Haki za Binadamu na Uelewa wa Haki ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Binadamu na Uelewa wa Haki kwa Upande wa Lugha na Sharia

Question

Ni nini uelewa wa haki katika Uislamu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1- Kwanza: Haki kwa upande wa lugha na kimsamiati: Ni kuwa haki katika lugha ya Waarabu inarejea kwenye asili inayoenesha usimamizi wa kitu, na usahihi wake haki ni kinyume na batili, na inasemwa haki ya kitu ni wajibu, na neno “Haka” maana yake ni Kiyama kwa sababu ni Siku ya Haki ya kila kitu.
2- Pili: Neno haki ni jina katika majina ya Mwenyezi Mungu, na haki ni kitu thabiti kisichokuwa na shaka katika kuthibiti kwake, na haki ni fungu la lazima kwa mtu au kundi la watu. Na haki za Mwenyezi Mungu: Ni yale mambo yaliyo lazima juu yetu kwake, na haki za nchi ni mali zake( ). Na kwa maelezo hayo tunafahamu kuwa haki kwa upande wa lugha ni neno linalomaanisha kuthitibi kwa usahihi na ukweli.
3- Tatu: haki kwa upande wa Istilahi: Ni hukumu inayoendana na uhalisia, na hutumika kwenye kauli, imani, Dini na madhehebu kwa kuzingatia kukusanya kwake maeneo hayo yote, na kinyume chake ni batili, hivyo haki ndiyo ambayo hukabiliana na batili, na vitu huenda vikawa wazi na kubainika kwa kinyume chake, kwani kila chenye kuelezewa ima kitakuwa ni batili moja kwa moja au kitakuwa ni kweli moja kwa moja, ima ni haki kwa upande mmoja na batili kwa upande mwengine, kilicho wajibu chenyewe hicho ni haki moja kwa moja na kisicho wajibu chenyewe, basi hicho ni batili moja kwa moja, chenye kuwezekana chenyewe na kuwa wajibu kwa wengine hicho ni haki kwa upande mmoja, batili kwa upande mwengine, kwa sababu hiyo Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Kila kitu kitaangamia isipo kuwa Yeye}( ). Naye yupo hivyo tokea enzi na milele, si katika hali pasi ya hali nyengine, kwa sababu kila kitu kisichokuwa Yeye ni batili chenyewe kina haki ya Mola, kwa sababu hii Yeye amekuwa ni haki moja kwa moja.
4- Ama ukweli: Umesambaa kwenye kauli maalumu, na unakabiliana na uongo, na hutenganishwa kati yake kwa sababu kukubaliana katika haki huzingatiwa ni upande wa uhalisia, na katika ukweli kwa upande wa kanuni, hivyo maana ya ukweli wa kanuni ni kukubaliana kwake na uhalisia, na maana ya haki yake ni kufungamana na uhalisia wake( ).
5- Sifa za Haki: Kwa maelezo yaliyotangulia tunaweza kuzikusanya kama ifuatavyo:
A- Ni kuwa haki ni thabiti.
B- Yenyewe imepangiliwa.
C- Yenyewe ni lazima.
D- Yenyewe ni sahihi.
E- Yenyewe ni kweli.
F- Yenyewe ina ulazima.
G- Yenyewe inaendana na uhalisia.
6- Na kwa msingi wa sifa hizi, tunaweza kuelezea maana na ufahamu wa haki katika Uislamu, ikiwa tutaongezea ufahamu na uelewa wa mwanadamu katika Uislamu, itatuwezesha kuzungumzia haki za mwanadamu kwa misingi iliyowazi.
7- Sehemu ya Pili: Haki katika Qur`ani Tukufu: Neno haki ndani ya Qurani Tukufu limetajwa mara 227, kitu cha kwanza anachoweza kuzingatia mtu katika matumizi ya Qur`ani Tukufu ni kuwa Qur`ani Tukufu haijatumia kabisa neno haki kwa muundo wa uwingi bali siku zote umekuja kwa muundo wa umoja, katika ashirio la wazi umoja wa haki, na kuwa tokea hapo enzi na kipindi chote haki ni moja tu, hata kama kutakuwa na matukio mengi haki itabakia kuwa ni moja tu.
