misingi ya sheria kama: “Kujua dalili za sheria kwa jumla, na jinsi ya kufaidika nayo. Na hadhi ya mnufaika,” inamaanisha kwamba, alizungumza juu ya vyanzo vya utafiti wa kifiqhi, kisha alizungumzia njia ya utafiti na mbinu zake, kisha akazungumza juu ya hali ya mtafiti, nazo hizi ni nguzo tatu katika hali zao ambazo baadaye zilichukua njia ya kielimu kama ilivyoamuliwa na “Roger Bacon” kuwa ni vyanzo, mbinu na mtafiti.
Na kabla hatujaingia katika mifumo ya kuzalisha elimu, lazima tutambue baadhi ya ukweli juu ya msimamo wa dini kuhusu elimu. Hatusemi kwamba Uislamu ni dini ya elimu tu, lakini tunaona msimamo wake juu ya utafiti wa kielimu, kama ninavyoona kwamba hakuna aibu na hakuna kizuizi kabisa katika utafiti wa kielimu, kwa hivyo atafute yeyote kuhusu anavyotaka kutafuta. Na ajaribu kutambua ukweli wa ulimwengu kama alivyotaka, na afunue uumbaji wa Mwenyezi Mungu katika ulimwengu wake kama anavyotaka, na hali hii ni dhamana ya ubunifu na inategemea ukweli kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha Aya hizi mwanzoni: {Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba (1) Amemuumba binaadamu kwa tone la damu (2) Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! (3) Ambaye amefundisha kwa kalamu. (4)} [AL-ALAQ: 1-4], Na imetajwa kwamba usomaji wa kwanza upo kwenye ulimwengu na wa pili uko katika ufunuo, na kwamba zilitolewa na Mwenyezi Mungu, usomaji wa kwanza kutoka kwa ulimwengu wa uumbaji, na usomaji wa pili katika wahyi (Ufunuo), na hali hizi mbili zilitokana na Mwenyezi Mungu; hali ya kwanza kutoka kwa Mwenye kujua ya uumbaji, na ya pili kutoka kwa Mwenye kujua ya amri {Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.} [AL AARAF: 54], na kwa hivyo hakuna mwisho kwa utambuzi wa ulimwengu; ambapo unawakilisha ukweli, kwa sababu umetolewa na Mwenyezi Mungu, na hakuna mwisho wa utambuzi wa ufunuo. Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alisema kuhusu Qura’ni: “Maajabu yake hayaishi, wala haichakai na kupitwa na wakati” na pia hakuna kutokubaliana kati yao, kwa kuwa vyote vinatokana na Mwenyezi Mungu, na msingi huu unathibitishwa kwa Aya zake, ambapo Mwenyezi Mungu anasema: {Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua?} [AZ ZUMAMR: 9].
Lakini, utumiaji wa maelezo lazima uwe chini ya upeo wa maadili Kwa kutekeleza yaliyochukuliwa kutokana na jukumu la binadamu katika ulimwengu huu: ibada, kurekebisha, na mapendekezo, upeo huo ambao unazuia utumiaji wa kile anachotupatia kinyume na amri za Mwenyezi Mungu. na unakataza au unakanusha dhamira ya jumla ya ubatili, kwa hivyo tutakuwa kati ya watu wa ujenzi, Sio kutoka kwa watu wa uharibifu, na upeo huo una umuhimu mkubwa kwani ndio dhamana ya pekee ya kurekebisha.
Mgawanyiko kati ya uhuru wa utafiti kufikia maarifa sahihi, na kizuizi cha matumizi kufikia kurekebisha, ni jambo ambalo limechanganywa na watu wengi ingawa jambo hilo lina uwazi na uhakika.
4- Pia miongoni mwa ukweli kwamba elimu ina picha kamili inayooneshwa katika mchakato jumuishi wa kufundisha kwa ajili ya kutambua maelezo, kulea kwa kupitisha maadili, na kuzoeza ili kukuza ustadi, na kwamba hii yote haigawanyiki au ikiwa imegawanyika, tutapoteza (mwongozo wa uendeshaji), kwa kusema, na upotezaji wa mwongozo wa uendeshaji unasababisha mkanganyiko na msukosuko, na inaonekana kwamba tumepoteza mwongozo huo wa uendeshaji katika nyanja nyingi za maisha yetu, sio tu ya kielimu, bali pia katika nyanja ya kisiasa, ya kijamii na ya kidini.
