Mufti wa Dharura.

Egypt's Dar Al-Ifta

Mufti wa Dharura.

Question

Wanachuoni wa Misingi wanataja katika vitabu vyao kwamba Sharti la Mufti anatakiwa awe Mujtahid, na kutimiza Sharti hili katika zama hizi ni jambo gumu mno. Je ni ipi hukumu ya kutoa Fatwa kwa mtu ambaye hajatimiza Sharti hili? Na ni ipi hukumu ya kuifanyia kazi Fatwa yake? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kutoa Fatwa katika lugha ni kubainisha, Tunaposema mtu ametoa Fatwa katika jambo fulani yaani amelibainisha jambo hilo. Na tunaposema kwamba nimemtolea Fatwa ndoto yake; yaani nimembainishia, na nilitoa Fatwa katika suala fulani yaani nilimfafanulia jambo hilo. [Tazama: kamusi ya Lisanu Al Arab 145/15, kidahizo cha: F T A, Ch. ya Dar Swader, Bairut].
Na maana ya kutoa Fatwa kiistilahi: ni kubainisha hukumu ya Kisheria kutokana na dalili kwa mwenye kuiulizia kwa kilichomtokea miongoni mwa Matukio, au kilichomtatiza katika hukumu za Kisheria. [Tazama kitabu cha: Sharhu Muntaha Al Iradat 456/3, Ch. Dar Al Fikr, Na Al Mausu'ha Al Fiqhiyah Al Kuwatiyah 20/32, Ch. ya Wizara ya Waqfu ya Kuwait]
Na Mufti ni: Mtaalamu wa Fiqhi ambaye hubeba jukumu la kuwatolea watu Fatwa kwa yale wanayoyauliza katika hukumu mbalimbali za kisheria au ni mtu ambaye anatimiza masharti yote maalumu yanayomwezesha kuzibainisha hukumu za Kisheria kutokana na dalili kwa mtu anayeulizia.
Na Mwanachuoni: ni Mujtahid na ni Mjuzi kwa vitendo au kwa uwezo unaokaribiana na utendaji, nao ni utayari wa kuzijua hukumu mbalimbali za Kisheria zinazofanyiwa kazi na ambazo yeye anajichumia kutokana nazo elimu yake kwa kuziangalia dalili zake fafanuzi.
Na imesemwa: kwamba Mjuzi au Mwanachuoni ni yule mwenye uwezo kamili unaomwezesha kuzijua hukumu mbalimbali za Kisheria pindi anapotaka pamoja na kuzijua kwake jumla nyingi za hukumu mbalimbali miongoni mwa hukumu za kimatawi, na kuzileta kwake kwa dalili zake zote, maalumu na kuu. [Tazama kitabu cha: Al Bahru Al Moheetw ka Az Zarkashiy 358- 359/8, Ch. ya Dar Al Kutubiy, Na kitabu cha: Sharhu Al Kaukab Al Muneer kwa Al Futuhiy Uk. 11-12, Ch. ya Matwba'at As Sunnah Al Mohammadiyah]
Na kujitahidi kujitenga vya kutosha kwa Mwanachuoni kwa ajili ya kupata dhana ya hukumu ya Kisheria, na maana ya kujitenga au kuwa na faragha ya kutosha: Ni kwamba Mwanachuoni ajitahidi awezavyo katika kuangalia Dalili kuu na Ndogo na aina za utoaji wa dalili na kukusanya na kurekebisha au kusahihisha na kadhalika, mpaka aweze kujua ndani ya nafsi yake kwamba hawezi tena kuongeza kitu, jambo ambalo linahitaji yeye kuwa mjuzi wa Elimu maalumu ambazo zinaimarisha ndani ya nafsi yake ya uwezo wa kujitahidi. [Tazama kitabu cha: Mukhtaswari Ibn Al Hajeb kwa Sharhu Al Aswfahaniy 288/3, Ch. ya Ofisi ya Utafiti wa Kitaaluma na kufufulisha Turaathi (Urithi wa Utamaduni) ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Umm Al Qoraa – Makkah Al Mokaramah]
Na asili ya Mtu anayebeba jukumu la kutoa Fatwa awe amefikia ngazi ya kujitahidi kuliko na mipaka mfano wake katika Fatwa mfano wa Kadhi.