8- Jambo la kwanza linaloangaliwa katika matumizi ya Qur`ani Tukufu ya neno haki ni kuwa lenyewe linakuja kwa upande wa Mola, kama ni jina katika jumla ya majina yake mazuri: {Kisha watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa Haki}( ), na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hayo ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki}( ).
9- Mara nyingi – ikiwa kama si mara nyingi zaidi – matumizi ya Qur`ani Tukufu ya neno haki yanakuja kama ishara ya jumbe za mbinguni na yaliyoteremshwa kwa Mitume na Manabii, kama vile kauli ya Mola: {Hakika Sisi tumekutuma kwa Haki uwe mtoaji wa habari njema, na mwonyaji}( ).
10- Wakati ambapo matumizi ya neno haki yanakuja kwenye maeneo mengine ikiwa ni ishara ya hukumu ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake: {Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu. Yeye anasimulia yaliyo kweli, naye ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote}( ). Baadhi ya matumizi yanaonesha neno haki kwa maana ya deni lililothibiti kwenye jukumu la mdaiwa, lenye kuendana na ukweli na uhalisia, deni kwa sifa hizi linakusanya sifa za haki ambazo tumeziashiria hapo mwanzo, hivyo Qur`ani Tukufu imeita deni kwa jina la haki ikiwa ni kuzindua juu ya umuhimu wa kutekelezwa kwake: {Na mwenye deni juu yake aandikishe, naye amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala asipunguze chochote ndani yake}( ).
11- Katika mwelekeo huo wa wasifu wa vitu ambavyo vinakusanya sifa za haki katika zama za Uislamu kuwa ni haki imepokelewa kwenye matumizi ya Qur`ani katika maeneo mbalimbali: {Hakika haya ndiyo maelezo ya kweli}( ), na kauli ya Mola: {Mwenyezi Mungu Atawaongoaje watu waliokufuru baada ya kuamini kwao, na wakashuhudia ya kuwa Mtume huyu ni wa haki, na zikawafikia hoja zilizo wazi?}( ).
12- Kwa upande mwengine matumizi ya Qur`ani Tukufu ya kitenzi cha wakati uliopita katika neno haki vitenzi hivyo vyote vimekuja katika mambo ya makafiri na waliopotea pamoja na kuthibiti adhabu na upotovu wao kwa sababu ya matendo yao, kama kwamba adhabu ni haki yao pia, wameistahiki kwa ukafiri wao, wakati ambapo kimetumika kitenzi cha wakati uliopo na kuendelea cha neno haki na kulazimisha mtendewa mmoja katika maeneo yote, nalo neno la haki: {Na Mwenyezi Mungu huhakikisha Haki kwa maneno yake}( ), na neno: {Ili ahakikishe Haki}( ), na yasiyokuwa hayo, kinachoendelea kwa sifa ya kudumu – ambacho kinaonesha kwenye kitenzi cha wakati uliopita – ni adhabu kwa mwenye kustahiki adhabu hiyo, na yenyewe hata kama batili itadhihirika vipi kwani haki – kwa dalili ya kitenzi cha wakati uliopita – itajirudia tena na kutoa ushindi.
13- Sehemu ya Tatu: Haki katika Sunna ya Mtume: Imepokelewa matumizi ya neno haki katika Sunna za Mtume S.A.W. kwa mamia ya maneno - bali maelfu - ya maeneo( ), mwenye kuperuza kurasa za maeneo haya ni lazima ataona sura ya wazi ya uelewa na maana ya haki katika Uislamu kupitia maandiko ya Sunna Takatifu za Mtume S.A.W. na maelezo ya wanachuoni kuhusu maana ya neno haki kwa pande zake zote.
