Jamii Bora – Nani Anayeweka Mising...

Egypt's Dar Al-Ifta

Jamii Bora – Nani Anayeweka Misingi ya Jamii Bora Katika Uislamu

Question

 Je! Kuna Jamii tunayoweza kuiita Jamii bora? Na ipi misingi ya Jamii hiyo katika Uislamu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Zaidi ya karne ishirini na tano zilizopita hali ya kifalsafa imetulia ambayo inawakilisha Upeo wa mawazo ya kifalsafa na kilele cha Ustawi wake, na hutoa muhtasari kamili wa wazo la mwanafalsafa husika, na hili ni suala ni: jamii bora kama inavyofikiriwa na wanafalsafa, ambao walijaribu kuwasilisha mifumo ya Utopia (Nchi iliyokamilika kwa Ustawi) na mifano kwa jamii zenye busara.
Jamii bora katika fikra za wanadamu inamaanisha mifumo mingi, na madhehebu tofauti katika siasa, sosholojia na uchumi, ilimradi kwamba katika uchunguzi wa Kiislamu wa Falsafa ya jumla, na madhehebu ya kijamii haswa, kile wanachopewa vijana wanaofadhaika katika Ulimwengu wa leo ni kama taa za mwongozo na za imani.
Hii ni kwa sababu Ulimwengu wote unamgeukia Mwenyezi Mungu kwa utii mtiifu na Uchamungu, ulimwengu uwe wote au sehemu yake au la. Mwenyezi Mungu anasema: {Na viliomo mbinguni na katika ardhi vinamsujudia Mwenyezi Mungu tu vikitaka visitake. Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni} [AR-RAAD: 15]
Na maisha kwa matumizi yake iko chini ya uwezo wa kimungu, na mwanadamu katikati ya ulimwengu huu anaweza peke yake kubeba amana ya kuongoza maisha kulingana na njia ya Mwenyezi Mungu, na kutoka hapa siasa na sosholojia zilikuwa sura moja ya za njia hiyo ya kimungu, na utafiti uliunganishwa na sababu na imani na itikadi.
Inayoonekana baada ya uchunguzi ambao ni muhimu wa jamii inayofaa katika fikra za kifalsafa katika nyakati tofauti za falsafa, kuanzia na Plato katika jamhuri yake, ambaye aliwasilisha uchambuzi wa kina wa urithi wa majimbo, na kujaribu kukuza nadharia iliyojumuishwa ya jamii bora kulingana na falsafa, na kupita kwa Al-Farabiy katika utopia, ambao msingi wake ni nguzo mbili: itikadi, rais, na hakujaribu kuwasilisha njia ya maisha, na hakuna katiba ya utawala, labda kutegmea Sheria ya Kiisilamu iliyowasilishwa kwa watu. Wanafalsafa wa enzi ya mwamko ambao ulidhihirisha ndani yao athari ya ustaarabu wa Kiislamu ambao walijua kupitia Andalusia na vinara vingine vya sayansi ya Kiislamu, haswa Jean-Jacques Rousseau, mwandishi wa nadharia ya mkataba wa kijamii, aliyefanya baadhi ya mikinzano na makosa, haswa kwa maoni yake juu ya dini ya asili na wito wake wa umoja wa dini na msimamo wake juu ya manabii na wajumbe, na juu ya msimamo wake juu ya wanawake, na pia kupitia Marx na falsafa yake ya nyenzo ambayo inasimama dhidi ya dini , na mwisho wa itikadi yake na katiba yake juu ya maisha ya kijamii ambayo inapingana na sheria ya maisha, hata kama falsafa yake inatumika yeye mwenyewe angekuwa mwathiriwa wake wa kwanza.
Jamii bora maana yake ni: jamii iliyo na lengo linalokusudiwa kutimizwa ili kurekebisha njia yake ya kijamii, kisiasa na kiuchumi… Kinachomaanishwa na neno “ubora” ni kile kinachopaswa kuwa, na kulingana na uhalisia, ambao ni uwakilishi wa kile kilichopo.
Ambayo inaonekana baada ya kusoma haya yote:
1) Kwamba Uislamu ndio dini pekee iliyoamsha ubinadamu na sifa zake kwa mwanadamu, ikampandisha hadi kwenye viumbe wakuu watukufu, ikamfanya kuwa kituo cha Ulimwengu, bwana ndani yake, na mrithi wa Mwenyezi Mungu katika ardhi yake.
2) Kwamba kiini cha ustaarabu kimejikita katika maadili ya ukweli, kheri na uzuri ambao Uislamu unaamini kwa nuru ya itikadi yake, upana wa sheria yake, na utimilifu wake wa mahitaji ya kiwango cha juu cha mwanadamu.
3) Pilato alitaka kila mtu awekwe katika nafasi ya kisayansi au ya vitendo ambamo anatofautishwa na wengine, na kwa njia ambayo kipaji na nguvu zake zinamstahiki. Na haya ndiyo maoni ya Kiisilamu yanayokubaliana nayo, na hakuna chochote ambacho kinapingana na kanuni zake, lakini jambo baya zaidi ambalo katika maoni ya Pilato ni maoni yake juu ya Ukomunisti ambapo alitoa wito wa kuwepo ukomunisti wa wanawake, watoto, na mali, ambapo alikosea katika njia hiyo, aliwasilisha uwongo ambao haukuwezekani kutekelezeka, na akawatazama wanawake kwa mtazamo usio na urafiki, wakati ambapo katika Uislamu mwanamke ni dada wa mwanamume, naye ametukuzwa kama mwanmume. {Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba} [AL-ISRAA: 70], na wanadamu ni pamoja na wanaume na wanawake, na kutukuza ni kwao wote. Ama kuhusu ukomunisti wa watoto na mali, Uislamu unalinda uhifadhi kamili zaidi ya familia na inaheshimu mali ya kibinafsi, na inaandaa haya yote kwa mifumo sahihi, ya haki na yenye usawa ambayo inahakikisha furaha ya ubinadamu. Katika mada tofauti, tutawasilisha muhtasari wa jumla wa nadharia ya Uislamu ya wanawake na familia.
