Lugha Takatifu na Utakatifu wa Lugh...

Egypt's Dar Al-Ifta

Lugha Takatifu na Utakatifu wa Lugha

Question

 Je! Kuna lugha takatifu? Nini maana ya utakatifu wake? Na tunazingatia utakatifu huo kwa kiwango gani?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
1- Lugha takatifu kwa wanaisimu inaelezea lugha ambazo zina matini matakatifu ambayo yana wafuasi ambao huyachukulia kama chanzo cha maarifa na hukumu za maisha yao, au kama mfumo wa tabia zao. Kwa ufafanuzi huu, lugha ya Kiheberu ambayo "Torati" iliandikwa kwayo, lugha ya Sanskriti ambayo "Veda" iliandikwa kwayo, na lugha ya Kiarabu ambayo "Qur`ani Tukufu" ilishuka na kuandikwa kwayo, ni lugha takatifu. Mwenyezi Mungu amesema: {Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani kwa Kiarabu ili mpate kuzingatia.} (Yusuf: 2) Mwenyezi Mungu amesema pia: {Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi.} [ASH-SHURAA: 195) {Qur'ani ya Kiarabu isiyo na upogo, ili wamche Mungu.} (AZ-ZUMAR: 28)
Wasemaji wa lugha hizi na wale ambao wanayaamini marejeleo ya matini hizi hawakubali kuziacha sio kwa maendeleo au kwa kuzorota, wala hawazibadilishii semantiki ya maneno, wala njia za kuelewa suala lolote la sarufi na mofolojia. Ambapo kufahamu hukumu kutoka katika matini kunahitaji hivyo, na hii inategemea na ukweli kwamba lugha ina kazi mbili: kazi ya kwanza ni utendaji, na kwa njia hii, msemaji anaelezea kile alichonacho akilini mwake kutokana na maana ya maneno iliyokubaliwa na watu wa lugha moja. Ambapo maneno haya yaliwekwa kwa maana hizo, na aliyeyaweka maneno haya kwa mtazamo wa baadhi yao ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu anasema:
{Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli.} (AL BAQARAH: 31). Kwa wengine, walioyaweka maneno haya ni wanadamu, na kundi la tatu linaamini kwamba asili ya lugha na sheria zao zimetoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba ni maneno yanayotokana na hali ya wanadamu, na hii sio muhimu sasa, lakini muhimu ni kwamba kuweka - kwa maana ya kuunda maneno yenye maana maalumu - ni lazima ili uelewa uwafikie wanadamu. Hii ni kwa sababu mzungumzaji huwasilisha maana ambazo zimewekwa akilini mwake kwa msikiaji ambaye hubeba maneno haya kwa maana ambazo mpangaji alikuwa amezisimamia hapo awali, na kwa hii dhana ya msikiaji hutimiza kazi ya pili ya lugha, ambayo ni kazi ya mapokezi.
Tuna hatua tatu: ya kwanza ni kuweka, ya pili ni matumizi, na ya tatu ni kufahamu. Hata wataalamu wa Usul Al-Fiqh walisema: Matumizi ni mojawapo ya sifa za mzungumzaji, na kufahamu ni mojawapo ya sifa za msikilizaji, na hali ya kuweka ni kabla ya sifa mbili.
Wengine kutoka Madhehebu ya Kisasa zaidi wanasema kuwa mchakato wa kuweka unapaswa kubadilika na sio kufungwa na jadi, na dhana hii haizuwii upanuzi wa lugha kulingana na kuongezeka kwa eneo la ulimwengu wa vitu, watu, matokeo, maoni, na mifumo; Nayo ni upana uliokubaliwa kwa kuzingatia na tendo, Bali, nia yao ni kubadilisha semantiki ya maneno ili eneo la uhuru wa akili liweze kuongezeka zaidi, na madhehebu mengine yenye msimamo mkali wa shule za Kisasa zaidi zinaamini kuwa kuna mambo matano ambayo yanapaswa kuondolewa ili mawazo ya mwanadamu yaweze kubuni na kuendelea bila kizuizi chochote na mambo hayo matano ni: Utamaduni, Dini, Familia, Serikali na Lugha.