14- Katika utafiti huu hatuwezi kuleta Hadithi zake wala baadhi yake, bali utaonesha na kuelezea baadhi ya Hadithi zilizonukuliwa kutoka kitabu cha Sahihi Bukhari na Sahihi Muslim, ambazo zinafidisha maudhui ambayo tupo nayo. Matumizi ya kwanza ya neno haki yaliyotumika ni matumizi yake kama fumbo kuhusu Ufunuo wa Mungu, jambo linaloashiria ukubwa wa utukufu uliopata neno haki, mpaka ikafanyiwa fumbo kwenye kiwango cha juu cha utambulisho wa mwanadamu na hali ya juu ya kibinadamu, nayo ni Wahyi au Ufunuo wa Kimungu, kutoka kwa Bibi Aisha Mama wa Waumini R.A. amesema: “Jambo la kwanza lililoanza kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu katika mambo ya Ufunuo ni kuona ndoto njema usingizini, alikuwa Mtume S.A.W. haoni ndoto isipokuwa hutokea asubuhi mfano wa alichokiona ndotoni, kisha akapenda kwenda sehemu ya pekee, alikuwa akificha eneo la pango la Hiraa, akijificha humo – hali ya kuwa akifanya ibada – nyakati za mchana kabla ya kurejea nyumbani kwake, na hufanya zaidi ya alivyofanya, kisha anarejea kwa mkewe Bibi Khadija na kuongeza kufanya hivyo mpaka ukamjia ufunuo hali ya kuwa yumo ndani ya pango la Hiraa, ndipo alipomjia Malaika na kumwambia: Soma ... ” ni Hadithi inayofahamika katika masuala ya kuanza kwa kushuka kwa Ufunuo, na ikateremshwa Surat Al-Alaq( ). Na katika mapokezi mengine yanasema: “Mpaka akastukizwa na Ufunuo akiwa ndani ya pango la Hiraa akajiwa na Malaika na kumwambia: Soma”( ).
15- Na kwa maelezo haya neno haki hutumika kwa maana ya Dini sahihi. Kutoka kwa Abi Wail amesema: “Tulikuwa eneo la Saffeen, alisema Sahlu Ibn Hanif, Enyi watu mjituhumu wenyewe, kwani sisi tulikuwa pamoja na Mtume S.A.W. siku ya Hudaibiyah, lau tungeona mapigano basi tungepigana, akaja Umar Ibn Khattab akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je sisi hatukuwa kwenye Dini ya haki na wao katika dini batili? Mtume akasema: Ndiyo, akasema tena Umar: Je haikuwa kupigana kwetu kunatupeleka peponi na kupigana kwao kunawapeleka motoni? Mtume S.A.W. akasema: Ndio, akasema basi inakuwaje tunajishusha katika Dini yetu, hivi kurudi hali ya kuwa Mwenyezi Mungu hajahukumu kati yetu na wao? Akasema Mtume S.A.W.: Ewe Ibn Khattab hakika yangu mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hatonipoteza milele”( ).
16- Wakati mwingine neno haki linakuja kwa maana ya ukweli halisi uliothibiti, kutoka kwa Ibn Abbas anasema: “Mtume S.A.W. alikuwa pindi anaposimama usiku kuswali Swala za Tahajudi anasema: Ewe Mwenyezi Mungu shukrani ni zako Wewe ndiye nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo, shukrani ni zako Wewe ndio msimamizi wa mbingu na ardhi na vilivyomo, shukrani ni zako Wewe ndiyo kweli na ahadi zako ni kweli, kauli yako ni kweli, kukutana na Wewe ni kweli, Pepo ni kweli, moto ni kweli, Kiyama ni kweli, Mitume ni kweli, Muhammad ni Mtume wa kweli, Ewe Mwenyezi Mungu kwako nimejielekeza, na kwako ndiyo nimetegemea, kwako nimeamini, kwako nimetubia, kwako nimejizuia na kufanya madhambi, kwako ndiko natoa hukumu, hivyo nisamehe kwa makosa niliyo yatanguliza na nitakayo yafanya, na yale niliyoyafanya kwa siri na kwa wazi, Wewe ndio wa mwanzo na ndiyo wa mwisho, hakuna Mola wa kweli isipokuwa ni Wewe”( ). Pia kuna Hadithi nyingine inayotokana na Qatadah R.A. amesema, amesema Mtume S.A.W.: “Mwenye kuniona mimi basi atakuwa ameona ukweli”( ).