Mwanachuoni Mkuu Al Kamal Ibn Al Hamam amesema katika kitabu cha: [Fat-hu Ak Qadeer 256/7, Ch. ya Dar Al Fikr]: "Tambua ya kwamba mambo yaliyotajwa katika Kadhi ndiyo yaliyotajwa kwa Mufti, na hatakiwi kutoa Fatwa isipokuwa Mujtahid, na Rai ya Wanachuoni wa Misingi imetulizana juu ya kwamba Mufti ni Mujtahid, na ama yule asiye kuwa Mujtahid katika wale wanaohifadhi Kauli za Mujtahid yeye sio Mufti, na pindi anapoulizwa, ni wajibu juu yake ataje kauli ya Mujtahid – kama vile Abu Hanifa – katika utaratibu wa kusimulia, na kwa hivyo inajulikana katika zile zinazojulikana kama Fatwa katika zama zetu hizi sio Fatwa, bali ni Kunukulu maneno ya Mufti ili Mtoaji wa Fatwa ayachukue na kuyatolea Fatwa.
Ingawa Jitihada inazingatiwa kama ni sharti la Mufti isipokuwa Wafuasi wa Madhehebu ya Imamu Abu Hanifah wa zama mpya wameeleza kuzingatia hiyo kama ni sharti yenye kupewa kipaumbele na wala sio Sharti ya kusihi Umufti na kwa hivyo inajuzu kwao kumpa Umufti Mwigaji; kutokana na kushindikana Jitihada katika zama mbalimbali mpya, lakini anapopatikana Mujtahid ni bora kupewa jukumu hilo la Umufti. [Tazama: Hashiyat Ibn Abdeen juu ya Ad Dur Al Mukhtaar 365/5, Ch. ya Dar Al Kutub Al Elmiyah]
Na Jitihada bila ya kikomo ilikuwapo kwa wingi katika Karne tatu za mwanzo ambazo ni Karne bora kuliko zote, kisha vuguvugu la Jitihadi likadhoofika pamoja na muda mwingi kupita wa kujitenga na zama za Utume na hapo ndipo viwango vya Jitihada. Na Wanachuoni wa zama mpya wamegawanya viwango vya Jitihada hadi kuwa vinne na kwa mujibu wake aina za Mamufti ziatofautina.
Wameigawa Jitihada na kuwa: Jitihada enevu (bila ya kikomo), na Jitihada fungamanifu, na wakaigawa Jitihada enevu kwa: Jitihada inayojitegemea na Jitihada inayonasibishwa na Madhehebu:: na wakaigawa Jitihada fungamanifu na kuwa Jitihada katika Madhehebu Maalumu na Jitihada katika Fatwa. [Tazama kitabu cha: Aqdu Aj Jed katika Ahkamu za Jitihadi na Taqleed kwa mwanachuoni Ad Dahalawiy, Uk.3, Ch. ya Al Matwuba'ah As Salafiyah- Al Qahirah], na kutokana na hayo; Aina za Mamufti zimekuwa aina tano, kama alivyozitajia Imamu An Nawawiy katika kitabu cha: [Al Majmou' 75-78/ /1, Ch. ya Matwuba't Al Muniriyah] nan azo ni:
Mufti Mujtahid Mwenye kujitegemea ni: yule ambaye anajitegemea kwa kuzidiriki kwake Hukumu za Kisheria kutokana na Dalili Kuu na Dalili Maalumu na wala hamuigi yoyote, sio katika Hukumu wala katika Misingi ya Kugundulia.
Mufti Mujtahid Mwenye kunasibishiwa ni: yule ambaye sio mwigaji wa Imamu wake, sio kwa Madhehebu au kwa dalili; kwani husifiwa kwa sifa ya kujitegemea lakini ananasibishiwa yeye Jitihada; kutokana na kupita kwake Njia yake katika Kujitahidi.
Mufti Mujtahid katika Madhehebu: naye ni yule anayekuwa Jitihada yake ina mfungamano na Madhehebu ya Imamu wake, na anajitegemea katika kuamua Misingi yake kwa Dalili, isipokuwa yeye havuki kwa Dalili zake Misingi ya Imamu wake na Masharti yaje: Kuwa kwake ni Mjuzi wa Fiqhi na Misingi yake pamoja na Dalili za Hukumu mbalimbali kwa undani, ana elimu ya kujua njia za vipimo mbalimbali na maana zake, yuko radhi kiukamilifu katika utohoaji na Ugunduzi.
