Miongoni mwa Haki za Binadamu Zina...

Egypt's Dar Al-Ifta

Miongoni mwa Haki za Binadamu Zinazofungamana na Makusudio ya Nafsi

Question

 Je, Haki nini za binadamu katika Uislamu zinazoendana na makusudio ya nafsi kuhusu Uadilifu, Kulindwa na Adhabu, na kulinda siri zake ?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wafuasi, na baada ya utangulizo huo:
4- Haki ya Uadilifu:
Uadilifu ni jina katika majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na ni sifa katika sifa zake, kisha imekuwa ni katika haki muhimu sana kwa ajili ya utulivu wa watu na jamii, na dhuluma ni sifa mbaya: {Wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja}( ).
Uadilifu ni moja ya Sifa za wajibu mkubwa ambao Mtume S.A.W ameletwa ili kuusimamia. Amesema Mola Mtukufu: {Na nimeamrishwa nifanye uadilifu baina yenu}( ).
Mwenyezi Mungu Ametutahadharisha na vitendo vya ugomvi unaopelekea ukiukaji wa uadilifu, na Akaunganisha kwa msisitizo kati ya uadilifu na uchamungu ambao ndio lengo la Mwislamu, Amesema Mola: {Walakuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mnona ucha-Mungu}( ).
Uadilifu ni sifa kubwa ya kimaadili inayoakisi pande zote za maisha ya Muumini.
Na uadilifu katika Uislamu ni msingi wa kimaadili kwa watu wote, na katika hali zote na mazingira yote.
Miongoni mwa haki ya kila mtu katika Uislamu kuhukumu kwa Sharia na kuhukumiwa kwa Sharia, kama vile miongoni mwa haki ya kila mwanadamu kujikinga na dhuluma: {Mwenyezi Mungu hapendi uovu uenezwe kwa maneno ila kwa mwenye kudhulumiwa}( )
Vilevile ni lazima kwa mwanadamu kumkinga mwenzake na dhulumu kwa njia anazomiliki, kwani amesema Mtume S.W.A: “Mtu amlinde ndugu yake mwenye kudhulumu au kudhulumiwa, ikiwa mwenye kudhulumu basi na amkataze, na akiwa mwenye kudhulumiwa basi na amtetee”( )
Miongoni mwa haki vilevile za mwanadamu ni kukimbilia kwenye mamlaka za kisharia kujilinda kutokana na madhara au dhuluma iliyomfikia, na kiongozi Mwislamu anapaswa kusimamia mamlaka haya, na kuimarisha ulinzi wa lazima na kusimamia utulivu wake, amesema Mtume S.A.W.: “Hakika kiongozi ni kinga na anapigana nyuma yake na uovu na kuogopwa”( )
Na haki za binadamu katika kujilinda ni haki takatifu haifai kudhulumiwa chini ya hali yoyote ile itakayokuwa, kwani Mtume S.A.W amesema pindi Myahudi alipotaka kulipwa deni lake na kisha kuongea maneno mazito, akiwafahamisha Masahaba na akasema: “Mwacheni kwani mwenye kudai ana nguvu”( )
Haki hii inaungana na haki ya mtu katika kuhukumiwa kwenye mahakama adilifu, katika uwanja huu Uislamu unazingatia kuwa kutokuwa na hatia kwa binadamu ndiyo asili, kwa kauli yake Mtume S.A.W: “Umma wangu ni wenye kusamehewa isipokuwa wale wenye kujitangaza”( )
Vilevile binadamu hazingatiwi mhalifu isipokuwa kwa Andiko la Kisharia. Amesema Mola: {Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume}( ).
Miongoni mwa aina za uadilifu katika Uislamu ni kuwa haifai kuongeza adhabu iliyopangwa Kisharia, kama ambavyo haifai kufanya usawa kati ya wahalifu wadogo na wakubwa. Amesema Mola: {Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu basi msiikiuke}( ).
