Haki za Binadamu katika Uislamu Zin...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Binadamu katika Uislamu Zinazohusiana na Kusudio la Dini.

Question

 Ni zipi Haki za Binadamu katika Uislamu Zinazohusiana na Kusudio la Dini?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Hakika Haki za Binadamu zinazohusiana na kusudio la Dini zinakusanya: Haki ya kuamini, kufikiria na kujielezea, haki ya kulingania na Kufikisha Ujumbe: haki ya kuomba ukimbizi, haki za watu wachache nchini na haki ya kushiriki katika maisha ya Umma.
Kwanza: Haki ya kuabudu, kufikiri na kujielezea :
1- Katika Uislamu, kila Mtu ana Haki ya Kuabudu,, kufikiri, na kuielezea itikadi yake na mawazo yake, bila ya kuingiliwa au kunyang'anywa haki hiyo na mtu yoyote, kwa kuwa tu itikadi hiyo, na mawazo hayo na kujielezea huko vinafuata mipaka ya Misingi Mikuu ambayo sharia ya Kiislamu imeipitisha. Na kwa hivyo basi haijuzu – kwa hali yoyote - kueneza maovu wala kuyatangaza mambo mabaya yaelekeayo katika matusi au kupunguza hima ya nchi za Kiislamu; Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu. Wamelaanika! Popote watakapoonekana watakamatwa na watauliwa kabisa}. [AL AHZAAB 60-61]
Hakika Uislamu umejaalia kufikiri kama kulivyo na huru ambako kunaitafiti haki kuwa ni wajibu juu ya waislamu na haijuzu kukuachia kamwe; Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili-wawili na mmoja-mmoja; kisha mfikiri}. [SABA' 46]
Na Uislamu kwa ajili ya kuyapangilia hayo, unaweka mipaka mikuu; mipaka ambayo inaainisha halali na haramu, na chini ya Msingi Mkuu (hakuna kujidhuru au kumdhuru mtu mwingine). Na kwa hivyo basi mwanadamu lazima afikiri, lakini katika mambo yanayofaa siyo yanayodhuru, yanayomfaa yeye mwenyewe na kuwafaa wengine, na yale anayojiepushia yeye mwenyewe au kuwaepusha wengine madhara na manyanyaso.
Hakika Uislamu unamtaka mwanadamu awaze na afikiri; jinsi ya kupanda na sio kushuka na kuporomoka, jinsi ya kujifunza na kuongeza elimu yake na sio jinsi ya kuachana na elimu na kuachana na maarifa, jinsi ya kufanya vizuri na sio kufanya vibaya, jinsi ya kujenga na wala sio kuharibu, jinsi ya kujijenga yeye mwenyewe na kuijenga nchi yake na wala sio kujiharibia na kuiharibia nchi yake.
Pia kila mtu ana haki, bali ni wajibu wa kupata nafasi ya kueleza na kupinga kwake dhuluma, na kuikana, na kupambana nayo, bila ya kumwogopa au kutishwa na mtu yeyote, kwani hiyo ni jihadi bora zaidi ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake wametuamrisha tuitekeleze. Na kwa hivyo, Mtume S.A.W. aliulizwa: "Jihadi gani ni bora zaidi? Akasema: Neno la haki kwa mfalme (Sultani) dhalimu" . Lakini pia kutangaza habari sahihi na za kweli ni jambo ambalo Uislamu haulizuii isipokuwa linapokuwa na hatari na lenye kuleta madhara na kuitishia Amani ya nchi na usalama wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Na linapo wafikia jambo lolote lilio husu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangelilipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangelilijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngelimfuata Shet'ani ila wachache wenu tu} [AN NISAA 83].
