Haki za Binadamu katika Uislamu Zin...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Binadamu katika Uislamu Zinazoambatana na Dini.

Question

Ya Pili: Haki ya Kulingania (Daa'wa) na Ufikishaji wa Ujumbe. 

Answer

Kila mwanadamu ana haki ya kushiriki katika maisha ya jamii ambayo anamoishi ndani yake, ikiwa haki hiyo ni haki ya dini, ya kijamii, ya utamaduni na ya kisiasa au nyinginezo. Na ana haki kuzianzisha njia ambazo zinamhakikishia haki hiyo na kuitimiza katika uhalisia. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanaonifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina}. [YUSUF 108]
Hakika kwamba ni wajibu ya kila Muislamu kuamrisha mambo mema na kukataza maovu, na kuiomba jamii yake ili kuwaanzishia watu mashirika, yanayowawezesha watu kutekeleza majukumu yao, na hayo ni kutokana na njia za ubora na uchamungu na kukataza maovu na ugomvi, kama anavyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio waliofanikiwa}. [AALI IMRAAN 108], Na anasema Mwenyezi Mungu: {Na saidianeni katika wema na uchamngu} [AL MAIDAH 2]
Kwa hiyo Mtume S.A.W, anatuonya dhidi ya ubaya wa mwisho wa kuacha kuamrisha mema na kukataza mabaya, na Mtume S.A.W. anasema: "Hakika watu wakiona dhalimu na wakashindwa kumzuia udhalimu wake, basi Mwenyezi Mungu anakaribia kuwaadhibu adhabu kali". [Hadithi hii imepokewa na Wanachuoni wa Sunna]
Na hakika Mambo yalivyo kuamrisha mema na kukataza maovu ni wadhifa wa Umma wa Kiislamu, kwa hiyo ni jukumu kubwa lenye umuhimu. Abu Hamed Al Ghazaliy amesema: "Kuamrisha mema na kuataza maovu ni nguzo muhimu zaidi katika dini, na huu ni ujumbe ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu amewatumia manabii wote kwa ajili hiyo, na kama utafanywa kuwa finyu na ukafanyiwa uzembe katika utekelezaji wake, basi unabii ungesita na kuzuilika, na dini imepungua, na fitina imeenea, na ufisadi umezidi kabisa na nchi zimeharibika"
Na Azimio la Umoja wa Mataifa limeitaja haki ya kulingania katika kauli yake:
"Kila mwanadamu ana haki ya uhuru wa kuhudhuria mikutano ya amani na kuunga mkono vyama au Jumuiya zenye malengo ya amani". "Haijuzu kumlazimisha mwanadamu kujiunga kwa nguvu katika Jumia au chama miongoni mwa vyama". "Kila mwanadamu ana haki ya kushiriki kwa utashi wake katika maisha ya jamii ya kiutamaduni " .
Ya Tatu: Haki ya Kuomba Ukimbizi:
Haki hiyo, Uislamu unamuhakikishia Usalama kila mwenye kudhulumiwa au kuteswa, awe Muislamu au sio Muislamu, mweupe au mweusi, kutoka Mashariki au kutoka Magharibi. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahala pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni watu wasiojua kitu}. [AT TAWBAH 6] Basi mwenye kudhulumiwa au aliyeteswa ana haki ya kuomba ukimbizi mahali panapoulinda usalama wake, katika mipaka ya mahali pa Uislamu. Na Nyumba ya Mwenyezi Mungu ya Makka (Al Kaabah), Mwenyezi Mungu akaijaalia iwe pahala pa kukusanyikia watu na pahala pa amani, basi Muislamu yeyote hazuiliwi kamwe mahali hapo. Kama anavyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mwenye kuingia humo anakuwa katika Amani} [AALI IMRAAN 78], {Na kumbukeni tulipo ifanya ile Nyumba (ya Al Kaaba) iwe pahala pa kukusanyikia watu na pahala pa amani} [AL BAQARAH 125].
Na Uislamu kwa kuithibitisha kwake haki hiyo, ulikuwa tayari umekwisha Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu ambalo linasema kama linavyonukuliwa: "Kila mtu ana haki ya kutafuta Kimbilio la Usalama katika nchi nyingine, kwa ajili ya kujiepusha na mateso".
Ya Nne: Haki ya Watu Wachache katika Nchi:
Uislamu umeweka msingi kamili wa kuyaongoza na kuyatolea Maamuzi Masuala ya Kidini ya wachache ndani ya Nchi ya Kiislamu, Msingi huo ni: {Hapana kulazimisha katika Dini} [AL BAQARAH 256].
