Urithi wa Kiislamu – Kupitia Vyombo...

Egypt's Dar Al-Ifta

Urithi wa Kiislamu – Kupitia Vyombo Vilivyoelezea – Falsafa ya Kilugha

Question

Ni ipi Falsafa ya Lugha na nafasi yake katika hatua ya kuufahamu Urithi wa Kiislamu? 

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Falsafa ya Lugha imekuwa na nafasi muhimu sana katika kuufahamu Urithi baada ya kufahamu taswira nzima ambayo imetawala kwenye Ufahamu na kuelewa Ulimwengu, Mwanadamu na Maisha. Lugha inarithiwa na haivumbuliwa, kwa maana mazingira ya matamshi ukiondoa maana, ni jambo analorithi mwanadamu wala halitengenezi, kwa sababu hiyo imekuwa ni lazima kufahamu hali hiyo na kufahamu miongozo ya semantiki, Waislamu wa zamani walilipa Suala hili la Somo la Semantiki umuhimu mkubwa sana.
Dalili za matamshi zinawafanya wazungumzie suala la “Mizizi ya Lugha” ambalo lipo kwenye makamusi ili kujenga mfumo wa matumizi ambayo kutokana na mizizi hii, hutengeneza kitenzi cha wakati uliopita, kitenzi cha wakati uliopo, kitenzi cha kuamrisha, jina la mtendaji, jina la mtendewa, chanzo, sifa mfanano, jina la mahali na wakati…..na mtumizi mengine ya kilugha ambayo hutumika ndani ya Mataifa mbalimbali, na hili walijifunza kwa kina sana na kufahamu kupitia masomo haya vitu vingi ambavyo tunaviita Falsafa za Lugha.
Ukweli ni kuwa somo hili la falsafa ya Lugha kwa mfano hatua hizi ambazo tutazielezea zinamfanya mwanadamu kuwa na ufahamu zaidi ni sawa sawa kwa upande wa matini za Kisharia au uandishi wa Urithi, na huenda ikawa wazi zaidi wakati wa mgongano wa matini za Kiurithi na utekelezaji wake.
Hapa tutaangalia baadhi ya chambuzi – ambazo hata kama zenyewe hazitapatikana – lakini zitachangia katika kuelezea tofauti iliyopo kati ya mtafiti wa sasa – mwanafunzi – na kati ya urithi wake, na kiwango cha umuhimu wa kuazima chombo cha kilugha kwa umuhimu mkubwa ili kufika kwenye lengo kwa ufanisi mzuri zaidi.
Tunaanza na kiunda neno cha msingi nacho ni Herufi. Na herufi zipo za aina mbili: Herufi ya kujengea neno, na Herufi ya maana ya neno.