Kwa upande mwingine ni kuwa, katika kusimamisha uadilifu, Uislamu umeweka kipaumbele cha kuchunga hali na sababu ambazo zimepelekea kufanyika kwa uhalifu, na kuzingatia kuwa adhabu huondoka kwa uwepo wa shaka hata kama shaka hiyo ni ndogo, amesema Mtume S.A.W: “Ondoeni adhabu kwa Waislamu kadri muwezavyo kukiwa na pakutokea basi wafutieni kesi”( ).
Hii ndiyo haki ya uadilifu kama ilivyopitishwa na Uislamu na kusisitizwa. Azimio la Kimataifa limeelezea haki za binadamu( ) kupitia haki hii. Imetajwa Azimio hilo: Binadamu wote ni sawa mbele ya sheria, ni haki yao wote kulindwa na sheria bila ya kubaguliwa, wote wana haki sawa ya kulindwa na sheria bila ya ubaguzi.
Kila binadamu ana haki ya kwenda kwenye mahakama maalumu za kitaifa ili kuzuia ukiukwaji wa haki zake za msingi( ).
5-Haki ya Kujilinda na Adhabu( ):
Kujilinda binadamu kutokana na adhabu ni haki takatifu katika Uislamu, wala haupungui utakatifu wake ulio sawa na haki yoyote nyengine katika haki za binadamu, kwani Uislamu umewajibisha kwa msimamizi wa mambo ya waislamu kutomfunga yeyote isipokuwa baada ya kuthibitika ulazima wa kufungwa, bali anapaswa kuwahakikishia wafungwa wanaotumikia adhabu ya kifungo chao, chakula chao na mavazi yao kama ni kuheshimu ubinadamu wao.
Ndiyo. Uislamu unaisimamia haki ya kila binadamu katika kuzuia uonevu wa mamlaka dhidi yake kwa sura yoyote, na haifai kumtaka mtu kutoa ufafanuzi wa kitendo katika vitendo vyake, wala kumwelekezea tuhuma isipokuwa kwa mujibu wa dalili zenye nguvu na zilizo wazi zinazoonesha kuhusika kwake katika yale anayotuhumiwa nayo: {Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhuluma kubwa na dhambi zilizowazi}( ).
Vilevile Uislamu unaisimamia haki ya kila mwanadamu ya kujilinda na adhabu, na wala haifai kumuadhibu mhalifu kwa kuzidisha adhabu husika na kumtuhumu, na katika hili amesema Mtume S.A.W: “Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale ambao wanawaadhibu watu duniani”( ).
Na akasema S.A.W.: “Mgongo wa Mwislamu unalindwa (si kwa njia yoyote ile) isipokuwa kwa njia ya haki”( ).
Akasema tena Mtume S.A.W.: “Mwenye kumuadhibu Mwislamu pasina haki basi atakutana na Mwenyezi Mungu hali ya kuwa ni mwenye hasira”( ).
Wala haifai pia kumlazimisha Mwislamu akiri uhalifu ambao hajaufanya, na kila kukiri kunakotokana na njia za kulazimishwa huko ni kukiri batili, amesema Mtume S.A.W.: “Hakika Mwenyezi Mungu Ameweka huruma kwa Umma wangu kwenye kufanya makosa na kusahau na katika yale ya kutenzwa nguvu”( ).
Vyovyote itakavyokuwa uhalifu wa binadamu, na vyovyote itakavyokuwa adhabu yake ambayo imepitishwa na Sharia ya Kiislamu, lakini ubinadamu wa mwanadamu na heshima yake ya kiutu vitaendelea kulindwa na kuheshimiwa.
Na haya yameelezewa na Azimio la Kimataifa( ) ambalo linasema kuwa: “Haifai kwa binadamu yeyote kuteswa au kuadhibiwa kwa adhabu na nguvu dhidi ya heshima ya utu wake”.
