Kupewa Zawadi kwa Kuzirejesha Nyaraka za Umiliki
Question
Mwanamke mmoja alifariki dunia na akaacha kipande cha ardhi na ana watoto wa kike watatu nje ya nchi hawakuwa wanajua urithi wao kwa mama yao, baadhi ya watu wakaichukua ardhi hiyo na wakagushi nyaraka za umiliki wake kwa masilahi yao na mimi nikagundua hivyo na nikafanikiwa kuzipata nyaraka zinazoonesha umiliki wa ardhi kwa wamiliki wake Halisi. Wanyakuzi wa ardhi walipotambua hivyo, wakapendekeza kunipa kipande cha ardhi kwa lengo la kuninyamazisha ili niwape nyaraka nilizonazo na ambazo zinawatia hatiani, na mimi nikakataa, kisha nikawafikia warithi halali baada ya juhudi pevu na nikawajulisha haki zao na kwamba mimi nina nyaraka zinazothibitisha haki hizo. Je, mimi nina haki ya kisheria ya kupata malipo ya kazi niliyoifanya kutoka kwa warithi? Na ni kiasi gani kama kuna haki hiyo? Na je, kinachosemwa kwamba mtu atakayeokota kitu ana haki ya sehemu ya kumi ya thamani ya kitu hicho ni sahihi? Na je, hilo linawezekana katika hali hii?
Jibu:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Unyang’anyi ni kuitwaa mali ya mtu mwingine kwa dhuluma nao ni katika Madhambi Makubwa yenye onyo kali. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma,isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe. Walamsijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni}. [AN NISAA 29]
Na Ahmad alipokea katika Musanad yake kutoka kwa Abi Harra Ar Rafashiy kutoka kwa ami yake kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Haiwi halali Mali ya Mtu isipokuwa kwa moyo wake mkunjufu".
Na katika Unyang’anyi wa ardhi hasa Al Bukhariy amepokea kutoka kwa Abdullahi Bin Omar R.A. wote wawili, kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Mtu yeyote atakayechukua kipande cha Ardhi ya Mtu Mwingine isiyo haki yake, atanyakuliwa nayo Siku ya Kiama, umbali wa Ardhi saba" [Tazama Kitabu cha Az Zawajer kwa Al Haitamiy 434 - 437/1, Ch. ya Dar Afikr]
Kama ambavyo uporaji wa ardhi ni Haramu, basi hata kusaidia uporaji wa ardhi au kumficha mporaji ni sawa na uharamu wa mtendaji: Atwabaraniy alipokea katika kitabu cha: [Al Kabiir] kutoka kwa Ibn Abbas R.A. wote wawili, kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Mtu yeyote atakayemsaidia dhalimu katika jambo ovu ili aufanye uovu wake, basi hakika hatakuwa na ulinzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na ulinzi wa Mtume S.A.W."
Al Menawiy alisema katika kitabu cha: [Faidhu Al Qadiir 72-73/6, Ch. ya Al Maktabah At Tojaria Al Kubrah] "Kwa maana ya ahadi na amana yake: kwa sababu kila mmoja ana ahadi ya kulinda na kuhifadhi, na pindi anapofanya aliyoharamishiwa, au akaenda kinyume na yale aliyoamrishwa kwayo, basi ulinzi wa Mwenyezi Mungu hautakuwa naye"
Na mtu anapochukua mali ili ainyamazie haki ya mtu na kuficha kinachoweza kuwafikisha wahusika basi hakika yeye kwa kufanya hivyo anakuwa amepokea hongo ambayo ni Haramu na ambayo imeahidiwa Laana kwa mwenye kutoa au kuichukua, nayo ni fedha inayotolewa kwa ajili ya kuibatilisha haki ya mtu au kuhalalisha kisicho cha haki. [Kitabu cha: At Ta'arifaat kwa Aj Jurajaniy, Uk. 49, Ch. Al Matwba'at Al Khairiyah]
Na pia wanavyuoni wanne wamepokea isipokuwa An Nssa'iy kutoka kwa Abdullahi bin Amru R.A. wote wawili, akasema: "Mtume S.A.W, amemlaani mla rushwa na mtoa rushwa". At Termizi amesema "Hadithi hiyo ni Hasan na sahihi", Na At Twabaraniy alipokea katika kamusi zake mbili Al-Kabiir na Al-Wasat, kwa sanadi yenye watu waaminifu, kutoka kwake pia kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Mtoa Rushwa na Mla Rushwa katika moto"
Imamu Al Ghazaliy amesema katika kitabu cha: [Al Ahyaa 917-918/2, Ch. ya Dar As Shaab]: "Mtoaji wa mali haitoi isipokuwa kwa lengo, na ikiwa ni kusaidia kwa kitendo maalumu basi hii ni zawadi yenye sharti la kupata thawabu hutambulika kwa kiambatanisho cha hali, basi naangalie katika kazi hiyo ambayo ni thawabu ikiwa ni Haramu; kama vile kuhangaikia ufanikishaji wa kuongeza Uharamu au kumdhulumu mtu au vinginevyo, basi ni haramu kuchukua. Na kama itakuwa ni wajibu; kama vile kuondosha dhuluma maalumu juu ya kila mwenye kukadiriwa au ushahidi maalumu, basi ni Haramu juu yake kile anachokichukua, nayo ni mlungula (Rushwa) usio na shaka katika uharamu wake".