17- Kwa vile haki na sifa zake kama tulivyoelezea hapo nyuma haipaswi kutekwa nyara, ni Hadithi inayotokana na Abdillah Ibn Masuud kutoka kwa Mtume S.A.W. amesema: “Hataingia Peponi mtu ambaye ndani ya moyo wake kuna chembe ndogo ya kiburi. Mtu mmoja akasema: Hakika mtu anapenda nguo zake kuwa nzuri na viatu vyake kuwa vizuri. Akasema Mtume S.A.W.: Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri na anapenda uzuri, kwani kiburi ni utekaji wa haki, na kuwadharau watu”( ). Hivyo haki haipaswi kupingwa wala kutekwa, na mwenye kufanya hivyo basi huyo atakuwa ni mwenye kiburi, na watu wenye viburi watakutana na adhabu.
18- Na kwa maelezo haya haki ni yenye kupiganiwa, haipaswi kwa Umma kuiachia, na nilazima kusimama kuitetea haki, kutoka kwa Jaabir Ibn Abdillah anasema nimemsikia Mtume S.A.W. anasema: “Hawataacha kundi la watu katika Umma wangu kuipigania haki, wakidhihirisha hilo mpaka Siku ya Kiyama”( ).
19- Na anapitisha Mtume S.A.W. kwa mtu mwenye haki yoyote ile, hapaswi kuzuiliwa pindi anapohitaji haki yake, na anatubainishia kuwa ana nguvu na nafasi ya juu kwa kuwa na hiyo haki, kutoka kwa Abi Hurairah R.A. amesema: “Kuna mtu mmoja alikuja kwa Mtume S.A.W. akitaka kulipwa haki yake hali amechukia, Masahaba wakataka kumlipizia hali hiyo. Mtume S.A.W. akawaambia mwacheni, kwani mwenye haki ana haki ya kutaka haki yake, kisha akasema: Mpeni sawa na haki yake, wakasema Masahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hatuna isipokuwa ni zaidi ya haki yake. Akasema Mtume S.A.W. mpeni kwani mbora wenu ni yule mwenye kulipa vizuri”( ). Mtume S.A.W. amechukua maamuzi kuwa mwenye haki ni ana haki ya kutaka haki yake, hata kama ikibidi kutumia nguvu kidogo, na hilo ni kutokana na kuwa na haki, ikiwa Hadithi imekuja katika uhalisia wa deni “Mkopo” lakini mazingatio hapa ni maana jumla ya tamko na wala sio umaalumu wa sababu, na hasa Mtume S.A.W. hakusema kuwa mtu mwenye deni, bali amesema: Mtu mwenye haki, ni sawa sawa haki hiyo ikiwa ni deni au sio deni, hii ina maana kuwa kila mwenye haki – haki yoyote ile itakayo kuwa – ni mwenye mamlaka na nguvu katika kuitaka haki yake.
20- Kwa maelezo hayo tunaweza kufikia maamuzi kuwa haki za binadamu katika Uislamu sio zawadi anayotoa hakimu kiongozi au mamlaka au shirika, bali ni haki iliyopitishwa na Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu, na mwanadamu anapaswa kupambana na kuitaka kwa mwenye kuipunguza amfikishie ikiwa kamili.