Kusudio la haki hii ni kuwa kila mmoja ana haki ya usalama, na kusimamia usalama wa mtu katika haiba yake heshima yaka na mali zake, wala haifai kushambuliwa mtu au kudharauliwa au kuadhibiwa, yawe hayo yanafanywa na serikali au na mtu binafsi.
Uislamu unaiwajibisha serikali kuwalinda watu kutokana na uadui na maudhi, na kutoa adhabu ya kukemea kwa kila mwenye kufanya vitendo vya dhuluma au uadui au kuvuka mipaka katika kutoa haki ya Kisharia. Na katika hilo Anasema Mwenyezi Mungu:
{Enyi mlio amini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika waliouwawa - muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke. Na anayesamehewa na ndugu yake chochote basi ashikwe kulipakwa wema, na yeye alipe kwa ihsani. Huko nikupunguziwa kuliko tokana na Mola wenu Mlezi, na nirehema. Na atakaye vuka mipaka baada ya haya, basi yeye atapata adhabu chungu}( ).
{Na haiwi Muumini kumuuwa Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipo kuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Naakiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni mwa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hekima}( ).
Anasema Mtume S.A.W.: “Kila Mwislamu kwa Mwislamu mwenzake ni haramu damu yake heshima yake na mali zake”( ).
Anasema Mtume S.A.W.: “Msiwaudhi Waislamu wala kuwaaibisha wala kufuatilia aibu zao, kwani mwenye kufuatilia aibu ya ndugu yake Mwislamu Mwenyezi Mungu Atafuatilia aibu yake”( ).
Vilevile, anaasema Mtume S.A.W: “Mwili wa Mwislamu unalindwa isipokuwa katika adhabu au haki”( ).
Na kufikia hilo Uislamu umeweka adhabu kwa amri zake na makatazo yake na kuweka Sharia kwa mkiukaji wa mipaka hii adhabu baadhi yake imekadiriwa kwenye adhabu yenyewe na zengine zimeachwa makadirio yake kwa Amiri nayo ni pamoja na adhabu za kinidhamu( ).
Tamko la Wanachuoni wamekubaliana kuwa adhabu za makosa ya jinai ni miongoni mwa zisizo thibiti kwa mtazamo na Kipimo bali zilimethibiti kwa maandiko, na katika hilo ikiwa ni kulinda uhuru wa mtu na kuukinga na uadui.
Ama adhabu za kinidhamu zinakuwa katika maasi ambayo hayana adhabu kali iliyopangwa wala kafara kama yule aliyeiba kitu kilichohifadhiwa sehemu imara, hata kama kitakuwa ni kidogo, au kuvunja uaminifu, au kuwafanyia udanganyifu wasimamizi wa mali za uma na mali za mayatima, au kufanya vitendo vya udanganyifu katika mashirikiano yake au kupunguza vipimo na mizani, au kutoa ushahidi wa uongo, au kuchukua rushwa au kufanya uadui kwa wananchi, na mengine mengi miongoni mwa aina ya mambo yaliyo haramu, watu hawa wanaadhibiwa kwa adhabu za kinidhamu na kutiwa adabu kwa kiwango anachokiona Kadhi kwa mujibu wa uwingi wa dhambi kwa watu, na kwa mujibu wa hali ya mwenye kufanya dhambi, na kwa mujibu pia wa ukubwa wa dhambi na udogo wake.
Adhabu za kinidhamu si adhabu za jinai, bali ni kwa ajili ya kumtia maumivu mtu kama vile kumwadabisha kwa mnasaha na makemeo au kwa makemeo ya sauti kali au kumhamisha eneo, na kuacha kumsalimia mpaka atubie, au Amiri kumuondoa kwenye uongozi, na wakati mwengine mtu anapata adhabu za kinidhamu kwa kupigwa, na katika baadhi ya hali kubwa, adhabu hizo kufikia adhabu ya kifo.