Na vilevile hakika kuhangaikia masilahi ya Waislamu na kujitahidi katika kufikisha haki zilizopotea kwa wenyewe na kumzindua aliyejisahau miongoni mwao juu ya haki zake zilizoporwa ni kazi ya kushukuriwa yenye thawabu nyingi kwa muhusika. Na Muslim amepokea katika kitabu chake: [Sahihi ya Muslim] kutoka kwa Abi Hurairah R.A. kwamba Mtume S.A.W. amesema: "Na Mwenyezi Mungu Mtukufu yu katika kumsaidia Mja kwa kuwa tu mja huyo anaendelea kumsaidia nduguye".
Na ikiwa wahusika wa haki zilizopotea au haki zao walizoporwa, wataamua kutenga kiasi maalumu cha mali kwa ajili ya mtu atakayewaletea ushahidi unaothibitisha haki zao, basi inajuzu kwao kufanya hivyo, na inajuzu kwa yule anayelifanikisha lengo hilo na hakuna zingatio lolote linalohusiana na uhalisia wa kazi kabla ya kutangazwa kiwango hicho cha fedha.
Na ikiwa wahusika wa haki zilizopotea au haki zao walizoporwa, wataamua kutenga kiasi maalumu cha mali kwa ajili ya mtu atakayewaletea ushahidi unaothibitisha haki zao, basi inajuzu kwao kufanya hivyo, na inajuzu kwa yule anayelifanikisha lengo hilo na hakuna zingatio lolote linalohusiana na uhalisia wa kazi kabla ya kutangazwa kiwango hicho cha fedha, basi hiyo ni sadaka tu, na mtu yeyote atakayekuta nyaraka za kuthibiti haki basi lazima azifikie kwa wenye nyaraka bila ya sharti lolote.
Sheikh Elesh Al Maliki amesema katika kitabu cha: [Manhu Aj Jaleel 71/8, Ch. ya Dar Al Fikr]: "Hakika mambo yalivyo, inajuzu kutenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kutaka kumrejesha mtumwa aliyetoroka na hajulikani aliko, na kwa upande wa mtu atakayempata akiwa ametoroka au amepotea, au nguo basi haijuzu kwake kuchukua kiasi cha fedha kwa sababu ya kumrejesha, na wala kwa kuonesha sehemu aliko kwani kufanya hivyo ni wajibu juu yake. Na kwa upande wa yule aliyempata baada ya Bwana wake kuweka kiwango cha zawadi kwa kupatikana kwake, basi analazimika kutoa hicho kiwango cha fedha, ziwe zimeeleweka fedha zilizowekwa au hapana, ziwe vinagharimu ombi la vitu hivi au hazigharimu".
Na imetajwa katika kitabu cha: [Al Minhaaj kwa Imamu An Nawawiy na Sharhu yake katika kitabu cha: Moghniy Al Mohtaaj kwa mwanachuoni mkuu As Shirbiny katika vitabu vya Kishafi 617/618/3, Ch. Dar Al Kutub Al Elmiyah]: "Na inashurutishwa - kwa maana ya fedha inayotengwa – kupatikana kwa tamko la mtoaji linalomaanisha idhini katika kulifanyia kazi hilo takwa,; kama vile anaposema: Mrejeshe mtumwa wangu au mtumwa wa fulani na utapata kiasi kadhaa cha fedha, au kwa sharti kama vile akisema: Iwapo utamrejesha mtumwa wangu basi unafungu kadhaa kwa ajili ya umaalumu wa kazi na yaliyokusudiwa na yaliyo wajibu kulipwa...; Kwa sababu ni mbadala, na kwa hivyo yamekosa tamko linalomaanisha kinachotakiwa na kiwango kinachotolewa…, na ikiwa …atafanya kazi hiyo bila ya idhini) kama vile akifanya kabla ya kutolewa wito basi hana atakacholipwa; kwani hiyo ni kazi ya kujitolea".
