Haki za Binadamu Katika Kipimo cha ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Binadamu Katika Kipimo cha Uislamu – Mfumo na Mtazamo wa Kimakusudio.

Question

 Ni zipi Haki muhimu Uislamu unazitangulia kwa binadamu? Na nini msimamo wa Fikra ya Kiislamu kuhusu Haki za Binadamu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
3- Kutokana na yaliyotangulia miongoni mwa maudhui tulizozitolea maelezo jumla juu ya maudhui ya Haki za Binadamu, inatubainikia kwamba dhana ya Haki za Binadamu bado ustaarabu wa kimataifa haujaafikiana nayo. Na ingawa pamekuwapo majaribio ya watu wa magharibi ya kutaka kutulazimisha mtazamo wao juu Haki za Binadamu, na ambayo kwanza kabisa yanaanzia katika misingi yao ya kifikra na ya kiustaarabu, na kwa hivyo basi tuna haki ya kuuleta mtazamo wetu hasa kwa Haki za Binadamu.
Mtazamo huu unaanzia katika misingi bora ya Kiislamu ya kiasili, na unaojengeka kwa kutegemea Misingi ya Sharia ya Kiislamu. Na tumejaribu katika maudhui zilizotangulia kuyatanguliza baadhi ya maelezo, na hasa hasa ya kifikra, ambayo yana athari kubwa katika dhana ya Haki za Binadamu kwa ujumla.
4- Na katika yafuatayo, sisi tutajaribu kulitanguliza jaribio la kwanza la Haki za Binadamu katika Uislamu, ambalo – bila shaka -- linahitaji kazi kubwa na bidii na kuendelezwa zaidi. Na tumetosheka na kwamba tumeitanguliza Mifumo ya Kinadharia ya Kiislamu ambayo inaweza kuwa Misingi ya kuzianzisha Haki za Binadamu katika Uislamu. Na kuzifungamanisha na Makusudio ya Sharia kwa ujumla, na Misingi yake Mikuu, na tunatarajia Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa tumeshinda katika jambo hilo.
5- Na miongoni mwa mitazamo hiyo ni mtazamo wa Uislamu wa Haki na Wajibu, vilivyopangwa pamoja kwa nithamu ya kiadilifu:- vinamuhakikishia kila mtu haki na wajibu wake. Na katika kivuli cha uadilifu wa Kiislamu kwa ujumla, haifai kumvunjia Mtu haki yake kwa sababu ya Mtu mwingine. Na pia katika kivuli cha uadilifu huo, hatuwezi kuona undumilakuwili wa vigezo, au tofauti ya utekelezaji, kwa mtu anayeufanyia kazi Uislamu, kazi iliyo sahihi na yenye mzinduko,, kwani hakika mambo yalivyo na Migogoro inajitokeza katika Uhalisia wa Maisha ya Duniani kutokana na matumizi ya fikra au ufahamu mbaya wa Misingi bora ya Uislamu.
6- Yako makusudio ambayo Sharia ya Kiislamu inayashughulikia na kuyahifadhi. Na makusudio hayo ni:
A- Makusudio ya Dharura; hayo ni makusudio yanayopelekea kuimarisha maslahi ya kidini na kidunia.
B- Makusudio ya Kimahitaji; hayo ni yale yanayohitajikia kupanua zaidi maisha na kuuondosha dhiki inayotokana na kusumbuliwa na kuwapo mashaka yanayosababishwa na kukosa Mahitaji au Matumaini.
C- Makusudio ya Kuboresha; nayo ni kuchukua mambo yanayofaa kutoka katika mila na desturi nzuri, na kujiepusha na mazingira ya mambo ya maovu ambayo akili safi huyachukua hayo kutokana na akili zenye busara.
7- Ama makusudio ya Kidharura ni: 1- Dini 2 - Nafsi 3 - Akili 4 - Hadhi na Heshima ya Ukoo 5 - Mali. Na Makusudio haya yamepangiliwa vyema, na kwa hivyo basi kuilindia Dini kunautangulia upinzi wa Makusudio yote yaliyobakia, na kutokana maelezo hayo, ni kwamba jihadi inawajibika kwa ajili ya kulindia Dini hata kama kufanya hivyo kutapelekea kuipoteza nafsi, kwani Ulinzi wa Dini unautangulia Ulinzi wa Nafsi, na hivyo hivyo Ulinzi wa Nafsi unautangulia Ulinzi wa Mali na Ulinzi wa Akili unautangulia Ulinzi wa Heshima na Hadhi ya mtu na Ukoo wake, na Ulinzi wa Mali unakuja katika ngazi ya mwisho kabisa ya Makusudio Makuu ya Kisharia..
