Mmoja wa Warithi Kuchapisha Vitabu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mmoja wa Warithi Kuchapisha Vitabu vya Marehemu Baba Yake Bila ya Idhini ya Warithi Wengine.

Question

Je, inajuzu kwa mmoja wa warithi kuchapisha vitabu vya marehemu baba yake bila ya idhini ya warithi wengine? Na yeye anatoa hoja kuwa kwa kufanya hivyo anatafuta ridhaa za Mwenyezi Mungu Mtukufu wala hakusudii kujinufaisha kifedha, na kwamba warithi wengine hawajui manufaa ya kueneza elimu, na kwamba kutovisambaza vitabu hivyo ni sawa na kuizuia Elimu na kuificha. 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Uislamu umekuja kulinda Mali, na kulifanya jambo hili kuwa ni moja ya Malengo Makuu Kamili Matano ambayo Sheria imekuja kuyalinda, nayo ni: Kulinda Nafsi, Heshima, Akili, Mali na Dini. Na ama udhibiti wa Mali ni: chochote chenye thamani kwa watu kwa sababu ya uwezekano wa kunufaika nacho na kumwajibisha aliyekiharibu akilipe.
Na kwa kuwa Utunzi wa vitabu na Uzalishaji wa Fikra ni katika yanayotolewa maamuzi yake kutokana na manufaa yake kwa namna ambayo kunapatikana Ubobezi zuizi, na ndani yake kunafanyika unyooshaji na mzunguko kwa kujua na huchukuliwa sehemu ya kutangamana na kupeana baina ya watu, na kuthibitika ndani yake haki ya kudai kisheria kwa mtazamo wa kisheria bila ya kupinga hilo katika sharia. Hakika hili linaifanya Hukumu ya kifedha katika kumiliki kwa Mwenyewe na kubobea kwake huzuia wengine kunufaika nacho au kukirekebisha bila ya idhini yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe. Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni} [AN NISAA 29]. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Wala msiliane mali zenu kwa baat'ili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua} [AL BAQARAH 188].
Imamu Al Qurtubiy amesema katika Tafsiri yake [338/2, Ch. ya Dar Al Kutub Al Masriyah] kwenye Aya hiyo: "Matamshi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Aya hiyo inakusanya umma wa Mohamad S.A.W, yaani Waislamu wote, na Maana ni: "Msile mali zenu kinyume na haki, na yanaingia katika maana hii; Kamari, Utapeli, Unyang’anyina kuzuia haki za watu, na kila kisichompendeza mmiliki wake, au Sheria imeharamisha, na hata ikiwa kitampendezesha mmiliki wake, kama vile; mahari ya kahaba, ujira wa padri, thamani ya mvinyo, nguruwe na nyinginezo, Mazungumzo kuhusu haki za mtunzi, yameandikwa katika vitabu wakati wa kuzungumzia juu ya adabu ya waandishi, na juu ya uaminifu wa kielimu katika utendaji, na adabu za kupokea elimu, na kuharamisha uongo na uharibifu, jambo ambalo kuna uwezekano kwa maana: -kuthibiti haki ya mwandishi – maana hii hata kama hana sifa ya pekee kwa maana ya jina kama inavyojulikana hivi sasa.
Na Sheria ya Kimisri imeonesha umuhimu wa haki hiyo kuanzia toka kuweka kanuni ya kuhifadhi haki ya umiliki wa kifikra, namba ya 82 ya mwaka wa 2002, endapo kanuni mpya hiyo imetaja katika mada 143 kwa kuwa: hakika mtunzi au mwandishi ana nafasi yake na wale walio nyuma yake wana haki za utunzi wao wa kiadabu usiotetereka au usiofaa kuachiwa, na haki hizi ni nyingi kama ifuatavyo:
Ya Kwanza: Haki ya kupeleka kitabu kwa watu wote kwa mara ya kwanza.
Ya Pili: Haki ya kunasibisha kitabu kwa mtunzi wake.
Ya Tatu: Haki ya kuzuia marekebisho yoyote ya utunzi, marekebisho ambayo ni kuiharibu kazi yake au kuipotosha.