Kuondoa mamlaka ya utamaduni mkuu ni jambo litakalosababisha mwelekeo wa "uuwiano wenyewe hasa" ambao shule hizi za fikra zinataka kuupitisha. Kuondoa mamlaka ya Dini tayari kumefanyika kwa ustaarabu wa Magharibi, na familia sasa inaitwa kwa majina mawili, katika kufanya hivyo maana haipo tena: mume na mke, mtoto, binti na baba mama ... familia, maana ile ile ambayo tuliirithi kutoka kwa wale waliotutangulia, na wanaichukulia hii kama ni moja ya maana, ambayo tumeipata katika kamusi ya leksimu, na kutoka katika uingiliaji huu ushoga - ambao ulilaaniwa na wanadamu katika dini zote - ni miongoni mwa haki za binadamu.
Na kuondoa mamlaka ya serikali na kuibadilisha kwa vyama visivyo vya kiserikali na asasi za kiraia - kunahitaji kubadilisha mfumo wa sheria na mfumo wa kijamii, bali sheria za fikra, mtindo wa maarifa na kumbukumbu.
Kuhusu kukomesha mamlaka ya lugha, ni jambo la kutisha sana, na tunakumbuka baadhi ya maneno ya kitabu cha Profesa Sherif El Shobashi "Litahiya Al-Lugha Al-Arabiyah; maana y will: Iishi Lugha ya Kiarabu", ambapo g nne kwenye ukurasa wa 24 kwamba: “Mbali na mchango wabjke wa kimsingi kama njia pekee ya kuhifadhib. urithi na kuipitisha kwa vizazi vyote, lugha ni mojawapo ya vitu muhimu zaidi vya ustaarabu na utambulisho wa ubinadamu katika kila mahali, na mawasiliano ya kwanza kati ya mwanadamu na mwingine ni kupitia lugha; viongozi, wanasiasa na wachumi wanahitaji watafsiri kwa uelewa, na ikiwa hakuna Wafasiri hawa ambao wanajua lugha zaidi ya moja, uelewa unakuwa mgumu sana au usiowezekana. Lugha ni chombo cha msingi cha ufahamu, lakini pia ni chombo cha maono ya mwanadamu kwa maisha. Kwa hivyo, lugha ndio kitu ambacho huunda utamaduni, fikira, falsafa na fasihi,” naye anathibitisha kile tunakichoamini katika suala la lugha.
2- Kulingana na Wafuasi hawa wa Usasa, kazi ya lugha ni upokeaji tu, na hii inamaanisha kuwa msikilizaji hubeba maneno kulingana na maana yoyote anayotaka, bila kujali nia ya mzungumzaji wa maneno yake, na kwa hivyo mlango wa tafsiri hufunguliwa bila udhibiti wowote au kiungo, na tunafikia uwiano wenyewe. Ambapo kila msikiaji anaelewa anachotaka kuelewa na haangalii makusudio ya maneno juu ya kile alichowekewa, kana kwamba anafuata usemi wa Mutanabi katika shairi lake la “Farasi na Usiku”:
Mimi ndiye yule kipofu alieiangalia adabu yangu
Na maneno yangu yakamsikiliza asiyesikia
Ninalala nikiwa nimezijaza kope zangu
Viumbe huangalia maneno hayo na kugombana.
3- Lugha takatifu ya Kidini katika lugha ya Kiarabu inatutaka tuzitambue takwimu zinazoonesha mambo ya kweli ambayo huwenda watu wengi hawayatilii maanani, na hivyo basi, zogo na mabishano kuongezeka juu ya mambo ambayo tunaweza kuwa tunakubaliana juu yake, au itupeleke kushusha daraja ya dalili iliyothibiti ikawa daraja ya dalili ya kutafutwa, na daraja ya dalili ya kutafutwa ikawa daraja ya dalili iliyothibiti, na kwa hiyo, kipimo cha Uadilifu ambacho tumeamrishwa sisi tukitumie katika kila sehemu ya maisha yetu na maswala yetu, kitavurugika.