Herufi za Kujenga:
Herufi za kujenga neno, zipo ishirini na nane katika lugha ya Kiarabu, hapo zamani zilikuwa zimetengenezwa katika sura inayoitwa “Abjad” kwa sababu zilikuwa zinaanza na neno “Abjad”, kisha zikaboreshwa baada ya hapo mpaka tukafika kwenye mfumo unaoitwa mfumo wa Alifu Bee nao ni mfumo ambao tumejifunza kupitia mfumo huu kwa miaka ya sasa, herufi hizi zinaitwa herufi za kujengea, nazo hazina maana kwa mfano herufi “Alifu” peke yake haina maana yeyote katika lugha ya Kiarabu.
Katika mnasaba huo huo, lugha za kilatini zinashiriki katika muundo huu wa herufi kwa kuwa na herufi ishirini na mbili, na kufanya lugha ya Kiarabu kuwa na tofauti na lugha za kilatini kwa herufi sita, hivyo herufi hizi sita wanaziita “Herufi za Visawe” na herufi hizi ishirini na mbili ni herufi shirikishi nazo zipo kwenye herufi za kilatini pia pamoja na kuiondoa herufi Hee na kuongeza herufi Thaa.
Herufi za kujenga ambazo zinapewa uzito mkubwa na wale wanaojifunza “Utendaji wa sauti” na wanaojifunza “Tajwiid”. Wanachuoni wa zamani wamezigawa herufi na kuzitengenezea sifa na njia za kutokea kinywani, kwa maana ya kutoa herufi kutoka kwenye niia zake maalumu za herufi hiyo: Kama vile matoleo ya kooni, katikati ya ulimi. kwenye ncha ya ulimi, kwenye mkusanyiko wa meno, kutoka kwenye midomo miwili na kutoka kwenye pua, pamoja na kuchunga sehemu ya herufi miongoni mwa herufi jirani na herufi hiyo na athari ya kutamka herufi zenyewe kwa zenyewe, na kwa hili, miongoni mwa miujiza ya Qur`ani Tukufu ni kupokelewa na kutufikia sisi kwa sauti ile ile ambayo ametuachia Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., kwa maana ya njia ya sauti maalumu ambayo inafanya kila herufi ina mazingatio yake, na kuna jedwali huwa linahifadhiwa na watu wa Tajwiid likiwa na vifanisi vya umoja na vya uwingi, kisha vinafuatanishwa na tunajifunza Elimu ya Tajwiid katika hukumu ya herufi yenye silabi ya Tanwiin na herufi ya Nuun yenye silabi ya Saknah, na hukumu ya herufi ya Miim herufi na Raa na herufi za silabi za Maddah….na zinginezo.
Hivyo herufi za kujenga – hata kama zikiwa zenyewe hazina maana – isipokuwa utendaji wa sauti sahihi ni jambo muhimu sana katika utamaduni uliozoeleka wa kuhamisha na kunukuu urithi wake kwa uwazi na kunukuliwa kwa njia hii Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Hadithi za Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., na kufungamana kwa njia hiyo na sanaa za ufasihi uzungumzaji na ubainifu katika urithi wa Kiislamu, nazo ni sanaa ambazo bado mpaka leo zina maandiko yake bali na huzingatiwa ni katika uwezo wa kijamii na kisiasa ambao hufundishwa na kuwa na maana kwenye staarabu mbalimbali.
Herufi zenye Maana:
Herufi hizi za kujenga huwa tunajengea neno, lakini hata hivyo hutofautiana na “Neno” lenyewe katika lugha ya Kiarabu ambalo tunalikuta likiwa na pande Tatu: Jina, Kitenzi na Herufi….herufi hapa sio herufi za kujengea neno bali hapa ni herufi za maana ambazo kila moja katika hizo huleta maana maalumu, nazo katika lugha ya Kiarabu kuna herufi Tisini zikiwa zimegawanyika sehemu Tano:
Miongoni mwake kuna herufi moja mfano: Herufi ya Waw, Baa, Kaaf, Alifu, Laam….na kuna zingine zina herufi mbili mfano: Min, Fiy, An, Lan, Inn…..miongoni mwake pia kuna muundo wa herufi tatu mfano: Ilaa, Alaa, Thumma, Inna….zingine zinaundika na herufi nne mfano: Laalla, Kaanna…..na zingine zinaundika na herufi tano mfano: Lakinna (Ambapo hutamkwa: Laakinna kwa Alifu ya silabai ya Maddah, huwa haiandikwi silabu hiyo na kuwekwa silabi ya kukaza kwenye herufi ya Nuun), hivyo hakuna katika herufi za maana inayoundika na zaidi ya herufi tano.
Herufi hizi Tisini, ima zina kazi za kinahau au hazina, kwa maana ima kuathirika kinahau au kutoathirika, baadhi yake huweka silabi ya Kasrah, baadhi yake huwekwa silabi ya Fat’ha, baadhi yake huwekwa silabi ya Saknah na baadhi zinakuwa hazifanyiwi kazi hizo wala kuwa na athari yeyote lakini athari ni kitu kimoja na maana ni kitu kingine, herufi hizi hutumika katika maana hamsini na sita, na maana hizi hamsini na sita miongoni mwake ni: Mwanzo, lengo, mwisho, baadhi, ongezeko, ufahamu, kuuliza, kuapa, kuhimiza, kutamani, kutegemea, kusisitiza…..n.k.
Pindi tunapochora jedwali kwa sura ya urefu na ndani yake kukiwa na herufi Tisini ikifuatiwa na kazi Hamsini na Sita kwa upana, tunakuta herufi moja huenda ikaleta maana moja au mbili au hata maana Kumi na Tano, kwa mfano: Herufi “Baa” inamaanisha vitu vingi miongoni mwavyo ni: Urafiki wa pande mbili, mvaano na sababu au jambo, mwanzo, ongezeko, sababu……katika kauli yake Mola Mtukufu {Na Mwenyezi Mungu alikwisha kunusuruni katika Badri} [AAL IMRAAN: 123]. Inaonesha kuna sehemu kwa maana “Katika Badri”. Au kauli yake Mola Mtukufu: {Basi kwa dhuluma yao Mayahudi} [AN NISAA: 160]. Hapa ina maana: “Kwa sababu ya dhulumu za Mayahudi”, tunasema: Dalili yake ipo kwenye sababu:

Min Ilaa Kam Hal Maa Baa Waw Inn Inna Au …
Sababu  

Kiunganishi   
Sharti  

Msisitizo   
Kuuliza
………….