Na kuthibitika kwa haki ya kihefadhi kwa mwandishi, ni jambo lililofikiwa kimaamuzi na Baraza la Fiqhi la Kiislamu la Kimataifa ambalo ni OIC, Jumuiya ya Mataifa ya Kiislamu katika mkutano wake wa tano uliofanyika nchini Kuwait, muda kutoka 1-6 mfunguo Tano, mwaka wa 1409, unaoafikiana na muda kutoka 10-15 mwezi wa Desemba, mwaka 1988, na baada ya kuangalia tafiti zilizopatiwa wajumbe pamoja na wataalamu mbali mabali katika maudhui ya haki za kimaana na kusikiliza mazungumzo yaliyofanyika kuhusu suala hili yaliamuliwa yafuatayo:
Ya Kwanza: Jina la kibiashara na anwani ya kibiashara au alama ya kibiashara na utunzi na uvumbushi au ugunduzi vina haki maalumu kwa wahusika wake, na vyote hivyo vinatambulika katika zama hizi kuwa na thamani yake, haki hizi kifedha inayozingatiwa kutokana na watu kulipia, na zinazingatiwa kisheria na haijuzu kuzishambulia haki hizo.
Ya Pili: Inafaa kulitumia jina la kibiashara au anwani ya kibiashara au alama ya kibiashara na kuhamisha chochote katika hivyo kwa kulipia fedha kamayatajitokeza madhara yoyote au kuvuruga ukweli na kughushi, kwa kuzingatia kwamba hiyo imekuwa haki ya kifedha.
Na kwa ajili hiyo, hakika mambo yalivyo ni kwamba haijuzu kuzishambulia haki za waandishi za kifedha kwa kuuza kazi zao na kujinufaisha nazo na haki ya kifedha ni jumla ya vinavyorithiwa na inatambulika hivyo kwa sheria za Kimisri na katika kanuni ya kulinda umiliki wa fikra ulioashiriwa, wanachuoni wa Fiqhi waliamua kwamba urithi ni upande mwingine wa ushirika wa miliki.
Hiyo ni kwa kuwa wanachuoni wa fiqhi wanaugawa ushirika kwa aina mbili: Ushirika wa Kumiliki pamoja na Ushirika wa Mkataba wa pamoja, na tofauti baina ya aina mbili ni kwamba Ushirika wa Mkataba haufanyiki isipokuwa kwa hiari tofauti na ule wa Kumili ambao unaweza kuwa ni wa lazima kama inavyokuwa katika Mali inayorithiwa baina ya wanaostahiki kugawiwa mafungu yao.
Na Miongoni mwa hukumu za ushirika wa Umiliki ni kwamba kila mmoja katika washirihi ni mgeni katika fungu la mwingine na wala hazingatiwi kama mwakilishi wa mwingine. [Jarida la Mahkumu, mada 1057] Na kwa ajili hiyo, mshiriki wa miliki hana sehemu yoyote katika fungu la mwenziwe, katika matendo ya kuweka mkataba, kama vile kuuza , kukodisha, kuazima na mengineyo, isipokuwa kwa idhini ya mshiriki mwenzake.
Na kutokana na hayo; Iwapo mtu atachukua hatua katika mali ya mwenzake kwa aina yoyote katika kinachomilikiwa na mshiriki wake basi hukumu yake ni hukumu ya udadisi, naye ndiye anayechukua hatua bila ya kumiliki au kuwa na jukumu au uwakala, na hatua zake hizo ni za kiudadisi ambapo hakuna yeyote miongoni mwa wanachuoni wa Fiqhi aliyesema zitekelezwe bila ya idhini ya mmiliki au wakili wake.
Bali kauli zao zinazungukia baina ua kutosihi uchukuaji wa hatua zake zozote na kubatilika kwa hatua hizo kama ilivyo katika madhehebu ya Imam Shafi na Imam Ibn Hanbali, au kufaya ijuzu kwa kutegemea ruhusa ya mmiliki au wakili kama ilivyo katika madhehebu ya Imamu Hanafi na Imam Maliki, na ikiwa hatajuzisha na akakataa basi hatua iliyochukuliwa itakuwa haifai.