Mwanachuoni Mkuu As Shamsu Ar Ramliy wa Kishafi alisema katika kitabu cha: [Nihayatu Al Muhtaaj 471/5, Ch. ya Dar Al Fikr]: "Na akisema: (atakayenijulisha ilipo mali yangu basi atapata kadhaa), na akaoneshwa na yule ambaye kitu hicho hakipo mikononi mwake basi atastahiki kupewa zawadi husika; kwani mara nyingi mambo yalivyo mtu huyo hukumbwa na mahangaiko ya kukitafuta kilichopotea, na hivyo hivyo ndivyo wasemavyo – kwa maana ya Raafiiyu na Nawawiy - . Amesema Adhraiy: Ni lazima iwe hii pindi anapokitafuta baada ya mmiliki wake kutenga fedha kama zawadi, ama kwa upande wa utafutaji wa mwanzo na kazi ngumu ya mwanzo kabla ya kutengewa fedha ya zawadi, basi vyote viwili havizingatiwi.
Na Sheikh Al Bahutiy alisema katika kitabu cha: [Sharhu Muntaha Al Iradaat kutoka vitabu vya Kihanbali 281/4, Ch. ya Mu'sasat Ar Resalah]: "(Na atakayefikiwa na zawadi) kabla ya kukamilisha jukumu lake, kwa maana ya: kazi inayotolewa zawadi atakuwa na haki nayo Kwa maana ya: kuifanyia kazi baada yake; kwa utulivu wake wa kukamilisha kazi yake; kama vile kupata faida katika uwekezaji wa mali. Na ikiwa itaharibika basi atalazimika mfano wa mfano wake na thamani nyingine, na mfanyakazi hawezi kukizuia kitu mpaka akichukue na atakayefikiwa na zawadi wakati huo huo wa kazi basi ana yeye sehemu ya zawadi hiyo, kwa maana ya kwamba: kwa kiasi cha kazi aliyoifanya baada ya kufikiwa na taarifa (kama ataikamilisha kazi hiyo kwa nia ya kupata zawadi). Kwa kuwa kazi yake kabla ya kuifikia hairuhusiwi. Na wala hastahiki malipo mbadala; kwa kutoa kwake zawadi ba atakayemfikishia habari baada yake kwa maana ya baada ya kazi yake, hatakuwa ni mwenyekustahiki kwa maana ya zawadi na hakuna chochote katika hilo; kwa namna ilivyotangulia kusemwa na imeharamika kwake kuchukua isipokuwa kama atajitolea mwenyewe kumpa hiyo zawadi baada ya kupewa habari.
Na akasema katika kitabu cha: [Kashaafu Al Qenaa' 203/4, Ch ya Dar Al Kutub Al Elmiyah]: "Na kama – kilichookotwa – kitakuwa mikononi mwa mtu na mmiliki akakiwekea zawadi ili akirejeshe basi haitakuwa halali kwake kuichukua".
Na kwa upande wa ilivyozoeleka kwa watu kwamba Mtu anapokipata kitu basi ana yeye sehemu ya kumi ya thamani ya kitu hicho, asili yake ni: kile kilichokuja katika amri ya Mahakama Kuu ya tarehe 18 Mei, mwaka wa 1898, ya kwamba Mtu yeyote atakaeokota kitu au mnyama aliyepotea, basi hakika mambo yalivyo, analazimika kufikisha taarifa katika kituo cha polisi kilicho karibu na eneo hilo ndani ya miji na mbele ya Kiongozi wa Kijiji, Na amkabidhi mmiliki wake.
Na amkabidhi mmiliki wake, Na ikiwa mmiliki wake hakukitaka kitu hicho basi kitauzwa ndani ya mwaka mmoja tangu kukikabidhi kwake, na ikiwa ni mnyama, basi atauzwa ndani ya siku kumi katika mnada wa wazi kupitia Idara husika, na inajuzu kupunguza muda unaotakiwa kwa ajili ya kuuza ikiwa kitu kilichopotea kinahofiwa kuharibika, na mwenye kukiokota anakuwa na haki ya kupewa asilimia 10 ya thamani ya kitu hicho , na uongozi utaendelea kuhifadhi mali iliyobakia, kwa ajili ya mmiliki kwa muda wa miaka mitatu. Na ikiwa mmiliki hatajitokeza ndani ya muda huu kuikabidhi basi mali iliyobakia nchi itahifadhi.