Jedwali hili jepesi linasaidia kwa nguvu kubwa kuingia kwenye undani wa lugha, na kumfanya mwadamu kuwa na karibu zaidi ya kufahamu Kiarabu kwa undani zaidi, uelewa wa falsafa wa herufi hizi za maana ni mwanadamu kuwa kwenye kina kingine, na kuongezeka kwa kuzitumia kwake pamoja na urithi ambao umeandikwa kwa Kiarabu – na wanachuoni wa lugha wenye kufahamu falsafa zake – na kuwa kwenye anga ya juu, mpaka awe mwanadamu kana kwamba amefunguka kwenye nuru baada ya kuwa kwenye kiza…kwa sababu mvuto mkubwa wa Qur,ani – ambao unalazimisha Muumini kuwa nao – unakuja kwa kufahamu kwake mjumuiko wa kanuni muhimu, kanuni ya kwanza ni kufahamu falsafa ya lugha na falsafa za herufi. Ibn Hishaam alifahamu masuala haya, na lugha ya Kiarabu inawezekana kuwa na chanzo cha herufi za maana, kwa maana achana na hivi vitabu vya Nahau na Irabu njoo tufahamu vizuri lugha ya Kiarabu kwa njia nyingine.
Kisha kuna suala linaloleta tofauti kati ya athari na maana katika herufi:
Athari ni ile inayotokana au kutengenezwa na herufi ikiwa na kufuatiwa na hali za Irabu kama vile silabi ya “Sakna, fat’ha, kasrah…..” kuna herufi Ishirini katika jumla ya herufi Tisini hutia silabi ya Kasrah kwa jina linalokuja baada ya herufi za silabi ya Kasra na huitwa herufi za Kasra:
Kuna herufi za kasrah nazo ni: Min na ilaa - hata, khalaa, haasha, a’ada, an, alaa. Man, mundhu, rubba, laam, kaafu na waw - Al-baau, al- kaafu, la’allaa na mataa.
Pia kuna herufi zingine hutia silabi ya Fat’ha kwa jina linalokuja baada ya herufi za silabu ya Fat’ha na huitwa herufi za Fat’ha, kwa mfano herufi Ka-anna: Huweka silabi ya fat’ha kwenye jina la mwanzo na kuweka silabi ya dhamma kwenye habari ya jina hilo ambapo ni tofauti na herufi ya Kaana na ndugu zake ambao ni:
Lianna, Anna, Laita, Lakinna, La’alla – Ka-anna ni kinyume na Maa ya Kana kiutendaji.
Ama Kana na ndugu zake hufanya kazi ya kuweka silabi ya dhumma kwenye jina la mwanzo na kuweka silabi ya fat’ha kwenye habari ya jina hilo:
Herufi ya kana huweka silabi ya dhamma kwenye jina linaloanza, na habari yake huwekwa silabi ya fat’ha kama vile “Omar alikuwa bwana”.
herufi hizi pia zinagawanyika sehemu tano: Miongoni mwa sehemu hizo ni pamoja na zile zinazoingia kwenye kitenzi na miongoni mwake zinazoingia kwenye nomino au jina na miongoni mwake zinazoingia sehemu zote mbili, miongoni mwake zipo zenye athari na zingine hazina athari, zingine ni zenye maana moja na zingine ni zenye maana zaidi ya moja au kazi zaidi ya moja kwa mfano herufi “Hal”: haina athari yeyote, na maana yake au kazi yake ni kuuliza, na huingia kwenye kitenzi na hata kwenye nomino au jina, herufi “Fiy” ni miongoni mwa herufi za silabu ya Kasrah kwa kuzingatia athari yake, na ni katika herufi ya sehemu au eneo kwa kuzingatia maana, wala haingii isipokuwa kwenye jina, herufi “Lam”: Ni miongoni mwa herufi za silabi ya Saknah kwa kuzingatia athari, nayo hufanya kazi ya kukanusha kwa upande wa maana na inafanya kazi kwenye kitenzi tu.
Kila herufi ina matumizi yake yanayowezekana na wala haiwezekani kutumia sehemu nyingine, kwani haifai kuleta herufi kama vile herufi ya “Kaaf” kwenye kuuliza, kwa sababu herufi ya Kaaf haifanyi kazi ya kuuliza na wala haiwezekani kuitumia herufi ya “Fiy” katika kuonesha sababu.
Katika jedwali hili jepesi ambalo tunalifikiria tunakuta jambo jingine: Ni kuwa herufi inaweza kutumika katika maana ambapo inawezafika maana kumi na tano kama tulivyosema, ni vipi hivyo? Wamesema kuwa: Maana maalumu zingine huwa ni kwa njia halisi, na maana zingine ni kwa njia ya ufupisho, hivyo herufi hutumika katika maana maalumu kwa sura iliyoenea sana, kisha kwa sura chache huenda ikatumika katika maana nyingine, kwa mfano herufi Baa kwa asili ni herufi ya sababu, ama ibara “Kwenye Badri” kama ilivyokuja kwenye maana ya Aya kuonesha sehemu ni mara chache sana, na hiyo ni kwa sababu hakuna mfano mwingine zaidi ya huu tu.