Mufti Mujtahid katika Fatwa zake: ni yule Mlinzi wa Madhehebu ya Imamu wake, Mjuzi wa Dalili zake, Mpitishaji wake lakini Cheo chake kinaishia katika aina zilizotangulia: kutokana na kuishia kwake katika kuhifadhi na kuyalinda Madhehebu, na kuzama katika Ugunduzi au kuijua Misingi na mfano wake miongoni mwa dalili mbalimbali.
Mufti asiyekuwa Mujtahid na ni Mnukuaji wa Madhehebu ni: yule anayeyalinda Madhehebu, na kuyanukulu pamoja na kufahamu katika Mambo ya wazi na yale yenyekutatiza, lakini ana udhaifu wa kuamua dalili zake na kuhariri Vipimo vyake.
Imamu An Nawawiy amesema katika kitabu cha: [Al Majmou' 78/1]: "Hizo ndizo aina za Mamufti ambazo ni tano, ni kila aina ndani yake inashurutisha kuyalinda Madhehebu na Fiqhi binafsi, na yeyote atakayeingia katika utoaji wa Fatwa na akawa hana sifa hii basi atakuwa amejiingiza katika jambo la hatari". [Tazama pia kitabu cha: Sifa ya Fatwa na Mufti na Mwombaji Fatwa kwa Ibn Hamdaan Al Hanbaliy Ku. 16-24, Ch. ya Al Maktab Al Islamiy]
Na jambo limetulizana kwa Wanachuoni wa zama mpya kutoshurutisha Jitihada kwa Mufti, mpaka wakafikia kujuzisha Fatwa ya Mwigaji na Mwenye kunukulu Madhehebu, bali wengi miongoni mwao wamelitaja hilo la kutoshurutisha Jitihada kwa Mufti kwa kukubaliana kwa hilo.
Mwanachuoni Mkuu Taqiy Ediin Ibn Daqiq Al Eid amesema: "Kutegemeza Umufti kwa sababu ya kumpata Mujtahid kunapelekea ugumu mkubwa sana, au watu kuwa karibu na matamanio yao, kwa hiyo basi kulichochaguliwa ni kwamba Mapokezi kutoka kwa Maimamu watangulizi, kama atakuwa mwadilifu na mwenye uwezo wa kuyaelewa maneno ya Imamu wake kisha akamsimulia Mwenye Kunukulu Kauli yake basi hiyo inamtosha; kwani hiyo ni katika yale mambo ambayo dhana ya watu wa kawaida hudhani kwamba ni hukumu ya Mwenyezi Mungu kwake. Na pamepatikana Makubaliano ya wengi (Ijmai) katika zama zetu hizi juu ya aina hii ya kutoa Fatwa". [Tazama kitabu cha: Al Bahru Al Muheetw kwa Az Zarkashiy 306/6, Ch. ya Wizara ya Waqfu na Mambo ya Kiislamu. Kuwait]
Na Imamu Ar Raziy amesema katika kitabu cha: [Al Mahswoul Ku. 97-98/6, Ch. ya Mua'sasat Ar Resala]: "Wamehitilafiana juu ya kwamba Mufti asiye Mujtahid, je inajuzu kwake kutoa Fatwa kwa yale anayoyasimulia kutoka kwa mwingine?... Wanachuoni wamekubaliana kwamba katika zama zetu hizi inajuzu kwa mtu kama huyu kuifanya kazi hiyo kwani katika zama hizi hakuna Mufti Mujtahid, na kwamba Makubaliano ya Wanachuoni ni hoja tosha".
Na Mwanachuo Mkuu Azarkashiy amesema katika kitabu cha: [Al Bahru Al Muheetw 209/6]: " Na ukweli uliopo ni kwamba zama hizi hazina Mujtahid asiye na mipaka, si Mujtahid katika Madhehebu Maalumu ya mmoja kati ya Maimamu wanne".
Imamu An Nawawiy amesema katika kitabu cha: [Al Majmou' 43/1]: " na kwa muda mrefu sana, amekosekana Mufti mwenye kujitegemea na utoaji wa Fatwa sasa umekuwa kwa wenye kujinasibisha na Maimamu wa Madhehebu yanayofuatwa".