21- Haki huenda ikatumika kwa maana ya wajibu wa kiraia kwa watu kuelekea kwenye jamii na serikali, kutoka kwa Ibn Masuud toka kwa Mtume S.A.W. amesema: “Hakika baada yangu kutakuwa na hali ya kujipendelea katika mali na kukiuka yaliyoharamishwa, wakauliza Masahaba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu unatuamrisha nini kwa wale watakao kutana na wakati huo? Akasema: Ni kuitekeleza haki ambayo ipo juu yenu, na kumuomba Mwenyezi Mungu kwa yale yaliyo yenu”( ).
22- Huenda ikatumika haki kwa yale yanayopaswa kwenye matumizi ya mali: Kutoka kwa Abdillah Ibn Masuud amesema Mtume S.A.W.: “Hakuna uhasidi isipokuwa kwa watu wawili, mtu ambaye Mwenyezi Mungu amempa mali na kuitumia mali yake kwenye njia za haki, na mtu ambaye Mwenyezi Mungu amempa busara na hekima, naye akawa ana hukumu kwa hekima hiyo na kuifundisha”( ).
23- Na asili ya haki katika Uislamu ni yenye kutafutwa katika kuitaka, kutoka kwa Abi Said Al-Khudry amesema: “Watu katika zama za Mtume S.A.W. waliwahi kuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je tutamuona Mola wetu Siku ya Kiyama? Mtume S.A.W. akawajibu: Ndiyo. Akawauliza: Je mnadhurika katika kuliangalia jua wakati wa mchana wa adhuhuri likiwa wazi kabisa bila ya kufunikwa na mawingu? Na je mnadhurika kuuangalia mwezi ukiwa wazi kabisa ndani ya usiku wa mwezi mkali ukiwa haujafunikwa na mawingu? Wakasema: Hapana Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume akasema: basi mtakachokiona katika kumuangalia Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama ni kama vile mnachoona katika kuangalia moja ya sayari hizi mbili, siku ya Kiyama ataita mwenye kuita ili kila Umma kufuata kile walichokuwa wakiabudu…. Kwa urefu wa Hadithi hii mwisho ikasema: Mpaka watakapo maliza kutolewa Waumini motoni, hivyo ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake hakuna yeyote miongoni mwenu atakuwa na maneno makali ya kufanya maombi kwa Mwenyezi Mungu katika kutafuta haki kuliko Waumini wa Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama kwa ndugu zao ambao wamo motoni, watasema: Ewe Mola wetu hao walikuwa wanafunga na sisi, wakiswali na sisi, wakihiji na sisi. Wataambiwa: Watoeni wale mnao wafahamu, sura zao zitaharamishwa na moto na watawatoa viumbe wengi….”( ). Hadithi hii pamoja na kuzungumzia mambo ya uombezi isipokuwa kauli yake Mtume S.A.W. pale aliposema: “Kutafuta haki” inaonesha kuwa swala la haki ni lakutafutwa kwa maana ya kutafutwa katika kupatikana kwake kikamilifu pasi na upungufu, na hii ikiwa itakuwa katika hali miongoni mwa hali za Siku ya Kiyama, basi ni bora zaidi kutafutwa huku kwa haki kuwe duniani.
24- Kwa maelezo haya anasema Mtume S.A.W. – katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abu Hurairah R.A. – amesema: “Mtarejesha haki kwa wenyewe Siku ya Kiyama, mpaka mbuzi asiye na pembe atalipiza kisasi kwa mbuzi mwenye pembe”( ). Haikuwa haki iliyopotea duniani ni yenye kupotea pia Siku ya Mwisho na kwa hili hakuna usafi katika haki isipokuwa ni kuitekeleza kwa ukamilifu wake duniani, kabla ya mja kuadhibiwa Siku ya Kiyama kisha kukawa hakuna kimbilio la kutoitekeleza.
