Msemo wa: "Ardhi ya Misri ni Ardhi yenye baraka na ndio mama wa nchi zote"
Question
Ni upi ukweli wa kauli msemo wa: "Ardhi ya Misri ni Ardhi yenye baraka na ndio mama wa nchi zote"
Answer
Misri imeitwa mama wa Dunia au mama wa nchi, kimbilio la watu" majina haya ameyaita nabii Nouh amani ya Mola imshukie; ameeleza Ibnu Abdulhakam katika "Futuh Misri wal Maghrib" uk. 27 kutoka kwa Ibnu Abbas R.A. yeye na na baba yake, kwamba Nouh amani ya Mola iwe juu yake alimwambia Mtoto wake alipoitikia wito wake: (Ewe Mola wangu hakika yeye ameitikia wito wangu; basi mbariki yeye na kizazi chake na mpe makazi katika Ardhi yenye baraka, ambavyo ndio mama wa Dunia, na kimbilio la waja, na ambayo mto wake ni mto Bora zaidi duniani, na jaalia humo bara tele, na mdhalilishie yeye na kizazi chake Ardhi hiyo na uwape nguvu) na hili limetajwa na wanazuoni wengine katika vitabu vyao akiwemo Al-Hafidh Al-Kandy katika " Fadhaail Misri Mahrous na mwana historia Al-Bakry katika "Masalik wal-mamaalik" na mwana historia Taghry Al- Burdy katika "Al-Noujoum Al-Zahira" na Al-Hafidh Alsouyouty katika "Husinil Muhadhara" na mwana chuoni Miqrizy katika "Al-mawaaidh wal-iitibaar" na wengineo.