Je inawezekana kutumia neno au herufi katika maana halisi mbili tofauti? Ndio, na hii inaitwa kwa jina la mshiriki, ambapo maana zake huwa ni maana halisi na wala hakuna maana ya ufupisho, na tutazungumzia hapo baadaye.
Kuungana:
Herufi hizi ni herufi za maana, kwa maana zenyewe zinafungamana katika kutengeneza jumla ya Kiarabu kwa kitenzi. Na hii inatupeleka kwenye kitu kingine, sisi mpaka hivi sasa tunazungumza katika umoja, kwa maana katika matamshi katika herufi zenye kujenga na zenye maana, kama vile matamshi na herufi za umoja, lakini pindi tunapo geukia kisa kingine ni lazima kusimama kwenye kisa hiko kwa lengo la kufahamu kwa kina zaidi ambapo sisi tupo kwenye mwelekeo huo, herufi hizi – katika mpangilio – ni lazima zifungamane na kitenzi au kile kinachochukuwa nafasi ya kitenzi, tutaona pia - hapo baadaye – ni kwa nini kitenzi au kinachochukuwa nafasi ya kitenzi? Na kipi kinachochukuwa nafasi ya kitenzi katika uhalisia? Ni mantiki walioleta kutokana na jaribio la nje mpaka lugha ikawa kana kwamba kiumbe hata katika kukuwa kwake na katika matumizi yake.
Kila herufi ina kitenzi chake maalumu kwa ajili ya herufi hiyo, huu ni uhalisia wa kwanza. Kwani vitenzi vipo aina mbili: Kitenzi chenye kuvuka na kufika mpaka kwa mtendewa na kufungamana na mtendewa moja kwa moja, na kitenzi kinafungamana na mtendewa kwa njia ya herufi, na hii aina ya pili – ambayo huitwa Kitenzi cha lazima – ndani yake kila kitenzi kina herufi, au sema ni lazima kila herufi iwe na kitenzi.
Katika utajiri wa lugha na undani wake ni pamoja na kile kinachoitwa Udhamini na Dhamira: Kwa maana kuwa wakati mwingine wanatumia herufi nyingine pamoja na kitenzi na wala sio herufi maalumu kwenye kitenzi hiko, na wao wakimaanisha kuwa kitenzi hiki kimejaa kitenzi kingine na kuwa mbele yangu kuna vitenzi viwili: Kitenzi nina kitamka na kitenzi kingine nakidhamini pamoja na maana ya kitenzi cha kwanza, ni kutoka wapi umekuja uelewa wangu kwenye kitenzi hiki kingine? Umekuja kutoka kwenye herufi.
Anasema Mola wetu Mtukufu: {Na wanapo kuwa peke yao na mashetani wao} Al-Baqarah: 14, ukifanya utafiti katika lugha tunakuta kuwa neno “Peke yao” limeungana na herufi ya “Baa” na wala sio herufi ya “Ilaa” na katika Hadithi Mtume anasema: “Asikae chemba mwanaume na mwanamke” ( ), nayo katika maneno ya Waarabu na mashairi yemejiridhisha katika hili, kana kwamba asili ya neno ni kuwa: “Pindi wanapokuwa kwa mashetani wao”, basi vipi kuhusu matumizi ya herufi “Ilaa” badala ya herufi “Baa”?
Ukweli ni kuwa kitenzi kinaweza kutosheka kwa kitenzi kingine kikija pamoja na herufi “Ilaa” nayo yenye kuleta maana ya utulivu, kwa sababu kinachofaa kwenye muundo huu ni kutumia herufi Ilaa, kisha ibara inakuwa wakati wa kuichambua: “Na pindi wanapokuwa peke yao na kutulia kwa mashetani wao wanasema hakika sisi tupo pamoja na nyinyi” utulivu huu umekuja kutoka wapi? Kutokana na herufi. Kisha kumekuwa na uelewa kina wa kujitenga, lau nisingekuwa nafahamu katika hilo kanuni ya udhamini “Kudhamini kitenzi kingine kinachoelezewa na herufi” nisingekuwa na msingi wa maana hii ya ndani ambayo unajenga taswira ya hali ya nafsi ya ubishi, hali inayotokana na nia iliyolala kutokana na kuridhika na unafiki ndani ya mioyo yao kwa kuzingatia ni jambo lenye kuleta utulivu bila hata kulirejea, hii inanipa hukumu na picha nyingine tofauti na ile iliyofahamika kutokana tu mmoja wao amejitenga na mwingine, yote hayo ndani ya neno moja, bali ndani ya herufi moja nayo ni “Ilaa”.