Na ikiwa atahifadhi kitu kilichopotea bila ya kutoa taarifa au bila ya kukikabidhi ndani ya Siku tatu akiwa mijini na siku nane kama atakuwa vijijini, basi hakika mambo yalivyo, wananyimwa haki ya kitu hicho ambayo ni sehemu ya kumi, na atatozwa faini. Na ikiwa atakihifadhi kwa nia ya kukimiliki basi hakika mambo yalivyo atazingatiwa kuwa mwizi – kwa Istilahi ya Kikanuni ambayo inapanua maana ya wizi kutokana na maana ya Kisheria.
Na kanuni hii, hakika mambo yalivyo ni kwa ajili ya Kiokotwa, nacho ni kitu kilichopotea ambacho mmiliki wake hakioni na hawezi kukipata, na kwa hivyo kinakutwa na mtu mwingine na kisha anakiokota. Na hakiwi isipokuwa ni katika vitu vinavyohamishika ambavyo vina Mwenyewe, na vimempotea; ni kule kukosa kuvimiliki mkononi mwake, na vikawa havipo kabisa kwenye miliki yake kikamilifu, naye akashindwa kabisa kuvihodhi, pamoja na kwamba umiliki wa vitu hivyo ni wake kisheria. [Tazama kitabu cha: Al Waswetw Fii Sharh Al Qanun Al Madaniy kwa Dkt. As Sanhuriy 35-36/9, Ch. Dar An Nashr Lil Jamaat].
Na kwa hivyo, na kwa mujibu wa Swali lililoulizwa: Hakika kitendo alichokifanya muulizaji cha kutopokea hongo, kwa lengo la kuinyamazia haki na kuuficha uovu ni kitendo cha wajibu kufanywa, na kina thawabu kubwa ndani yake mbele ya Mwenyezi Mungu ambazo hazilingani na mapambo ya Dunia.
Na kwa upande wa juhudi zake za kutaka kufikia usahihi wa kumiliki ardhi na kuhangaikia jinsi ya kuzipata nyaraka zake ambazo zinathibitisha haki ya wenye ardhi na zinawasaidia kuepusha mkono wa waporaji wa ardhi huko ni kujitolea tu, na hakuna ulazima wowote kwa wamiliki wa kweli kumpatia zawadi yoyote; kwani hakuna makubaliano yoyote baina yake na wao yaliyofikiwa juu ya malipo ya alichokifanya. Na kwa hivyo, analazimika kukabidhi nyaraka hizo kwa wenyewe ili aweze kuepukana na dhima mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wala haijuzu kwake kuzuia kuzikabidhi nyaraka hizo mpaka apewe chochote, isipokuwa kama atakuwa msaidizi wa kuendeleza dhuluma na unyang’anyi na kupoteza Haki.
Na kama atawataka wahusika ili awape nyaraka zao na wampe chochote kama sadaka bila ya yeye kuwashurutisha wafanye hivyo, basi hapana ubaya wowote kwa yeye kuchukua atakachopewa wakati huo, na pia kama wao wenyewe watajitolea kitu na kumpatia kama tuzo bila ya yeye kuomba basi inajuzu kwa njia ya kwanza, na kiwango cha zawadi katika hali mbili ni juu yao wao; kwa kuwa huko ni kujitolea na wala sio wajibu wao.
Pamoja na hayo, ikiwa Mtu atatumia kiasi cha fedha maalumu anachokijua na anahifadhi kiasi chake ili ajipatie nyaraka basi ana yeye haki ya kudai alichokitoa na kugharamika kwa ajili ya kulinda haki ya warithi waliotajwa.
Na katika sheria ya Misri ni kwamba mtu yeyote atakayeokota kitu chochote basi ana haki ya kupewa sehemu ya kumi ya hicho kitu baada ya idara kukiuza, haiendani katika uhalisia wake na muhusika wake; kwani maudhui yake sio ya kinachookotwa, na kama tungejaalia kiwe ni kitu kilichookotwa basi hakika mambo yalivyo, ni kwamba Kanuni imeweka Masharti na mafungamano ya kuchukua sehemu ya kumi ya kilichookotwa, na yote yanaenda tofauti na Swali lililoulizwa.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.
Ofisi ya Kutoa Fatwa.