Ama hali za kiraia na hali za binafsi kwa watu wachache, basi sheria ya Kiislamu inawahukumu Kiislamu iwapo wataomba kuhukumiwa Kiislamu na Waislamu, hata hivyo hawalazimishwi kuzifuata hukumu hizo, bali wana haki ya kujihukumu kwa Sheria zao wenyewe, na wana haki pia ya kuomba wahukumiwe Kiislamu, kama na wao wataridhia na kukubali hivyo bila ya kulazimishwa kufuata Sheria hizo za Kiislamu.
Na kutokana na hayo, katika Nchi ya Misri, mifumo na kanuni zimeendelea kuitegemea kwa Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi wakikujia, wahukumu baina yao au jipuuze nao. Na ukijipuuza nao, basi wao hawatakudhuru kitu. Na ukiwahukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda waadilifu}. [AL MAIDAH 42] Basi wasipoomba kuhukumiwa Kiislamu na Waislamu, basi watalazimika kuomba kuhukumiwa kwa kutumia Sheria zao wao wenyewe zenye asili ya kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati yenye hukumu za Mwenyezi Mungu? Kisha baada ya hayo wanageuka. Na hao si wenye kuamini} [AL MAIDAH 43], na kauli yake: {Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu ndani yake} [AL MAIDAH 47].
Na Uislamu umewahakikishia wachache hao, haki zao, kama vile, kuwaheshimu wao, kuzilinda roho zao, mali zao, heshima zao, dini zao kwa njia iliyo bora zaidi kuliko dini na sheria zote.
Na watu wenye dhima, (ni makafiri waliolipa kodi katika nchi za Kiislamu) wao wakristo na mayahudi na wengineo walioahidiana na Waislamu na wamekaa katika nchi za Kiislamu na wanawajibika kufuata hukumu za Uislamu.
Usawa huo umethibitishwa na Qur'ani Tukufu, Sunna, Wanachuoni wa Fiqhi, kauli za makhalifa na Wanachuoni wa Fiqhi.
Na miongoni mwa dalili za Qur'ani Tukufu ni:
Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Walio amini, na Mayahudi na Wakristo, na Wasabai; yeyote atakaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akatenda mema basi watapata malipwa yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika} [AL BAQARAH 62]. Na maana ya hayo ni kwamba usawa wa thawabu ni kiasi cha kazi, bila ya kuyaangalia yale ambayo yalikuwapo kabla ya Uislamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa waliopewa Kitabu kabla yenu, mtakapowapa mahari yao, mkafunganao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anayekataa kuamini bila shaka a'mali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara} [AL MAIDAH 5] Na hayo yanataka wawapo mabadilishano ya manufaa baina ya Waislamu na wenye dhima na ujirani mwema kwa kuishi nao kwa amani.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [AL MUMTAHINAH 8]. Na katika hayo kuna ulinganiaji ulio na ubora na uadilifu kwa wenye dini tofauti kwa sharti moja tu, nalo ni wao kutowapiga vita Waislamu.
Na miongoni mwa dalili za Sunna tukufu:
Hadithi zinazouzungumzia uadilifu pamoja na watu wenye dhima, na hadithi hizo ni nyingi; miongoni mwake ni: kauli ya Mtume S.A.W.: "Itambulike kuwa mtu yeyote atakayemdhulumu (asiye muislamu anayeishi katika nchi ya Waislamu) au akambebesha majukumu zaidi ya uwezo wake au akamdharau au akachukua kitu chochote kutoka kwake bila ya ridhaa ya nafsi yake basi mimi nitakuwa hoja kwake Siku ya Kiama"
Na Mtume S.A.W. amesema: "Mtu yoyote atakayemuudhi Dhimiy basi mimi ni mgomvi wake, na Mtu yoyote ambaye mimi nitakuwa Mgomvi wake basi nitakuwa Mgomvi wake Siku ya Kiama"
Na imetajwa katika wasia wa Omar Bin Al Khatwab katika siku za mwisho wa maisha yake: " Ninamuusia Khalifa atakayekuja baada yangu mimi, ninamuusia kheri juu ya Watu wa Dhima, autekeleze Mkataba wao ipasavyo na apigane vita pamoja nao na asiwabebeshe majukumu Mazito kuliko uwezo wao"