5- Vile vile miongoni mwa ukweli kwamba kuna tofauti kati ya elimu ya dini na ya udini. Ya kwanza hufanywa na kikundi cha kielimu na ina vyanzo vyake, mbinu, na mchakato wa elimu - kama tulivyosema hapo awali - ina nguzo zake ambazo lazima zikamilishwe na sehemu zake tano: mwanafunzi, profesa, mtaala, kitabu, na mazingira ya kielimu,
Lakini ya pili ni udini ni ombi ambalo linahitajika kwa kila mtu anayekalifishwa ili kupanga uhusiano wake na yeye mwenyewe, ulimwengu wake na Mola wake .
6- Miongoni mwa ukweli pia ni kwamba kuna tofauti kati ya Fiqhi na fikira. Fiqh mada yake ni “tendo la anayekalifishwa” na elimu ya Fiqhi inahusika na kuelezea vitendo vya wale wanaokalifishwa kwa kufanya au kuacha kufanya, na kwamba hali hii inaruhusiwa na hali ile imekatazwa kufuatana na hukumu tano za kisharia, ambazo ni wajibu, kupendekezwa, haramu, kuchukiza, na kuruhusiwa. Kuhusu fikira, mada yake ni “Ukweli wa maisha ambao ni kiasi, mchanganyiko na unaobadilishwa” fikiria hii ambayo mwanadamu hupanga vitu vinavyojulikana kama utangulizi wa kufikia kitu kisichojulikana kama matokeo, na mchakato wa kifikra ni daraja kati ya sheria na ukweli, kwa hivyo, inahitaji elimu ambayo hufanywa upya na kuzalishwa kila wakati ambapo kawaida ya ukweli ambao tunataka kuutambua una utata mkali na mabadiliko.
7 - Ikiwa haya yote hapo juu yataamuliwa, basi urithi wa Kiislamu umeweka kile kinachoitwa misingi kumi ili mtafutaji wa maarifa azitumie, kuangalia elimu ambayo ataisoma, au kujua ni nini lazima ajue, ambazo zenyewe ni sehemu zinazopaswa kuzingatiwa wakati wa kutengeneza elimu.
Baadhi ya wanachuoni waliiweka misingi hiyo katika mfumo wa shairi lililokaririwa na wanafunzi wachanga ili watake kujifunza elimu, ambayo baadaye ilipungua kati ya Waislamu katika hali ya kupokea bila kuanzishwa kwa elimu na mwendelezo wa mawazo.
Misingi kumi ni ufafanuzi wa elimu, mada yake, ni nani aliyeiunda, na sifa yake kwa elimu zingine, na kutoka kwa elimu gani, hukumu zake na maswala yake, ni nini faida yake, ni zipi hukumu zake, na lipi jina lake, na ipi faida inayotokana nayo? Hii misingi kumi inachukuliwa kama utangulizi wa elimu ambayo inasukuma mtafutaji wa maarifa kuisoma na kuipata elimu, na mfikiriaji akitaka kuijenga elimu, anaweza kuifafanua msingi hiyo kama mwanzo wa uhuru wa elimu au ubunifu, kwa hivyo, ni vipi? (inaendelea).
Miongoni mwa mifano ya elimu zinazozalishwa: Elimu ya mazungumzo ya Kiislamu:
1- Yeyote anayetaka kuangalia mfano ambao tunatoa maarifa ambayo hutumikia Uislamu na Waislamu, aanze na elimu ambayo tunaweza kuiita elimu ya mazungumzo ya Kiislamu, nayo inahitajika sana, elimu hii inayoshughulikia mwenye kutoa hutuba, mwalimu, mhubiri, na kiongozi wa Fatwa na mwongozaji wa kidini ambaye watu humchukua kama mfano mzuri. Wao hali yao ni kutambua jinsi ya kushughulika na watu, na kuhisi shida zao, na jinsi ya kuziingiza katika mlango sahihi! Tunasikia mengi juu ya pingamizi la watu kwa wanaotoa hutuba na wahubiri wengi, na juu ya hali ya machafuko ambayo ilizunguka vituo vya setilaiti, na hali hii ya machafuko ambayo ilizunguka waandishi wa habari katika kushughulika na dini, na ikiwa elimu kama hiyo ilikuwepo katika tabia hii ambayo tutaielezea itakuwa rejeleo na kiwango ambacho hupimwa kujua tofauti kati ya makosa na usawa, na mwongozo ambao unazuia kupotoka, mapungufu, au uzembe, na msukumo wa utendaji endelevu unaozaa matunda kila wakati kwa idhini ya Mola wake.