Adhabu za kinidhamu kwa ujumla hazifai kufikia kiwango kidogo cha mipaka yake( ). Na hekima ya kuacha kukadiria adhabu katika adhabu za kinidhamu kwa wasimamizi ni kutokana na tofauti ya maasi haya kwa kutofautiana muda sehemu na mazingira, basi ni katika uadilifu kuacha amri ya kukadiria adhabu yake kwa wasimamizi na mahakimu ili kuweka kila moja katika hizo yale yanayoendana kwa mujibu wa wigo ambao unaweza kupelekea kuwa adhabu nyepesi au nzito( ).
Vilevile, wamekubaliana katika kuzuia uadui isipokuwa kwa mtu dhalimu, na katika jambo hilo ni pamoja na kuwa malipo ya uadui kwa mtu dhalimu yalingane na uadui wake bila ya kuzidisha chochote( ).
Yote yaliyomo ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume wake miongoni mwa makatazo ya dhuluma na maudhi kwa mtu ni msisitizo wa haki ya binadamu ya usalama na amani kutokana na kero za mwengine( ).
6- Haki ya Binadamu katika Kulinda Siri zake.
Hakika siri za mtu hakuna wa kuziangalia isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake, na katika hili amesema Mtume S.A.W: “Je uliufungua moyo …”( ).
Siri za watu hulindwa, na hairuhusiwi kuzisambaza {Wala musichunguzane}( ).
Na Mtume amekataza kufuatilia aibu za watu, na kujaribu kufahamu yaliyo ndani mwao na yaliyofichikana katika mambo yao, akasema Mtume SAW.: “Enyi watu mwenyekusalimika kwa ulimi wake na ikawa haikuharibika Imani yake ndani ya moyo wake: Asifanye vitendo vya maudhi kwa Waislamu wala vya kuwaumbua na asifuatilie aibu zao, kwani mwenye kufuatilia aibu ya ndugu yake Muislamu basi Mwenyezi Mungu atafuatilia aibu zake, na mwenye kufuatiliwa aibu zake na Mwenyezi Mungu basi atamfedhehesha hata akiwa safarini”( ).
Katika kulinda uhai binafsi wa mwanadamu Uislamu umeelezea njia nyingi ambazo zinasimamia ulinzi huu, miongoni mwa njia hizo ni kuomba ruhusa kabla ya kuingia ndani ya nyumba ya mtu, ikiwa ni kwa lengo la kulinda siri zake.
Amesema Mola: {Enyi mlioamini! Nawakutakeni idhini iliyowamiliki mikono yenu ya kulia na walio bado kubaleghe miongoni mwenu}…. kisha Mola akasema: {Na watoto wanapo fikia umri wa kubaleghe basi nawatake ruhusa, kama walivyo taka ruhusa wa kabla yao}( ).
Kutoka kwa Abi Huraira R.A. anasema Mtume S.A.W: “Mwenye kuangalia ndani ya nyumba ya mtu bila ya ruhusa yake, basi ni halali kwake kulipasua jicho lake”( ).
Kutoka kwa Sahl Ibn Saad amesema: “Mtu mmoja aliangalia ndani nyumbani kwa Mtume S.A.W na kumuona Mtume akichana nywele zake. Mtume S.A.W akasema kumwambia yule mtu: Lau ningefahamu kuwa wewe unaangalia ndani mwangu basi ningelipasua jicho lako, kwa sababu umewekwa utaratibu wa kuomba ruhusa ambao ni kwa sababu ya jicho”( ).
Kama ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W. amekataza mtu kuangalia ndani ya kitabu cha ndugu yake pasipo ya ruhusa yake, lengo ni kulinda siri zake za alichokiandika( ).
Marejeo: Kitengo cha Tafiti za Kisharia, Ofisi ya Mufti wa Misri.

 

Share this:

Related Fatwas