Na kwa kuwa asili ya Mufti ni kujitahidi, basi Mufti asiye Mujtahid anakuwa kinyume na asili ya Umufti, hakika mambo yalivyo, Waanachuoni wa Fiqhi wamejuzisha udharura au uhitaji wa kile kinachowatokea watu kikawa katika nafasi ya dharura، na hakika wamedharurika pia mfano wa hivyo katika mlango wa Ukadhi na hapo ukajitokeza msamiati wa Kadhi wa Dharura, naye ni yule anayehitajika kupewa nafasi ya Ukadhi au aliyepewa jukumu hilo la Kadhi na Kiongozi aliye madarakani na akawa amepungukiwa na baadhi ya masharti ya Ukadhi; kama vile kujitahidi.
Mwanachuo Mkuu Ibn Hajar Al Haitamiy wa kishafiy amesema katika kitabu cha: [Tuhfat Al muhtaaj 114/10, Ch. ya Dar Ihiyaa At Turaath Al Arabiy. Na tazama pia kitabu cha: Nihayat Al Muhtaaj kwa Ar Ramliy 240/8, Ch. ya Dar Al Fikr]: " Na Mkusanyiko wa Wanachuoni wa zama hizi, wamesema kuwa Kadhi wa Dharura ni yule ambaye amekosa baadhi ya Masharti yaliyotangulia kutajwa na anawajibika kumtaja anayemtegemea katika Masuala yote ya Hukumu zake, na wala haikubaliki kauli yake binafsi, kwa mfano anaposema: Nimetoa hukumu hii bila ya kutoa maelezo ya niliyemwegemea, na hali ilivyo ni kama vile kuwa na udhaifu wa madaraka yake".
Na kwa matokeo hayo, inawezekana kuweka Istilahi ya jina la Mufti asiye Mujtahidi kama Mufti wa dharura; kwa kukosa kwake masharti muhimu kama Kujitahidi, pamoja na kuwepo dharura ya kumpa nafasi ya Mufti.
Na Udharura unaonekana wazi kwa kuangalia kuwa Ulinzi wa Dini ni moja kati ya Makusudio Makuu Matano ya Lazima ambayo Sheria zote za Mwenyezi Mungu Mtukufu zimekuja nayo na wanavyuoni wa kisheria wameafikiana kuyaita kuwa ni: Mambo ya Dharura, au Makusudio Makuu Matano ambayo ni: Kuilinda Nafsi, Kulinda Akili, kuilinda Dini, kuilinda Heshima ya Mtu na kuilinda Mali ya Mtu.
Kwa hiyo Kuilinda Dini kunakuwa kwa kuibainisha kwa watu wote mpaka wajifunze Dini hiyo na waifikishe kwa watakaokuja baada yao, na jukumu la msingi la Mufti ni kuweka wazi mambo ya kweli ya Dini na hukumu zake kwa watu wote ili wayajue vilivyo, na wayafuate ipasavyo, ili Maisha yao ya Duniani na ya Akhera yatengemae kwayo.
Na iwapo nafasi ya Mufti haitakuwa na Mufti yeyote miongoni mwa Mamufti basi hali hiyo itapelekea kuzorotesha jukumu la kuiweka wazi Dini jambo ambalo litapelekea kuzorotesha utekelezaji wake kwa njia sahihi na kusababisha watu kuwa wajinga wa Dini yao, na kuacha kuifanyia kazi ipasavyo; kutokana na wao kukosa mtu wa kumrejea Kidini wakati wanapomhitahi mno Mufti wa kuwabainishia hukumu za Sheria za yale yanayowatokea na yanawakwaza miongoni mwa mambo mbalimbali ya Kimaisha; na kwa hivyo, nafasi ya Mufti kutokuwa na Mamufti – hata kama watakuwa wale wa Kunukulu hukumu kutoka kwa Mwingine – kuna madhara makubwa ya kutolindwa kwa Dini.
Na kwa Kauli ya kutojuzu Zama kutokuwa na Mufti Mujtahid basi hakika mambo yalivyo, hitajio ambalo linachukua nafasi ya dharura linatosha kujuzu kumweka Mufti wa dharura madarakani, ingawa Mufti Mujtahid anapatikana; kwani sio rahisi kwa kila mmoja kumfikia kwa ajili ya kumfikishia maswali ya Fatwa, na ni vigumu pia kwa Mufti Mujtahid kuwa na nafasi ya kuyashughulikia Maswali yote kikamilifu kwa wakati wote ili kufutu masuala ya kila mwislamu hapa Duniani.