2- Elimu zinatofautishwa na mada yake, na mada ya elimu ndio inatafutwa kwa dalili zake ili maswala katika elimu hii yawe na mada na ufafanuzi unaofaa kwake, na maswala ni sentensi muhimu ambazo tumezijua katika lugha ya Kiarabu katika elimu ya sarufi na zingine, na ambazo zinajumuisha Kiima na Kiarifu, au Kitenzi na mtenda, hizo zote ni sawa katika kuonesha sentensi muhimu ambayo msikilizaji anajua nia ya mzungumzaji kutoka maneno yake hayo. Kwa hivyo, tunaona wanabalagha na wanamantiki wanaifanya kuwa moja, kwa hivyo wanabalagha huita nguzo hizi mbili za sentensi: Kiima na Kiarifu, na wanamantiki huziita: mhukumiwa na kinachohukumiwa.
Somo la elimu ya matibabu ni mwili wa binadamu kwa suala la afya na magonjwa; Kwa hivyo, mwili wa mwanadamu ni kiima, na kile kinachowasilishwa kwake kwa suala la afya na magonjwa, jinsi ya kutibu na sababu za yote hiyo ni kiarifu ambacho ni sentensi ina maana sahihi katika elimu ya matibabu, kwa hivyo mwili wa mwanadamu ni kiima - au mtenda - ni mhukumiwa, na kile kinachoarifu juu yake ni kiarifu - au kitenzi - na kinachohukumiwa na mada hiyo, kwa hivyo tunasema: Mwili wa mwanadamu huugua na vijidudu na huponeshwa na dawa – hizo zote ni sentensi ambazo zina maana sahihi na ambazo matokeo yake ni elimu, na vivyo hivyo elimu ya Fiqhi ambayo mada yake ni tendo la mtu anayekalifishwa. Kama vile Swala na Zaka, au hata wizi na mauaji, na kiarifu huja kwa njia ya hukumu, kwa hivyo tunasema: Swala ni faradhi, wizi umekatazwa, na mazungumzo ya hovyo huchukiza. Kwa hivyo sentensi hizi ni masuala la elimu ya Fiqhi.
3- Je, mada ya mazungumzo ya Kiislamu ni yapi? Tunaweza kutengeneza mada yake (kulingania dini) na hapa tutahitaji kurekebisha dhana ya kulingania, na kwamba ina nguzo tatu: msemaji, msikilizaji, ujumbe, mazungumzo au maneno, na tunaanza kuelezea sifa za msemaji, masharti ambayo lazima yatimizwe ndani yake, na elimu ambazo lazima awe nazo, Na ukweli ambao lazima aujue, zana ambazo anapaswa kuwa nazo, njia, mbinu, vyanzo na namna gani yeye lazima umiliki. Na msikilizaji, ni aina zake? Je! Viwango vyake ni vipi? Na njia ya mawasiliano inayomfaa, na njia za kupima ili kuonesha kufanikiwa kwa lengo ambalo alilokuwa nalo, na njia ambazo mawasiliano yanaambatana na kila aina ya wasikilizaji. Kisha tunageukia mazungumzo na kusoma aina yake na maudhui yake, aina na njia zake, lugha yake, kiwango chake, kipimo chake na tathmini yake, na tofauti yake, maendeleo yake na mpangilio wake. Halafu tunahamia kusoma dhana ya dawa na sifa zake ambazo hutoa mazungumzo yenye ladha nyingine na upendeleo ambao hauwezi kuwa katika aina zingine za mazungumzo, jinsi ya kuunganisha msemo na tendo, mfano mzuri, shida zinazozunguka na njia za kuishughulikia au kuikabili au kuizuia ... nk.