Na kutokana na hayo: hakuna yeyote katika warithi mwenye haki ya kuchukua hatua peke yake kwa kusambaza vitabu vya mzazi wao bila ya idhini ya warithi wengine waliobakia, na wala halikubaliki dai lake la kutokusudia kujinufaisha kwa hatua hiyo; kwani kujinufaisha kwa mali hiyo sio haki yake pekee hata aamue kuchukua hatua kama hii peke yake bila idhini ya wengine.
Ama kwa upande wa kauli ya kutosambaza vitabu hivyo inazingatiwa kuwa ni kwa lengo la kuzuia na kuificha Elimu, sio sahihi, na yaliyokuja katika suala la kuficha Elimu, katika yalipokelewa na Ahmad kutoka Hadithi ya Abu Huraira R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W. aliyesema; "Mtu yeyote atakayeulizwa Elimu na akaificha basi atafungwa nayo mnyororo motoni siku ya Kiama" Basi Al Khatwabiy amesema katika kitabu cha: [Ma'alim As Sunan 185/4, Ch. ya Al Maktabah Al Elmiyah]:
Hii ni katika Elimu ambayo ni lazima ifundishwe na yeye kwa watu wengine, na inakuwa ni lazima kwake kuifundisha, kama vilie aliyemwona kafiri anataka kusilimu anasema: Nifundisheni Uislamu ni nini na dini ni kitu gani, na anayeona mtu aliyeingia katika Uiislamu hawezi kuswali vizuri, na wakati wa Swala umefika anasema: Nifundisheni jinsi ya kuswali, na kama kuhusu vile mfano wa mtu aliyekuja kuomba Fatwa ya jambo uhalali na uharamu wake.
Anasema: Ninakuombeni mnitolee Fatwa na mniongoze, basi hakika mambo yaliyo, ni lazima katika mambo kama hayo, kutozuia majibu kwa anayeulizia katika Elimu, na yeyote atakayefanya hivyo atakuwa amepata madhambi, msahihishaji wake amesema: Havyo ndivyo ilivyo, na inadhihiri kwamba kuna neno kabla yake lilidondoka; nalo ni: Atakuwa anastahiki adhabu kali na onyo, na haiwi hivyo katika mambo ya Sunna ambayo sio ya dharura kwa watu kuyajua.
Ama kuhusu mambo yanyaofungamana na faradhi za kutoshelezana na mfano wake, sio Haramu, na wanachuoni wametaja hali ambazo ndani yake kuficha elemu si haramu, bali lazima kwa mtu kuficha baadhi ya mambo hayo.
Na Mwanachuoni Mkuu As Shatwbiy ameifupisha hiyo katika kitabu chake cha: [Al Mwafiqaat 167/5, Ch. ya Dar Ibn Affaan] basi akasema: "Yanatakiwa sio kila yanayojulikana kuwa ni haki kusambazwa, hata kama yatakuwa ni katika Elimu ya Sheria na ni katika mambo yanayonufaisha kwa hukumu zake, bali hilo linagawanyika: Yamo ndani yake ambayo yanatakiwa Kusambazwa -nayo mara nyingi ni Elimu ya Sheria- Na miongoni mwake kuna yale yasiyotakiwa kusambazwa kwa hali yoyote iwayo, na miongoni mwake yaliyotakiwa kusambazwa katika hali fulani au wakati fulani au mtu fulani, na katika hilo kuna kuainisha tofauti hizi, na hata kama itakuwa ni haki kwani kunaweza kuleta fitna, na ukawa upande huo unazuiwa kabisa, na katika hayo ni Elimu ya Mambo yanayoshabihiana na maneno yaliyomo ndani yake, kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema amekemea mtu atakayeyafuata mambo hayo.