Na Uislamu unakiri uwepo wa haki ya kuabudu na kujielezea, basi kutokana na hayo Uislamu haumhalalishii mtu yoyote kuzikebehi na kuzipuuzia itikadi za mtu mwengine, na wala hauruhusu kuichochea jamii dhidi yake, kwani kuheshimu hisia za wanaohitilafiana naye katika dini ni miongoni mwa maadili ya mwislamu wa kweli. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyokuwa wakiyatenda}. [AL ANAAM 108]
Na ni haki ya binadamu awe na uhuru wa kufikiri kwake, kuabudu kwake na kujielezea kwake, na haya yametajwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu : "Kila mwanadamu ana haki ya uhuru wa kufikiri, dhamira na Dini", na "Na kila mwanadamu ana haki ya uhuru wa kutoa rai na kuielezea, na haki hiyo inakusanya uhuru wa kufuata rai maalumu bila ya mtu yeyote kuingilia kati, na uhuru wa kupata maarifa, mawazo na kuyapokea na kuyatangaza kupitia vyombo vyote vya mwasiliano (redio na kadhalika) bila ya kuwekewa mipaka ya nchi"
Na kinachokusudiwa katika uhuru wa Akida ni kwamba mwanadamu ana yeye haki ya kuchagua aliyoyapata kwa jitihada yake katika dini, na kwa hivyo basi, mtu mwingine hana haki ya kumlazimisha afuate Akida maalumu au kuibadilisha Akida yake kwa kulazimishwa kwa njia yoyote iwayo .
Hakika mambo yalivyo, mfumo wowote unatakiwa kuulinda uhuru wa Akida na kuashiria wazi jinsi unavyouheshimu na kuwahakikishia watu usalama wa uhuru huo na kuujengea mazingira mazuri zaidi na Misingi bora ya Nidhamu.
Kwa hiyo Qur'ani inawafichua na kuwatia dosari watu ambao Imani yao imejengeka kwa kuwaiga wengine bila ya kuwa na mzinduko au kufikiri. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu; wao husema: Bali tutafuata tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka?} [AL BAQARAH 170]
Baada ya maelezo hayo yanayoonesha umuhimu mkubwa wa kufikiri na kutazama kwa kwa kina ili kuchagua Akida sahihi ambayo mwanadamu anaridhika nayo, Qur'ani imeeleza wazi kwamba: {Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shetani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisichovunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.} [AL BAQARA 256]
Kwa hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amemwambia Mtume wake S.A.W, akimbainishia ujumbe wake, na akasema: {Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji. Wewe si mwenye kuwatawalia} [AL GHASHIYAH 21-22]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Angeli taka Mola wako Mlezi wangeliamini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?} [YUNUS 99].
Na Sharia ya Kiislamu inaufuata mfumo wa wazi na unaohimiza na kuulinda uhuru wa Akida, Mfumo huo unaendana njia mbili :
Ya Kwanza: kuwalazimisha watu waheshimu haki ya mwingine ya kufuata Imani yoyote anayoitakia, na kwa hivyo basi, hakuna mtu yeyote anaeweza kumlazimisha mtu mwingine kufuata au kuacha Imani nyingine.
Ya Pili: Kumlazimisha Mtu mwenye Imani sahihi ana haki ya yeye mwenyewe kulinda Imani yake, na hasimamii katika msimamo dhaifu, hata kama jambo hilo litampelekea kuhamia nchi nyingini ambayo inalinda uhuru wa Imani yake na anaweza katika nchi hiyo kuitangaza Imani yake hiyo bila ya woga wowote, kwa hivyo basi kama hakuhama na alikuwa na uwezo wa kuhama, basi atakuwa anajidhulumu yeye mwenyewe kabla ya kudhulumiwa na mtu mwingine yoyote, na atapata madhambi makubwa, na anastahiki kuadhibiwa, lakini anapokuwa na mapungufu yanayompekekea asiweze kuhama, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu haikalifishi nafsi isipokuwa kwa yale inayoyaweza. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Hakika Malaika watawaambia wale ambao wamewafisha nao wamejidhulumu nafsi zao: Mlikuwa vipi? Watasema: Tulikuwa tunaonewa. Watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa wa kuhamia humo? Basi hao makaazi yao ni Jahannamu, nayo ni marejeo mabaya kabisa. Isipokuwa wale walio kuwa wanyonge miongoni mwawanaume na wanawake na watoto wasio na uweza wa hila ya kuongoza njia ya kuhama. Basi hao huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wamaghfira. Na mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na anaye toka nyumbani kwake kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti njiani basi umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu.} [ANISAA 97-100]