4- Hali zote hizi zinahitaji elimu zingine ambazo tunapata ujuzi wetu mpya, pamoja na elimu ya mawasiliano, vipimo vya maoni ya umma, vyombo vya habari, elimu ya kutoa hutuba, elimu ya Sharia, lugha na semantiki, uchambuzi wa yaliyomo na utafiti wa ndani, na matumizi ya zana zingine ambazo hutumiwa katika elimu ya kijamii na ya binadamu, kutokana na Ufuatiliaji na uchambuzi, na njia za ufafanuzi, na pia kutumia njia zinazopatikana za habari kama mtandao wa habari wa kimataifa, vituo vya setilaiti, na njia za kisaikolojia katika saikolojia ya raia na saikolojia ya mawasiliano ... n.k.
5- Tukiweka kikomo cha elimu na kujua mada yake, na kuainisha elimu ambazo tunazipatia maswala yake, na imedhihiri kwetu faharisi ya maudhui yake, na tukaipa jina kati yetu; tukashughulikia faida zake, matunda yake na matokeo yake yanayotokana nayo, na jinsi ya kuitumia, na ni lazima ujengwe mfumo wa wazi ambao unaweza kuongezwa, kukuzwa, kufanywa upya na kutoa elimu zingine zinazotokana nazo. ili tujifunze kwa kujitegemea, na kuweka miguu yetu kwenye ardhi thabiti wakati tunapolingania kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu anasema: “Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.”(YUSUF: 108).
Kwa ajili ya kutekeleza Aya hii, na ili tulinganie kwa kujua, lazima tuanzishe elimu hiyo kufundishwa kwa viongozi wa wito katika kila mahali, na kuwa hoja kwao na juu yao, na hili ndilo lengo la wito wangu wa kuzalisha elimu. Ili ustaarabu wa Kiislamu urejee katika hali yake ya hapo awali, na hatuhitaji kusikia kutoka kwa baadhi yao usemi kwamba ulikuwapo na kwa sasa haupo tena.
6- Baada ya hapo, tutapata nafasi kwa elimu ya mazungumzo ya Kiislamu kati ya elimu za kijamii kwa upande mmoja, na elimu za kisheria kwa upande mwingine, na tutajifunza faida ya elimu hii na kwamba kuishughulikia ni moja ya faradhi Kifayah (ya kutoshelezeana) ambayo yanaweza kuongezeka kwa faradhi ‘Ain (Lazima kwa kila Muislamu) kwa wale ambao walitoa wito na kuwasilisha dini kwa wale walio baada yao.
7- Kwa mwenye kuweka elimu: atakuwa mmoja wa wale wa kwanza ambao waliijumuisha, na ikiwa kikundi kimeundwa mara moja, mzozo utatokea ni yupi aliyeiunda mwanzoni, na tunarudi katika uzuri wa mjadala wa kielimu na ubishi mwingi ulioizonga akili, kuelimisha roho kukubali maoni mengine, na kufundisha wanafunzi na wasomi kufanya utafiti, kupanga ushahidi, kutafuta hoja na kuonesha umuhimu wake, na kutoka kwa akili ya Kiislamu katika kifungo cha mila, ugumu na shida ya kifikra kwamba inapita kwa aina nyingine ya kina katika uelewa na ufahamu wa kile kinachoendelea karibu nayo, na uwezo wa kuandaa mazingira ya kurudi kwa wenye kujitahidi wakubwa mara nyingine tena kuweza kuwasilisha walicho nacho kwa mantiki na uthibitisho ambao unakubaliwa na wote, hata ikiwa hawaichukui kama njia kwao, lakini wanaheshimu mtaala na wanathibitisha usahihi wake, bila ya kujali matokeo na bila ya kujali matakwa ya watu.
8- Ukweli ni kwamba elimu haijitokezi kamili, hata elimu ya Urudhi / Prosody - ambayo Al-Khalil bin Ahmed Al-Farahidi alikamata mashairi ya Kiarabu – haikujitokeza kamili, ingawa ilikuwa karibu ya kuwa kamili, isipokuwa tu kwamba tuliona Al-Akhfash akiongeza Bahr Al-Mutadarak, na tukaona wataalamu wa uelewa huu wakianzisha mizani mingine, Ni kweli kwamba Waarabu hawakuzungumza juu yake, na hakuna chochote kilichotolewa kutoka katika mashairi yao kulingana na mizani yao. Walakini, iliongeza katika elimu na kupanuka dhana ya mashairi kama ilivyoelezwa na Al-Damanhouri katika kitabu chake cha: [Al-Kafi Fi Al-Arudh wal Qawafi], hadi mkuu wa washairi Ahmed Shawqi alipounda baadhi ya mizani ambazo hazikuwa kabla ya yeye kusema:
Hali hii inafuata kile walichofanya Waandalusi hapo awali “Paukwa pakawa” na "Al-Mawaliya" na nyinginezo.