25- Huo ndio mtawanyiko wa Sunna Takataifu za Mtume zinazotubainishia kuwa katika haki kuna heshima kubwa, na ni yenye ulazima na wajibu wa kutekelezwa, na kwa mwenye kulazimikiwa haki basi anapaswa kufuatilia na ana jukumu la kuitekeleza haki ambayo ime muwajibikia.
26- Sehemu ya Nne: Haki kwa Wanasheria( ): Wanasheria wanaielezea haki kuwa: Ni kiunganishi cha kisheria ambacho kwa hukumu yake kinamuwezesha mtu binafsi kuwa na mamlaka juu ya kitu, au kutakiwa kutekeleza kitu maalumu kwa mtu mwingine( ). Kama vile wanagawa haki sehemu mbili: Kuna Haki za Kisiasa na Haki za Kiraia. Haki za Kiraia. Ima: A- Haki za Wote: Nazo ni haki za lazima kwa mtu kama vile kulinda haiba yake kulinda uhuru wake. B- Haki Maalumu: Nazo ni haki za familia na haki za mali.
27- Haki za wote ni maudhui ya sheria ya kikatiba, mfano wake ni kama vile uhuru, uhuru wa kutoka sehemu moja kwenda nyengine, uhuru wa kukutana, uhuru wa kutoa mawazo, uhuru wa Imani na uhuru wa makazi. Hizo ni haki za pamoja kati ya watu, haiwezekani mtu kuitumia peke yake, na kwa hali hiyo haikubaliani na maana ya kimsamiati ya kina ya haki isipokuwa wakati huo huo humpa mtu mamlaka maalumu inayotengenezwa na sheria kumlinda na uadui wowote unaomtokea. Hivyo imeitwa na wanachuoni wengi wa sheria kwa jina la haki.
28- Kama vile uhuru wakati mwingine huzaa haki miongoni mwa haki, kwa maana ya kina ya kimsamiati ni kuwa, pindi unapofanyika uadui wakati huo huzaliwa kiungo cha kisheria kinampa mtu aliyefanyiwa uadui huo mamlaka au hukumu, kwa mfano uhuru wa wote ni ruhusa au ni halali, nao ni mashine zinazofahamika na sheria kwa watu wote pasi ya kuwa sehemu ya kuhusishwa na umaalumu, isipokuwa huzaa haki kisheria pindi panapofanyika uadui( ). Tukitoa mfano wa kumiliki kitu hivyo uhuru wa kumiliki ni ruhusa, ama umiliki wenyewe ni haki( ). Hivyo uhuru ni mashine ya kupata haki kwa maana ya kimsamiati.
29- Baadhi ya Wanachuoni( ) wanasema kuwa haki kwa aina yoyote itakayokuwa hukutana na wajibu. Mwanadamu pindi anapomiliki uhuru wa kufanya kitu basi kwa watu wengine ni wana wajibu wa kutomkwamisha, huenda wajibu unaotengeneza wajibu kwa mtu mwenyewe mwenye haki na uhuru jumla – mbele ya hawa – ukatengeneza haki ya wote. Hali ya asili kwa upande wa haki ni uhalali wake na kinyume ni kuifungia hiyo haki.
30- Katika hayo mijadala kuhusu haki kwenye matumizi yake membamba na matumizi yake mapana na kuhusu haki za binadamu na uhuru na kuwa kwake ni haki kwa maana ya ndani kabisa na kuhusu kuitwa kwake haki au ruhusa au uhalali na kuhusu fikra ya mfungamano wa haki na wajibu hupelekea kupinga wanachuoni wa sheria kuongeza jina la haki kwenye uhuru, haki za wote, na haki za binadamu, kunapelekea kuchanganyika kati yake na haki za kisheria ambazo zinasimama kwenye vigezo vinavyotenganisha makundi mengine ya haki zinazosimama juu ya sheria za kimaadili au sheria asilia, na tamko la haki katika matumizi yake mapana hukubaliwa na pande zote mbili za haki.