Na Uislamu unahimiza jinsi ya kuwahakikishia amani na usalama watu wenye akida nyingine na kuwalinda, na nyasia zake katika mambo haya ni nyinge. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema nauadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, walahawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [AL MUMTAHINAH 8]
Na kwa kuyathibitisha, hayo watu wenye dhima na watu wa kitabu, waliishi katika nchi ya Kiislamu bila ya kushambuliwa akida yao, na wala hawajawahi kulazimishwa waziache dini zao, kwani Msingi Mkuu ambao Uislamu umeuweka na unaukiri ni ule uliopo katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Nyinyi mna dini yenu, na mimi nina Dini yangu} [AL KAFERUUN 6]
Na kwa kuongezea hayo, Uislamu unadhamini uhuru wa majadiliano ya kidini, ya kielimu, yaliyo sahihi na yenye uhakika, na kukabiliana baina hoja kwa hoja ili kufikia ukweli na Imani iwe imeanza kwa ridhaa kamili na yenye uhuru, mbali ya kelele zisizo na uthibitisho wowote katika kujadili, na kuuliza au kuelezea mambo yasiyo na ukweli wowote, na machachari juu ya mwenye ugomvi bila ya kuwa na utashi wa kweli katika majadiliano yenye uhakika na yenye lengo na kujenga na sio kubomoa.
Na kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amewatuma manabii kwa ajili ya kuleta habari njema na sio kwa ajili ya kuleta habari mbaya na kuwatisha watu, wakaletwa kwa ajili ya kufundisha na kuweka wazi ujumbe walioupewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu ili atakaeangamia aangamie kwa dalili zilizo dhahiri, na asalimike wa kusalimika kwa dalili zilizo dhahiri.
Na hiyo ilikuwa njia ya manabii wote, na kwa hivyo Ibrahimu A.S. alikuwa akibatilisha mwito wa kujitia Uungu, wa wanadamu kwa njia ya kuridhisha. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Hukumwona yule aliye hojiana na Ibrahim juu ya Mola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim alipo sema: Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia nahuishana kufisha. Ibrahim akasema: Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua Mashariki, basi wewe lichomozeshe Magharibi. Akafedheheka yule aliye kufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu} [AL BAQARAH 258].
Na pia Mwenyezi Mungu Mtukufu amewatuma Musa na Harun A.S. wote wawili kwa Firauni kwa kuzijadili rai zake na kutoa hoja kwa hoja, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa} [TWAHA 44].
Na hivi ndivyo ulivyokuwa Mfumo wa majadiliano ya kidini, ulikuwa kama ulivyobainishwa na Qur'ani, na lengo la kuifanya Imani iwe inategemea kufikiri na kuridhika.
Na Uislamu unawawajibisha Waislamu kudhihirisha sifa nzuri za Dini yao kwa watu wengine, na kuwafikishia ujumbe. Bali Muislamu anakuwa ni mwenye kuchuma dhambi kwa kuificha Dini yake, na kutoitendea haki ya kuieneza na kuifikishia kwao, na kwa hivyo basi ikiwa ni heri watamjibu kwa ulinganiaji wake huo, na ikiwa ni shari watambainisha shari hiyo, kwa kutoa dalili kwa dalili, kukinaisha kwa kukinaisha, hoja na uthibitisho.
Na Mfumo wa Uislamu katika hayo unapatikana katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake}. [AL ANKABUUT 46]
Na kwa huo, unapatikana pia katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi walioongoka}. [AN NAHLI 125]
Na Mfumo huo ambao Uislamu umeupitisha kwa uhuru wa majadiliano, Mtume S.A.W, alipeleka kwa Wafalme mbalimbali Wajumbe waliozibeba Risala na wengine kujadiliana na Wafalme hao juu ya Dini na Kwamba Mtume Muhammad anawaita waingie na kuifuata Dini hiyo aliyokuja nayo.