9- Kuzalisha elimu ni njia inayofaa ya kutoka kwa njia ya kielimu kutokana shida ya msuguano ambao umma unapitia, na kutokana na njia ya waadilifu ni kwamba walikwenda kwa elimu na sanaa na aina zake zote wakati Watatari waliposhambulia nchi za Waislamu, na miji ilikuwa bado ipo chini ya utawala wa Jeshi la msalaba.
Tujifunze mfano wa Imam Al-Nawawiy, ambaye alikuwa akifanya kazi masaa ishirini kwa siku kuhifadhi elimu na kuipeleka kwa wale waliomfuata. Hakulala ubavuni mwake kwa miaka miwili, na hakuoa kwa sababu ya kujishughulisha sana na elimu hadi alipokufa akiwa mdogo, chini ya umri wa miaka arobaini na tano, kulingana na hesabu ya mwaka wa Hijria. Tutaje mfano wa Al-Nuwairiy katika kitabu cha: [Nihatul Arab], Al-Qalqshandiy katika kitabu cha: [Subhu l-Asha], na Ibn Mandhur katika kamusi ya “Lisan Al Arab”, Na wengine wenye ensaiklopidia, na jinsi walivyokabiliana na madhalimu, uadui na mabadiliko ya wakati.
Je! Waislamu kweli wanahitaji ujuzi mpya ambao huitwa "elimu ya mazungumzo ya Kiislamu"? Jibu: Ndio, wanahitaji. Mahitaji ya uwepo wao, uhifadhi wa kitambulisho chao na kuishi kwao katikati ya ulimwengu ambao umekuwa kama kijiji kimoja, ambapo, kupitia usafirishaji, mawasiliano na teknolojia za kisasa, imefikia kile tunachokiona kutokana na ujirani na kuathiriana; Na hadi vizuizi kati ya mambo ya ndani na nje vilipokaribia kutoweka, na hata tuliona hoja za kutwaa ardhi yetu nchini Iraq na tishio la kuchukuliwa nchi nyingine na hali hii inaathiri kile kinachotokea nyumbani, na haifai tena kushikilia kwamba hilo ni jambo la ndani, na kwa kukataa kwetu msingi huu ambao nguvu hutumia katika kulazimisha utawala wao wa kikoloni na kufanikisha masilahi yao ya kiuchumi, ni lazima tuyafanyie kazi yale yanayobadilisha hali yetu katika njia ya Mwenyezi Mungu. Ili Mwenyezi Mungu atuangalie kwa jicho la rehema, abadilishe tulivyo navyo, na atuwezeshe kufanya kile anachopenda na anafurahishwa nacho; {Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao. Na Mwenyezi Mungu anapo watakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake} [AR-RAAD: 11].
1- Katika kongamano la nchi ya Kuwait lililoandaliwa na Kitivo cha Sheria na Masomo ya Kiislamu huko, chini ya anuani “Mazungumzo ya Kiislamu katikati ya matukio na maendeleo”, na kwamba katika kipindi cha 17-18 Mei 2004 BK, Mei. Mufti wa Misri, Prof. Dkt. Ali Jumaa alitafiti asili ya mada hii na akataka kuanzishwa kwa elimu mpya iitwayo “Mazungumzo ya Kiisilamu” .Waliohudhuria kongamano walikubaliana kati ya wasomi juu ya pendekezo hili, na waliliweka katika mapendekezo yao, jambo ambalo linaonesha umuhimu wa wito huu na umuhimu wa kuharakisha kupitishwa kwake, na kujumuisha elimu hii kuwa miongoni mwa inayofundishwa katika Vitivo vya Sheria katika Vyuo Vikuu vya Kiislamu, haswa Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na kasi ya ushirikiano wa wasomi katika uandishi kuhusu elimu hii na kuikuza, na ipate kupitiwa kutoka katika elimu kadhaa ambazo kundi la wasomi linashirikiana; Ili elimu hii iwe wazi.