Na katika maelezo pia ya muundo tunakuta maneno “Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa huruma Mwenye kurehemu” ambapo tunakuta herufi “Baa”, na tunaamini moja kwa moja kuwa herufi hii itakuwa imeungana na kitenzi, basi kikowapi kitenzi hapa? Hakipo, hivyo ni lazima nikadirie kwa maana ya kufikiria. Na hapa inakujaa aina miongoni mwa aina za uelewa na ufahamu wa kina kwa munasaba ambao ni lazima ndani yake nikadirie kitu ambacho hakipo mbele yangu, na hii ndio inaitwa “Dhamira” na yepi yanayo nionesha hayo na kunisukuma kwenye hilo? Ni kanuni ambayo tumeitaja: Kuwa ni lazima kila herufi katika lugha ya Kiarabu iungane na kitenzi. Basi kitenzi kipo wapi? Kipi kinachokubaliana?
Inawezekana makadirio yakawa ni jumla yasio ainisha eneo: Tunaanza na Bismillah Rahman Rahiim, inawezekana kuwa na makadirio maalumu yanaoainisha eneo: Ninasoma au unasoma Bismillah Rahman Rahiim, na inaweza kuwa makadirio kwa kitenzi “Ninaanza, Ninasoma…..” au kwa kile kinachochukuwa nafasi ya kitenza kama vile chanzo kwa mfano: Mwanzo au Kisomo changu Bismillah, na inaweza kukadiriwa kwa kutangulia: “Ninasoma Bismillah”, au makadirio kwa kuchelewa, mfano: “Bismillah Naanza” uwezokano wa aina nane, na uwezekano huu wa aina nane ninafikiria iliyokuwa bora zaidi na kufaa zaidi.
Hivyo basi, herufi zina simulizi kubwa zingine, tunapaswa kutosimama tu kwenye athari ya herufi, wala kwenye kazi yake, isipokuwa tunapaswa pia kutafiti masuala mengine ya matamshi: suala la mgawanyiko, suala shirikishi, suala halisi na ufupisho lakini pia kutafiti katika jumla: Muundo, mfumo, kutangulia, kuchelewa na mengineyo, uchambuzi huu haukuwa isipokuwa ni jaribio la kuiangaisha akili ya kisasa ili ivaane na safari hii muhimu.
Hali ya kwanza ya tamshi “Mgawanyiko”:
Pindi tulipokusanya maneno ya Kiarabu tulikuta mara nyingi yanayotengeneza neno ni harufi tatu, kwa kawaida pia tumekuta baadhi ya maneno ambayo yanaundika na herufi mbili na herufi mfano wa herufi “Wa, Au” lakini neno mara nyingi asili yake ni herufi tatu, tukakuta herufi ishirini na nane tunataka kutengenezea maneno ya herufi tatu tatu, kwa maana kila neno herufu tatu, kwa mabadilishano na makubaliano inatokea kwetu kiasi cha uwezekano wa maneno milioni tano, maneno haya yanawezekana kutengeneza maneno ya herufi tatu tatu, lakini yaliyopokelewa kwetu kutoka kamusi ya Lisaanu al-Arab haizidi mashina ya kilugha elfu themanini iliyobakia ni haina uzito…iliyotumika na Waarabu iliyowezekana ni michache sana kuliko ile iliyotupwa na kutopewa uzito na umuhimu ni kama matumizi ya (0.2%) katika elfu moja yaliyowezekana.
Mashina haya elfu themanini ni karibu ya maneno milioni mbili kasoro kidogo, shina ni la herufi tatu mfano neno (Akala) kwa Kiarabu, kwa Kiswahili lina maana ya amekula au alikula, kitenzi hiki ndio shina asili na mgawanyiko wake ni: (Akala, Aakilu, Maakuul, Aklah, Maakalah……nk) hiki ni kitenzi cha Kiarabu na sio Kiswahili.