Kwa hiyo, kwa kuutumia mlango wa kumuondoshea uzito, pamoja na kuuondoshea uzito umma, ni lazima kumsindika madarakani Mufti kwa ajili ya dharura katika kila nchi, Mufti ambaye atakuwa anamwakilisha Mufti Mujtahid – kama atapatikana – na aegemeza Fatwa zake kwake na atatangulizwa yule mwenye kukidhi zaidi vigezo na masharti ya Mufti Mujtahid, kisha anayemfuatia na kuendelea hivyo hivyo. Kwani chepesi hakiachwi kwa kigumu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo, na sikieni} [AT TAGHABUNI 16]. Na Mtume S.A.W. amesea: "Ninapokukatazeni kitu basi jiepusheni nacho, na ninapokuamrisheni kitu basi kifanyeni kwa kiasi mwezacho". [Imepokelewa na Masheikh wawili kutoka kwa Abu Hurairah R.A.]
Mufti kuwa madarakani ni dharura; kwa ajili ya kuondosha dharura, kwa rai ya wale wasemao kuhusu kujuzu kutokuwepo Mufti Mujtahid katika zama husika au kwa sababu ya kutatua tatizo lililojitokeza na ambalo linachukua nafasi ya dharura kwa rai ya wale wasemao kuhusu zama fulani kutokuwa na Mufti Mujtahid.
As Swafiy Al Hindiy amesema katika kitabu cha: [Nihayat Al Wuswuul 3886/8, Ch. ya Al Maktabat At Tojariyah – Makkah Al Mokaramah]: Katika maneno yake juu ya kujuzu Kwa Fatwa za Mufti asiyekuwa Mujtahid ambaye ni mwadilifu anayeaminika, mwenye umadhubuti wa kuelewa maneno ya wenye kujitahidi na Makusudio yake, na akayapokea kwa ajili ya Mtu wa kawaida aliyehitaji fatwa ili aweze kuifanyia kazi:- basi kilicho bora katika hili ni kushikamana na dharura pamoja na haja, na hakika mambo yalivyo kama sisi hatukujuzisha jambo hili, basi ingelipelekea kwamba Sheria haitoshi kubainisha matukio mapya zaidi na lililobainika ni kwamba jambo hilo linapelekea fujo na ufisadi wa hali za wanadamu.
Ndio. Asili ya Mufti anatakiwa awe Mujtahid, na Mufti anayeiga huwa badala ya Mufti Mujtahid, na wala hatafutwi wa pili isipokuwa kwa ugumu wa kukosekana wa kwanza lakini kuifanya maana ya udhuru au dharura katika Sura ya kukosekana Mujtahid sio sahihi kabisa; kwa sababu kuwa na udhuru au kushindikana kama inavyokuwa kihisia huwa pia kimaana kwa kutokuwepo asili itakayochukua nafasi, inakuwa ya kimaana kwa kutotosheka na asili kukidhi haja. Kutokana na wingi wa wanaoomba kutoa Fatwa na umbali wa nchi zao, na uhaba wa wenye kujitahidi, na ugumu wa kuwafikia, ni kweli kwamba njia za kisasa za mawasiliano zimefanya Ulimwengu uwe kama kijiji kimoja, lakini bado kuna uzito mkubwa kwa Mufti Mujtahid kuweza kujibu yeye mwenyewe kiwango kikubwa cha maombi ya Fatwa za kila Siku kutoka pande mbalimbali Duniani, na nyingi miongoni mwazo ni zile zinazokaririwa; na kwa hivyo, umuhimu wa kuwepo Mamufti wenye Kunukulu Fatwa ni sawa na ule wa Mufti Mujtahid.
Na kutokana na maelezo yaliyotangulia; Hakika mambo yalivyo, inajuzu kutoa Fatwa kwa Mufti asiyekuwa Mujtahid na katika Fatwa yake ikiwa kuna jumla nzuri ya Kisheria na Kilugha na akawa ni mwenye kujidhibiti, mwadilifu na Mjuzi wa nafsi yake na anafikiri vyema, na anautambua uhalisia. Kwa sharti la kuiengemeza Fatwa yake hiyo kwa Mujtahid, na awe Mujtahid huyo asiye na madhehebu maalumu au mwenye madhehebu ya mmoja kati ya Maimamu wenye Kujitahidi na wanaofuatwa, na amwige katika kutohoa Hukumu za Kisheria kwa Misingi ya Mujtahid asiye na mipaka na katika kuelewa Kauli zinazokubalika Kisheria na pande mbalimbali katika Madhehebu anayoyatumia kutolea Fatwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Ofisi ya Kutoa Fatwa.

 

Share this:

Related Fatwas