Na Uislamu umewahakikishia Wafuasi wa wa Imani tofauti na ya Uislamu, haki yao ya kutekeleza ibada zao, kama ulivyowahakikishia haki hiyo Waislamu, na yote hayo yakiwa ndani ya mpaka wa Mfumo Mkuu, na Mfumo mzuri wa kulinda maadili na ukawaachia uhuru wa kutendeana na kuhukumia katika mambo yanayohusiana na Imani yao kwa mujibu wa Sharia zilizopitishwa kwao. Kwani Mkataba wa dhima unaambatana na kupitishwa na Kiongozi mwenye dhima juu ya Akida yao na kutopingana nao kwa sababu ya dini yake.
Na kwa hivyo basi Mtume S.A.W, aliishi pamoja na mayahudi wanayozunguka mji wa Madina kwa kuwapa Uhuru wa kufanya ibada zao za kidini. Na pia Omar Bin Al Khatwab R.A. aliwatuliza watu wa Iliya kwa kuwapatia usalama wa nafsi zao, mali zao, makanisa yao na misalaba yao.
Na Khalifa Abu Bakari R.A. alipomtuma Yaziid Bin Abi Sufiyaan kiongozi wa jeshi, alimwambia: "Wewe utakutana na watu watakaodhani kwamba wao wamejitolea muda wao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika maghala, basi uwaachie ibada zao walizoziwekea muda wa kuzifanya .
Na kama vile, Kaled Bin Al Walid R.A. alivyowanasihi watu wa Al Hirah kwamba wasivunje ahadi au kanisa na hawazuiliwi kupiga kengele na wala kutoka misalaba yao katika sikukuu yao.
Na imetajwa katika Mkataba wa Amru Bin Al Aswi kwa watu wa Misri: "Haya ndiyo aliyowapa Amru Bin Al Aswi watu wa Misri ambayo ni Usalama wa nafsi zao, Dini zao, mali zao, makanisa yao, mislaba yao, nchi kavu yao, na bahari yao, hakiingizwi kitu chochote katika hayo na wala hakipunguzwi.
2- Haki ya Kufikiri na Kujielezea:
Na mtu anayetazama katika aya za Qur`ani Tukufu atakuta kwamba Qur'ani imekuja na Ulinganiaji muhimu kwa ajili ya kuzingatia, kufahamu na kufikiri, na kwa hivyo basi Uislamu ni wito uliotolewa wa kutumia akili, kufikiri, na kutong'ang'ana. Na miongoni mwa hayo ni katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Tumekubainishieni Ishara ili mpate kuzingatia} [AL HADID 17] na pia katika kauli yake: {Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao fahamu} [AL ANAAM 98] Na pia katika kauli yake: {Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri} [AJ JATHIYAH 13] Na pia katika kauli yake: {Je! Hawaizingatii hii Qur'ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli?} [MUHAMMAD 24]
Na ili kufikiri kutendewe haki kama inavyotakiwa na Qur'ani, inahitajika kutumia elimu ya kuitumia katika kuutafuta ukweli na kufikia yakini.
Na Qur'ani Tukufu imewekwa kwa utaratibu katika kuzoeza watu kufikiri kwa hatua za mfululizo.
Na Njia ya Kwanza: Kutumia njia ya kufikiri katika mambo yanayohisika na yanayoonekana, na miongoni mwa hayo, ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa? Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa? Na milima jinsi ilivyo thibitishwa? Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?} [AL GHASHIYAH 17-20]. Na pia katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyozijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa. Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna. Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea.} [QAAF 6-8]
Na Njia ya Pili: Qur'ani inawasemesha watu kuwashawishi kwa njia ya kuwapa sababu na yanayosabaisha uwepo wake, na miongoni mwa hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Yeye ndiye anaye kuteremshieni maji kutoka mbinguni. Katika hayo nyinyi mnapata ya kunywa, na miti ya kulishia. Kwa hayo Yeye anaizalisha kwa ajili yenu mimea, na mizaituni, na mitende, na mizabibu, na kila namna yamatunda. Hakika katika haya zipo ishara kwa watu wanao fikiri. Na amefanya ukutumikieni usiku na mchana, na juana mwezi, na nyota zikutumikieni kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa watu wenye akili. Na hivi alivyo vieneza katika ardhi vya rangimbali mbali. Hakika katika hayo ipo ishara kwa watu wanao waidhika.} [AN NAHL 10 – 13].