Pindi tunapolinganisha lugha ya Kiarabu na lugha ya Kiingereza tunakuta kuwa maneno ambayo yaliyopo kwenye Kiarabu ni kiasi cha maneno laki nane na elfu sitini ambayo yanakubaliana ukiacha yale yaliyoingia kwenye lugha ya Kiingereza kutoka lugha Jurmiya Kiarabu Kilatini na lugha zingine, haya yamo kwenye kamusi ya Oxford kubwa ambayo ina juzuu ishirini na tano, maneno katika Webster hayazidi laki moja maneno yasiyo na mashina, na katika Michael West kuna maneno kiasi cha elfu ishirini na nne. Ama katika lugha ya Kiarabu tunayo: Mashina elfu themanini katika kamusi ya Lisaanu al-Arab ya Ibn Mandhuur, ni kamusi elezo kubwa zilizopo kwenye mlango huu, kuna mashina elfu thelathini katika kamusi ya Muujam al-Waseet ambayo imetolewa na jopo la wasomi wa lugha ya Kiarabu nchini Misri, na mashina elfu arobaini ndani ya kamusi ya al-Muheet ya Feiruz Abaady.
Mashina mangapi katika mashina haya yanakusanywa na Qur`ani Tukufu? Qur`ani ina mashina 1840, kwa maana ya chini ya 2.5% ya jumla ya mashina yanayotumika katika lugha. Haya yanaonesha kuwa jambo ni jepesi kwa kiasi fulani kwa sababu lau nitaleta mashina haya 1840 na kuyafanyia kazi kwa kina hiki basi nitafahamu Qur`ani kwa kina zaidi, na kuwezekana – pamoja na baadhi ya kanuni za viwango mbalimbali vya kufahamu - kufahamu ufahamu mwingine.
Kwa upande mwingine, ni kuwa baada ya shina linakuja tawi, na tawi huitwa mikondo, kuweka tawi huitwa migawanyo, na hii migawanyo inakamilika kwa kanuni na wizani ambayo huitwa kwa jina la “swarfu” matumizi au matumini ya kanuni za uundaji kitenzi, na wizani huu ni wenye maana na miongozo katika maneno yote, wizani inawezekana kutumika kwa ajili ya suala au maana maalumu, mfano: Neno lililokuwa kwenye wizani wa “Faalalah” lina uhusiano wa sauti kama vile: Swalswalah, Salsalah, Balbala, Jaljalah…..nk, na lililo kwenye wizani wa “Tafaala” linaelezea uhusiano kati ya pande mbili, mfano: Tabaayaa, Tashaajara, takaatala….nk.
Tamko kati ya ushiriki mfungamano tofauti.
Ushirika katika lugha ya Kiarabu ni tamko moja linachukuliwa kuwa na maana zaidi moja. Mfungamano ni kuwa maana moja inaelezea matamshi mengi. Tofauti ina maana ya kuna tofauti kati ya maana mbili ya matamko mawili pamoja na kufanana.
Kwa mfano, kuna tofauti kati ya fukara na masikini pamoja na kufanana hali hizi, na pamoja na matumizi yetu ya matamshi mawili ni kama visawe katika hali nyingi, basi haiingii akilini Mwenyezi Mungu Mtukufu kusema: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri na masikini} At-Taubah: 60, fakiri ni masikini na masikini ni fakiri, ni lazima kuwepo na tofauti, fakiri ni kana kwamba mtu aliyekosa ni kama ambaye anamiliki pato la watu wawili naye ana zaidi ya watu kumi, kwani tofauti ni kubwa, na huyu masikini ana hali nzuri kidogo ni kama yule ambaye anapato la watu saba lakini anahitaji cha kutosheleza watu kumi.
Hapa ni kitu kidogo, wanasema kuwa: Hivyo maneno mawili yamekutana katika utajo lakini yametofautiana katika maana, hivyo katika utajo yametofautiana katika maana yamekutana.
Uongo kuongopa na uzushi ipi tofauti? Ikiwa matamshi haya yatatenganishwa na kushirikiana katika kuelezea maana ya uongo hata kama itakuwa kwa viwango na sura mbalimbali, kwani uongo ni simulizi kuhusu ukweli kwa kitu kisicho na ukweli, ama uzushi ni simulizi kuhusu jambo halijatokea kwa asili, kwa maana mzushi anafanya kazi ya kutunga kisa, kuongopa ndani yake kunapatikana kero kwa anayeongopewa, ikiwa utataja matamshi haya, itakuweka wazi tofauti iliyopo, ikiwa utataja kila moja peke yake itakupa maana ya uongo…..na kama hivyo.
Sehemu hii inawezekana kuiweka katika misingi ya kilugha, kwani kuna hali ya kushirikiana kufungamana na kutofautiana….wasomi wa zamani walitunga kitabu kwenye mlango kilichoitwa “al-Furuuk” kwa maana ya tofauti, ni utafiti unaohitaji upembuzi wa kina ili kusonga mbele katika safari ya kufahamu akili za urithi wa Muislamu.
Tamko kati ya uhalisia na ufupisho:
Vilevile miongoni mwa misingi ya tamshi la Kiarabu ni ukweli kwa maana ya uhalisia na ufupisho, pindi ninaposema: Nimemuona simba kwenye wanyama wanaowinda, huu ni ukweli, lakini ikiwa nitasema: Nimemuona simba nikiwa nina maanisha mtu shujaa hii inazingatiwa ni ufupisho, hivyo matumizi huathiri katika tamshi. Mlango huu ni mpana tunaelezea baadhi ya alama zake katika maeneo yafuatayo:
Hii ni kuhusu misingi ya tamshi au tamko katika lugha ya Kiarabu kwa sura ya juu juu, lakini katika ukweli wa kisa ni mkubwa unahitaji jitihada za mtafiti wa maana kupitia urithi.
Muundo wa sentensi ya Kiarabu:
Ni lazima kujifunza muunda wa kilugha, kwani jumla au sentensi ya Kiarabu inaundika kutokana na nguzo mbili zilizo wazi na nguzo ya tatu imejificha:
1- Nguzo ya Kwanza – “Unganisho” katika elimu ya mantiki huitwa “Maudhui” katika elimu ya Sarufi Nahau huitwa “Mwanzo” katika sentensi iliyoanza na jina, na huitwa “Mtendaji” kwenye sentensi iliyoanza na kitenzi, katika elimu ya Ustadi na Ufasaha wa lugha “Balagha” huitwa unganisho, kwa maana ya tamshi ambalo linaunganishwa na maneno mengine.
2- Nguzo ya Pili – “Tegemezo” na huitwa katika elimu ya mantiki “Habari” na huitwa kwenye elimu ya sarufi pia “Habari” katika sentensi iliyoanza na jina, na “Kitenzi” kwenye jumla iliyoanza na kitenzi, katika elimu ya ustadi na ufasaha wa lugha huitwa “Tegemezo” kwa maana tamshi ambalo linakamilika kuunganishwa na maudhui ili kukamilisha maana, basi huwa lina habarisha “Maudhui”.
3- Nguzo ya Tatu – “Egemezo” nayo ni ibara ya kiunganishi kati ya Tegemezo na Unganisho, wakati mwingine huitwa “Uhusiano” au “Hukumu” au “Habari” au “Wasifu”…. Matamshi ni mengi na yapo tofauti, lakini maana ni moja.
Mfano: Waumini ni wenye kufaulu, hakika wamefaulu Waumini, suala la kufaulu limeunganishwa kwa Waumini, hivyo Waumini ni waunganishwa, au maudhui ninayoizungumzia, na egemezo hapa ni “Wenye kufaulu na hakika wamefaulu” mwisho kabisa nina vipengele vitatu: Viwili vipo wazi navyo ni Tegemezo na Unganisho, cha tatu ni maana nayo ni kazi ya Egemezo lenyewe.
Sarufi:
Waarabu wametangulia katika kutamka sentensi hii kwa njia sahihi na kusimamiwa kwenye sura za Sarufi, kwa maana ya elimu ya Nahau, na nahau au sarufi ni usimamizi ambao unaipa sentensi maana yake, nayo inasimama kwenye maana pia, kama walivyosema: “Sarufi huzaa maana”. Maana hukaa kwenye akili na ufahamu kama vile taswira, kisha mtu anataka kuitoa kupitia maneno na kuanza kazi ya “Kuelezea” ambayo ni lazima itengenezwe kwenye uwanja wa lugha, inaanza kwa kufahamu herufi za ujenzi na kutokana na herufi hizo hutengenezwa tamshi kwa matumizi ya (Uboreshaji wa mikondo kutokana na mashina ya vitenzi vya herufi tatu), kisha huchunguza hali ya tamshi katika uhusiano wake na matamshi mengine (Ushirika Mfungamano tofauti na…..) mara nyingi huchunguzwa matumizi (Halisi na ufupisho kwa kutanguliza na kuchelewesha….) na kazi za matamshi (Maana na miongozo) kisha muundo wa sentensi kwa kukusanya tegemezo kwenye unganisho, na muundo huu au muunganisho wa mwisho sio tu kupanga maneno kuwa karibu na pamoja, kwani inaweza isipelekee kwenye maana inayo hitajika. Katika mifano iliyopita haifai kusema: Wenye kufaulu Waumini, wala kusema: Hakika kufaulu Waumini. Muundo na mpangilio huu si sahihi, na sababu ni kutofuata kanuni za sarufi ambapo hutiwa “Irabu” kwenye maana na hutolea maana ya wazi wakati wa mkusanyiko wa matamshi kwa sura iliyosimamiwa vizuri.