2- Miongoni mwa tafiti za kongamano hilo - ambalo walihudhuria kutoka Misri: Prof. Dkt. Ahmed Omar Hashim, Mkuu wa zamani wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na mwanachama wa Chuo cha Utafiti wa Kiislamu, na Prof. Dkt. Nabil Ghanayim, profesa katika Kitivo cha Dar Uloom, na Prof. Dkt. Ibrahim Abdul Rahim, Profesa katika Kitivo cha Dar Al Uloom Chuo Kikuu cha Cairo, na kutoka Sudan, Prof. Dkt. Essam Al-Bashir, Waziri wa Waqfu, pamoja na kikundi cha wasomi kutoka Uswizi, Ufaransa, Tunisia, Saudi Arabia na Syria, pamoja na wasomi wa Kitivo cha Sheria nchini Kuwait na kutoka nchi nyingi - kinachoweza kutumiwa katika kujenga mfumo wa jumla wa elimu hiyo, naanza na kutaja haswa utafiti wa Prof. Dkt. Ahmed Jaballah, Mkuu wa Kitivo cha Ulaya cha Masomo ya Kiislamu huko Paris, chini ya anuani “Uwazi wa Mazungumzo ya Kiisilamu na Mahitaji ya Hatua ya Kisasa” ambapo alisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya Kiislamu katika uwanja wa uhusiano wa kibinadamu.
Marehemu Dkt. Mahir Alish ‘alikuwa akiwaambia wanafunzi wake wakati akifundisha “Mahusiano ya Binadamu” kwamba alikwenda Marekani kupata Digrii ya Uzamifu katika “Mahusiano ya Binadamu”, jambo ambalo halikuwa na umri wa zaidi ya miaka thelathini tangu kuzaliwa kwake, kwa hivyo akaenda kwenye maktaba katika Chuo Kikuu anachosoma; Akifikiri kwamba atapata vitabu viwili, vitatu au kumi ndani yake, atamaliza kuvisoma kisha aende kwenye digrii ya Uzamifu na kurudi Misri ndani ya miezi sita. Alimuuliza katibu wa Maktaba kuhusu vitabu vya “Mahusiano ya Binadamu” na akamuomba avilete bila kujali idadi yake, kwa hivyo akampelekea kwenye moja ya eneo la maktaba, ambalo lina duara kubwa ambapo gari linaizunguka, Naye akamwambia: Vyote vilivyo mbele yako kutoka ardhini mpaka sakafuni kwa urefu huu wote vyote ni vitabu vya Mahusiano ya Binadamu!.
Dkt. Maher Alish hakutaja tukio hili kama burudani, na sio kwa ajili ya kufunga midomo yetu kwa mshangao kwa elimu ambayo haina mwisho, lakini badala yake alilitaja tukio hili ili kuwafundisha wanafunzi wake ustadi muhimu wa kutaka kupata maarifa, upendo wa maarifa, utafiti, uandishi na maarifa, Mwenyezi Mungu amrehemu profesa huyo. Alimwamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na aliipenda Misri.
3- Halafu Prof. Ahmed Jaballah alizungumza juu ya uwingi wa njia za mazungumzo na sifa za mazungumzo ya Kiislamu, na akasema kuwa ni hotuba inayotimiza kufikisha ujumbe kwa uwazi, ina sifa ya hekima, sifa ya huruma, na inazingatia utu wa msikilizaji, hufuata msingi wa uhuru na msingi wa usawa, na huepuka kuchochea uadui na athari hasi, hujitolea kwa unyenyekevu, na haizuiliwi na upinzani na swali, nayo ni mazungumzo ya wazi; Kwa sababu anaamini ukweli wa tofauti kati ya watu, na haki ya mwingine katika itikadi yake kwa usahihi wa kile anachoamini, na hufanya jukumu la kushuhudia watu, na anajua kuwa katika enzi ya vyombo vya habari ambavyo ni wazi na utandawazi, na uwazi huu unahitaji kwamba mazungumzo hayo yawe msingi wa kusadikika kwa msemaji na utayari wa kutambua na kuelewa hoja ya mkosaji, na kufaidika kwa kuwasiliana na yule mwingine Kujihakiki mwenyewe, kurekebisha kosa, na kuonesha alama za muunganiko pamoja na anayekiuka.