8- Ama kuhusu Makusudio ya Kimahitaji ni: Ibada, mila na desturi, matendeano, makosa ya jinai. Na kwa hivyo basi, katika Ibada ni kama vile ruhusa ya kupunguza ibada ya Swala kwa sababu ya ugonjwa au safari, na katika mila na desturi ni kama vile, kuhalalisha kuwinda na kujichumia chakula kizuri, kinywaji kizuri na nguo nzuri. Na katika matendeano; ni kama vile kuhalalisha kukopeshana, kukulimana na kushirikiana katika biashara, na katika Makosa Ya Jinai ni kama vile, kufaradhisha fidia ambayo inaitwa "diah", juu ya mtu mwenye Akili na kuwawekea dhamana Wenye viwanda
9- Ama Makusudio ya Kuboresha; Makusudio haya yanakusanya tabia nzuri kama vile kuondosha najisi, twahara, kuficha uchi, kuchukua pambo, na kukaribisha kazi nzuri kama vile, sadaka, kufanya mema, adabu ya chakula na kunywa .
10- Hakuna shaka kwamba maana ya Makusudio katika Sharia ya Kiislamu ni pana zaidi kuliko dhana ya Haki za Binadamu kwa maana yake ya Kimagharibi. Na pia dhana ya Makusudio ni ya kuimarisha ya kudhibiti zaidi, na inayaainishia yanayostahiki kutangulizwa au kucheleshwa na yanayostahiki kuchelewa.
11- Tunakuta kwamba Makusudio Matano ya Kisharia ambayo ni ya Kidharura, ni Misingi ya Haki za Binadamu katika Uislamu. Na katika Makusudio Matano, kunajitokeza makusudio ya kukamilisha na kutimiza ambayo makusudio ya kiasili hayawezi kutimia isipokuwa kwayo.
12- Hapa tunajaribu kuleta jaribio la awali linaungana baina ya Haki za Binadamu na baina ya makusudio ya kisharia, kuanza kwa msingi kutoka nadharia ya makusudio ya kisharia ya kidharura, na juu ya yaliyotangulia kuelezewa kwa ujumla, tukitarajia kuendeleza jaribio hilo, hadi kufikia nadharia ya Kiislamu kwa Haki za Binadamu, ambazo zinatokana na Misingi ya sharia na makusudio yake.
Haki na Makusudio ya Kisharia :
13- Na tukiyatekeleza hayo juu ya Makusudio ya Sharia ya kidharura tunakuta kwamba katika juhudi zetu za Kuilinda Dini: Uislamu unamlinda na kumlea mtu kwa kuamua kwake kufuata Imani yoyote, na kuitekeleza ibada yake atakavyo, na Uislamu unayasthibitisha haya katika Aya ya Qur`ani kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema: {Hapana kulazimisha katika Dini} [AL BAQARAH 256] Na Uislamu unausisitizia uhuru huo na ukikanusha kulazimisha, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema kwa Mtume wake karimu: {Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?} [YUNUS 99].
14- Na kwa kuhifadhia dini: Uislamu unasimamia ukikabiliana na wanaoeneza ukafiri muda wa kuwa wametoka katika mipaka ya Akida kwa kushambulia dini na kubashiri ghasia na fujo, kwa hiyo msimamo wao unakuwa umetoka katika haki na kupigana na heri, kwa hiyo inalazimika kupunguza uhuru wao.
15- Na kwa kuilinda Hadhi na Heshima: Uislamu umehalalisha ndoa kwa ajili ya kuunda familia na kuizuia nafsi na machafu, na umeupitisha uhuru wa mume na mke katika kuchagua mwenza, na kwa hivyo basi katika kutoa wito wa kutaka Watu waoane, Mtume S.A.W. anasema: "Enyi wavulana! Mwenye uwezo wa matumizi ya ndoa basi na aoe, na asiyeweza basi afunge, kwani kufunga kwake ni kinga" . Na Mtume S.A.W. akasema: "Mwanamke mjane anajistahikia nafsi yake kuliko mlezi wake" na pia kumshauri mwali ni sharti katika mkataba wa ndoa.
16- Kwa hivyo basi mtu anapopindukia katika kuvunja heshima, na akahalalisha uzinifu, na akapoteza heshimu ya familia, na akajidhuru nafsi yake, na akaupeleka ufisadi huo kwa watu wengine, basi ni wajibu kumsitisha na kumpunguzia uhuru wake. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini} [AN NUUR 2]