Na Njia ya Tatu: ni njia ya mwelekeo wa juu, baada ya akili kupiga hatua ya kufikiri mpaka ilifikia kiwango hiki, na katika hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?} [AD DHARIYAT 21].
Vilevile kuna njia nyingine mbalimbali za kufikiri ambazo zimekusanywa ndani ya Aya moja ambayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali nakatika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je! Haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi wa kila kitu?} [FUSSILAT 53].
Na miongoni mwa hayo tunaona Uislamu katika kuilingania kwake Akida ya Kiislamu, unawalingania watu katika viwango vyao vyote kwa uhuru wa kufikiri ili wafikie ukweli na matokeo yanayoelekea kwenye Imani hiyo kutokana na kufikia katika kukubali kwa uhuru na utulivu wa Nafsi.
Na kulingania Kufikiri katika Uislamu hakuishii kwenye mpaka maalum, na kwa hivyo basi, kufikiri huko hakuhusiki na mambo ya kidunia peke yake tu, kwani Uislamu hauogopi Kufikiri, bali Uislamu unategemea katika ulinganiaji wake juu ya kuitendea haki akili na kuitumia ipasavyo ili iwe Mja awe na imani inayotokana na ridhaa yake kamili na huru.
Na uhuru wa kufikiri katika chanzo cha Uislamu ulitekelezwa kwa utekelezaji uliopevuka na kunawiri, na kwa hivyo basi kujitenga kwa Kundi lililojiengua kutoka kwa Imamu Ali Bin Abi Twaleb R.A. na kuwa dhidi yake na walikuwa na Fikra maalumu katika suala ya uamuzi na Masuala mengineo, basi Imamu Ali hakugombana nao na wala hajawalazimishia waiache Fikra yao, bali aliwaambia hivi: " Mna nyinyi kwetu sisi haki tatu: Hatukuzuiini kuingia misikiti ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya kulitaja jina la Mwenyezi Mungu ndani yake na wala hatuanzishi sisi vita dhidi yenu, na wala hatukuzuiini ngawira kwa kuendelea kwenu kuwa na sisi.
Na As Sarkhasiy amesema katika kitabu chake cha; [Al Mambsuutw] akitoa maelezo juu ya maneno ya Imamu kwa Makhawaariji; "Kuna dalili juu ya kwamba wao kama watakuwa hawajaazimia kutoka basi Imamu hatachukua hatua ya kuwaweka kifungoni au kuwaua, (na ndani yake kuna dalili ya kwamba kutukanwa hakuwajibishi kuadabisha kwani hakika mambo yalivyo yeye hakuwaadabisha wakati wao walipomtusi kwa kumnasibisha na Ukafiri, na ndani yake kuna dalili ya kwamba wao wanaua kwa msukumo wa kushambuliwa kwao pindi wanapoazimia kupigana vita kwa kukusanyika na kumili kwa wasio waadilifu".
Na ili Uhuru wa kufikiri upatikane, Wanachuoni wa Kiislamu waliutetea na hata kama kwa kufanya hivyo wangelinyanyaswa na kufanyiwa ubaya kama ilivyotokea kwa Imamu Ahmadi bin Hanbali.
Na kutokana na hayo, unadhihirika upeo wa jinsi Wanachuoni wa Fiqhi walivyoshikamana na Uhuru wa kufikiri na kuulinda mpaka ikawa hata kama serikali ilikosea njia yake na ikajaribu kuuzuia Uhuru huo wa kufikiri na msimamo wa Wanachuoni wa Kiislamu katika hilo ni sababu ya wao kuwarudi watawala kutokana na kupotosha kwao na Kushinda kwa Maadili yaliyoletwa na Uislamu katika kila zama.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Rejea: Idara ya Tafiti za Kisheria katika Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Misri.
 

Share this:

Related Fatwas