Alihitimisha kutokana na haya yote kwa umuhimu wa utaalamu wa kina ulio mbali kutokana na ujumuishi wa ujinga, na akataka mchanganyiko wa uhalisi na upya, kutunza mwelekeo wa kibinadamu katika mazungumzo ya Kiislamu, kukabiliana kwa ujasiri na maswala yaliyoibuliwa, kushinda kwa hoja ya kielimu inayotokana na ushawishi badala ya mazungumzo yasiyo na maana, na kuchanganya kati ya dhana na ukweli, na kudhihirisha vipimo vya kielimu, kiroho na ustaarabu wa mazungumzo ya Kiislamu, kuboresha mazungumzo ya kuuhubiri mfumo na maudhui, na kutumia vizuri mbinu za mazungumzo ya kisasa na mbinu zake, na jambo muhimu zaidi katika yote haya ni kuwa mazungumzo ya Kiislamu yawe chini ya kalenda ya kudumu.
Na alisisitiza katika nukta hii ya mwisho kwamba kuelezea mazungumzo ya Kiislamu haimaanishi kuwa kupo juu ya ukosoaji wa kila wakati ambao unasababisha kuboresha uundaji wake, kuupanga upya na kufanya kazi ya kurekebisha njia yake ikiwa kitu kitatokea ambacho kinafedhehesha au kinafanya upungufu au uzembe, nalo ni suala muhimu sana ambalo halipo kwa viongozi wengi wa mazungumzo ya Kiislamu, na hata kwa wakosoaji; Mkosoaji mwenyewe alihisi kana kwamba alikuwa dhidi ya Uislamu wakati akipinga uundaji wake na mazungumzo yake; Kwa sababu “Haki ya wazo haihitaji kiasi cha uundaji wake na uwasilishaji mzuri. Badala yake, wazo hilo linaweza kuwa mwisho wa nguvu, na upotoshaji wake wa mfumo na mtindo hupoteza nguvu,” kulingana na usemi wa Dkt. Ahmad Jaballah katika utafiti wake uliotajwa hapo juu.
4- Halafu Mheshimiwa Mufti Prof. Dkt. Ali Jumaa alikwenda na kikundi cha wasomi na wanafikra London kuanzia tarehe 6-14 Juni 2004 BK kujadili taswira ya Uislamu na Waislamu na watu wengine wenye nia ya mawazo, elimu, siasa na sosholojia, akisema: Nimeongeza uhakika wangu katika hitaji la kuanzisha elimu hii itakayoshughulikia maswala haya magumu, maalumu ambayo yamewashangaza Magharibi na kufanya mgongano wake na urithi wa kikoloni wa ustaarabu katika nchi za Kiislamu katika machafuko mkubwa na mkanganyiko katika kushughulika hata na raia wake.
5- Halafu akasema pia: Nilipata shida ya kizazi cha tatu na matokeo yake ambayo mababu zao walihama kutoka bara la India na kwingineko, na walishiriki katika mapinduzi ya viwanda na watoto wao walishiriki katika vita ambavyo Uingereza ilipigana, na Mwislamu huyu alizaliwa ambaye hajui nchi isipokuwa hii ardhi. Na licha ya yote aliyojifunza na malezi yake, huenda kwenye vitendo vya kujiua hapa na pale, na akili ya Kiingereza haiwezi kuelewa shida hii, na mtu anakuja kwake kumwambia: kwamba Uislamu wenyewe ndio sababu; Kwa sababu ni dini inayopingana. Bernard Lewis anasema: Magaidi hutumia Uislamu, sio kwamba wamejitenga nao, na mkanganyiko huanza kati ya wasio Waislamu; Kwa sababu waliwaona wanajenga na wana amani, na ghafla aina hii hutoka kwao na "Bernard" yuko tayari na tafsiri yake hii. Kwa kweli, baadhi ya wale ambao majina yao ni majina ya Waislamu wako katika hali ya kuchanganyikiwa pia, wakieneza hapa na pale ushahidi wa kutokea kwa utata wa akili zao.