17- Na katika kulinda Mali: Uislamu umeweka sharia ya uhuru wa kazi, uhuru wa kuchuma mali, na haki ya umiliki ili kutengeneza uhai na kuyatunza maisha, na kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini! Msiharimishe vizuri alivyokuhalalishieni Mwenyezi Mungu} [AL MAIDAH 87]. Na pia Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, [AL AARAF 32]. Na Mtume S.A.W. akasema: "Hakika wewe ukiwaacha warithi wako wakiwa wanajitosheleza ni heri zaidi kuliko kuwaacha wakiwa mafukara wenye kuwaombaomba watu wengine" Na kwa ajili ya kulinda mali; Uislamu umehalalisha biashara na umelingania kazi, na ukasifia Chumo linalopatikana kwa kazi kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba}. [AL BAQARAH 275]. Na Mtume S.A.W, anasema: "Hakika Mtu yeyote atakayelala usingizi kwa mchoko wa kazi ya mikono yake, basi ataamka asubuhi hali ya kuwa amesamehewa madhambi yake" Na Mtume S.A.W. anasema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda kuona athari ya neema yake kwa mja wake" Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na neema za Mola wako Mlezi zisimulie} [AD DHUUHA 11].
18- Hayo yote yamo katika mipaka ambayo mali haiwezi kuichupa, au kuvunja mipaka ya manufaa ya Umma. Na kwa hivyo basi, mali ikifikia kiwango maalumu lazima itolewe Zaka katika mali hiyo, ili kuhakikisha usawa katika jamii na uadilifu vinapatikana, na kuzuia madhara kwa wengine na kuogopea mwanadamu akosee neema. Na pia Uislamu ukazuia kwa kuharamisha kupata mali kwa njia za haramu, na ukaharamisha Riba, na ukaweka adhabu dhidi ya mwizi, lakini pia Uislamu umezua mfumo wa kuhodhi bidhaa na Kuzilangua, na ukahalalisha kutwaliwa kwa mali inayolimbikizwa. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyo yachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima}. [AL MAIDAH 38]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba}. [AL BAQARAH 275]. Na Mtume S.A.W. amesema: "Mtu yeyote atakayelimbikiza chakula (kwa lengo la kulangua) muda wa siku arobaini basi dhima ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawatakuwa na dhima yoyote kwake" . Na Mtu anapotumia mali yake katika mambo ya haramu basi Uislamu humzuia kufanya hivyo, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika wabadhirifu ni ndugu wa Mashet'ani. Na Shet'ani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi} [AL ISRAA 27]. Kwani mali inatakiwa irejeshe kwa manufaa kwa jamii yote, na katika ubadhirifu wa mali hiyo kuna kupoteza rasilimali ya Jamii na kuidhuru Jamii hiyo.
19- Na matumizi ya mali katika mambo machafu ni marufuku, kwani unamdhuru mwenye mali mwenyewe, kwa hiyo jamii ina haki kuzuia, na inapunguza uhuru wa mbadhirifu katika matumizi ya mali yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyajaalia yawe ni kiamu yenu} [AN NISAA 5]. Licha ya hayo, ingawa kutoa sadaka ni fadhila, na wasia ambao ni zawadi lakini Kiwango chake Maalumu kinapozidi, basi Uislamu unazuia utekelezaji wa wasia huo kwani kuzidi huko kutawadhuru warithi wa mwenye kutoa sadaka hiyo au mwenye wasia huo. Na kwa hivyo basi Mtume S.A.W. alimwambia Saad Bin Abi Waqasw: "Toa sadaka theluthi ya mali yako na theluthi ni nyingi" Na Uislamu hauruhusu wasia isipokuwa kwa kutoa thuluthi ya mali ya marehemu.
20- Na katika kuihifadhi Nafsi; basi Mwenyezi Mungu Mtukufu amemtukuza Mwanadamu na akamfanya akawa Bora zaidi kuliko viumbe vyote, akampa akili na busara, na akamhakikishia Ulinzi na Usalama. Mtume S.A.W, amesema: "Kila Muislamu juu ya Muislamu ni haramu; damu yake, Hadhi na Heshima yake yake na mali yake", Haijuzu kwa mtu yeyote kuushambulia uhai na mwili wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Na humo tuliwaandikia ya kwamba roho kwa roho, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, na jino kwa jino, na kwa majeraha kisasi} [AL MAIDAH 45].