Kuna kanuni za Irabu au sarufi na vipengele vinavyo rahisisha kufanyia mazoezi, navyo vinafahamisha hali zote za sentensi ya Kiarabu, na hali za matamshi (Herufi kitenzi na jina): kama vile kitenzi ni wakati gani kinakuwa ni silabi ya dhumma? Na wakati gani kinakuwa na silabi ya fat’ha au saknah? Kuna vipengele vya silabi za fat’ha na silabi za sakna, navyo ni vipengele huipa kitenza umbile la silabi ya fat’ha na saknah kama vile hutoa maana ya kukanusha au amri au katazo au sababu…..n.k.
Vilevile jina linakuwa kati ya silabi ya dhumma fat’ha na kasrah kwa mujibu wa nafasi yake katika sentensi na vile vinavyoitangulia miongoni mwa vyombo na maneno, inakuwa na silabi ya dhumma kwa kuwa ni mwanzo au jina la herufi ya “Kaana na ndugu zake” ambayo jina la mwanzo wa sentensi hupewa silabi ya dhumma na habari yake hupewa silabi ya fat’ha, au habari ya herufi “Inna na ndugu zake” ambapo hupewa jina mwanzo wa sentensi hupewa silabi ya fat’ha na habari yake hupewa silabi ya dhumma na kuendelea, yote haya ni ibara ya elimu ya Nahau au sarufi.
Ustadi na ufasaha:
Lakini kuna elimu nyingine inayofungamana na “Njia ya utengenezaji wa sentensi au jumla ya Kiarabu” katika muundo unaokamilisha sura ya falsafa ya lugha ya Kiarabu, nayo ni Elimu ya balagha au Elimu ya Ustadi wa lugha, njia ya kutengeneza jumla inafanyika kwa kanuni: Kukubaliana maneno na mazingira ya hali iliyopo, hii ndio elimu ya ustadi wa lugha. Mazingira ya hali ni yapi? Ni mazingira ya hali ya msikilizaji, msikilizaji huenda akawa akili yake haipo kwenye suala ambalo linazungumzwa, na huenda akawa ni mwenye kusuasua kwenye suala linalozungumzwa, na huenda akawa hakubaliani na suala lenyewe au maudhui yenyewe, ikiwa msikilizaji hayupo kiakili kwenye maudhui basi ibara inakuwa ni nyepesi (Mti una majani), hii ndio hali pindi ninapozumgumza na mtu anayetaka kujifunza, naye ndio ananisikia kwa mara ya kwanza, hakuna kati yangu na yeye kitu chochote kinachozuia kuamini maneno yangu, lakini mtu mwenye shaka shaka ambaye bado anajiuliza: Je mti ni una majani au hapana? Ninamwambia: (Hakika mti ni una majani), katika jumla ya kwanza hakukua na msisitizo wowote tofauti na jumla ya pili ambayo ndani yake kuna herufi au chombo cha msisitizo nayo ni herufi ya “Inna” katika lugha ya Kiarabu au neno hakika kwa lugha ya Kiswahili. Ama katika jumla ya tatu ndani yake kuna ongezeko la msisitizo kwa sababu msikilizaji ni mwenye kupinga suala, kwa mfano nanisema: (Hakika mti ni wenye majani, au Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika mti ni wenye majani) kama hivi kumekuwa na herufi tatu za msisitizo na uthibitisho.
Baadhi ya nyakati mtu anakuwa yupo mbali kiakili au hayupo kiakili lakini – kwa ufahamu wangu mbaya wa hali yake au yale yanayopaswa kwenda nayo na hali mbalimbali – naweza kumsababisha kuwa ni mwenye kusuasua au kupinga, kwa sababu hiyo ninazungumza naye kama vile ni mtu mwenye kupinga au kujiulizauliza, kama vile mazingira ya hali na kujieleza kunapelekea kufahamu nafsi ya mzungumzaji na mtazamo wake kwa anayepokea mazungumzo, hii hakuna shaka ni mambo yenye umuhimu mkubwa kwa kila mtafiti ambaye kazi zake zipo kati ya kusoma “Kupokea” kuelewa “Kugundua” na kuandika “Kuelezea”, kama vile ni jukumu la mlinganiaji, kila Muislamu mwenye kulingania kwenye Dini yake.
Lugha ya Kiarabu ndio ambayo inaelezea kuhusu akili ya Muislamu, nayo inabeba katika mwenendo wake msingi wa akili hii ya kiurithi na vinavyozalishwa na mfumo wake wa kwenda sawa na uhalisia au uwepo, hiko ndio chombo cha fikra ya Kiislamu na chombo cha elimu ya Kiislamu, kisha inapaswa kuwa asili katika jaribio la kurudisha ujenzi wa mfumo katika sayansi ya sasa ya jamii na ubinadamu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

 

 

 


 

Share this:

Related Fatwas