6- Elimu ya mazungumzo itasisitiza dhana nyingi zinazoelezea hali hii, kuifanya hali ya kasoro, na kuonesha sababu ya kasoro hii bila hitaji la kuchanganyikiwa. Elimu ya mazungumzo itasisitiza wazo la umma, lakini pia itaisisitiza dhana ya marejeleo, dhana ya utaalamu, na tofauti kati ya elimu ya dini na udini, na itasisitiza dhana ya masharti ambayo yako hairuhusiwi isipokuwa kuyatenda. Haijuzu kuswali bila udhuu, hata akiswali rakaa mia moja, wala kwa kibla zaidi ya Kaaba hata ikiwa anaswali rakaa elfu moja, wala kabla ya mwanzo wa wakati ambao unazingatiwa kisheria, na pia jihadi hairuhusiwi isipokuwa chini ya bendera, na wakati bendera ikipotea, hakuna jihadi, na itageuka kuua badala ya kupigana hata kama mtendaji wake akidai kuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Kupoteza kwa rejeleo na masharti ndiyo sababu ya jambo hilo, na dhana ya umma imeanzishwa katika akili ya kijana huyo, ambayo ni dhana sahihi, lakini hakuifikia ikiwa imefungwa na masharti ya kazi kupitia hayo. Kwa hivyo usawa ulisumbuliwa mkononi mwake na kuharibu zaidi ya alivyotengeneza.
Khabbab Bin Al-Arat R.A. alikuja kwa Mtume S.A.W. wakati wa udhaifu na mateso walipokuwa bado wapo Makkah: Tulimlalamikia Mtume S.A.W. (juu ya mateso kutoka kwa washirikina) akiwa amekaa katika kivuli cha Ka’ba, ameegemea juu ya Burd (guo la kujifunika). Tulimwambia: “Kwani hututakii sisi nusra? Kwani hutuombei sisi kwa Mwenyezi Mungu?” Akasema, “Alikuwa mtu wakati wa kabla yenu akichimbiwa shimo akitiwa na kuwekewa msumeno juu ya kichwa chake na kukatwa vipande viwili; lakini hilo halikumfanya kuachana na Dini yake. Mwili wake ukichanwa kwa shanuo la chuma ambapo huondoa nyama yake kutoka kwenye mifupa na mishipa, lakini hayo hayakumfanya aachane na Dini yake. Naapa kwa Mwenyezi Mungu, jambo hili (yaani Dini ya Uislamu) itaenea ambapo mtu atasafiri kutoka Sanaa (Yemen) hadi Hadhramaut bila kumhofu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, au mbwa mwitu kuhofia wanyama wake, lakini nyinyi mna pupa.”
Vile vile imethibitika katika Sunna ya Mtume S.A.W.: kwamba Abdul-Rahman bin Awf na wenzake walikuja kwa Mtume S.A.W. huko Makka na kusema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tulikuwa matajiri, wakati tulikuwa washirikina, lakini tulipoamini, tulidhalilika. Alisema: “Nimeamriwa kusamehe, kwa hivyo msipigane.”.
Na Mungu Mwenyezi amesema - kana kwamba alikuwa akihutubia wale watu wajinga ambao walipofushwa na shauku na kumtii Mola wao: {Na lau si wanaume Waumini na wanawake Waumini msio wajua mkawasaga na mkaingia makosani kutokana nao bila ya kujua ...Mwenyezi Mungu (amefanya haya) ili amuingize amtakaye katika rehema yake.} [AL FAT-HI: 25].
Kilichoshangaza katika mkanganyiko wake kati ya matini za Qura’ni zinazothibitisha jihadi, na matini zake zinazothibitisha uvumilivu, msamaha, na kukubalika kwa mwingine - hayakufahamika masharti ya kila aina moja miongoni mwao, na kujitenga kwa upande hufanya tofauti ni tofauti sio tofauti ya kupingana.
Tunasisitiza tena kwamba ni lazima elimu hii ianzishwe; tunaomba tuone tafiti zake katika miaka ishirini ijayo ikijaza sakafu nzima kwenye maktaba kuu au kupakiwa kwenye "C.D" mpaka sehemu hifadhi ya kompyuta ijazwe kwayo … Amina.
Na Mwenyezi Mungu Mtukfu ni Mjuzi zaidi.
Marejeo: Kitabu cha: Simaatul ‘Asri, kwa Mufti Mkuu wa Misri, Prof. Dkt. Ali Jomaa.


 

Share this:

Related Fatwas