Na kutoka kwa Aliy Bin Abuu Twaleb amesema: " Hakika mambo yalivyo, ni kwamba wao waliukubali Mkataba na Dhimiy ili Mali zao ziwe kama zetu na damu yao iwe kama yetu".
Na katika kitabu cha: [Sharhu Asier As Swaghiir cha Imamu As Sarkhasiy anasema kwa kauli yake: "Na kwa sababu wao walikubali Mkataba na Dhimiy ili Mali zao na haki zao zilindwe kama vile zilivyo Mali za Waislamu na Haki zao"
Na Wanachuoni wa Fiqhi wa madhehebu zote wameeleza kwamba waislamu walipowapa dhima basi walikuwa na jukumu la kuwalinda na kuwaepushia dhulumu. Na kwa hivyo basi, watu Wote wenye dhima walikuwa miongoni mwa Wananchi wa nchi za Kiislamu".
Ya Tano: Haki ya Kushiriki katika Maisha ya Umma:
Uislamu umemuhakikishia kila mtu haki ya kuyajua yanayotendeka katika maisha ya umma wake katika mambo yanayoambatana na masilahi ya jamii yake. Basi kila mwanadamu ana haki ya kushiriki katika mambo hayo kwa kiasi Uwezo wake alionao na utayari wa Kiakili, uwezo na ujuzi, na hayo yote ni kwa ajili ya kumwezesha kutekeleza Msingi muhimu katika sheria ya Uislamu, nao ni Msingi wa Ushauri. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameuzungumzia Wasifu wa Waumini: {Na wanao mwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao} [AS SHURA 38].
Na kutoka hapa, hakika kila mwanadamu ana uwezo wa kushika vyeo na nyadhifa mbalimbali za Umma, pindi mtu huyo anapokuwa na vigezo na uwezo wa kutekeleza masharti ya lazima kisheria kwa ajili ya nyadhifa husika. Na haki hii kamwe haiwezi kudondoka kwa sababu zozote za kimatabaka au za kibaguzi au zingine zozote ziwazo, kwani, anasema Mtume S.A.W: "Waislamu Wote Damu zao zinalingana na wao ni wamoja kwa wengine, wanamhangaikia kwa Dhima yao hata mtu aliye chini". [Imepokelewa na Ahmad].
Na Msingi wa Ushauri ni Msingi wa uhusiano baina ya mtawala na mtawaliwa, na kwa ajili hiyo basi, watawaliwa wana haki ya kumchagua mtawala wao kwa utashi wao huru kwa kutekeleza Msingi huo muhimu, pia wana haki – Wakati huo huo – ya kuanzisha njia za kisheria na zinazopangilia – kama vile mabaraza ya ushauri na ya Uwakilishi – ambayo yanawahakikishia wao uangalizi na usimamizi kwa serikali na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya yoyote anaekiuka Sheria za Nchi na kushindwa kuyatekeleza Majukumu yake ipasavyo. Na kwa hivyo basi, Abu Bakr Sidiiq, R.A. amesema alipoongoza kama khalifa wa Waislamu: "Hakika Mimi nimepewa jukumu la kukuongozeni na wala mimi si bora zaidi kuliko nyinyi, na iwapo mtaniona katika Haki basi nisaidieni, na mkiniona katika jambo Batili basi nirekebisheni, na mnitii Mimi na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake, na ikiwa mtaasi basi sina mimi Utiifu wowote juu yenu". Na mtawala ana haki ya kumtii na kumnusuru watawaliwa wake.
Na kwa hakika, Ushauri ni Msingi miongoni mwa Misingi muhimu ya Uislamu, na ni moja ya nguzo za Mfumo wake wa kisiasa. Na hoja yake na uwajibu wake vimethibiti katika Qur'ani Takatifu na Sunna Tukufu na Kazi za Wema Waliotutangulia wa Umma huu. Na sheria ya Uislamu, katika kutekeleza Ushauri, imesifia kwa ujumla na kuwepesisha pale ilipouruhusu Umma wa Kiislamu kuchagua wawakilishi katika serikali kuwa ni wajibu wa Ushauri; mfumo ambao unafaa katika hali, nyakati na mahali popote.
Na haki ya mwanadamu katika kushiriki katika maisha ya Umma imetajwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa kwa kauli yake: "Kila mwanadamu ana haki ya kushirikia katika serikali ya nchi yake, iwe kushiriki huko ni moja kwa moja au kwa njia ya wawakilishi ambao wanachaguliwa katika uchaguzi huru" "Watu wote kwa usawa wana haki ya kushiriki nyadhifa za Umma katika nchi zao".
Rejea: Sehemu ya Tafiti katika Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Misri.
 

Share this:

Related Fatwas