4- Qura'ni ilikuja kwa ajili ya kuboresha lugha ya Waarabu, ambayo ilikuwa imejaa maneno ya kushangaza na ya kinyama.
5- Maneno ya Qura’ni yanakaribia 1810 ambayo yanawakilisha mizizi ya maneno yote ya Qura’ni, wakati kamusi ya "Lisan Al-Arab" ya Ibn Mandhur ina vidokezo karibu elfu themanini - namaanisha mizizi - ikimaanisha kwamba mizizi ya Qura’ni inawakilisha karibu asilimia mbili (haswa 2.25%) ya mizizi ya Lugha ya Waarabu, mizizi iliyotajwa katika Hadithi za Mtume ni 3600, ambayo inawakilisha (4.5%) ya Lugha ya Waarabu, na Qura’ni ni matini takatifu kabisa, na idadi ya maneno yake ni kama maneno elfu 66, ambayo maneno 1620 hayakuonekana ndani ya Qura’ni isipokuwa mara moja tu, na baadhi yao husema: Mwandishi wa Urusi Tolstoy hakurudia maneno 4 katika kitabu chake, “Vita na Amani”, kwa hivyo alihesabu hayo kutokana na ufasaha na umahiri wake wa lugha. Kama hii ni kweli, basi upekee huu wa Qura’ni Tukufu na idadi kubwa ya maneno haya ambayo hayajarudiwa itakuwa muujiza Kwani maana ya neno liliongezwa katika nyanja za miujiza yake ambayo huiondoa kwenye mfumo wa maneno ya kawaida ya wanadamu.
6- Ukweli huu unatufanya tufikie hitimisho kwamba kuna lugha takatifu, lakini lugha hii takatifu lazima ihifadhiwe ndani ya mipaka ya maandiko matakatifu jinsi tutakavyo, na katika mipaka ya zana za ufahamu wake katika kiwango cha matamshi yake, maana zake, na kwa kiwango cha miundo yake na maana za miundo hiyo mbalimbali, na kwa kiwango cha muktadha wake pia. Ukuaji wa lugha unawezekana, lakini kwa njia ambayo haipotezi mawasiliano yeyu na mkusanyiko wa maarifa ya jadi kwa upande mmoja, na kwamba ni chombo kinachoweza kuzindua mawazo katika nyanja zake zote; mawazo ya kisayansi, ya hisia, ya majaribio na hata ya falsafa, na kutumia akili; ili mwanadamu abaki kuwa mwanadamu anayetimiza wajibu wake wa kumwabudu Mwenyezi Mungu, kujenga dunia, na kusafisha roho, na kwamba mabadiliko haya pia hayapaswi kuathiri msimamo wa wanadamu, na kwamba awe na uwezo wa sawa na upanuzi wa asili ambao unatokana na Sheria za Mwenyezi Mungu katika Ulimwengu wake:
{Tutawaonesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je! Haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi wa kila kitu?} (Fusilat: 53)
Ni lazima pia tujue wakati wa hatua za upanuzi wa mikondo yenye misimamo mikali ambayo imeenea katika wakati wetu, na ambayo kusudi lake haliendani na maono yetu ya Ulimwengu, au na maamuzi ya Dini yetu, misingi ya Ustaarabu wetu na Historia yetu, na kwamba shughuli zetu pamoja na lugha ni za kujenga sio za uharibifu.
7- Ukweli huu pia unatufanya tuende kwenye kutokuwepo kwa utukufu wa lugha, na kwamba kuna tofauti kubwa kati ya lugha takatifu ambayo lazima ihifadhiwe ili kuelewa matini, na utakatifu wa lugha inayoizuia kupanuka na kutekeleza jukumu la enzi yake na wakati wake.
Rejeleo: Kitabu cha: [Simaat Al-Asr, kwa Mufti Mkuu wa Misri, Dk Ali Jumaa].

 

 

 

 

Share this:

Related Fatwas