Na yanapotajwa na kuwekwa wazi maneno yaliyomo ndani yake huenda hilo likapelekea katika yale yasiyohitajika, basi imekuja katika Hadithi kutoka kwa Ali "Zungumzeni na watu kwa yale wanayoyajua, Je mnaelewa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake wanaweza kukadhibishwa? Na katika kitabu Sahihi kutoka kwa Muadhi kwamba Mtume S.A.W. akasema: "Ewe Muadhi, Je unaijua ni ipi haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake? Na ni ipi haki ya waja kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu? … Hadithi, mpaka aliposema: nilisema Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Niwabashirie watu? Akasema: Usiwabashirie watu basi wategemee"
Na miongoni mwa kuificha Elimu ni asimwambie yule anayeanza katika yale yanayomfaa anayemaliza, bali awalee masuala ya Elimu wenye ujuzi mdogo wa Elimu kabla ya wakubwa wao, na wanachuoni wamefaradhisha masuala ambayo haijuzu kuyatolea fatwa hata kama itakuwa sahihi kwa mtazamo wa Fiqhi. Na miongoni mwa hayo: Swali la wengi kuhusu sababu za masuala ya Fiqhi na hukumu za kuweka sheria, hata kama yatakuwa na sababu sahihi na hukumu zilizonyooka, kwa ajili hiyo Bi Aisha alikana kwa yule mwanamke aliyeuliza: Kwanini mwanamke mwenye hedhi hulipa Saumu yake wala halipi Swala zake? Basi Bi Aisha akasema kwa mwanamke huyo: Je wawa ni Mhurairiya?
Na Omar Bin Al Khatwab R.A. alimpiga mwenye kupaka rangi nguo, na kumtoa pale, alipokuwa ana maswali mengi yanayohusu mambo ya Elimu ya Qur'ani na hayafungamani na kazi, na huwenda yangezua mambo ya shaka na fitna hata kama yalikuwa ni sahihi. Na akasoma kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na Matunda na Malisho ya wanyama", basi akasema haya ni matunda, basi malisho ya wanyama yako wapi? Kisha akasema:
Hatukuamrishwa kuafanya hivi, na mengine mengi yanayoonesha kwamba sio kila Elimu husambazwa na kuenezwa hata kama ni ya kweli. Na Imamu Malik amejieleza kuhusu ambapo yeye mwenyewe kwamba ana Hadithi na Elimu hakuihadithia au hajawahi kuisema, na alikuwa anachukizwa sana kuyasema maneno mengi yasiyo na utendaji ndani yake. Na akaelezea juu ya wanachuoni waliomtangulia, kwamba wao walikuwa wanachukia jambo hilo, basi akatanabahika kwa maana hii, na udhibiti wake ni: kwamba wewe unayaleta masuala yako kwa kipimo cha sheria, na ikiwa yatasihi katika kipimo chake, basi yaangalie malengo yake kwa kiasi cha hali ya zama na watu wake, kama kuyataja kwake hakuleti uharibifu, basi yaweke wazi kwa wengine na ikiwa yatakubalika basi unaweza kuyazungumza. Yanaweza yakakawa ni kwa watu wa kawaida, yakiwa ni yanayaokubaliwa na akili za watu wa kawaida, au yatakuwa ni kwa watu maalumu basi hayafai kwa watu wote, na hata kama hayakuwa ni katika masuala yaliyorahisishwa basi ni bora zaidi kuyanyamazia, na hivyo ndivyo inavyofanyika kwa ajili ya maslahi ya kisheria na ya kiakili.
Na kwa kuyawekea misingi yale yaliyotangulia: Hakuna haki yoyote kwa mmoja miongoni mwa warithi ya kujichukulia hatua peke yake ya kusambaza vitabu vya baba yake bila ya warithi wengine waliobakia kujua, na kutojua kwa baadhi ya warithi fadhila za kuisambaza Elimu na thawabu ya kufanya hivyo hakuzingatiwi kuwa ni udhuru wa mtu kujichukulia hatua peke yake, hata kama mrithi huyo mmoja atakuwa anajua fadhila hii na thawabu hizi basi ana haki ya kuzuia usambazaji wa vitabu hivyo ikiwa ni bure bila malipo au kwa sababu yoyote anayoiona yeye, na huko hakuzingatiwi kama ni kuificha Elimu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Ofisi ya Kutoa Fatwa ya Kimisri

 

Share this:

Related Fatwas