21- Hakuna utawala wowote unaoruhusiwa kumuudhi mtu yoyote, kwani Mtume S.A.W, amesema: "Maisha ya Muumini yoyote yanalindwa, isipokuwa katika dhambi au haki" . Maana yake ni kwamba hakuna ruhusa yoyote ya kumshambulia Muumini kwa kumpiga au kumchapa mijeledi isipokuwa kwa kumkosea mtu mwingine au kuingilia haki ya Mtu huyo, na kwa ajili hiyo kisasi lazima kilipizwe.
22- Na makazi yake yanalindwa na kuheshimiwa na wala hayashambuliwi. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Msiingie nyumba zisio nyumba zenu mpaka muombe ruhusa, na muwatolee salamu wenyewe. Hayo ni bora kwenu mpate kukumbuka. Na msipo mkuta mtu humo basi msiingie mpaka mruhusiwe. Na mkiambiwa: Rudini! Basi rudini. Hivi ni usafi zaidi kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnayoyatenda.} [AN NUUR 27-28]. Na kwa hivyo basi mwanadamu akipuuza Hadhi na Heshima ya Kibinadamu na akaitendea kinyume na inavyostahili au akamshambulia mtu mwingine, basi Jamii yote kwa pamoja itasimama dhidi ya uhuru wake na itamsitisha.
23- Na katika Kuihifadhi Akili; Uislamu umetoa wito wa kuitumia akili katika kufikiri, katika Elimu na katika Kuzingatia. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri?} [AL ANAAM 50] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili} [AZ ZUMZR 9]
24- Na Uislamu umemuhakikishia kila Mtu Uhuru wake wa kuwaza na umekuwa na Uhodari wa Utafiti wake, na kwa hivyo basi, Uislamu umemjaalia mtu yoyote mwenye kujitahidi katika Dini, kuwa anapata thawabu mbili pale anapofanikiwa na kupatia, na kumpa thawabu moja pale anapokosea, na huko ni kupevuka kwa akili na kuiheshimu, na kwa hivyo basi, silika inapomdanganya Mtu na kumpeleka katika shari, na ikaelekea katika mambo yanayoiharibu akili na kuizuia kufikiri, kama vile kuivuruga akili kwa kunywa mvinyo au kuwa na uraibu wa mihadarati,, Uislamu ulisimamisa silka na ukapunguza maelekeo yake ili kuilinda akili na kuzuia madhara ya nafsi yake, au kuzuia madhara kwa mwingine, na kwa hiyo ndipo Uharamu wake ulipokuja; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?} [AL MAIDAH 91]. Na Mtume S.A.W, amesma: "Kila kilevi ni haramu" . Na kwa hivyo basi, vidhibiti ambavyo Uislamu unaviweka juu ya uhuru wa Mtu katika nyanja zake zote; za kisiasa, kiuchumi na kijamii, havilengi isipokuwa kwa ajili ya kusisitizia na kutilia mkazo maslahi ya Kijamii katika Umma, na Uislamu hauhalalishi kuingika mmoja kwa nguvu ili kuelekeza nishati ya mwanadamu panapokuwapo hatari inayoitisha Jamii.
25- Na kutokana na maelezo yaliyotangulia hapo juu, Haki za Binadamu zilizotajwa katika Azimio la Umoja wa Kimataifa la Haki za Binadamu zinaweza kugawanyika kwa upande wa makusudio ya kisharia kama ifuatavyo:
A- Haki za Binadamu zinazohusiana na Kusudio la Dini; nazo ni: Haki ya Kuwa na Imani, Haki ya Kufikiri, na Haki ya Uhuru wa Kujieleza, Haki ya Kulingania na kufikisha Ujumbe wa Dini; Haki ya Kuomba Hifadhi, Haki za Watu Wachache katika Nchi, na Haki ya Kushiriki Maisha ya Umma.
B- Haki za Binadamu zinazohusiana na Kusudio la Nafsi; Haki ya Maisha, Haki ya Uhuru, Haki ya Usawa, Haki za Uadilifu, Haki ya Kulindwa na dhuluma na kuadhibu, Haki ya Mwanadamu ya Ulinzi wa anavyovimiliki yeye Mwenyewe, Haki ya Kukaa na Kuondoka popote atakapo, Haki ya mwanadamu ya kujipatia mahitaji ya kutosha katika Maisha yake na pia kuyalinda Maisha hayo.
C- Haki za Binadamu zinazohusiana na Kusudio la Akili; Haki ya Kutoa rai yake, Haki ya Malezi na Elimu.
D- Haki za Binadamu zinazohusiana na Kusudio la kuhifadhia Hadhi na heshima; haki ya kulinda Utukufu, haki ya familia.
E- Haki za Binadamu zinazohusiana na Kusudio la Mali; Haki za Kiuchumi na za wafanyakazi, Haki ya Kumiliki.

Rejea: Sehemu ya tafiti za kisharia katika Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Misri.

 

 

Share this:

Related Fatwas