31- Pindi tunapoangalia katika Fiqhi ya Kiislamu tunakuta neno haki hutumika kwa ajili ya kuashiria maana nyingi, lenyewe hutumika ili kuelezea kitu kwa mtu – au yanayopaswa kuwa kwake – miongoni mwa wajibu kwa mwingine kama vile haki ya mlelewa kwa mlezi, haki ya mlezi kwa mlelewa, nayo ni katika haki za wote. Kama vile huitwa haki kwenye haki za watu katika mahusiano ya kifamilia kama vile haki ya mume kwa mkewe na haki ya mke kwa mumewe. Ni haki zinafungamana ndani yake na fikra ya haki na wajibu.
32- Wakati mwingine hutumika neno haki kwa maana ya jambo lililothibiti kutokea kwake kama vile kauli yake Mola: {Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini}( ). Kama vile huitwa haki kwenye haki za mali katika kauli yake Mola: {Na ambao katika mali zao kuna haki maalumu * Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba}( ). Na kauli yake Mola: {Na mpe aliye jamaa yako haki yake, masikini, na msafiri, wala usitumie ovyo kwa fujo}( ). Na kauli yake Mtume S.A.W.: “Hupewa kila mwenye haki haki yake wala hakuna usia kwa mrithi”( ).
33- Wakati mwingine haki huwa ni haki ya kimaadili na kibinadamu, kama ilivyoelezwa kwenye kauli ya Mtume S.A.W.: “Mambo matano ni lazima kwa Muislamu kumfanyia ndugu yake”( ). Miongoni mwa hayo ni pamoja na aliyoyataja Imamu Al-Ghazali( ) katika kitabu chake cha Ihyaai, kuhusu haki za Muslamu kwa Muislamu na haki za jirani pamoja na haki za urafiki na haki za undugu. Na inaweza kuwa haki na maana ya kijamii, kutokana na hilo ni pamoja na yaliyokuja katika Hadithi Takatifu ambayo imepokelewa na Abu Mussa Al-Ash’ari: “Muumini kwa Muumini ni kama jengo lenye kushikana lenyewe kwa lenyewe”( ) akashikanisha vidole vyake. Anasema Al-Qastalany katika sherehe ya Hadithi: Muumini anaposhikamana na Muumini anakuwa amemtetea na ndani yake kuna utukuzo wa haki za Waislamu wao kwa wao.
34- Kama ilivyopokelewa haki katika amri na makatazo, maelekezo ya Uislamu katika mahusiano kati ya kiongozi na anayeongozwa yanabainisha haki ya watu katika uadilifu, na kukataza kuingia nyumba za watu wengine mpaka muingiaji aombe ruhusu kwa mwenye nyumba na kusalimia wenyeji wake ndani yake kuna ubainifu wa utukufu wa makazi ya watu.
35- Kuamrisha uadilifu katika hukumu hata kama kwa ndugu wa karibu inathibitisha ukweli wa usawa, mara nyingi hutumika neno haki kwa maana ya wajibu kama kauli yake Mtume S.A.W.: “Ipeni njia haki yake”. Katika hilo kuna wajibu uliowekwa kwa watu wakati wakukaa kwao barabarani. Katika Hadithi zenye maana jumla ya maana ya haki ni kauli ya Mtume S.A.W.: “Hakika Mola wako kwako ana haki, nafsi yako kwako ina haki, na kwa watu wako kwako wana haki”( ).
36- Pindi tunapozisoma kurasa za kanuni za Sharia ya Kiislamu katika kutambua kwake haki na amri tunakuta kuwa, yenyewe inakusudia kufikiwa kwa masilahi ya watu, na maslahi haya yanaweza kuwa ni maslahi ya jamii nzima, au maslahi maalum kwa watu, na huenda yakawa ni maslahi ya pamoja kati ya pande hizo mbili( ).
Chanzo: Kitengo cha Utafiti wa Sharia ya Kiislamu Ofisi ya Mufti wa Misri.


 

Share this:

Related Fatwas