4) Kwa tathmini yetu ya uchambuzi wa kina uliowasilishwa na Plato kuhusu urithi wa majimbo na sababu za kuzorota, ambayo ilisababishwa na sababu mbili: ubaguzi wa rangi na mapigano ya kitabaka, ambayo yote yanatokana na maoni yake juu ya ufisadi wa mtaala wa elimu. Hakika Uislamu una nafasi yake tukufu kuhusu ufisadi wa mataifa, ambayo tutaiwasilisha katika mada tofauti.
5) Mawazo ya Kiislamu yanaamini kuwa jamii inahitaji wakulima na wenye viwanda, kama mahitaji yake kwa wanajeshi na watawala, na wote ni sawa katika utu wa kibinadamu, na wote wamehakikishiwa haki zao hata kama wako katika ngazi ya chini kabisa ya ngazi ya kijamii. Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu ulioje kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu.} [AL-HUJURAAT: 11]. Na Mtume S.A.W. amemwita mtumishi ni ndugu kwa bwana wake, na akampa haki zake kamili: "Watumishi wenu ni ndugu zenu walio wekwa na Mwenyezi Mungu chini yenu. Hivyo, ataye kuwa na mtumishi chini ya ulinzi wake, amlishe anacho kula yeye na amvishe anacho vaa yeye, na kamwe msiwakalifishe kufanya wasiyo weza kuyafanya, na ikibidi basi wasaidieni kuyafanya." Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhariy (J.30) na Muslim (J. 1661) kutoka kwa Abu Dhar R.A.
6) Uislamu katika Utukufu wake na hadhi yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, unatangaza kwamba ubinadamu una asili moja {Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni.} [AN-NISAA: 1].
7) Uislamu unazingatia tofauti za lugha na jamii kama ishara miongoni mwa ishara za Mwenyezi Mungu, na sio sababu ya kutokuelewana na kutokubaliana, bali ni kwa ajili ya kujuana na kushirikiana. Mwenyezi Mungu anasema: {Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi.} [AR-ROM: 22]. Vile vile Mwenyezi Mungu anasema: {Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.} [AL-HUJURAAT: 13]
8) Ufunuo wa kimungu katika Uislam sio tu kwa mila ya kidini tu, na huwaacha watu peke yao maishani mwao. Akili ni kwa ajili ya kuelewa sheria za maisha kwa ukamilifu wao na nyanja zake zote tu, na haiwezi kuondoa ufichaji wake na sheria zake za kimazingira au tabia zake za kijamii, kwa hivyo Qur’ani Tukufu ilikuja na sheria na mambo ya jumla. Na Sunna ilielezea mambo haya vizuri sana, na sheria ya Kiislamu imekuja kwa ajili ya masilahi ya mwanadamu, na mamabo ambayo ni halali yaliunganishwa mambo mazuri, na mambo ambayo ni haramu yalihusiana na mambo mabaya, Mwenyezi Mungu anasema {anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao.} [AL-AARAF: 157].
9) Sheria ya Kiislamu imetia misingi ya jamii yake kwa utulivu na kukataa aibu na kuongeza ugumu, Mwenyezi Mungu anasema {Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito} [AL-BAQARAH: 185], na Mwenyezi anasema {Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.}[AL-MAIDAH: 6].
10) Uislamu imetia misingi ya jamii yake kwamba hakuna ukuhani sio ukiritimba wa sheria katika jamii kwa taifa bila lengine, lakini kuna wanavyuoni katika dini na wanafiqhi Mwenyezi Mungu anasema: {Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipo kuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo.} [ATt-TAWBAH: 31].
11) Miongoni mwa misingi ya jamii bora katika Qur’ani Tukufu ni: kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu anasema: {Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.} [AN-NISSA: 59].
12) Na miongoni mwa misingi yake: kwamba jamii ya Waislamu ina ujumbe ambao unaleta matokeo ya utekelezaji wake na ufikishaji yake. Mwenyezi Mungu anasema: {Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu. } [AL-BAQARAH: 143].
13) Na miongoni mwa misingi yake: kwamba Uislamu ni kikomo, ambacho kinamalizia uwezo ya watu wa matabaka yote na vikundi vyote na nguvu zote, Mwenyezi Mungu anasema: {Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi wa watu ni wapotofu.} [AL-MAIDAH: 49].
14) Na kati ya misingi yake ni: kuamrisha mema na kukataza maovu Mwenyezi Mungu anasema: {Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.} [AALI IMRAAN: 110]
15) Na kati ya misingi yake ni: kwamba mambo ya jamii kwa ujumla yanatokana na mashauriano, uaminifu, haki na usawa kati ya kila mmoja, na katika viwango vyote. Mwenyezi Mungu anasema: {Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona.} [AN-NISAA: 58], na Mwenyezi anasema vile vile: {Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda} [AL-MAIDAHA: 8].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Rejeo: Profesa Muhammad Sayed Ahmed Al-Musair, Al-Mujtamaa Al-Mithali Fii Al-Fikr Al-Falsafi, wa Mawqif Al-Islam Minhu, Cairo: Dar Al-Maarif, Toleo la 2, 1989 BK, (uk. 9-22, 86 95, 112-119 ).

Share this:

Related Fatwas